Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 25 & 26 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 25 & 26 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Wednesday, February 1, 2017 | 12:52:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Rahab akanyanyuka kitandani na kuondoka, akamuachia maswali mengi Eddy, dakika hata mbili hazikupita Shamsa akaingia chumbani kwa Eddy bila hata ya kubisha hodi, mkononi akiwa ameshika bastola huku mkono mwingine akiwa ameishika simu ya Lube, huku akiwa ameiweka sauti iliyo rekodiwa, sura yake akiwa ameikunja kwa hasira akichefuliwa na tukio alilo lifanya Eddy pamoja na mke wa raisia, kwa bahati mbaya akamkuta Eddy ndio ananyanyuka kitandani akiwa kama alivyo zaliwa na wote wakabakiwa wakiwa wametazamana.

ENDELEA
“SHAMSAAAAAAA…………………..”
Eddy alijikuta akipiga kelele huku akimtazama shamsa aliye ingia, Shamsa akageuka na kumpa Eddy mgongo, akimuashiria ajisitiri kwa chohote, haraka haraka, Eddy akajifunga taulo alilo jifutia mji Rahab kisha akaguna, Shamsa akageuka akiwa na sura ya kukasirika aliyo ingia nayo ndani humo.
‘Eddy huu ndio ujinga gani unaufanya, hata wiki haijaishi ta mazishi ya mama leo hii unakuja kulala na mke wa raisi hivi akili yako ina akili kweli wewe”
 
“Nena haitoshi umeamua kufanya nae huo ushenzi ndani ya chumba alicho kuwa ana lala mke wako kipenzi, juu ya kitanda chake hivi ni haki kweli eheeee?”
Maswali yote ya Shamsa hapakuwa na jibu lolote kutoka kwa Eddy, kichwa alikiinamisha chini kwa aibu ambayo ameipata kutoka kwa binti huyo anaye mchukulia kama mwanae.
“Sikiliza ujinga wenu huu na umesha tumwa kwa raisi sasa wewe angalia ni kipi ambacho kitatokea muda wowote kuanzia sasa hivi”
 
Shamsa akamrushia Eddy simu iliyo rekodiwa sauti zao wakiwa kitandani, Eddy akazisikiliza kwa umakini, mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbia kiasi kwamba akatamani ardhi ipasuke ili aingie na kujichimbia humo. Ila haikuwa hivyo, akarudia tena kuisikiliza akihisi kama sauti sio zao ila sauti ya Rahab na yake zilisikika vizuri kutoka kwenye simu hiyo.
“Haya ona sasa, sura yako utaiweka wapi Eddy, Sura zetu tutaziweka wapi, hivi hiyo zipu yako huwezi kuifunga unapo ona ku** za wanawake eheeee?”
 
Shamsa alizungumza kwa hasira kali hukuy machozi yakimwgika kwa uchungu.
“Hembu tazama jinsi jamii inavyo kuchukulia, halijaisha tatizo moja umezua jengine kweli, kweli Eddy huu ndio uwaziri wako jinsi unavyo kutuma kufanya. Unadhani kifo chako kipo mbali kwenye hii dunia?”
“Nilitegemea kuwa na kiongozi bora mwenye kuipenda na kuiheshimu thamani yake ila wewe, sijui humo akilini mwako unategemea nini”
 
Eddy taratibu akanyanyuka kitandani na kuanza kupiga hatua za kumfwata Shamsa sehemu alipo simama, ila kambla hajamkaribia, akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola aliyop ishika Shamsa.
“Ukinisogelea Eddy ninakumwaga ubongo”
Shamsa alizungumza huku akiikoki vizuri bunduki yake tayari kwa kufyatua risasi
 
 ***
    Jaclline akampitia Agnes kwenye sehemu aliyo muambia wakutane na safari ya kuondoka katika eneo la karibu na ikulu ikaanza.
“Ilikuwaje kuwaje hadi wakakufahamu?”
“Hata mimi mwenyewe sifahamu”
“Muda mwengine tuwe makini Agy hii nchi ulinzi wake ni mkali kama tumeamua kufanya tukio kama hilo tunatrakiwa kuwa makini, hapa kama walisha weza kuidaka sura yako basi watatufwatiliwa kwa satelait kujua ni wapi tulipo”
 
“Sasa itkuwaje?”
“Hapa ni lazima tuondoke ndani ya Marekani hatuna jinsi tena”
Wakiwa barabarani gafla mwanga mkali kutoka juu ukalimulika gari lao linalo kwenda kwa kasi kubwa. Kila mmoja wao akatambua tayari mambo yamesha haribika na hapo wanafwatiliwa na helcoptar ya polisi.
 
Jaquline akazidi kuongeza mwendo kasi wa gari hiyo ndogo aina ya Ferrari Spide yenye spidi mita zaidi ya mia tatu. Risasi kutoka juu zikaanza kuilenga gari yao, jambo lililo mfanya Jaquline kuiendesha gari hiyo kwa kuiyuimbisha yumbisha ili mradi risasi zisije kuingia kwenye gari yao.
 
Askari mji mzima wakap[ewa taarifa juu ya magaidi wawili wanawake walio kuwa wamejipanga katika kuishambulia ikulu ya Marekani, kile eneo la mji vikosi vyote vya ulinzi vikajiweka sawa, kuhakikisha magaidi hao hawatoke ndani ya mji huo
“Ndio bosi”
Sauti nzito ya mwanaume ilisikika baada ya kupokea simu kutoka kwa bosi wao wanaye muheshimu sana.
“Hakikisheni hao magaidi wanao fukuzwa hawaingii mikononi mwa askari, wachukueni na kuwatorosha”
“Sawa mkuu”
 
Bosi wao akakata simu huku macho yake akiyatupia kwenye luninga yake kubwa akitazama taarifa ya moja kwa moja kwenye kituo cha CNN, wakionyesha jinsi askari wanavyo ikimbiza gari ndogo ya magaidi hao wanao sadikika ni wanawake.
Gari za polisi zinazo wafukuzia, kwa nyuma zikazidi kuwachanganya Agnes na Jaquline, kila jinsi wanavyo zidi kwenda ndivyo jinsi gari hizo zilivyo zidi kuongezaka na kuja kwa mwendo wa kasi, huku baadhi ya helcoptar za polisi zikizidi kuwaandama.
 
Katika daraja refu, wanalo pita, linalo unganisha mji mmoja na mji mwingine chini yake kukiwa na maji ya bahari, umbali wa kilomota mbili mbele, askari wengi wenye silaha tayari walisha iziba njia, wakiwa tayari kwa kuisubiria gari hiyo inayo endelea kuandamwa vikali na gari nyingine za polisi pamoja na kikosi cha FBI. Ukimya ndani ya gari ukatawala, Jaquline kazi yake ikawa ni kijitahidi kuhakikisha anaiendesha gari hiyo kwa kasi jinsi awezavyo kulipita daraja hilo pasipo kujua kama mbele kuna kizuizi kikubwa cha askari. 

Agnes kazi yake ikawa ni kumuomba Mungu kuwafanyia muujiza wowote ili mradi waweze kuitoroka mikono hiyo ya askari tena wakimarekani. Askari wa gari za nyuma hawakusita kufyatulia gari la kina Jaquline risasi kila walipo pata nafasi ya kufanya hivyo, Agnes akakoki bastola yake na kushusha kioo
 
“Unataka kufanya nini?”
“Nahitaji kujibu mashambulizi hawawezi kutuonea kiasi hichi”
Agnes akatizama kioo cha pembeni upande wake, akazihesabu gari hizo zinavyo kuja kwa kasi, kwa haraka akachomo mkono wake kwa kupita kioo hicho kwa kutazamia juma, akafyatua risasi kadhaa zilizo piga kwenye kioo cha mbele kwenye moja ya gari ya polisi. Ikampata dereva na kuifanya gari hiyo kuyumba baadhi ya gari za nyuma zikajikuta zikiigonga gari hiyo na kusababisha ajali mbaya sana, iliyo ambatana na mlipuko mkubwa.
“Yes”
Agnes akajipongeza huku akifunga kioo cha gari yake akitazama jinsi baadhi ya gari zikianguka vibaya sana.
 
“Nice shoot”
“Thank you”
Wote wakatabasamu, nakazi ya Jaquline ikaendele kuliendesha gari hiyo kwa spidi kadri ya uwezo wake. Gafla kwa mbali kidogo wakaona kizuizi cha askari wakiwa na magari yao pamoja na bunduki na mbaya azidi kwenye daraja hilo refu hakuna sehemu ya kukimbilia zaidi ya kujitosa kwenye maji ya bahari ambapo ni mbali sana kutoka juu sehmu walipo
 
 ***
   Kitendo cha mlango kugongwa kikamfanya Madam Mery kusimama kwa muda huku akiutizama kwa wasiwasi kwani ni muda mchache tangu alipo ingia ndani ya chumba hicho na hapakuwa na agizo lolote alilo litoa kwa wahudumu wa hoteli hiyo.
 
Madam Mery akataka kuzuuliza ni nani ila akasita kutokana na mlango kugongwa tena, ikambidi apige hatua za taratibu hadi kwenye mlango taratibu akaishia funguo, akaizungusha mara mbili, akishika kitasa na kuufungua mlango, teke kali lililo tua kwenye kifua chake likamfanya arudi ndani huku akianguka chini. Manka akaufunga mlango kwa haraka na kumtazama Madam Mery anaye gugumia kwa maumivu makali akijaribu kunyanyuka kutoka chini.
“MANKA…….!!!”
“Jina langu”
 
Manka alizungumza huku akiishikilia bastola yake vizuri akiwa amemuelekezea madam Mry
“Natambua kwamba baba yako ndio amekutuma kuja kuniua si ndio?”
“Hiyo siyo kazi yako kujua kwamba ni nani aliye nituma kuja kwako, ila ni kwanini umetusaliti?”
“Manka siwezi kuendelea tena kwenye umoja wa baba yako, huku nikiwa ninataka kuwahukumu watu ambao hawana hatia kwenye maisha yao,tazama jinsi baba yako alivyo iteketeza familia ya mdogo wako Eddy”
 
“Ishia hapo hapo Eddy si mdogo wangu, si damu yetu”
Manka alizungumza kwa hasira kiasi cha kumfanya Madam Mery kutetemeka kiasi.
“Manka, Manka utaendelea kutumikishwa hadi lini mdogo wangu. Ni lini ambapo utaamua kuwa na familia yako, kuwa mama wa wanao. Umeona vizuri jinsi mtoto mdogo wa mdogo wako alivyo uliwa si ndio”
 
Madam Mery alizungumza huku machozi yakimwagika.
“Machozi yako hayata nizuia mimi kufanya nilicho agizwa kukifanya kwako sawa wewe Malaya…..”
Madam Mery hakuzungumza chochote zaidi ya kumwagikwa na machozi mengi. Manka hakuwa na huruma kwa mwanamke mwenzake huyo, akavuta triga iliyo ruhusu risasi moja kuchomoka kwa kasi na kutua kwenye paja la madam Mery na kumfanya adondoke chini huku akitokwa na ukunga mkali wa maumivu.
 
“Shiiiiiii………..  Leo sinto kuua ila hakikisha unajificha maisha yako yote hadi kufa kwako na enndapo utajitokeza tena mbele ya macho ya baba yangu nitakuua sawa”
 Madam Mery akatingisha kichwa akikubaliana na agizo la Manka, aliye toka ndani ya chumba hicho pasipo kuaga.Madama Mery akajikongoja hadi kwenye meza yenye simu akachukua mkonga wa simu hiyo na kuminya namba ya kuomba msaada kwa wahudumu wa hoteli hiyo.
                                                                                          ***
Jaquline akafanga breki za gafla hadi gari tairi zikaserereka na kuifanya gari hiyop kuyumba kiasi ila kajitahidi hadi ikakaa sawa.
 
“Shiti…….”
“Tunafanyaje Jack”
Agnes alizungumza kwa kubabaika, kila mmoja wasiwasi mwingi ukamtawala kwenye moyo wake, si mbele wala nyuma waliweza kuzingirwa na gari za polisi, isitoshe juu angani kuna helcoptar za polisi zinao wamulika kwa mwanga mkali mweupe.
“Kuna umbali mrefu kutoka chini kwenye hili daraja la Golden gate’
 
Jaquline alizungumza huku mapigo ya moyo yakimwenda mbio, gari za polisi zinazo wafukuzia zikazidi kuwasogelea kwa ukaribu zaidi. Gafla helecoptar mbili za polisi zikaalipuka na kuangukia kwenye kwenye bahari, Helcoptar moja kubwa ya kivita iitwayo AH-64AVD APACHE, ikaanza kushambulia garo za polisi zote zilizo kuwa zikiwasogelea Agnes na Jaquline. Polisi wakachanganyikiwa kwa shambulizi hilo kwani Helcoptar nyingine aina hiyo hiyo ya AH-64AVD APACHE, ikawashambulia askari wote ambao waliweka kizuia, hadi Agnes na Jaquline wakabaki wakishangazwa na tukio hilo
 
“Ni kina nani hao?”
Agnes alizungumza akizitazama Helcoptar hizo zifanya kazi yake. Helcoptar moja nyingine ya tatu aina ya UH-72A LAKOTA LIGHT, ikasimama juu usawa wa gari la kija Jaquline wakashuka vijana wawili kwa kutumia kamba maalumu huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi pamoja na vinyago vinavyo waonyesha macho tu. Kila mmoja akapita pande wake akiwa  wa gari, wakiwa na bunduki mikononi, wakavunja vioo vya gari ya kina Jaquline.
 
“Tokeni nje, tumekuja kuwachukua”
Mmoja wao alizungumza na kuwafanya Agnes na Jaquline kutoka nje ya gazi yao, hapakuwa na aliye hitaji kuuliza swali, kwani tayari walisha anaza kuwaamini watu hao kutokana na msaada walio wafanyia na fika wanaonekana si watu wa serikali.
 
Kila kijana mmoja akamkumbatia Agnes na kujifunga kamba waliyo shuka nayo, huku mwingne akimkumbatia Jaquline na kufanya kama alivyo fanya mwenzake. Kamba hizo zikaanza kuvutwa kwenda juuu, wakaingia kwenye helcoptar hiyo na kuondoka katika eneo la tukio na kuwaachia msiba mzito ndugu wa askari hao walio kuwa wakijaribu kuwazuia magaidi hao.
 
Jaquline na Agnes wakavishwa vigunia vyeusi kichwani wasijue ni wapi wanapo pelekwa na watu hao wasio wafahamu, Safari yao ikachuku lisaa moja wakafika katika kambi moja yenye ulinzi mkali. Wakashushwa kwenye helcoptar na moja kwa moja wakapelekwa kwa mkuu wa eneo hilo, huku wakiwa wamevalishwa vigunia hivyo.
 
“Mkuu hawa hapa”
Mmoja wao alizungumza, Agnes na Jaquline wakavuliwa vigunia vyao macho yao yakakutana na mtu mmoja aliye kalia kwenye kiti kidogo cha matairi cha kusukuma, pembeni yake kukiwa na mijitu mikubwa miwili iliyo panda hewani na kujazia vifua vyao. 

Mtu huyo aliye kaa kwenye kiti hicho akageuzwa na baunsa mmoja, sura ya mtu huyo haikuwa nzuri sana kwani upande mmoja upo kama umeuguzwa na kitu, huku katika eneo la miguuni akiwa amefunikwa na kitambara chekundu, mikono yake akiwa amevaa gloves yeusi.
 
Mtu huyo akawatizama wasichana hao, kisha akaachia tabasamu pana, akionekana kufurahishwa na vijana wake kwa kazi waliyo ifanya.
“Karibuni sana katika makao makuu ya D.F.E, jina langu ninaitwa JOHN”
                                                                                
SORRY MADAM (26) (Destination of my enemies)

“Niliagiza vijana wangu kuweza kuwakokomboa kwa lengo moja tu nahitaji muwe huru na kufanya kazi chini yangu kama hamto jali”
“Hatuhitaji kufanya kazi chini ya mtu yoyote”
Jaquline akajibu kwa kujiamini huku akimtazama John machoni mwake.
 
“Nambueni kwamba hadi sasa hivi umesha kuwa wakimbizi, munatafutwa kila mahali je mupoo tayari kwenda gerezani kama walivyo wezenu”
Maneno ya John yakamstua Agnes, akamkazia macho vizuri John, kisha akamgeukia Jaquline ambaye ajajiuliza juu ya hao wezao, John amaewajuaje.
“Musishangae kuona ninawafahamu Fatuma, Halima, na Anna, wote hawa walikwenda jela kwa ajili yako wewe unaye nitumbulia macho kwa kushangaa”
 
John alizungumza kwa dharau huku akiachia tabasamu pana usoni mwake na kuifanya sura yake kuzidi kuwa mbaya. John akamnong’oneza mlizi wake mmoja sikioni kisha, mlizi huyo akaondosha na John akawageukia Agnes na Jaquline walio kaa kimya wakimtafakari huyu nimtu wa aina gani.
 
Mlinzi wake aliye mnongoneza, baada ya muda kidogo akarejea akiwa na laptop, John kwa ishara akamuomba aifungue, mlinzi wake huyo akaimiminya minya kwa muda kisha John akamuamuru kuwapa Agnes watazame kilichomo ndani ya Laptop hiyo.
                                                                                                     ***
    Eddy akazidi kupiga hatua za kumfwata Shamsa aliye mshikia bastola, Shamsa akazidi kumwagikwa na machozi akimuomba Eddy asimama katika sehemu aliyo muamuru kusimama ila Eddy hakulifanya hilo hadi alipo mfikia, akaishika bastola na kuigandamiza kifuani mwake kwa uchungu.
 
“Niuea”
Eddy alizungumza kwa sauti ya utaratibu na kumfanya Shamza aanguae kilio kikubwa na kuitupa bastola chini na kumkumbatia kwa nguvu Eddy. Dakika tatu nzima zikapita huku wote wakiwa wanamwagikwa na machozi mengi.
“Shamsa samahani sana mwanangu sinto weza kufanya ujinga kama nilio ufanya awali”
 
“Kweli baba?”
“Ndio mwanangu”
Shamsa akazidi kumkumbatia Eddy kwa nguvu, akijaribu jaribu kuyafuta machozi yake. Shamsa akatoka ndani ya chumba cha Eddy akiwa na furaha na amani moyoni mwake, akiamini baba yake hato fanya ujinga kama alio weza kuufanya. Moja kwa moja akaelekea kwenye bustani moja kubwa iliyomo ndani ya jumba lao na nipembezini kabisa kwa fensi inayo elekea kwenye ufukwe wa bahari. Akiwa katika dimbwi la mawazo sauti nzito ikamstua nyuma yake.
 
“Unamuwaza nani?”
Kitendo cha Shamsa kugeuka akakutana na ngumi nzito ya uso iliyo mpotezea muelekeo, gafla kitambaa chenye hewa nzito kikatua puani mwake ndani ya dakika kadhaa akapoteza fahamu. Brian akatazama pande zote za bustani hapakuwa na mtu aliye weza kumuona akifanya tukio hilo, akamnyanyua Shamsa na kumuweka bgegani, akavuka naye kwenye fensi na kwenda kumuweka kwenye moja jabali lililopo pembezoni mwa bahari akisubiria giza litawale anga aweze kuondoka na binti huyo. 

Brian akarudi kwenye jumba la Eddy,kujua ni nini kinacho endelea, hapakuwa na mlinzi aliye weza kustuka kwamba Shamsa hayupo katika eneo hilo, akaingia ndani ya gari lake na kuondoka, akaenda kulisimamisha mbali kidogo na jumba la Eddy, ila ni pembezoni mwa ufukwe wa bahari, akarudi hadi sehemu alipo mlaza Shamsa na kumkuta hayupo jambo lililo mchanganya sana Brian.
 
 ***
   Majira ya saa nne usiku Manka akafika katika kijiji cha Namanga akitokea katika kazi aliyo pewa na baba yake. Akawakuta Mzee Godwin na Tom, wakiwa wanamsubiria.
 
“Umekamilisha?”
“Ndio baba kila kitu kimekwenda sawa”
“Kazi nzuri usafiri upo tayari unatusubiria”
“Sawa”
Wakaondoka na kuingia kwenye roli moja kubwa, lilio andikwa AU, linalo milikiwa na jeshi la umoja wa mataifa, huku mzee Godwin akiwa na watu wake katika jeshi hilo wanao muheshimu na kumtumikia, kwa lolote lile atakalo waeleza kuweza kukifanya. 

Safari ikazidi kusonga mbele huku wakipita katika baadhi ya vituo vya ukaduzi vya kijeshi, pasipo kustukiwa na mavazi yao ya kijeshi waliyo weza kuyavaa, wakawa wanapita salama hadi wanaingia nchini Somali, wakitokea Tanzania kisha Kenya na kutua kwenye ardhi hiyo, aliyo jiwekea kikosi kikubwa cha magaidi anacho kihudumia kwa pesa pamoja na silaha. 

Wakapokelewa na mkuu wa kikosi hicho cha kigaidi cha Al-Shabab, bwana Abdulah Mohamed. Mzee Godwin akawatambulisha John na Manka kwa kiongozi huyo aliye waandalia sherehe ndogo ya kuwakaribisha katika ngome hiyo inayo lindwa kwa ulinzi mkali sana.
“Naona D.F.E, inazidi kukua siku hadi siku kiongozi”
Bwana Abdulah Mohamed alizungumza huku akishushia bkinywaji alicho kishika kwenye mkono wake
 
“Ndio kila siku tunahakikisha tunatengeneza umoja wa siri ambao utadumu miaka na miaka katika vizazi na vizazi”
“Kweli, hivi bado Tanzania, haijastukia juu ya kikosi chako hicho?”
“Hapana hakuna aliye weza kustuka, kwani hata ndani ya ikulu nina watu ambao wapo mikononi mwangu na siku ya siku ikifika, wewe mwenyewe utashuhudia kitakacho tokea”
 
“Usijali Generali Godwin, nitakusaidia kwa lolote ambalo utaliomba nikusaidie katika kukamilisha mipango yako”
“Nitashukuru sana”
Usiku huo mzima ukawa ni stori za hapa na pele kwa viongozi hao wawili wanao pendana sana na kuheshimiana. Tom na Manka kila mmojaa alikabidhiwa chumba chake cha kujipumzisha ndani ya ngome hiyo, wakisubiria kuendelea na safari katika siku ya pili inayo fwata.
                                                                                             ***
“Nini?”
“Ndio mueheshimiwa tumemtafuta eneo zima la hapa nyumbani hatujamuona”
 
Mlinzi mmoja wa Eddy alizungumza huku mikono yake akiwa ameiweka nyuma akimtazama Eddy usoni anaye onekena kuchanganyikiwa kwa taarifa ya Shamsa kuto kuonekana hadi mida hii ya saa tano usiku. Eddy akayafumba macho yake kila anacho kifikiria akaishi kichwa kinampasuka, kwani amesha poteza, mama, mke na mtoto, ila Shamsa ampoteze pia. Likawa ni jambo gumu sana kuweza kuliruhusu kuingia katika ubongo wake.
 
Wazo la kwanza kumjia kichwani mwake ni mtu gani ambaye anaweza kulifanya tukio la kumfanya Shamsa kupotea, moja kwa moja mawazo yake yakaangukia kwa Mzee Godwin.
 
‘Godwin Godwin, mmmmmmm’
Alisemea kimoyo moyo huku nafsi yake moja ikimkatalia kwa nguvu zote kwamba Mzee Godwin hausiki katika tukio hilo la Shamsa kupotea. Wazo la pili ni simu ambayo Shamsa alimletea chumbani majira ya mchana. 

Kwa haraka akafumbua macho yake na kuanza kupandisha ngazi kwenda gorofani na kuwaacha walinzi wake wakishangaa kwa nini bosi wao amekurupuka na kukimbilia juu gorofani mmoja wao akataka kwenda ila mkuu wake akamzuia asimfwata, cha msingi watawanyike kwenda kumtafuta Shamsa, hata maeneo ya nje ya jumba hilo.
 
Eddy akaichukua simu aliyo pewa na Shamsa akaanza kupekua upande wa picha, katika simu hiyo na kuioa sura ya Lube mmoja wa walinzi wa Raisi Praygod Makuya. Hapo ndipo picha ikaanza kumjia kichwani mwake, akaanza kujaribu kutengeneza matukio ya jinsi Shamsa alivyo weza kuichuku simu hiyo, jibu likamjia aliichukua kwa nguvu na si kwakuomba. 

Kumbu kumbu ya mguno wa mtu kama kupigwa ukamjia kwenye mfumo wa akili zake. Kwa haraka akatoka nje na kusimama mlangoni kwake, akalitazama eneo hilo kwa umakini akaona baadhi ya mikwaruzo kwenye ukuta. 
 
     Macho yake akayatupia tena kwenye mlango wa kuingilia chumbani kwa Shamsa, taratibu akapiga hatua hadi ndani ya chumba hicho. Akakuta jinsi vitu vilivyo changuka, ikionekana Lube alibananishwa kwenye chumba hicho.
‘Alimuachia’
Eddy alijisemea, huku akiutazama mlango wa Shamsa, kwani hapakuwa na tone lolote la damu ndani ya chumba hicho akiamoni kwamba Lube hakuweza kujeruhiwa na Shamsa.
 
“Huyu ndio atanieleza mwanangu yupo wapi?”
Eddy akatoka na kurudi chumbani kwake, akachukua moja ya funguo ya gari lake, kabla hajatoka akaiona bastola aliyo kuwa ameishia Shamsa, akaiikota chini, akaitazama na kukuta risasi za kutosha. Akashuka hadi sebleni ila hakukuta mlizi hata mmoja. 

Moja kwa moja akaelekea kwenye maegesho ya magari yake, akaingia kwenye gari yake aina ya Verosa na kuondoka nyumbani kwake akidhamiria kwenda Ikulu kumbananisha raisi ili azungumze ni wapi alipo mficha Shamsa wake.
                                                                                                 ***
     Kwa usiri mkubwa raisi Praygod akapanga kikosi cha walinzi wake wanne anao waamini, akiwemo Lube, wahakikishe wanamtia nguvuni waziri Eddy. Ambaye tayari amesha anaza kumlia utamu wake wa kitandani(Rahab). Kazi hiyo raisi Praygod aliwaagiza vijana wake wafanya chochote wawezalo ila sura zazo, zisiweze kuonekana kwani itakuwa ni kasfa mbaya kwa wananchi, ambao wanajiandaa kwenda kwenye uchaguzi wa awamu yake ya pili.
 
“Kuna kitu kama sikielewi kwa meheshimiwa”
Samson alizungumza baada ya kukutana na Rahab kwenye moja ya bustani iliyomo ndani ya ikulu
“Mbona unazungumza hivyo?”
“Kuna watu amewaagiza kwa Eddy, sasa sijajua kama dhamira yao ni nzuri au mbaya”
 
Maneno ya Samson yakamstua sana Rahab, akajaribu kuvuta hisia zake, akawaona Eddy akiwa barabarani akija katika eneo la ikulu, huku akioenekana akiwa katika hali ya kukasirika sana.
“Samson chukua gari uwafwatilie hao vijana na kila kitakacho endelea ninakuomba unifahamishe”
“Sawa Madam”
Samson akachukua gari na kuondoka eneo la ikulu akifwata amri ya Rahab. Lube akiwa barabarani na wezake, wakapishana na gari aina ya Verosa na macho yake yakamshuhudia ni Eddy ndio aliyomo ndani ya gari hiyo.
”Geuza geuza mshenzi tumepishana naye”
 
Lube aliumuamrisha dereva, akafunga breki za gafla huku akiigeuza gari hiyo kwa utaalamu mkubwa, hadi wezake ndani ya gari hiyo wakashangaa. Kwa uwezo wa gari yao kubwa aina ya VX V8, ikawa ni rahisi kuweza kuifukuzia gari hiyo ya Eddy. Waliyo ipita kwa kasi na kuikatizia kwa mbele na kumfanya Eddy kufunga breki za gafla na kusimama.
Lube na wezake wakavaa vinyago vyao vilivyo wabakisha macho tu, wakashuka kwenye gari yao, huku wakimtazama Eddy aliyomo ndani ya gari akijishauri nini cha kufanya. 
 
‘Hawanijui hawa’
Eddy alizungumza huku akishuka kwenye gari bastola yake akiwa ameichomeka kwa nyuma.
“Nyinyi ni wakina nani?”
Eddy aliwauliza huku akijiweka sawa kwa lolote litakao kwenda kujitokeza, ukimya wa barabara hiyo inayo elekea ikulu na majira haya ya usiku iliwafanya Lube na wezake kuweza kuilisikia swali hilo walilo ulizwa. Hapakuwa na aliye jibu zaidi ya wao kuanza kujitawanya na kumzingira Eddy na kumuweka kati tayari kwa kumshambulia.

==> ITAENDELEA
 
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com  
Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts