Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 39 & 40 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 39 & 40 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Sunday, March 12, 2017 | 11:00:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
“Moja, hakikisha kwamba unaurudisha uhai wa Eddy Godwin”
“Mbili ndani ya masaa 48, Eddy awe amerudi madarakani la sivyo bomu hili litaisambaratisha ikulu yako”
Simu hiyo ikakata, huku video iliyo kuwa inaonekana kwenye tv hiyo ikapotea na kubakisha mwanga wa bluu wa tv hiyo kubwa, watu wote waliomo ndani ya ofisi
hiyo wakabaki wakimtazama raisi Praygod azungumze kitu juu ya hilo.

ENDELEA
Jasho jingi likazidi kumwagika raisi Praygod, hakuwa na jambo la kuweza kuzungunza na wala hakuweza kutambua ni wapi alipo Eddy.
"Muheshimiwa Eddy si amesha kufa sasa itakuwaje?"
Mmoja wa wafanyakazi wake walinuuliza
"Yupo hai"
Kila mmoja akabaki akiduwaa, baada ya kulisikia hilo swala, raisi alipo ligundua hilo akakohoa kidogo.
 
"Endeleeni na kazi"
Akatoka ndani ya ofisi yake na kuelekea katika eneo lake la kulala, kichwani mwake akazidi kujiuliza ni nani aliye weza kuufanya mchezo huo kwani wataalamu wake walipo jaribu kutafuta ni eneo gani simu hiyo ya vitisho ni wapi ilipo tokea hawakuweza kuipata. Kitu kilicho zidi kumuumiza zaidi ni wapi alipo kuwepo mke wake kipenzi Shamsa, kwani inasadikika tangu atoke jana majira ya asubuhi kutokana na taarifa aliyo pewa, hakuweza kurejea kabisa hadi majira haya ya asubuhi.
 
Akafungua moja ya droo yake na kutoa vidonge viwili na kuvimeza pasipo hata kunywa maji, akavisukumiza kwa mafumba kazaa ya mate kisha akasimama mbele ya kioo kikubwa kilichopo mbele ya chumba chake na kujitazama uso wake ulio jaa wasiwask, iliyo changanyikana na hasira kali sana.
 
"EDDY, EDDY, EDDY"
Raisi Praygod alizungumza huku jazba ikizidi kuongezeka kifuani mwake. Taratibu akakisogelea kitanda na kujilaza, huku akihema taratibu taratibu.
 
***
Mwanga mkali wa jua ukaanza kupenya kwenye macho ya mtubaliye lala kitandani huku mwilini mwake akiwa amebakiwa na boksa tu. Akajaribu kunyanyuka kitandani ila maumivu makali ya paja yakamfanya kurudi tena kitandani. Kwa sekunde kadhaa akatumia kuchunguza kufahanu ni wapi alipo, ila ikawa ni swali gumu sana Kwakwe kuweza kufahamu alipo, kwani chumba hicho kimetawaliwa na mitambo mingi ya kushangza. 

Kitanda alicho lalia pembeni yake kuna bomba lililo ning'inizwa dripu ya maji iliyo peleka mrija wake moja kwa moja hadi kwenye mkono wake wa kulia na kisindano kidogo kilicho weza kuunganishwa na mrja huo, kimeingia moja kwa moja kwenye mshipa wake wa damu.
 
"Hapa ni wapi?"
Alizungunza huku akijaribu kujikaza kunyanyuka, mguh wake ulio fungwa bandeji zilizo badikika rangi kutokana na dawa akiyo pakwa, ukazidi kumuuma. 

Akiwa katika kutazama tazama mlango wa chumba hicho kikubwa kinacho onekana kwamba kipo juu ya gorofa kubwa, ukafunguliwa. Akaingia mwanaume aliye valia koti jeupe pamoja na miwani kubwa kiasi. Katika kumtazama kwa haraka haraka ni lazima utagundua kwamba mtu huyo ni daktari.
"Karibu tena duniani Mr Eddy Godwin"
Mtu huyo mwenye asili ya kizungu izungumza kiswahili sahihi kilicho mshangaza hata Eddy mwenyewe.
 
"Wewe ni nani?"
Lilikuwa ni swali la kwanza la Eddy huku akimkazia macho daktari huyo aliye zidi kupiga hatua kumfwata katika kitanda alicho lala.
"Kuna hofu ya kuhofia, mimi ni rafiki yako wa karibu. Naitwa dokta William"
Alizungumza huku akigeuza geuza dripu linalo endelea kushusha maji kwenye miishipa ya Eddy.
 
"Unajisikiaje?"
"Nina maumivu kwenye mguu. Kwanza hapa ni wapi?"
"Hapa upo Mosscow Russia"
"Nilifikaje hapa?"
Eddy aliiza huku akizidi kumkazia macho daktari huyo kwani jibu lake tayari lilianza kumpa wasiwasi mkubwa.
"Nilikutoa Tanzania siju chache za nyuma. Niweza kukufwatilia wewe kwa ukaribu mkubwa hadi nikafanikiwa kukupata"
 
"Ulinijuaje mimi?"
"Nilikujua kupitia mama yako, alikuwa ni rafiki yangu wa karibu sana. Kiufupi mama yako alikuwa ni mwema sana kipindi nilipo kuwa nikiifanya kazi ya kuwafundisha madktari wa jeshi nchini Tanzania.
"Usiwe na shaka kwani Tanzania ni moja ya nchi niliyo ipenda sana na ni nchi ambayo viongozi wake baadhi ni wakatili sana wakiongozwa na raisi Praygod"
 
Eddy akastuka kusikia jina jilo, katika kumchunguza chunguza dokta William kwa haraka haraka akatambua kwamba ni mtu ambaye hakuwa na nia mbaya sana kwake japo hakuhitaji kuliamini hilo kwa asilimia mia moja.
"Nil stori ndefu sana mimi na Tanzania pamoja na viongozi wake na sasa nipo katika mpango wa kuhakikisha kwamba nina lipa kisasi kwa nchi hiyo."
 
"Kwa nini unahitaji kulipa kisasi?"
Dokta William akaivua miwani yake taratibu, kwa mbali machozi yakawa yanamlenga lenga, hakuhitaji kuzungumza kitu cha aina yoyote. Akaondoka na kusimama kwenye moja ya mashine inayo ongozwa na kompyuta aina ya Laptop. Akaanza kuiminya minya batani zake kwa mwendo wa kasi akionekana kuseti baadhi ya vitu katika mtambo huo. Kila alivyo zidi kuminya batani za kumpyuta hiyo asira dhidi ya Tanzania hususani raisi Praygod zikazidi kumpanda mara dufu.
***
 
Kwa mwendo wa boti waliyo kuwa nayo, haikuwasaidia sana kuweza kupasua mawimba makubwa ambayo yanaendelea kuikumba bahari ya hindi mara mwa mara. Upepe mkali na wenye nguvu wa kuyumbisha hata meli kubwa ulizidi kuirusha boti hiyo waliyo panda Shamsa na Briton kutoka upande mmoja kwenda mwengine.
 
Halo hiyo kikaifanya boti hiyo kuzima gafla, hofu ya kufa ndani ya maji ikaanza kumtawala Shamsa ambaye kwa Mara kadhaa alionekana kumkumbatia Briton huku akilia sana. Alihisi hakuwa na bahati ya kuishi jwani familia yake aliyo kuwa akiitegemea tayari ilisha fariki kuanzia Eddy hadi mtoto wake Junio.
 
"Bray tunakufa mpenzi wangu"
"No hatuwezi kufa, tusonge Mbele"
Briton alizungumza huku akiendelea kujitahidi kuhakikisha kwamba boti huyo inasonga Mbele. Bahari ikazidi kuchafuka, hats akari ambao walikuwa doria katika maji waka waliamriwa kughairisha msako huyo kwank hali ilitisha sana. Mvua taratibu ikaanza kunyesha jambo lililio zidi kuwachanganya Briton na Shamsa. Radi zikaanza kutawala kila kona. Gafla boti yao ikabenuliwa na kuzamishwa ndani ya maji, kila mmoja akaangukia upande wake. Hali ikazidi kuwa mbaya kwani radio, mawimbi Na upepeo vikazidi kuongezeka kadri ya muda ulivyo zidi kwenda ndivyo ikawa afadhali ya dakika moja nyuma.
 
Kila mmoja alijikuta akiwa katika upande wake, baridi kali ikazidi kuunynyasa mwili wa Shamsa, maumivu makali ya tumbo yakarejea gafla mwilini mwa Shamsa na kumfanya aanze kuishi wa nguvu, dakika kadhaa mbeleni akapoteza fahamu.
***
Hali ya usalama ikazidi kuimarishwa maeneo mbali mbaali ndanj na nje ya jiji la Dar es Salaam. Wanaanchi kupitia katika vyombo vya habari. Video, redio na magazetini raisi Praygod akatangaza hali ya usalama katika maeneo yote yanchi, akiendelea kuwahakikishia kwamba hakuto kuwa na jambo lolote bays litakalo weza kujitokeza. Wanaanchi pamoja na wafanya biashara wakarudi katika maeneo yao ya kazi.
 
Kitu kilicho zidi kimchanganya raisi Praygod ni wapi alipo mke wake kipenzi Rahab. Msako wa kuhakikisha kwamba mke wa raisi anapatikana ukazidi kuendelea. 

Kwa siku ya pili mfululizo hapakuwa na askari akiye weza kulaza kichwa chake kwenye kitanda chake kama ilivyo siku za nyuma. Kuanzia wakuu wa majeshi hadi waliopo ngazi za chini, kazi ikawa ni kuhakikisha kwamva mke wa raisi anapatikana. Hapakuwa na mtu mwenye wazo la kujua kwamba mke wa raisi yupo kwenye pango ambalo lilitumiwa Na waasi wanawake ambao kwa sasa baadhi yao wapo katika mikono ya wamarekani.
"Madam tutaendelea kukaa humu hadi lini?"
"Hadi siku ambayo nitaamua mimi kutoka ndani ya handaki hili"
 
"Ika utakuwa unampa wasiwasi muheshimiwa raisi"."Nalitambua hilo ila sinto hitaji kurudi ikulu hadi nihakikishe ninampata Eddy, iwe kwa kuua au kufanya lolote ni kuhakikisha kwamba tunampata Eddy"
Priscar hakuwa na kitu chochote cha kuzungumza zaidi ya kuyasikiliza matakwa ya bosi wake.
"Ila kuna kitu kimoja nahitaji tuweze kukifanya kwa pamoja"
"Kitu gani madam"
"Nilazima kuhakikisha kwamba tunapata pesa tena pesa ya kutosha"
 
"Kama ni pesa mbona mume wako anazo za kutosha?"
"Ndio anazo ila nitahitahi za kwangu, BOT ipo kwenye mpango wangu wa kuchukua pesa zote zilizomo ndani ya benki hiyo"
Rahab izungunza huku akiishika bastola yake, akiigeuza upande mmoja hadi mwingine, heshima ya kuwa mke wa riasi akaiweka kando na kuamua kurudi katika kazi yake aliyo kuwa akiifanya miaka kadhaa ya nyuma.
***
Mpango wa kuwahamisha wafungwa watatu, ambao wanachuliwa kama magaidi katika nchi ya Marekani. Ikawadia, vikosi vyabulinzi vilivyo kabidhiwa kazibya kuwatoa wafungwa hao ambao ni Fetty, Halima na Anna. 

Ulinzi mkali ukaimarishwa kuanzia kwenye helcoptar zao wakihakikisha kwamba hakuna jambo lolote ambalo litaweza kujitokeza. Helcoptar zipatazo sita zilizo jaa askari wa kikosi cha FBI, zikazidi kukizunguka eneo la kikosi, huku ndege moja kubwa inayo tumika kubeba wafungwa kuwatoa katika gereza hilo, ikawekwa tayari.
 
Ulinzi ndani ya gereza ukazidi kuimarika. Fetty, Halima na Anna wakawekwa tayari kwa kutolewa katika vyumba vyao maalumu walivyo kuwa wamefungiwa kwa kipindi chote hicho. Walifungwa pingu mikononi na kufungwa cheni ngumu kwenye miguu yao. 

Kila sehemu walipo pita wafungwa wezao waliweza kuwashangilia kwa jinsi wanavyo tolewa kwenye gereza hilo. Japo miili yao imedhohofika sana ika tayari walisha jijengea umaarufu mkubwa ndani ya gereza hilo. Hii nikutokana na msaada ambao mara kadhaa waliweza kuwapatia wafungwa wezao ambao mara kadhaa walikuwa wakionewa vikali wa wasichana wengine wababe ndani ya jengo hilo. 

Kabla hawajafikishwa nje kulipo na uwanja mkubwa sana wa ndege. Wakavalishwa vigunia vyeusi wakatolewa nje ya gereza wakiwa katika ulinzi mkali, wakizungukwa na askari walio jazatiti kila idara, ili kuhakikisha tu kwamba magaidi hao ambao ni tishio hawawezi kufanya kitu chochote cha ajabu.
 
Wakiwa njiani wakielekea kwenyebuwanja wa ndege katika eno hilo, gafla moja ya helcoptar ikalipuliwa hewani na kuwafanya askari na watu wote kustuka ni kitu gani kilicho tokea huku askari wapatao kumi na mbili, walio kuwa wakiwasindikiza Fetty, Halima na Anna, wakawazingira na kuwalaza chini huku mitutu yao ya bunduki wakielekezea juu na pande zote kutazama maadui wapo eneo gani.


SORRY MADAM (40) (Destination of my enemies)

Ukimya wa dakika kadhaa ukapita huku macho ya askari yakitazama jinsi helcoptar iliyo lipuka ikimalizikia vipande vipande kutua chini. Hapakuwa na askari aliye weza kutoka kwenye helcoptar iliyo lipuka, uangalizi wa kitu kilicho ipelekea helcoptar hiyo kulipuka ukazidi kufanyika kwa haraka na uamkini. Rada zote nje ya gereza zikaendelea kuangaza kila sehemu ya kona ya gereza hilo lililopo kwenye kisiwa ambacho hakina makazi ya watu zaidi ya gereza hilo pekee. 

Wakawasimamisha Fetty, Halima na Anna, wakaendelea kusonga mbele tena kwa mwendo wa kukimbia na si kutembea huku askari kadhaa wakiwa wamewashikilia kwenye mikono kuwasaidia kuweza kukimbia pasipo kuanguka kutokana hawaoni kitu chochote cha mbele. 

Wakawaingiza ndani ya ndege hiyo, kila askari akazidi kuimarisha ulinzi kuhakikisha ndegehiyo haishambuliwi kwani hali ya hatari imesha anza kutwala kwa kila mmoja. Gafla askari mmoja baada ya mwengine wakaanza kuanguka ndani ya ndege huku risasi za vichwa zikiwa ndio halali yao. Mianguko hiyo ikazidi kuwapa matumaini Fetty na wezake wakiamini anaye fanya msaada huo ni mtu ambaye amekuja kuwachukua.
***
Garim nyeusi aina ya BMW X5, ikasimama kwenye moja ya maegesho ya benki kuu ya Tanzania. Msichana mrefu iye ziweka nywele zake ndefu mgoilngoni. Miwani yake ya macho aliyo ivaa, imezidi kumpendezesha, mkoba wake mkubwa alio shuka nao kwenye gari unaashiria kwamba msichana huyo ni mtu mwenye uwezo wa kifedha. Suti ya rangi ya kaki iliyo mkaa vizuri mwilini mwake ikilichora umbo lake jembamba kiasi huku makalio madogo kiasi yakijitokeza kwa nyuma.
 
"Nimefika"
Msichana huyo alizungumza kwa sauti ya chini. Akaanza kupiga hatua kwa mwendo wa madaha, kila aliye muoana alibaki akimtumbulia macho hususani wanaume ikiwemo na askari kadhaa àmbao wanaendeleza ulinzi nje ya benki hiyo inayo heshimika kwa kiasi kikubwa ndani na nje ya Tanzania. Akakaguliwa kama kawaida ya watu wanao ingia ndani ya Benji huyo. moja kwa moja akaelekea katika dirisha la kuhudumia Wateja.
 
"Dada habari yako?"
"Salama nikusaidie mini?"
"Nahitaji kuonana na meneja sijui inawezekana?"
"Una ahadi Nate?"
"Kusema kweli hapana, ila kama unaweza kunisaidia nakuomba nionane nae"
Dada huyo akatazamana na muhudumu kwa sekunde kadhaa, kisha muhudumu huyo akanyanyua mkonga wa simu iliyopo pembeni yake, akaminya batani moja Na kumpigia meneja wake.
 
"Bosi kuna mgeni hapa dirishani anahitaji kuonana na wewe"
"Anaitwa nani?"
Kwa haraka dada huyo akaibana sehemu ya kinasa sauti kwa kutumia kiganja chake kisha akamuuliza swali binti huyo.
"Paulina Thomas"
"Anaitwa Paulina Thomas"
Meneja huyo taratibu akaigeukia TV kubwa ikiyomo ndani ya ofisi yake, akaiwasha na kutazama ni Paulina gani. Kamera ya ulinzi iliyopo kwenye dirisha hilo ilimchukua Paulina kwa nyuma.
 
"Muambie atazame camera nimuone"
"Dada hembu geuka utazame hiyo kamera"
Paulina bila ya wasiwasi akageuka, akaitazama kamera hiyo kwa dakika moja kisha akamgeukia muhudumu huyo.
"Muambie aingine"
Paulina akaruhusiwa kuingia ndani ya ofisi ya meneja wa BOT. Akakaribishwa na kukaa kwenye kiti. 
 
"Nikusaidie nini binti?"
Mzee huyo wa makamu alizungumza huku akiendelea kumtazama Paulina kwa macho ya matamanio sana. Paulina akatabasamu, akaiweka miwani yake sawa kisha akasimama, akafungua kifungo kimoja cha shati lake, maziwa yake yaliyo chora alama ya vii kutokana na sidiria yake kuyabana vizuri yakamfanya meneja wa benki kushusha pumzi nyingi za uchu, taratibu uume wake ukaanza kusimama taratibu ndani ya suruali yake.
***
Taratibu hali ya hewa ikaanza kutulia ndani ya bahari. Upepo ulio kuwa Mkali ukatulia, mvua pamoja na radi vikakata. Briton akaanza kutazama kila sehemu kumtafuta Shamsa ila hakumuona. Akaanza kumuita kwa nguvu ila hapakuwa na jibu lolote lililo weza kutokea katika juhudi zake za kumuita Shamsa. Wasiwasi mwingi ukaanza kumtawala hisia mbaya za Shamsa kufikwa na mauti zikaanza kumtawala. 
 
Akaanza kupiga mbizi huku na kule akiemdelea kumuita Shamsa ila hapakuwa na jibu, Machozi yakaanza mumwagika, akiwa katika kuendelea kumtafuta Shamsa, mwanga Mkali wa boti kama mbili, ukawa unakuja katika eneo ambalo yupo. Ndani ya dakika kadhaa boti hizo mbili zikawa zimemzunguka huku mwanga mkali wa taa kubwa za boti hiyo zikiwa zimemmulika. Amri mmoja iliyo tolewa na watu walio valia mavazi meusi huku wakiwa na bunduki mikononi mwao, ni Briton kutulia kama alivyo na akileta ujinga risasi zitauchangua mwili wake na itakuwa ni mwisho wa maisha yake.
 
***
Machozi yakaanza kumwagika Doktar William, kumbukumbu za mke wake lamoja na wanae wawili kuuliwa kikatili nyumbani kwake. Jinsi damu ya zilivyo kuwa zikiwamwagika wanae walio pigwa risasi za vichwa. Ndio jinsi alivyo zidi kuhisi kuchanganyikiwa.
 
"PRAYGOD NILAZIMA NIKUUE"
Maneno ya dokta William yalisikika vizuri masikioni mwa Eddy, akajiweka vizuri kitandani akatamani kuzungumza kitu ila mdomo wake ukawa mzito kiasi. Hakujua ni kwanini Dokta huyo anazungumza hivyo. 
 
Akashangaa kumuona dokta huyo akivuruga kila kitu kilichokuwa juu ya meza hadi laptop yake pia ilianguka chini.
"Agrhaaaaaaaaaaaaaa"
Dokta William izungumza huku akisimama kwa hasira macho yake yakimwagikwa na machozi mengi. Akamtazama Eddy kisha akatoka ndani ya chumba hicho kwa mwendo wa kasi na kumuacha Eddy akijiuliza maswali juu ya kitu gani kinacho endelea kati yake na raisi Praygod.
 
***
Kati ya askari kumi walio ingia ndani ya ndege hiyo ya wafungwa ni askari watatu tu ndio walibaki wakiwa wamesimama, huku wao ndio wakiwa wameifanya kazi hiyo ya kuwauwa wezao. Mmoja wao moja kwa moja akaelekea chumba cha marubani Wawili wanao irusha ndege hiyo.
 
"Munaweza kuendelea"
Sauti ya kike ilisikika ikiwaamrisha marubani hao ambao tayari mashime za ndege hiyo walisha ziweka tayari na zilikuwa zikinguruma taratibu. Nje ya ndege hapakuwa na mtu aliye weza kujua kitu kilicho endelea ndani ya ndege. Kila askari aliye baki nje ya ndege akawa na kazi ya kuhakikisha ulinzi unaendelea vuzuri katika eneo zima la gereza. Wengine waliendelea kuzima moto kwenye helicopter iliyo anguka. Ndege hiyo ikaanza kushika kasi taratibu. 

Dakika chache baadae tayari ikawa imesha iacha ardhi ya kisiwani na kuanza kupasua mawingu. Helicopter nyingine za kijeshi zilizo kuwana na kazi ya kuhakikisha inalinda usalama wa eneo zima katika tukio zima la kuwasafirisha wafungwa hao, zikaondoka na kurudi makao makuu ya FBI. Huku majibu ya uchunguzi kuhusiana na helicopter iliyo anguka zikidai kwamba ajali hiyo imetokea kutokana na itilafu katika katika injini yake. Ila hayakuwa ni majibu ya kumtosheleza raisi, akaagiza uchunguzi uzidi kufanyika.
 
Mstuko mkubwa ukawapata watu wote waliomo ndani ya ofisi ya makao makuu ya FBI. Mlipuko mkubwa wa ndege ya wafungwa, wanayo ifwatilia kupitia mitambo ya satellite ikawafanya kila mtu kubaki mdomo wazi. Vipande vidogo vidogo vya ndege hiyo vikazidi kuchanguka na kupotelea hewani na hapakuwa na mtu aliye weza kutoka ndani ya ndege hiyo.
***
Paulina akafungua kifunguo cha pili cha shati lake na kuifanya sidiria hake nyeupe kuonekana vizuri, maziwa yake yakajitokeza vizuri kifuani mwake, taratibu akaweka mikono yakemiwili kwenye meza. Macho ya meneja yakatua kwenye kifua cha Paulina.Hapakuwa na mtu aliye zungumza zaidi ya meneja kutetemeka kwa hisia kali za mapenzi. Meneja akameza tena fumba la mate, akatamani kuusogeza mdomo wake hadi kwenye maziwa ya Paulina ila akasita kidogo. 
 
"U...uuu unata..ka nini binti"
Meneja alibabika huku akianza kumwagikwa na jasho la mabaha mwilini mwake, akazidi kuibana miguu yake kuuzuia uume wake usizidi kugombana na nguo yake ya ndani.
 
"Unajua nini nataka"
Paulina akafungua kifungo cha tatu cha shati lake, maziwa yake pamoja na tumbo lake vikaonekana vizuri. Paulina akauchukua mkono wa kulia wa meneja na kuukandamiza kifuani mwake, akamshikisha maziwa meneja, akabaki akiwa ameduwaa huku akihema. Gafla Paulina akamshika meneja Shingo yake, akamgandamiza kichwa chake kwenye meza kwa nguvu na kumuachia. Paji zima la uso wa meneja likawa linavuja damu nyingi na kumfanya atoe kilio cha maumivu.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts