Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 53 & 54 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 53 & 54 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Saturday, April 22, 2017 | 1:29:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Shamsa akajikuta akistuka baada ya kumuona Phidaya akimfwata katika sehemu alipo shikiliwa na polisi.
“Hawa ndio majambazi eheee?”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali, askari mmoja akamuitikia, Phidaya bila hata kujiuliza mara mbili, akamzaba kofi Shamsa, aliye kuwa akimshangaa, pasipo kuamini kwamba huyo ni Phidaya au laa, kwa maana wamefanana kila kitu. Ilibidi baadhi ya askari wamzuie Phidaya asiendelea kuwashambulia majambazi hao walio ivamia hospitali yake.

ENDELEA
   Shamsa na majambazi wengine watatu wakaingizwa ndani ya gari tatu tofauti za polisi, tukio hilo Sa Yoo aliweza kulishuhudia ila hakujau ni kitu gani kimetokea hadi Shamsa kukamatwa na askari, isitoshe akiwa katika mavazi ya unesi, wakati si mavazi ambayo alikuwa nayo.
 
Gari za polisi zilizo beba wahalifu zikaondoka Sa Yoo naye akaingia kwenye gari lake na kuzifwatilia hadi kituoni. Shamsa na waalifu wengine wawili wakaingizwa mahabusu, kusubiria mahojiano yatakayo fwanywa dhidi yao.
Akilini mwa Shamsa kumbukumbu za Phidaya, zilizidi kujirudia kichwani mwake. Hakuelewa ni jambo gani ambalo limetokea hadi Phidaya kuwa hai.
 
“Au sio yeye?”
Alijiuliza mwenyewe, huku akiwa amesimama kwenye moja ya kona ya mahabusu, huku mahabusu wezake wengine wakike wakiwa wamejilaza, kwenye sakafu.
“Kwa usiku huu hautaweza kumuona”
Askari mmoja alimueleza Sa Yoo, ambaye alihitaji kukutana na rafiki yake ili amuhoji kuhusu jambo lililo jitokeza muda mchache ulio pita. Sa Yoo kwa haraka akampigia simu daktari wa Shamsa, akamueleza kila kitui kilicho tokea, daktri hiyo aliye kabidhiwa jukumu la kumuangalia Shamsa, kwa haraka akafika kituo cha polisi akiwa ameongozana na mwanasheria wake kuhakikisha kwamba Shamsa anaachiwa huru.
                                                                                                           ***
  Maisha ya madam Mery yalizidi kuwa mazuri kadri siku zilivyo zidi kwenda, jeraha la risasi aliyo pigwa na Manka lilisha pona muda mrefu sana. Maisha yake aliamua kuyahamishia mkoani Mwanza, ambapo alifanikiwa kufungua mgahawa mmoja mkubwa wa kisasa, ambao kwa siku una uwezo wa kuhudumia wateja mia tisa hasi alfu moja kwa siku. 
 
Umaarufu wa mgahawa wake uliendana moja kwa moja na jina lake, jumba kubwa la gorofa la kifahari, lililopo maeneo ya majango mapya. Aliliwekea ulinzi mkali kutoka katika mashirika mawili tofauti yanayo jishuhulisha na ulinzi. Uzuri wake uliwanyima usingizi wanaume wengi wa jijini Mwanza, umri wa miaka arobaini na moja alio nao, kwa haraka haraka ukimtazama utahisi ni msichana mwenye umri wa miaka ishirini na tano.
 
  Kwa siku hiyo, madam Mery alijawa na furaha sana moyoni mwake, pale alipo toka katioka banki ya Bacrays, na kukuta kiasi cha miliomi moja dola za kimarekani zikiwa zimeingizwa kwenye akaunti yake hiyo.
“Ranjiti nitakutesa hadi kufa kwako”
Madam Mery alizungumza baada ya kupokea risiti yake inayo onyesha kiasi hicho kikubwa cha pesa kikiwa kimeingizwa kwenye akaunti yake. Kwa mwendo wa madaha akaanza kutembea huku mlinzi wake wa kike akiwa ameibeba pochi lake kubwa. Wakaingia kwenye gari, walipo muacha dereva wake.
 
“Nirudishe nyumbani nahitaji kupumzika kwa sasa”
“Sawa madam”
Safari ya kutoka benk hadi nyumbani kwake iliwachukua dakika ishirini, geti kubwa linalo funguliwa na umeme likafunguka. Gari yake aina ya Hammer, likaingia na dereva akalisimamisha kwenye maegesho ya magari, ambapo kuna gari nyingine nne za kifahari zikiwemo, Range rover sport, Aud Q7, Ferrari spider na BMW X6. Milinzi wake kwa haraka akashuka na kumfungulia mlango.
 
“Lete tu pochi pumzika”
Madam Mery alizungumza huku akiichukua pochi yake kwa mlinzi wake huyo, akaelekea ndani, alipo pokelewa na mfanyakazi wake wa ndani.
“Mama utakula nikuandalie chakula?”
Hapana sijisikii kula”
Kwa furaha ambayo madam Mery anayo, hakutamani siku hiyo kuweza kuingiza kiu chochote mdoni mwake, kwani utajiri wake unazidi kuongezeka mara dufu, akaingia chumbani kwake, ajitupa kwenye tanda lake kubwa linalo nesa nesa.
 
“Mery sasa hivi mimi ni milionear”
Alizungumza huku akiliachilia tabasamu lake pana, akakaa kitako, akaichukua rimoti ya Tv yake kubwa ilipo ukutani, akaiwasha na kuanza kutafuta chaneli ambayo ina kipindi kizuri cha kutazama. Chaguo la chaneli likaangukia katika chaneli ya ITV, ambapo amekuta mwenyekiti wa chama cha upinzani cha  TDPP(Tanzania Democras People Party), bwana Kibwila, akizungumza na waandishi wa habari.
Masikio na macho ya Madam Mery yote yakaelekea kwenye Tv yake, mapigo ya moyo yakaanza kumdunda pale alipo muona Manka akiwa pembeni ya kiongozi huyo.
 
“Huyu mtoto amefwata nini kwenye hichi chama?”
Madam Mery aalijiuliza huku akiongeza kidogo sauti ya Tv hiyo. Mwenyekiti wa chama hicho bwana Kibwila, akafikia wakati wa kumtangaza mgombea uraisi wa chama chake.
“Mgombea wetu atakaye ipeperusha bendera ya chama chetu atakuwa ndugu Godwin, gererali mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania”
Madama Mery, akahisi kizunguzungu kikali kikitaka kumchukua, baada ya kulisikia jina la Mzee Godwin, kwa kudhibitishiwa kwamba mwenyekiti huyo hajakosea kabisa, akaonyesha picha ya Mzee Godwin, hapo ndipo furaha yote ya Madam Mery ikayeyuka kama barafu liwekwapo juani.
                                                                                                                ***
  Taratibu Rahab akamfikia Raisi Praygod kwenye mlango alipo simama, kwa haraka akamkumbatia, na kuanza kumwagikwa na machozi jambo lililo mshangaza raisi Praygod.
“Mume wangu nisamehe”
 
Rahab alizungumza huku machozi yakimwagika, raisi Praygod, alizidi kuendelea kushangaa, kumuona Rahab akiwa amerejea katika hali ya kawaida. Rahab, hakusita kuanza kuzinyonya lipsi za mume wake, joto la hisia za kimapenzi likaanza kupanda katikati yao. Kila mmoja akajikuta akiwa na hamu ya kupata penzi la mwenzake, ambalo walilikosa kwa kipindi fulani. Ndani ya dakika kadhaa wote wawilili wakajikuta wakiwa hawana nguo katika miili yao.
Kila mmoja alipo hakikisha kwamba amemuandaa mwenzake vya kutosha, mechi ikaanza, si raisi wala Rahab aliye onekana kuchoka, kila mmoja alihakikisha kwamba anampa mwenzake kile kitu roho inapenda, huku wote wakiwa wamejawa na furaha mioyoni mwao.
                                                                                                             ***
   Iliwalazimu Black Shadow kuhamishiwa katika chumba kingine cha siri, kilichopo chini ya ardhi ndani ya hospitali hiyo. Kazi hiyo ilifanywa na dokta Ranjiti na wasaidizi wake, usiku huo huo, baada ya tukio la uvamizi kutokea katika hospitali yake. Polisi wakatoa tamko kwa watu ambao walijitokeza kumuombea shujaa huyo, kwamba warudi majumbani kwao na kuanzia siku hiyo watu hawata ruhusiwa kuja kujazana katika hospitali hiyo, hadi pale afya ya Black Shadow itakapo imarika. 
 
Lilikuwa ni pigo kwa mashabiki wa Black Shadow, ila hawakuwa na jinsi, ni lazima waweze kutii tamko hilo la askari. Ulinzi ukazidi kuimarishwa kwenye hospitali hiyo, hata dhiara ya raisi, ikakatishwa hadi pale mambo yatakapo kuja kuwa sawa ndipo raisi aweze kumtembelea mpiganaji huyo.
 
Uwepo wa Black Shadow katika chumba cha siri ulijilukana kwa watu wachache tu akiwemo Sabogo, ambaye yeye pekee ndiyo alipewa ruhusa ya kwenda kumuona Black Shadow katika chumba hicho. Asubuhi na mapema, Sabogo akawa yupo ndani ya chumba hicho cha siri kilicho jaa taa nyingi zenye mwanga mweupe.
    Sabogo akatoa kinyago kingine kilicho tengenezwa, kwa ajili ya Black Shadow, akamvua kinyago cha mwanzo na kumvalishi kingine kipaya lilicho mkaa vizuri, alipo hakikisha rafiki yake yupo salama, akatoka ndani ya chumba hicho na kurudi kwa daktari mkuu wa hospitali bwana Ranjiti.
 
“Itamchukua muda gani hadi kupata fahamu?”
“Itamchukua kipindi kidogo, ila kutokana bado tunaendelea kumuangalia kwa usalama mkubwa, basi tumuombe Mungu, kila jambo litakwenda sawa”
“Sawa dokta ila hakikisha kwamba hakuna mtu ambaye atagundua kwamba yupo chumba cha siri”
“Usijali kwa hilo”
Yote yakiwa yanazungumza ndani ya ofisi ya dokta Ranjiti Phidaya aliweza kuyasikia akiwa nje ya mlango, moyo wake ulizidi kumsumbua kila alipo fikiria juu ya donge nono ambalo polisi walilitangaza kwa mtu ambaye angelisaidia jeshi hilo kumkamata Eddy.
 
Phidaya akarudi kwenye ofisi yake akiwa na mawazo mengi, akilini mwake akaanza kulifikiria tukio la jana alipo weza kuiona sura ya Black Shadow, pili akafirikiria jinsi, majambazi walivyo vamia kwenye hospitali yake, na kutaka kumuua Black Shadow.
“Ina maana wanamjua kwamab ni Eddy nini?”
Phidaya alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti chake na kuanza kuzunguka zunguka ndani ya ofisi yake.
“Ngoja nikamueleze kila kitu mume wangu”
Phidaya alizungumza, kwa haraka akaanza kupiga hatua hadi mlangoni kwake, akavuta kitasa cha mlango huo, akaufungua na kuanza kutembea kuelekea katika ofisi ya mume wake.
                                                                                                 ***
   Baada ya Sabogo kutoka ofisini kwake, dokta Ranjiti, akawasha Tv yake, moja ya taarifa aliyo ikuta ni jinsi hospitali yake ilivyo vamiwa. Ila kati ya majambazi walio kamatwa, mmoja wao akamstua kidogo. Akajikuta akisimama kabisa na kwenda kuikodolea macho Tv hiyo. Jina la Shamsa Eddy, ndio kabisa zikazidi kumpagawisha. Na moja ya picha ikapita kwenye taarifa hiyo ya habari jinsi mke wake alivyo mtandika kofi jambazi huyo wa kike.
 
‘Mungu wangu siri inakwenda kufichuka’
Dokta Ranjiti alizungumza huku kijasho kikianza kumpiga na mapigo yake moyo yakizidi kwenda mbio. Akaanza kujipapasa kuitafuta simu yake ya mkononi sehemu alipo iweka, kwa bahati nzuri akaikuta kwenye koti lake, akaichomoa kwa haraka na kuminya baadhi ya namba kisha akaiweka sikioni, baada ya muda ikapokelewa upande wa pili.
“Ehee mkuu habari yako bwana”
‘Salama vipi dokta nikusaidie nini?’
“Naamini hao majambazi walio kuja kuvamia hospitalini kwangu wapo mikononi mwako”
‘Ndio na wanaendelea kufanyiwa mahojiano, ila huyu mmoja wa kike hana hatia ndio tumemuachia mida hii’
“Mungu wangu…….!!!”
‘VVipi kuna tatizo kwani?’
“Aha…ahaaa hapana”
‘Basi kila litakalo kuwa linaendelea nitakujulisha’
“Sawa mkuu”
 
Dokta Ranjiti baada ya kukata simu alipo maliza kuzungumza na mkuu wa kituo cha polisi, akili yake ikaanza kufanya kazi kama compyuta pale inapo tafuta, majina yaliyo hifadhiwa kwenye kumbukumbu zake. Kwa haraka mkumbukumbu zake zikatua kwenye moja ya mtu ambaye kazi zake ni umafia na huzifanya kazi za matajiri wengi ndani na nje ya Japani, pasipo kukosea wala kukamatwa na askari polisi kutokana na kujibadilisha badilisha sura na yeye huwa mara nyingi huwa ndio mtu anaye mfanyia upasuaji wa kumbadilisha sura.
 
“Ndio Kim upo wapi?’
‘Yokoma, vipi kuna tatizo dokta?’
“Ndio kuna tatizo bwana, kuna binti anaitwa Shamsa Eddy nahitaji uweze kumuondoa dunia”
‘Amekufanyaje tena dokta?’
“Ni binti ambaye anaitambua siri ya yangu juu ya mke wangu Phidaya, si unatambua kwamba huyu Phidaya ni mwanamke niliye mpora waziri mmoja nchini Tanzania”
‘Yap nalitambua hilo ulisha wahi kuniambia’
“Ndio basi binti huyo ni kati ya wale majambazi walio kamatwa jana na polisi na yeye anamtambua vizuri Phidaya kutokana ni mama yake”
  Mazungumza ya simu ya dokta Ranjiti yakamfanya Phidaya kusimama nje ya mlango, aliweza kusikia kila kitu alicho kizungumza mume wake, ila hakuweza kusikia mazungumzo na mtu wa pili.
 
‘Phidaya kutokana ni mama yake’
Maneno hayo yakaanza kujirudia kwa nguvu akilini mwake, machozi yakaanza kumlanga lenga Phidaya, hakuona haja ya kuendelea kukaa mlangoni mwa mume wake kwa haraka akaanza kutembea kurudi ofisini mwake. Akaufunga mlango wake kwa ndani, akavuta kiti chake, akawa kama mtu aliye changanyikiwa mara kadhaa akijiuliza maswali mengi kuhusiana na kitui alicho kisikia.
“Shamsa Eddy”
‘Ni binti ambaye anaitambua siri yangu juu ya mke wangu Phidaya’
 
Phidaya akajikuta akizidi kuyakumbuka maneno ya mume wake bwana Ranjiti, kiu na hamu ya kumuona Shamsa, ikaanza kumjaa moyoni mwake, kwani anatambu ni kati ya majambazi ambao walikamatwa jana na ni yule aliye mtandika kibao jana usiku. Kwa haraka Phidaya akavua koti lake na kuvaa koti la baridi, akajifutamachozi usoni mwake, wala hakuhitajki tena kuzungumza na mumewe kwa kitu alicho wahi kukiona. Kwani roho ya kumchukia mwanume huyo ilianza kumvaa. Swali ambalo mara kwa mara alijiuliza kichwani mwake, kwamba yeye ni nani, taratibu alihisi linaanza kupata jibu.
“Lazima nijijua mimi ni nani”
Phidaya alizungumza peke yake huku akitembea kwenye kordo ya kuelekea nje ya hospitali.
                                                                                                        ***
    Kwa juhudi za mwana sheria aliye msimamia Shamsa, kwenye mahojiano kati yake na polisi, yalizaa matunda, kwani hadi inatimu alfajiri tayari Shamsa alionekana kwamba hana hatia kutokana na maelezo yake aliyo yatoa. Uchunguzi ulio fanywa kwa nesi ambaye aliuawa na Shamsa, ulionyesha kwamba hakuwa ni nesi wa hospitali hiyo kutokana na kukutwa na michoro mingi(tattoo) mwilini mwake.
 
Pia katika kubanwa kwa waalifu wawili wa kiume walio kamatwa, walidhibitisha kwamba Shamasa sio mwenzao, hilo pia lilichangia kwa Shamsa kuachiliwa huru.
“Inabidi sasa twende nyumbani ukapumzike”
Sa Yoo alizungumza mara baada ya Shamsa kuachiliwa huru, kwani naye pia alishinda kituoni hapo kuhakikisha kwamba rafiki yake anaachiwa huru.
“Hapana nahitaji kwenda hospitali kumuona Black Shadow ndio niweze kwenda nyumbani’
 
Kutokana Shamsa ni mtu wa kung’ang’ania maamuzi yake mwanzo mwisho,  Sa Yoo na daktari hawakuwa na hiyana zaidi ya kuanza safari kuelekea katika hospitali aliyo lazwa Black Shadow. Akilini mwa Shamsa hakumfikiria Phidaya kutoka alihisi labda alimfananisha, isitoshe tayari walisha mzika mama yeka huyo. Kutokana ni asubuhi, barabara ilijaa foleni nyingi, kwa hiyo iliwachukua muda mwingi sana hadi kuweza kufika katika hospitali hiyo. Wakiwa getini, wakapishana na gari aina ya Aud A4. Hakuna aliye weza kuifwatilia sana, haswa Shamsa ambaye muda wote alimuwaza Black Shadow wake.
 
Wakaegesha gari walilo jia kwenye maegesho ya hospitalini hapo, Shamsa akawa wa kwanza kushuka kwenye gari huku akifwatiwa na Sa Yoo pamoja na daktari wake.
Kila nesi aliye muona Shamsa, alijikuta akimuogopa sana, kwani kila mmoja anatambua ni miongoni mwa majambazi walio sababisha kifo cha nesi mwezao aliye pigwa risasi jana usiku akijaribu kuyaokoa maisha yake.
 
“Daktari mkuu yupo wapi?”
Sa Yoo alimuuliza nesi wa mapokezi, aliye baki akimtumbulia macho Shamsa asijue ajibu nini.
“Dada nakuuliza daktari mkuu bwana Ranjiti yupo wapi?”
“Ahahaa ameetoka”
“Una uhakika?”
Shamsa alimuuliza nesi huyo huku akiwa amekazia jicho.
“Yupo ofisini kwake”
Sa Yoo alijikuta akiangua kicheko, baada ya kumuona nesi huyo akiwa anababaika babaika, wote watatu wakamuaga nesi huyo na kuelekea katika ofisi ya bwana Ranjiti.
                                                                                                  ***
Gafla Phidaya akajikuta akifunga breki za gari lake, alihisi kama mtu aliye muona kwenye gari aliyo pishana nayo getini, hajakosea.
 
”Ndio yeye”
Alizungumza huku akikunja kona ya haraka na kunza kurudi hospitalini kwa mwendo wa kasi, haikumchukua muda tayari akawa amesimama kwenye geti la kuingilia hospitalini kwake. Askari wakamfungulia geti hilo kuwa, kwa haraka akalisimamisha gari lake kwenye maegesho, kisha akashuka na kuanza kutembea kwa kasi kuelekea ndani. Akakuta manesi wa mapokezi wakiwa wanajadiliana kitu, walipo muona kila mmoja akajifanya kama anaendelea na kazi zake.
 
“Kuna nini hapa?”
“Hakuna kitu madam”
“Muna nidanganya eheee?”
“Madama kusema kweli yule jambazi wa kike amekuja tena, na sasa hivi ameelekea ofisini mwa mume wako”
“Muna sema kweli?”
“Ndio”
Phidaya akaanza kukimbia kuelekea ofisini mwa mume wake na kuwaacha manesi hao wakimshangaa boasi wao, Phidaya bila hata kubisha hodi akaufungua mlango wa ofisi ya mume wake, macho yake yakagongana na macho ya Shamsa, aliye aliye geuka kutazama mtu aliye ingia ndani ya ofisi ya daktari bila kubisha hodi.
                                                                                          
 SORRY MADAM (54) (Destination of my enemies)

  Macho yakamtoka dokta Ranjiti, akimkodolea mke wake. Phidaya akamtizama kwa muda Shamsa kisha akapiga hatua hadi alipo kaa mume wake, akambusu shavun kisha akawasalimia wageni alio wakuta ndani ya chumba hicho, hapo ndipo Shamsa alipo amini kwamba huyu si Phidaya anaye mtambua, na Phidaya alisi walisha mzika.
“Kama nilivyo waeleza, kwa sasa hatuto ruhusu mgonjwa kuonewa na mtu wa aina yoyote, kutokana na tukio ambalo limejitokeza jana”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akiwataza Shamsa na Sa Yoo pamoja na daktari wa Shamsa.
 
“Ila dokta kumbuka pasipo mimi, jana Black Shadow, angefariki dunia je mungekuwa na lipi la kuzungumza katika jamii, ni kwamba ulinzi wenu ni wakipumbavu ehee”
Shamsa alizummgumza kwa hasira, kila mmoja ofisini hususani dokta Ranjiti alibaki kimya.
 
“Samani binti kwani huyo Black Shadow ni nani kwako?”
Phidaya alizungumza kwa sauti iliyo zidi kumchukiza Shamsa.
“Hakuhusu”
“BInti jibu lako lingekuwa ni msaada kwako, ila kama hayanihusu sawa”
“Hembu sikiliza wewe mwanamke, hunijui na wala hunitambu vizuri mimi, nimehatarisha maisha yangu kwa ajili ya mpenzi wangu, kwa hiyo kaa mbali na mimi”
Shamsa alizungumza huku akisimama, kwa jazba hadi Sa Yoo na daktari wakamzuia.
 
“Ahahaa kumbe ni mpenzi wako ni kitu gani ambacho kinakufanya unapanic, wenye maamuzi ni sisi, unaweza kumuona huyo Black Shadow au usimuone sawa binti”
PPhidaya alizungumza huku akimpandisha na kumshusha Shamsa, aliyezidi kukasirika akarusha kibao ambacho Phidaya aliweza kukiona na kurudi nyuma.
“Weweeeee unataka kunipiga”
Phidaya alizungumza huku akijiweka sawa kwa mashambulizi, kwa haraka dokta Ranjiti akamshikilia mkewe. Sa Yoo na daktari kazi ikawa ni kumshikilia Shamsa.
“Phidaya mke wangu tuilia basi, mbona unataka kunidhalilisha mbele za wageni”
 
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya ukali. Jina la Phidaya likamstua Shamsa na kujikuta hasira yake ikishuka, kwa haraka akili yake akaipelekea katika kumchunguza Phidaya kuanzia juu hadi chini, hakuwa na tofauti yoyote na mama yake waliye mzika.  Shamsa alipotaka kuzungumza kitu kwa haraka Phidaya akamkonyeza pasipo dokta Ranjiti kumuona, mkonyezo huo ndio ukampa Shamsa ishara kwamba huyo ni Phidaya mama yeke, kwani ni mara kadhaa Phidaya alitumia kuwakonyeza yeye na Juio, pale anapo waaga kwenda mahali fulani.
“Phidaya mke wangu nakuomba uende ofisini kwako tafadhali”
 
“Nakwenda ila wageni kama hawa sihitaji kuwaona kwenye hospitali yetu”
“Sawa mke wangu nimekuelewa”
Phidaya akatoka na kuwaacha watu wote ndani ya ofisi wakikodolea macho hadi alipo ufunga mlango wake. Dokta Ranjiti akashusha pumzi nzito na kukaa kwenye kiti chake, ikambidi achukue rimoti na kuongeza upepo mzuri(A.C).
  Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita baina yao, ikabidi dokta Ranjiti kuuvunja ukimya huo.
“Naombeni munisamehe kwa yale yaliyo tokea kwa mke wangu”
“Hakuna tatizo si unajua mambo ya wanawake bwana”
“Kweli wanawake ni viumbe ambao tunatakiwa kuishi nao kwa akili sana”
 
“Hembu acheni unyanyapaaji wenu, nyinyi pia munatakiwa tuishi na nyinyi kwa akili”
Sa Yoo alichangia mada ya madaktai wawili hao, muda wote Shamsa alimuwazia Phidaya, alama zote ambazo Phidaya alikuwa nazo, huyu naye pia anazo. Swali imekuwaje kuwaje hadi awe hai, pili imekuwaje hadi aolewe na dokta Ranjiti.
‘Kuna kitu’
Shamsa alijisemea kimoyo moyo, akainyanyua sura yake na kumtazama dokta Ranjiti, jinsi anavyo zungumza na daktari mwenzake pamoja na Sa Yoo.
‘Huyu kuna jambo analificha’
“Shamsa, Shamsa, Shamsa”
Sa Yoo aliita, ikabidi amtingishe kidogo Shamsa, maana hakusikia jinsi anavyo muita.
 
“Eheeee…..”
“Vipi mwenzetu haupo nasi”
“Ahaa hamna, mumefikiwa wapi?”
“Tumekubaliana na daktari kwamba mgonjwa atakapo zinduka basi atatupigia simu na kuja kumuona”
“Ahaaa sawa”
Wakaagana na dokta Ranjiti, huku Shamsa akiendelea kukiumiza kichwa chake kwa maswali lukuki kuhusiana na mama yake huyo. Wakatoka nje ya ofisi hiyo, wakiwa wanasindikizwa na dokta Ranjiti jambo ambalo si lakawaida kwa daktari huyo kulifanya kwa wageni wake.
Akawasindikiza hadi sehemu ya maegesho ya magari ambapo Shamsa, Sa Yoo na daktari wao wakaingia ndani ya gari hilo na kumuacha dokta Ranjiti akiwasindikiza kwa macho.
 
Mambo yote yaliyo kuwa yakifanyika, Phidaya aliweza kuyaona akiwa amesimama dirishani, machozi yalimwagtika kumuona binti anaye utambua ukweli kuhusu yeye akiwa anaondoka katika eneo hilo la hospitali.
‘Ohh Mungu wangu nisaidie nikutane naye tena’
Phidaya alizungumza huku akilishuhudia gari hilo likitoka getini na kuingia kwenye barabara yenye magari mengi sana na kutokomea kwenye upeo wa macho yake.
“Ina maana hawajatambuana?”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akiwa anarudi ndani kwenye ofisi yake, hakuhitaji kuyapa mawazo yake asilimia mia moja kwamba hawajafahamiana. 

Nafasi nzuri aliyo kuwa nayo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba maisha ya msichana huyo yanatoweka dunia. Kutona na akili yake kuto kuwa sawa hakuona haja ya kuendelea kukaa hospitalini kwake, akampigia simu Kim, waonane kwenye moja ya mgahawa. Dokta Ranjiti akiwa anatoka, akakutana na Phidaya mlangoni.
“Vipi baby unatoka?”
“Ndio kidogo kuna mtu nahitaji kwenda kuonana naye”
“Wapi?”
“Ahaa ni hapa hapa mjini, kukiwa na tatizo nipigie nitakuja”
Dokta Ranjiti akambusu Shamsa mdomoni na kuanza kutembea kwa mwendo wa kujihami hami kwa mara kadhaa aligeuka nyuma na kumtazama mke wake, ambaye aliendelea kumtazama kwenye kordo hiyo ndefu hadi pale alipo kunja kona na kuingia kwenye lifti.
 
“Kuna kitu anahitaji kukifanya huyu”
Phidaya alizungumza huku akiwahi kuingia ofisini kwake kwenye dirisha lililo elekea kwenye maegesho ya magari. Dakika moja mbeleni akamuona mume wake akiwa anaingia kwenye gari lake na kuondoka hospitalini hapo. Kwa haraka akakaa kwenye kiti chake na kuifungua laptop yake aina ya ‘Mac Book Air’. Akaingia kwenye moja ya mtandao ambao unaweza kukupa ramani ya gari unalo hitaji kujua linakwenda wapi, ikakuonyesha kupitia satelaiti. Huduma hiyo ya haraka, Phidaya aliweza kujibiwa kila kitu na ndani ya dakika mbili, ramani iliyo jitokeza kwenye kioo cha lapotop yake hiyo, alama nyekundu ilionekana ikiashiria ndio gari la mume wake, linavyo tembea.
 
  Kwa haraka Phidaya akatoa simu yake na kumpigia kijna wake aitwaye Lee Si.
“Kuna ramani nakutumia hakikisha kwamba unalifwatilia gari la mtu huyo na hadi sehemu anapo ingia hakikisha kwamba unmfwatilia”
“Sawa madama”
“Ila hakikisha muhusika hatambua kwamba unamfwatlia?”
“Sawa madam”
Phidaya akaituma ramani hiyo kwa kijana wake ambaye mara nyingi huwa anamtumia katika maswala yake binafsi ikiwemo ulinzi wake, pale anapokuwa anakwenda katika sehemu za mbali.
 
***
  Karibia umma wa Watanzania wote walijikuta wakipigwa na butwaa, baada ya chama pinzani cha TDPP(Tanzania Democras People Party), kumsimamisha Mzee Godwin, wapo wananchi walio mkubali kutokana na kusikiliza vizuri hotuba ya mwenye kiti wa chama hicho bwana Kibwila, akimuelezea Mzee Godwin kuanzia mwanzo wa matatizo yake hadi mwisho, huku akilaumu kwamba matatizo yote hayo yamesababisha na waziri mkuu mstaafu aliye kuwa mke wake. Wananchi wengi wakatokea kuhuzunishwa na historia hiyo ambayo imetengenezwa huku vitu vichache sana vikiwa na ukweli ndani yake.
 
   Mgawanyiko wa kisiasa ukaanza kutokea ndani ya chama tawala cha TSD(Tanzania Society Development), viongozi wa ngazi za juu mmoja baada ya mwengine akaanza kuhamia katika chama cha upinzani cha TDPP. Wengi wao wakiwa ni wanachama wa siri wa kundi la D.F.E(Destination of my Enemies). Wananchi pasipo kujielewa husasani vijana wakajikuta wakiwafwata viongozi walio kuwa wakiwapenda na kujiunga na chama pinziani.
 
Maelefu ya wananchi wakaingia katika chama cha DTPP. Hali ya kiasiasa ikazidi kuwa tumbo joto kwa chama tawala cha TSD. Wananchi wengi walio kusanyika katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, wakiwa ni wanachama wa chama cha DTPP, hamu yao kubwa waliyo nayo ni kumuona mgombea wao uraisi Mzee Godwin. Helcoptar zipatazo nne, zikatua kwenye viwanja hivyo, huku helecoptar moja ikiwa imewabeba Fetty, Halima, Anna. Agnes, Jackline na Manka wote wakiwa wamevalia suti nyeusi, miwani nyeusi, gloves nyeusi na kila mmoja aliweza kuichomeka bastola yake kiunoni mwake na kuifunika na koti lake. 

Fetty na Halima wakaisogelea helcoptar aliyo panda mzee Godwin, wakafungua mlango. Mzee Godwin akavuta pumzi nyingi kisha akashuka. Wananchi wengi wakaanza kumshangilia kwa furaha, Manka na wezake wote wakamzunguka na kumuwekea ulinzi, ambao kila mtu alifurahia kuona walinzi wa kiongozi huyo wakiwa ni wanawake shupavu.
   Mzee Godwin akaanza kuwapungia wananchi mkono kila alipokuwa anakatiza, wamama, vijana na wababa walijitokeza katika viwanja hivyo huku kauli mbio ya chama hicho ikisema kwamba TUNATAKA MABADILIKO.
 
Mzee Godwin akapokelewa na viongozi wa chama hicho, ambao wengi wao leo ndio waliweza kumtia machoni mwao. Kwa nguvu kubwa ya pesa aliyo kuwa nayo mzee Godwin basi hapakuwa na kiongozi ndani ya chama aliye weza kwenda naye kinyume hata kidogo, kwani kila mmoja alipenda pesa yam zee Godwin, ili ajikimu kimaisha yeye na familia yake.
Manka na wezake, wakasimama jukwaa zima wakiimarisha ulinzi kwa Mzee Godwin, macho yao yote yalikuwa yakitazama tazama kila kona kuhakikisha kwamba hakuna jambo baya ambalo litampata kiongozi wao huyo.
                                                                                                  ***
   Macho ya Rahab hayakung’atuka kwenye kioo cha Tv kubwa iliyopo sebleni, viongozi kadhaa akiwemo mume wake, nao waliweza kukusanyika katika sebule hiyo ya ikulu kufwatilia mkutano mkubwa wa chama cha upinzani. Rahab aliweza kuwatambua wezake vizuri na hakuhitaji kuzungumza chochote kwa viongozi  waliomo ndani ya seble hiyo wakifwatilia mkutano huo. Kwani wengi wao wanatambua wasichana walio kuwa magaidi walisha fariki wakiwa mikononi mwa jeshi la Wamarekani.
 
“Mkuu wanaonekanawamejipanga sana hawa”
Makamu wa raisi alimuambia raisi Praygod ambaye muda wote aliendelea kuikazia macho Tv hiyo.
“Ni kweli, ila na sisi inatubidi tujipange sana, kwa maana safari hii wananchi wana uelewa mkubwa”
“Kweli muheshimiwa”
“Ila huku kiongozi wao si mtuhumiwa?”
“Ndio ni mtuhumiwa ila kwa sasa vithibitisho vya kumkamata hatuna, tayari amesha watek watu wengi”
“Kazi ipo”
“Ila niwatoe hofu, lazima tutashinda kwa maana wananchi bado wanaimani na sisi”
“Kweli kweli”
Viongozi wengine wakajikuta wakipiga makofi, wakimpongeza mwenyekiti wao wa chama kwa kauli aliyo izungumza.
 
Kichwani mwa Rahab, akawa anachanganua ni jinsi gani anaweza kukutana na rafiki zake hao pasipo kustukiwa, isitoshe kwa wakati huu ulinzi juu yake umeimarishwa kupita maelezo. Wakaendelea kutazama mkutano huo unao rushwa moja kwa moja kwenye televishion ya Star Tv, hadi ukaisha. Raisi Praygod wakamuomba Rahab awapishe ili wazungumze mambo ya kufanya katia wakati huu mgumu wa kuelekea kampeni.
Ikawa ni nafasi kwa Rahab, akaingia chumbani kwake, akavaa sweta jeusi pamoja na suruali nyeusi, akachukua miwani nyeusi, kisha chini akapigilia viatu virefu vya kisasa aina ya Travota. Alipo hakikisha kwamba yupo poa, akatoa simu yake na kumpigia Priscar. 
 
“Andaa gari binafsi nahitaji kutoka, nilikute nje ya ikulu”
“Sawa mdam”
Rahab akatoka chumbani kwake huku miwani akiwa ameificha kwenye mfuko wa sweta lake, akafanikiwa kutoka nje pasipo mume wake kumuona, kwani aliweza kuwapita sebleni na kuwakuta wakiwa katika mjadiliano mkali sana. Akatembea hadi kwenye geti la kutoka nje ya ikulu.
“Madam ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunakulinda kila unapo kwenda”
Mlinzi wake mpya mmoja alizungumza.
“Hata nikienda chooni pia munataka kunilinda humu ndani?”
“Hapana sio hivyo madam”
“Sikieni mimi ninakwenda kukimbia kimbia sihitaji ulinzi kwa maana ninaweza kujilinda mwenyewe sawa”
Rahab alizungumza kwa sauti ya ukali hadi walinzi wake hao wakatingisha vichwa kwamba wamemuelewa, akatoa nje ya geti na kuanza kujifanya kama mtu anaye fanya mazoezi ya kukimbi, alipo kunya kona akalikuta gari  jeusi aina ya KIA likiwa limesimamishwa.
 
Akalifwata akafungua mlango na kuingia, akamkuta Priscar akiwa amejiandaa, kwa safari atakayo ambiwa na bosi wake huyo.
“Twende hapo Serena”
“Sawa madam, ila leoumetokelezea”
“Hahaa, usiniambie”
Rahab alizungumza huku akiwa anajitazama kwenye kioo cha pembeni cha gari hilo, akatabasamu kweli alipo jiona amependeza na si rahisi kwa mwananchi wa kawaidia kuweza kumtambua kwamba ni mke wa raisi. Hawakuchukua muda sana kufika katika hoteli ya Serena, akashuka na kuanza kuelekea mapokezi huku akimuomba Priscar amsubirie ndani ya gari.
 
“Chumba walichopo walinzi wa mzee Godwin ni kipi?”
Rahab alimuuliza msichana wa mapokezi aliye onekana kumkodolea macho, ikambidi Rahab kuivua miwani yake, hapo kidogo msichan huyo wasiwasi ukamtoka baada ya kugundua kwamba ni mke wa raisi.
 
 Akamtajia namba ya chumba ambacho walinzi wa mzee Godwin wapo, Rahab akaingai kwenye lifti, akapandisha hadi gorofa ya nne. Akaanza kutembea kwenye kordo moja nzuri iliyo pabwa na vioo katika kuta zake. Akafika hadi kwenye mlango, wa chumba alicho ambiwa na muhudumu, akagonga mara mbili, mlango ukafunguliwa.
Mtu aliye simama mbele yake, Rahab alimtambua vizuri sana kwani ni Fetty, taratibu Rahab akavua miwani yake na kofia la sweta lake.
 
“What………..!!!!”(Nini……….!!!)
Fetty alizungumza huku akitoa macho ya mshangao, Rahab akaanchia tabasamu pana, sekunde kadhaa wakajikuta wakikumbatiana kwa furaha. Wakaingia ndani, Halima, Anna na Agnes walipo muona Rahab wakawa kama wamechanganyikiwa, kila mmoja akaacha alicho kuwa anakifanya na kwenda kumrukia rafiki yao huyo waliye potezana naye miaka mingi ya nyuma. Machozi ya furaha, yaliwatawala kati yao, wote watano wakajikuta wakikumbatiana kwa pamoja, jambo lililo wafanya Manka na Jaqline wabaki na mshangao.
                                                                                                       ***
   Kwa mbali macho ya Eddy yaliyo jaa, ukungu yakaanza kufunguka. Akaanza kujitahidi kutazama kwamba ni wapi alipo, ila mwanga mkali wa sehemu aliyopo, hakuweza kupata jibu. Akajitahidi kufumbua macho yake kabisa akafanikiwa, akakigeuza kichwa chake kushoto mwa kitanda alicho lala, akaona mashine za kupumulia pamoja na dripu moja la maji, likiwa limening’inizwa juu kidogo. 

Akilini mwake akatambua kwamba sehemu hiyo aliyopo ni hospitalini. Kumbukumbu zake za mwisho zikampeleka uwanjani, alipo kuwa akipambana na mpiganaji hodari Young Po. Akajaribu kunyanyuka ila maumivu makali katika mbavu zake yakamfanya arudi tena kulala.
 
  Phidaya baada ya kukaa ofisini mwake kwa muda akaamua kwenda katika chumba cha siri kumtazama mgonjwa ambaye ni mpenzi wa binti anaye fahamu ukweli kuhusu yeye. Phidaya akashuka kwa kutumia lifti hadi chini kabisa ya chumba hicho akiwa amevalia koti lake yeupe. Akapiga hatua hadi kwenye mlango wa chumba hicho akaufungua kidogo ila simu yake mkononi ikaita. Akakuta ni namba ya kijana wake Lee Si aliye mpa kazi.
“Umefikia wapi?”
‘Nimeweza kumuona katika mgahawa akizungumza na mwanaume mmoja anaye onekana ni hatari sana’
“Ulifanikiwa kuyasikia mazungumzo yao”
‘Ndio nilisikia akipmpa kazi ya kutaka kumuua binti anaye itwa Shamsa’
 
“Anataka kumuua Shamsa…..?”
Sauti ya Phidaya ilijipenyeza hadi ndani ya chumba alicho lazwa Black Shadow. Sauti hiyo haikuwa ngeni masikioni mwa Eddy, ni sauti ya mke wake Phidaya, aliye fariki mwaka mmoja nyuma.
‘Au nipo peponi?’
Eddy alijiuliza maswali huku akijitahidi kutega sikio lake, ila alipo sikia Phidaya anataja jina la Shamsa, akajihakikishia kwamba yupo dunia, hamu yake ikawa kubwa ni kumuona mwanamke huyo anaye zungumza na simu nje ya chuma alicho lazwa.
 
“Hakikisha unamfwatilia huyo mtu na unanipa ripoti”
‘Sawa madam’
Phidaya akakata simu, hakuona haja ya kuingia tena ndani ya chumba hicho kwani taarifa aliyo pewa imemchanganya, kwani binti anaye muhitaji ili apate kutambua ukweli wa yeye ni nani, maisha yake yapo hatarini. Akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye lifti ila kabla hajafika mbali akasikia kitu cha bati kikianguka kutokea ndani ya chumba cha mgonjwa, akaanza kurudi kwa kasi na kukuta mlango aliusahau kuufunga, kwani aliufungua kidogo kabla ya kupokea simu. Akaufungua mlango na kuingia ndani, akakuta bomba la kusimamishia dripu likiwa limeanguka chini, huku mgonjwa akiwa naye ameanguka chini, akiugulia maumivu
 
“Mungu wangu…..!! Umezinduka?”
Phidaya alizungumza huku akipiga magoti chini, akakinyanyua kichwa cha Black Shadow, akakiweka kwenye mapaja yake, akijaribu kumpa huduma ya kwanza mgonjwa, macho ya Eddy yaliyo jaa machozi ya maumivu makali ya mbavu zake zilizo piga chini, alipo kuwa akijaribu kunyanyuka kitandani ili kumuona mwanamke mwenye sauti ya inayo fanana na Phidaya, yakatua usoni mwa nesi huyo, akajikuta akistuka kwani ni Phidaya mwenyewe, ndiye aliyepo mbele yake akimuhudumia.
  
  ==>ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com    

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts