Home » , » Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 03 na 04

Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 03 na 04

Written By Bigie on Monday, February 26, 2018 | 5:00:00 PM

Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
***ilipoishia***

wachawi wachawi wenzake walimpokea kwa furaha...bi'chenda alizipiga hatu mpaka kwa mkuu wa wachawi na kumkabidhi mtoto huyo mchanga sherehe kubwa ikafanyika usiku huohuo....walicheza ngoma za kichawi huku wakila nyama za binadamu....ghafla mkuu wa wachawi akapaza sauti na kusema,,"Tusikilizane......kijiji kizima kikawa kimya kisha akazipiga hatua huku kambeba doto...akapanda na kusimama juu kwenye mgongo wa binadamu waliyemchukuwa kichawi usiku huo kwaajili ya kumfanya jukwaa la kumkuu wa wachawi..kisha akasema...........

***Endelea***
Siku ya leo,,,ni siku ambayo itakuwa ni yenye baraka kubwa katika kijiji chetu....mtoto huyu mchanga....ameteuliwa na miungu ya kuzimu....wachawi wengine wakaanza kupiga makofi huku wakiongea Lugha ambayo haina maneno ya kibantu..
(lugha isiyokuwa rasmi.haieleweki)..kisha mkuu wa wachawi akachukua kisu pamoja na sumu ya nyoka iliyochanganywa na dawa ya kichawi..akamchana doto kiunoni kwa kutumia kisu hicho kisha..akachukua ile sumu ya nyoka iliyochanganywa na dawa ya kichawi akampaka kwenye jeraha hilo kililokuwa likitoa Damu....

kutokana na maumivu makali Doto alilia kwa mfululizo bila kunyamaza....kisha mkuu wa wachawi akamteuwa mwanamke mmoja aliyekuwa anamtoto anayemnyonyesha miongoni mwa wachawi wa kijiji hicho..(GAMBOSHI) akamkabidhi Ili awe anamnyonyesha Doto pamoja na kumlea... mlaka atakapofikisha umri wa kuitumikia kazi ya miungu wa kuzimu rasmi..baada ya kumaliza sherehe hiyo..wachawi walitawanyika,,,kila mmoja alipanda kwenye ungo wake na kutoweka kimiujiza...
Bi'chenda ajajitokeza chumbani mwake...akavua ile kaniki nyeusi..pamoja na irizi zake mbili akaziweka kwenye kimkoba chake,,kisha akaweka ndani ya begi na kufunga zipu ya begi..akapanda kitandani akaanza kuutafuta usingizi..

******************
asubuhi palipokucha alionekana Rose akiwa ameketi kitandani huku macho uamevimba kutokana na kulia usiku kucha....Rose hakuweza kabisa kuoata usingizi usiku wa jana...Seba alikuwa na kazi kubwa ya kumbembeleza mkewe usiku kucha...wlikesha bila kutarajia.....
ghafla mlango wa chumbani ukagongwa......seba akanyanyuka,,akazipiga harua kwenda kufungua mlango...... alipofungua alimuona mama yake Bi'chenda akiwa amebeba beseni lililokuwa na maji ya moto ndani yake kwa ajili ya kumkanda Rose sehemu zake za siri.... seba aliamua kutoka nje ya chumba ili kumpisha mama yake akamkande mkwe wake..
 
Bi'chenda alijifanya kumbembeleza rose akimsihi anyamaze huku akisema,,"nyamaza mwanangu ni mipango ya Mungu...atakujalia utapata watoto tena usilie.... Rose alimtazama mama mkwe wake kwa huzuni huku akionekana kufarijika na maneno hayo akasema"asante mama yangu...kisha akavua nguo na kulala chali kitandani....bi'chenda akaanza kumkanda..

*******BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA******
Maisha yaliendelea hatimae kulwa akatimiza umri wa mwaka mmoja...Rose alianza kusahau kifo cha Doto akiamini kuwa doto amefa..
Bi'chenda aliendelea na mambo yake ya kichawi pasipo rose wala Seba kujua...
siku ya leo,,Bi'Chenda aliamka usiku wa manane ili aende Kule kwenye kiniji cha wachawi(GAMBOSHI) siku ya leo kulikuwa na ngoma maalumu ya kuongezewa nguvu za kichawi kwa kila mwanachama....
 
Bi'chenda alipomaliza kujiandaa alipanda juu ya ungo wake wa kichawi na kutoweka kichawi akajitokeza (GHAMBOSHI) ni kitendo cha sekunde tatu alikuwa ameshafika....
walionekana,,wanaume pamoja na wanawake wakicheza ngoma...walisebuka huku wakikata mauno.. huku wakiwa uchi wa mnyama.....baada ya dakika kumi kupita wanachama wote walikuwa wameshatima idadi....kisha mkuu wa wachawi akaamuru ngoma isitishwe na watu wabaki kimya...kisha akasema,,""Kwa kila mwanachama mmoja anatakiwa atoe sadaka Chimbuko la Damu yake...ambayo itakuwa ni kafara kwa ajili ya Miungu wa kuzimu.... wachawi walibaki kimya huku wakimsikiliza mkuu wao....akasema"" ndani ya siku tatu kila mmoja lazima awe ametimiza Masharti...............na baada ya kumaliza kikao hicho wachawi walikula nyama iliyoonekana ni mbichi kisha kila mmoja akapanda juu ya ungo wake wa kichawi wakatoweka....kurudi majumbani kwao...

Bi'chenda alipofika nyumbani hakutaka kuwa na subira...akaamua kuifanya kazi hiyo usiku huohuo...akapitiliza na kujitokeza kichawi ndani ya Chumba cha mwanae Seba......aliamua kumtoa kafara mwanae wa pekee Seba....ali kutimiza mashart ya Miungu wa kuzimu...akafungua kile kimkoba kilichotengenezwa kwa ngozi ya nyumbu kisha akatoa unyoya wa ndege aitwae FUNDI CHUMA...ndege huyu huoatikana kwenye misitu yenye miti mikubwa na mirefu...pia huoatikana Tanzania pekee...alipotaka kuuweka unyoya huo kwenye kifua cha Seba ghafla akajigeuza na kulala kifudifudi...

Bi'chenda alistuka sana akaona kazi imekuwa ngumu...wazi likamjia achukue dawa maalumu iliyokuwa ndani ya kimkoba hicho....dawa hiyo ilikuwa na uwezo wa kumfanya mtu asiweze kusikia chochote kinachoendelea....hata akibebwa na kutolewa nje hawezi kustuka kwa sababu anakuwa katika hali ya kutojitambua......akakifungua kichupa kidogo cha kioo kilichokuwa n dawa hiyo ndani yake
ghafla kikamponyoka na kudondoka chini kikapasuka....mlio wa mpasuko wa chupa hiyo ulimfanya Rose astuke usingizini akajigeuza na kuangalia upande mwingine huku akiwa bado kasinzia.........

Bi'Chenda akakimbia haraka kuelekea kwenye pembe ya chumba ili aweze kutoweka kichawi... akashindwa kutoweka kichawi kwa sababu ni mwiko kuvunja chupa hiyo au kudondosha kitu chochote cha kichawi unapokuwa unawanga...endapo itatokea hivyo basi utaharibu nguvu zako za kichawi kwa wakati huo..na utaonekana kwenye macho ya binadamu ya kawaida....ghafla kulwa akaanza kulia....
sauti ya kulwa ilimfanya Rose astuke usingizini akaamua kunyanyuka kitandani ili akawashe taa amnyonyeshe na kulwa alale......akazipiga hatua kuifuata swichi ya kuwashia taa iliyokuwa ukutani alipoikaribia..........

 SEHEMU YA NNE(04)

Bi'chenda akajificha nyuma ya kabati lililokuwa limeacha nafasi kutoka ukutani hivyo pakawa na upenyo bi'chenda akaweza kuingia . Rose alipowasha taa alistuka kuona kuna vipande vya chupa kwenye sakafu alistaajabu sana, akamwamsha Seba na kumuonyesha vile vipande vya supa vilivyokua chini ya sakafu, hata Seba alistaajabu hakuna hata aliefahamu vipande vya chupa vimefikaje chumbani mwao..... hawakujali wakaaa kuzima taa wakalala, wakati huo Bi' chenda hofu kubwa ilitanda juu yake akajiuliza je!akioneka akaulizwa umeingia humu chumbani atajibu nini? Bi' Chenda alisimama nyuma ya kabati mpaka kukakucha.

************
Kulwa alidamka asubuhi na mapema akaanza kulia ilibidi Rose aamke amunyonyeshe kulwa wakati huo huo pia Seba aliamka akaingia bafuni kuoga alipomaliza alijiandaa ili alipeleke gari lake gereji kwa sababu lilikua na hitirafu,akatoka nje ya nyumba na kuondoka zake........

Ilipofika saa mbili za asubuhi Rose alishangaa mpaka muda huo mama mkwe wake hajaamka na sio kawaida yake, akajisemea moyoni""leo mama mkwe kachelewa kuamka!!! Rose aliamua kucheza na mwanae kulwa..baada ya lisaa limoja kupita Rose alianza kupata wasiwasi....hata zile pirikapirika za bi'chenda kila anapoamka...leo hazisikiki.....ikabidi anyanyuke kitandani akazipiga hatua akafungua mlango na kuelekea jikoni....Rose alistahajabu kukuta hata jiko halijawashwa....akazipiga hatua za harakaharaka kwenda chumbani kwa bi'Chenda,,huenda anaumwa!!!!
wakati huohuo bi'chenda alionekana mule chumbani kwa Rose akichungulia ili aone kama rose hayumo chumbani atoke haraka....

*********************

upande mwingine alionekana Rose akigonga hodi kwenye mlango wa Bi'chenda...Rose aliugonga mlango huo mfululizo lakini hakuona dalili yoyote ya bi'chenda kuja kufungua mlango...kutokana na desturi ya waafrika ni mwiko mkwe kuingia chumbani kwa mama mkwe wake au baba mkwe wake... hivyo hakuweza kufungua mlango akazipiga hatua kuelekea upande wa nje ya nyumba....alipofika aliangaza angaza lakini hakumuona bi'chenda......akapaza sauti akimuita,,"MAMAA.......ghafla ikasikika sauti ya kulwa akilia kule chumbani,,Rose akaamua kurudi ndani...ya nyumba ili ambembeleze mwanae

Wakati huohuo bi'chenda alionekana bodo yupo chumbani kwa Rose amejificha nyuma ya kabati...alipogundua Rose kuwa yupo nje ya nyumba...akaamua kutoka haraka kule nyuma ya kabati akazipiga hatua za harakaharaka huku macho. yakionesha kuwa na wasiwasi mkubwa...

********************

wakati huohuo upande mwingine kule gereji alionekana Fundi akimuelekeza Seba kuwa kunakifaa kimevunjika kwenye uoande wa injini(Engine( ya gari lake.. kutokana spea(spare) ya kifaa hicho hakikuwepo hapo gereji hivyo ilimlazimu Seba aende kukitafuta madukani...ili anunue na kumpelekea fundi akakifunge kwenye gari.....
seba akakodi bodaboda ili aelekee dukani kununua kifaa hicho...alipofika dukani aligundua kuwa kasahau pochi(warlet) yake kwenye suruali aliyokuwa ameivaa jana......akaamua kumwambia dereva bodaboda ampeleke nyumbani.....ili akachukue pesa kisha amrudishe dukani hapo.

wakati huo huo alionekana Bi'Chenda akigusa kitasa cha mlango wa Rose ili afungue mlango atoke nje haraka kabla Rose hajafika....
ghafla akasikia vishindo vya Rose akikimbia kwenye kordo iliyokuwa karibu kabisa na mlango wa chumbani...Bi'chenda akastuka akatimua mbio haraka kurudi kule nyuma ya kabati...ghafla akakanyaga kipande cha chupa kilichokuwa kwenye sakafu kikamchoma kwenye unyayo...damu nyingi zilimtoka mfululizo zikadondoka kwenye sakafu.... bi'chenda alihisi maumivu makali sana akajikaza akaingia nyuma ya kabati akajificha......

Rose akadungua mlango kwa pupa ili amuwahi kulwa ambembeleze.....akazipiga hatua za harakaharaka ghafla akakanyaga ile damu akateleza na kuanguka chini...akatazama rahaka aone ni nini kimemfanya ateleze mpaka kudondoka kwenye marumaru....Rose akastuka baada ya kuona damu nyingi huku matone mengine ya damu yalionekana kuelekea nyuma ya kabati.....akanyanyuka haraka akaanza kumkagua kulwa kwa kugisi huenda damu hizo zinamtoka mwanae....alistahajabu kumkuta kulwa hana jeraha lolote.....

Rose akaamua kuzipiga hatua za taratibu huku hofu kubwa imetanda juu yake....macho ya Rose yalionekana kutazama kwa tahadhari kubwa.....wakati huo bi'chenda macho yalimtoka akawa na wasiwasi....jasho lilimtoka mfululizo hata hakusikia maumivu ya lile jeraha alilochomwa na kipande cha chupa..
Rose alipokaribia kuifikia kabati,,,ghafla ikasikika Honi ya pikipiki......upande wa nje ya Geti......

ITAENDELEA.......

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts