Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 07 na 08)

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 07 na 08)

Written By Bigie on Saturday, February 24, 2018 | 2:35:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   
“Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu aje kituoni?”
Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya. Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu, wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni.
“Jamani huyu ni jambazi”
Askari huyo aliuzungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama mimi huku wengine walio na bunduki kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha mikono juu kwa ukali sana.

ENDELEA
    Nikafwata kama wanavyo hitaji, nikainyoosha mikono yangu juu huku nikimtazama askari aliye nichomoa bastola yangu.
“Piga magoti wewe mjinga”
Askari mwengine alisisitiza kwa sauti ya ukali, taratibu nikapiga magoti. Askari huyo akachuka waleti yangu na kuifungua, akaanza kuikagua vitambulisho vyangu. Nikamuona akistuka baada ya kutoa kitambulisho changu cha kazi. Akanitazama mara mbili mbili huku macho yakimtoka na jasho likimwagika.
 
“Kuna nini kinacho endelea hapa”
Nilisikia sauti ya kike, nyuma yangu. Ikanibidi kugeuka na kumkuta mkuu wa polisi ambaye ninamtambua ni rafiki wakaribu sana na K2 na mara nyingi niliweza kumuona akija ofisini kwetu.
“Mkuu kuna huyu kijana alifanya fujo, ndio tumemleta hapa kituoni”
Mwanamama huyo mrefu kwenda juu, aliye valia suruali ya kaki pamoja na shati la kaki, lenye nyota kadhaa kwenye bega lake, akazunguka na kuja kusimama mbele yangu.
“Mumegundua nini?”
Alimuuliza askari aliye shika kitambulisho changu. Askari huyo akaonekana kupata kigugumizi na kujikuta mkuu wake akikichukua kitambulisho hicho na kukikoma. Akanitazama kwa haraka kisha akayarudisha macho yake kwenye kitambulisho hicho.
 
“Nani aliwapa oda ya kwenda kumkamata?”
Askari wote wakaka kimya. Kila mmoja alimtazama mwenzake, mwanamama huyo kwa ishara akaniomba ninyanyuke juu. Nikannyanyuka na kuwafanya askari wote kuduwaa.
“Mrudishieni kila kitu chake, unatoa toa macho ya nini?”
Askari aliye chukua waleti na bastola yangu, akanirudishia huku mwili mzima ukimtemeka. Sikulijali juu ya woga nikachukua kila kitu changu, nikavaa mkanda pamoja na viatu vyangu.
“Samahani kijana, naomba tukayazungumze ofisini kwangu”
Mwana mama huyo alizungumza huku akinitazama. Nilipo maliza kufunga kamba za viatu vyangu, nikaongozana naye hadi kwenye ofisi yake iliyopo gorofani. Akanikaribisha kwenye kiti kilichopo mbele ya meza yake kisha yeye akaka kwenye kiti kilichopo nyuma ya meza yake hiyo yenye mafaili mengi pamoja na meza ya mezani na simu ya upepo.
 
“Samahani kwa usumbufu wa vijana wangu, naona walikuchukua pasipo kujua kwamba wewe ni nani”
“Kwa hilo halina tabu, ni vyema nikaondoka na kwenda kuripoti kazini kwangu kwamba kazi yangu iliziwa na vijana wako”
“Hapana hapana, wachukulie ni vijana wezako wale. Endapo wataingia kwenye tabu wengine ndio kwanza hata pesa ya serikali hawajaitafuna”
“Kwa hiyo na mimi nikafukuzwe kazi kwa ajili ya vijana wako, unatambua kabisa kazi yangu ilivyo na uhatari wa hali ya juu, ila bado vijana wako wakaamu kuniharibia ndio nini sasa”
Nilizungumza kwa kumkoromea mama huyo baada ya kugundua amingiwa na hofu kidogo.
“Basi ngoja niweza kuzungumza na bosi wako, ili kukukingia kifua, si unajua tena sote sisi ni watumishi wa uma na kazi yetu ni moja”
Mama huyo alizungumza huku akichomoa simu yake aina ya Samsung Galaxy note 3. Akaminya minya baadhi ya namba ambazo sikuziona na kuiweka simu yake sikioni huku akinitazama usoni.
 
“Shosti vipi?”
“Safi vipi”
Kutokana na simu hiyo kuwa na sauti kubwa kidogo niliweza kuisikia sauti ya K2, nikatamani kumpokonya simu mama huyo ila nikajikuta nikishindwa na kubaki nikiwa nimemkazia macho.
“Safi tu, bwana nina ombi moja”
‘Ombi gani?’
“Kuna kijana wako hapa alikamatwa na vijana wangu akiwa kwenye kazi yake wakidai alifanya vurugu kwenye moja ya ofisi sasa nikaona nikujulishe mapema isije akaja huko ukawajibisha”
‘Anaitwa nani?’
“Anaitwa Daniel Thamson Kajenge”
‘Mmmmm’
“Mbona unaguna sasa?”
‘Hapana, upo naye hapo au amesha ondoka?’
“Nipo naye hapa ofisini kwangu”
‘Hembu mpatie simu’
Mama huyo akanipatia simu yake, taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Hallo”
“Hivi Dany unachanganyikiwa siku hizi?”
K2 alizungumza kwa ukali na kunifanya nimtazama mama huyo kwa jicho la kuiba nikagundua anayafwatila mazungumzo yangu kwa umakini.
 
“Hapana mkuu”
“Ni kitu gani kilicho kupeleka huko kituani. Mbona uinafanya kazi zako kipuuzi kama sio professional aliye fuzu mafunzo eheee?”
“Hapana mkuu haito jitokeza tena”
“Au unahisi kukupa ku* yangu ndio kunakufanya uwe unakuwa mbovu kwenye kazi, mbona hapo nyuma ulkuwa unafanya kazi zako kwa umakini eheee?”
K2 alizidi kunifokea hadi mama huyo nikaamini anayasikia mazungumzo hayo. Nikaka kimya kwani sikujua cha kumjibu K2 ambaye tangu asubuhi alisha nivuruga.
“Sasa hiyo ripoti hadi inafika kesho saa moja asubuhi ninaihitaji ofisini kwangu. Sasa wewe kaa kaa na kuwaza ku* na mku* wangu uone mwisho wake utakuwa ni nini. Utavuna upuuzi wako huo”
Simu ikakatwa, nikaishusha taratibu sikioni mwangu na kumkabidhi mwana mama huyo aliye baki akiwa amenikodolea macho.
“Hivi nilicho kisikia ni kweli au……?”
Mwana mama huyo alizungumza huku akiendelea kunikodolea macho yake. Sikuwa na kitu cha kumjibu zaidi ya kukaa kimya.
“Nakuomba niondoke tafadhali”
“Sawa unaweza kwenda”
Nikanyanyuka na kumuacha mwana mama huyo akinisindikiza kwa macho hadi natoka ofisini mwake. Nikashuka kwenye ngazi na kukutana na askari aliye kuwa akisoma kitambulisho changu cha kazi. Sikumsemesha kitu zaidi ya kumpita. Nikapita mapokezi kila askari akabaki akiwa amenikodolea macho. Moja kwa moja nikatoka kituoni. Kusema kweli akili yangu haikuwaza chohote zaidi ya kurudi nyumbani kwangu.
 
“Bosi nikupeleke wapi?”
Dereva mmoja wa pikipiki alisimama pembeni yangu huku akinitazama. Taratibu nikajikuta nikipanda pikipiki hiyo.
“Nipeleke Sinza kwa Remy”
“Sawa mkuu”
Dereva huyo mwenye pikipiki aina ya boksa akaanza safari. Hadi tunafika maeneo ya Sinza ndipo nikaanza kumuelekeza hadi mtaa ninao kaa. Nikamlipa kiasi alicho nitajia na kuingia ndani. Nikamkuta Mariam akiwa amekaa kwenye kibaraza anasikiliza miziki kwenye simu yake. Nikampita bila samu, na kwa jinsi shati lango lilivyo katika vifungo nahisi aliweza kujiuliza maswali.
Niakatiza kwenye kordo na kukutana na Asma akiwa anatoka kuoga, huku amejifunga tenga moja tu.
“Dany mambo?”
Asma alinisalimia huku akiwa na tabasamu pana usoni mkwa.
“Poa za kushinda?”
“Salama”
 
Sikutaka kukenua kenua meno, nikafika mlangoni mwangu. Nikafungua mlango na kuingia, nikaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine hadi nikabakiwa na boksa. Nikawasha feni na kujitupa kitandani, kilia nikiwaza jinsi ya kuifanya kazi niliyo pewa na ofisi nikajiona nimevuruga mpangilio mzima.
“Ohooo Mungu wangu nisaidie”
Nilizungumza huku nikiwa nimetizama juu. Sikuwa na jibu la uhakika wa nini nifanye. Mazingira ya chumba changu nilivyo yaacha asubuhi kwa muda huu hayaniridhishi kabisa. Nikaanza kuifanya usafi wa kubadilisha mashuka na kuweka shuka jengine, nilipo maliza hapo nikahamia kwenye kufagi na kufuta futa vumbi kwenye meza ya Tv pamoja na redio yangu. Sikuishia hapo nikavaa pensi na tisheti nikatoka nje nikiwa na ndoo ndogo nikinga maji nusu na kurudi nayo chumbani kwangu na kuanza kudeki kila sehemu.
    Nikamaliza kufanya usafi wangu huo, nikachukua nguo zangu zote chafu na kutoka nazo nje, nikiwa nimeziweka kwenye dishi langu. Nikaanza kufua, nikiwa ninaendelea kufua Asma akatoka akiwa amevalia suruali iliyo mbana makalio yake makubwa.
 
“Nakuona leo umeamua kuwa dobi”
“Yaa kidogo dogo si unajua maisha ya ubachela”
“Kweli ila unabidi ufanya uoe Dany, kazi ndogo ndogo kama hizo za kufua zitakuondokea”
“Ni kweli ila bado nipo nipo kwanza si unajua wanawake wa sanana ni pasua vichwa  na wengine hatupendi mambo hayo ya kuumizwa kichwa”
Asma akachukua kidoga kilichopo eno hilo la uwani ambapo kuna jiko la wamama kupikia. Akakaa pembeni ya tanki kubwa la maji lililopo hapa nyumani kwetu.
“Ni kweli, lakini kwa sasa hata wanaume munapasua vichwa. Wanake wanawapenda ila hampendeki sijui kwa nini?”
“Sio wote. Hivi jana ilikuwaje kwa jamaa kwa maana ninaona alitaka kukua?”
“Yaani Dany kaka yangu mimi nimesha jichokea. Mwanaume hapendeki, mwanaume ana wivu nashindwa hata nimfananishe na kitu gani. Yaani unavyo niona hapa hata kwenda kwa majirani hataki. Kila kitu amenunua na kuweka ndani, ni mimi na Tv na Tv na mimi, nikichoke ni kulala tu”
“Kwa nini auakuwa hivyo, hakuamini au?”
“Kigezo chake kwamba mimi ni mzuri kwa hiyo nikitoka nje watu wataniiba”
 
“Hahaaa sasa jana ilikuwaje hadi akakupiga?”
“Jana unajua kisa cha kupigwa ni kwamba. Tulikuwa tunaangalia myereka ya kina Jonh Cena, sasa mimi nikasema John Cena ni mzuri ana kifua kikubwa, basi hapo ndipo ugomvi ukaanza. Akaanza kuseme ohooo sijui umalaya umezidi hadi ninawasifia wanaume kwenye Tv ohooo kimepanda kimeshuka. Sasa nikawa ninamjibu mwenzangu kama ninamtania kumbe akachukulia serious, ndio akaanza kunipiga na kutaka kunichoma na kisu”
Mazungumza ya Asma yakanifanya nicheke na kujikuta hata mawazo ya kazini kwangu yakikaa pembeni kwa maana kwatika maisha yangu sikuwahi kuona wivu wa namna hiyo.
“Yupo wapi sasa mume wako?”
“Kasafiri kaenda Arusha, kapeleka mzigo wa mafuta”
“Mzigo wa mafuta?”
“Ndio mume wangu ni dereva wa magari makubwa yale ya mafuta, siku nyingine hupeleka mafuta Rwanda, Burudi, Congo”
 
“Ahaaa, sasa jana ulivyo rudi chumbani hakukoroma?”
“Wee ana ubavu, akikoroma tu namwambia ninakuja kukugongea basi anakaa kimya”
Nikamaliza kusuuza nguo zangu, Asma akaniomba kunisaidia kwenda kuzianika. Sikuwa na hiyana nikamuachia kindoo nilicho jaza nguo hizo na mimi nikamalizia kuyafua mashuka yangu.
“Asante mwaya”
“Usijali kaka yangu, sasa ngoja mimi niandae chakula cha usiku”
“Nihesabu basi”
“Usijali, ila unakula ndizi nyama wewe”
“Ahaa hapo mbona umenifikisha”
“Basi ngoja niandae chap chap, si unajua muda umesonga”
“Poa”
Asma akaondoka na kuniacha nikiwa ninasuuza mashuka yangu. Nikamaliza shuhuli hiyo na kuzunguka nyuma ya nyumba kwneye kamba za kuanikia nguo, nikaanika mashuka yangu na kurudi sehemu nilipo kuwa ninafulia. Nikamwaga maji ya mapovu chooni na kuanza kuyasuuza mabeseni hayo. 
 
“Nani amemwaga maji ya mapovu chooni?”
Mariam alizungumza huku akinitazama usoni, tambambua analifahamu jibu lake, ila anatafuta mbinu za kuzungumza na mimi. Sikujibu chochote zaidi ya kubeba mabeseni yangu yote na kurudi nayo chumbani kwangu. Nikayaweka chini ya uvungu na kujitupa kwenye sofa.
“K2 mamae ipo siku nitakuonyesha kwamba mimi mtoto wa mbwa”
Nilijikuta nikizungumza mazungumzo hayo huku nikikagua namba zilizo piga kwenye simu yangu kipindi nikiwa nipo nje ninafua, na namba ya K2 ni moja wapo.
‘Huyu ataniletea chakula kweli, au ana nizingua?’
Nilijiuliza swali hilo huku nikiwasha Tv kufwatilia taarifa ya habari ya saa mbili usiku inayo rushwa na kituo cha ITV.
   Hadi taarifa ya habari inamalizika saa tatu kasoro Asma hakuleta chakula chochote. Nikataka kunyanyuka kwenye sofa ili nijiandae kwenda kununua chakula ila, mlango wangu ukagongwa.
“Nani?”
“Mimi”
Nikasikia sauti ya Asma, kwa haraka nikanyuka na kwenda kufungua mlango. Nikamkuta akiwa amesimama huku mkononi mwake ameshika ‘hotpot’ kubwa pamoja na sahani isiyo na chakula.
 
“Karibu ndani, si vyema kupeana chakula mlangoni”
Asma akatabasamu na kuingia ndani. Moja kwa moja akaelekea mezani na kuweka ‘hotpot’ hilo mezani pamoja na sahani hiyo.
“Chumba chako umekipangilia vizuri, unaweza kusema unaishi na mwanamke”
“Unajua usafi mimi nilifundishwa tangu kipindi nipo sekondari ya bodi, kwa hiyo nimekulia kwenye mazingira ya usafi safi hadi hapa nilipo”
“Kweli Dany, kuna waaume ukiingia vyumba vyao utatamani kukimbia kwa manaa vimepangiliwa vibaya kama stoo”
Asma alizungumza huku akipakua chakula hicho, kinacho nukia vizuri hadi nikajikuta utumbo wangu ukitetemeka kwa njaa na hamu ya kula chakula hicho.
“Oooho nimesahau kijiko”
“Usijali kijiko ninavyo”
“Umeviweka wapi?”
Nikamuenyesha kiji trei cha kuwekea vyombo, akachukua kijiko kimoja na kuja kukiweka kwenye sahani ya chakula. Kabla hatujazungumza chochote sote wawili tukaisikia sauti ya Jumaa huko nje.
“Mariam umemuona wapo Asma?”
Nikamuona Asma akihisi kuishiwa nguvu, kutoka chumbani kwangu akwa anatamani kutoka ila anashindwa atatoka vipi kwa maana chumba change ndio cha kwanza kabisa kwa upande wa uwani isitoshe endpo atatoka na kukutana na mume wake basi inaweza kuzuka kesi nyingine ya kufikiriana vibaya.
 
  AISIIIII……….U KILL ME 08

“Jamani Dany nitafanyaje, huyo ni mume wangu?”
Asma alizungumza kwa sauti ya chini huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga, hata shuhuli ya kuniandalia ikakata. Kwa haraka haraka nikafikiria kitu cha kufanya. Nikatoka nje na kukuta Jumaa akiwa amesimama uwani, akanitazama kwa jicho kali linalo onyesha dhairi kwamba bado ana kinyongo na mimi. Mariamakanitazama kwa macho ya kuiba na kukaa kimya hata swali alilo ulizwa na Jumaa hakulijibu.
 
“Mariam mbona unanichunia, si nimekuuliza swali?”
“Mimi sijui ni wapi alipo mke wako”
Kabla Jumaa hajazungumza chochote, nje tukasikia kelele za watu. Kwa haraka Mariam akanyanyuka na kukimbilia nje, Jumaa naye akafwata wote wawili wakatoka nje. Nikarudi chumbani kwangu na kumkuta Asma akiwa amesimama, huku akiwa hana raha kabisa. Nikafungua pazia na kuchungulia kwenye kordo sikumuona mtu wa aina yoyote aliye simama.
“Njoo njoo”
Asma akanyata hadi sehemu alipo mimi, nikatazama tena hakuna mtu na mlango wa mbele ukawa umefungwa na si rahisi kwa mtu kumuona akitoka. Kwa haraka Mariam akatoka na kukimbilia uwani na moja kwa moja nikamshuhudia akikimbilia bafuni. Kidogo na mimi nikashusha pumzi na kupata amani kwa maana ninaamini kitu ambacho kingekwenda kudhaniwa na kila mtu ni kwamba mimi na Asma tuna mahusiano ya kimapenzi wakati si kitu sahhihi.
 
Kelele zilizidi kusikika nje na kujikuta na mimi nikitoka kwneda kuhushudia ni kitu gani kinacho endelea. Nikiwa nimefika mlango wa kutokea nje, kabla sijaufungua akaingia mama mwneye nyumba.
“Mama vipi huko kuna nini?”
“Nyuma yam zee Jongo inawaka moto”
Mama Mariam alizungumza kwa haraka haraka huku jasho likimwakia, akaingia chumbani kwake na kunifanya na mimi kutoka kwa haraka na kwenda kushuhudia. Nikatoka getina na kupishana na watu wengi wakikimbilia ilipo nyumba ya mzee Jongo. Na mimi nikaungana nao na kwenda hadi sehemu ilipo nyumba hiyo.
   Nikafika na kukuta nyumba hiyo ya kifahari ikiteketea kwa moto. Mwingi huku vijana na wamama wakijitahidi  kuuzima moto huo na kuokoa baadhi ya vitu vya garama vilivyomo kwenye nyumba hiyo.
 
“Jamani mwanangu”
Mzee Jongo alilalama huku machozi yakimwagika, watu cha kushangaza walibaki wakimkodolea macho. Kwa haraka nikamsogelea na kumuuliza mwanye huyo yupo wapi.
“Ndani baba yangu, gorofani kule”
Mzee Jongo alinijibu huku akinitazama usoni mwangu. Nikatazama moto huo unao endele kuteketea. Kwa haraka nikafanikiwa kuona sehemu ambayo ninaweza kuingilia na haina moto mwingi. Nikaanza kukimbia kuelekea ndani. Nikafika kwenye mlango wa uwani ambao wanautumia kama dharura, nikasukuma kwa kujirusha na kuanguka nao hadi chini. Moshi mwingi nilio kutana nao hakunizuia kuweza kuingia huku nikiwa nimebana pumzi zangu kwa umaridadi mkubwa kabisa ili nisiweza kuvuta moshi huo. Nikapandisha gadi gorofani, nikasikia sauti ya msichana ikilia kwenye moja ya chumba ambacho mlango wake umefungwa.
 
Nikajivuta nyuma kwa haraka na kuupiga teke mlango huo ulio funguka na kunipa nafasi ya mimi kuweza kuingia ndani. Nikamkuta binti mrefu akiwa ameanguka chini, hii ni baada ya mimi kuusukuma mlango wake. Kitanda chake kilisha anza kushika moto kitu ambacho kimemuokoa na kumuweka hai hadi sasa hivi ni ukubwa wa chumba chake na uchache wa vitu vya ndani.
“Panda mgongoni mwangu haraka”
Nilimuambia binti huyo ambaye mara nyingi niliweza kumuona akitoka kwenye nyumba hiyo ya kifahari siku za nyuma akitumia gari lake aina ya Harrier Lexux na ni msichana mwenye nyodo sana na asiye penda hata kusalimiwa na vijana wa hapa mtaani kwetu.
Akapanda mgongoni mwangu. Nilipo hakikisha amekaa vizuri, nikavuta pumzi nyingi itakayo nisaidia kutoka na kuupita moshi huo mwingi.
 
“Moja, mbili, tatuuuu”
Nikatoka kwa haraka na kuanza kushusha ngazi hizo zilizo tengenezwa kwa saruji. Moshi mwingi na mkali na uzito wa msichana huyualiye nishikila vizuri, vilichangia sana kuanza kunifanya nianza kuhisi kuishiwa na nguvu. Nikaanza kupita katika njia ambayo nilipita hapo awali, kwa bahati mbaya nikakuta apande wa mbao unao waka moto ukiwa umeziba mlango wa dharura hata mlango weyewe nilio kuwa nimeusikuma umeanza kushika moto.
“Shuka mgongoni upite”
“Eheee……?”
Binti huyo aliniuliza huku akizidi kuning’ang’ania kwa nguvu akionyesha ni dhairi kwamba anaogopa kabisa kushuaka. Ikanibidi kumshusha kwa nguvu kisha nikauchukua mlango ambao unawake moto, sikujali kama ninaungua au laa. Kwa kuutumia mlango huo nikaanza kusukuma mbao iliyo zuia hapo mlangoni.
Binti huyo badala ya kunisaidia alianza kulia huku akipiga mayowe, nikatamani hata kumziba makofi ila nikaona nikitumia hasira sote tutateketea kwa moto ndani hapo.  Cha kumsukuru Mungu mbao hiyo ikakatika na kutupa uwazi wa kuweza kupita.
 
“Pita wewe”
Nilizungumza kwa ukali, binti huyo akaanza kuweweseka. Nikamtandika kofi moja la shavu kumtoa mawenge yake ambayo ninahisi yanataka kutupelekea kifo.
“Eheee”
“Mseng* nini, nimekuambia pita unashangaa nini?”
Binti huyo akapita kwa haraka na kufanikiwa kutoka nje, nikapita na mimi ila kabla sijafanikiwa kupita kuna kipande cha bao kinacho waka moto kikaniangukia mgongoni na kushika kwenye tisheti yangu, nikahitahidi na kutoka nje na kuanza kuminyana na tisheti yangu ambayo imenibana mwili wangu, kuivua. Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuivua, japo kuna baadhi ya maeneo ya mgongoni nilipata majeraha ya kuungua pamoja na mikononi.
“Umeungua”
Aliniambia binti huyo niliye muokoa kutoka ndani, Mzee Jongo akatufwata hadi sehemu tulipo simama na binti yake. Wakakumbatiana na mwanaye kwa furaha. Nikataka kuondoka ila mzee Jongo anakizuia.
“Nakushukuru sana kijana”
 
“Asante”
“Unaitwa nani kijana?”
“Dany”
“Asante sana”
“Dany umeungua mgongoni?”
Binti huyo alizungumza na kumfanya baba yake kunitazama mngongoni.
“Mungu wangu, unatakiwa kwenda hospitalini”
“Hakuna haja mzee wangu”
“Noo umeungua sana, sema hujioni”
Mzww Jongo alizungumza kwa msisitizo.
“Lucy si unaweza kuendesha gari vizuri?”
“Ndio dady”
“Mpeleke mwezako, hospitalini akapatiwe matibabu”
“Sawa dady”
Lucy akaelekea kwenye maegesho ya magari yao ambayo yapo mbali kidogo na nyumba yao kubwa inayo zidi kuteketea kwa moto. Lucy akapiga honi na kuniashiria nimfwate kwenye gari lake. Nikaeleke hadi sehemu alipo, kwa ishara akaniomba kuingia ndani ya gari, tukatoka kwenye geti la upande wa pili wanyumba hiyo ambalo ametufungulia mlinzi wao.  Safari ya kuelekea hospitali ikaanza, ndani ya gari sote tulikaa kimya, ikanibidi kuuvunja ukimya wetu.
“Chanzo cha moto ni nini?”
“Kusema kweli sifahamu kwa maana mimi mwenyewe nilikuwa nimesha anza kulala”
 
“Ahaa sawa”
Kutokana damu imesha anza kutulia, hapo sasa ndipo nilipo anza kuyasikia maumivu ya majeraha ya moto niliyo yapata mgongoni na mikoni. Tukafika hospitalini, kwa haraka tukaelekea mapokezi huku nikiwa kifuwa wazi, sikuona aibu ya kutembea hivyo ila nilicho kifikiria kwa muda huo ni jinsi gani majeraha hayo yanavyo weza kutulia kwa maana yananiuma kupita maelezo. Lucy akawaelezea manesi tatizo langu, kwa haraka nikaingizwa kwenye chumba cha matibabu, nikachomwa sindano kwenye mkono wangu wa kushoto.
“Hii ni sindano ya nini?”
“Kutuliza maumivu”
“Sawa”
Nesi anaye nihudumia akaanza kunipaka dawa ya maji maji, aliyo nieleza ni ya kusafisha kidonda na kuua backteria ambao wameingia kwneye majeraha yangu. Alipo maliza akanipaka dawa nyingine kisha mikononi akanifunga bandeji.
“Itabidi leo upumzike hapa, kesho tunaweza kukuruhusu”
“Sawa. Ninaomba uniitie huyo msichana niliye kuja naye hapo nje”
“Sawa”
Nesi huyo akakusanya vitendea kazi vyake kisha akatoka, akaingia Lucy huku akinitazama usoni.
“Vipi wamekuhudumia vizuri?”
“Ndio”
“Ohmm masikini pole mwaya”
“Asante”
 
“Sasa wamekuambiaje?”
“Wameniambia leo nipumzike hapa kesho ndio wanaweza kuniruhusu”
“Daaa, sawa basi nitalipia kila kitu, kisha nitakwenda nyumbani kuangalia ni kitu gani kinacho endelea na asubuhi na mapema nitakuwa hapa”
“Sawa”
Lucy akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akatoka ndani humo. Baada ya dakika kama sita hivi nesi mwengine akaja na kunimba nimfwate, tuakaelekea kwenye moja ya chumba chenye kitanda cha peke yake, huku kikiwa na Tv, sofa pamoja na choo cha ndani kwa ndani.
“Utalala humu kaka, ukiwa na tatizo lolote basi utawasiliana na mimi, simu ipo hapo mezani”
“Sawa dada yangu”
Nikaingia bafuni na kukuta kioo, hapo ndipo nikageuka na kujitazama mgongoni. Nikatamani kuzimia, kwa maana kidondo ni kikubwa sana karibia nusu ya mgongo mzima.
“Haya ndio matatizo ya kujifanya shujaa”
Nilizungumza huku nikiendelea kujitazama, jinsi gozi ilivyo babuka. Nikarudi chumbani nikawasha tv, hapakuwa na jipya.
‘Kesho kazini itakuwaje?’
Ni swali jengine nililo jiuliza huku nikilala kifudi fudi juu ya kitanda hicho. Kuchoka ukijumlisha na mawazo mengi yanayo kisumbua kichwa changu nikajikuta nikiwa nimelala fofofo.
                                                                                                              ***
“Unaendeleaje?”
Nilisikia sauti ya Lucy iliyo nifanya kufumbua macho yangu. Nikamkuta Lucy na mzee Jongo wakiwa wamesimama pembeni ya kitanda nilicho lala.
 
“Kijana vipi?”
“Safi mzee shikamoo”
“Marahaba, unajisikiaje na hali”
“Ahaa maumivu kwa mbali tu”
Nilizungumza huku nikinyanyuka kitandani. Nikakaa kitako hukuna kuwatazama. Leo ndipo nikapata nafasi ya kumtazama Lucy vizuri. Kusema kweli ni msichana ambaye amebarikiwa asilimi tisini na tisa ya uzuri. Kila sehemu ya mwili wake imeumbwa na kuumbika, ninaamini mwenyezi Mungu alitumia muda weke mwingi sana wa kuumba Lucy. Urefu wake wa futi sita na pointi kadhaa kwenda juu, uliweza kuendana kabisa na muenekano wa sura yake iliyo kaa kama Mrwanda.
Kifua chake kimebeba maziwa madogo wastani, huku tumbo lake kikiwa limepigwa pasi. Sasa maeneo ya kiunoni sasa hapo ndipo kwenye kila aina ya maufundi ya mola. Kuna msemo unao sema ukisikia kwamba kunawanawake wameumbwa ni kweli wameumbika, basi Lucy naye yupo kwa wale ambao ni kweli wameumbika.
Kiuno chembamba wastani, kimeshikilia hispi zilizo jichora kama namba nane, makalio makubwa kiasi yanayo shikiliwa na hipsi hizo zilizo shikiliwa na miguu iliyo jaziwa. Unywele mrefu ambao ni waasili wa Lucy unao fika mgongoni ndio unao zidi kumpa vigezo vingi vya uzuri.
 
“Dany mbona unamshangaa sana binti yangu?”
Sauti ya mzee Jongo ilinistua na kujikuta nikimtazama usoni mzee huyo.
“Ahaa hapana nafikiria ile ajali ya jana ya moto. Vipi mzee mumepata kutambua chanzo ni nini?”
“Ndio, ni mtungi wa gesi, msichana wa kazi aliweza kusahau kuufunga sasa sijui ikawaje ukalipuka na kusababisha moto”
“Pole sana mzee”
“Ahaa nimesha poa. Lucy kamuite nesi waje kumshuhulikia kijana kama kuna chochote cha kufanya waje kumfanyia”
“Sawa baba”
Kitendo cha Lucy kutoka, kwa kona ya jicho langu la kushoto ndipo nikapata nafasi ya kuona wezere la Lucy jinsi linavyo tingishika kwenye suruali yake aliyo ivaa. Kitendo cha macho yangu kumtazama mzee Jongo macho yetu yakakutana na kumfanya mzee huyo kutabasamu naamini alinistukia kwa kile nilicho kifanya.
“Kijana hivi unafanya kazi gani?”
“Ahaa mimi, mimi nipo ofisi moja hivi ya serikali”
“Ofisi gani kwa maana mimi nipo ofisi ya raisi”
Kusikia hivyo nikastuka kidogo ila nikajikaza kwa maana hawa ndio watu wakubwa wa nchi hii.
 
“Mimi nipo ofisi ya usalama wa taifa”
“Ohoo, safi sana. Ndio maana jana usiku nikawa ninakufikiria kijana jasiri kama wewe kwa mtaa ule wetu sijaona, kumbe upo huko?”
“Ndio”
“Basi inabidi nifanye kitu kwa ajili yako kwa maana nisiwe mnafki, pasipo wewe leo hii mimi nisinge kuwa na firaha hii”
“Kwa nini mzee”
“Huyu ndio binti yangu wa pekee, tangu mama yake afariki akiwa binti mdogo basi upando wangu nikaumalizia kwa mke wangu, na endapo kama jana angefariki nahisi hata mimi leo nisinge kuwa hai”
“Usijali mzee wangu”
“Lazima nijali, wewe ni mtu ambaye hukunitazama kama wale watu walio kuwa wamenizunguka. Uliweza kuyahatarisha maisha kwa ajili ya Lucy wangu. Sasa ni kwanini nisikupe zawaidi”
Mzee Jongo alizungumza huku akitabasamu. Wakaingia Lucy na nesi aliye nihudumia jana. Akaja akiwa na vifaa vyake, akasalimiana na mimi pamoja na mzee Jongo kisha akaanza kunisafisha kidonda change.
 
“Kimesha anza kukauka, usivae nguo za kubana sana”
“Sawa nesi”
“Je kidonda chake kitapona baada ya muda gani?”
Mzee Jongo alizungumza huku akimtazama nesi huyo usoni.
“Siku nne hadi tano kitakuwa kimesha kauka. Tutamuandikia sindano za kukausha hicho kidonda kwa haraka na kila siku atakuwa anakuja kuchoma ndani ya siku hizo nne”
“Sawa, Lucy jukumu hilo utalichukua wewe sawa”
“Sawa dady”
“Je leo tunaweza kuondoka naye?”
“Ndio leo hali yake ni nzuri sio kama jana”
“Sawa, Dany utaongozana na sisi sawa”
“Sawa mzee”
“Lile shati umekuja nalo”
“Ndio baba, ila nimelisahau kwenye gari”
“Nenda kachukue mwenzako atatokaje”
Lucy na nesi wakatoka na kutuacha mimi na mzee Jongo.
“Lucy mwanangu anamatatizo ambayo, yanatakiwa kutatauliwa na mwanaume”
“Matatizo gani tena mzee”
“Ahaa bwana mdogo, usitake nikufanulie naamini umesha jua. Mwanangu ana tatizo ambalo akipata mwanaume shababi basi anaweza kulitatua kwa haraka na atajivunia kuwa na mwanagu”
 
Nikatambua mzee Jongo ana maanisha nini, ila sikujau ni kwanini ameamua kuniambia mimi swala hilo.
“Kwa nini umeniambia mimi hilo swala”
“Ahaaa nimekuambia hilo ili umchangamkie bwana. Niliweza kumtunza mwangu hadi sasa amefikisha miaka ishirini na nne naaamini bado kufu……”
Mzee Jongo akanyamaza baada ya Lucy akuingia akiwa amesika shati jipya lililopo kwenye mfuko wake wa nailon. Lucy akaufungua mfuko huo na kulitoa shati hilo ambalo kwa haraka haraka ni saizi yangu kabisa.
“Mvalishe mwenzio, si unaona mikononi ana mabandeji”
Lucy akanza kunivalisha, alipo maliza nikanyanyuka kitandani. Tukatoka nje tukiwa tumeongoza, tukaingia kwenye gari na safari ikaanza huku Lucy akiwa ndio dereva.
“Daughter utaniacha kazini, kisha mutaelekea home sawa”
“Sawa Dady”
Sikujua ni nyumbani wapi tunapo elekea, tukafika kazini kwa mzee Jongo akashuka, akiwa anashuka akaninkonyeza hapo ndipo nikajua kwamba mzee alicho kuwa anakizungumza kina ukweli na si masihara.
 
“Njoo ukae siti ya huku mbele”
Lucy alizungumza, ikanibidi kushuka kupanda siti ya mbele ambayo hapo awali alikwa amekalia mzee Jongo. Safari ikaanza kuelekea nyumbani kwao.
“Tunakwenda wapi?”
“Nyumabani, kuna nyumba yetu ipo masaki ndipo tunapotakiwa kwenda kuishi”
“Ahaa sawa, ila itabidi unipeleke kwangu”
“Huko labda baadaye kwa maana baba ameagiza nikupeleke kwanza Masaki na ameagiza uishi hapo hadi utakapo pona”
Lucy alizungumza huku akizidi kuendesha gari lake. Tukafika kwenye jumba jengine la kifahari ambalo linaonekana ndio lipo kwenye hatua za mwisho kabisa za matengenezo.
“Karibu Dany”
Lucy alizungumza mara baada ya kushuka kwenye gari, tukaelekea ndani. Nimsha wahi kuingia kwenye majumba ya kifahari ndani ya hili jiji la Dar es Salaam ila katika hili jumba la Mzee Jongo ni maradufu. Jumba limejengwa kwa ustadi wa hali ya juu huku nashi zake kwenye kuta na milango kwa ndani zikiwa ni dhahabu.
 
“Twende”
Lucy alizungumza mara baada ya kuniona nikiwa ninashangaa shangaa. Tukaingia kwenye lifti japo ni nyumba ya gorofa moja ila ina lifti yake. Tukafika juu, nikakuta seble nyingine hii ikiwa imeizidi seble ya chini mara dufu.
“Hichi ndio chumba utakacho kuwa unakitumia kwa maagizo ya baba kama jinsi alivyo sema”
Nikaingia kwenye chumba hicho, kwa jinsi kilivyo kikubwa kikanifanya nibaki nimeduwaa.
“Njoo nikuonyeshe kitu”
Lucy alizungumza huku akielekea kwenye mlango mmoja ulipo ndani ya chumba hicho, akaufugua na kuingia ndani na mimi name nikaingia ndani.
“Hili ni bafu, sinki hilo la kuogea lote limetengenezwa na dhahabu hata hayo mabomba unayo yaona hapo pembeni yametengenezwa na dhahabu”
Lucy alizungumza, kitendo cha yeye kugeuka na kunitazama, usoni tukagonda vifua na kujikuta chocho zake zilizo simama vizuri zikigusana na kifua change kilicho jengeka vizuri kwa mazoezi.
 
 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts