Home » , » Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 07 na 08

Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 07 na 08

Written By Bigie on Wednesday, February 28, 2018 | 5:07:00 PM

Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
***ilipoishia***

akajisemea moyoni,,"huenda panya hao ndio wamevuruta mkoba huo labda upo chini ya kabati..akainama haraka alipochungulia akauona mkoba wake wa kichawi akauvuta haraka akauchukua na kusimama...akaufungua ili ahakikishe kama irizi zake zimo ndani ya mkoba ule akafurahi sana kuona vitu vyake vyote vya kichawi vipo salama akatoa irizi zile mbili akazishikilia akizitaza huku akitabasamu,,akajisemea moyoni,,"mimi ndiye Bi'chenda,,sio mtu wa sport sport kabisa...akiwa bado kashikilia zile irizi mbili.....ghafla mlango ukafunguliwa....

***Endelea***
Akazivaa haraka akatoweka kimiujiza kabla Rose hajaingia chumbani.....Rose alipoingia upande wa ndani hakujua kilichokuwa kinaendelea chumbani kwake...akachukua shuka akamfunika kulwa....kisha akatoka na kurudi jikoni....

***************
upande mwingine alionekana Bi'Chenda akiwa chumbani mwake.....alionekana kufurahi sana...akavua irizi akaziweka ndani ya mkoba wake wa kichawi kisha akafungua begi lake na kuuweka mkoba huo ndani ya begi......akafungua mlango akatoka nje na kuzipiga hatua kuelekea jikoni....alipofika wakaendelea na mapishi....lakini Rose alistahajabu sana..uchangamfu wa bi chenda uliongezeka tofauti na mwanzo....sasa hivi aliongea mfululizo bila kunyamaza...stori zilikuwa nyingi,,Rose alibaki kuitikia na kucheka tu.....
 
Ghafla bi chenda akanyamaza baada ya wazo kumjia...alikumbuka kuwa mkuu wa WACHAWI aliagiza kila mwanachama,atoe sadaka ya damu amboyo ni lazima iwe chimbuko la damu yako...mtoto,,,,,baba/mama mzazi....au ndugu yeyote wa damu....Bi'Chenda alionekana kukosa furaha ya ghafla baada ya kukumbuka agizo hilo kutoka kwa mkuu wa WACHAWI...

******************

upande mwingine alionekana Seba akiwa njiani,,ndani ya gari lake........ lilikuwa tayari limeshatengenezwa...Seba alizipanga gia huku akiliendesha gari lake kwa mwendo wa wastani..hatimae akafika nyumbani kwake....akashuka kutoka ndani ya gari akazipiga hatua kuelekea upande wa mlango wa kuigia ndani ya nyumba.

wakati huo huo Rose na Bi'Chenda kule jikoni ukimya ulitawala...Bi'chenda alinyanyuka na kusema,,"wacha nikaoge..
Rose akajibu,,"sawa mama ngoja mimi niandae chakula mezani naona kipo tayari...
Bi'Chenda alizipiga hatua za kinyonge..kuelekea chumbani kwake alipofika..akaketi kitandani akajisemea moyoni,," hakuna namna itabidi nimtoe sadaka mwanangu Seba....

wakati huo huo alionekana Seba akiingia ndani ya nyumba,,baada ya kulipaki gari lake upande wa nje....Rose alimpokea Seba kwa mabusu motomoto....Seba akasema,,"aisee nahisi njaa kali,,umepika nini mke wangu??
Rose akajibu,,,"Utaona mwenyewe chakula kipo mezani mme wangu....Rose alisema hivyo huku akitabasamu.....Seba akazipiga hatua kuelekea kwenye meza ya chakula...
baada ya sekunde kadhaa kupita alionekana Bi'Chenda akitokea chumbani,,,,akazipiga hatua kuelekea sebuleni...
wakala chakula kwa pamoja.......baada ya kumaliza Rose aliingia chumbani kwake ili kumuangalia kama kulwa kaamka...
hisia zake hazikuwa tofauti na alivyohisi..alimkuta kulwa katoka kuamka sekunde chache zilizopita..akamchukua na kumnyonyesha...kisha akamuogesha.......
baada ya muda Seba aliingia bafuni akaoga...
wakati huohuo alionekana Bi'Chenda akizipiga hatua kuingia chumbani kwake...akapanda kitandani kwake akaanza kuutafuta usingizi...

********************

ilipofika majira ya saa nane za usiku Bi'Chenda aliamka...akatoka kitandani na kulifuata begi lake akafungua zipu akatoa ule mkoba wake wa kichawi uliotengenezwa kwa ngozi ya Nyumbu..
akauweka juu ya kitanda chake....akachukua Kaniki yake nyeusi.....akavua nguo na kubaki uchi wa mnyama..akajifunga kaniki....kisha akachukua ule mkoba wake wa kichawi akaufungua na kutoa irizi mbili akazivaa shingoni,,kisha akaurudisha ule mkoba wake wa kichawi ndani ya begi....akazipiga hatua akainama akatoa ungo wake wa kichawi uliokuwa uvunguni......akasimama juu ya ungo huo,, akatoweka kichawi.........kuelekea GAMBOSHI
,,ni kitendo cha dakika kadhaa akafika GAMBOSHI

alikuta kikao bado hakijaanza,,wanachama wa chama hicho cha wachawi..waliendelea kufika kila mtu kwa wakati wake.....baada ya nusu saa wachawi wote walikuwa tayari wanetimia wote.....
kwa mbali alionekana mkuu wa wachawi akizipiga hatua kuja pale kwenye kiti chake...
alipofika akapaza sauti,,"siku ya leo ni siku maalumu ya kuandaa mashamba yetu yaliyopo hapa GAMBOSHI...hivyo basi tawanyikeni,,, na kila mmoja ahakikishe anatafuta mtu akalime usiku huu huu....wachawi wakaanza kuondoka mmoja mmoja kwa kupanda juu ya ungo wake na kupaa angani.....Bi'chenda akawa wa mwisho kuondoka.....akapanda juu ya ungo wake akatoweka kichawi....
 
akajitokeza ndani ya chumba chake....akabaki amesimama wima huku akitafakari nini cha kufanya au amroge nani ili amchukue kichawi akamfanyishe kazi ya kulima huko kwenye kijiji cha Wachawi.....wazo likamjia akamchukue kichawi jirani yake.....baada ya sekunde kadhaa akatoweka kichawi akajitokeza ndani ya nyumba ya jirani yake....upande wa sebuleni....akanusa kwa kutumia nguvu za kichawi,,, akafanikiwa kujua chumba alichokuwa analala jirani yake..akaingia kichawi ndani ya chumba hicho.....akavua irizi moja akaitemea mate,,akawa anaizungusha kwenye kichwa cha jirani yake pamoja na mkewe..kisha akawanyanyua kwa kuwashika mikono wakanyanyuka kitandani bila wenyewe kujitambua.......akatoweka nao kichawi....mpaka kule Gamboshi(kijiji cha wachawi) akawapeleka moja kwa moja mpaka shambani akawakabidhi majembe..wakaanza kulima bila wenyewe kujijua...

**************

Wakati huohuo alionekana Doto akilia sana usiku huo wa manane kumbe ilikuwa imefika wakati muafaka wa Doto kupakwa dawa maalumu ya kichawi ili kumfanya azidi kukua katika hali malezi ya kichawi,,kwa kuchanjwa mwilini kwa kutumia wembe mkali ili apakwe dawa hiyo hizo sehemu alizochanjwa....kutokana na maumivu Doto alilia sana...hali hiyo ilimfanya hata kulwa kule nyumbani ahisi maumivu makali sana..naye pia akaanza kulia.....kwa sababu kulwa alikuwa analia mfululizo!!!Seba na Rose waliamka...Rose akambeba kulwa akaanza kumbembeleza...lakini kulwa hakuinesha dalili yoyote ya kunyamaza,,aliendelea kulia,,,,

Rose akajaribu kumnyonyesha huenda akanyamaza,,,lakini badohali ilikuwa vilevile......Seba akasema embu nenda kamuamshe mama huenda akagundua tatizo ni nini,,kwa sababu yeye amelea watoto kwa miaka mingi sana......
Rose akanyanyuka haraka kutoka kitandani akazipiga hatua akafungua mlango...na kuelekea kwenye chumba cha mama mkwe wake....akagonga hodi.......

 SEHEMU YA NANE(08)

Rose aligonga hodi kwa mara nyingi sana...lakini hakuona dalili yoyote ya Bi'Chenda kufungua mlango...akaamua kuzipiga hatua kurudi chumbani kwake....akamkuta seba kasimama huku akimbembeleza kulwa.......kutokana kulwa alikuwa analia mfululizo... Rose akaanza kulia alihisi labda kulwa amepatwa na maradhi....Seba akawa na wakati mgumu wa kumbembeleza mkewe Rose pamoja na mtoto wao kulwa..

upande mwingine alionekana Bi'Chenda akiwa kule katika kijiji cha wachawi(GAMBOSHI) na baada ya masaa mawili kupita..wale watu waliochukuliwa kichawi,,walikuwa tayari wameshamaliza kulima mashamba.......
kila mchawi alichukuwa watu wake alio waleta,,ili kuwarudisha majumbani mwao......wakaanza kutoweka kichawi...pia Bi'Chenda alionekana akiwashika mikono wale watu aliowaleta..akatowekanao kichawi....ni kitendo cha dakika kadhaa,,Bi'chenda akawa ameshafika kule kwenye nyumba ya jirani...akajitokeza ndani ya chumba..akawajudisha kitandani kisha akachukua irizi akakizunguka kitanda kwa mara kadhaa..kisha akawagusa kichwani kwa kutumia ile irizi...akazipiga hatua mpaka kwenye kona ya chumba hicho akatoweka kimiujiza...

*******************

upande mwingine kuele nyumbani kwa Seba alionekana Seba bado akiwa na Rose wakihangaika kumbembeleza Kulwa...
wakati huohuo kule Gamboshi alionekana yule Mama miongoni mwa wachawi waliopo katika kijiji cha wachawi..... mama huyo alionekana akimnyonyesha Doto huku akimbembeleza,, na baada ya dakika kadhaa Doto alinyamaza...akaanza kusinzia.....
hata kule nyumbani kwa Seba,,,,,muda huu huo Kulwa alinyamaza akasinzia......

*****************

Bi'chenda alionekana akijitokeza chumbani kwake baada ya kuhakikisha amewarudisha wale watu aliowapeleka Gamboshi kuwalimisha...akazipiga hatua akalisogelea begi lake akafungua zipu akavua ile kaniki yake nyeusi akaiweka ndani ya begi..akafunga zipu akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi.... bi chenda alikuwa amesahau kuvua zile irizi mbili za kichawi alizokuwa amezivaa shingoni..akalala bila kuzivua

*************

asubuhi palipokucha..yule jirani pamoja na mkewe walionekana wakiwa ndani ya nyumba yao....kila mmoja alilalamika kuwa anahisi uchovu kupita kiasi...na mwili wote unauma....walibaki kulalamika hivyohivyo pasipokujua kuwa usiku wa jana walikuwa wakilimishwa shambani....

wakati huohuo alionekana bi'chenda akiwa jikoni akifanya usafi...kama ilivyo kawaida yake kuamka na kufanya usafi kwa kuanzia jikoni.....wakati Bi'Chenda akiendelea kufanya usafi ikasikika sauti ya Rose ikiita,,"Mama.....
Bi'chenda akastuka kusikia Rose akimuita akageuka huku uso na macho yake yakionekana kuwa na wasiwasi....Akasema,,"haujambo mwanangu? umeamkaje??
Rose akajibu,,"sijambo mama shikamoo..
 
Bi'chenda akaitikia salamu huku akigeuza shingo yake na kuendelea kufanya usafi....Rose akaziona zile ilizi shingoni wa Bi'chenda...akastuka akataka kumuuliza lakini akasita......akaamua kuondoka
na kurudi chumbani kwake... lakini akawa na maswali kichwani mwake...akajiuliza inamaana mama mkwe anamambi ya kishirikina!!!!mbona inashangaza????Rose alipoingia chumbani kwake alibaki kimya hakutaka kumwambia Seba..kwa kuhofia huenda seba ataona kama yeye anamuona mama mkwe wake ni hhlllhll""lllLh...au kamchoka kuishinae ndani ya nyumba hivyo anatafuta sababu ili mama mkwe wake aondoke..

wakati huo huo alionekana bi chenda akimalizia kufanya usafi kule jikoni akalifuata kabati la vyombo ili afute vumbi kwenye vioo vya milango ya kabati hilo...ghafla akajiona kuwa shingoni mwake kuna irizi..akastuka akazivua harakaharaka..huku akijisemea moyoni,,"sijui Rose kaona irizi hizi!!!! mbona itakuwa aibu jamani mimi naumbuka...akaamua kuziweka kwenye mfuko wa dela alilokuwa kalivaa...ghafla Rose akarudi jikoni na kusema,,"mama wacha mimi niende sokoni nikanunue mboga ya kupika kwa ajili ya chakula cha mchana....wakati Rose anaongea hivyo alikuwa akimtazama Bi'chenda Shingoni,, akastahajabu kutokuziona tena zile irizi...Bi'Chenda akagundua kuwa Rose aliziona....
Rose akaelekea sebuleni akafungua mlango akatoka nje na kuzipiga hatua kuelekea sokoni...
Bi'chenda akabaki akiendelea kufanya usafi..
wakati anaendelea kusafisha kumbe zile irizi hakuziweka vizuri ndani ya mfuko wa dela alilokuwa amelivaa zikadondoka pasipo yeye kujua zikaanguka nyuma ya mtungi wa jiko la gesi..hivyo hakuweza kuziona

baada ya nusu saa kupita Bi'Chenda alimaliza kufanya usafi....akatoka na kuelekea chumbani kwake...wakati huohuo alionekana Rose akiingia ndani ya nyumba kutokea sokoni..akapitiliza moja kwa moja mpaka jikoni...akachukua sufuria pamoja na kisu ili akatekate nyama aliyoinunua buchani..ghafla kisu kikamponyika na kudondoka nyuma ya mtungi wa gesi...

ITAENDELEA.......

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts