Home » , » Taarifa ya Wizara ya Habari kuhusu kutoweka kwa Roma Mkatoliki

Taarifa ya Wizara ya Habari kuhusu kutoweka kwa Roma Mkatoliki

Written By Bigie on Saturday, April 8, 2017 | 8:08:00 AM

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo imesema imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki”  tangu tarehe 5 Aprili 2017.

Katika taarifa yake iliyotolewa  jana jioni na kusainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara Zawadi Msalla, alisema kuwa wizara hiyo kwa dhamana yake katika tasnia ya sanaa, imefuatilia kwa karibu suala hilo kwa kuwa lina muelekeo wa jinai na kwamba hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.

"Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi".Alisema Zawadi.

Alisema kutokana na hali hiyo, wizara imewaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts