Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 100 na ya MWISHO (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 100 na ya MWISHO (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Tuesday, February 20, 2018 | 10:57:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   

“Shitiii”
Agnes akaikoki bunduki yake na kumuelekezea mtu huyo na kumpima maeneo ya kichwa. Mzee Godwin hadi anakaribiana na Erickson akaweza kuona alama nyekundu ya buduki ikiwa imemlenga Erickson kifuani. Kwa haraka Mzee Godwin akamuwahi Erickson ambaye anatambua ni mkwe kwa mwanaye Manka, akamsukuma na risasi ambayo ilipangwa kumpiga Erickson ikapiga mzee Godwin mgongoni na kumuangusha chini na kumfanya Eddy kushangaa na kwaharaka akaipiga magoti chini na kumgeuza Mzee Godwin na kumkuta akimwagikwa na damu mdomoni.
“BABABAAAAAAAAAA”
Eddy alipiga kelele humu machozi yakianza kumwagika usoni mwake na kumfanya Mzee Godwin kutabasamu na kumshika mkono wa kulia Eddy na kuuweka kifuani mwake.

ENDELEA
“Eddy”
Mzee Godwin aliweza kuitambua sauti ya Eddy na kulia kwake. Eddy kwa hasira akaanza kuivua sura yake ya bandia, japo imeshikana sana na ngozi ya uso wake, ila hakujali hayo maumivu.  Mzee Godwin akaendelea kumuangalia Eddy kitu anacho kifanya hafi ikafikia hatua akamaliza kabisa kuivua sura yake na kubaki na sura alisi.
“Baba fungua macho please”
Eddy alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Japo baba yake huyo ameweza kumfanyia mambo mengi mauvu katika maisha yake yote ila damu ni nzito kuliko maji.
“Ku….uu…wa…..jasiri D.F.E1993”
 
Mzee Godwin alizungumza maneno hayo kwa shida kidogo na hapo hapo akakata roho. Kitendo cha mzee Godwin kuanguka chini na kunyanyuliwa na Erickson, kiliweza kumstua Manka aliye anza kushuka kwenye gari kwa garaka, na kuanza kukimbilia eneo alipo kaa Mzee Godwin na Erickson. Agnes hakutaka kumpa nafasi nyingine mlinzi wa John ambaye alikuwa akihangaika kuikoki bunduki yake. Akamtandika riasi moja ya kicha na kumchangua hapo hapo. Makachero wengine walipo ona makubaliano yameingia dosari wakaanza kufaya mashambulizi kwa kina Rahab na Fetty, ambao nao waliweza kuyajibu mashambulizi hayo huku wakiwa amejificha pembeni ya gari lao.
Agnes akashusha pumzi huku akimtazama Manka kwa kutumia lenzi ya bunduki yake, akikimbilia eneo alipo Erickso.
 
“Mpumbavu wewe”
Agnes alizungumza huku akiikoki bunduki, yake. Alipo hakikisha Manka amekaribia kufika karibu kabisa na walipo Eddy na mzee Erickson, akaivuta traiga ya bunduki hiyo na kuiruhusu risasi moja kutoka kwa kasi. Kitendo cha Manka kumtazama Erickson na kukuta akiwa ni Eddy, alistukia akianguka chini na hapo hapo akakata roho, risasi aliyo ifyatua Agnes iliweza kutua kichwani mwa Manka ndio iliyo yakatisha maisha ya msichana huyo.
 
Eddy alihisi kuchanganyikiwa, baada ya kumuona Manka akiwa amelala chini, damu nyingi zikiwa zimesambaa kwenye  lami. Halima na Anna wakiwa chini ya maji, waliweza kupambana na makachero wengine ambao walitumwa kuimarisha ulinzi chini ya daraja hilo. Mapambano yao yakawa ni kufa na kupona. Halima akajitahidi kupambana kadri ya uwezo wake, ila kwa leo bahati haikuwa kwake kwani kachero aliye kutana naye aliweza kumzidi kwa kila kitu na kujikuta akifia kwenye mikono ya kachero hiyo kwa kuchomwa kisu cha shingoni. 

Kifo cha Halima, kilimshangaza sana Anna, aliye jikuta akiivunja shingo ya kachero aliye kuwa akipambana naye na kuimtoa mtungi wa gesi alio jifunga nao mgongoni. Akamfwata kachero aliye muua Halima, akaanza kuparanganaye, mapigano kati yao yaliweza kumpa ushindi Anna japo naye aliweza kujeruhiwa na kisu cha kachero hiyo ila akafanikiwa kummaliza maisha yake. 

Taratibu Anna akaanza kuufwata mwili wa Halima sehemu unapo elea elea. Akaushika, na kujikuta akianza kulia kwa uchungu, kwa maana hakutarajia kama rafiki yake huyo anaweza kukutwa na mauti. Agnes kazi yake ikawa ni kuwaua makachero wote ambao wanapambana na kina Fetty na Halima. Haikuwa kazi ngumu kwake kwa maana sehemu alipo jificha ni si rahisi kwa mtu kuweza kumuona ila yeye aliweza kuona eneo zima.
                                                                                                       ***
    Wanajeshi na walinzi walio weza kubaki ikulu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kwa siku hiyo hawakuwa na bahati, kwa maana waliweza kushambuliwa na wanajeshi ambao wamevalia kombati za jeshi la taifa, ila utoafuti ni kwamba karibia wote wamejifunga vitambaa vyekundu katika mikono yao ya kushoto. Walijitahidi kuilinda Ikulu ila hawakuweza kwa maana shambulizi hilo ni kubwa na la kustukiza. Meja Paul Msuya aliweza kuwaongoza vijana wake katika kufanya mapinduzi hayo ya kuing’oa serikali yam zee Godwin madarakani. 
 
   Zoezi lao halikuchukua muda mrefu sana, wakawa wamesha maliza kazi yao na kuiwek aikulu chini ya ulinzi wao. Meja Msuya akatuma wanajeshi wengine kwenda katika daraja la kigamboni kumsaidia mkuu wao ambaye ni Rahab. Milio ya risasi, iliwafanya wakazi wa maeno ya Posta na Kigamboni kuingiwa na hofu kubwa sana, kwa maana sio hali ya kawaida na hawakujua ni kitu gani kinacho endelea. Wananchi wengi walio ingiwa na woga, kila mmoja aliweza kujificha sehemu ambayo alihisi anaweza kuokoa maisha yao. 

Wapo ambao waliweza kujificha chini ya vungu za vitanda vyao, wengine walijificha kwenye makabati, wengine waliamua kujifuanika mashuka gubigubi na kujinyoosha vitandani mwao na kuigiza kama wamekufa. Ukawa ni usiku mgumu sana kwao. Wanajeshi wanao muunga mkono Rahab, wakafika katika dareja la Kigamboni na kukuta mambo ndio yanamalizikia malizikia, huku walinzi wengi wa raisi Godwin wakiwa wamesha potea maisha yao. Wakaweza kuuona mwili wa mzee Godwin na mwanaye Manka wakiwa tayari wamesha teketea kwa kupigwa risasi.
 
   Ushindi huo uliweza kumfurahisha kila mmoja aliye husika katika oparesheni hiyo ya kuipindua serikali yam zee Godwin, mtu ambaye walimuona ni kama diktekta katika kuiongoza nchi.
“Kwa nini mumuue na Manka ana kosa gani?”
Eddy alizungumza huku akimgandamiza Rahab kwenye gari huku akiwa amemkuja kombati la jeshi alilo kivaa maeneo ya kifuani.
“Eddy please reduce your anger”(Edd tafadhali punguza hasira yako)
“Nipunguze vipi hasira, wakai mumemuua mtu ambaye hata hatia eheee”
Eddy aliendelea kufoka, huku akiendelea kumkandamiza Rahab kwenye gari hilo. Fetty na Agnes ambao wapo pembeni, walikaa kimya huku Agnes akiwa haamini macho yake kwamba Erickson ambaye alikuwa anampenda siku zote kumbe ni Eddy ambaye tayari alisha weza kuiona sura yake kwenye picha na kuelezwa na Manka kwamba waweze kumuangamiza.
 
“Eddy am sorry”
Agnes alizungumza huku akipiga magoti chini, Agnes akatoa bastola yake na kumkabidhi Eddy.
“Niue kwa sababu mimi ndio niliye muua Manka”
“Umemua Manka kwa wivu wako wa kijinga, Manka mimi ni dada yangu”
Eddy alizidi kuzungumza kwa hasira, akaitazama bastola aliyo ipokea kutoka kwa Agnes, kwa hasira akachomoa magazine yake na kuigawanya vipande viapnde na kuitupia ndani ya bahari. Eddy akaondoka eneo hilo huku akiwa analia kwa uchungu. Akaeleka hadi kwenye mwili wa Manka ulio zungukwa na wanajeshi wa mapinduzi. Taratibu Eddy akapiga magoti chini, kisha taratibu akamnyanyua Manka kwa mikono yake miwili na kuanza kutembea naye kuelekea kwenye gari walilo kuja nalo. Wanajeshi wote wakasimama kwaenye mstari mmoja na kumpigia saluti Eddy anaye elekea kwenye gari. Akauingiza mwili wa Manka na kuulaza katika siti ya nyuma ya gari hilo kisha akapanda mbele, taratibu akalirudisha nyuma, akakunja kona na kuondoka na kuwaacha wanajeshi pamoja na Rahab wakimshangaa.
 
    Rahab akawagiza wanajeshi wengine kuingia ndani ya maji na kuanza kumtafuta Halima na Anna. Kwa bahati nzuri akawaona wakiwa wapo eneo moja. Wakamsaidia Anna kutoka kwenye bahari, huku wengine wakiubeba mwili wa Halima na kutoka naye kwenye bahari. Rahab, Fetty na Agnes walivyo muona Anna ametoka ndani ya maji hayo akiwa anamwagikwa na machozi, wakatambua kwa haraka kwamba kuna jambo baya limeweza kutokea.
Walipo uona mwili wa Halima ulio bebwa na wanajeshi hao, machozi yakaanza kumlenga lenga kila mmoja wao. Fetty na uhodari wake wote akajikuta akiangua kilio huku akiumtazama Halima kuhakikisha kama kweli amekufa au wanatania.
 
“Halipa tafadhali huwezi kufa kirahisi kiasi hichi”
Fetty alizungumza kwa uchungu na kuwafanya wezake wengine nao kuangua kilio, japo Rahab alijikaza na kulia taratibu taratibu. Wanajeshi hao, wakauchukua mwili wa Halima na kuupakiza kwenye gari, na kuondoka nao kueleka katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuihifadhi. Wanajeshi wengine walio salia wakauchukua mwili wa Mzee Godwin ambao hakuna mtu aliye uthamini, sana. Wakautupia ndani ya gari na kuondoka nao.
“Muheshimiwa Ikulu ipo tayari kwa ajili yako”
Mwanajeshi mmoja alizungumza na Rahab. Wakaingia nanye kwenye gari moja ya ikulu walio kuja nayo eneo hilo na kuondoka naye. Fetty na wezake wakapanda katika magari mawili waliyo kuja nayo na kuongozana na gari hiyo kueleekea Ikulu.
                                                                                                               ***
“Hii Laptop ni ya nani?”
Sa Yoo aliuliza huku akiitazama Laptop aliyo ipakata kwenye mapaja yake wakiwa ndani ya gari kurudi Dar es Salaam.
“Nimeikuta humu humu, nahisi itakuwa ni laptop ya Eddy”
Shamsa alijibu huku akeindelea kuongeza mwendo kasi wa gari hiyo.
“Sasa tunakwenda wapi Shamsa?”
“Mama tunakwenda nyumbani kwako”
“Huoni kama kuna harari?”
Hakuna mtu, kupo salama kabisa”
Waliendelea kuzungumza huku wakizidi kusonga mbele. Safari yao haikuchukua masaa mengi hii ni kutokana hakuna magri usiku huo. Wakafanikiwa kufika nyumbani kwa Eddy,  Shamsa akashuka na kufungua geti kisha akarudi kwenye gari akaingia ndani, na kulisimamisha gari hilo mbele ya ngazi za kupandia kueleka kwenye mlango wa kuingilia ndani ya jumba hilo.
Wote wakashuka na Shamsa akaeleka getini na kulifunga geti. Wote kwa pamoja wakaingia ndani. Moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa Shamsa, ambapo Phidaya na Sa Yoo wakaanza kuoga kwa kupokezana kwani ni kwa muda sasa miili yao haijagusa maji kabisa.
 
“Shamsa hivi hii tv inafanya kazi kweli?”
Sa Yoo aliuliza huku akiitizama tv uliyopo ukutani yenye ukubwa wa nch 41.
“Ahaa wala sifahamu ni muda sana sijaiwasha”
“Waya wake upo wapi?”
“Huo hapo chini una ning’inia”
Sa Yoo akauchukua waya huo na kuuchomeka kwenye soketi. Akawasha Tv hiyo, kwa bahati nzuri ikawaka na haikuwa na tatizo la aina yoyote.
“Ina king’amuzi chake ndani kwa ndani, unaweza kupata local chanel”
“Ahhha sawa”
Sa Yoo akaanza kutafuta chaneli zinazo patikana kwenye tv hiyo, kwa bahati nzuri akapata chaneli ya TBC1. Miziki inayo onekana kwenye Tv hiyo, ikawafanya waburudike japo wote sio wapenzi wa muziki ila wanaburudika kiaina. Phidaya akatoka bafuni akiwa amejifunga taulo.
 
“Jamani nimeimisi nyumba yangu”
Phidaya alizungumza huku akijitupa kitandani. Akalala chali huku akisikilizia ubaridi mkali wa AC(Air condition) unavyo ipuliza ngozi yake.
“Breking News?”
Sa Yoo alizungumza huku akiongeza sauti ya Tv hiyo. Wote macho wakayatolea kwenye Tv hiyo. Wakamuona muandishi wa kike aliye jitambulisha jina lake na kuzungumza alicho kizungumza.
“UTAWALA WA RAISI GODWIN UMEPINDULIWA, NA SASA UTAWALA HUO UNAONGOZWA NA MKE WA ZAMANI WA RAISI PRAYGOD MAKUYA ALIYEKUWA RAISI ALIYE SHINDWA KWENYE UCHAGUZI MKUU BI RAHAB PRAYGOD. TUUNGANE NA MUANDHISHI WETU ALIYOPO IKULU KWA TAARIFA ZAIDI”
 
Wote ndani ya chumba wakabaki kimya huku wakishangaa, hakuna aliye fahamu kitu kinacho endelea kwa wakati huo. Swali walilo jiuliza ni kwamba yupo wapi raisi Godwin. Wakamuona Rahab aliye kaa kwenye meza iliyo jaa maiki za waandhisha wa habari, huku yeye akiwa amevalia mavazi ya kijeshi huku usoni mwake akiwa na tabasamu pana.
“Ndugu zangu Watanzania. Nimatumaini yangu mupo salama, japo wengi wenu muliweza kupatwa na wasiwasi mkubwa juu ya mapinduzi haya yaliyo weza kutokea. Ninamshukuru Mungu mapinduzi ya serikali hii yamekwenda salama. Huku nikiwa ndio kiongozi wa mapinduzi haya. Ninawahakikishia wananchi wote wapenda amani na wapenda nchi yetu kwamba, kuanzia sasa nchi hii ni nchi ya amani na utulivu”
 
“Nipo tayari kuweza kusikiliza maoni ya wananchi juu ya nani aweze kuongoza nchi hii. Mimi sio mroho wa madaraka. Ninawatangazia rasmi kwamba nchi kuanzia leo itaongozwa na jeshi hadi pale atakapo patikana raisi ambaye mumemchagua nyinyi kwa kura zetu”
“Pia ninawatangazia kwamba aliye kuwa ni mtawala wa hi inchi, akatumia madaraka yake vibaya kwa manufaa yake na familia yake hususasi mwanaye wa kike, basi hadi ninapo zungumza sasa hatunao kwenye huu ulimwengu. Nitaandaa utaratibu ambao kila mwananchi atashiriki kupiga kura yake kwa haraka iwezekanavyo ili kuweza kuhakikisha kwamba nchi inapata kiongozi mahiri na hodari. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika, asanteni waandishi wa habari”
 
Rahab alimaliza kuzungumza, na habari hiyo ikaisha na miziki ikandelea. Kila mtu ndani ya chumba hicho akawa kimya, hakuna aliye weza uzungumza kitu chochote. Sa Yoo akashusha pumzi huku akitabasamu.
“Sasa imekwisha”
Hata kabla hawajajibu chochote, wakastukia kishindo kizito getini. Wote wakakurupuka, na kushuka gorofani huko na kupita sebleni kwa kasi na kutoka nje. Wakakuta gari moja  nyeusi ikiwa imesimama nyuma ya gari lao wlilo kuja nalo, huku geti kubwa likiwa lienguka chini, inaonyesha limegongwa na gari hiyo. Wote wakabaki kimya huu wakilitazama gari hilo, hawakuweza kumuona mtu aliyopo ndani ya gari hilo kutokana na vioo vyote vya gari hilo nivyeusi.
 
Mlango wa dereva ukafunguliwa, ukatangulizwa mguu wa kulia, kisha mtu huyo akatoka. Wote hawakuamini walipo muona ni Eddy, akishuka kwenye gari hilo akiwa katika sura yake ya asili. Kwa haraka Phidaya akaanza kushuka kwenye ngazi hizo, akamkimbili Eddy aliye simama pembeni ya gari hilo akimtazama. Wakakumbatiana kwa pamoja, huku wakipigana mabufu mfululizo.
Hakuna kati yao aliye weza kuzungumza zaidi ya kumwagikwa na machozi tu. Sa Yoo na Shamsa wakabaki wakitabasamu.
“Upo salama mke wangu?”
“Ndio honey”
“Matatizo yamekwisha mke wangu”
“Asante honeny”
Wakaachiana, Eddy akanyoosha mikono yake huku kwa ishara akiwaita Sa Yoo na Shamsa ambao nao walishuka kwenye gari hizo kwa kasi, na wote wawili kwa pamoja wakamkumbatia Eddy kwa nguvu. Furaha ikatawala kati yao, kila mmoja alipatwa na furaha ambayo tangu azaliwe hajawahi kuipata furaha hiyo. Phidaya naye akamalizia kwa kuwakumbatia wote watatu kwa pamoja.
 
“Nawapenda sana, bila ninyi mimi sio kitu”
Eddy alizungumza. Wakaachiana kisha Eddy akafungua mlango wa nyuma ya gari hilo.Wote watatu wakastuka baada ya kuukuta mwili wa Manka akiwa amelala kwenye siti hizo.
“Mungu wangu!!”
Phidaya alizungumza huku akijiziba mdomo kwa kiganja, hakuamini, msichana mzuri kama Manka anaweza kupoteza maisha kwa wakati kama huo. Wakiwa wanaendelea kuutazama, simu iliyo mfukoni mwa Manka ikaanza kuita, wote wakasita kuitoa, ila Eddy akajikaza na kuingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali ya Manka, akatoa simu hiyo na kukuta namba mpya. Wakatazamana na Eddy akaipokea na kuiweka sikioni.
“Manka ni kweli eti umekufa?”
Ilikuwa ni sauti ya madam Mery ambayo Eddy aliweza kuitambua kwa haraka. Akashusha pumzi kisha akazungumza.
“Manka amekufa”
“Ed…..d….e….d..y unach……o zaungu…..mza ni kweli?”
Madam Mery alizungumza kwa kubabaika akionyesha dhairi kwamba amesha patw na hisia za kulia.
“Ndio mdam Mery na hapa nina mwili wake na nipo nyumbani kwangu”
 
“Na…na….akuja”
Simu ikakatwa, Eddy akairudisha simu hiyo mfukoni mwake, akiwa ana mawazo mengi, hakujua ni nini anacho weza kufanya kwa wakati huo juu ya mwili wa dada yake. Taratibu Eddy akautoa mwili huo na kuubeba, akapandisha nao ngazi na kuingia nao sebleni, akaulaza kwenye kochi taratibu. Kwa haraka haraka ukiingia sebelni hapo na ukiwa haujui ni kitu gani ambacho kinaendelea unaweza kusema kwamba Manka amelala tu na yupo hai. Haukupita muda mrefu wakasikia mngurumo wa gari nje. Wakasikia hatua za miguu zikianza kupanda kwenye ngazi hizo, mlango ukafunguliwa kwa nguvu, akaingia madam Mery ambaye nywele za kichwani mwake zimechanguka changuka kwa kuchanganyikiwa.
    Akaangaza macho yake huku na kule, yakatua kwenye sofa alilo lazwa Manka huku pembeni ya sofa hilo akiwa amekaa Eddy aliye jiinamia.
 
“Manka mwanangu vipi mama, mbona unalala hivyo jamani”
Madam Mery alizungumza huku akiangua kilio kizito. Akamkumbatia Manka huku akiendelea kulia kwa uchungu. Hakuna ambaye aliweza kuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kukaa kimya, ila Eddy machozi yalizidi kumtiririka, hakuona sababu ya Manka kuweza kupoteza maisha kwenye siku kama ya leo. Alianza kujilaumu moyoni mwake kwa kuona kwamba kuvaa sura yake ya bandia kulipekea Manka kuweza kumpenda pasipo kufahamu kwamba wao ni ndugu.
“Ohooo Manka, tazama sasa mdogo wako amebaki peke yake, unahisi haya maisha yatakuwa vipi sasa?”
 
Madam Mery alizidi kulalamika huku akiwa analia na mikono yake akiwa imemkumbatia Manka. Masaa yakazidi kwenda na kukatika hadi ikafika majira ya asubuhi. Sa Yoo akatoa wazo la Manka kupelekwa katika chumba cha maiti ili kuhifadhiwa na wao wafanye harakati za mazishi.
Hakuna ambaye aliweza kupinga wazo lake kwa maana, endapo watazidi kukaa na mwili huo humo ndani, utaharibika. Eddy na Shamsa wakaupeleka mwili huo hospitali ya Muimbili na kuwaacha Sa Yoo, Phidaya na madam Mery wakimfariji.
 
   Wakafanikisha kuuhifadhi mwili huo. Wakaanza kutafuta sehemu za majeneza, ambapo wakamchongeshea jeneza zuri lenye rangu nyeupe pamoja na gauni moja zuri jeupe. Wakalipeleka hospitalini hapo, ambapo mwili wa Manka ukaoshwa kwa mara nyingine na wahudumu wa chumba hicho cha kuifadhia maiti, walipo maliza wakamvisha Manka gauni hilo, kisha wakamuweka kwenye jeneza. Ukimtazama kwa haraka unaweza kusema Manka ataamka pale utakapo muita, ila sivyo tayari amesha ondoka duniani.
   Wakatafuta gari maalumu la kubebea amiti wakaongozana nalo hadi nyumbani kwa Eddy ambapo wakakuta watu ambao Sa Yoo aliweza kuwatafuta, wakawa wamesha maliza kuchimba kaburi na kulijengea, karibu kabisa na kaburi la mama Eddy.
 
“Samahani tunaweza kupata mchungaji?”
Sa Yoo alimuuliza mmoja wa watu hao, walio chimba kaburi hilo na kulijengea. Mtu huyo akamjibu anaweza kupata mchungaji, akatoa simu yake na kumpigia mchungaji wa kanisa lake analo sali. Akamueleza kila kitu mchungaji huyo hakuchukua muda mwingi sana, akafika katika eneo hilo. Japo Manka ni mtu aliye kuwa akiheshimika katika serikali ya baba yake, ila mazishi yake yalihudhuria watu wachache sana, kama mazishi ya raisi Praygod. Mchungaji akafanya taratibu zote za mazishi na wakamzika Manka, na watu hao wambao ni wataalamu sana kwa kujengea makaburi, siku hiyo hiyo wakajengea makaburi hayo na wakalipwa ujira wao na kuondoka.
                                                                                                    ***
    Viongozi na vijana wote wa kikosi cha D.F.E, walipata pigo ambalo kila mmoja lilimgusa sana kwenye maisha yake. Kufa kwa kiongozi na mmiliki wa kikosi hicho chenye viongozi wengi kutoka nchi mbalimbali duniani, kuliashiria hali ya kikosi hicho kwenda kuanguka. John naye alihisi kuchanganyikiwa baada ya kutuma vijana wake wengien kwenda kumfwatilia kijana wake na kukuta amekufa kwa kupigwa risasi na kazi ambayo alimtuma iliwezza kushindwa.

Mikakati na mipango ya kuuiba mwili wa mzee Godwin ndani ya mochwari ya hospitali ya Muimbili ikaanza, hadi inatimu saa sita mchana tayari mwili wa mzee Godwin ukawa umesha ibwa ndani ya hospitali hiyo na moja kwa moja ukasafirishwa kwa ndege hadi katika makao makuu ya kikosi hicho. Kisiwa kizima ambacho ndio kina kambi ya D.F.E kikagubikwa na majonzi. Wakaandaa mpango mzima wa mazishi wa kiongozi wao. Mazishi hayo yakaudhuriwa na viongozi wengi kwa siri, sana pasipo wengine nchi zao kuweza kutambua. 
 
Mazishi ya mzee Godwin yakafanyika kwa mfumo wa kijeshi. Mwili wa mzee Godwin ukachomwa sindano ya kukaushwa ambayo inaweza kufanya kazi katika mwili huo zaidi ya hata miaka kumi. Wakautengenezea jeneza la vioo na kuihifadhi mwili huo kwenye moja chunba maalumu, ambacho kinalindwa kwa masaa ishirini na nne.
“Ni lazima tulipize kisasi juu ya kifo cha mkuu wetu”
John alizungumza kwenye kikao hicho na kuwafanya viongozi wezake ndani ya ukumbi huo kukubaliana na wazo lake.
                                                                                                               ***
    Rahab, Anna, Agnes na Fetty nao wakajumuika na vionozi wengine serikalini kufanya mazishi ya kiongozi wao Halima, ambayo yalifanyika katika makaburi ya Sinza. Mazishi hayo pia yaliudhuriwa na wananchi wengi ambao wamebeba mabango yaliyo andikwa meseji tofauti tofauti. Huku wengine wakisemea Halima, umekufwa kwa ajili ya watanzania wote. Wengine waliandika na kusema kwamba Halima ni mama wa taifa. Kila mmoja aliweza kuguswa na kifo chake. 
 
Mazishi yakamalizika, siku hiyo ikapita, siku iliyo fuata kwa kupitia vyombo vya habari Rahab akawatangazia wananchi jinsi ya kufanya maamzi ya kumchagua ni nani wanaye ona anaweza kuchukua kiti cha mzee Godiwn.
Japo Rahab hakujiweka kwenye kinyang’anyiro hicho zaidi ya kuwataja viongozi ambao walikuwa madarakani, ila wananchi karibia aslimia tisini na sita wakamchagua Rahab na kumuhitaji awe raisi wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.
 
“Hii ni nafasi ya pekee watanzani walio kupatia, waonyeshe kwamba wanawake tunaweza na sisi ni zaidi ya wanaume wao”
Fetty alimuabia Rahab, ambaye hakuwa na kipingamizi. Hapakuwa na mwananchi ambaye alimkataa Rahab, kwa kura hizo za mauoni Rahab akachukua kiti cha uraisi. Siku ya kuapishwa ikapangwa, katika uwanja wa taifa wa mpira wananchi wengi wa kila rika waliweza kuhudhuria eneo hilo, ambapo waliweza kushuhudia jaji mkuu akimuapisha Rahab Praygod kuwa ndio raisi mpya wa Tanzania. Shangwe nderemo zilirindima nchi nzima, natumaini ya mabadiliko kwa Watanzania, yakaanza kufufuka tena.
                                                                                                                  ***
“Jamani mimi ninaomba niondoke na kurudi kwetu Japani”
Sa Yoo alizungumza huku akitazama jinsi Rahab akiapishwa kupitia tv kubwa iliyopo hapo sebleni. Eddy na Phidaya wote wakamgeukia na kumtazama.
“Sa Yoo kwa nini usibaki hapa?”
“Nimepakumbuka nyumbani nahitaji kwenda kuwaona ndugu zangu, jamaa zangu na watu wengine”
“Kusema kweli kwa mimi kama mimi siwezi kukuzuia, ila kikubwa nakushukuru kwa msaada wako wote ulio weza kunipatia”
 
“Na mimi nitamsindikiza”
Shamsa alizungumza, huku akishuka kwenye ngazi za gorofa
“Ehee na wewe unataka kutukimbia?”
“Nitarudi, ila ninamsindikiza rafiki yangu nitakwenda kukaa naye huko siku mbili tatu kisha ninarudi”
“Mimi sina maneno”
Eddy alizungumza huku akitabasamu, kutokana baba amekubali basi Phidaya hakuwa na namna yoyote ya kuwazuia mabinti hao walio ishi nao kwenye shida na raha. Siku iliyo fuata Shamsa na Sa Yoo wakaanza mikakati ya kutafuta hati za kusafiria, kwa kutumia pesa ya kuwahongo watu wanao shuhulika na utengenezaji wa hati za kusafiria, kazi kwao ikawa ni rahisi. Siku hiyo hiyo wakapata hati za kusafiria na kurudi nyumbani. Walishangazwa sana kukuta gari nyingi nyumbani kwa Eddy huku kukiwa na walinzi wengi wanao onekana kumlinda raisi.
 
“Ina maana Rahab yupo hapa?”
“Nahisi”
Walinzi baada ya kuwahoji maswali wakawaruhusu kuingia ndani. Wakamkuta Rahab akiwa amekaa sebleni pamoja na Eddy. Wakamsalimia, kisha wao wakamuulizia ni wapi Phiday alipo, wakaelezwa yupo jikoni na wao wakaenda eneo hilo na kuwaacha waendelee na mazungumzo yao.
“Eddy bila ya wewe mimi siwezi kuiongoza hii nchi peke yangu”
“Sasa Rahab unataka mimi nifanye nini?”
“Nataka uwe msaidizi wangu, nataka nikuteue kuwa makamu wa raisi”
 
Eddy akaka kimya na kushusha pumzi. Akafikiria ombi hilo kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyua sura yake na kumtazama Rahab.
“Nimekubaliana na ombi lako muheshimiwa raisi”
Eddy alizungumza huku akitabasamu. Wakanyanyuka kwa pamoja na kupeana mikono, Rahab akaonekana kuwa na furaha sana kwa Eddy kukubali.
“Ila vipi kidonda chako?”
“Kina endelea kukauka taratibu”
“Basi jiandae kesho uweze kufika ikulu nianze kukutangaza”
“Sawa”
Wakapata chakula cha mchana kwa pamoja kisha Rahab akaondoka na kumuacha Eddy akiwa na furaha sana, pamoja na familia yake kwa ujumla. Eddy akawaelezea Rahab, Sa Yoo na Shamsa ombi alilo elezwa na Rahab, wote wakafurahi na kumuomba aweze kuhakikisha kwamba anafanya kazi yake kwa juhudi na kwa manufaa ya watanzania wote kwa maana nafasi hiyo waliitafuta kwa muda mrefu.
“Madam Mery yupo wapi?”
Sa Yoo aliuliza huku akimtazama Phidaya usoni.
“Amesha ondoka na kuelekea Mwanza nyumbani kwake”
“Hata kutuaga?”
 
“Nyinyi si muliondoka na kumuacha amelala”
“Sisi tutaondoka kesho mchana saa saba kuelekea Japani, tumesha weka booking ya ndege”
“Ahaa basi, kila mmoja nitampatia kiasi cha dola milioni tano tano”
“Kweli Eddy?”
“Ndio”
“Wee Sa Yoo sasa hivi usimuite Eddy, muite makamu wa raisi Eddy”
Phiday alizungumza kwa utani na wote wakacheka. Eddy akaingia kwenye chumba chake cha siri, akatoa kiasi kikubwa cha pesa ambacho ni sawa na milioni kumi. Sa Yoo na Shamsa akawapatia kila mtu kiasi sawa, kisha wakazipakiza pesa hizo kwenye magari lao na kwenda nazo benki. Shamsa akaziingiza kwenye akaunti yake na Sa Yoo akaiziingiza kwenye akaunti yake ya benki ya Japani yenye tawi lake nchini Tanzania. Wakarudi nyumbani na kufanya maandalizi ya kila kitu. 
 
   Siku iliyo fwata alfajiri na mapema gari kutoka ikuku zipatazo nne zikafika nyumani kwa Eddy. Kiongozi wa msafara huo akamtaarifu Eddy juu ya ujio wao hapo ni kuwachukua na kuwapeleka Ikulu, ambapo shamra shamra za kumuapisha makamu wa raisi zimeanza.
Eddy na Phidaya wakajiandaa vizuri sana, Eddy akavalia suti nyeusi na shati jeupe pamoja na tai ndogo nyeusi, huku Phidaya akivalia gauni refu jeupe lenye mstari mmoja mkubwa kiunoni wenye rangi nyeusi. Huku miguuni akiwa amevalia viatu vyeusi ambavyo ni virefu kiasi. Wakaagana Sa Yoo na Shamsa, kwa maana hawato weza kuhudhuria sherehe hizo za kuapishwa kwa Eddy kutokana na ndege yao kuondoka saa saba mchana.
 
Eddy na Phidaya wakaingia kwenye gari hizo na kuondoka. Sa Yoo na Shamsa nao wakaingiza mabegi yao kwenye gari lao.
“Hiyo laptop si uingize chumbani kwa Eddy?”
“Yaa ndio nataka niipeleke”
Shamsa akaipeleka laptop ya Eddy ndani kwake, kisha akatoka, wakaondoka na Sa Yoo. Wakapitia kwenye maduka ya simu wakanunua simu nzuri, na kuelekea uwanja wa ndege. Kutokana muda wa kuripoti kwa abiria uwanjani hapo ni saa moja kabla ya ndege kuondoka, ikawalazimu kuti sheria hiyo. 
 
“Hapa si kuna wifi?”
Sa Yoo alimuuliza Shamsa, ambaye alimjibu kwa kutingisha kichwa. Sa Yoo akaanza kuperuzi kwenye mtandano kwa kutumia Internet iliyopo hapo uwanja wa ndege. Muda wa andege yao kuondoka, ukawadia. Wao nao waka ni miongoni mwa abiria wlio ingia kwenye ndege hiyo ya shirika la ndege la Air Ways. Wakaka kwenye siti moja, huku Shamsa akiwa ameweka earphone zake masikioni.
Abiria wakatangaziwa kufunga mikanda yao, ndege inaondoka. Shamsa na Sa Yoo wakafanya hivyo, taratibu ndege hiyo ikaanza kuondoka eneo hilo la uwanje wa Mwalimu J. K Nyerere. Ndani ya dakika kadhaa tayari ikawa imesha iacha ardhi ya Tanzania.
 
“Shamsa muone Eddy”
Sa Yoo alizungumza na kuonyesha video inayo onekana kwenye simu yake, mbayo hayo ni matangazo ya moja kwa moja  yanayo ruka kutoka katika viwanja vya Ikulu. Shamsa akamtazama Eddy aliye shika biblia akiapa juu ya kulitumikia taifa la Tanzania kwa haki na uadilifu.
“Ohooo mwangu, tazama ulivyo pata baba mzuri na anaye jituma. Mungu akubariki nikuzae kwa amani?”
Shamsa alizungumza huku akilishika shika tumbo lake kwa kiganja cha kulia.
“I….iii ina maana Shamsa una mimba ya Eddy?”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakimtoa
“Ndio, nina mimba yake. Na wewe ndio mtu wa kwanza kukuambia hili. Na ninapo kwenda sinto rudi tena nchini Tanzania”
 
“Kwa nini sasa?”
“Endapo Phidaya atagundua kwamba nimebeba mimba ya Eddy, basi visa na mikasa mipya inaweza kuibuka, jambo ambalo silitaki kuliona linatokea katika maisha ya mwangu wala katika maisha ya mwanangu. Nitamlea mwangu kwa kadtr ya uwezo wangu na atapata malezi bora. Ninakuomba Sa Yoo unitunzie siri hii”
“Usijali rafiki yangu siwezi kuitoa siri hii na sinto fungua kinywa changu kuweza kumueleza yoyote juu ya hii siri”
Sa Yoo alizungumza na wote wakashikana mikono, na safari ikazidi kusonga wakielekea nchini Japani, wote wakiwa na furaha na amani katika maisha yao kwani kila kitu cha ubaya kimesha fika tamati.
                                                                                                      MWISHO

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts