Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 82 & 83 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 82 & 83 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Thursday, September 14, 2017 | 9:54:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Jamani hii ni kama suprize kwa waziri wetu Agnes, kwa mana hakutarajia ujio kama huu wa watu katika siku kama hiiya leo”
Mshereheshaji alizungumza, akawaomba watu wote kusimama. Wakatii hadi Eddy mwenyewe. Mshereheshaji akawaalika wageni rasmi. Ambao walianza kuingia ndani ya ukumbi huo wenye mlango nyuma. Eddy na wageni wengine waalikwa wakageuka kuangalia ni wageni gani hao rasmi. Macho yakamtoka Eddy baada ya kuwaona raisi Godwin akingiia ukumbini hapo huku mbele yake akimuona John akisukumwa kwenye kiti cha matairi, na wote wakapitiliza moja kwa moja hadi kwenye meza ambayo Eddy ameketi, na taratibu raisi Godwin akampa mkono Eddy kama salam, aliye utazama pasipo kuupokea.

ENDELEA
  Taratibu Eddy akaupokea mkono wa raisi Godwin, huku akiachia tabasafu usoni mwake ambalo fika alifanani na kitu anacho kifikiria akilini kmwake. Eddy akamsalimia John kwa ishara, naye akaachia tabasamu. Msherehekaji akwaruhusu watu kuweza kukaa kwenye viti vyao na kuendelea na ratiba iliyopo mbele yao. Kwa mara kadhaa Eddy aliweza kumtazama raisi Godwin na John ambao wanaonekana hadi sasa hivi hadi sasa hawajamgundua Eddy.
“Kijana unaitwa nani?”
 
Raisi Praygod alizungumza huku akimtazama Eddy usoni.
“Naitwa Erickson. Erickson Forrd”
“Ahaa ninaamini unanifahamu?”
“Ndio ninakufahamu, wewe ndio raisi wetu. Mimi ni mmoja kati ya watu nilio kuwa mstari wa mbele kukupigia kampeni chuoni”
Eddya alizungumza kwa sauti ambayo sio rahisi kwa mtu kuweza kuigundua kwa haraka haraka. Uso wa raisi Praygod ukatawaliwa na tabasamu baada ya kusikia maneno ya Eddy.
“Kweli kijana?”
“Kweli muheshimiwa, nilihakikisha kwamba wanavyuo wanakuchagua na kuhitaji mabadiliko ya kisiasa. Hatuwezi vijana tangu tunazaliwa tuwe tunatawaliwa na chama kimoja”
“Unachukua fakati gani?”
 
“Nachukua utawala bora”
“Ahaaa, sawa sawa. Hivi unauonaje uongozi wangu?”
“Kusema kweli machoni mwa watu wengi wanaweza kusema uongozi wako unamapungufu. Ila kwa sisi waelewa tunaelewa uongozi wako ni mzuri kwa maana serikali yetu inapunguza matumizi ambayo si ya msingi. Kwa mfano hili swala la kutaka kuibadili nchi na kuwa nchi ya kifalme, ninakuunga mkono wa asilimia mia”
 
Eddy alizungumza kwa kuajiamini na kumfanya raisi Godwin kuzidi kufurahi pasipo kugundua kwamba Erickson Forrd ndio Eddy Godwin mwanaye wa pekee wa kiume ambaye ni adui yake namba moja.
“Unajua muheshimiwa, ukiweka nchi kuwa na uongozi wa kifalme, tutapiga hatua kubwa ya kiuchumi. Tazama Uingereza hadi leo wanamilikiwa na Malikia. Tazama uchumi wao ulipo kwa sasa. Wapo mbali sana muheshimiwa, na mimi ninazidi kukuunga mkono hata chuoni nitahakikisha kwamba uongozi unabadilika”
Muda wote Eddy akizungumza John alimtazama kwa umakini mdomoni mwake, akataka kuzungumza kitu ila akanyamaza.
 
“Unaonekana upo vizuri kijana”
“Kidogo tu muheshimiwa”
“Na unasoma chuo gani?”
“Ninasoma Mlimani”
“Ahaaa kumbe ni hapa hapa Dar es Salaam”
“Ndio muheshimiwa”
“Basi nitafanya mawasiliano na wewe ili tuyazungumze mengi”
Raisi Godwin kwa ishara akamuita mlinzi wake na kumnong’oneza kitu. Mlinzi wake akatoa kadi ya mawasiliano na kumkabidhi raisi kisha raisi Godwin akampatia Eddy.
“Tutawasiliana kijana hii ni namba ya simu yangu ya mkononi”
“Asante sana muheshimiwa”
“Hivi umesema unaitwa nani?”
“Erickson Forrd muheshimiwa”
“Jamani naona mtoto wetu leo anahitaji kuzungumza kitu, ngoja nimpatie maiki”
 
Mshereheshaji alizungumza na kuwafanya Eddy na raisi Godwin kuangalia alipo Agnes, aliye kabidhiwa maiki namshereshaji. Agnes akasimama kwenye kiti huku macho yake akimtazama Eddy aliye kaa meza moja na raisi Godwin.
“Napenda kuwashukuru jamani kwa kuweza kunifanyia sherehe hii, ambayo siku ya leo kwangu ni muhimu sana kwangu. Nikisema niwataje mmoja mmoja basi nahisi nitataja ukumbi mzima. Ila kusema kweli shukrani yangu inatoka ndani ya moyo wangu.”
 
Agnes alizungumza na kuwafanya watu wote ndani ya ukumbi kuwa kimya na kuendelea kumsikiliza kwa kile ambacho anakizungumza.
“Katika maisha yangu, naamini rafiki zangu wa karibu hawajawahi kusikia wala kuniona nikiwa nina mchumba. Ila leo ninahitaji kuwaeleza hili. Nina mchumba  wangu na yupo hapa, nitakapo mtaja basi nitaomba aje hapa mbele watu wote mumuone”
Eddy kidogo mapigo ya moyo yakamuenda kasi kidogo ila akajikaza na kujidai kama sio yeye ambaye atakwenda kutajwa.
“Laazizi wangu, Asali wangu, mume wangu mtarajiwa Erickson Ford popote ulipo ninakUomba unyanyuke”
Watu wote wakaanza kutazama tazama, raisi Godwin na John wakabaki wakimkodolea macho Eddy waliye kaa naye kwenye meza moja.
 
“Kumbe ni wewe bwana mdogo?”
Raisi Praygod alizungumza huku akitabasamu na kumtazama Eddy aliye achia tabasamu pana. Eddy akatingisha kichwa na kusimama taratibu, akaanza kupiga hatua za taratibu hadi alipo kaa Agnes, aliye mkumbatia kwa muda kisha akamuachia. John sura yake dhairi ikaonyesha kujawa na hasira kwa kitendo hicho hadi raisi Godwin akakigundua.
“Vipi mbona umekasirika ?”
“Ahahaa hapana muheshimiwa”
John alizungumza kwa kuzuga, ila kusema kweli moyoni mwake kwa haraka ametokea kumchukia Erickson Forrd, hii yote ni kutokana na hisia za mapenzi alizo kuwa nazo juu ya Agnes, ila ukaaji kimya wake ndio ulio mponza.
‘Erickson Forrd lazima nikuue’
 
John aliwaza huku akimtazama Eddy jinsi anavyo lishwa kipande cha kike na Agnes. Si John peke yake bali hata Manka aliyte kaa viti vya nyuma kidogo hasira kali, ikazidi kuutesa moyo wake, kwa mara kadhaa akawa anafikiria ni jinsi gani anavyo weza kumuangamiza Agnes ili kubaki na Erickson Forrd peke yake.
‘Lazima nimuue, Erickson ni wangu. TENA WANGU PEKA YANGU’
Manka alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, kiasi kwamba akatamani anyanyuke na kwenda kuwatengenisha Erickson na Agnes wanao pigana mabusu kiholela holea. Sherehe ikazidi kuendelea hadi ikafikia tamati. Raisi Godwin akawafwata Eddy na Agnes walipo simama kwa ajili ya kuwaaga.
 
“Agnes hongera, umechagua kijana mzuri sana”
“Asante sana muheshimiwa nakushuru sana kwa kuweza kuhudhuria”
“Usijali, unajua nilikwenda Marekani kwa ajili ya mapumziko, ila Manka alipo nieleza juu ya sherehe yako ikanilazimu jana turudi”
“Asante sana muheshimiwa, umenipa nafasi ambayo ni ya pekee sana”
“Usijali wewe ni kati ya watu ninao waheshimu na kuwajali sana, ingeuwa si vyema kama leo nisinge weza kuhusika katika hafla hii, naamini usinge jisikia vizuri”
“Hapana muheshimiwa, mimi ni muelewa kwa maana sikutegemea kabisa ujio wako”
 
“Usijali, Erickson Forrd ngoja mimi niwaache mukapumzike. Ila kesho wasiliana na mimi na kama ikiwezekana njooni  wote ikulu tuzidi kuyajenga”
Raisi Praygod alizungumza huku akimpa mkono Eddy, ambaye kwa haraka akaupokea huku akiwa na furaha kubwa ambayo furaha yote ni feki, kwani kisasi na chuki dhidi ya mzee Godwin imejaa moyoni mwake.
“Asante sana muheshimiwa nina amini bibie atanileta”
“Haya ngoja tuondoke nawatakia usiku mwena”
“Nawe pia muheshimiwa raisi”
 
Eddy akamtazama kwa macho makali jinsi raisi Praygod wanavyo ongozana na John anaye sukumwa kwenye kiti cha matairi na mlinzi wake.
“Honey mbona umewakazia macho”
“Ahaa hapana honey katika maisha yangu sijawahi kuonana na raisi uso kwa uso”
“Kweli mpenzi wangu”
“Kweli siwezi kukutani, leo ndio mara yangu ya kwanza”
Eddy aliongopea ila anacho kijua moyoni mwake ni kulipiza kisasi dhidi ya Mzee Godwin pamoja na John ambaye amepunyuka punyuka katika kisasi cha kwanza alicho kuwa anahitaji kuweza kumfanyia.  Agnes na Eddy wakaondoka na kuelekea katika hoteli walio lipiwa kama zawadi ya kwenda kustarehe kwa siku mbili mfululizo.
                                                                                                                   ***
   John njia nzima akiwa kwenye gari pamoja na mlinzi wake aliwaza ni jinsi gani ya kumuuErickson Forrd, kwa maama ameingia katika kumi na nane zake. 
 
“Ninakazi ambayo ninahitaji kukupatia”
John alimuambia mlinzi wake, kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo mingi dhairi akionekana kusumbukiwa na jambo fulani moyoni mwake ambalo hakulihitaji kuliweka wazi kwa mtu yoyote kwani, katika maisha yake hakuwahi kujikuta akiingia kwenye hisia hali za mapenzi kama alizo hizo.
“Kazi gani bosi?”
“Ulimuona yule kijana anaye itwa Erickson Forrd?”
“Ndio bosi nilimuona”
“Nahitaji umfwatile hatua kwa hatua, kila detail zake ninaomba uniletee”
“Sawa muheshimiwa”
“Na akionekana humuelewi, hakikisha unampoteza”
“Sawa mkuu”
                                                                                                                    ***
   Si Phidaya wala Shamsa aliye weza kupata lepe la usingizi, kila mmoja akili yake ameielekezea kwa Eddy. Kila mmoja aliamuwazia jinsi Eddy anavyo banjuka na mwanamke ambaye anaye kwa usiku huo. Shamsa maumivu aliyo yapata yaliweza kujidhihirisaha hadi usoni mwake na kumfanya Sa Yoo kuweza kumuuliza ni kitu gani kinacho endelea.
“Ahaaa wee acha tu”
“Si wezi kuacha tu, ikiwa ninakuona unajambo ambalo linakusumbua. Ni vyema tuzungumze kwa pamoja kama ni mawazo niweze kukusaidia”
“Sa Yoo si kila jambo ni la kukushirikisha wewe, mengine ni mambo binafsi”
 
Shamsa alizungumza huku kwa mbali machozi yakimlenga lenga. Sa Yoo akaka kitako kitandani, akamuangalia vizuri, taratibu Sa Yoo akashuka kitandani na kwenda hadi sehemu ilipo swichi, akawasha taa na kurudi kurudi kitandani.
“Shamsa nakuomba uzungumze, ni nini kinacho kusumbua eeheee”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akimnyanyua Shamsa kutoka kitandani. Kichwa cha Shamsa akakiweka kwenye bega lake..
“Niambie sasa, ni nini kinacho kusumbua rafiki yangu?”
“Ni Eddy”
“Eddy kafanya nini?”
Shamsa akashusha pumzi kidogo huku akijifuta machozi usoni mwake.
 
“Eddy ana mwanamke mwengine”
“Sasa Shamsa huyo mwanamke ambaye anaye si anatusaidia katika kuikamilisha kazi yetu”
“Ndio Sa Yoo, ila roho yangu inaniuma”
“Inakuuma kwa nini sasa?”
“Bado ninampenda Eddy, huyu ndio Black Shadow wangu. Upendo wangu kuondoka kwake ni ngumu kama unavyo fikiria”
Sa Yoo akajikuta akishusha pumzi kidogo huku akimtazama Shamsa anaye endelea kutiririkwa na machozi.
“Lakini Shamsa, si umesha ufahamu ukweli kwamba Eddy ni baba yako, inakuwaje sasa bado una hisia za mapenzi juu yake?”
“Hata kama ukweli ni kwamba tayari amesha nivunja bikra yangu?”
“NI NANI AMEKUVUNJA BIKRA YAKO?”
Sauti ya Phidaya ikawastua wote na kujikuta macho yao wakiyaekekezea mlangoni, na kumuona Phidaya akiwa amesimama huku akiwa amevalia nguo zake za kulalia.
                                                                                                                 ***
    Asubuhi na mapema Eddy akawa wa kwanza kuamka kitandani, moja kwa moja akaelekea bafuni, akaoga kisha akarudi chumbani akavaa nguo zake alipo hakikisha amemaliza, akamtazama Agnes kwa muda akamtingisha huku anamuita.
“Honey honey”
“Mmmmmmm”
Agnes aliitika kivivu huku akijigeuza kitandani na kumtazama Eddy usoni.
 
“Nahitaji kwenda nyumbani kwangu mara moja”
“Kwa nini jamani, wakati tunakaa hapa siku mbili”
“Nalitambua hilo mpenzi, nakwenda kuchukua nguo. Unahisi ikulu tutakwendaje”
“Mmmm kama ni hivyo tutakwenda kununua madukani”
“Mmmm honey kuna vitu nahitaji kuvikamilisha asubihi ya leo kisha nitatarudi kabla ya saa nne asubuhi”
“Sawa naomba unibusu”
Eddy taratibu akamuinamia Agnes na kumbusu mdomoni.
“Usichelewe mume wangu”
 
“Sawa”
Eddy akatoka chumbani, akaingia kwenye moja ya lifti iliyopo hapo gorofani. Akashuka hadi chini moja kwa moja akaelekea kwenye gari lake.  Kitu cha kwanza kukifanya akaiwasha simu yake, kwa haraka akaitafuta ni sehemu gani ilipo namba ya raisi Praygod, akampigia.
“Habari za asubihi muheshimiwa?”
“Salama, vipi mpango waku upo vipi?”
“Nimefanikiwa kuonana na raisi Godwin, cha kumshukuru Mungu hajanistukia. Na kikibwa zaidi amenipatia namba yake ya simu”
 
“Kweli?”
“Ndio muheshimiwa na hapa amehitaji leo niweze kwenda ikulu kuonana naye”
“Safi sana ni mwanzo mzuri ninaimani kazi inakwenda kuwa rahisi kwa upande wetu”
“Ni kweli hapa nahitaji kurudi huko nibadilishe nguo, kisha nionana na huyu mwanamke, ila mke wangu nikionana naye nahisi uchungu mwingi moyoni mwangu”
“Basi usirudi nyumbani cha kufanya tuonane Mlimani City tuzungumze”
“Kwa nini nisirudi?”
“Kwa maana ukimuona Phidaya unaweza kushindwa kuifanya kazi yako, na kumbuka kuna shambulizi leo limepangwa kufanywa kwenye onyesho la huyo msanii”
“Kweli muheshimiwa nitajitahidi kuhakikisha halifanikiwi”
“Sawa tuonane Mlimani City”
 
Eddy akakata simu, akawasha gari lake na kuondoka eneo hilo la hotelini. Mlinzi akafungua geti na Eddy kuondoka, safari ya Mlimani City ikianza. Akiwa njiani akahisi kuna gari nyeusi inamfwatilia, tangu alipo toka pale hotelini, ila hakuitilia mashaka sana kwa maana anajiamini kutokana na sura ya bandia aliyo kuwa nayo. Hadi anafika Mlimani City, gari hiyo bado ilizidi kumfwata, akaegesha gari lake kwenye maeneo ya maegesho, gari hilo nalo lilifika kwenye maegesho likasimamishwa.
 
Eddy akashuka kwa kujiamini moja kwa moja akeleeka kwenye mgahawa wa Samaki Samaki, akatafuta sehemu na kukaa. Mwanaume mwenye asili ya kizungu akashuka kwenye gari hilo jeusi, naye akaenda kuketi kwenye moja  ya mgahawa uliopo karibu na mgahawa wa Samaki Samaki.
 
Haukupita muda mrefu Raisi Praygod akiwa amevalia kofia kubwa ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kumtambua akafika eneo hilo akiwa ameongozana na Rahab aliye valia dera na kujitanda mtandio. Moja kwa moja wakafika katika meza aliyo kaa Eddy.
“Karibuni”
Eddy alizungumza huku akiwapa mikono. Wakakaa kwenye viti na kuagiza kinywaji walicho kihitaji kwa wakati huo.  
 
“Jamani inakwenda kuwa rahisi sana”
Eddy alizungumza huku akitabasamu.
“Wewe ndio utakayo ifanya iwe rahisi na wewe ndio utakayo ifanya iwe ngumu”
“Kwa nini unasema hivyo Rahab”
“Kwa sasabu uhalisia wako endapo utajulikana basi tambua kila jambo kwetu litaharibika”
“Ni kweli ndio maana najitahidi uhalisia wangu usiweze kujulika”
Muda wote wakiwa wanazungumza raisi Praygod macho yake, akawa anayaangaza angaza, hadi kwenye mgahawa wa pili, akamshuhudia mwanaume mwenye asili ya kizungu akinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia na kuelekea kwenye maesho ya magari.
 
“Nakuja”
Raisi Praygod alizungumza huku akinyanyuka, akaelekea kwenye kiti alicho kuwa amekalia mwanaume huyo wa kizungu na kuisahau simu yake inayo onekana ni ya gharama sana. Raisi Praygod akaitazama kwa sekunde simu hiyo, kisha akaichukua, kitendo cha kupiga hatua mbili mbele, simu hiyo ikatoa kijimlio, huku kwenye kioo chake sekunde zilizo baki tatu zikaanza kurudi nyuma na kumfanya raisi Praygod kushangaa. Hadi inafika sekunde sifuri, mlipuko mkubwa ukatokea eneo hilo na kusambaratisha kila aliye kuwepo katika eneo hilo.

 SORRY MADAM (83)  (Destination of my enemies)

 Ukimya wa takribani dakika tano ukatawala eneo zima la Mlimani City. Eddy kwa mbali akaanza kufumbua macho yake, kuangalia kitu kilicho toke. Moshi mwingi mweusi, uliendelea kutawala katika anga zima la mlimani city. 

Vilio na kelele za ving’ora vya zima moto vikaendelea kusikika masikioni mwa Eddy, anaye jizoa zoa kunyanyuka kutoka chini alipo angukia, ambapo ni umbali mkubwa sana kutoka sehemu alipo kuwa amekaa. Kizunguzungu, kikali kikaanza kumuandama Eddy kila alipo jaribu kusimama, alijikuta akiyumba. Eneo zima lililokuwa na mgahawa uliopo pembezoni mwa mgahawa wa samaki kujijaa damu nyingi za watu walio kuwa katika sehemu hiyo. Taratibu Eddy akajikaza hivyo hivyo na kusimama wima.
“Raisi”
Ndio kitu cha kwanza Eddy kuweza kukifikira, akaanza kutembea huku akiyumba yumba kwa kizungu zungu, ila akazidi kujikaza.
 
“Mr hutakiwi kuingia sehemu hii sio salama”
Askari mmoja alijaribu kumzui Eddy katika kuingia katika eneo lilipo tokea mlipuko, ila Eddy akamsukumia mbali askari huyo na kuzidi kutembea kwa kuyumba yumba. Macho yake yaliweza kushuhudia jinsi vipande pande vya nyama za wanadamu vilivyosambakaa chini, huku damu ikiwa ni nyingi sana. Eddy akaweza kuona kiatu cha raisi Praygod alicho kuwa amekivaa kipindi amekuja eneo hilo kikiwa kimebakia na kipande cha mguu wa raisi. 
 
“Ohooo Mungu wangu”
Eddy alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, hakuamini kitu kilicho tokea. Waandishi wa habari nao hawakucheza mbali, mara moja wakaweza kufika katika eneo la Mlimani City na kuyarusha matangazo hayo moja kwa moja kwenye vituo vyao ya televishion na radio. Eddy akahisi nguvu zikimuishia, baada ya kuuona kiwili wili cha kati cha raisi Praygod kikiwa hakina mikono, huku kichwa chake kikiwa kimechanguliwa vibaya sana.
“Khgaaaaaaaaaa”
Eddy alipiga ukunga mkubwa huku akikaa chini machozi yakimwagika kama mtoto mdogo. Wanajeshi na askari walio weza kufika eneo hilo, wakajitahidi kumtoa Eddy katika eneo hilo huku wakiwasaidia watu wengi walio jeruhiwa vibaya mno.
                                                                                                 ***
“Ahaa….ahaa hakuna mama ni stori tu”
Sa Yoo akawa mtu wa kwanza kuweza kujibu swali la Phidaya alilo ulia akiwa anaingia ndani ya chumba chao pasipo kubisha hodi.
“Mmmm ya kweli hayo?”
Phidaya alizungumza huku akikaa kitandani, macho yake akimtazama Shamsa anaye endelea kuyapangusa macho yake akionekana kuwa kuja jambo ambalo linamsumbua.
 
“Ndio madam”
“Shamsa kuna kitu gani ambacho kina kusumbua?”
“Hakuna mama”
“Shamsa ninakutambua wewe na ninakuelewa, kuna jambo ambalo linakusumbua nieleze mimi ni mama yako. Hata kama kuna mwanaume amekuumiza nieleze niweze kukupa ushauri”
“Hapana mama ni stori ya nyuma ndio niliikumbuka ikaniumiza moyo wangu”
“Inahusiana na mapenzi?”
“Ndio”
Phidaya akatabasamu huku akimtazama Shamsa usoni mwake, taratibu akaupeleka mkono wake wa kuli hadi kwenuye uso wa Shamsa, akamfuta machozi ambayo yanatiririka tena kwenye uso wake.
 
“Wanaume ni watu ambao mioyo ya wanawake wanaichukulia ni kama eneo la majaribio katika maisha yao. Wapo tayari kumtumia mwanamke na kumuumiza ili mradi tu waweze kufanikiwa katika mpango ambao anahitaji kuufanya hadi ufanikiwe”
Phidaya alizungumza kwa sauti iliyo jaa usikivu mkubwa na kuwafanya Shamsa na Sa Yoo kumsikiliza kwa umakini huku wakimtazama usoni.
“Pia wanaume ni watu ambao, pasipo sisi kuweza kuwaelekeza na kuwaeleza juu ya hisia zetu usidhani wanaweza kuziheshimu. Mwanaume ni sawa na mtoto, hata kama anafanya kosa unatakiwa kuweza kumuelewa na kumshauri juu ya hilo na akabadilika”
 
“Eddy ni mume wangu, tena ni mwanaume wa ndoto zangu. Eddy katika maisha yake yote hakuweza kuishi kwa furaha na amani zaidi ya kunihangaikia mimi na marehemu mwanangu Junio”
Phidaya alizungumza huku machozi yakimlenga lenga na kumfanya Shamsa kuzidi kumwagikwa na machozi.
“Eddy ninampenda kuliko hata maisha yangu, nipo tayari kufa kwa ajili yake. Hata swala hili ambalo analifanya analifanya kwa uchungu na maumivu makali moyoni mwake, naelewa sababu ya yeye ni kwanini akija hapa haitaji kuzungumza na mimi muda mrefu”
 
“Ila mama si kwamba anakuwa na mama mwengine na atakuacha wewe”
Swali la Shamsa likamfanya Phidaya kutabasamu kwa muda huku akimtazama Shamsa usoni.
“Eddy ananipenda, ila kazi hii ikimalizika ninaamini tutaishi kwa amani na upendo”
“Jamani tubadilisheni mada”
Sa Yoo alizungumza baada ya kuona Shamsa na Phidaya wametawaliwa na huzuni kubwa kati yao. Sa Yoo akasimama, akavaa jinzi yake haraka haraka pamoja na tisheti yake. 
 
“Unakwenda wapi?”
“Nakwenda kaunta kuchukua vinywaji. Madam unakunywa nini?”
“Niletee red’s”
“Shamsa na wewe?”
“Na mimi niletee hicho hicho kinywaji alicho kihitaji mama”
“Ok dakika sifuri nitakuwa nimesha rudi”
Sa Yoo akavaa vindala vya kuogea na kutoka chumbani hapo, akatembea kwa haraka hadi kwenye kaunta ya vinywaji, akaagizia vinywaji anavyo hitaji, Akachukua katoni mbili za bia hizo za kopo na kurudi nazo chumbani. 
 
“Yaani hapa tungepata na nyama choma, zingeenda kama nini”
Phidaya alizungumza huku akitabasamu, baada ya vinywaji hivyo kuwekwa mezani.
“Ohooo ungeniambia madam, basi ngoja niende kutoa oda jikoni”
“Ahaaa ngoja niwapigie simu”
Shamsa alizungumza huku akishuka kitandani, akachukua mkonga wa simu ya mezani, akaminya namba zinazo onyesha zainahusiana na watu wajikoni katika hoteli hiyo.
“Ninahitaji nyama choma ya ng’ombe kilo tatu”
 
Shamsa alizungumza na muhudumu, aliye hitaji kuelezwa oda hiyo inatokea chumba namba ngapi, Shamsa akamueleza namba ya chumba.
“Ohooo ngoja ngoja. Weka kachumari nyingi pamoja pilipili”
“Weee Shamsa, muambie pilipili aweke pembeni”
Sa Yoo aliingilia mazungumzo hayo ya Shamsa na muhudumu wa jikoni.
“Pilipili weka pembeni, na usiniwekee mifupa fupa, weka steki ya kutosha “
“Sawa ndugu mteja”
Shamsa akaurudisha mkonga wa simu hiyo alipo utoa, akawageukia Phidaya na Sa Yoo na kuwakuta tayari kila mmoja amesha fungua bia yake na kuendelea kunywa taratibu.
 
“Jamani mumesha anza kunywa”
“Ndio njoo uchukue ya kwako”
Shamsa akachukua kopo moja la bia, akafungua na kuanza kunywa taratibu, yote wanayafanya kwa kupoteza mawazo ya mambo yanayo endelea. Baada ya robo saa mlango ukangongwa, Sa Yoo akanyanyuka na kuufungua mlango, akakuta muhudumu wa hoteli akiwa amewaletea nyama walizo ziagiza. Akamruhusu kuingia ndani, alipo weka chakula hicho meza, akampatia pesa ya chakula hicho na muhudumu akatoka.
 
Wakaendelea kunywa huku wakipiga stori ambazo hazina mbele wala nyuma, kila aliye jisikia kuzungumza aliweza kuzungumza.  Wa kwanza kupitiwa na usingizi akiwa amejawa na kilevi ni Phidaya mbaye pombe hajaizoa sana. Shamsa na Phidaya wakaendelea kupiga stori za hapa na pale na wao wakajikuta wakipitiwa na usingizi na kulalal fofo.
 
     Kwa jinsi mlango unavyo gongwa kwa nguvu, ukamfanya Sa Yoo kunyanyuka akiwa na malepe ya usingizi. Kitu cha kwanza kukitazama ni dirisha, mwanga mkali wa jua unao ingia katika chumba chao ukamtamjulisha tayari kumesha pambazuka. Kabla ya kunyanyuka kwenye kochi alilo kuwa amekalia, akashangaa mlango ukafunguliwa, na madam Mery akaingia akinekana kuhema na wasiwasi mwingi ukiwa umemtawala.
 
“Madam Mery kuna nini mbona hivyo?”
“Washa washa Tv uoneeee”
Madam Mery alizungumza huku mikono na macho yake yote akiyaelekezea kwenye Tv iliyopo ndani ya chumba hicho. Sauti ya madam Mery ikawaamsha Shamsa na Phidaya ambao hadi madam Mery anaingia ndani humo bado walikuwa wamelala. Sa Yoo akachukua rimoti ya Tv, akaiwasha na kusimama huku akitazama Tv hiyo.
 
“Weka chaneli ten”
“Ni namba ngapi?”
Madam Mery alipo ona Sa Yoo ana maswali mengi kwa haraka akaichukua rimoti ya king’amuzi na kuweka chaneli ten na wote wakabaki wakitazama taarifa hiyo ya dharura(Breaking News), inayo rushwa muda huu. Gafla Phidaya akasimama wima, wenge lote la pombe likakata kichwani mwake, macho yakamtoka na kupiga hatua mbili mbele kuangalia vizuri mtu anaye muona ndio yeye au ni pombe alizo amka nazo.
“Huyu si Eddy?”
Phidaya aliuliza huku akimtazama Shamsa aliye itikia kwa kutingisha kichwa na kuwafanya waanze kuchachawa kwa wenge.
 
“Ni nini kimetokea Mery?”
“Bomu, bomu limelipuka”
“Wapi?”
“Mlimani City”
“Ohooo jamani mume wangu”
“Jamani twendeni twendeni”
Wote wakatka pasipo kujali kama Phidaya amevaa nguo za kulalia zinazo muonyesha  nguo zake za ndani alizo vaa. Wote wanne wakakimbilia hadi kwenye maegesho ya madereva taski, wakavamia kwenye moja ya taski na kuingia pasipo hata kukaribishwa na dereva taski.
“Niwapeleke wapI?”
Dereva taksi alizungumza mara baada ya kuwaona abiria wake wakiwa ameingia hata ya kutoa salamu, kwa haraka haraka akagundua kwamba wateja wake wana matatizo.
 
“Tupeleke mlimani City?”
“Jamani Mlimani City mimi siendi kuna mabomu huko”
Dereva taksi alizungumza huku akizima gari lake mara baada ya kusikia habari ya kwenda Mlimani City.
“Wee kaka fala kweli mbona kuna waandhisi wa hahbari hembu tupeleke bwana usituletee mambo ya kifala”
Shamsa alizungumza kwa kufoka, ndio kwanza dereva taski akashuka kwenye gari na kufunga mlango wa ke alio tokea. Kwa haraka Shamsa akashuka kwenye gari akiwa amejawa na hasira, akazunguka upande wapili wa gari na kumshika tai dereva taski aliye baki ameshikwa na mshangao mkubwa.
 
“Inakuwaje dada yangu, huvi unataka na mimi niende kufa huko ehee”
Derevs taksi alizungumza huku akimtoa  Shamsa mikono yake kwenye kifaa chake.         
“Shamsa, Shamsa achana naye bwana twende kwa mwengne”
Sa Yoo alizungumza huku akiongoza kwa madereva taksi wengine waliopo upande wa pili wa barabara. Sa Yoo akamueleza mmoja wao juu ya safari ya kwenda Mlimani City, ila kila mmoja akaonekana kusita sita.
“Dada kama unalaki na nusu twende”
“Sawa twende”
Dereva taksi huyo alikubali na kumfanya Sa Yoo kuwaita wezake walio vuka varabara na kwenda kuingia kwenye taski hiyo, na kuondoka kwa mwendo wa kasi katika eneo hilo.
                                                                                                            ***
Mlio wa simu inayo ita, ukamuamsha Agnes kitani, taratibu akapapasa pembeni ya mto wake, akaichukua simu hiyo huku akiwa na tabasamu akitambu anaweza kuwa ni Erickson mpenzi wake aliye toka na kumuacha akiwa amelala kitandani. Akakuta ni namba ya Halima, akashusha pumzi kidogo huku akiitazama namba hiyo, akaipokea na kuiweka sikioni mwake. 
 
“Hallooo”
“Shosti upo na Erickson wako hapo ulipo?”
“Mmmmm Halima umesha anza, asubuhi asubuhi yote hii unamuulizia mume wangu”
“Hapana sina nia hiyo ya kumuulizia yeye, nijibu yupo au hayupo, ili nijue kama nimemfananisha au laa”
Agnes kusikia hivyo kwa haraka akaka kitako kitandani ili kujua Halima anamaanisha nini kwa maana wivu wa mapenzi tayari umesha utawala moyo wake na akili yake ikaanza kuwaza labada Erickson yupo na mwanamke mwengine.
“Hayupo ameondoka hapa asubuhi na mapema”
“Si upo karibu nba Tv?”
“Ndio”
“Hembu iwashe na weka ITV”
“Kuna nini kwani?”
“Wewe washa utajionea wewe mwenyewe, nisije nikakupa presha bure”
 
Kwa haraka Agnes akashuka kitandani, akachukua rimoti ya Tv, akawasha haraka haraka kwa bahati nzuri, king’amuzi jana usiku walisahau kikizima na chanel walio kuwa wakiitazama ni hiyo hiyo ITV. Macho yakamtoka Agnes, baada ya kuona habari hiyo ya kuogopesha juu ya mlipuko wa bomu ulio tokea Mlimani City. Katika kutazama tazama akamuona Erickson akiwa ananyanyuliwa na askari, huku akilia kwa uchungua, akijitahidi kutoa kuondoka katika eneo lililo jaa damu.
 
Agnes bila ya kujiuliza mara mbili, akavaa nguo zake haraka haraka, akatoka ndani ya chumba chake huku simu yake ikiwa sikioni akimpigia Erickson. Simu ya Erickson, iliita pasipo kupokelewa. Mapigo ya moyo yakazidi kumenda kasi Agnes, kwa mbali machozi yakimlenga lenga machoni mwake. Kitu kilicho mtoa wasiwasi ni jinsi alivyo muna Erickson wake kwenye Tv, na hicho ndicho kinacho mfanya atembee kwa kasi kuelekea nje ya hoteli hiyo. Akatoka kwenye lifti huku akiendelea kupiga simu ya Erickson ila haikupokelewa, kitendo kilicho zidi kumpa wasiwasi. 
 
“Nipeleke Mlimani City”
Agnes alimuambia dereva bodaboda, ambaye alibaki kumshangaa kwa maana anamtambua vizuri kwamba huyu ni waziri.
“Unanitolea nini mimacho nipeleke Mlimani City”
Agnes alizungumza kwa sauti ya kufoka na kumfanya dereva huyo wa bodaboda kusha pikipiki yake haraka, Agnes akapanda, hakujali mpasuo wa gauni lake, limeacha paja lake wazi. Yeye alicho kijali ni kuweza kufika mlimani City kwa muda huo.
“Ongeza kasi wewe, unaogopa hapo kupita eheeee”
Agnes alifoka, baada ya bodaboda kusimama kusimama kwenye mataa ya Mwenge.
 
“Muheshimiwa magari hayajaruhusiwa ya upande wetu”
“Wewe ingia bwana acha woga wa kike kike. Mimi mtoto wa kike si muoga wewe dume zima ndio unaogopa”
Dereva bodaboda wa watu hakuwa na jinsi zaidi ya kuingia barabarani japo anatambua anahatarisha maisha yake na maisha ya mteja wake. Ila kutokana yupo na kiongozi akaamini usalama wake utakuwa upo pale atakapo kamatwa na polisi wa usalama barabarani. Dereva bodaboda akajitahida na kuendelea kuendesha kwa kasi huku akiyapita magari kwa kupenya penya.
 
Wakafanikiwa kufika mlamani City, Agnes akaruska kwenye pikipiki hata kabla haijasimama na kuwafanya watu wote walio ona tukio hilo kushangaa, hadi dereva bodaboda anasimamisha pikipiki yake na kuangalia nyuma, hakumuona Agnes. Akaangaza macho yake huku na kule akamuona Agnes akiwa amesimama kwenye geti alilio jaa askari ambao waliwazuia watu kuingia eneo la Mlimani City zaidi ya wakaruhuhu walio salimika kutoka.
“Mimi waziri”
Agnes alimfokea askari mmoja aliye jaribu kumzuia.
“Hata kama huruhusiwa kuingia humu ndani si eneo la salama”
 
Agnes akamshushia kibao kizito askari huyo, aliye shangaa. Askari huyo akajaribu kurudisha kibao hicho, ila akashtukia akichotwa mtama mkali na Agnes ulio muangusha chini wezake wakabaki wamemtumbulia macho. Dereva bodaboda baada ya kuliona tukio hilo hata hamu ya kwenda kudai pesa yake ikamuisha kabisa. Agnes akapita pasipo askari yoyote kuweza kumzuia. Macho yake akawa anayaangaza huku na kule ndipo alipo weza kumona Erickson akiwa amezungukwa na askari wapata sita wakiwa na mitutu ya bundiki, wakimzuia kunyanyuka katika eneo hilo.
 
Kwa haraka Agnes akafika katika eneo hilo, akapita katikati ya askari na kumkumbatia Eddy kwa mapenzi mazito huku machozi yakimwagika usoni mwake.  Phidaya akwa wa kwanza kushuka kwenye taski hiyo iliyo chelewa chelewa kutokana na foleni za hapa na pale. Shamsa na Madam Mery wakafwatia kwa nyuma na kumuacha Sa Yoo akimlipa dereva taski aliye walete. Askari wakawazuia kuingia ndani kama wanavyo fanya kwa watu wengine.
 
“Twendeni huku”
Shamsa alizungumza huku akiongoza jahazi, wakeelekea hadi kwenye moja ya ukuta. Wakatazama pande zote na kuona hakuna askari wanaye mfwatilia. Kwa haraka wakapanda kwenye ukuta huo ulipo karibu na maegesho ya magari. Wote wakafanikiwa kuingia hadi Sa Yoo.  Ikabidi kusimama kwa pamoja kuangalia ni wapi wanaweza kumuona Eddy.
“Eddy…yu…..”
Sa Yoo hakumalizia sentensi yake kwa maana aliweza kumona Eddy akiwa amekumbatiwa na mwanamke wengine, tena mwanamke huyo akionekana kumpiga mabusu mfululizo kila sehemu ya uso wake. Madam Mery akafanikiwa kuona tukio hilo.
 
“Yupo wapi?”
Phidaya aliuliza, huku akitazama sehemu aliyo kuwa ameangalia Sa Yoo, Phidaya na Shamsa wote wakastuka kwa kumuona Eddy akiwa anadendeka na mwanamke mwengine, wote wawili kwa pamoja wakaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea katika eno alilo simama Eddy na Agnes, wanao dendeka pasipo kujali wingi wa watu walio kuwa katika eneo hilo.   


 ==>ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts