Home » , » Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 01 na 02

Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 01 na 02

Written By Bigie on Sunday, February 25, 2018 | 5:36:00 PM

 Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA

Ilisikika sauti ya mwanamke akilia kwa sauti kali sana ndani ya sekunde chache.....kisha sauti hiyo ikatulia kimya....baada ya sekunde kumi ikasikika sauti ya mtoto mchanga akilia.....baada ya dakika kumi kupita,,zikasikika sauti zikisikika zikisema"sukuma kwa nguvu....usibane mapaja utamuuwa mtoto...ghafla ikasikika sauti ikisema ""mama weee...
 
baada ya sekunde tatu hivi ikasikika sauti tena ya mtotochanga akilia....mwanamke huyo aitwae Rose alijifungua watoto mapacha wote wa kiume.walipishana dakika kumi za kuzaliwa...Rose alifurahi sana..Akamshukuru Mungu kwa kujifungua salama...baada ya masaa mawili kupita alikuja mumewe aitwae SEBA....alifurahi sana akasema,nitakupa zawadi mke wangu..nakuahidi nitakununulia gari...Rose alifurahi sana kusikia kauli hiyo ya mumewe..

***************
kesho yake majira ya saa nne za asubuhi.. madaktari walimruhusu Rose kwenda nyumbani..kutokana Rose alikuwa na nyonga pana sana hivyo haikuwa vigumu yeye kuzaa.. alijifungua salama bila kufanyiwa upasuaji wala kuongezewa njia kwa kuchanwa ukeni.
Seba alimchukua mkewe pamoja na mama yake mzazi ambayae ni mama mkwe wake Rose wakatoka nje ya hospital,,waliingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea nyumbani.

*************
ilipofika majira ya saa saba za usiku....mama yake na Rose aliamka....akanyanyuka kutoka kitandani akafungua begi lake na akatoa kaniki nyeusi akajifunga rubega...kisha akatoa mkoba mdogo uliokuwa umetengenezwa kwa ngozi ya Nyumbu.. akaufungua na kutoa irizi mbili zilizokuwa zimefungwa kamba nyeusi nyemba....akazivaa irizi hizo.....akazipiga hatua mpaka kwenye kona ya chumba akasimama wima. huku makalio kayageuzia ukitani......akatoweka kichawi....akajitokeza ndani ya chumba cha mwanae.....Rose alikuwa kalala fofofo pamoja na mumewe Seba...Mama huyo aitwae Bi'CHENDA  akavua irizi moja yenye rangi nyekundu..akaitemea mate kisha akazipiga hatua kukifuata kitanda...alipofika karibu sana...akaanza kukizunguka kitanda mara tatu..kisha akamgusa pacha mmjoja kichwani kwa kutumia irizi hiyo...
 
akazioiga hatua na kueleke kwenye kona ya chumba hicho akageuka na makalio yakageukia ukutani kisha akatoweka kichawi.....akajitokeza chimbani kwake..akarudisha zile irizi kwenye kile kimkoba kilichotengenezwa kwa ngozi ya nyumbu..akavua ile kaniki nyeusi na kuirudisha ndani ya begi lake,,, akapanda kitandani na kujifunika shuka tayari kwa kuutafuta usingizi.. ghafla kulwa akaanza kulia kwa sauti kali...na doto akaanza kulia ..ghafla doto alinyamaza akatulia tuli...kama amelala.....kulwa aliendelea kulia kwa mfululizo mpaka Seba na Rose wakaamka...Rose alimbembeleza kulwa lakini aliendelea kulia mfululizo..akaamua kumnyonyesha lakini aliendelea kulia bila kunyamaza....rose alifanya jitihada za kumbembeleza ili anyamaze asije akamuamsha doto....hatimae kulwa akanyamaza..na baada ya dakika kadhaa kupita kulwa alisinzia kabisa....wakati huo Rose na Seba hawakujua kuwa doto tayari ameshachukuliwa kichawi na bibi yake...na kitandani kuna kipande cha mgomba wa ndizi na si mtoto..

*****************
asubuhi palipokucha Mama Rose alidamka mapema akafua nepi za mapacha hao ambao ni wajukuu zake..kisha akachemsha maji kwa ajili ua kumkanda Rose sehemu zake za siri....baada ya dakika kadhaa Seba alidamka akajianda na kwenda kazini aliamua kujiwekea maji ya kuoga pamoja na kunyoosha nguo zake kwa sababu alimuhurumia mkewe kwa kuwa ametoka kujifungua juzi....baada ya seba kutoka,, Rose naye alidamka akanyanyuka kutoka kitandani akaelekea chooni....aliponyanyuka tu kulwa akaamka akaanza kulia akamchukua na kumnyonyesha...alipomaliza kumnyonyesha,akambadilisha nepi...baada ya lisaa limoja kupita alistahajabu mpaka muda huo doto hajaamka..akaamua kumtikisa ili aamke..lakini doto hakuamka alipomgeuza akaona mikono na miguu ya doto imekakamaa..rose akapaza sauti,,"MAMAAAA njoo haraka..

upande wa nje alionekana Bi'Chenda amestuka kusikia sauti ya Rose....akajisemea moyoni,,"Tayari kumeshakucha..akazipiga hatua kuingia chumbani kwake akachukua ule mkoba mdogo akatoa kichuoa kidogo kilichokuwa na unga wa mfupa wa ALBINO uliochomwa na kusagwa ukawa unga .ili akampake doto asionekane kuwa ni kipande cha mgomba..kipindi watu watakapokuja msibani..akazipiga hatua kuelekea chumbani kwa Rose...

 SEHEMU YA PILI(02)

Bi'Chenda alikuwa anajua wazi kuwa Rose anamuita kwa sababu ameshahisi kuwa doto kafariki..akaingia chimbani kwa Rose huku akijifanya hajui kinachoendelea,,Rose akasema,,"Mama embu mtazame mwanangu mbina kama amekufa!!? Bi'chenda akasema,,"nenda kaweke maji kwenye beseni kisha lete haraka: kumbe ilikuwa janja ya Bi'chenda kumtuma Rose maji..ili apate nafasi ya kupaka ule unga wa mfupa wa albino kwenye kile kipande cha mgomba ili mtu yeyote asijue kuwa aliyekufa sio binadamu bali ni kipande cha mgomba...na mtoto amemechukuliwa kichawi.
 
Rose alitoka chumbani haraka akaingia bafuni na kuleta maji kwenye beseni...kumbe alivyotoka tu bi'chenda aliupaka mgomba huo ule unga wa mfuoa wa albino..uso wa rose ulionekana kuwa na huzuni kubwa huku machozi yakimtiririka.....

bi'chenda alipokea beseni na kuudumbukiza kile kipande cha mgomba...wakati huo Rose hakujua kinachoendelea,yeye aliona ni mtoto.. kwa sababu
hakuwa na uwezo wa kuona jambo hilo la kishirikina. ..bichenda aliendelea kukimwagia maji kipande hicho cha mgomba...na baada ya dakijamoja kupita,,akahifanya amestuka na kuanza kulia...Rose alichanganyikiwa baada ya kumuona mama mkwe wake akilia!!! naye pia akaangua kilio...kwa kuamini kuwa mwanae huyi mchanga amefariki....wakati huohuo kulwa alikuwa akilia kwa mfululizo...Rose hakuweza kumjali kichanga huyo..kwa sababu akili na mawazo yake yalikuwa yakimuwaza doto....Rose alilia kwa uchungu sana...bi'chenda akachukua simu yake na kuanza kuwapigia ndugu na jamaa wa karibu, akawapa taarifa ya msiba wa kifo cha mjukuu wake.

***************
baada ya masaa kadhaa kupita ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wakafika..pamoja na majirani waliokuwa karibu na familia hiyo hata Seba alifika haraka baada ya kupata taarifa hizo za kifo cha mwanae...
kwa sababu mtoto alikuwa mchanga familia ilikaa na kujadili..wakakubaliana doto azikwe siku hiyohiyo......kaburi likachimbwa pembeni ya nyumba ya familia hiyo..
 
ilipofika saa saba za mchana wakajiandaa kwa ajili ya kumzika doto..kulwa alikuwa akilia sana kwa mfululizo..lakini hakuna mtu aliyetambua kulwa analia hivyo kwa sababu gani..wenyewe waliamini huenda njaa ndio inamsumbua...kumbe alikuwa analia kwa sababu doto alikuwa ananjaa hakunyonya tangu usiku wa jana..na kwa sababu alichukuliwa kichawi hivyo huko aliko hajanyonya mpaka muda huo....kwa kuwa walikuwa mapacha wenye uwezo wa ajabu...waliweza kuwasiliana kwa hisia na fikra...wazo lao lilikuwa moja kwenye ubongo ingawa wapo katika miili tofauti....doto alipokua anapata mateso ya njaa hata kulwa mateso hayo pia yalimuumiza tumboni mwake....
likaletwa jeneza la doto...mlikafunguliwa ili wazazi wake pamoja na ndugu waage mwili wa doto tayari kwa kuuzika...wakati huo bichenda alikuwa akimtazama Rose anavyolia kwa uchungu mpaka akapoteza fahamu....bi'chenda hakuonesha kusikitika kwa sababu ni yeye pekee anajua kuwa doto hajafa bdo yupo hai ila kamchukua kichawi..

**************
upande mwingine ndani ya nyumba ya Seba na Rose aliinekana doto kalala sakafuni nyuma ya mlango wa sebuleni....huku akilia,,lakini hakuna hata mtu mmoja aliye sikia sauti hiyo isipokuwa bi'chenda pekee...
mazishi yakafanyika wakaliingiza jeneza la doto ndani ya kaburi na kumzika bila kujuwa kuwa wamezika kipande cha mgomba wa ndizi..walipomaliza kuzika bi'chenda alikuwa mtu wa kwanza kuingia ndani ya nyumba akamchukua doto na kuingia chumbani kwake haraka...hakuna mtu aliyeshuhudia kitendo hicho...

**************
bi'chenda aliingia jikoni na kuchukua maziwa ya kopo akayachanganya kwenye maji ya uvuguvugu na akayakoroga kisha akayaweka kwenye chuchu
na kumpa doto...
ilipofika majira ya usiku wa saa nane bi'chenda aliamka kisha akafungua begi lake na kutoa ike kaniki nyeusi akachukua kile kimkoba kidogo akatoa hirizi zake mbili na kuzivaa shingoni.akatoa ungo wake wa kichawi chini ya uvungu wa kitanda..kisha akamchukua doto amembeba...akasimama juu ya ungo ili aianze safari ya kumpelea doto GAMBOSHI kwenye kijiji cha WACHAWI...baada ya sekunde tatu akatoweka kichawi... 

akajitokeza kule kwenye kiji cha wachawi wachawi wenzake walimpokea kwa furaha...bi'chenda alizipiga hatu mpaka kwa mkuu wa wachawi na kumkabidhi mtoto huyo mchanga sherehe kubwa ikafanyika usiku huohuo....walicheza ngoma za kichawi huku wakila nyama za binadamu....ghafla mkuu wa wachawi akapaza sauti na kusema,,"Tusikilizane......kijiji kizima kikawa kimya kisha akazipiga hatua huku kambeba doto...akapanda na kusimama juu kwenye mgongo wa binadamu waliyemchukuwa kichawi usiku huo kwaajili ya kumfanya jukwaa la kumkuu wa wachawi..kisha akasema..............

ITAENDELEA.......

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts