Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 29 & 30 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 29 & 30 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Sunday, February 12, 2017 | 10:17:00 AM

ILIPOISHIA
“Muheshimiwa kama ni ushahidi basi hiyo kazi niachie mimi, nitahakikisha nay eye tunamfanya kama tulivyo mfanya baba yake”
 
Wote watano akiwemo raisi Praygod wakajikuta wakitabasamu wakiamini mpango wao umekwenda sawa sawa, lakini yote yaliyo kuwa yakiendelea ndani ya ofisi hiyo Rahab aliweza kuyasikia, hii ni baada ya kuingiza kinasa sauti kwenye suti ya mumewe pasipo yeye kujijua wakati akiwa anamuandaa wakati wa asubihi akielekea kwenye kikao hicho na washauri wake. 

Rahab akatabasamu huku akiitazama simu yake aliyo iunganisha moja kwa moja na kinasa sauti hicho. Akaachia tabasamu na kujiapiza washauri wote wa ofisi ya mume wake ni lazima wafe kwani wanataka kuipoteza furaha yake ambayo ni Eddy Godwin.

ENDELEA
***
Taarifa ya Eddy kujiuluzu katika nafasi yake ya uwaziri wa ulinzi, iliwashangaza sana wananchi wengi wa Tanzania, kila kona ya Tanzania watu walizungumza maneno yao, wengine wakimlaumu ni kwanini amefanya hivyo. 

Baadhi ya watumishi katika jeshi, wakajikuta wakiumia mioyo yao kwa kiongozi huyo waliye tokea kumpenda kutokana na utendaji wake wa kazi na kutetea masilahi yao ambayo mara nyingi huwa yanacheleweshwa sana katika kuyapata.
 
Simu ya mzee Godwin ikaingia ujube wa video, kwa haraka akaifungua video hiyo, akaanza kuitazama jinsi Eddy anavyo jiudhuru katika nafasi ya uwaziri jambo lililo mstua sana.
 
“Baba ni nini?”
Manka alimuuliza, huku akimtazama usoni mzee Godwin
“Eddy amejiudhuru uwaziri”
“Ana maana gani ya kujiudhuru”
“Hakuna anaye fahamu”
Safari yao ikachuku masaa kadhaa hadi wakafika katika nchi ya Mexco kwenye makao makuu ya kambi yake. Wakapokelewa na John akliwa na wapambe wengine. Kama kawaida wakampa heshima Mzee Godwin ambaye ndio mmiliki wa ngome nzima. 
 
“Muheshimiwa kila kitu kipo sawa”
“Kazi nzuri nahitaji uitishe kikao sasa hivi”
“Sawa muheshimiwa”
Wote wakaingia kwenye magari ya kifahari, yaliyo wapeleka mpaka kwenye jumba kubwa la kifahari waitokea kwenye uwanja wa ndege mdigo ulipo kwenye ngome hiyo. Kikao cha dharura kikaitishwa, mzee Godwin akakutana na wanajeshi wake wengi wakiwa ni waasi katika nchi zao walizo toka, ambao idandi yao ni sawa na watu elfu hamsini.
 
Nacho ya Mzee Godwin kila anavyo watazama wanajeshi wake hao walio jipanga mitsari iliyo nyooka, moyoni mwake akajihisi nguvu ya ajabu, kwani taratibu malengo yake yanazidi kuongezeka siku hadi siku. 

Agnes na Jaquline nao ni miongoni mwa wanajeshi walio panga mtari katika kundi la wanajeshi wa kike katika kiwanja kikubwa ambacho mara kwa mara hutumika kama makutano ya wote pale kiongozi wao mkubwa anapo hitaji kuzungumza nao.
 
“Destinatio of our enemies oyeeeeeeeeeeeeee”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti kubwa na yenye ukakamavu wa hli ya juu, wanajeshi wake wote wakitikia kwa sauti ya juu huku, wakinyoosha mikono yao ya kushoto juu huku ikiwa na kofia wanazo zivaa. Mzee Godwin akarudia tena salamu hiyo, na wanajeshi wake wakajibu kama walivyo jibu mara ya kwanza kwa sauti za juu.
“Nimerudi, sasa ni mwendo wa kuhakikisha kwamba kikosi  chetu kinakua zaidi ya hapa”
 
“Mishahara ya kila mmoja wenu kuanzia mwezi huu, itaongezeka mara mbili ya jinsi anavyo lipwa”
“Sinto hitaji uzembe kati kazi yoyote ambayo itapangwa, umakini uskivu na uwajibikiaji ndio ngao yetu”
“Kiongozi wenu nipo salama kama mulivyo sikia kwamba ninatafutwa inchioni Tanzania, ila kwa uwezo wangu ninamshukuru Mungu nipo salama”
Mzee Godwin akanyamaza kidogop huku akiwatazama wanajeshi wake jinsi walivyo simama kwa uimara wa hali ya juu.
 
“Munaweza kutawanyika na kurudi kwenye shuhuli zenu”
Wanajeshi hao wakatawanyika kila mmoja akaendelea na majukumu yake ambayo wanayafanya katiaka ngome hiyo, huku wengine wakijihusiha na utengenezaji wa madawa ya kulevya aina ya Cocein, jambo linalo ifanya ngome hiyo kuzidi kutajirika siku hadi siku, wengine kazi yao ni kufanya kazi za uhalifu, kuvamia watu matajiri, mabenki makubwa, yote ni kujitahidi kuweza kuingiza kiasi kikubwa cha pesa ili huduma zao ziweze kusonga mbele. 

Wengine kazi zao ni kutengeneza silaha za kivita zenye ubora wa hali ya juu. Wengine kutengeneza ndege za kivita pamoja na magari ambayo yana uhimara mkubwa sana katika swala zima la kupambana. 

Kusema ukweli kambi ya D.F.E imakamilika kila idara, kila mmoja aliutumia ujuzi wake katika kuhakikisha kwamba maisha yake ndani ya ngome hiyo yanakuwa ni bora zaidi ya mwanzo alipo tokea.
“General kuna wageni wawili ambao tuliweza kuwaongeza kipindi haupo”
John alizungumza mara baada ya kufika katika ofisi ya mzee Godwin
 
“Kina nani?”
John akamnong’oneza mpambe wake aende akawaite Agnes na Jaquline, akafanya hivyo. Mzee Godwin akatumia fursa hiyo kuwatambulisha Tom na Manka kwa John. Baada ya dakika chache mpambe waka akarudi akiwa ameongozana na Agnes pamoja na Jaquline. Wasimama kwa heshima mbele ya Mzee Godwin huku mikono yao ikiwa nyuma. John akaanza kuwatambulisha kisha akaanza kutoa maelezo ya jinsi walivyo weza kuwapata wasichana hao, ambao wanatafutwa na serikali ya nchini Marekani.
 
“Jisikieni huru mabinti, hapa ni kama nyumbani kwenu, chochote mutakacho kihitaji basi musisite kuzungumza nasi, mimi au huyo bwana mdogo”
 
“Asante general”
Walijibu kwa pamoja, kwa heshima kubwa pamoja na unyenyekevu, kwani tayari walisha anza kuyazoea maisha ya humu ndani.
“Mimi nina ombi”
Jaqulie alizungumza kabla Mzee Godwin hajafungua kinywa chake
 
“Ombi gani?”
“Ili kuweza kuimarisha ngome hii, nimejaribu kutazama mafunzoi yanayo tolewa kila siku, ila kuna mafunzo ya uninja ambao sote wawili tunayo, hapa hayafundishwi, naoana ni vyema tukanza kuyafundisha”
“Ahaa hilo tu nawapeni ruhusa, tena itakuwa vizuri mukianza na huyu mjukuu wangu Tom”
 
“Hata mimi baba nahitaji”
Manka alizungumza huku akitabasamu
“Sawa tena huyu munatakiwa kumpa tizi la uhakika kwa maana amekuwa mzembe sana”
“Asante muheshimiwa kwa kukubali kwako”
“Musijali munaweza kwenda”
Watu wote wakatoka ofisini na kuwaacha John na mzee Godwin kuzungumza mambo mengine ya muhimu wanayo yafahamu wao wenyewe.
 
“General madam Mery yupo wapi mbona hujarudi naye?”
“Ameungana na Eddy”
Jibu la Mzee Godwin likamstua sana Joihn na kujikuta akimtumbulia macho mzee huyo kwani anamfahamu vizuri sana Eddy, akiamua lake huwa anaamua hata liwe jambo la kuhatarisha maisha yake basi atafanya hivyo ili mradi aweze kufanikiwa. Swali la kwanza alilo jiuliza endapo Eddy atagundua kwamba yeye yupo hai itakuwaje, swali hilo halikupata jibu zaidi ya kujifajiri atajua mbele ya safari
                                                                                                   ***
“Eddy kwa nini umejuzulu?”
“Sikia Samson, katika serikali hii nina maadui wengi sana, na nikiwa katika kiti cha uongozi sinto weza kufanya kazi yangu vizuri. Nahitaji kurudi kuwa Eddy, Eddy yule niliye zoea mateso na machungu ya haya maisha”
 
“Ila huoni hivi itakuwa ni hatari sana kwako?”
“Natambu ila nikiendelea kuwa katika uongozi itakuwa ni hatari sana kwani D.F.E wananitafuta kulilo kitu chochote”
“D.F.E ndio nini?”
Swali la Samson likamfanya Eddy kumtazama Samson usoni, hapo ndipo alipo amini kwamba D.F.E bado ni chama cha siri sana na hakijajulikana kwa watu wengi ndani ya Tanzania
 
“Usijali nitakuambia”
Wakiwa ndani ya handaki, wakasikia mngurumo wa gari kusimama, ikamlazimu Samson kuanza kutoka ndani ya handaki hilo na kupanda juu, akiwa makini kutazama ni nani aliye fika katika eneo hilo. Akamkuta Rahab akiwa na mlinzi wake wa kike, wamesimama nje ya gari walilo jia, lenye namba sa usajili T288 DCS, ambayo si gari ya ikulu
 
“Karibu Madam”
“Asante Eddy yupo wapi?”
“Yupo chini huko”
“Nisubirini hapa”
Rahab akawaacha Samsonm na mlinzi wake wa kike yeye akshuka chini, ikiwa nio baada ya miaka mingi sana kupita tangu alipo ondoka ndani ya handaki hilo. Gafla akastukia ngumi nzito ilioyo mfwata, kwa wepesi wake akajikuta akiikwepa na kupita pembeni.
 
“Eddy ni mimi?”
Rahab alizungumza mara baada ya kumuona Eddy akijitokeza kwenye kona aliyo kuwa amejificha akihisi kuna uvamizi umetokea kwani hakumuona Samson kushuka sehemu walipo.
“Umefwata nini huku?”
“Eddy hata salamu”
 
“Nijibu kilicho kulete wewe huku ni nini?”
“Nimekuja kukuona mpenzi wangu”
“Rahba sinto hitaji kuwa na wewe tena, nahitaji kuishi maisha yangu. Huyo memwa wako amemteka mwanangu kisa ni wewe, huoni unazidi kuniweka mimi matatani?”
Eddy alizungumza kwa kufoka hadi Rahab akatulia tuli, akimsikiliza mwanaume huyo aliye anza kufura kwa hasira na taratibu kifua chake kikianza kujaa.
“Eddy……”
“Eddy nini, unahisi kwamba nitakuelewa kwa utakacho niambia eheee?”
“Nisikilize basi mpenzi wangu, nipo tayari kufanya chochote kwa ajili yako, ili mradi nisikupoteze wewe”
“Upo tayari eheee?”

“Ndio niambie mimi nitafanya”
“Niletee Shamsa mwanangu hapa, kisha ndio tutaendelea na mambo mengine”
“Sawa”
Rahab akajisogeza karibu na Eddy akataka kumpiga busu la mdomoni, ila Eddy akamzuia kukataa busu hilo.
“Fanya hivyo umenielewa?”
“Sawa mpenzi”
Rahab alijibu huku machozi yakimlenga lenga, akatoka ndani ya pango huku akiwa na hasira kali ni kwanini mume wake amefikia mbali hadi hatua ya kumteka binti asiye na hatia katika vita hiyo inayo endelea kimya kimya.
 
“Madam….”
Samson aliita baada ya kumuona Rahab akiwapita kwa hasira na kuingia ndani ya gari na kuubamiza mlango kwa nguvu, mlinzi wake akaingia kwenye gari na yeye, akakiweka vizuri kioo chake cha mbele kinacho muwezesha kuweza kumuangalia abiria wake wa nyuma, kwa mara ya kwanza akamshuhudia bosi wake akimwagikwa na machozi, hakuelewa ni nini kilicho mfanya atokwe na machozi.
“Muheshimiwa tunaelekea wapi?”
“Popote enmdesha gari?”
 
Mlinzi wake akabaki akiduwaa, kwani jibu hilo lilimfanya ashindwe kujua ni nini cha kufanya
“Prisca endesha gari unashangaa nini?”
Rahab alifoka kwa hasira na kumfanya Prisca kuwasha gari, akaligeuza na kuondoka katika eneo hilo, lililopo katikati ya msitu wenye miti mingi sana. Priscar akaamua kuelekea jijini Dar er Salaam, ikiwezeklana weende ikulu kabisa. 

Kutokana safari yao ilikuwa ni ya siri, pamoja na gari wanayo itumia haina usajili wa namba za ikulu, ikawalazimu kusimama kwenye foleni kama watu wengine wanavyo simama, huku akilini mwake Rahab akifikiria kumuonyesha mume wake jinsi uhatari wake ulipo pale anapo jaribu kuingia katika anga zake hususani anga za mapenzi
                                                                                                      ***
“Una itwa nani?”
Dulla alimiiliza binti aliye mpakiza kwenye gari lake kwa mara ya pili wakiwa katika foleni ya mataa maeneo ya Ubungo maji.
 
“Jina langu halite kusaidia chochote”
Shamsa hakuhitaji kumuamini Dulla moja kwa moja kwani wasiwasi wa usalama wake bado anao. Wakiwa kwenye foleni pembeni yao gari nyeusi aina ya land cruser, ilisimama, huku vioo vyake vikiwa ni vyeusi, na si rahisi kwa mtu yoyote kuweza kuona ndani. Brian akiwa katika dibwi kubwa la mawazo ni jinsi gani anaweza kumpata Shamsa ambaye hajui ni jinsi gani ametoroka, kwani kwa dawa aliyo muwekea kwenye kitambaa alicho mziba puani, huwa inachukua hata masaa 48 kuweza kuondoka mwili mwa mtu na kumfanya azinduke katika usingizi mzito. 

Katika kupitisha pistisha macho yake kutazama huku na kule, pembeni yake akaona gari ndogo, ila katika kutazama vizuri akamuona Shamsa akiwa amekaa pembeni ya siti ya dereva, kijana ambaye hajawahi kumuona. Ili kuhakikisha kwamba ndio Shamsa anaye mtafuta ikalazimu kushushakioo kumtazama vizuri, hapo ndipo macho yake yakagongana na Shamsa, aliye achia tabasamu pana.
 
“Mlinzi wetu yule pale ngoja nishuke”
Ikambidi Dullah kumtazama mlinzi mwenyewe ni nani, alipo muona kumbukumbu kichwani kwake ikarejea haraka kwamba huyo ndio mlinzi ambaye aliye mteka Shamsa, ambaye tayari amesha fungua mlango kwa ajili ya kushuka.
“Noo usiendeeeeeee”
 
Dulla alizungumza huku akimuwahi kumshika mkono Shamsa, na alipo geuka kumtazama mlinzi huyo, akakuta akiwa amenyooshewa bastola ya uso, huku mlinzi huyo akimueleza kwa ishara ya mdomo amuachie Shamsa aondoke naye.

   SORRY MADAM (30)(Destination of my enemies)

 “Unatatizo gani wewe Dulla?”
Shamsa aliuliza kwa sauti ya ukali, huku akichungulia kwenye gari kumtazama Dulla aliye mshika mkono. Brian akairudisha bastola yake haraka, kitendo ambacho Shamsa hakuweza kukiona. 
 
“Shamsa huyo jamaa ndio aliye kuteka wewe”
Gari za mbele yao zikaanza kuondoka taratibu, Shamsa akafunga mlango huku akiwa na wasiwasi mwingi, akilitazama gari la Brian walilo liacha nyuma kidogo. Wakakunja na kuelekea njia iendayo Mwenge, ikamlazimu Brian na yeye kujichochomeka kwenye magari yanayo kunja kuelekea mwenge, nusu asababishe ajali ila hakulijali sana jambo hilo. 
 
“Una uhakika kwamba ndio yeye aliye niteka?”
“Ndio ninauhakika, ndio yeye siwezi kukudanganya nilimuona kwa macho yangu mawili, akikuteka”
Shamsa akatazama nyuma huku akitazama kama gari ya Brian inawafwata, hakuweza kuiona kwani nyuma yao kuna gari ya abiria iendayo Kawe.
 
    Wakafika maeneo ya Mlimani City, wakaingia  kwenye eneo hilo na moja kwa moja akatafuta eneo lenye nafasi ya maegesho na kulisimamisha gari lao, Brian akiwa katika mwendo kasi, aliwashuhudia Shamsa na Dulla wakishuka maeneo ya mlimani City na kuingia ndani,
 
“Shittiiii………”
Brian alijikuta akiminya honi, kumuashiria dereva wa mbele alipishe gari lake huku macho yake akitafuta sehemu ambayo anaweza kuligeuza gari lake, akafanikiwa kufika kwenye eneo ambalo aliweza kuligeuza gari lake na kurudi katika eneo la mlima city huku akiwa  na hasira kali sana
“Humu ndani tutampoteza hawezi kutufwatilia huku”
Dulla alizungumza huku wakijichanganya katikati ya watu wanai ingia katika jengo kubwa hilo, Shamsa kazi yake ikawa ni kutazama kila eneo, kuona kama Brian anawafwatilia.
 
“Una simu hapo?”
“Ndio”
Brian akatoa simu yake na kumkabidhi Shamsa aliye minya minya baadhi ya namba na kuiweka simu yake sikioni. Majibu aliyo kutana nayo ni kwamba namba ya simu ambayo anaipigoa haipatikani kwa muda huo, akarudia tena kuipiga ila jibu likawa ni moja kwamba namba anayo ipiga haipitikani kwa wakati huo.
“Baba hapatikani”
“Hembu jaribu kumpigia tena inawezekana ikwa ni mtandao unasumbua”
 
Shamsa akajaribu kuipige tena namba ya Eddy ila haikuwa hewani, wakatafuta moja ya mgahawa na kutafuta sehemu iliyo jificha na kukaaa. Hapakuwa na aliye kuwa na hamu hata ya kuweka kitu chochote mdononi mwake.
“Ila unajua serikali ya Tanzania inavituko sana”
Kijana mmoja aliye kaa pemebi yao pamoja na na mwenzake alisikika akizungumza huku akiwa ameishika simu yake mkononi aina ya Samsung Note 3.
“Kwa nini?”
 
“Sijui ni sababu zipi zilipelekea hadi yule waziri wa ulinzi kujiudhuru hadharani”
Taarifa hiyo ikamstua kidogo Shamsa na kujikuta akiwatazama vijana hao kwa macho ya kuiba huku masikio yake akiwa moja kwa moja ameyeelekezea kwa vijana hoa.
“Serikali yetu bwana ina mambo, unajua jamaa alikuwa mkweli, inawezekana amaeona upuuzi unaoa endelea akaamua kujiudhuru”
“Niwasaidiea nini?”
Dada mmoja aliye valia sketi fupi huku kitambaa cha rangi nyekundu akiwa amekifunga kiunoni mwake, aliwauliza Shamsa na Dulla walio jikuta wote wakimtazama.
 
“Mimi mimi maji”
Dulla alibabaika kujibu swali hilo jepesi, dada huyo alimtazama Shamsa akisubiria kulipata jibu lake
“Dada na wewe nikuletee nini?”
“Juisi yoyote”
Dada huyo aliandika kwenye kikaratasi chake kidogo na kuondoka, kwa mwendo wa kawaida, akafika sehemu ya vinjwaji, akatoa simu yake na kumpigia Brian.
 
“Bosi wapo hapa”
Maneno hayo yalitosha kabisa kumjulisha Brina ni wapi walipo  vijana anao watafuta. Brian akageuza mulekeo wake, akaenza kutembea kwa mwendo wa kasi kuelekea kwenye mgahawa, hata kabla hajafika kwenye mgahawa huo simu yake ikaita, ikaitoa mfukoni haraka haraka na kuipokea.
“Umefikia wapi?”
“Mkuu nipo mlimani City, ndio ninawafwatilia”
“Sasa kuna vijana wnafika hapo, kuna plani nimeipanga sasa wewe wasubirie”
“Plan, Plan gani muheshimiwa”
 
“Subiria”
Sauti ya mmoja wa viongozi waliopo ikulu ya raisi praygod ilisikika kwenye simu ya Brina, kisha ikakatika, Brian akajikuta akiwa amesimama huku akiwa hafahamu ni nini cha kufanya.
“Ina maana baba yangu amejiudhuru?”
“Baba yako yupi?”
“Waziri Eddy”
“Ina maana waziri Eddy ni baba yako?”
“Ndio”
Dulla akabaki akiwa amemtumbulia macho Shamsa, huku akiwa kama haamini fulani kwamba Shamsa ni mtoto wa waziri Eddy.
 
***
   Hali ngumu ya mateso makali ikazidi kuongezeka siku hadi siku kwa kina Fetty na wezake wawili, manyanyaso ya kupigwa shoti za umeme pamoja na sindano za maumivu makali zilifanyika mara kwa mara wakiwa ndani ya gereza. Yote hayo walihitajika kuweza kusema ni wapi ilipo ngome yao ya walio kuwa wakiwatumikia.  Hapakuwa na mtu aliye weza kusema lolote si Fetty, Halima wala Anna. 
 
Afya zao siku hadi siku zikazdi kuzorota kwa mateso hayo makali wanayo yapata, kila mmoja alijiapiza moyoni mwake ni bora kufa kuliko kusema ni wapi walipo kuwa wakitokea isitoshe, kila mmoja tayari alisha pata mateso yakutosha.
Ulinzi mkali ulizidi kuwekwa dhidi yao, hadi vyumba vya kulala kila mmoja aliweza kuingizwa kwenye chumba chake tofauti ambacho kina kamera ya ulinzi inayo mmulika masaa yote atakapo kuwa ndani ya chumba hicho.
 
Hapakuwa na mwana harakati aliye weza kutokea kuzitetea haki zao, kwani manyanyaso yalipita kikomo. Mpango wa kuwahamisha katika gereza hilo na kuwapeleka katika gereza jengine, lenye mateso makali kupindukia ukaanza kupangwa taratibu, kikosi cha FBI, kikiwa kinahusika katika kusimamia kusafirishwa huko kwa waalifu watuta wambao wanasadikika ni kati ya wale walio husika katika kifo cha waziri wao wa mambo ya nje bwana Paul Henry Jr.
“Ni lini wana hamishwa gereza”
Agnes aluliza kwa shahuku kubwa mara baada ya kusikia taarifa hiyo kutoka John.
 
“Siku maaalumu bado haijapanmgwa, ila kuna watu wentu wanaendelea kulifwatilia hilo swala kuhakikisha wanatupa taarifa kwa kila jambo ambalo litaendelea ndani ya gereza hilo”
“Ila wanasafirishwa kwa usafiri gani, kutokana wao wapo katikati ya kisiwa”
Jaquline aliuliza huku akimtazama John usoni
“Hapo kweli ndipo hata sisi tunapo takiwa kuwa makini napo, kufahamu siku ambayo wanasafirishwa peke yake haitoshi kujifariji kama tunaweza kuwaokoa”
 
John akamuamuru mpambe wake ambaye muda wote anatembea naye kuwapa baasha ya kaki Agnes na mwenzake kutazama baadhi ya picha zilizopo ndani ya bahasha hiyo. Kila picha ambayo Agnes aliitazama akajikuta machozi yakimwagika kwa wingi, wezake hao walio kuwa mabinti warembo wa kuvutia sana, wamechakaa kiasi cha kuonekana kama vizee omba omba sana. 

Nywele zao na miili yao ilizidi kudhohofika na kuwa wembama sana, mithili ya watu ambao ni wagonjwa sana. Kwa hasira Agnes akajikuta akikunja moja ya picha ya Halima, aliye chakaa kupita wote, kisha akaondoka kwa hasira huku akilia, Jaquline naye akaondoka kwa haraka kuelekea alipo kwenda Agnes
                                                                                                ***
“Sasa unahisi madam anaweza kufanikisha kumpata mwanao?”
“Natambua anaweza kumpata mwanangu, kutokana mume wake yeye ndio aliye nyuma ya tukio zima hili”
 
Samson akabaki kimya hakuwa na swali jengine kwa Eddy, aliye kaa kwenye kiti pembezoni mwa computer zilizomo ndani ya handaki hilo. Eddy akaendelea kuperuzi peruzi kwenye mtandao, habari ya yeye kujiudhuru ndio habari inayo zungumziwa kwa sana katika mitandao mingi ya kijamii. Gafla sura yake ikaanza kubadilika, huku akiikazia macho cumputure hiyo akisoma habari ambayo ameiona kwa wakatia huo katika moja ya ukurasa wa kituo kikubwa cha habari.
“Samson njoo uone”
Samson kwa haraka akasogea eneo ambalo yupo Eddy, kitendo cha yeye kuisoma taarifa hiyo naye sura yake ikabadilika na kujikuta akishangaa
                                                                                                   ***
   Moshi mkali wa gesi na unao nuka vibaya ukaanza kusambaa ndani ya jengo kubwa la kibiashara la Mlimani City. Milio ya risasi ikaanza kurindima kila mhala jambo lililo wafanya wananchi wengi walio kuwemo ndani ya jengo hilo kuanza kutawanyika huku wakipiga kelele, na kila mmoja akijitahidi kuyaokoa maisha yake.
 
Amri moja ikatolewa watu wote walale chini ya sakafu huku mikoo yao ikiwa kichwani, na wananchi nao wakafanya hivyo kwani aliye kuwa mbishi katika hilo aliambulia kupigwa risasi hadi kufa. Watu wapatao ishirini walio valia nguo nyeusi pamoja na vitambaa vyeusi usoni mwao vilivyo wabakisha macho, walitawanyika  na kulizunguka eneo zima la jengo la Mlimani City, wakiwa na silaha nzito mikononi mwao. Polisi pamoja na walinzi wote walio kuwepo katika jingo hilo waliuawa kikatili. wengine walichinjwa na wengine walipigwa risasi za vichwa na kupoteza maisha yao.
 
Vijana wawili wakamtafuta Brian alipo wakamnyanyua mzoga mzoga hadi kwenye moja ya vyoo, kisha wakavua vitambaa vyao usoni.
“Samahani muheshimiwa mimi ninaitwa Ahemed”
“Mimi ninaitwa Briton, ndio viongozi wa kundi hili, tuliingia jana usiku hapa Tanzania tukitokea Somalia, sisi ni miongoni mwa wafuasi wa D.F.E, tukishirikiana na Al-Shabab”
 
Hapo ndipo Brian akatambua maana ya simu aliyo pigiwa na kiongozi wake kutokea ikulu
“Kazi nzuri vijana, sasa mpango ni upi unao endelea kati yenu”
“Ngoja tukuonyeshe”
Briton akapiga simu ya upepo kwa jamaa anaye itwa Lukuma, wakamuelekeze sehemu walipo, ndani ya dakika tatu jamaa akwa ameingia kwenye vyoo hivyo na kukutana na wezake. 
 
“Vua kitambaa chako muheshimiwa akuone”
Lukuman akafanya hivyo, Brina akajikuta akimshanga sana Lukuma.
“Huu ndio mpango wetu kwa sasa”
Briton alizungumza huku akimruhusu Lukuman kuvaa kitambaa chake. Wakatoka na Brian wakijifanya kama wamemshikilia mateka moja kwa moja wakaelekea kwenye chumba cha kamera za ulinzi za jengo zima ambapo wezaowengine wawili tayari walisha waweka wafanyakazi wote ndani ya chumba hicho chini ya ulinzi.
 
“Unganisha tv zote za humu ndani zionyeshe viseo hii”
Briton alimuamrisha mmoja wa mafundi mitambo wanao shuhulika ndani ya chumba hicho, jamaa akaminya minya kwenye computer yake, Tv zote zilizomo ndani ya jengo zima zikawa zinaonyesha kitu kimoja tu, mistari mistari myekundu, njano, myeupe na bluu. 

Ahmed akavua begi lake dogo alilo kuwa amelivaa mgongoni akatoa kamera moja ndogo pamoja na vimuguu vya kusimamishia kamera hizo. Wakaiunganisha na mtambo unao ungoza tv zote ndani ya jengo la Mlimani City. Lukuman akasimama mbele ya kamera hiyo huku akiwa ameshika bastola,  kwa ishara ya vidole Briton akaanza kuhesabu moja hadi tatu, Lukuma akavua kitambaa cheka cha usoni.
 
    Kukohoa kwake kidogo kukawafanya baadhi ya watu kunyanyua vichwa vyao kutazama tv zilizomo kwenye maeneo yao, akiwemo Shamsa, aliye stuka sana kumuona Eddy kwenye Tv hizo, akionekana yeye ndio kiongozi wa kundi hilo lililo teka jengo zima la Mlimani City
 
“Baba…………………!!!”
Shamsa alizungumza huku akikinyanyua kichwa chake juu kabisha bila hata ya kuhofia ulinzi mkali walio wekewa, hapo ndipo alipo mfanya Dulla naye kunyanyua kichwa chake na kumuona waziri Eddy akiwa katika mavazi mengine ya kikazi zaidi tofauti na asubuhi alivyo kuwa amevaa, pale alipokuwa akitangaza kujiudhulu.
 
Vyombo vyote vya habari vikarusha tukio zima, ikiwa ni habari ya dharura(breaking news). Kwa kamera moja ya muandishi wa habari aliye kuwemo ndani ya jengo hilo na kujibanza kwenye moja ya kona pasipo kuonekana, aliitegesha kuelekea moja ya tv kubwa, na mawasiliano yakaruka moja kwa moja kwenye  kituao anacho kifanyia kazi, na kwakupitia video hiyo vituo vyote vya televishion nchini Tanzania vikawa vinaonyesha tukio hilo walilo liita la kigaidi, likiongozwa na waziri mstafu bwana Eddy Godwin, jambo lililo wastua wananchi wengi na kutambua maana ya waziri huyo kujiudhuru ndio hiyo.

==> ITAENDELEA
 
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com  


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts