Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 47 & 48 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 47 & 48 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Saturday, April 8, 2017 | 11:42:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Rahab akamtazama raisi Praygod na kumkumbatia, wote wakajikuta wakimwagikwa na machozi, jambo lililo wafanya makachero wengine kuwa katika hali ya simanzi iliyo changanyikana na furaha. 

Gafla Rahab akaanza kuisikia milio ya risasi masikioni mwake, alipo nyanyua kichwa chake akawaoa makachero walio mpiga risasi kwenye handaki. Macho yake gafla yakabadilika na kuzidi kuwa mekundu,  akamsukuma raisi Praygod pembeni na kumrukia kachero mmoja aliye mpiga risasi, akambwaga chini na kuanza kuliminya koo la kachero aliyeanza kutapatapa akijitahidi kuutoa mkono mmoja wa Rahab ulio mkaba shingoni

ENDELEA
  Kwa haraka makachero wakaanza kumtoa Rahab juu ya mwili mwa kachero anaye kabwa koo. Japo ni wanaume wa nguvu ila kijasho kilianza kuwamwagika kutoka na jinsi Rahab anavyo washinda nguvu.
 
Zoezi la kumtoa Rahaba likafanikiwa. Japo kachero aliye nusurika kuyaonja mauti hali yake kidogo ni mbaya. Hapakuwa na mtu aliye weza kuelewa ni kitu gani ambacho kimepata mke wa raisi. Kila mmoja akatokea kumuogopa sana Rahab, hata raisi Praygod mwenyewe hakusubutu kumsogelea karibu mke wake.
 
 “Madam”
Priscar aliita kwa mara nyingine tena ila safari hii hakudhubutu kusogea karibu na Rahab, aliye geuza shingo yake na kumgeukia na kumtazama. Gafla Rahab akapoteza nguvu za miguu na kuanguka chini, akapoteza fahamu.
 
 ***
Japo Eddy ana uwezo wa kupambana ila si kwa idadi kubwa ya vijana wa Kijapan walio mzinguka na kumuweka kati huku kila mmoja wao akiwa na silaha ya kisu mkononi mwake.
 
Vijana hao wanao onekana ni wahuni wa mtaani wakatulia wakimtazama Eddy, huku baadhi yao wa nyuma wakianza kumpisha kiongozi wao akisogea mbele taratibu. Kiongozi wao ni jitu moja refu lililo jazia misuli kifuani mwake pamoja na mikononi, kwa kimo cha Eddy anamfikia mtu huyo maeneo ya kifuani na kumlazimu Eddy kunyanyua sura yake juu ili kuweza kumtazama vizuri mtu huyo.
 
“Wewe ni NSS(Nation Securty Service)?”
Kiongozi wao huyo alimuuliza Eddy kwa kingereza, huku likikunja kunja vidole vyake vilivyo komaa.
“Hapana”
“Umefwata nini wewe mbwa mweusi?”
Eddy akatabasamu kisha akapiga hatua moja mbele kulisogelea jitu hilo karibu kabisa na sehemu alipo simama.
“Nimekufwata wewe mbwa Malaya wa kike”
“Nini……..!!!”
Jibu hilo likamkasirisha jamaa huyo, akamshika Eddy maeneo ya mabegani, akamnyanyua juu kama futi tano na kumsukumia chini. Wapambe wake wakataka kumvamia Eddy ila likawazuia ili apambane mwenyewe.
 
Eddy akapunguza uzito wa koti alilo livaa, akabakiwa na tisheti nyeusi iliyo mbana vizuri mwilini mwake na kulichora vizuri umbo lake la mazoezi. Akarudi hatua mbili nyuma, akavuta kasi ya kulivamia jitu hilo. Hata kabla hajalifikia akarudishwa na teke zito la kifua lililo mrusha kurudi alipo toka.
Wapambe wa jitu hilo hawakusita kushangilia kwa kitendo alicho kifanya mkuu wao. Eddy akajizoa zoa chini alipo anguka akajipanga tena kwa mashambulizi, akalitazama jitu hilo kuanzia chini hadi juu, kisha akakunya ngumi na kujiweka sawa.
 
Jitu hilo likaanza kurusha makonde ambayo Eddy alijitahdi kuyakwepa kwa maana endapo konde moja kitampata mwilini mwake ni sawa yeye akimpiga jitu hilo ngumi sehemu moja ya mwili si chini ya kumi tena mfululizo.
 
Kadri jinsi jitu hilo lilivyo zidi kurusha ngumu ndivyo jinsi Eddy alivyo zidi kujitahidi kumkwepa hadi jitu hilo likaanza kuchoka, na jasho jingi likaanza kumwagika. Ikawa ni kazi kwa Eddy kujipatia maujiko kama wasemavyo watoto wa mtaani. Kwa maana alizitambua sehemu zenye udhaifu kwa jitu hilo. Ngumi iliyo komaa kwa mazoezi makali ya miezi mingi ya nyuma, ikaanza kutua kwenye viungio vya mikono vya jamaa huyo. 
 
   Kila lilipo jaribu kurusha ngumu ili mradi amfikie Eddy, ila ndivyo jinsi lilivyo zidi kupiga sehemu ya viungio vya mikono yake hadi ikafikia hatua likashindwa kabisa kurusha mikono yake. Likamlazimu kutumia mateke, ila hali ikawa ni hiyo hiyo, kila alipo rusha teka basi alijikuta akipigwa teke kwenye viungio vya miguu yake, taratibu likaanza kuyumba. Wapambe wake wakajikuta wakikaa kimya wengi wao wakiwa hawaamini kwamba kiongozi wao ndio huyo anaye pigika kama mtoto mdogo. Kwa mwili mkubwa wa jamaa hili likajikuta likipiga magoti yote mawili chini, huku likiwa limeorojeka twipwili tipwili.
 
“Ahaaaaa”
Jamaa hilo lilijikuta likipiga mayowe, huku likifumba macho, baada ya kuiona ngumu nzito ikija kuharibu pua yake. Likasubiria kwa sekunde kadhaa ngumi hiyo kutua kwenye pua yake ili isambaratike, ila haikuwa hivyo, taratibu likafumbua macho na kukutana na ngumi hiyo ikiwa imemsogelea karibu kabisa na uso wake.
 
“Nikubamize?”
Jitu hilo likatingisha kichwa huku woga mwingi ukiwa umemjaa, Eddy akaishusha ngumi yake, wapambe wote wakawa kimya wakikosa cha kuzungumza. Taratibu jitu hilo likainamisha kichwa chini likaishiria kwamba limemkubali Eddy. Wapambe wake nao wote wakapiga magoti na kuinamisha vichwa vyao chini wakimpa heshima Eddy.
Eddy akatabasamu kisha akaelekea alipo libwaga koti lake, akaliokota na kulikung’uta vumbi kisha akalivaa vizuri. Akaanza kupita katikati yao kabla hajawamaliza akasikia sauti ikimuita.
“Heei usiondoke kiongozi”
Jitu lile lilimsemesha Eddy kwa heshima kubwa.
“Kama hutojali tunakuomba tulifahamu jina lako”
 
Eddy akageuka na kulikukuta jitu hilo likisaidiwa na wapambe wake kunyanyuka kutoka chini.
“Unahitaji kulijua jina langu?”
“Eddy alizungumza huku akilifwata jitu hilo”
“Ndio”
Lilizungumza kwa kuto kujiamini sana.
“Black Shadow ndio jina langu”
“Mimi naitwa Sabogoo. U…uu unakwenda wapi?”
“Sina makazi popote mimi ninaishi”
“Basi twende kwangu ni jirani na hapa”
Sabogoo alizungumza huku akiachia tabasamu pana dharau zote alizo kuwa nazo zimeyanyuka kama barafu, heshima ikachukua nafasi yake juu ya Eddy.
                                                                                                  ***
  Kazi ya kumbembeleza Sa Yoo, ilichukua masaa kadhaa, hadi akaukubali ukweli kwamba bibi yake kipenzi amefariki dunia. Kwa tamaduni za Kijapan, endapo kunatokea msiba basi nyumbani kwamfiwa ama ndugu wa mfiwa. Kutaandaliwa sehemu maalumu ambayo watu watahudhuria kumpa pole mfiwa huku picha kubwa ya marehemu iliyo pambwa kwa maua pamoja na kuwashiwa ubani pembei yake. Ikiwa katika eneo hilo.
 
  Hivyo ndivyo ilivyo kuwa kwa Sa Yoo. Alirudi nyumbani akiwa ameongozana na Shamsa pamoja na dakari. Shamsa akajikuita akiwa na majukumu ya kuwa karibu sana na Sa Yoo. Urafiki wao wa muda mfupi tu, walijikuta kila mmoja akimpenda mwenzake hadi baadhi ya watu ambao ni watu wa karibu na Sa Yoo, wakabaki wakiwa wanamshangaa Shamsa kwani hawakujua ni wapi ametoke na ni nani katika familia ya Sa Yoo. Kwani Shamsa aliketi jirani kabisa na Sa Yoo na kila sehemu ambayo Sa Yoo alikwenda basi Shamsa yupo nyuma yake.
 
    Msiba ukachukua siku kadhaa hadi kumalizika. Kutokana Shamsa alisha zoeana na Sa Yoo, ikawalazimu kuishi pamoja katika nyumba ambayo Shamsa amepangishiwa kwa ajili ya mapumziko yake. Furaha ya urafiki ikazidi kutawala kati yao, Sa Yoo akazidi kumtembeza Shamsa sehemu mbali mbali ndani ya Japan. Walitembelea sehemu nyingi za vivutio vya asili na vilivyo tengenezwa na binadamu.
“Hivi Shamsa huwa unapendelea kutazama mchezo wa mapambano?”
Sa Yoo alimuuliza wakiwa ndani ya gari lao wakirudi kutoka kwenye jengo la mauonyesho ya mashujaa walio pigana vita ya kwanza na yapili ya dunia.
“Ndio napenda kutazama”
 
“Basi leo usiku tutaelekea kwenye ukumbi mmoja unaonyesha mapambano ya ulingoni”
“Sawa ila hakuna fujo?”
“Hapana hakuna fujo kila kitu huko kina ulinzi wa kutosha. Tena ngoja tupitie kwenye ukumbi huo tununue tiketi mapema za kwenda kwenye maonyesho”
“Hakuna tatizo”
   Ndani ya dakika kumi Sa Yoo akasimamisha gari kwenye moja ya ukumbi mkubwa wenye mapicha picha mengi ya mapambano yatakayo fanyika usiku wa siku hiyo. Idadi ya watu wanao nunu tiketi katika siku hiyo ni kubwa sana.
“Huyu BLACK SHADOW ni nani?”
 
Sa Yoo alimuuliza  mmoja wa wauzaji wa tiketi baada ya kuona picha kubwa ya mpiganaji huyo, aliye valia kinyago cheusi usoni mwake na kuyaacha macho yake tu.
“Huyu ni mpiganaji mwengine mpya kabisa anazaminiwa na Sabogoo. Nasikia kwamba huyu jamaa ni mkali sana japo sijawahi kumuona na mimi”
Muuza tiketi huyo alizungumza kwa shauku iliyo zidi kuwatamanisha Sa Yoo na Shamsa. Wakanunua tiketi mbili za siti za mbele kabisa kisha wakaondoka kurudi nyumbani wanapo ishi kujiandaa kwa ajili ya usiku.
                                                                                                         ***
     Eddy hakuwa na jinsi ikamlazimu kukubaliana na Sabogo kujiunga katika kikosi chake, ambacho mara nyingi kinajishuhulisha na maswala ya upambanaji wa ulingoni. Eddy kutokana anatafutwa na polisi wa Japani, ikambidi atumie kikundi hicho kama sehemu ya kujihifadhia huku akiendelea na upelelezi wake wa maeneo kuweza kutafuta sehemu ambayo alipaswa kwenda kukutana na mwalimu ambaye angeendelea kumfundisha mafunzo ya upiganaji.
“Ila kabla sijaingia ulingoni na kupambana inabidi tukubaliane mambo mawali”
Eddy alizungumza akiwa na Sabogo kwenye ndani ya ofisi zikiwa zimebakia siku chache kabla mashindano ya kumtafuta mpambanaji wa ulingoni ndani ya Japan hayajaanza.
 
“Mambo gani tena kiongozi”
“Nahitaji kwa kila pambano munilipe asilimia ishirini ya pesa ambayo nitashinda. Mbili nitahitaji kuwa na mavazi ambayo ni meusi na yenye kinyago cheusi sihitaji sura yangu kuweza kuonekana na watu wa aina yoyote”
“Hayo yote mawili hayana tatizo nakuahidi kiongozi kila jambo litakwenda vizuri, swala la mavazi kuna mwana mitindo nitamuita sasa hivi aje akupime kisha leo leo hii hii mambo yatakwenda safi”
 
“Sawa”
Sabogo akampigia simu mwanamitindo anaye tengeneza nguo za wapambanaji katika maonyesho hayo makubwa ndani ya Japan. Akaifanya kazi hiyo ndani ya masaa kadhaa ambapo nguo imare za Eddy zikamalizika kutengenezwa huku kinyago chake anacho kivaa kichwani mwake kikimkaa vizuri kabisa hadi mwenyewe akajikubali.
“Unaonekana vizuri kiongozi”
Sabogoo alimsifia Eddy baada ya kumuona akiwa amevalia mavazi hayo, yenye maandishi makubwa mngongoni BLACK SHADOW.
“Huyu jamaa ni mtaalamu sana”
 
“Ndio maana nikaamua kumpa tenda yeye, na endapo utafanya vizuri basi nguo zako zinaweza kutengenezwa nyingi na kuuzwa kwa watu wa kila rika. Ukajikuta ukiingiza pesa nyingi sana”
“Kweli?”
“Ndio huku kwetu kila jambo zuri basi ni fursa ya kuingiza pesa”
“Basi nitahakikisha ninafanya kazi nzuri kadri ya uwezo wangu”
    Siku iliyo fwata wakaelekea kwenye studio za kupigia picha ambapo, Eddy akapiga picha zipatazo mia moja, akiwa amevalia mavazi yake hayo, na picha hizo zikapelekwa moja kwa moja kwa waandaaji wa mashindano hayo makubwa kwa ajili ya matangazo.
 
Siku na masaa yuakakatika, watu wengi ndani ya Japan, wakiisubiria siku ya mashindano ya mapambano ya ulingoni. Vituo vingi vya redio na televishion, vikazidi kutangaza juu ya mashindano hayo ambayo yana zawadi kubwa kwa mshindi, ikiwemo mkanda wa dhahabu wenye dhamani ya dola za kimarekani milioni ishirini.
 
Watu wengi kutoka maeneo mbali mbali ya Japan wakaanza kuingia kwenye ukumbi mkubwa unao ingiza watui zaidi ya laki sita kwa wakati mmoja, tiketi nyingi sana ziliuzwa majira ya asubuhi na mchana, wengi wakiwa na hamu ya kwenda kumuona mpiganaji mpya black shadow, ambaye anadhaminiwa na mpiganaji mbabe Sabogo, ambaye amewashangaza watu wengi sana kuto kushiriki katika mapambano hayo, na kusimamisha mtu mwingine kabisa.
 
Kila mmtu alisikika akisema yake, wengine wakidai labda Sabogo amestafu kupigana, wengine wakidai labda ameishiwa kutokana na kupoteza pambano la fainali mwaka jana na mpinzani wake ajulikanaye Young Poo.
 
   Eddy na wapamba wake Sabogo, wakaingia ndani ya jengo la mapambano, kupitia mlango wa nyuma ili asionekane na watu wengi akiwa amevalia mavazi yake ya kazi. Wakaelekea kwenye vyumba maalumu vya wapambanaji, wakakuta chumba chake kikiwa kimendaliwa vizuri na Sabogo akiwa na baadhi ya wadhamini wezake.
 
Akamtambulisha Black Shadow kwa wazamini wezake na kutoa majigambo mengi kwamba lazima mtu wake ataibuka mshindi na kuchukua mkanda, huku mamilioni ya dola ya ushindi yakiingia mikononi mwake.
“Kiongozi namba yako ya ushindani ni kumi na mbili”
Sabogo alimumbia Eddy huku akimpa kikaratasi mkoni mwake chenye namba.
“Sawa”
“Ukiingia usiwasikilize mashabiki, wewe hakikisha kwamba unacheza na mpinzani wako. Natambua mashabiki wako humu ndani ni wachache haswa ni hawa vijana wangu”
“Usijali kwa hili kila kitu kitakwenda poa”
“Nakuaminia”
                                                                                              ***
   Sa Yoo na Shamsa hawakupoteza muda baada ya kurudi nyumbani, wakaingia bafuni na kuoga kisha kila mmoja akavalia vazi ambalo anaona linaweza kumtoa kutona na umbo lake alilo jaliwa na Mungu. Kila mmoja alionekana kuwa katika hali ya kupendeza sana, walipo jitazama kwenye kioo kikubwa kilichomo ndani mwao kila mmoja alijikuta akimsifia mwenzake kwa alivyo pendeza.
 
  Wakatoka hadi nje, ila Shamsa akarudi ndani alipo isahau simu yake. Akaingia chumbani kwake na kuichukua simu yake, akakuta pia wamesahau kuizimi tv kubwa iliyomo ndani ya chumba chao. Akiwa anaangaza macho yake huku na kule kuitafuta rimoti ya kuzimia tv hiyo, taarifa ya habari ikaonyesha picha ya Eddy kwamba bado anaendelea kutafutwa na polisi.
 
   Mwili wa Shamsa ukawa kama umeingiwa na ganzi alipo isikia taarifa hiyo. Hakujua ni wapi alipo Eddy, hakujua ni kwa nini anazidi kutafutwa na polisi wa nchi ya Japani. Honi ya gari kutoke nje, ikamstua na kumtoa katika hali hiyo ya kujiuliza maswali mengi, kwa haraka akaizima tv na kutoka zake nje, akaingia ndani ya gari na wakaondoka zao.
 
  Wakafika kwenye ukumbi, idadi kubwa ya watu walio panga foleni kuingia kweye ukumbi huo, ikawapa hofu kidogo kuona kwamba wamechelewa. Kwa haraka na wao wakapanga foleni hiyo ikawachukua dakika kumi kufika mlangoni, wakakabidhi tiketi zao kwa wachukua tiketi, zikagongwa mihuri wakarudishiwa na kuingia ndani.
Wakakuta pambano la kwanza likiwa ndio linaanza. Wakakatiza katiza hadi kwenye sitiu zao zilizopo karibu kabisa na kwenye ulingo. Kila mmoja akakaa kwenye siti yake na macho yake akayaelekezea kwenye ulingo huo kutazama pambano linalo endelea.
 
   Wapo walio piga na walio pigwa kwenye mzunguko wa kwanza wa mapambano hayo, na kila aliye shinda aliweza kusonga mbele kwenye hatua inayo fwata. Ikafika pambano la kumi na mbili ambapo alianza kuingia jitu kubwa ulingoni lilio jazia nyama na lenye upara. Watu wengi wakalishangilia sana, kila lilivyo nyanyua mikono yake juu kuwaashiria watu wake washangilie ndivyo jinsi ukumbi ulivyo tia fora kwa makelele ya kushangilia.
 
“Anaye fwata sasa ni black shadooooowwwwwww”
Mtangazaji wa mashindano hayo alizungumza, ukumbi umzima ukafifia kwa sauti kila mmoja akisubiria kumuona black shadow. Taa kubwa yenye mwanga mweupe ikammulika Eddy katika sehemu anayo tokea. Kila mmoja akabaki akishangaa kwani mpambanaji aliyopo uliongoni ni jitu la maana ila black shadow mwenyewe ana mwili wa kawaida. Hata Eddy mwenyewe alipo liona jitu hilo alijiokuta akiingiwa na wasiwasi mwingi, kwani ni kubwa zaidi ya Sabogo na linatisha kwa michoro ya ajabu ajabu aliyo ichora mwilini mwake.
  Baadhi ya watu wakaanza kumzomea Eddy aliye ingia kwenye ulingo ulio zungushiwa kamba nne kwa kila upoande zilizo kuwa ngumu kupindukia.
 
“Si atabondwa bondwa”
Sa Yoo alimuuliza Shamsa huku wote wawili wakizidi kumzomea huyo black Shadow.
“Kweli atapigwa hakuna cha black shadow wala nini.”
Shamsa aliunga mkono huku akiruka ruka kwa kuzomea. Refarii akasimama katikati ya Eddy na jitu hilo kubwa ambalo Eddy kwa urefu analifikia tumboni.
“Mupo tayari?”
Refa aliuliza huku akijihami,
“Ndio”
Jitu hilo lilijibu huku likihema kwa hasira, mihemo iliyo zidi kumuogopesha Eddy, akajihisi haja ndogo inaweza kumwagika wakati wowote. Refa akatoa ishara ya kengele kugongwa, pambano lianze.
 
Bao moja zito likatua usoni mwa Eddy, akayumba mithili ya mlevi wa pombe za kienyeji, akastukia akinyakuliwa kama mwewe anapo nyakua kifaranga cha kuku, akazungusha haweni mara kadhaa, na kutupiwa pembeni. Ukumbi mzima ukanyanyuka kwa kushangilia. Macho yaliyo jaa ukungu na kizungu zungu kikali. Yakatua kwa binti aliye karibu kabisa na ulingo akishangilia kwa nguvu zote kama wanavyo fanya mashabiki wengine
“Shammm…..”
Hata kabla Eddy hajaimalizia sentesi yake hiyo akastukia jitu hilo likitua juu ya mwili wake na kumuangukia mgongoni na kumzidishia maumivu ya mwili.

SORRY MADAM (48)   (Destination of my enemies)
 
Eddy alajikuta akinyanyuliwa tena juu na kurushiwa nje kabisa ya ulingo, hapo ndipo kelele za mashabiki zikazidi mara dufu. Refa rii kwa haraka akamfwata Eddy na kumuuliza kama anaweza kuendelea na mchezo huo.
 
“Ndio naweza”
Eddy al;izungumza huku akijizoa zoa kunyanyuka katika sehemu aliyo angukia. Akanyanyua kichwa chake kutazama sehemu alipo kaa msichana aliye mfananisha na Shamsa, kweli macho wala akili yake haikuweza kukosea kabisa kwani binti huyo ni Shamsa. Kushangilia kwake, kukarudisha kumbukumbu, kipindi wapo katika fukwe za kopa kabana, nchini Brazil. Alipokuwa akicheza mpira na mwanaye Junio, huku Shamsa akiwa mshabiki mkubwa wa Junio.
 
   Uchungu na maumivu kuhusiana na familia yake iliyo potea duniani. Familia aliyo ihangaikia miaka kadhaa kuweza kuitia mikononi mwake, ila iliweza kuiondoka ndani ya siku moja, tena mauaji yaliyo sababishwa na baba pamoja na dada yake Manka.
Machozi yakaendelea kumwagika, taratibu akaanza kurudi ndani ya ulingo huku akijipenyeza kwenye uwazi wa kamba ya chini kabisa. Jitu linalo pigana naye lililopo muona tu Eddy likamkimbilia na kutaka kumkumba. 
 
Kwa bahati mbaya haikuwa hivyo tena kwani, lilijikuta likipita lenyewe na Eddy kumkwepa, likajibamiza kwenye kamba za ulingo zinazo futika na kulifanya lirudi kwa kasi sehemu linapo tokea. Jinsi linavyo kuja kwa kasi ndivyo jinsi macho ya Eddy yalivyo weza kulitazama kwenye mguu wa kustoto. Bila hata ya kujiuliza mara mbili, kwa miguu yake yote miwili, Eddy akajirusha na kugonga sehemu ya goti la kushoto la jitu hilo. 
 
Sehemu ya goti la jitu hilo, ikapelekea kutenguka na kugeuka nyuma. Anguko la jitu hilo huku likipiga mayowe ya maumivu makali, yakapelekea uwanja mzima kukaa kimya, hapakuwa na mtu aliye weza kuamini kwa pigo hilo jitu hilo litaanguka. Watu wa Sabogo, ndio pekee wakaanza kusikika wakishangilia huku wakilitaja jina la black shadow.
 
Madaktari wa dharara wakaingia ulingoni kulitazama jitu hilo, kila daktari aliye mtazama mguu wa jitu hilo linalo endelea kulia kama mtoto mdogo na kupiga piga kiganja chake chake chini kwa maumivu makali anayo pata. Wakajikuta wakitingisha kichwa wakimuashiria refarii kwamba jitu hilo haliweza kuendelea na mashindano hayo.
 
Refarii bila hiyana akamfwata Eddy na kumshika mkono wake wa kushoto na kuunyanyua juu kuashiria kwamba yeye ndio mshindi wa mechi hiyo. Baadhi ya mashabiki wakajikuta wakibadilisha msimamo wao na kuanza kumshangilia black shadow, wengine wakajikuta wakishikilia msimamo wao na kuanza kuzomea.
   Eddy akatoka ndani ya ulingo, taratibua akaanza kutembea kuelekea sehemu kilipo chumba cha kupumzikia akisubiria mzunguko unao fwata.
“Kazi nzuri kiongozi”
Sabogo alizungumza huku akimpiga piga Eddy mgongoni
“Asante”
                                                                                                            ***
  Tukio la mauji ya madaktrari walio kuwa wakimfanyia upasuaji mke wa raisi, zikazidi kuwaumiza kichwa watu walio shuhudia tukio hilo ambalo raisi aliagiza liweze kuwa siri kwa watu walio weza kushuhudia na endapo mtu ataitoa siri hiyo basi anaweza kukutana na jambo baya ambalo hakuwahi kuweza kulipata tangu alipo toka tumboni mwa mama yake.
 
Kila mtu alibaki akilinda kinywa chake kisizungumzie wala kichwa chake kisiliwazie sana jambo hilo kwani ni jambo la kutisha pili ni jambo ambalo hata ukilizungumza kwa watu kwamba mke wa raisi si binadamu, watu watakushangaa. Utata ukabaki kwa ndugu wa marehemu ambao walianza kuhoji ni wapi walipo ndugu zoa. Ila uongozi wa hospitali haukusita kudanganya kwamba wamewapeleka watumishi wao nje ya nchi kwa kazi maalumu.
“Jamani ila hata kama ni safari ya gafla mume wangu angenipigia simu kunijulisha?”
Mamammoja alimlalamikia daktari mkuu aliye bosi wa mume wake
 
“Ndio mama Kigadi angekupa taarifa, ila kutokana hali ya safari hiyo, ilikuwa ni ya gafla sana hapakuwa na daktari aliye weza kupiga simu.”
Daktari mkuu aliendelea kumuongopea mama huyo kwani anafahamu kila jambo lililo weza kutokea
“Sawa na wamekwenda nchi gani?”
“Pakistani, kisha watakwenda Iraque huko ndipo watamalizia kazi yao na kurudi nchini”
Daktari alisemea hivyo akimaanisha nchi zote hizo mbili ni nchi ambazo hazina amani sana, na lolote linaweza kutokea hata wakisema kwamba madaktari wao wamelipuliwa kwa mabomu, itakuwa si ja,bo la kushangaza sana zaidi itawauma wana familia ambao bado wanaendelea kufichwa juu ya vifo vya ndugu zao.
 
 ***
 Wiki nzima ikakatika, pasipo Rahab kurudisha fahamu yake. Madaktario maalumu kutoka nchini Mexco ambao kwa mara ya kwanza waliweza kumibu Rahab na kugundua tatizo la yeye kuwa na nguvu za ajabu, wakaweka kambi ndani ya ikulu wakiendelea kuifwatilia afya ya Rahab, huku wakiwa wamemuweka katika chumba maalumu.
 
  Hapakuwa na jibu lolote juu ya ugonjwa ambao unao msumbua Rahab. Raisi Praygod akazidi kudhohofika kwa mawazo juu ya mke wake. Moyoni mwake anampenda mke wake kupita kitu cha aina yoyote. Mapenzi yake juu ya Rahab, yamemfanya aonekane kama mwendawazimu. Shuhuli zake zote za uongozi amemuamchia makamu wake wa raisi. Kitu anacho kiangalia kwa sasa ni jinsi mke wake anaweza kupona. Kila mara aliingia kwenye chumba ambacho amelazwa Rahab na kuwekewa mashine ambazo zinamsaidia kupulia, na kusoma mapigo yake ya moyo, huku mirija isiyo pungua sita inayo peleka damu na maji ikiwa imechomwa mwilini mwake.
 
“Mke wangu anaweza kupona kweli?”
“Ndio anaweza kupona bado hatujapata kujua ni kitu gani ambacho kinaweza kumsaidia akapona”
“Jamani naombeni mufanye jitihada zenu mke wangu aweze kupona”
“Kila jambo muheshimiwa linawezekana ila kikubwa pia tusisahau kumuomba Mungu ashushe wepesi wake katika hili”
“Amen atasaidia”
Raisi Praygod alizungumza kwa unyonge huku akimtazama mke wake aliye lala kitandani, akionekana kuwa ni nusu mfu
                                                                                              ***
“Kiongozi jiweke tayari kwa pambano lijalo”
Sabogo alimuambia Eddy aliye kaa kwenye moja ya kiti kilichopo ndani ya chumba cha kupumzikia”
“Pesa ya pambano la kwanza mumesha niwekea”
“Ndio ipo”
“Mapambano yatakuwa mangapi?”
“Kwa leo yatakuwa manne kama utashinda yote kesho itakuwa ni fainali”
“Poa ila ku……”
Eddy akaona anyamaze hakuhitaji kuzungumza chochote juu ya Shamsa japo anamfahamu vizuri kama ndio yeye aliye kuwa miongoni mwa mashabiki ila hakuhitaji kujihusisha naye hadi pale atakapo dhibitisha kwamba kweli ni Shamsa kwani hisia za kwamba watu wanafanana duniani zilianza kumjia kichwani mwake.
 
Muda wa pambano lake la pili ukawadia, safari hii kidogo Eddy akawa amejipatia patia mashabiki, walio mshangilia.  Wapo walio anza kumkubali kwa kuweza kumuangusha jitu ambalo si rahisi kwa wau kuweza kuamini kama lingepigwa kirahisi kiasi hicho.
Eddy akaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea ulingoni. Alipo karibia ulingoni akaanza kutembea kuuzunguka ulingo lengo lake ni kufika katika sehemu ambayo amekaa Shamsa. Alipo muona Sa Yoo kidogo akastuka kwani anamfahamu msichana huyo, ndiye aliye weza kumsadia kuwakimbia polisi kwenye baa aliyo fikizia.
 
‘Ina maana wanajuana au?’
Eddy alijiuliza kimoyo moyo huku akiwatazama kwa jicho la kuibia, kuna kidoti cheusi kidogo ambacho kipo shingini mwa Shamsa, hichi ndicho kilicho mpa uhakika kwamba huyo ni Shamsa.  Bila kuchelewa akaingia uwanjani kumsubiria mpinzani wake ambaye anakuja kupambana naye.
Mpinzani wa sasa hivi hakuwa na umbo la kutisha sana, ila amejengeka vizuri kwa misuli yake, pambano likaruhusiwa kuanza, hapo ndipo Eddy akagundua kwamba mpinzani wake ana utaalamu mkubwa wa kupambana. Ikawa ni piga ni kupige, pambano likazidi kuvuta hisia za mashabiki waliomo uwanjani na hata wale walipo nje ya uwanja wanao tizama pambano hilo kupitia televishion.
 
   Mapigo ya black shadow yakaanza kumstua Shamsa na kuhisi kuna sehemu alisha wahi kumuona mtu huyo jinsi anavyo pigana ila kumbukumbu za haraka hazikufanya kazi kwani umahiri wa black shadow ukazidi kumchanganya Shamsa, aliye zidi kuvuta hisia kujua ni nani anaye pigana kama black Shadow.
Kumbukumbu zake hazikuwepo kabisa juu ya Eddy, kwani anatambua kwamba Eddy anatafutwa na jeshi la polisi nchini humo Japan na ningumu kwa yeye kuweza kushiriki mashindano kama hayo.
 
Kitu kilicho zidi kumchanganya ni jinsi black Shadow anavyo rusha mateke na ukunjaji wake wa ngumi. Kumbukumbu kadhaa za mwanaume aliye kuwa akipambana Mlimani City akiwa amevaliaa koti kubwa lenye kofia iliyo mficha sura yake, zikaanza kumjia kichwani mwake.
Akakumbuka mwanaume huyo jinsi alivyo kuwa anapambana na Eddy baba yake. Hapo ndipo akaanza kupata picha.
‘No hitahitaji kumfahamu huyu mpiganaji’
Shamsa alijisemea kimoyo moyo huku akimtazama black Shadow aliye mzidi mpiganaji mwanzake aliye anza kupoteza umahiri wa kupambana na mwisho kabisa mpiganaji huyo aliangushwa na black Shadow chini na kushindwa kunyanyuka kabisa.
 
Uwanja mzima ukanyanyka na kuanza kuchangilia, Shamsa naye hakusita kusimama na kumshangilia black shadow kwani mechi hiyo imeleta msisimko mkubwa kwa mashabiki wengi, wale ambao hawakumkubali walijikuta wakimkubali wenyewe.
“Sa Yoo, nimempenda sana yule black shadow”
“Umempenda?”
“Ndio nimependa”
“Umempendaje sasa wakati mtu mwenyewe hata sura humjui”
“Nihitaji kuweza kuiona sura yake, hata nimuelezee hisia zangu juu yangu”
“Sasa Shamsa rafiki yangu umechanganyikiwa, mara moja hii umetokea kumpenda mtu usiye mjua sura yake”
“Sa Yoo wewe niache tu. Hapa mwili wangu unachemka kweli kweli”
 
“Hembu acha masiraha bwana”
“Haki ya Mungu, nahisi si mara yangu ya kwanza kuweza kumuona huyu mpiganaji?”
“Umemuonea wapi?”
Swali hilo likamfanya Shamsa kuto kulijibu na kukaa kimya akimshuhudia black Shadow akizama kwenye mlango wa kutokea katika ukumbi huo kuelekea kwenye vyumba maalumu vya wapiganaji.
Mapambano yote yaliyo kuwa yamepangwa kwa watu watakao weza kushinda na kuelekea fainali siku inayo fwata yakamalizika huku Eddy akiwa amefanikiwa kushinda mapambano yake yote mane.
Mpiganaji anayo ogopwa Yong Po naye akafudhu kuingia fainali huku mapambano yake yote manne akiwavunja vunja wapiganaji alio shinda nishwa nao.
 
 Kila watu walio shuhudia mtanange wa siku ya kwanza wakatamani kushushudia na kesho yake fainali itakuwaje. Katika watu kutoka ukumbini, Shamsa na Sa Yoo wakafanikiwa kuelekea katika vyumba vya wapiganaji wajikijifanya kama waandishi wa habari. Kwani waandishi ndio watu pekee ambao wameruhusiwa kuingia katika  vyumba hivyo japo wamejitetea mbele ya walinzi kwamba wamesahau vitambulisho vyao na hapo walikuja kama washabiki, ila wanaomba kuweza kuwahoji washindi.
 
   Kutona na uzuri wao na mapozi kazaa ambayo Sa Yoo amekubuhu nayo kwenye biashara ya ukahaba aliyo kuwa anaifanya, ikawawia urahisi sana kuingia kwenye chumba cha Young Poo, wakakuta akiwa amezungukwa na waandhishi wengi wakimuhoji.
 
Moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha black shadow, ambacho nacho pia kimejaa waandhishi wengi wa habari wenye kamera kurekodia video na kamera za kupigia picha. Hawakuweza kumuona black shadow zaidi ya Sabogo na wapamb wengine.
“Wanasemaje?”
Shamsa alimuuliza Sa Yoo kwa kingereza kutokana hafahamu kijapan wanacho zungumza waandishi na Sabogo.
“Anasema kwamba black shadow, yupo bafuni hawezi kuzungumza na waandhishi wa habari”
 
“Hilo bafu lipo wapi?”
“Nahisi ni huo mlango walio simama mabaunsa”
Shamsa akautazama mlamgo uliopo mota chache kutoka sehemu walipo simama, wanaume walio jazia na kukatika miili yao kwa misuli ndio walio simama kwenye mlango wenye maandishi yanayo somekaa kwamba ni bafu. Wanaume hao ambao ni walinzi hawakuhitaji mtu yoyote kuweza kusogelea mlango huo wala kupiga picha na kama ni mazungumzo yote ya waandhishi wa habari yafanyike kwa Sabogo.
 
“Tutafanyaje sasa?”
“Sijui rafiki yangu itakuwaje”
“Hembu jifanye kama umechanganyikiwa unapiga makelele”
Shamsa alimshauri Sa Yoo, ambaye kwa mara ya kwanza alisita ila alipo shawishiwa sana na rafiki yake aliye tokea kumzoea, akaanza kupiga kelele huku akigaragara kuelekea kwenye mlango wa bafu. Mabaunsa hao wawili walio kaa mlangoni wakalazimika kupiga hatua kadhaa mbele kumzuia Sa Yoo asiwafwate, wandishi wa habari kadhaa wakageuka na kamera zao kuchukua tukio hilo. Shamsa akapata nafasi ya kuufungua mlango huo na kuzama ndani, lengo lake ni kwenda kumuona black shadow. Waandishi wa habari baadhi nao walipo ona mlango umeacha wazi wa bafuni wakajipenyeza na kuzama ndani.
 
Kwa bahati nzuri, Shamsa akamkuta Eddy akiwa tayari amemaliza kuoga na kuvaa nguo zake pamoja na kinyago chake. Eddy katika kumduwaa, Shamsa aliye mjia kwa kasi, ndani ya bafu hilo akiongozana na waandhishi wa habari. Akastukia Shamsa akimkumbatia kwa nguvu bila hata kusita Shamsa akaanza kumnyonye denda black shadow, huku waandishi wakifyatua kamera zao kupiga picha za kuweka kwenye magazeti yao.

ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com 

 

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts