Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 70 & 71 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 70 & 71 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Sunday, June 18, 2017 | 9:23:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Eddy alipo isikia sauti ya Ranjiti kwenye simu ya raisi Praygod, akasimama kwa haraka kwenye sofa alilo kaa, kisha akaikwapua simu kutoa mkononi mwa raisi Praygod na wafanya watu wote wamshangae.
“RANJITI, SIKU NIKUKITIA MIKONONI MWANGU NITAHAKIKISHA KWAMBA KICHWA CHAKO KINAKUWA MALI YANGU”
“Wee…..weee si Eddy”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa wasiwasi mkubwa
“NDIO MIMI NI EDDY, MUME HALALI WA PHIDAYA”
Eddy alizungumza kwa sauti yanye msisitizo na kuwafanya Rahab na raisi Praygod wote kushtuka na kujikuta wakinyanyuka kwenye sofa na kumshangaa, kwani kati yao hakuna aliye weza kumgundua kwamba kijana huyo ni Eddy, ambaye alikuwa ni waziri wa ulinzi katika serikali yao na ni adui wa mapenzi wa raisi Praygoda, kwani aliweza kugundua Eddy alishirikia tendo la ndoa na mke wake kipenzi Rahab.

ENDELEA
   Simu ikakatwa na kumfanya Eddy kuishusha simu hiyo kutoka sikioni mwake kwa hasira. Hakuhitaji kuujali mshangao wa Rahab na raisi Praygod kwa maana alitambua ya kwamba ni lazima watapata mshangao huo ndio maana hakuhitaji sauti yake iweze kusikika kwa Rahab na mumewe.
“Eddy ni wewe?”
Raisi Praygod alizungumza huku akiendela kumshangaa Eddy aliyesimama, akionekana ni mwingi wa hasira.
“Hilo ni jibu na si swali”
 
Eddy alizungumza huku akimrudishia simu raisi Praygod. Eddy akamtazama Sa Yoo, na kumpa ishara ya kunyanyuka ili waondoke.
“Ahaa hapana Eddy, tukae tuzungumze”
Raisi Praygod alizungumza kwa busara sana, huku akimtazama Eddy machoni.
“Nikae wakati sifahamu mke wangu ni wapi alipo”
“Ndio maan mke wangu alimfwata huyo binti akimini ya kwamba yupo peke yake na alihitaji anahakikisha kwamba anamkomboa mkeo”
“Eddy, natambua haupo vizuri, hembu kaa basi tuangalie ni nini cha kufanya kwa wakati huu, ili kumuokoa Phidaya”
“Eddy kaa”
 
Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya upole. Taratibu Eddy akakaa sehemu ambayo alikuwa amekaa kwa mara ya kwanza.
“Ila ninawazo moja. Munaonaje tukaifwatilia simu hiyo kupitia satelaiti”
Sa Yoo alizungumza huku akiwatazama watu wote, Rahab akanyanyuka na kuwaomba wamsubirie. Akaingia chumbani kwake, alipo toka akarudi akiwa amebeba laptop aina ya Apple(macbook air), huku mkono wake mwingine akiwa ameshika karatasi mbili ndogo. 
 
“Kuna namba za simu yangu ile nilizo zinunua, hizi hapa”
Sa Yoo akanyanyuka na kusogea sehemu alipo Rahab, akachukua karatasi hizo na kuzitazama vizuri, akaiziona namba ambazo zimesajiliwa simu hiyo na hata endapo itakuwa imezimwa, kwa kupitia sateleitii ni lazima utaipata. Kwa haraka Sa Yoo akaanza kuifanya kazi hiyo kutokana ana ujuzi wa kazi hiyo.
 
Kila mtu macho yake akayaweka kwenye kioo cha Laptop hiyo, inayo tafuta kwa kasi ni wapi ilipo simu ya Rahab. Ndani ya sekunde arobaini na moja, tayari ramani ikaanza kujitokeza kwenye lapotop, alama ya kijana ikaanza kujionyesha kwenye ramani hiyo ikiashiria kwamba ndipo sehemu ilipo simu hiyo. 
 
“Hii simu ipo katika mtaa El khaing, na sisi tupo huku Al Kerdas. Ili kuweza kufika sehemu naamini ilipo kambi hiyo ni lazima kupita katika daraja la Qasr al-nil ili kuweza kufika. Na kwa haraka haraka tunaweza kuchukua muda kama lisaa moja na nusu hivi”
Sa Yoo alizungumza huku akiwaonyesha kwa kidole jinsi ramani hiyo inavyo kwenda.
“Ila simu yangu nahisi kama niliipoteza walivyo nitelekeza”
“Ulirudije huku?”
Sa Yoo alimuuliza Rahab huku akiwa amemtumbulia macho
“Nilirudi kwa kukimbia, kutokana huo mtaa walio niacha niliweza kuufahamu kwani ni kwa mara kadhaa ni kichukua mazoezi asubuhi huwa ninapita hapo”
 
“Ulilipita hili daraja?”
Ikambidi Rahab kuitazama vizuri ramani hiyo.
“Hapana sikupita”
“Basi, inabidi kuweza kuifwatilia simu hii sehmu ilipo”
Sa Yoo alizidi kuzungumza kwa kujiamini na kwa msisitizo mkubwa.
“Sa Yoo unaweza kuitafuta namba ya huyo Ranjiti sehemu ilipo tokea”
“Yaa ngoja mara moja”
Sa Yoo akaaiombanamba hiyo na kuonyeshwa na raisi Praygod, ndani ya dakika moja akafanikiwa kujua ni wapi namba hiyo inapotokea.
 
“Sehemu ni ile ile kama nilivyo sema”
Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo huku akiwaonyesha sehemu alama ya simu hiyo inapo onekana.
“Inabidi twende muda huu huu”
Raisi Praygod alishauri, hapakuwa na mtu aliye weza kupinga swala hilo, wakatoka wote huku Sa Yoo akiwa ameibeba laptop. Wakaingia kwenye gari, na Rahab akawa dereva wa safari hiyo.
                                                                                                                    ***
Dokta Ranjiti akakata simu huku mwili mzima ukiwa unamtetemeka, akahisi kitu alicho kisikia labda inaweza kuwa ni ndoto. Adrus akabaki akimtumbuli macho bosi wake huyo asijue ni kitu gani ambacho amezungumza na mtu aliye mpigia simu.
“Bosi”
Adrus aliita, ila dokta Ranjiti hakuzungumza chochote zaidi ya kubaki akimtazama, Adrus aliye jawa na shauku ya kuhitaji kujua ni kitu gani ambacho kimetoka.
 
“Bosi kuna kitu gani kilicho endelea?”
“Amepokea EDDY”
“Eddy ndio nani?”
Dokta Ranjiti hakujibu kitu chochote zaidi ya kunyanyuka kwenye kiti alicho kalia, akatoka ofisini kwake pasipo kulijibu swali la Adrus, moja kwa moja akaelekea chumbani alipo muacha Phiday, akamkuta akitoka bafuni kuoga.
“Vaa vaaa nguo tunaondoka”
Dokta Ranjiti alizungumza huku jasho likimwagika, mwili mzima. Phidaya akagundua kwamba kuna tatizo ambalo limetokea kwa Ranjiti.
 
“Tnakwenda wapi?”
“Kwani hapa ni kwako. Vaa tuondoke sasa hivi”
Ikambidi dokta Ranjiti aanze kutafuta nguo za Phidaya alizokuwa amezitupa chini, kipindi akimlazimisha kufanya tendo la ndoa.
“Vaa vaaa…mama”
Ranjiti akaendelea kumsisitiza Phidaya, ambaye akaanza kuvaa huku kichwani mwake akijiuliza ni nini kinacho endelea. Alipo maliza kuvaa nguo zake, dokta Ranjiti akamshika mkono na wote wawili wakatoka kwenye chumba hicho na moja kwa moja dokta Ranjiti akaelekea sehemu kulipo na gari lake. 
 
“Adrus ingia ndani ya gari munisindikize bandarini”
“Sawa mkuu”
Adrus akaingia ndani ya gari, akawasha gari hilo aina ya BMW X5. Wakati wote huo Phidaya, alikaa kimya, ila moyoni mwake akawa anaomba Mungu amsaidie lolote liweze kutokea, ila si kuendelea kukaa mikononi mwa Ranjiti. Wakaondoka eneo la ngome yao kwa mwendo wa kasi hadi walinzi wengine wakabaki wakishangaa.
                                                                                                               ***
Madam Mery baada ya kuamka moja kwa moja akaelekea chumbani kwa Eddy kutazama kama yupo, ila hakumkuta. Hakuwa na wasiwasi wowote zaidi ya kuamua kueleka katika chumba wanapo lala Shamsa na Sa Yo, akaugonga mlango mara tatu, hakusikia kitu chochote, alicho kifanya ni kuusukuma mlango huo na kuukuta upo wazi, akaingia ndani na kumkuta Shamsa akiwa amelala kitandani. 

Akamsogelea huku akimuita jina lake, ila Shamsa hakuitika. Akafika kitandani na kuanza kumtingisha, ila Shamsa hakuitika, kitu kilicho anza kumpa wasiwasi madam Mery. Akajaribu kumpima mapigo yake ya moyo na kukuta yakiwa hayafanyi kazi.
 
“Mungu wangu”
Madam Mery alistuka, kiasi cha kuanza kutokwa na kijasho chembamba usoni mwake.
“SHAMSA, SHAMSA, SHAMSA”
Madam Mery akajaribu kumtingisha tena, ila Shamsa hakujibu chochote, Madam Mery kwa haraka akanyanyuka kitandani hapo, kwa haraka akafungua mlango wa bafuni na kuchungulia kama Sa Yoo atakuwepo, ila hakukuta
mtu.
 
“Sa Yoo, Sa Yoo”
Madam Mery kwa kuchanganyikiwa, alijikuta akiita huku akimtafuta Sa Yoo hadi ndani ya kabati la kuhifadhia nguo. Hakumkuta mtu, wazo la kuomba msaada katika uongozi wa hoteli hiyo ukamjia kichwani, akataka kukimbia na kutoka nje, ili kwenda kuwaita, ila akahisi kwamba atachelewa zaidi, akaisogelea simu iliyopo mezani na kuminya namba za wahudumu.
“Nahitaji msaada”
Madam Mery alizungumza kwa sauti iliyo jaa wasiwasi mwingi, muhudumu akauliza ni chumba namba, ngapi. Akamtajia namba ya chumba.  Hazikupita dakika tatu wahudumu wawili wa kike walio valia sare zilizo wakaa vizuri mwilini mwao, wakaingia ndani ya chumba hicho.
 
“Mwanangu hapa anatatizo”
Madam Mery alizungumza huku akiwaonyesha wahudumu hao sehemu alipo Shamsa. Wahudumu hao, wakamsogela Shamsa, wakajaribu kumtingisha, kila mmoja wasiwasi ukamuingia kwani Shamsa hakujibu chochote. Muhudumu mmoja akajaribu kumpima kama ana pumua, ila jibu alilo lipata ni sawa na jibu alilo lipata Madam Mery.
 
“Piga simu kitengo cha dharura”
Muhudumu huyo alimuambia muhudumu mwenzake, kwa haraka akatoa simu zao maalumu wanazo zitumia wakiwa kazini, akapiga simu kwenye kitengo cha dharura kilichopo hapo hotelini. Muhudumu akaelezea tatizo lililomo ndani ya chumbu hicho.
“Tunakuja”
Sauti nzito ya kiume ilizungumza, na simu ikakatwa.
“Amefanya nini huyu?”
 
Muhudumu mmoja alimuuliza Madam Mery, ambaye macho yote yalisha anza kutwaliwa na wekundu na machozi kwa mbali yalisha anza kumwagika.
“Mimi sifahamu nimekuja kuwatembela asubuhi, wezake hawapo nay eye nimemkuta hapo kalala, nimemuita ila hakujibu chochote.”
“Mwenzake ameenda wapi?”
Kabla madam Mery hajajibu chochote, mlango ukafunguliwa, wakaingia wanaume watatu huku wote wakiwa wamevalia makoti meupe, mmoja wao akiwa amevalia kipimo cha kupimia mapigo ya moyo shingoni mwake. Kwa haraka haraka Madam Mery akatambu kwamba hao watakuwa ni madaktari. 
 
“Mgonjwa yupo  wapi?”
Dokta aliye valia kipimo hicho alizungumza, muhudumu mmoja akamuonyesha kwa kidole. Pasipo kupoteza muda daktari huyo akaanza kumpima Shamsa kifuani mwake. Madam Mery alipo yatupia macho yake usoni mwa dokta huyo akagundua kwamba kuna tatizo, kwa maana sura ya daktari, ilanza kubadiliika kila alipo jaribu kukihamisha hamisha kipimo chake kifuani mwa Shamsa.
                                                                                                       ***
“Ngoja ngoja mara moja”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakiwa yametoka akiitazama laptop. Alama inayo onyesha simu ya dokta Ranjiti lianza kutembea. Kitu kilicho ashiria kwamba dokta huyo anaondoka katika sehemu alipo kuwepo.
“Kuna nini?”
Rahab aliuliza huku akipunguza mwendo kasi wa gari.
“Anaondoka katika eneo alilo kuwepo”
Sa Yoo aliye kaa siti ya nyuma na Eddy alimuonyesha Eddy kwa kidole.
 
“Hembu nione”
Rahab alizungumza na kumfanya Sa Yoo kumpa laptop, hiyo. Rahab akasimamisha gari pembani na kuanza kuangalia ramani hiyo. Akashuhudia jinsi alama hiyo inavyo tembea kwa kasi kueleka upande mwingine ambao si ule ambao wanao tokea.
“Honye hembu naomba umpishe Sa Yoo akae hapa mbele”
Raisi Praygod hakubisha, Sa Yoo akapita katikati ya siti baada ya raisi Praygod kushuka, kisha akaka mbele na kuichukua laptop hiyo.
“Naamini unatambua kazi ambayo imekuweka hapa mbele”
“Ndio, twende”
 
Rahab akawasha gari na kuanza kuondoka kwa mwendo wa kasi kiasi, kila muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kuongeza mwendo kasi wa gari. Sa Yoo kazi yake ikawa ni kumpa maelekezo ya kuweza kukunja katika njia za vichochoro zinavyo onekanana kwenye ramani hiyo ili kuweza kuiwahi gari hiyo.
“Tunaikaribia, ipo kama kilomita moja mbele”
“Usijali”
Kwa muda wote huo, Eddy hakuzungumza kitu cha aina yoyote, akilini mwake akawa anafikiria ni adhabu gani ambayo anaweza kumpatia dokta Ranjiti pale tu atakapo mtia mikononi mwake. 

Picha ya jinsi Phidaya akiingiliwa kimwili na dokta Ranjiti ikaanza kumjia kichwani mwake, jambo lililo mfanya hasira yake izidi kumpanda. Raisi Praygod, mara kwa mara akawa anamtazama Eddy kwa jicho la kuiba, akaweza kugundua hasira aliyo kuwa nayo Eddy, kwa maana kwa mara kadhaa, aliweza kuona jinsi kifua chake, kinavyo panda na kushuka kwa kuhema kwa nguvu. Breki za gafla alizo zifunga Rahab, zikamstua Eddy na kumtoa kwenye dibwi la mawazo mabaya aliyo kuwa nayo. 
 
“Fala kweli huyu”
Rahab alizungumza huku akiminya honi, akimpigia dereva wa gari ndogo aliye simama gafla barabarani kwa lengo la kugeuza, pasipo kuonyesha ishara yoyote.
“Pita huko pembeni”
Raisi Praygod alimshauri, Rahab akafanya hivyo, uzuri ni kwamba Rahab, katika swala zima la uendeshaji wa gari yupo makini sana na ni mtaalamu wa kufanya hivyo. Alipo hakikisha gari limekaa sawa barabarani, akaendelea kuongez amwendo kasi wa gari hilo.
 
“Inavyo onyesha hapa, wanaelekea baharini”
Sa Yoo alizungumza huku akiitazama Ramani hiyo.
“Si tunakaribia kuwafikia?”
“Ndio, tunawawahi”
Rahab kusikia hivyo, ikawa ndio kama ametekenywa, akazidi kuendesha gari hilo kwa kasi, hadi mlio wa hatari ukaanza kupiga taratibu. Kila mtu ndani ya gari akawa kimya, hakuna aliye hitaji kumshauri Rahab kupunguza mwendo, kwani wote lengo lao ni kumuwahi dokta Ranjiti asikimbie, wakiamini atakuwa yupo na Phidaya.
                                                                                                             ***
   Adrus alizidi kuongeza mwendo kasi wa gari, pasipo kujua kwamba wanafwatiliwa. Alicho weza kukiamini hapo ni kufwata amri ya bosi wake, ambaye alimuamuru kuendesha kwa kasi ili kuweza kuwahi boti inayo ondoka saa sita kamili machana. Simu ya dokta Ranjiti ikatoa mlio mmoja, ulio mfanya kuitoa simu yake mfukoni.
“Ahaaa”
Dokta Ranjiti alitoa mguno wa kukasirika, kwani simu yake imeonyesha alama ya kuishiwa kwa chaji.
“Simu linazima chaji, alafu sijawampigia nahodha wa boti anisubiri”
 
“Mpigie kabla haijazima”
Adrus alishauri na kumfanya dokta Ranjiti kupiga simu kwa nahodha wa boti anayo iwahi. Simu ya nahodha huyo ikaanza kuita, baada ya sekunde kadhaa ikapokelewa.
“Haloo”
“Vipi muheshimiwa Ranjiti”
“Safi nipo karibu na bandari hapo nahitaji kusafiri kwenye boti yako”
“Ohooo muheshimiwa leo sijaingia kazini nipo likizo, labda nikupatie namba ya nahodha mwengine”
“Sawa fanya hivyo”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akikata simu. Simu yake ikarudia kupiga mlio wa kuishiwa na chaji. Baada ya dakika moja meseji ikaingia, kitendo cha dokta Ranjiti kuufungua ujumbe huo wa meseji, simu ikazima chaji na kumfanya macho yamtoke na kukasirika.
                                                                                                               ***
“Shiitiiiii SIGNAL IMEPOTEA”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakimtoka, alama aliyo kuwa akiifwatilia ilipotea kwenye ramani inayo waongoza.
“Unasemaje?
“Rahab aliuliza huku naye macho yakimtoka, Sa Yoo akamgeuzia laptop ili kudhibitisha kwamba ni kweli alama hiyo imepotea.
“Sasa tutafanyaje?”
Rahab aliuliza kwa sauti inayo onyesha kukataa tamaa, jambo lililo mfanya Eddy kuzidi kuchanganyikiwa.
                                                                                        
SORRY MADAM (71)   (Destination of my enemies)

“Hembu tusonge mbele musikate tamaa mapema”
Alizungumza raisi Praygod, Rahab akaaendelea kuendesha gari, ila kwa muda huu kila mtu macho yake yalikuwa makini kutazama tazama barabarani, ili hata wakihisi gari lolote, waweze kulisimamisha.
                                                                                                    ***
“Adrus simu yako ina chaji?”
“Hapana mkuu jana sikupata muda wa kuweza kuichaji”
“Shitii sasa itakuwaje kwa maana…..daaa”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akiangaza angaza kandokando ya barabara, kwa bahati nzuri akabahatika kuona duka moja la simu.
“Simamisha hapo pembeni nichukue simu mara moja”
“Sawa mkuu”
Adrus akafanya kama alivyo agizwa na bosi wake, akasimamisha gari pembeni, moyoni mwa Phidaya akawa anapiga sala kumuomba Mungu wake, dokta Ranjiti aweze kushuka yeye kwenda kununua simu hiyo. 
 
“Adrus hembu shuka unichukulie simu hapo”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akijipapasa mifukoni mwake, kwa bahati mbaya hakuwa na kiasi chochote cha pesa zaidi ya kadi yake ya malipo kwenye duka lolote ambalo anaweza kununua bidhaa kupitia kadi hiyo.
“Ahaaa, nimeacha pesa, ngoja nishuke mwenyewe”
Phidaya akashusha pumzi taratibu huku moyoni mwake furaha ikaanza kutawala taratibu, kwa maana hilo ndilo lililokuwa ombi lake. Dokta Ranjiti pasipo kuwa na wasiwasi wowote akashuka kwenye gari, na kuelekea kwenye duka moja kubwa, linalo uza simu.
 
Phidaya akamtazama Adrus jinsi alivyo kaa ndani ya gari pasipo wasiwasi wowote, tarattibu akasika kitasa cha kufungulia mlango wa gari, akajaribu kukifungua, kwa bahati nzuri akakuta mlango upo wazi. 

Pasipo kujishauri mara mbili Phidaya akafungua mlango wa gari na kujirusha nje, kwa kupiti kioo cha pembeni Adrus aliweza kumuona Phidaya akinyanyuka kwa haraka chini, na kuanza kuvuka barabara hiyo yenye magari mengi yanayokwenda kwa kasi. Honi mfululizo ziliweza kusikika kila sehemu Phidaya alipoweza kuvuka, hii ni kutokana na ukubwa wa barabara hiyo. Phidaya hakujali kelele za honi hizo, aliona ni bora agongwe na gari kuliko kukamatwa na dokta Ranjiti.
 
Adrus kwa pupa akashuka kwenye gari na kuanza kumfukuzia Phidaya, kitendo cha Adrus kufika barabara ya nnze, gari ndogo aina ya Nadia, ikamgonga, akarushwa juu kimo cha ng’ombe na kutupwa pembeni ya barabara ya tatu, kitu kilicho sababisha gari linalokuja kwa kasi dereva wake kufunga breki kali ili aimkanyage mtu aliye gongwa.
Mlio wa breki kali za magari ziliweza kuwastua watu wote waliopo eneo hilo, ikiwemo dokta Ranjiti aliye jikuta akitazama barabarani, kushuhudia ni nini kincho endelea.
                                                                                                              ***
Kufumba na kufumbua Rahab, aliweza kuona jinsi mtu aliye gongwa, akiangukia katika usawa wa gari lake linapo pita. Kwa juhudi zake zote akakanyaga breki watu wote ndani ya gari lake, wakajikuta wakisogea mbele kutoka kwenye siti zao, huku Sa Yoo, akijigonga kwenye dasbody, hii ni kutokana hakufunga mkanda. Gari ya Rahab ikasimama sentimita chache kutoka ulipo mwili wa Adrus, anaye endelea kutoka damu za puani na masikioni. Gari zinazo pita barabara hiyo zikabidi  kusimama.
 
Mapigo ya moyo ya Rahab, yakaanza kwenda kasi, baada ya gari kusimama. Sa Yoo, alihisi kizunguzungu ambacho tangu kuzaliwa kwake hajawahi kukipata. Raisi Praygod, alibaki akiwa katika bumbuwazi huku macho yamemtoka. Eddy kidogo, aliweza kuutoa wasiwasi moyoni mwake. Kwa haraka akashuka kwenye gari na kupita mbele na kutizama mtu aliye lala barabarani.
 
Phidaya baada ya kufanikiwa kuvuka barabara, akageuka nyumba kumuangalia Adrus kama anamkimbiza, aliweza kumuona akiwa amelala chini, barabarani, huku kukiwa na mtu mmoja akionekana kumchunguza. Akajaribu kukimbia, ila kwa woga miguu ikamuishia nguvu na kujikuta akitetemeka. 
 
Dokta Ranjiti katika kutizama vizuri, akamuona Adrus akiwa amelala barabarani, akimwagikwa na damu, kwa kasi dokta Ranjiti akatoka dukani, hata simu aliyo panga kuinunua akagahiri. Kitu cha kwanza kukifanya akakimbilia kwenye gari lake kumtazama Phidaya wake kama yupo, akafungu siti ya nyuma alipokuwa amekaa Phidaya, hakumkuta, wala hakumuona Adrus. Akaanza kukimbilia alipo angukia Adrus, akiungana na wasamaria wema,  wanao kwenda kutoa msaada sehemu ilipo tokea ajali hiyo. 
 
Dokta Ranjti akafika eneo hilp huku akihema. Eddy akasimama baada ya kugundua Adrus tayari ameshapoteza maisha. Dokta Ranjiti alisimama nyuma yake pasipo wote kuonana. Eddy katika kuyaangaza angaza macho yake upande wa pili wa barabara aliweza kumuona msichana anaye fanana na Phidaya. Akaanza kuvuka barabara kwa uangalizi mkubwa huku macho yake akiwa ameyalengesha kwa Phidaya ambaye naye anamtizama anavyo kuja.
 
 ‘Mungu wangu’
Phidaya alizungumza kimoyo moyo baada ya kumuona mwanaume aliye kuwa akimkagua Adrus akimfwata, huku akionekana kumkazia macho yeye. Phidaya akapata ujasiri wa haraka akaanza kijichanganya kwenye watu wanao kimbilia sehemu ilipo tokea ajali. Kila jinsi alivyo zidi kukimbia ndivyo jinsi mwanaume huyo aliye hisi ni mtu wa dokta Ranjiti, alizidi kumfukuzia kwa nyuma.
                                                                                                              ***
Taratibu raisi Praygod naye akashuka kwenye gari, na kujipenyeza penyeza kwenye kundi la watu walio mzunguka Adrus, akakuta mwanaume mmoja, akiwa anamtingisha kijana huyo huku akimwita jina lake, akionekana anafahamiana naye.
“Adrus, Adrusssssss”
 
Dokta Ranjiti aliita huku akionekana kuchanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilicho sababisha hadi kinana wake huyo kukutwa na mauti hayo. Rahab baada ya wasiwasi kumpungua kidogo, naye akashuka kwenye gari kutazama kinacho endelea. 

Akajipenyeza penyeza katikati ya watu, na kufika eneo alilo lala Adrus. Mtu wa kwanza kumuona ni dokta Ranjiti, Bila hata kujali kama kuna ajali iliyo tokea, Rahab akarusha teke, lililo tua kifuani mwa dokta Ranjiti na kumuangusha chini, jambo lililo washangaza watu wote waliopo kwenye eneo hilo.
 
Dokta Ranjiti alipo nyanyua macho yake, na kumtazama mtu aliye mpiga teke hilo, macho yakamtoka, baada ya kumuona Rahab akiwa amejiandaa kwa kumvamia. Watu waiopo eneo hilo kwa haraka wakamuwahi Rahab asilete fujo eneo hilo la ajali.
 
Dokta Ranjiti kwa haraka akanyanyuka na kujipenyeza penyeza katikati ya watu na kukimbilia lilipo gari lake. Hakuhitaji kukaa eneo hlo kwa maana alisha jionea hali halisi, Na endapo akiendelea kushanga shangaa maisha yake yanaweza kubadilika muda wowote, na anaweza kumfwata Adrus alipo elekea.
Watu walio mshikilia Rahab, walizidi kuongezeka kumzuia kufanya fujo eneo hilo, kitendo kilicho zidi kumpandisha hasira Rahab.
                                                                                                               ***
Kwa haraka madaktari wakamuweka Shamsa kwenyekitanda cha matairi, wakaanza kukisukuma kueleka kwenye lifti huku Madam Mery akifwata kwa nyuma, akili yake yote iliweza kuchanganyikiwa na hakutambua ni kitu gani ambacho kiliweza kumpata Shamsa hadi wakati huu.  Ndnai ya dakika moja na sekunde kadha wakawa tayari wamesha fika chini na kukuta gari la wagonjwa linalo tumika hapo hotelini likiwa tayari limesha wekwa tayari kwa ajili ya kumpeleka Shamsa hospitalini tena.
 
Safari ikaanza huku madam Mery akiwa ndani ya gari hilo, muda wote alipo mtazama Shamsa aliye wekewa gesi ya oxgen puani mwake, kwa ajili ya kujaribu kuyapa mapafu yake uzima. Machozi yalimwagika. Kitu kilicho muumiza kichwa madam Mery ni kuhusu Eddy na Shamsa, hakufahamu ni wapi walipo kwa sasa, hata swala la Phidaya kwa wakti huo likawa halipo tena kichwani mwake. Wakafika hospitalini madaktari ambao walisha taarifiwa wakampokea Shamsa kwa haraka na moja kwa moja wakamkimbiza katika chumba cha uchunguzi.
 
“Tunaomba ukae tu hapo usubirie majibu;”
Daktari mmoja alimuongelesha Madam Mery aliye onekana kupagawa hadi akataka na yeye kuingia katika chumba hicho. Akatii, alilo agizwa na daktari huyo, moyoni mwake, akaanza kumkumbua Mungu, kwamba anaweza kumsaidia katika swala la kumponyesha Shamsa.
 
Vipimo vya madaktari, vikagundua kwamba pombe kali pamoja na dawa za kutuliza maumivu ya kichwa alizo kunywa Shamsa masaa kumi nyuma ziliweza kutenge sumu kali iliyo pekelea mapigo ya moyo kushindwa kwenda jinsi inavyo takiwa. Juhudi za madaktari za kupandisha mapigo ya moyo ya Shamsa, hazikuzaa matunda, kwani yaliweza kupanda kwa asilimia tano tu, kisha baada ya hapo yakashuka chini kabisa na kubaki sifuri. 
 
Madaktari wakajaribu kuyapandisha mapigo ya moyo kwa kutumia sindano kali, ambayo ikishindikana hiyo basi, hawana jinsi tena. Kila daktari aliweza kuyapeleka macho yake kwenye kioo cha tv ndogo kiasi ilivyomo ndani ya chumba hicho akisubiria kuweza kuona mapigo ya Shamsa yanaweza kupanda kwa muda, wa dakika tatu hadi tano, kutokana na sindano hiyo. Kadri dakika zilivyo zidi kujisogeza mbele, ndivyo jinsi ukimya ulivyo zidi kutawala ndani ya chumba hicho. Mapigo ya moyo ya Shamsa hayakuweza kupanda hata kwa asilimia moja. 
 
“Dokta tunafanyaje, ni dakika ya saba sasa hajazinduka”
“Tumpe muda, siamini kama msichana mzuri kama huyu anaweza kufa”
“Ila sumu ilisha samba kwa kiasi kikubwa kwenye mwili wake”
“Ndio maana tukawa madaktari, sote topo humu ndani kwa ajili ya kuyaokoa maisha ya watu, haijalishi amepata tatizo la sumu ama tatizo la aina gani tutajaribu kadri ya uwezo wetu kuweza kuyaokoa maisha yake.”
Daktari mkuu bi Sharmaa, alizungumza huku akimtazama daktari wake msaidizi aliye onekana kukata tama kwa ajili ya Shamsa.
                                                                                                       ***
Eddy akaanza kuchanganyikiwa baada ya kumpoteza Phidaya kweye wingi huo wa watu japo, alijaribu kumkimbilia, ila kutokana na kusukumana sukumana na watu walioo kuwa wakikimbia kwenda kushangaa ajali hiyo, ndipo alipo mpoteza Phidaya.
“PHIDAYA UPO WAPIIIII”
Eddy alizungumza kwa sautri ya juu huku akijaribu kuangaza huku na kule kama anaweza kumuona Phidaya. Phidaya aliweza kuisikia sauti hiyo ikimuita, kutoka nyuma ya kibanda cha simu alipo jificha. Hakutaka kuweza kujiaminisha moja kwa moja kwamba mtu huyo labda ni mumu wake Eddy. Aliamini kwamba watu wa dokta Ranjiti wana mbinu nyingi sana za kuzitumia kuhakikisha kwamba wanamrudisha tena mikononi mwa Ranjiti.
 
“PHIDAYA NI MIMI MUMEO EDDY, TAFADHALI NAOMBA USINIKIMBIE”
Eddy alizungumza huku akiwa amesimama mbele ya kibanda hicho cha simu pasipo kufahamu ya kwamba nyuma ya kibanda hicho ndipo alipo weza kujificha Phidaya.
“TAZAMA MKE WANGU NI KWA MUDA MWINGI HATUJAONANA, NJOO BASI”
Eddy aliendelea kuzungumza kwa sauti ya juu, watu wangine walibaki wakimshangaa kwa maana hawakuelewa ni kitu gani anacho kizungumza hii ni kutokana na kutokujua Kiswahili.
 
‘No Eddy hawezi kuwa na sura kama ile, japo sauti ni yake, ila si yeye’
Phidaya alijishauri mwenye akiwa nyuma ya kibanda hicho huku mwili mzima ukimtetemeka, kwa woga mwingi. Taratibu akaanza kumchungulia mwanaume huyo anaye muita. Kwa bahai nzuri mwanaume huyo amempa mgongo na anavyo onekana amechoka sana kwa kutafuta na ndio maana akaamua kujihifadhi kwenye kivuli cha kibanda hich. Phidaya akabaki akiwa ameganda, kwa maana mtu huyo kwa nyuma, anafanana sana na Eddy, ila kitu kilicho mchanganya inakuwaje anakuwa na sura tofauti na sura ya mume wake Eddy anaye mtambua vizuri.
 
Eddy akaendelea kutazama pande zote za sehemu hiyo alipo, na kujikuta akisonga mbele akiendelea kumtafuta Phidaya, kosa kubwa alilo lifanya ni kuto kutazama nyuma ya kibanda cha simu, alicho kuwa amekipa mgongo.
Phidaya taratibu akatoka na kutazama sehemu alipo elekea Eddy, akamuona akitokomea kwenye mitaa, akiendelea kutafuta tafuta. Kwa haraka Phidaya akaita taksi, akaingia na kuondoka zake.
                                                                                                              ***
Rahab akarudi ndani ya gari akiwa na hasira, macho yalimtoka kiasi kwamba hadi  Sa Yoo akajikuta akimuogoa.
“Eddy atakuwa amekwenda wapi?”
Raisi Prarygod aliuliza swali ambalo alitegemea kabisa kati ya Rahab na Sa Yoo hakuna ambaye angeweza kumjibu kwa wakati huo. Rahab akafumba macho yake na kuanza kuvuta hisia, ili kufahamu Eddy yupo wapi. Alipo pata jibu hakumjibu mtu yoyote, alicho kifanya ni kuwasha gari, kwa kupitia upenyo wa barabara ya pembeni, akalitoa gari lake, huku akiwapigia watu walio kusanyika honi. 
 
“Tunaelekea wapi?”
“Hapo mbele”
Rahab alimjibu Sa Yoo, huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake, akakunja kushoto wakatembea kwa dakika moja, wakamkuta Eddy akiwa amesimama pembezoni mwa barabara, huku mikono yake yote miwili ikiwa kiunoni mwake, akihema sana.
“Ingia twende”
Rahab alizungumza na kumfanya Eddy kuwatazama kwa maana hadi wanafika hapo Eddy hakujua lolote kwani akili yake kwa muda huo inamuwaza Phidaya tu. Eddy akaingia ndani ya gari, jasho likimwagika mikononi.
“Nilimuona Phidaya”
“Usijali tutampata”
Rahab alizungumza kwa kujiamini huku akigeuza gari, na kuondola
                                                                                                                    ***
Dokta Ranjiti kwa kiwewe, breki ya kwanza akaifungia bandarini, kwa haraka akili yake ikamuongoza kukodi boti, itakayo mpeleka mbali kwenye moja ya kisiwa ambacho si rahisi kwa yeye kuweza kupatikana. Safari ikaanza huku moyoni mwake akijiapiza ni lazima atahakikisha anarejea kumtafuta mke wake Phidaya. Safari yake ikawachukua takribani masaa manne na nusu. Wakafika kwenye moja ya kisiwa chenye ulinzi mkali, kinacho milikiwa na Mzee Godwin na ndio kisiwa chake cha maficho.
 
“Wewe ni nani?”
Dokta Ranjiti aliulizwa na mlinzi mmoja mara baada ya kushuka kwenye boti. Dokta Ranjiti akatoa kadi yake ya uwanachana wa D.F.E. Huku yeye akiwa ni miongoni mwa madaktari wakuu wanao wahudumia wanachama wa chama hicho na hata utajiri wa hospitali yake kubwa iliyopo nchini Japani umetokana na pesa nyingi anazo jivunia kwa kumtibu msaidizi mkuu wa kikundi hicho ambaye hadi sasa hali yake ni nzuri. 
 
Askari huyo hakumzuia, akamkaribisha na kumuingiza kwenye gari, moja kwa moja doka Ranjiti akapelekwa kwenye moja ya jumba kubwa la kifahari lililopo hapo kisiwani.
“Mkuu yupo wapi?”
Dokta Ranjiti alimuuliza mlinzi mwingine wa kike, ambaye kwa ishara akamuomba waongozane naye. Dokta Ranjiti akapelekwa hadi kwenye mlango wa chumba cha mkuu wake, akakaguliwa na walinzi waliopo nje ya chumba hicho, kisha akaruhusiwa kuingia ndani.
“Habari yako dokta Ranjiti”
Mwanaume mmoja aliye kaa kwenye kiti cha kusukumwa na matairi alizungumza huku akiachia tabasamu pana usonimwake. 
 
“Salama vhabari yako mkuu JONH”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akiinamisha kichwa chake chini, kwa kutoa heshima kwa John, ambaye kiumri ni mdogo ila kimamlaka katika kikundi hicho ni mkubwa sana, akiwa hayupo mzee Godwin, yeye ndio anakaimu mamlaka yote katika eneo hilo.
“Mimi nipo salama ni muda mwingi, sana hatujaonana?”
“Ni kweli muheshimuwa, ila ni mizunguko ya kutanua chma chetu kiweze kutawala na kuzunguka katika nchi nyingi ulimwenguni”
“Kazi nzuri nipe ripoti”
“Muheshimiwa ninatatizo”
“Tatizo gani?”
Dokta Ranjiti akaanza kuadisia tatizo lake tangu alipo anza mauhusiano na Phidaya hadi kumpoteza.
 
“Huyo mumewe anaitwa nani?”
“Anaitwa EDDY”
“Eddy! Eddy nani?
“EDDY GODWIN”
John akastuka kulisikia jina hilo, macho yakamtoka, laiti angekuwa na miguu angenyanyua, ila sema ulemavu alio kuwa nao wote umetokana na Eddy anaye zungumziwa
“PUMBAVUUUUUUUUU NI HUYU EDDY TENAAAA”
Dokta Ranjiti alistuka kuisikia sauti ya John aliye kunja sura yake ambayo kwa upande mmoja imeharibika kutokana na mlipuko wa bomu alio weza kuupat.
“Muheshimiwa unamfahamu Eddy?”
“EDDY NI LAZIMA AFEEEEE”
                                                                                                                 ***
Nusu saa zima likakatiaza, Shamsa mapigo yake ya moyo hayakuweza kurudi, kila daktari aliye kuwemo kwenye chumba hicho akakata tamaa. Hadi daktari mkuu Bi. Sharmaa.
“Dokta mgonjwa ameshafariki huyu”
Daktari msaidizi alizungumza kwa msisitizo.
“Muandaeni kwa ajili ya kumpeleka Mochwari”
Bi Sharmaa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Kwa kipindi cha miaka ishirini katika kazi yake ya udaktari hakuna siku ambayo aliweza kuguswa na kifo cha mgonjwa, kama kifo cha Shamsa. Hakuhitaji kulia mbele za watu, akafungua mlango na kutoka
 
“Dokta hali ya mgonjwa vipi?”
Madam Mery alimuuliza Bi Sharmaa, huku akimtazama mwana mama huyo. Bi Sharmaa, akamtazama madam Mery kwa macho yaliyo jaa huruma, mbaya zaidi machozi akajikuta yakimwagika. Kitu kilichomfanya madam Mery kuhisi hali ya hatari imetoke
“SHAMSA AMEFARIKI DUNIA. SAMAHANI KWA HILO”
Bi Sharmaa alizungumza na kuondoka na kumuacha Madam Mery akiwa mdomo wazi asijue afanye nini.

==>ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com    

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts