Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 88 & 89 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 88 & 89 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Sunday, February 11, 2018 | 9:20:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
   Phidaya akageuka nyuma na kuwaona askari wawili walio valia suti wakimfwata kwa kasi kitendo kilicho mfanya kuzidi kukimbia kwa uwezo wake wote. Rahab akiwa kwa mbali akamuona Phidaya akikatiza kwa kasi, mara hajakaa sawa akawaona askari wawili wakimfwata kwa kasi wakitoka katika majengo wakielekea kwenye maegesho ya magari. Rahab akafwata kwa nyuma ili kuwazuia askari hao, huku naye akiwa katika mwendo kasi.
 
Phidaya katika kutizama tizama kwake kwenye maegesho ya magari, akaona gari moja likisimama kwenye maegesho ya hapo hospitalini. Kwa haraka pasipo hata kuuliza Phidaya akafungua mlango wa nyuma wa gari hilo na kuingia na kumfanya muendeshaji aliyopo humo ndani kugeuka kwa kasi na kumuangalia.
“WEWE NI NANI?”   
Muendeshaji ambaye ni mwanamke mwenzake, alimuuliza kwa sauti ya ukali huku akiwasha taa ya ndani ya gari lake kuiona sura ya Phidaya vizuri.

ENDELEA
   Macho ya Agnes yakabaki yakimshangaa mwanamke huyo ambaye leo ndio mara yake ya kwanza kumuona. Kabla hajazumgumza kitu Agnes akashuhudia wanaume wawili mbele ya gari lake wakipokea kipigo kwa msichana ambaye anamfahamu fika. Wanaume hao wanao onekana kuwa ni walinzi wa kiongozi wa nchi, walijikuta makonde yao hayafui dafu mbele ya makonde ya Rahab anaye shusha kipigo kikali juu yao.
 
“Rahab”
Agnes alizungumza huku akiwasha taa za mbele za gari yake kushuhudia jinsi kifinyo hicho kinavyo tembea kwa wanaume hao. Ndani ya dakika tano wanaume hao wakawa wamevunjwa vujnwa viongo na Rahab aliye simama kwa kijiamini mbele ya gari la Agnes. Kwa haraka Agnes akashuka kwenye gari hukku akiwa na tabasamu usoni mwake.
“Rahab”
Agnes aliita huku akianza kumfwata Rahab sehemu aliyo simama, kabla hajamfikia walinzi wengine watatu wenye mitutu ya bunduki wakanza kuzifnyatua risasi zao sehemu alipo simama Rahab, ambaye hakuwa mzembe kwa kiasi hicho kwani hata kabla risasi hizo hazijamfikia akaanza kuruka sarakasi kuelekea naapo tokea Agnes ambaye kwa haraka akarudi kwenye gari na kujitosa kama alivyo ingia Phidaya.
 
Kwa haraka Rahab akaingia kwenye gari la Agnes.
“Go go goo”(Nenda ndenda nendaaa)
Rahab alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya Agnes kuwasha gari lake kwa haraka, akalirudisha nyuma kwa mwnedo wa kasi, akakata kona moja kali, alipo hakikisha amelilenga geti la kutokea, hakufanya kosa zaidi ya kukanyaga mafuta na kuondoka eneo la hospitali na kuwaacha walinzi hao wakifyatua fyatua risasi pasipo mafanikio yoyote. Mlinzi mmoja akarudi sehemu walipo acha magari yao akaingia kwenye gari moja na kuliendesha kwa kasi hadi sehemu walipo simama wezake, wakaingia ndnai ya gari na kuanza kuwafukuzia Phidaya na wezake.
                                                                                                                  ***
 Milio ya risasi inayo endelea nje ikawafanya watu kadhaa ndani ya hospitali waliyo isikia kuchanganyikiwa, mtu aliye toka katika chumba cha wagonjwa mahututi, akamfanya Shamsa kumtazama kwa muda, huku akiwa amemkazia macho.
“Huyu si Manka aliye mchukua Eddy”
Shamsa alizungumza huku akianza kupiga hatua za haraka kuelekea katika mlango alio simama Manka pamoja na walinzi wa wawili wa mzee Godwin.
“Huruhusiwi kuingia hapa binyti”
 
Mlinzi mmoja alizungumza huku akimzuia Shamsa kwa mkono, Manka akamta jicho la dharua Shamsa, kisha akaendeleak usikilizia milio hiyo ya bunduki ni wapi inapo tokea. Kwa kasi ya ajabu Shamsa mguu wake mmoja akaukanyaga kwenye paja la mlinzi huyo, akajirusha kwajuu na kumkalia mabegani, bila hata ya huruma akamvuja shingo na kuanguka naye chini na kumfanya Manka na mlinzi aliye baki kubaki wameduwaa. Mlinzi akataka kuchomoa bastola yake, ila tayari amesha chelewa kwani Shamsa alisha mfikia na kumpiga mtama ulio muangusha chini, hata kabla hajajinyanyua tayari shingo yake ilisha vunjwa.
Shamsa akanyanyuka huku akimkazia macho Manka aliye anza kurudi nyuma na kuingia chumbani huku Shamsa akimfwata kwa mbele.
 
Shamsa alipo muona Eddy akiwa amelala kwenye kitanda akabaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, jambo lililo kuwa ni kosa kubwa sana kwake kwa maana Manka, alimshushia teka zito la tumbo lililo muangusha chini. Maumivu ya tumbo aliyo yapata Shamsa yakamfanya ajinyanyua chini taratibu huku akimtazama Manka aliye jiweka tayari kwa mashambulizi.
Sa Yoo na madam Merry wakakutana kwneye kordo inayo elekea kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi. Wakashuhudia walinzi wawili wakiwa wamelala chini ya sakafu nje ya chumba kimoja. Kwa haraka wakaanza kukimbia hadi kwenye mlango wa chumba hicho na kumshuhudia Shamsa anavyo pokea kichapo kutoka kwa Manka. Wote wawili wakaingia ndani na kuanza kumshambulia Manka, kila mmoja aliweza kumshambulia jinsi alivyo weza, aliye rusha kofi sawa, aliye vua kiatu na kumtandika sawa, ilimradi walihitaji kumuokoa Eddy aliye muona amelala kitandani.
 
“Mchukueni Eddy muondoke naye mimi ninamshuhulikia huyu”
Shamsa alizungumza huku akinyanyuka, Madam Merya na Sa Yoo hawakupoteza muda baada ya kumuona Manka amelala chini akiwa yupo hoi taabani. Kutokana kitanda alicho lalia Eddy kina matairi, walicho kifanya ni kuchomoa waya wa umeme wa mashinye ya kuhesabu mapigo ya moyo iliyopo pembeni ya kitanda hicho, na kuanza kukisukuma kutoka nje.
“Tupite njia hii”
Madam Mery alizungumza, Sa Yoo akatii wakaanza kukisukuma kitanda hicho hadi nje kwenye maegesho ya magari cha kushukuru Mungu hapakuwa na mtu hata mmoja, kutokana milio ya risasi hiyo ilisikika katika eneo hilo na raisi wote walikimbia japo ni usiku.
 
“Kwenye gari hili hawezi kuingia”
“Itakuwaje sasa?”
Sa Yoo akaitazama gari la wagonjwa lililopo kwenye maegesho hayo kwa haraka akalikimbilia, akajaribu kufungua mlango wa upende wa dereva kwa habati nzuri akaukuta upo wazi, kwnai ni muda mchache gari hilo limeleta mgonjwa hapo hospitalini, kingine cha kumshukuru Mungu hata dereva aliweza kusahau fungua kwneye mskani wa gari hilo. Kwa haraka Sa Yoo akaingia na kuliwasha gari hilo akalirudisha taratibu hadi sehemu kilipo kitanda, akshuka kwa haraka, akazunguka nyuma wakasaidiana na Madan Mery kumuingia Eddya kaiwa na kitanda chake kisha madam Mery akaingia nyuma na kufunga mlango na Sa Yoo akarudi mbele, akakanyaga mafuta na kuondoka eneo hilop la hospitali.
                                                                                                                      ***
    Shamsa akaanza kummalizia hasira Manka kwa kumbamiza ngumi mfululizo za uso. Kisha akamnayanyua na kumkalisha kitako na kutaka kumvunja shingo, ila kabla hajafanya hivyo raisi Godwin na mlinzi wake wakawa wameingia kwenye chumba hicho wakiwa na silaha mikononi mwao baada ya kuwakuta walinzi walio nje ya chumba hicho wakiwa wamekufa.
 
“Mikono juu”
Mlinzi huyo alizungumza kwa sauti kali huku bastola yake akiwa amemuelekezea Shamsa, aliye tii amri hiyo. Raisi Godwin macho yakamtoka kwa hasira huku akimtazama mwanaye Manka akiwa amelala chini huku damu zikimtoka puani na mdomoni.
Mzee Godwin wala hakuwa na haja ya kumtazama Shamsa, macho na akili yake vyote akavitupia kwa Manka wake, taratibu akapiga magoti chini huku machozi ya hasira yakimtoka usoni mwake, msichana wake muri na mrembo haswahaswa, amegeuzwa kuwa mbaya ndani ya muda machache alio muacha.
“Manka, Manka”
Mzee Godwin aliita huku kichwa cha Manka akikiweka kwenye mapaja yake.
 
“Ni nani aliye fanya hivi mwanangu eheee”
Manka taratibu akayageuzia macho yake kwa Shamsa aliye nyoosha mikono juu, na kumfanya Mzee Godwin na yeye kuyageuza macho yake na kumtazama Shamsa, kwa jicho lililo kolea wekundu wa hasira. Mzee Godwin kwa haraka akaikoki bastola yake kuruhusu riasi zake kukaa tayari kwa kutoka pale tu atakapo vuta traiga ya bastola hiyo na riassi zote zimalizikie mwilini mwa Shamsa.
“Usimu….ue baba”
Manka alizungumza huku akiushika mkono wa Mzee Godwin uliyo shika bastola huku ukitetemeka kwa hasira kali.
“Huyu si ndio amekufanya hivi?”
Cha kushangaza Manka akatingisha kichwa, hadi Shamsa akabaki ameduwaa, kwani tayari kimoyo moyo alisha anza kusali sala yake ya mwisho kwani tayari kifo kimesha simama mbele yake.
 
“Wawili wamemchukua, Erickson wang…….”
Manka hakumalizia sentensi yake akawa amepoteza fahamu na kumfanya Mzee Godwin mimacho kumtoka, akaanza kumtingisha Manka huku akimuita kwa sauti ya juu iliyo jaa hasira.
“Muheshimiwa ngoje nimbebe nimuwahishe kwa madaktari”
Mlizni wake alizungumza huku akimsogeza pembeni mzee Godwin anaye lia sasa kwa uchungu. Mlinzi wake akamnyanyua Manka kwa mikomo miwili na kutoka na Manka kwa kasi na kumpeleka mapokezi, ili aanze kupewa huduma ya kwanza.
Mzee Godwin kwa hasira akanyanyuka na kuanza kufnyatua risasi juu zilizo toboa toboa sing’bodi iliyopo hapo hospitalini. Shamsa kuona mzee amechanganyikiwa akaanza kupiga hatua kabla hajafika mlangoni akasikia sauti nzito nyuma yake ikizungumza
 
“Simama wewe binti, utanionyesha ni nani aliye mchukua Erickson”
Shamsa akasimama na kugeuka nyuma, akamkuta raisi Godwin akiwa amemuelekezea bastola, huku anamsogelea taratibu.
‘Siwezi kukamatika kijinga hivi’
Shamsa alizungumza huku akizitazama hatua za raisi Godwin zinavyo msogelea, Mzee Godwin hadi akamkaribia akastukia teke zito likitua kifuani mwake, ila kutokana na mazoezi mazito anayo yafanya, teke hilo lilimyumbisha kidogo na kumrudisha nyuma, Sa Yoo akafungua mlango na kutoka kasi, Mzee Godwin akafungua mlango na yeye akatoka huku bastola yake akiwa amemuelekezea Shamsa anaye karibia kukata kona. Akafyatua risasi moja iliyo mpata Shamsa nyuma kwenye bega la mkono wa kulia na kumuangusha chini.
 
Shamsa akajikanza hivyo hivyo na kunyanyuka kwa haraka huku akisikilizia maumivu makali aliyo yapata, na kuendelea kukimbia. Kabla mzee Godwin hajachukua maamuzi ya kumkimbiza mlinzi wake aliye kuwa amempeleka Manka mapokezi akarudi eneo hilo huku akiwa anakimbia kwa mwendo wa kasi.
“Muheshimiwa hali ya Manka sio nzuri”
Mzee Godwin kusikia hivyo akachomoka kasi kuelekea sehemu alipo pelekwa Manka huku mlinzi wake akiwa nyuma.
Shamsa akafika lilipo gari lao, akafungua mlango na kuingia. Huku maumivu ya risasi aliyo pigwa yakiendelea kumtesa sana huku damu nyingi zikiendelea kumwagika. Shamsa hakukuta funguo alicho kifanya ni kukata nyanya mbili za hasi na chanya akazikutanisha na kulifanya gari hilo kuwaka. Kwa haraka akaondoka eneo la hospitali huku akijikaza na maumivu hayo makali.
                                                                                                      ***
  Agnes akazidi kuongeza mwendo kasi wa gari huku akimtazama  Rahab aliye keti siti ya pembeni. Hapakuwa na mtu aliye zungumza chochote hadi pale walipo anza kusikia milio ya risasi ikirindima nyuma yao.
“Wanakuja”
Phidaya alizungumza huku akilala chini. Agnes kwa kioo cha pemeni akaona gari moja nyeusi aina ya Aud Q5 ikija kwa kasi, huku watu wawili wakiwa wamechomoza kwenye vioo wakiwa namitutu ya bunduki wakilishambulia gari lake.
“Rahab mimi mbona sielewi ni kitu gani ambacho kinaendelea hapa?”
“Wewe enesha gari utajua mbele ya safari”
“Sasa tunaelekea wapi?”
“Popote ili mradi tuwakimbie watu hawa”
“Ahaaaa”
 
Agnes akaonekana kuchukizwa kwa tukio hilo la hatari kwenye maisha yake kwani hata leongo ambalo lilimpeleka hospitalini hapo halikuweza kukamilika. Agmes kiroho upande, akaongeza mwendo kasi wa gari lake, kutoka na kujua njia nyingi za vichochoro, akajitahidi kwa uwezo wake kuwapotea watu wanao wakimbiza, hadi akafanikiwa. Breki ya kwanza akafika nyumbani kwake, honi moja aliyo ipiga, ikamfanya mlinzi kufungua gate kwa haraka kwa maana anatambua bosi wake hapendi akiwa nje ya geti apige honi zaidi ya mara moja. Geti lilipo funguliwa Agnes akaliingiza gari lake kwa kasi hadi sehemu ya maegesho ya magari na kushuka kwa hasira.
 
Rahab na Phidaya nao wakashuka, wote macho yao wakamtazama Agnes aliye kunya sura yake akilitazama gari lake lilivyo tobolewa tobolewa baadhi ya maeneo ya risasi.
“Rahab hembu naomba unieleze ni kitu gani ambacho kinaendelea mimi mbona siwaelewi nyinyi watu”
“Punguza hasira, kwanza nashukuru kwa msaada wako ulio weza kutusaidia”
“Hilo mimi haliniusu, hivi bado hujaacha ujambazi Rahab, umetoka kuwa mama raisi hadi kazi yako ya zamani si ndio?”
Agnes aliendelea kuzungumza kwa hasira na kumfanya Rahab kumfwata kwa kasi hadi sehemu alipo simama na kumsogelea kwa ukaribu zaidi huku akiwa amemkazia macho ya hasira Agnes, kitu kilicho muogopesa Phidaya, aliye simama pasipo kujua ni jinsi gani watu hao wanavyo juana.
                                                                                                               ***
“Madam sasa tunampeleka wapi Eddy?”
Sa Yoo aliuliza huku akizidi kukimbiza gari hilo la wagonjwa.
“Njia ile ya bagamoyo imefungwa na askari. Tumpeleke nyumbani kwake”
“Nyumbani kwake mimi sipajui”
“Wewe twende nitakuelekeza”
Madam Mery alizungumza huku macho yake yote yakiwa mbele. Akaanza kumuelekeza Sa Yoo njia za kupita hadi wakafanikiwa kufika nyumabi kwa Eddy. Madam Mery akashuka na kuingia ndani, akafungua geti na Sa Yoo akaingiza gari kisha madam Mery akalifunga geti hilo. Kwa haraka Sa Yoo akashuka baada ya kulisimamisha gari akazunguka nyuma alipo kuta madam Mery tayari amesha fungua milingo iliyopo nyuma ya gari hilo. Wakasiaidiana kumshusha Eddy na kitanda chake, moja kwa moja wakampeleka hadi kwenye sebule. Madam Mery akatafuta sehemu yenye swichi ya kuwashia taa, hadi akafanikiwa.
“Tumuweke hapa hapa”
 
Sa Yoo alizungumza na kuanza kukisukuma kitanda hadi sehemu alipo hitaji kumuweka Eddy. Walipo hakikisha wamemuweka sehemu sahihi, kila mmoja akajikuta akishusha pumzi kwa kuchoka. Sasa Sa Yoo ndio akaanza kupata muda wa kuanza kuikagua nyumba hiyo ambayo inaonekana fika kwamba haitumiki kwa muda mrefu kwa maana kuta zake pmoja na samani zilizopo zote zimejaa vumbi jingi sana pamoja ma mitando ya buibui
                                                                                                          ***
    Akili ya Shamsa, haikupafikiria sehemu nyinyinge yoyote ya kwenda ziaid ya nyumbani kwa Eddy kwa maana ndipo karibu na sehemu alipo. Kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nguvu zilivyo zidi kumuishia mwilini mwake hii ni kutokana na kumwagikwa na damu nyongi mwilini mwake. Hadi anafanikiwa kufika nje ya geti la nyumba ya Eddy alilo kuta limefungwa, nguvu zote za mwili zilisha muishia. Taratibu akajikuta akiulalia mskani wa gari hilo na kufanya gari hilo kupiga honi mfululizo. Honi hizo zikawastua Madam Mery na Sa Yoo walipo ndani ya nyumba hiyo. Sa Yoo aliye kuwa gorofani kwa haraka akashuka hadi sebleni na kumkuta Madam Mery akiwa amesimama huku akiwa na wasiwasi mwingi.
“Ni nani huyo?”
Sa Yoo aliuliza huku naye akionyesha dhairi ana wasiwasi mwingi
“Hata mimi sifahamu kwa maana hakuna mtu anaye fahamu kama sisi tupo hapa”
“Isije ikawa ni wale walinzi wa raisi?”
“Si dhani kama wanaweza kuja hapa kwa manaa hakuna anaye fahamu uwepo hapa”
 
“Hembu zima zima taa”
Madam Mery akakimbilia sehemu yeney swichi, akazima taa ya sebleni. Kisha kwa haraka akarudi sehemu alipo Phidaya.
“Twende tukaangalie ni nani”
“Wee mtoto huogopi, wanaweza kuwa majambazi hao?”
“Hapana Madam hakuna majambazi wanao kuja kwa kupiga honi kwa kiasi hicho”
“Mmmmm”
“Yaa twende”
Wakatoka kwa tadhari kubwa huku kila mmoja akiwa makini kwa kutazama kila upande wa eneo hilo la nyumba. Wakafika getini, Sa Yoo akawa wa kwanza kuchungulia nje, hapo ndipo akaliona gari la madam Rahab.
“Ni madam Rahab”
Sa Yoo alizungumza huku akitoka kwenye kageti kadogo, madam Mery kusikia hivyo naye akatoka akionekana kutokuwa na wasiwasi wa aina yoyote. Sa Yoo alipo ona honi hizo zinaendelea kupigwa kwa haraka akaelekea upande wa dereva, baada ya kuchungulia dirishani akamuona Shamsa akiwa amelalia mskani huku kichwa chake kikiwa kwenye honi ndio maana inapiga kwa mfululizo.
 
“Madam ni Shamsa”
Sa Yoo alizungumza huku akiufungua mlango wa upande wa Shamsa, kitu kilicho mstua Shamsa ni damu zilizo tapakaa kwneye siti aliyo ikalia Shamsa, hata kabla hajafanya kitu chochote akastukia gari yenye mwanga mkali aina ya defender likisimama nyuma ya gari la Shamsa, wakaruka wanaume wawili  walio kuwa nyuma ya gari hilo huku wakiwa wamevalia nguo za kiaskari pamoja na makoti makubwa meusi, huku mikononi mwao wakiwa na bunduki aina ya SMG.
“Munafanya nini hapo”
Mwanaume mmoja alizungumza na kumfanya Sa Yoo kwa haraka kufunga mlango wa gari na kusimama huku akimwatizama wanaume hao ambao ni polisi wa doria, wakimfwata huku wamemnyooshea mitutu ya bunduki.


SORRY MADAM (89) (Destination of my enemies)

“Ahaaa tunamfungulia huyu ndugu yetu amerudi amelewa”
Sa Yoo alizungumza huku akiwa amesimama huku ameuegemea mlango wa gari hilo.
“Sasa muambieni asipige honi anawasumbua majirani walio lala”
“Sawa afande nitamnyanyua”
Afande hao baada ya kuwatazama Sa Yoo na madam Mery wakawaamini kwamba huyo ndugu yao amelewa sana hadi hajiwezi. Wakarudi kwenye gari lao, wakapanda na kuondoka zao. Kila mtu akashusha pumzi, hususani madam Mery ambaye mwili mzima ulikuwa unamtetemeka, ila Sa Yoo alijikaza.
 
“Madam anatokwa na damu”
“Damu?”
“Ndio?”
Sa Yoo alizungumza huku akimtaza Shamsa aliye poteza fahamu kabisa. Wakajitahidi na kumuweka siti ya nyuma ya gari huku wakiwa wamemlaza kifudi fudi kwa maana risasi hiyo ipo begani kwa nyuma. Madam Mery akaingia na kufungua geti kisha  Sa Yoo akaliingiza gari hilo, akalisimamisha karibu sana na sehemu ya mlango. Wakamshusha Shamsa, kwa haraka haraka wakamuingiza ndani na kumlaza kwenye sofa. Madam Mery akawasha taa, na kurudi kwenye sofa walipo mlaza Shamsa
 
“Aiiii risasi amepigwa hapa”
Sa Yoo alizungumza huku akiichana nguo ya Shamsa sehemu kwenye jereha. Madam Mery alipo litazama jeraha hilo kwa haraka akaelekea jikoni, akafungua friji ambalo halijawashwa, kwa muda mrefu. Akatoa pombe aina ya Vodka kisha akarudi nayo sebleni.
Akaifungua, pombe hiyo ambayo ni kali sana, akamwagia Shamsa kwenye jeraha lake. Kwa maumivu makali Shamsa akajikuta akizinduka.
“Shamsa tulia tulia”
Sa Yoo alizungumza huku akimzuia Shamsa kunyanyuka, madam Mery kwa vidole gumba vya viganja vyake vyote viwili, akanza kuliminya jeraha la Shamsa kwa staili ambayo anaweza kuipandisha risasi ili kutoka katika kidonda hicho. Shamsa akazidi kutoa ukelele wa maumivu makali hadi Sa Yoo akamsokomeza vitambaa kadhaa mdomoni mwake ili aiweze kuungata ulimi wake.
 
“Madam jitahidi inatoka inatoka”
Sa Yoo alizungumza huku akiliangalia jeraha hilo linalo vuja damu nyingi sana. Madam Mery akazidi kujitahidi hadi akafanikiwa kuitoa risasi hiyo. Sa Yoo akachukua pombe hiyo na kumwagia kidonda hicho, kuua bacteria ambao wameweza kuingia.
Walipo maliza zoezi hilo wakamfunga Shamsa jeraha lake, kwa kipande cha nguo ambacho Sa Yoo alichana kwenye shati lake, kwa maumivu makali, Shamsa akajikuta akipitiwa usingizi na kulala fofofo.
                                                                                                             ***
  Jinsi Rahab alivyo zidi kumkazia macho Agnes ndivyo jinsi Agnes alivyo zidi kumkazia macho Rahab. Wakasimama zaidi ya dakika tano, wote kwa pamoja wakajikuta wakimwagikwa na machozi kisha wakakumbatia kwa nguvu.
“Ohooo Rahab”
Agnes alizungumza huku akizidi kumkumbatia kwa nguvu. Wakaachiana kisha wakamgeukia Phidaya ambaye naye machozi yalikuwa yakimlenga lenga baada ya kuwaona wezake hao wakimwagikwa na machozi.
 
“Phidaya huyu ni Agnes, ni miongoni mwa marafiki zangu wa kitambo sana. Agnes huyo ni Phidaya ni rafiki yangu sana”
“Nashukuru kukufahamu Phidaya”
“Hata wewe nashukuru kukufahamu”
Kwa haraka Phidaya kumbukumbu zikamjia na kugundua kwamba Agnes ndio mwanake ambaye ana mahusiano na mume wake Eddy, ila akajikausha kwa maana yupo kwenye mamlaka ya mtu ambaye ameweza kumuepusha mikononi mwa mzee Godwin. Agnes akawakaribisha ndani.
“Niwapatie nini?”
“Mimi nina njaa mshikaji wangu. Alafu umejipanga kishenzi au ndio huo uwaziri?”
“Daa wee acha tu maisha ndugu yangu nakumbuka enzi zile tunatumia mitutu, pale benki nakumbuka tulivyo kwapua ile mihela, alafu sijua ilikwendaga wapi mshikaji wangu”
“Aisee hata mimi sikumbuki zilikwenda wapi kwa maana kila mtu alitawanyika, kuja kusikia wezangu mumekamatwa, nikajaribu kuwaokoa ila ndio hivyo nikashindwa”
 
“Ahaa nakumbuka ulisha tuelezaga hiyo ishu kipindi kile cha kampeni tunamlinda huyu mzee”
Rahab na Agnes walizungumza huku wakieleka jikoni na kumuacha Phidaya sebleni akitazama tazama mazingira. Phidaya akakumbuka tukio la dokta Nelson alivyo weza kujirusha dirishani. Kitu alicho kikumbuka kingine ni bahasha aliyo kuwa ameiokota chini, kwa haraka akajipapasa na kuitoa bahasha hiyo na kuifungua. Akatoa karatasi zilizo kuwemo humo na kuanza kupitia moja baada ya nyingine. Kabla hata hajazisoma Agnes akarudi sebleni hapo huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.
 
“Phidaya tumesha andaa chakula chap chap njoo tule”
“Sawa”
Phidaya akazirudisha karatasi mbili kwenye bahasha hiyo na moja akaisahau juu ya sofa kwa haraka alizo kuwa nazo. Wakaongozana na Agnes hadi kikonni na kumkuta Rahab akiendelea kula.
“Unatumia kinywaji gani?”
“Ahaa mirinda nyeusi”
“Ngoja nikakuletee, zipo kwenye friji la sebleni”
Agnes akatoka jikoni na kurudi sebleni, akafungua friji na kutoa soda hiyo, akiwa anakatikaza hapo sebleni macho yake yakatua kwenye karatasi ambayo Phidaya alizisahau. Akaona sio vyema kuiacha karatasi hiyo ikiwa nje ya bahasha hiyo ni vyema airudishe ndani ya bahasha hiyo.  Kabla hajairudisha macho yake yakatua kwenye maandishi meusi na yaliyo kulea vizuri yaliyo andikwa ‘DNA TEST BETWEEN MANKA GODWIN AND ERICKSON FORRD’(Vipimo vya DNA kati ya MANKA GODWIN na ERICKSON FORRS)
 
Kwa haraka Agnes akaanza kuipitia karatasi hiyo huku akisoma majibu hayo. Mwili mzima kahisi ukiishiwa nguvu kwa maana majibu yanaonyesha Erickson na Manka ni mtu na ndugu yake wa damu moja.
‘Ina maana Manka na Erickson ni ndugu?’
Agnes alijiuliza huku akiirudia kuisoma tena hiyo karatasi, akashusha pumzi nyingi na kuirudisha karatasi hiyo sehemu ilipo kuwa na wala hakuhitaji kuirudisha kwenye bahasha hiyo. Akaondoka sebleni hapo akiwa katika dibwi la mawazo, hakuamini kitu ambacho amekiona kitu kikubwa anacho jiuliza, kuna uhusiano gani katia ya Erickson na Manka.
 
“Vipi mbona umechelewa?”
Rahab aliuliza huku akimtazama Agnes machoni, aliye mtazama Phidaya na kuachia tabasamu la kujilazimisha na kumpatia soda aliyo muagiza.
“Ahaa nilikuwa sizioni hadi nikaenda kuchukua chumbani kwangu”
“Ahaa kumbe hata wewe ni mtumiaji wa hizi soda?”
“Sana huwa nazitumia ila ndio hivyo mara nyingi nakuywaga whyne”
Agnes hakutaka kuuliza kitu cha aina yoyote zaidi ya kujifanya hajui chochote, alicho hitaji ni kuanza kufanya upelelezi wake taratibu hadi afanikiwe kutambua ni mchezo gani upo katikati ya Manka na Erickson mwanaume anaye mpenda.
                                                                                                   ***
    Alfajiri na mapema Eddy ayakafumbua macho yake, kila sehemu aliyo itazama ndani humo, hakuweza kupakumbuka na wala hakujua amefikaje fikaje eneo hilo kwa maana kumbukumbu zake za mwisho zinamkumbuhsa kuhusiana na gari lake alio kuwa amebeba silaha.
‘Nipo wapi hapa?’
Eddy alijiuliza huku akijaribu kutazama tazama kila sehemu, picha kubwa ya ukutani inayo muonyesha yeye pamoja na familia yake, ikamfanya taratibu anze kupachunguza ndani humo kwa umakini na kugundua kwamba yupo nyumbani kwake, akatazama kwenye makochi akamuona Sa Yoo akiwa amelala huku amekaa, akatazama kochi la pembeni yake akamuona Shamsa akiwa amelala kifufidi fudi.
Kabla hajazungumza chochote, akamuona Madam Mery akishuka kwenye ngari za gorofa, huku mkononi mwake akiwa ameshika kikombe kinacho onyesha kuna chai.
“Umeamka”
 
Madam Mery alizungumza huku akipiga hatua hadi kwenye kitanda cha Eddy.
“Madam kumetokea nini?”
Eddy aliuliza huku akihitaji kukaa, ila madam Mery akamzuia, ili asiweza kuutibua mshono alio weza kufanyiwa.
“Ahaa ni maelezo marefu kidgo ila kusema kweli polisi jana walikupiga?”
“Ahaaaaa!! Sasa mbona nimelazwa hapa nani kanileta?”
“Aliye kuleta ni mimi na Sa Yoo tulikuuiba hospitalini baada ya Manka kukuchukua”
“Manka!! Manka alinichukua mimi?”
“Ndio alikuchukua, mikononi mwa polisi, ila sisi tukakuiba”
“Yupo wapi mke wangu Phidaya?”
Madam Mery akaka kimya asimjibu Eddy swali lake kwa maana hata yeye hatambua ni wapi alipo Phidaya na Rahab ambo tangu walipo achana hospitali jana usiku hapakuwa na mawasiliano ya aina yoyote.
Gafla Shamsa akakurupuka, kwenye kochi alipo kuwa amelala, huku mkono mmoja akiuweka mdomoni mwake, akakaa kitako na kuanza kutapika kitendo kilicho washangaza Eddy na madam Mery wanao mtazama.

                                                                                                   ***
   Hadi inafika majira ya saa kumi na mbili alfajiri, Manka ndio anazinduka kutoka katika usingizi wa nusu kifo, mtu aliye muona pembeni yake hakuwa mwengine zaidi ya Mzee Godwin ambaye alipo muona mwanaye huyo amezinduka, akaachia tabasamu pan asana.
“Baba”
“Naam mwanangu”
“Umempata Erickson wangu?”
“Ndio walinzi wapo kwenye harakati za kumtafuta, ninaamini watampata”
Manka machozi yakaanza kumtiririka, usoni mwake, na kumfanya mzee Godwin kuchukua kitambaa chake na kuanza kumfuta mwanaye huyo machozi.
“Usilie mwanangu, nitahakikisha kwamba Erickson anarudi mikononi mwako”
“Asante baba, ila kwa nini wamchukue Erickson wangu wakatia anaumwa”
 
“Hivi unawakumbuka walio mchukua?”
“Ndio ninawakumbuka na ndio walio nipiga mimi”
Mzee Godwin akatoa simu yake mfukoni na kumpigia mkuu wa usalama wa taifa na kumuagiza awalete vijana wawili wenye ujuzi wa kuchora sura za watu pale wanapo elezwa watu hao wanaonekana vipi. Alipo toa maagizo hayo akakata simu na kumgeukia Manka aliye kuwa amempa mgongo kipindi akizungumza na simu hiyo.
“Kuna wataalamu watakuja hapa na utawaelezea jinsi watu hao wanavyo onekana kisha picha zao zitatumika katika kuwatafuta kimya kimya hadi tuwapate”
 
“Sawa baba”
“Uletewe kifungua kinywa?”
“Ndio”
Mzee Godwin akatoka na kumuita mmoja wa walinzi wake, akamuagiza akasimamie kifungua kinywa cha mwanae jinsi kinavyo andaliwa, ili kusije tokea makosa yoyote kama ya kuwekewa sumu. Haukupita muda mrefu, vijana wawili wenye ‘brufcase’ zao mikononi wakaruhusiwa kuingia kwneye chumba alipo mzee Godwin na Manka. Wakampa salamu mzee Godwin pamoja na mwanaye kisha wakaandaa vitendea kazi vyao ikiwemo karatasi nyeupe pamoja na penseli zao za kuchorea na rangi kadhaa. Manka kwa masaada wa mzee Godwin, wa kumnyanyua kitandani, akaka kitako na kuanza kutoa maelezo ya watu hao wambao waliweza kumvamia. 
 
“Kumbe ni wanawake?”
Mzee Godwin aliuliza kwa mshangao, baada ya Manka kutamka jinsi nywele zao zilivyo. Manka akatingisha kichwa na kuendelea kuwaelezea wachoraji hao jinsi Sa Yoo na madam Mery walivyo, hadi zinatimu dakika arobaini na tano, picha ya Madam Mery na Sa Yoo zikawa tayari zimesha kamilika na akakabidhiwa Mzee Godwin.
Macho yam zee Godwin yakatua kwenye picha ya madam Mery na kujikuta akimkazia macho, akamgeukia Manka aliye kaa kitandani, akataka kuzungumza kitu ila akanyanyamaza na kuwaruhusu wachoraji hao kuondoka ili kuzungumza na mwanaye huyo.
 
“Unataka kusema huyu mwana mama naye alikuwepo?”
“Ndio alikuwepo kwani baba unamfahamu?”
Mzee Godwin akajikuta akitingisha kichwa cha kukubali kwamba ana mfahamu madam Mery ambaye hadi leo anatambua kwamba amefariki kutokana na siku ya mwisho kuwa naye alipiga risasi wakiwa nyumbani kwa Eddy katika zoezi la kumteka Phidaya.
 
“Unamjuaje juaje baba?”
Mzee Godwin akashusha pumzi huku taratibu akikaa kitandani, hakujua aanzie wapi katika kumueleza Manka ni kitu gani kilitokea katia yake na mwana mama  huyo.
“Baba mbona hunijibu?”
“Huyu alikuwa mama yako mdogo na pia alikuwa ni mwali wake Eddy”
Manka akaishika picha hiyo ya madam Mery na kuitazam tena vizuri, kumbukumbu zake zikarudi zaidi ya mika kumi na mbili nyuma. Akamkumbuka mwanamke huyo kipindi hicho alikuwa kijana mzuri, alikuja nyumbani kwa mjomba wake ambaye alidai ni mwalim anaye fundisha naye shule moja na shule hiyo hiyo ndio shule ambayo Eddy alisoma.
 
Kumbukumbu za Manka kwa haraka zikarudi hadi kwenye tukio lililo tokea jana usiku wake, alipo msikia binti mmoja ambaye hakuhitaji kumtaja kwa baba yake, akiwaeleza madma Mery na Sa Yoo wamchukue Eddy na kuondoka naye.
“Huyo ni mama yako mdogo kabisa, japo sikuhitaji kuliweka wazi hilo na yeye wala halijui hilo kwamba nilisha wahi kuzaa na dada yake ambaye alisha fariki siku nyingi”
“Baba ni kitu gani hicho unanieleza leo?”
Manka aliuliza kwa ukali huku machozi yakimtoka, kila anacho kisikia mbele ya baba yake leo ni kitu kipya kwenye maisha yake.
 
“Usi kasirike mwanagu, kwani hata yeye hafahamu kwamba dada yeke nilisha wahi kuzaa naye, na pia hafahamu kwamba wewe ni mtoto wa dada yake”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge huku kichwa chake akiwa amekiinamisha chini wala hakuhitaji kumtazama Manka usoni.
“Huyo anaitwa Mery na alisha wahi kuwa mapenzi wangu hadi siku ninampiga risasi nikiamini atakuwa amekufa”
“Dady ni roho gani hiyo uliyo kuwa nayo, tazama sasa, mama yangu mdogo anahitaji kuniua je utakwenda kumuua kwa mara ya pili kwa hili alilo nifanyia mimi eheee?”
 
Swali la Manka kwa mara ya kwanza, likaanza kuibua hisiaza machozi za Mzee Godwin. Ambaye kwa muda huu kumbukumbu za maisha yake ya nyuma zinaanza kujirudia kichwani mwake.
“Baba na je Eddy unahitaji kumuua kisa kikiwa ni nini, ikiwa ni mwanao wa damu moja na pia umenipandikiza chuku ya kumchukia mdogo wangu Eddy ili mradi utimize matakwa yako ya kuendelea kumwaga damu za watu wasio na hatia, baba kumbuka kuna usemi unao sema,  what gose around, always come aroud”
 
Manka alizungumza huku akichomoa mrija wa dripu na kushuka kitandani akiwa na hasira kali ya kusikia ukweli kwa baba yake huyo.
 
“Na tambua Eddy nimesha mfahamu, na Eddy huyo huyo ndio atakaye kuja kuja kukuangamiza, na kuanzia hivi sasa usinihusishe na mipango yako ya kikatili”
Manka alizungumza kwa hasira huku akijikongoja kutoka mlangoni ila kabla hajafika mlangoni huku nyuma akasikia bastola  ikikokiwa, taratibu akageuka na kumkuta Mzee Godwin akiwa amemnyooshea bastola ya uso, huku macho yam zee Godwin yakiwa yametawaliwa na ukungu mwekundu wa hasira hadi mkono wake ulio shika bastola ukawa unatetemeka.

   ITAENDELEA...........USIKOSE SEHEMU YA 90 

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts