Home » , » Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 05 na 06

Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 05 na 06

Written By Bigie on Tuesday, February 27, 2018 | 5:21:00 PM

Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
***ilipoishia***

akanyanyuka haraka akaanza kumkagua kulwa kwa kugisi huenda damu hizo zinamtoka mwanae....alistahajabu kumkuta kulwa hana jeraha lolote.....Rose akaamua kuzipiga hatua za taratibu huku hofu kubwa imetanda juu yake....macho ya Rose yalionekana kutazama kwa tahadhari kubwa.....wakati huo bi'chenda macho yalimtoka akawa na wasiwasi....jasho lilimtoka mfululizo hata hakusikia maumivu ya lile jeraha alilochomwa na kipande cha chupa..
Rose alipokaribia kuifikia kabati,,,ghafla ikasikika Honi ya pikipiki......upande wa nje ya Geti...

***Endelea***
Rose akastuka.....akazipiga hatua za harakaharaka mpaka dirishani, alipochungulia aliona pikipiki nje ya uzio..kutokana geti lilikuwa na uwazi kuanzia katikati mpaka upande wa juu..akamuina Mumewe Seba amerudi...Rose akaamua kutoka chumbani na kuelekea upande wa nje ili akafungue geti....
Bi'chenda akaona hiyo ndio nafasi pekee ya kutoka chumbani humo......akatoka haraka kule nyuma ya kabati,huku akichechemea akazifuta yale matine ya damu iliyokuwa kwenye sakafu.......kisha akafungua mlango alipotoka nje,,,akakutana uso kwa uso na Rose huku akiwa Seba kwenye korido....Bi'chenda alistuka sana..hakutarajia kukutana na Rose akimshuhudia akitokea chumbani kwake..wakati tangu asubuhi alionekana kuwa hayupo ndani ya nyumba hiyo...Rose alistahajabu kumuona mama mke wake akiwa ameva kaniki nyeusi kwa kujifunga rubega.....Seba hakushangaa,, hakujua kilichokuwa kinaendelea ndani ya nyumba hiyo...
 
Rise akauliza kwa mshangao....Mama ulikuwapi nimekutafuta tangu asubuhi haukuwepo ndani!!!....Bi'Chenda akajibu kwa kudanganya,,huku akitabasamu akasema,,"mimi nilikuwemo chumbani kwangu nimelala najisikia homa,,,nimeamka baada ya kumsikia kulwa akilia...ndio nikawa nimeingia humu chumbani kuona kapatwa na nini,,,sijakukuta..
nimembembeleza amekwisha nyamaza...Rose hakujali akajisemea moyoni,,"kumbe alikuwemo chumbani kwake...mmh!!!niliogopa...
Rose na Seba wakaingia chumbani....
*******************
Bi'chenda aliingia chumbani kwake haraka huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi...akajisemea moyoni,,"agh mtu mzima ningeumbuka leo...kisha akavua kaniki ili aiweke ndani ya begi..alipojipapasa shingoni alistuka baada ya kuina zile irizi zake mbili hazipo shingoni hata ule mkoba mdogo uliotengenezwa kwa ngozi ya nyumbu...haukuwepo mikononi mwake..akaingiwa na wasiwasi mkubwa.....kumbukumbu ikamjia kuwa alipokuwa amejificha kule nyuma ya kabati...alizivua zile irizi mbili na kuziweka ndani ya mkoba wake wa kichawi...kisha akauweka chini kando ya alipokuwa amejificha...kutokana na wasiwasi na haraka ya kutoka nje ya chumba cha Rose kabla Rose hajarudi chumbani humo....Bi'chenda aliusahau mkoba huo huko nyuma ya kabati....
 
jasho lilitoka mfululizo akajiuliza ataingiaje tena chumbani kwa Rose ili akachukue mkoba wake wa kichawi aliousahau kule nyuma ya kabati.
wakati huo huo kule chumbani kwa Rose..alionekana Rose akitazama kwa mshangao huku macho yake yakiangaza angaza kwenye sakafu... .akajiuliza,,"hivi nilikuwa naota au nilishuhudia kwa macho yangu...mbina kama niliona damu haka kwenye sakafu!!!tena zikionekana matone matone yakielekea kwenye upande wa pembeni ya kabati.??? ghafla Rose akastuka baada ya kusikia sauti ya seba ikisema,,"Rose,WE ROSE unamawazo gani? mbina kama unatafakari kitu!? Rose akaji,"Damu...
ghafla ikasikika sauti ya Bi'chenda akimuita Mwanae Seba...
Seba akaitika kwa kulaza sauti,"Naam Mama. huku akizipiga hatua akafungua mlango na kwenda kumsikiliza Mama yake...
 
Rose aliamua kukaa kitandani akambeba kulwa na kumuangalia kama kajisaidia ili ambadilishe nepi..
ghafla ikasikika sauti ya Seba ikimuita Rose.....
Rose akamchukua kulwa na kuelekea sebuleni ili akamsikilize Mumewe anachomuitia......alipofika sebuleni...akakuta wameketi,,naye akaketi.
Kimya kikatawala ndani ya sekunde kadhaa kisha Bi'chenda akasema,,"nimewaita hapa tupige story wanangu siku ya leo najisikia kuongea na nyinyi..Rose akatabasamu...Seba akasema,,"Hah! Mama kulikoni leo?hahhahaha haya tule hizo story......
Bi'chenda akaanza kusimulia mambo mengi ya kuchekesha...Rose alicheka sana akasema ,,"mama umeifanya siku yangu ya leo iishe vizuri..Seba akadakia na kusema,,"yani mama umenikumbusha mbali sana zamani kioindi nipo shule ulikuwa mkali sana uliku hutaki mzaha....hahahhahahahhah..
 
Kumbe hiyo ilikuwa janja ya Bi'chenda kuwaita hapo ili wasikae kule chumbani huenda wakauona ule mkoba wake wa kichawi na ni mwiko mtu mwingine ku uona au kuugusa....endapo ikiwa hivyo basi yatatokea matatizo makubwa yatakayo sababisha maafa....Bi'chenda akamwambia Rose,, "Leo tutapika pamoja chakula cha jioni...Rose alifurahi sana akajibu,,"sawa mama kisha Rose akanyanyuka na kumpa Mumewe ambebe kukwa....wao wakapike.....wakazipiga hatua na kuelekea upande wa jikoni....Bi'chenda alihakikisha hampi nafasi Rose aingie chumbani..
Seba alinyanyuka huku akisema,,""aisee nimekumbuka ,,leo wanacheza Azam FC na Simba akaiwasha Runinga..
 
****************
kule jikoni alionekana Rose akichambua mchele huku Bi'chenda akichambua mboga za majani....ghafla akasema,,nakuja ngoja nikajifunge kitenge,akanyanyuka na kuzioiga hatua........kumbe lengo la bi'chenda ilikuwa aingie chumbani kwa Rose haraka akauchukue mkoba wake wa kichawi awe ameuoata kabla haijafika saa saba za usiku kwa sababu irizi zake zinazomuwezesha yeye kufanya mambo yake ya kichawi zimo ndani ya mkoba ule alafu usiku wa leo ni lazima aende kwenye kikao cha wachawi kule GAMBOSHI bila irizi hizo hatoweza kuwa na nguvu za kupaa juu ya ungo wake wa kichawi.....alipogusa kitasa cha mlango wa chumba cha Rose ghafla Simu ya Rose ikaita mfululizo..Rose aliweza kuisikia simu akanyanyuka haraka kuelekeka chumbani.....
Bi'chenda akaachia kitasa na kuzipiga hatua za haraka kuingia chumbani kwake kabla Rose hajamkuta....akaketi kitandani huku akijisemea moyoni,,"mambo yanaanza kuwa magumu!!!hii itanigharimu....ghafla wazo likamjia akanyanyuka haraka........

 SEHEMU YA SITA(06)

usiku wa leo ni lazima aende kwenye kikao cha wachawi kule GAMBOSHI bila irizi hizo hatoweza kuwa na nguvu za kupaa juu ya ungo wake wa kichawi.....alipogusa kitasa cha mlango wa chumba cha Rose ghafla Simu ya Rose ikaita mfululizo..Rose aliweza kuisikia simu akanyanyuka haraka kuelekeka chumbani.....
Bi'chenda akaachia kitasa na kuzipiga hatua za haraka kuingia chumbani kwake kabla Rose hajamkuta....akaketi kitandani huku akijisemea moyoni,,"mambo yanaanza kuwa magumu!!!hii itanigharimu....ghafla wazo likamjia akanyanyuka haraka......

***Endelea***

Kule sebuleni alionekana Seba.....akionekana kustuka...akakumbuka kuwa kamuacha dereva Bodaboda nje ya geti la nyumbani kwake akazipiga hatua za haraka haraka kuingia chumbani kwake,,akamkabidhi Rose ambebe kulwa na kusema,,"wacha nirudi gereji aises yani nimefika nyumbani,,si nikasahau kuwa nimekuja na bodaboda nimemuacha nje ya geti....Rose alitabasamu akasema,,"Utamu wa story za mama hahahaha,,ok mume wangu...simu ya Rose ikaita tena akaipokea na kuiweka kwenye sikio...

Seba akachukua suruali aliyokuwa ameivaa jana, akatoa pochi(warlet).kwenye mfuko wa suruali hiyo... akafungua mlango akazipiga hatua za haraka haraka kutoka upande wa nje ili aondoke kwenda kununua kile kifaa kikafungwe kwenye gari lake...seba akajisemea moyoni,," nimwmkalisha hapo nje sasa ni lisaa la pili linakaribia kuisha...sijui atanielewaje.....Seba akafungua geti,,alipotoka nje ya geti hakumkuta yule dereva bodaboda....
kumbe aliamua kuindoka zake baada ya kuona abiria wake amekaa muda mrefu..akahisi huenda ni wale watu wajanja wajanja wa mjini.....labda kaingia ndani ya uzio huo na kutokezea upande wa pili akaondoka zake......
ilibidi Seba atafute bodaboda nyingine....akazipiga hatua kuelekea barabarani....akakodi bodaboda na kuelekea madukani kununua kifaa kile..

******************

Upande mwingine kule nyumbani kwa Seba,,alionekana Rose akitoka chumbani mwake huku kambeba kulwa...mkono mwingine kashikiria simu sikioni....akazipiga hatua kurudi upande wa jikoni...
wakati huohuo alionekana Bi'Chenda akiwa chumbani mwake,,akiandaa mikakati ya kufanikisha kuupata mkoba wake wa kichawi kabla haujafika muda wa kikao cha wachawi kule GAMBOSHI.akazipiga hatua kurudi jikoni.... alipofika akaendelea kukatakata zile mboga za majani huku wakipiga stori na kicheka...
 
lakini akili na mawazo ya Bi'Chenda...alikuwa akiwaza juu ya kuupata mkoba wake...wakati huo huo kulwa akaanza kulia.....Bi'Chenda akasema,,"mlete nimbembeleze..........Rose hakupinga.......Bi'Chenda akamchukua Kulwa na kuanza kumbembeleza,,kulwa akanyamaza kulia na baada ya dakika kadhaa akasinzia kabisa.....wazo likamjia Bi'Chenda kuwa liwalo na liwe lazima aingie chumbani kwa Rose,,akachukue Mkoba wake wa kichawi......akasema,,"Kha!Mjukuu wangu anavyopenda kulala...amesinzia sasa...Rose akasema,,"wacha nikamlaze chumbani...Bi'chenda akasema endelea tu na uoishi wacha mimi nimpeleke huko chumbani nikamlaze.....Rose akatabasamu na kusema,,"sawa mama hakuna tatizo.....Moyo wa Bi'Chenda ukatulia..akajisemea,,,"Laiti ungejua.....
huku akizipiga hatua kuelekea chumbani kwa Rose......

wakati huohuo mule chumbani kwa Rose walionekana Panya Dume na Jike waakikimbizana kutoka uvunguni kuelekea nyuma ya kabati....kutokana kile kimkoba kilikuwa kimetengenezwa kwa ngozi ya nyumbu..kwa njia ya kienyejienyeji....kilikuwa bado na harufu ya ngozi iliyo kauka....harufu hiyo ilisababisha panya wahisi ni chakula panya Dume akang'ata kimkoba hicho na yule panya Jike pia akang'ata wakawa wanavuruta ukuingia chini ya kabiti mpaka katikati kabisa...mkoba haukuonekana kabisa pale ulipokuwepi mwanzo.....

wakati huo huo alionekana Bi'Chenda akifungua mlango na kuingia chumbani kwa Rose akazipiga hatua za haraka haraka akamtupia kulwa kitandani kwa kumrusha.....akazipiga hatua kuelekea nyuma ya kabati.....alipotazama alistuka!!! macho yakamtoka huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu....hakuamini macho yake..pale alipokuwa kaweka kile kimkoba chake cha kichawi chenye irizi ndani yake hakikuwepo kabisa....
nguvu zikamuishia akagisi kuchanganyikiwa....akajisemea moyoni,,"Mungu wangu eee nani kachukua mkoba wangu jamani!!!
mbona mambo yameanza kuwa magumu kwa upande wangu?? aliongea maneno hayo huku macho na uso wake kuonekana kuwa na wasiwasi mkubwa.....ghafla akaona panya wawili wakitimua mbio kutokea chini ya kabati....wazo likamjia akajisemea moyoni,,"huenda panya hao ndio wamevuruta mkoba huo labda upo chini ya kabati..akainama haraka alipochungulia akauona mkoba wake wa kichawi akauvuta haraka akauchukua na kusimama...akaufungua ili ahakikishe kama irizi zake zimo ndani ya mkoba ule akafurahi sana kuona vitu vyake vyote vya kichawi vipo salama akatoa irizi zile mbili akazishikilia akizitaza huku akitabasamu,,akajisemea moyoni,,"mimi ndiye Bi'chenda,,sio mtu wa sport sport kabisa...akiwa bado kashikiria zike irizi mbili.....ghafla mlango ukafunguliwa....

ITAENDELEA.......

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts