Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 61 & 62 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 61 & 62 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Sunday, May 14, 2017 | 9:34:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Gafla hata kabla hajaanza kuvuka barabara, gari moja jeusi aina ya haisi, likasimama sehemu alipo simama Phidaya, wakashuka watu wawili walio valio vinyago vyeusi wakamata kwa nguvu na kumuingiza ndnai ya gari hilo na kuondoka naye kwa nguvu, kitendo kilicho shuhudiwa na Eddy pamoja na Shamsa, kupitia kwenye kioo kikubwa akiwa ndani ya duka hilo. Eddy akavuka kwa kasi bilia kujali magari yanayo pita kwenye barabara hiyo huku Shamsa naye akitoka kwa kasi nje, wote wawili wakajikuta wakisimama katika sehemu aliyo tekewa Phidaya na macho yao wakilishuhudia gari hiyo ikitokomea kwa mbali.

ENDELEA
  Kila mmoja alishusha pumzi, akifikiria cha kufanya,  Sa Yoo, akatoka huku akiwa ameshika mfuko ulio jaa nguo
“Kumetokea nini?”
Wote wawili wakamtazama Sa Yoo, ambaye kidogo akaonyesha mstuko baada ya kumtazama Eddy usoni, Eddy naye aliweza kumtambua Sa Yoo. 

Ni binti aliye weza kumsaidia na aliachana naye siku walipo kwenda hospitalini. Jinsi Sa Yoo alivyo kuwa akimtazama Eddy machoni huku akimsogelea taratibu, kukamfanya Shamsa naye kumtazama mwanaume aliye kuja kusimama naye hapo akionekana aliliona tukio hilo. Macho yalimtoka Shamsa, mapigo ya moyo kidogo yakaanza kumenda mbio, akatamani kuliita jina la Eddy ila kigugumizi cha gafla kikamfanya aishie kupanua mdomo wake akimshangaa Eddy.
“Wewe si Eddy?”
 
Sa Yoo alizungumza huku akibonyea kidogo na kuchungulia Eddy, usoni mwake kwani kofia yake iliuziba uso wake kwa kiasi kikubwa. Japo amevaa ndevu za bandia ila Sa Yoo aliweza kumtambua haraka na kulitaja jina lake. Eddy hakujibu chochote iku kuwazugisha akajifanya akigeukia kule lilipo kuwa linaelekea gari. 

Macho ya Eddy yakawashuhudia askari wawili wakija katika eneo hilo, Eddy hakuona haja ya kuendelea kusiamam hapo kwani alitambua askari hao wanaweza kumuharibia siku yake, akatazama barabara pande zote mbili hapakuwa na gari inayo kuja akavuka kwa haraka, Shamsa akataka kumfwata ila Sa Yoo akamzuia kwani kuna gari ambayo ilikuwa inapita kwa kasi na endapo angepita basi angegongwa.
 
“Heii miss, mbona huangalii magari?”
Askari mmoja alizungumza huku akimtazama Shamsa usoni mwake.
“Ohoo samahani maafisa, kidogo ana mawazo?”
“Kwani kuna tatizo kati yenu?”
Askari mwengine aliuliza huku akimtazama Eddy aliyekuwa akipanda pikipiki, akiondoka na mzee Yo.
“Ahaaahah hakuna”
Sa Yoo yeye ndio alikuwa mjibuji wa maswali hayo, kwani Shamsa wakati wote macho yake aliyaelekezea kwenye pikipiki iliyo kuwa ikitokomea upande wa pili, ikakunja kona kulia na hakuiona tena.
 
“Madam una mawazo sana”
“Eheeee”
Shamsa akastuka kutoka kwenye dibwi zito la mawazo akimfikiria mtu aliye muna ni Eddy, swali alilo jiuliza mbona mtu huyo hakuweza kusema kitu chochote zaidi ya kuondoka. Wazo la Phidaya kutekwa likamjia upya akilini mwake.
 
“Mama ametekwa”
“Ametekwa, ametekwa saa ngapi si alitoka nje kuzungumza na simu?”
“Sa Yoo kuwa muelewa mama ametekwa”
Habari hiyo ikawastua hadi polisi hao, wakaanza kumuhoji maswali Shamsa, akaelezea jinsi alivyo weza kushuhudia, askari mmoja akaondoka kulifwata gari lao na kurudi nalo katika sehemu alipo mwezake kwa ajili ya kumchukua Shamsa kwenda naye kituoni kutoa maelezo yakutosha.
 
Shamsa akamkabidhi Sa Yoo funguo ya gari la Phidaya na kumuomba awafwate kwa nyuma, na awasiliane na Lee Si na kumpa habari ya kutekwa kwa Phidaya. Sa Yoo akaingia kwenye gari la     Phidaya akiwa na fuko lake lililo jaa nguo nyingi. Akaanza kulifwata gari la polisi kwa nyuma, akatoa simu kwenye mfuko wa jinzi alilo livaa, akatafuta namba ya Lee Si kwenye orodha ya majina yake kweney simu hiyo na kumpigia, siku kwa mara ya kwanza ikaita na kukatwa, akapiga tena akakuta simu ikiwa imezimwa kabisa.
“Mmmmmmm……….”
Aliguna Sa Yoo na kuirudisha simu yake mfukoni na kuzidi kulifwata gari la polisi kwa nyuma hadi katika kituo kikuu cha polisi nchini Japani
                                                                                           ***
   Mawazo mengi yakazidi kukisonga kichwa cha Eddy, akajiona ni mkosaji kushindwa kuzungumza chochote mbele ya Shamsa, ili kujulikana. Kila alipo likumbuka busu la Shamsa, machozi yakamtoka akatambua ni wazi kwamba mwanaye huyo amempenda, pasipo kujua kwamba amempenda mtu anaye muheshimu kama baba yake japo hakumzaa. Jambo jingine lililo zidi kumchanganya Eddy akilini mwake ni uwepo wa Phidaya nje ya duka ambalo Shamsa aliweza kutoka.
‘Ina maana Shamsa na huyu nesi wanajuana?’
‘Na wamejuana vipi? Au ni Phidaya mke wangu?’
‘Mmmm Phidaya wangu amekufa huyu si yeye’
 
Eddy aliwaza huku akiwa juu ya pikipiki ya Mzee Yo, ambaye ndio dereva, wakafika kwenye moja ya soko huku Eddy mara zote akiwa sura yake ameiweka chini, hakuhitaji kuinyanyua isije watu wakaistukia kama Sa Yoo ameweza kumtambua kwa haraka kiasi kile japo kuwa ameweka ndevu za bandia usoni mwake basi akaamini kwamba hata mtu wa kawaida anaweza kumtambua na ikawa ni tatizo kubwa kwake kutokana donge nono la zawadi ambalo wamelitangaza polisi, kila mwananchi aliamini kwamba analitamani kulipata.
 
Baada ya kununua manunuzi walio ona yanatosha, wakaanza safari ya kwenda mapangoni wanapo ishi. Mzee Yoo, alikituma kipindi hichi cha likizo vizuri kukaa mapangoni akifurahia uwepo wa Eddy aliye mchukulia kama mwanaye wa kumzaa
                                                                                             ***
    Kitendo cha Phidaya kumueleza Lee Si mpango wa Shamsa wa kutaka kumvamia dokta Yan usiku, hakujua ni jambo gani ambalo lingeweza kutokea. Lee Si alipo maliza majukumu ya kumrudisha bosi wake nyumbani kwake, akarudi hotelina ambapo amepangishiwa kwa muda na boasi wake hapo, kujificha kuepuka uvamizi wa Kim, ambaye hadi sasa hivi atambui yupo wapi wala ana mpango gani ambao anahitaji kuweza kuufanya. 
 
Lee Si, akachukua bastola yake, iliyo jaa risasi za kutosha, akaifunga kiwambo cha kuzia sauti alipo, hakikisha kwamba majukumu yake yamekamilika, akajilaza kitandani kwake, mara kwa mara macho yake akawa anayatupia kwenye saa ya ukutani. Ilipo jiri saa nne kamili usiku akanyanyuka kitandani, akavaa mavazi meuzi, kisha akachukua koti lake kubwa jeusi na refu, akilivaa linamfika magotini.
Alipo hakikisha yupo vizuri akashuka hadi gorofa ya chini, akaelekea kwenye maegesho ya magari, akaingia kwenye gari lake na safari ya kueleka kwa dokta Yan ikaanza.
 
Akalisimamisha gari lake mbali kidogo na ilipo nyumba ya dokta Yan, akalivaa koti lake pamoja na miwani nyeusi. Akaanza kutembea kwa tahadhari hadi karibu kabisa na yumba ya dokta Yan. Kitu kilicho mtisha ni kukuta walinzi wakiwa wamelundikwa kwenye stoo, hawajitambui, machale yakaanza kumcheza na kutambua kwamba Shamsa si msichana wa kawaida kama alivyo kuwa akimchukulia hapo awali, kwani ni yeye pekee ndio alikuwa na mpango wa kufika katika nyumba hiyo.
 
Akajibanza kwenye moja ya ua alipo muona dokta Yan akishuka kwenye gari lake, akataka kumvamia ila akasita alipo muona dokta huyo akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.  Alipo muona dokta huyo akiingia ndani ya gari lake na kutoka na bastola akatambua kwamba lazima daktari Yan atakuwa ameshtukia hali inayo endelea. Kitu kingine alicho hitaji kujua ni nani aliye ifanya kazi hiyo ya kuwapiga walinzi, japo ana muhisi Shamsa, basi akahitaji kudhibitisha kwamba ni yeye, au laa. 
 
Akanyata hadi kwenye dirisha, la kioo, akasikiliza jinsi dokta Yan akijitetea, akaisikia pia sauti ya Shamsa, ila katika sehemu alipo simama hakuweza kumuona Shamza zaidi ya dokta Yan, aliye anza kupiga magoti taratibu.
 
Lee Si, hakuhitaji siri ambayo ipo kati ya bosi wake na mke wake iweze kutoka, kwani anaitambua vizuri sana, akaikoki bastola yake vizuri, akavuta jicho moja, akakiweka kichwa cha dokta Yan katikati ya shabaha yake, na kufyatua risasi moja iliyo tua kichwani mwa dokta Yan na kumuangusha chini na kufa hapo hapo.
 
Hapakuwa na mlio wa risasi hiyo iliyo kuwa ikitoka kwenye bostola yeke kwani tayari alisha ifunga kiwambo cha kuzuia risasi. Kwa haraka akaondoka na kukimbilia kwenye gari lake, akaondoka kwa kasi na kurudi zake hotelini, kuhakikisha kwamba Shamsa hawai kufika kabla yake.
Akafika hotelini, kwa haraka akapandisha gorofani kwake huku koti lake akiwa amelishika mkononi, akaingia chumbani mwake, akatoa simu yake mfukoni na kumpigia dokta Ranjiti.
“Bosi nimemaliza kazi”
“Safi kijana wangu, hakikisha na kesho unaifanya kazi niliyo kuagiza madhubuti”
“Sawa mkuu”
Lee Si, akakata simu akavua nguo zake zote na kuingia bafuni kuoga.
                                                                                                          ***
  Maelezo ya Shamsa, yakachukuliwa vizuri na askari wapelelezi, wakamuhoji na Sa Yoo, akaelekeza alicho kishuhudia, kisha wakaruhusiwa kuondoka kituoni. Upelelezi wa kupotea kwa mke wa daktari maarufu nchini Japan bwana Ranjiti, ukaanza mara moja, ulinzi ukaimarishwa kwenye sehemu muhimu, kama katika viwanja vya ndege, bandari na stendi zote za mabasi yaendayo nje ya mikoa. 
 
Swala hilo likavuja kwa waandishi wa habari ambao hawakusita kutumi taaluma yao, katika kuwajulisha wananchi kwamba mke wa dokta Ranjiti amatekwa na watu wasio julikana. Picha za Phidaya zikaanza kuonyeshwa kwenye vituo mbalimbali vya televishion pamoja na kwenye magezeti yanayo toka majira ya jioni yakiwa yamekusanya habari za kutwa nzima kuanzia asubuhi hadi jioni.
Habari hizo zilizidi kuwakosesha amani Shamsa na Sa Yoo, pia walihofia usalama wao kwani hawakujua ni kitu gani kinaweza kutokea wakato wowote.
 
Wakarudi hotelini wakiwa katika mashaka makubwa, wakiwa wanasubiria lifti ya kupanda gorofani ifunguke, lifti ya pembeni ikafunguka, akatoka Lee Si, akionekana mwenye wasiwasi mwingi.
“Madam mu…muunataka kuniamb….ia amete…kwa?”
Lee Si, aliuliza akiwa na wasiwasi mwingi sana usoni mwake.
“Ndio mbona nilikuwa nakupigia simu hupokei?”
Sa Yoo alimuuliza Lee SSi huku akiwa amemkazia macho na kwajinsi macho yake yalivyo kuwa makubwa kiasi na makali pale anapo mkazia mtu, basi Lee Si, akajikuta akizidi kuogopa.
 
“Nilikuwa nimelala na simu ikawa imezima chaji”
“Mende mkubwa wewe, unajali usingizi kuliko boasi wako…..”
Sa Yoo alizungumza kwa kufoka huku akiuvuta mdomo wake, Shamsa akamzuia asimrushie kofi Lee Si, kwani alimuona hana hatia yoyote kwani kosa kubwa amelifanya Phidaya kwa kuto mtaarifu mlinzi wake huyo kwamba anatoka kama anavyo fanya siku zote. Ikabidi Lee Si, arudi nao, wakaingia kwenye lifti na kurudi hadi kwenye chumba wanacho ishi Shamsa na Sa Yoo.
 
Kila mmoja akakaa kwenye sehemu aliyo ona inamfaa, mawazo mengi yalizidi kumchanganya Shamsa, hakujua afanye nini ili kumkomboa mama yake.
“Wewe unakaa kimya nini sasa, toa mawazo tujue tunafanyaje”
Sa Yoo alizungumza huku kidole chake akiwa amemnyooshea Lee Si, aliye kiinamisha kichwa chake chini, Lee Si akamtazama Sa Yoo kwa macho yaliyo jaa huruma, hakuzungumza chochote zaidi ya kuangalia chini tena.
“Tusubirie tuone polisi watatuambia nini”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akimtazama Sa Yoo aliye kasirika kwa kununa.
                                                                                                  ***
   Furaha na amani ikatoweka moyoni mwa Eddy, jambo ambalo Mzee Yo alilistukia mapema, akajitahidi anampikia Eddy chakula anacho kipenda, kisha aweze kumfariji mwanaye huyo. Mzee Yo alipo maziza kupika chakula akamkaribisha Eddy mezani.
 
Eddy hakuzungumza chochote zaidi ya kutala taratibu, mara kadhaa alisikika akisunya, Mzee Yo akuzungumza chochote hadi walipo maliza kula chakua.
“Mbona leo una mawazo mengi?”
“Namfikiria yule nesi aliye tekwa?”
“Ahaa yule ni mke wa bwana Ranjiti, kwa jinsi ya kifo cha dokta Yan kilivyo tokea basi nahisi hapa kuna mtu anawafwatilia wafanyakazi wake”
“Una taka kuniambia yule nesi ni mke wa daktari aliye hitaji kuniua mimi?”
“Ndio”
“Hapa kuna jambo ambalo linaendelea na halieleweki?”
“Kivipi?”
“Si fahamu ila nahisi kuja kitu kinacho endelea kinacho peleka mambo yote hayo kutoke”
 
”Kuna haja ya kufanya uchunguzi wa chini chini”
“Basi nitaomba tuunze kuufa leo hii hii”
“Kwa leo kwako haitakuwa salama, ninaimani sasa hivi kutakuwa na msakako mkali unaendelea kwa mtu aliye mteka mke wa dokta”
“Hivi anaitwa nani?”
“Anaitwa Phidaya”
Moyo wa Eddy ukapiga paaa, akahisi labda hajalisikia vizuri jina alilo tajiwa, akamuomba Mzee Yo alitaje tena, bila hata kukosea Mzee Yo akalitaja jina hilo kama lilivyo, akazidi kumchanganya Eddy, na kumpa hisia ambazo masaa machache ya nyuma alizikataa na kuamini kwamba mke wake kwa sasa ni marehemu.
 
Mzee Yo majira ya jioni akaondoka mapangoni na kuelekea mjini kuchunguza ni nini kinacho endelea, huku akiwa ameagiziwa na Eddy kumnunulia nguo za Black Shadow, ili kurudi kazini kwa lengo moja kufahamu mke wa dokta Ranjiti ni Phidaya wake au laa na kama ni Phidaya wake, basi dokta huyo atatoa maelezo yakutosha juu ya kitu alicho kifanya hadi kumchukua mke wake.
                                                                                                   ***
   Sindano ya usingizi aliyo chomwa Phidaya mara baada ya kukamatwa na kuingizwa ndani ya gari, na watu walio zifunika nyuso zao. Ilimfanya kulala fofo na kuto kujitambua ni wapi anapo pelekwa. 

Lee Si, akavua kinyago chake na kumuangalia bosi wake huyo, ambaye kusema kweli ni msichana mzuri na mrembo sana. Ila kutokana yeye anafwata maagizo yake kama alivyo ambiwa na bosi wake, ilibidi kuziweka hisia za kimapenzi kando na kuangalia kazi ambayo amepewa. 

Akavaa kinyago chake. Wakafika kwenye karakana na dokta Ranjiti, wakaingia ndani Lee Si akambeba Phidaya begani na kumuingiza kwenye ndege moja iliyo andaliwa kwa safari ya kuelekea Korea kusini. 

Alipo hakikisha amekabidhisha kwa wahudumu wa ndege hiyo, wanao fwata amri za dokta Ranjiti, akashuka na kuhakikisha ndege inaondoka eneo hilo pasipo mchezo wowote kuweza kufanyika. Marafiki zake alio saidiana nao kwenye kazi hiyo, akawapa kila mmoja kiasi cha pesa walicho kubaliana wao wakaondoka kisha yeye akaingia kwenye gari lake na kurudi hotelini haraka.
 
Akafika hotelini na kufikiria ni mbinu gani  anayo weza kuitumia kuhakikisha kwamba si Shamsa wala Sa Yoo anaweza kumstukia kiurahisi. Muda wote aliweza kusimama dirishani  akitazama nje kuona kama wamerudi, haukupita muda mrefu sana akawaona wakishuka kwenye gari la Phidaya, lwa haraka akavaa nguo nyingine tofauti na alizo  kuwa amezivaa  wakati alipo kuwa akienda kufanya kazi yake. Akaingia kwenye moja ya lifti  akiwa na imani kwamba atawawahi  Shamsa na Sa Yoo  wakiwa bado hawajaingia kwenye lifti na ndivyo alivyo wakuta wakisubiria lifti ya kupandishia gorofani.
                                                                                                    ***
  Dakika chache yangu ndege aliyo pkizwa Phidaya kuwa hewani, ikaanza kuyumba. Upepo mkali, ulio sababishwa na hali ya hewa mbaya ukapelekea ndege kupoteza mawasiliano.  

Ndege hiyo ya kifahari inayo ingia abiria wanne pamoja na wahudumu walili, ikazidi kwenda mrama. Msukosuko mkali huo uiwafanya wahudumu hao kujkibamioza kwenye siti, wote wawili kila mmoja  aliliita jina la mama yake. Kwani wanaelewa kitu kinacho kwenda kutokea kwa wakati huo ni ndege hiyo kuanguka chini na wote watakuwa  marehemu ndani ya dakika chache zijazo. 
 
Kelele za wasichana hao kwa mbali zikaanza kupenya masikioni mwa Phidaya aliye jitahidi kuyafumbua macho yake yaliyo jaa ukungu wa usingizi.  Akafanikiwa kuyafungua macho yake, ila akastuka kujikuta miguu yake ikiwa juu, huku kichwa chake kikiwa chini, akiwatazama wasichana hao wawili wakiwa wamelala kila mmoja sehemu yake katika sehemu ambayo endapo  ndege isinge geuka basi sehemu hiyo ingekuwa juu. Kitu kilicho msadia Phidaya kuto kufwatana na wasichana hao ni mkanda pekee wa siti alio kalio ulio mbana vizuri kiunoni mwake. 
 
Kabla hata hajafacha chochote akastukia ndege hiyo ililala ubavubavu na kuanza kwenda kasi kuelekea chini jambo ambalo naye pia aliweza kuogopa na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada

SORRY MADAM (62) (Destination of my enemies)

   Rubani hakukata tama kuweza kuhakikisha anaiweka ndege hiyo kwenye hali yake ya kawaida, kwa bahati nzuri taratibu juhudi zake zikazaa matumaini, ndege akaiweka  sawa, na kuhakikisha kwamba inaanza kupanda juu taratibu kwani ilishuka chini kwa kiasi kikubwa na uzuri ni kwamba ipo katika usawa wa bahari. Ikamachukua dakika kumi hadi ndege kurudi katika hali yake ya kawaida. Kila mmoja ndani ya ndege hiyo akawa anahemea upande wake hususani waudumu wa ndege ambao mmoja kidogo alipata majeraha kwenye paji la uso wake. 
 
“Samahani ndugu abiria, kwa hali iliyo jitokeza na kwa sasa hali imekuwa shwari samani kwa usumbufu”
Sauti ya rubani ilisikika kwenye kipaza sauti kilicho fungwa ndani ya ndege hiyo. Phidaya akaichunguza ndege hiyo na kugundua ni malia ya mume wake. 
 
“Munanipeleka wapi?”
Phidaya aliwauliza wahudumu, ambao, kila mmoja anajikanda katika jeraha lake sehemu alipo umia.
“Madam hii ni safari ya Cairo Misri”
“KKufanya nini?”
“Muheshimiwa anakusubiria huku”
“Ina maana yeye ndio aliye niteka?”
Phidaya aliuliza kwa sauti ya hasira huku machozi yakimlenga lenga. Hapakuwa na muhudumu aliye weza kulijibu swali hilo, kila mmoja alikaa kimya huku akiinamisha kichwa chake chini asiitazame sura ya Phidaya iliyo fura kwa hasira.
                                                                                                          ***
   Wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Dar er Salaam, wamekusanyika katika kiwacha cha mpira cha Mwalimu Julius K.Nyerere. Wengi wao ni wapinzani wa chama kilicho kuwa kinaongoza nchi, wengi walifika kushuhudia jinsi raisi mpaya Mzee Godwin akiapishwa. Ulinzi mkali ukazidi kuimrishwa kila kona ya uwanja na maeneo ya uwanja. Vyombo vya kisasa vya ulinzi viliweza kufungwa sehemu mbalimbali kuhakikisha kwamba hapajitokezi shambulizi lolote ambalo litahatarisha maisha ya wananchi walio jitokeza. 
 
Askari polisi nao hawakuwa nyuma katika kuangalia swala zima la ulinzi, waliweza kubeba bunduki za moto huku wengine wakiwa na virungu pamoja na mbwa wanao nusa mabomu.
  Shangwe na nderemo zilisikika kila sehemu, uhasama wa kisiasi tayari ulisha yayuka mioyoni mwa watu wengi na kujikuta ni wamoja. Wakaanza kuingia viongozi mbalimbali kutoka maeneo tofauti, ndani na nje ya nchi, ikiwemo maraisi wa Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda. Nao walifika kuona kuapishwa kwa raisi mpya kutoka chama pinzani.
 
   Kati ya wananchi ambao waliweza kukusanyika eneo hilo, Madam Mery naye nimiongoni mwao. Sura yake aliyo ificha kwa kofia pamoja na nywele ndefu za wigi alilo shonea, alijiweka katikati ya wafuasi wa chama cha Mzee Godwin, ili kuhakikisha kwamba ni Godwin anaye mjua yeye au laa. Haikupita muda mwingi msafara wa Mzee Godwin ukaingia, uwanjani, ukiwa katika ulinzi mkali sana, watu walinyanyuka na kushangilia kwa furaha sana.
 
Chuki juu ya Mzee Godwin, ikazidi kuongezeka moyoni mwa Madam Mery, machozi ya uchungu yalizidi kumtiririka, kila alipo mtazama jinsi anavyo punga mkono kwa wananchi. Aliamini wananchi hawajui maovu ya mzee huyo na endapo wangeyajua basi wasinge dhubutu kumpa hata kura moja.
Taratibu za kuapishwa zikaanza, raisi Praygod akakabidhi cheo na majukumu yake kwa raisi mpya bwana Godwin, wakakumbatia kila mmoja akiwa na chuki moyoni mwake ila hawakuzihitaji kuzionyesha hadharani kwa watu walio kusanyika.
“Nakupa masaa ishirini na nne uwe umefunga virago vyako na kuhama hii nchi”
Mzee Godwin alimnong’oneza raisi msatafu bwana Praygod, aliye stuka kwa maneno hayo ambayo inadhihirisha kwamba bifu kati yao lipo palepale.
                                                                                                           ***
  Mzee Yo akarudisha ripoti kwa Eddy, akamueleza hali alisi jinsi inavyo endelea kwenye jiji kwa wakati huu, akamuelezea jinsi askari wanavyo endeleza msako wao nchi nzima. Vijana wengi wahuni waliweza kukamatwa na askari. Wengi waliingizwa kwenye vyumba vya mahojiano kuhojiwa kwa tukio la utekwaji wa mke wa dokta Ranjiti. 
 
“Nahitaji kumfahamu huyo dokta Ranjiti”
“Mmmmm nahisi kama picha yake ninayo hapa kwenye simu yangu”
Mzee Yoo, akatoa simu yake ya mkononi, akaingia upande wa picha ambapo kuna picha kadhaa alipiga na bosi wake huyo kipindi cha nyuma. Akamakabidhi Eddy simu. Moyo wa Eddy ukastuka kidogo, akasimama kutoka kwenye kiti alicho kikaa, picha ya daktari huyo haikuwa ngeni kichwani mwake, akajaribu kuvuta kumbukumbu kwenye ubongo wake, jibu likatua Tanzania kwenye hospitali ya Agakgani. 
 
“Huyu daktari nilisha wahi kumuona Tanzania?”
“Tanzania, mwaka gani?”
”Mwaka ulio pita?”
“Basi atakuwa ni yeye”
“Kwa nini unasema ni yeye?”
“Mwaka jana nilimpeleka Tanzania, nikiwa rubani wake, kisha nilirudi kumchukua baada ya mwenzi na nusu hivi”
Eddy akahisi akili yake ikipata moto, habari hiyo ya Mzee Yo, ikaanza kumpa picha ambayo alianza kuiaminbi kwamba mke wake bado yupo hai na hajafa. 
 
“Naanza kupata picha mzee wangu”
“Picha gani?”
“Yule mke wa dokta Ranjiti ni mke wangu?”
“Ni mke wako unamaanisha nini?”
“Ni mke wangu mzee, kwani mulimtoa wapi?”
“Mimi nakumbuka kwamba alikuwa ni mgonjwa ambaye aliingizwa kwenye ndege kulekule Tanzania na kuletwa huku baada ya muda akaolewa na dokta”
Eddy akahisi moyo ukitaka kumpasuka kwa wivu, hakuamini kama mke wake kipenzi anaye mpenda anaweza kuolewa. Swali jengine lililo muumiza kichwa, yule aliye zikwa Tanzania, alikuwa ni nani. Usiku wa siku hiyo Eddy hakuhitaji kulala pasipo kuhakikisha anainza kazi yaka ya kutambua ni wapi alipo mke wake. Akavaa nguo zake za kazi(Black Shadow) Akachukua pikipiki ya Mzee Yo na kuingia kazini.
‘Phidaya kuwa basi ni wewe mke wangu, sitaku kuamini kwamba umekufa’
 
Eddy alizungumza huku machozi yakimwagika, akazidi kuongeza mwendo kasi wa pikipiki, akielekea kwa rafiki yake Sabogo. Majira ya saa tano usiku akawa amefika nyumbani kwa Sabogo. Akatazama mazingira ya eneo zima, akakut a yapo vizuri, akapenya dirishani na kuwakuta vijana wa Sabogo wakicheza karata huku wengine wakinywa pombe kali.
Wote walipo muona walishikwa na bumbuwazi, hawakuamini kama mtu ambaye wamemtafuta kwa wiki kazaa hadi wakakata tamaa leo amesimama mbele yao.  Eddy akatoa ishara ambayo wanaitumia vijana wa kundi hilo, wote wakaitikia kwa ishara, wakaamini kwamba mtetezi wao amefika.
 
Mmoja wao akachomoka kwa kasi na kupandisha gorofani, akamuita Sabogo, ambaye naye alishuka kwa kasi huku akiwa na furaha sana, hakuamini alipo muona Black Shadow akiwa amesimama mbele yake. Akamkumbatia kwa furaha hadi kumnyanyua, nyuu kidogo kutokana na yeye kuwa ni mrefu kuliko Eddy.
“Ulikuwa wapi kaka?”
“Ni stori ndefu ila ninakuomga tukazungumzie chumbani”
Wakapandisha hadi chumbani, ambapo Sabogo, akawafukuza machangudoa wawili ambao walikuwa wakimburudisha kama kawaida yake.
 
“Ehee niambie kaka?”
“Ndugu yako nashukuru nipo salama, kuna mzee mmoja alinitorosha hospitali baada ya kutaka kuuliwa”
“Mzee gani tena?”
Eddy akaanza kumuadisia Sabogo mwanzo hadi mwisho tukio zima alilo simuliwa na  mzee Yo. Pia akamuelezea jinsi anavyo hisi kwamba Phidaya ni mke wake. Hilo jambo Sabogo naye akaliunga mkono, kwani siku ya kwanza kwenda hospitalini aliweza kuonana na Phidaya, ambaye alimuuliza kama anamtambua Eddy.
 
“Ulimjibuje?”
“Nilimuambia kwamba sikufahamu, sikutaka hata watu waweza kulijua hilo swala”
“Sasa hapo utanisaidiaje rafiki yangu?”
“Kaka ngoja tuanze kufanya uchunguzi tutambue kwamba mke wako kwa sasa yupo wapi kwa maama nasikia kwamba ametekwa”
“Nitashukuru kaka, yaani hata kama si mke wangu nitahitaji kumchukua hivyohivyo ili mradi anaifanana na mke wangu basi nafsi yangu itatulia”
“Usijali ndugu yangu nitakusaidia bega kwa bega kuhakikisha kwamba tunampata mke wako”
                                                                                              ***
“Hadi sasa hivi hakuna ripoti yoyote kutoka polisi na sisi tumekaa tu humu ndani, hatujui madama anaendeleaje?”
Sa Yoo alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, Shamsa hakuzungumza kitu chochote wala Lee Si, wote walishinda macho hadi majira hayo ya asubuhi. Kila mmoja alijihisi mpekwe isipokuwa Lee Si, kwani anatambu mpango mzima ambao alipewa na dokta Ranjiti kama mlinzi wa mkewe.
 
Simu ya Lee Si ikaingia meseji kupitia mtandoa wa Whatsapp, akaufungua ujumbe huo na kukuta picha ya Black Shadow, akiwa na kingago huku pembeni yake sura yake ikiwa haina kinyago.
Ujumbe wa maneno ukaingia kwenye simu yake, kutoka kwa dokta Ranjiti
”Hakikisha kwamba unamuua huyo kijana roho yangu iwe na amani”
Lee Si akashusha pumzi akanyanyua kichwa chake na kuwatazama Shamsa na Sa Yoo ambao nao pia walimkodolea macho wakihitaji kujua labda kuna habari yoyote ambayo ameipata
 
“Nakwenda chumbani”
Lee Si aliwaaga Shamsa na Sa Yoo, aliye mkazia macho hadi anatoka kwenye chumba hicho.
“Shamsa ninamashaka na Lee Si”
Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya chini kidogo
“Kwa nini?”
“Yaani mimi wala sielewi, ila moyo wangu umejawa na mashaka naye”
“Unamdhania vibaya kaka wa watu, laiti kama angekuwa ni mtu mbaya basi asinge tusaidia ile siku”
“Mmm haya mwaya ila nikimuona nahisi uzito fulani, moyoni mwangu”
 
“Ondoa imani potofi Sa Yoo”
Sa Yoo akanyanyuka na kuaanza kuandaa kifungua kinywa, alipo maliza wakajumuika kwa pamoja kupata kifungua kinywa. Walipo malinza wakaingia bafuni kwa pamoja, akaoga na kurudi seblen, macho yao wote wakayaelekezea kwenye kioo cha Tv, kuangalia habari yoyote ambayo inaendelea.
Hapakuwa na abari ambayo waliona inawahusu, wakazima Tv, akajiandaa na kuelekea kituo cha polisia kujua ni kitu gani ambacho kinaendelea. Majibu waliyo pewa polisi yakazidi kuwakatisha tama, kwa maana waliambiwa bado upelelezi unafanyika. 
 
“Shamsa mimi nakuomba uanze kumfwatilia Lee Si, akiwa yeye kama mlinzi wa madam ni lazima atatambua kitu kinacho endelea”
“Nitamfwatiliaje?”
“Ile siku ambayo wewe ulikwenda kwa dokta Yan, usiku Lee Si, naye alitoka mara baada ya wewe kutoka”
“Eheeee”
“Nilimchungulia kwa dirishani na kumuona akiingia kwenye gari lake na kwenda njia ambayo wewe ulikwenda, baada ya masaa machache kupita alirudi kwa haraka na haikupita muda mrefu na wewe ukawa umerejea. Isitoshe nilikwenda kutega sikio mlangoni kwake nikamsikia akizungumza na simu na mtu aliye muita ni bosi”
 
Sa Yoo alizungumza huku akipunguza mwendo kasi wa gari analo liendesha kwa maana mazungumzo hayo anayo yazungumza ni nyeti sana kwake.
“Ulimsikiaje?”
“Nilisikia akisema kwamba Bosi nimemaliza kazi, sasa sikujua ni kazi gani, nikahisi labda anazungumza na madam, ila uliporudi ukaniambia kwamba dokta Yan amakufa nikaanza kumtilia mashaka Lee Si”
Shamsa akabaki kimya na kushusha pumzi, yake maneno aliyo elezwa na Sa Yoo kidogo yameanza kumfungua akili yake, akamuomba Sa Yoo simu, akachukua namba ya Lee Si, na kuipiga ikaita kwa muda, ikapokelewa.
“Upo wapi?”
“Nipo mjini naendelea kutafuta kufahamu ni wapi alipo madam au kina nani ambao wamehusika katika kumteka”
 
“Ahaa sawa badae?”
“Vipi kuna tatizo?”
“Ahaa hapana nilitaka kujua kuwa upo wapi, kwa maana ulitoka pasipo kutuaga”
“Ahaa nafwatilia fwatilia kujua ni wapi alipo madam”
“Poa badae”
Shamsa akakata simu na kuachia msunyo mkali, akaingiza namba ya Lee Si, kwenye call traker, kuangalia ni wapi alipo, akakuta inmamuonyesha anaelekea kwenye moja ya mji, akamueleza Sa Yoo.
“Hiyo sehemu kuna kituo cha watoto yatima”
“Sasa ndio madama atakuwepo huko au anafwata nini?”
“Hembo ngoja twende”
Sa Yoo akageuza gari na kueleka anapo kwenda Lee Si, wakiongozwa na ramani kwenye simu ya Shamsa.
                                                                                                         ***
   Lee Si akafika kwenye kituo cha kulelea watoto yatima, kwa lengo moja la kumuona Soroo, kwa mamaana alimsikia akimnong’oneza Phidaya kwamba anatambua sehemu alipo Black Shadow. Akashuka kwenye gari lake moja kwa moja akaelekea kwenye ofisi ya walezi wa kituo hicho. Akajitambulisha, haikuwa ngumu kwa walezi hao kuweza kumtambua, kutokana ni juzi tu aliweza kuja akiwa na bosi wake Phidaya wakilete mizigo. Akaomba aweze kuitiwa Soroo, akiwaongopea kwamba kuna zawadi aliweza kukabidhiwa na bosi wake kabla hajapatwa na matatizo, kutokana wanamuamini, Soroo akaenda kuitwa
 
“Ankooo”
Soroo akamkumbatia Lee Si, wakatoka nje ya ofisi hizo wakiwa wanatembea kuelekea kwenye moja ya bustani wakaka kwenye moja ya viti.
“Unajua ni sehemu gani alipo Black Shadow?”
Lee Si alimuuliza Soroo, mara baada ya kutoa noti ya dola mia na kumkabidhi, Sa Yon a Shamsa waliweza kumuona Lee Si akiwa na mtoto mmoja, Shamsa alipo jaribu kumkazia macho mtoto huyo akagundua ni Junio, jambo lililo mfanya ashuke kwenye gari na kuanza kukimbia kuelekea kule walipo kaa Soroo na Lee Si

 ==>ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com    
   


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts