Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 90 & 91 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 90 & 91 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Monday, February 12, 2018 | 11:58:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   

“Na tambua Eddy nimesha mfahamu, na Eddy huyo huyo ndio atakaye kuja kuja kukuangamiza, na kuanzia hivi sasa usinihusishe na mipango yako ya kikatili”
Manka alizungumza kwa hasira huku akijikongoja kutoka mlangoni ila kabla hajafika mlangoni huku nyuma akasikia bastola  ikikokiwa, taratibu akageuka na kumkuta Mzee Godwin akiwa amemnyooshea bastola ya uso, huku macho yam zee Godwin yakiwa yametawaliwa na ukungu mwekundu wa hasira hadi mkono wake ulio shika bastola ukawa unatetemeka.

ENDELEA
“Na mimi unahitaji kuniua, kama unavyo hitaji kumuua Eddy?”
Manka alizungumza huku machozi yakimwagika, Mzee Godwin akaendelea kumshikilia Manka bastola huku akizidi kutetemeka kwa hasira.
“Kwa nini hukumuua Mery nilipo kuagiza pale Arusha?”
“Damu ni nzito kuliko maji baba, na Mungu aliweza kunipa roho ya ujasiri ya kumuacha akiwa hai, kumbe ni mama yangu mdogo. Nimekua bila ya kuwa na mama, ila wewe hulioni hilo hadi unahitaji nimuue mama yangu mdogo si ndio?”
 
Hasira ya Manka na kulia kwake kukamfanya aishiwe nguvu, za miguu na kujikuta akianguka chini. Kwa haraka mzee Godwin akairudisha bastola yake mkononi na kumnyanyua Manka na kumuweka kitandani kisha akatoka chumbani humo akiwa na hasira kali.
“Hakikisheni Manka hatoki humu ndani”
“Sawa mkuu”
Mzee Godwin akaondoka huku akiwa na mlinzi wake anaye muamini, moja kwa moja wakarudi ikulu kuendelea na majukumu yao.
                                                                                                               ***
Rahab, Phidaya na Agnes walikesha wakipiga hadithi mbalimbali, kila mmoja akijaribu kusimulia maisha yake ya utotoni na usichana.. Hadi inafika alfajiri hapakuwa na aliye pata hata lepe la usingizi, kila mmoja wao aliweza kufikiria mambo yanayo muhusu kwenye maisha yake hususani kwa wakati huu.
“Yaani Erickson ninampenda sana, na endapo nitakuja kujua ana mwanamke mwengine nitahakikisha nina muua huyo mwanake”
Agnes alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya Phidaya na Rahab kutazama, kabla ya Phidaya ajazungumza kitu Rahab akamuwahi.
 
“Shoga wewe nawe kwa wivu, unamuua mwanamke mwenzako kisa mwanaume?”
“Ahaaa weee Erickson wangu mtamu sana, yaani ni mwanaume shababi, anaye jua kucheza na mwanake sita kwa sita”
“Cha kufanya inabidi ikitimu saa mbili uende ukamuangalie hospitalini”
“Hapo Rahab umezungumza poit huwa ninakupendea hapo tu”
“Ndio hivyo usijikalie hapa kumbe kama ulivyo tuambia mpenzi wako ni mgonjwa”
“Sawa”
Muda wote huo Phidaya alikaa kimya akiyafikiria maneno ya Agnes jinsi yalivyo utibua moyo wake, hata urafiki ambao ulikuwa kwa masaa machache tayari umesha ingia shubiri. Wakaandaa kifungua kinywa, kila mtu akanywa kwa jinsi alivyo weza kunywa chai hiyo yenye itafunwa vingi.
 
Phidaya akarudi sebleni alipo iacha bahasha yake, akaichukua pamoja na karatasi iliyopo pembeni ambayo hakuiweka kwenye bahasha hiyo. Kabla hajaiingiza karatasi hiyo ndani ya bahasha akaipitishia macho taratibu ili kufahamu ni karatasi za nini. Phidaya hakuamini kitu alicho kiona kimeandikwa kwenye karatasi hiyo, maelezo yanaonyesha uhusiano alio kuwa nao Erickson ambaye ni Eddy pamoja na Manka ambaye ni wifi yake.
 
‘Imekuwaje hadi ukweli umejulikana?’
Phidaya alijiuliza huku akiketi kwenye sofa, macho yake yakawa na kazi ya kuirudia rudia karatasi hiyo mara kadha.
‘Ila dokta aliye fanya hivi alisha kufa’
Phidaya alizidi kuzungumza mwenyewe huku akiitazama karatasi hiyo, hadi Rahab anafika sebleni hapo, ndipo alipo iingiza karatasi hiyo kwenye bahasha.
“Karatasi za nini?”
Rahab aliuliza huku akijirusha kwenye sofa. Phidaya hakujibu kity chochote zaidi ya kukaa kimya.
“Vipi mbona kimya?”
“Agnes yupo wapi?”
“Nimemuacha akielekea chumbani kwake kuoga”
“Kuna kitu nahisi hakipo sawa”
“Ahaaa kama ni mada hizo tutazizungumza tukiondoka hapa”
Rahab alizunguzma kwa sauti ya chini huku akimtazama Phidaya kwa macho makali. Haukupita muda sana Agnes akatoka akiwa amevalia suti nyeusi. Akamrushia Rahab funguo ya gari moja huku yeye akiwa na funguo ya gari la serikali.
“Mutatumia gari hiyo”
 
“Una magari mangapi shosti?”
“Mmmm huko uwani yamejazana mengi, sikumbuki kwa haraka nina magari mangapi, si unajua kwamba starehe yangu kubwa ni magari”
“Wewe kiboko”
Wakatoka kwa pamoja na kuelekea eneo la nyuma la nyumba ya Agnes ambapo kuna banda kubwa alilo lijenga lenye magari mengi yaliyo funikwa. Rahab akayahesabu kwa haraka haraka akapata idadi ya magari ishirini na tano.
”Wee mtoto wa kike magari yote haya ni ya nini?”
“Wee acha tu sina mtoto sina ndugu, pesa yangu yote ninayo ipata ni kununua magari. Hapo kuna magari ambayo tangu niyanunue, nimeyaendesha kutoka bandarini hadi hapa”
“Wee kiboko sasa hii funguo uliyo nipa nitafungulia gari lipi?”
“Minya rimoti, litakalo piga alamu ndio hilo hilo”
Rahab akafanya kama alivyo ambia, gari la pembeni lake likaanza kupiga alamu, wakalifunua turubai lililo lifunika gari hilo. 
 
“Hiyo ni Alteza new modern zimetoka mwaka huu”
Agnes alizungumza huku akilitazama gari yake hiyo mpya kabisa. Rahab akaingia na kuliwasha gari hilo.
‘Mamaeee huyu msenge ana hela’
Rahab alijisemea kimoyo moyo, baada ya gari hiyo kumuonyesha tanki lake limejaa mafuta.  Rahab akafungua kioo cha upande wake ili kuzungumza na Agnes.
“Wee mtoto sikuwezi”
“Kwa nini?”
“Gari ipo full tank, nilidhani itakuwa na mafuta ya kulisukumia hadi sheli”
“Nyoo, gari zote hapa unapo ziona zipo full tank. Sasa utawasiliana na mimi ukiwa na simu, au hadi simu nikupe”
“Acha ujinga, nitanunua”
“Haya mwaya, Phidaya karibuni tena jamani”
“Asante”
 
Phidaya akaingia ndani ya gari, wakaondoka na kumuacha Agnes akiingia kwenye gari lake lenye namba za usajili za wizara yake. Moja kwa moja Agnes akaanzia hospitali ya Agakhan, ambapo akaelekea kwa daktari mkuu wa hospitali hiyo. Akamuuliza kuhusiana na mgonjwa wake ambaye ni Erickson Ford, majibu aliyo kutana nayo yakamshosha sana.
“Ameibiwaje ibibiwaje?”
“Kusmea kweli mimi jana sikuwepo usiku, ila nasikia hata walinzi wa raisi walishindwa kuwazuia hao walio muiba”
“Mungu wangu sasa itakuwaje?”
“Ndio hapo naona muheshimiwa ana lishuhulikia huli, naamini atapatikana tu”
“Sawa nashukuru dokta”
Agnes akaondoka hospitalini hapo huku akiwa amejawa na mawazo chungu nzima, hakujua ni nini anacho weza kukifanya ili kumpata Erickson wake.
                                                                                                           ***
“Tunaelekea wapi?”
“Tunaelekea Bagamoyo”
“Hivi unatambua kwamba hatujampata Eddy na kitu kilichopo kwenye hizi karatasi zinaonyesha kwamba Eddy na Manka ni ndugu na inavyo onyesha kuna kamchezo ambacho kamechezeka hapa”
 
Ikambidi Rahab kusimamisha gari lake pembeni na kuchukua karatasi anazo pewa na Phidaya, akazitoa kwenye bahasha na kuzitazama kwa umakini. Macho yakamtoka alipo weza kuona majibu hayo ya DNA
“Umezipatia wapi hizi karatasi?”
“Kwa daktari mmoja  ambaye alijirusha dirishani baada ya kuniona anaoneka alisha wahi kufanya mpango wa kuniua akiwa na Ranjiti aliye kuwa mume wangu”
Rahab akazipitia karatasi hizo zenye maelezo ya kina hadi jina la Eddy liliandikwa humo ndani, anaye tajwa kwamba ndio Erickson Forrd.
 
“Na ninavyo hisi huyo rafiki yako Agnes atakuwa amezisoma karatasi hizi”
“Mungu wangu”
“Yaani hapa tunatakiwa kuhakikisha kwamba tunampata Eddy na kama ni vipi ni lazima tuweze kurudi Agakhan, tukamtafute”
Rahab akafikiria kwa sekunde kadhaa, hapo hapo akageuza gari kwa kasi na safari ya kuelekea hospitali ya Agakgan ikaanza huku mawazo yao yote yakimuwaza Eddy.
Wakafika hospitali ya Agakhan, wakalikuta gari ambalo alikuwa akilitumia Eddy likiwa katika eneo la maegesho. Wakiwa hapo wakamuona raisi Godwin akiingia kwenye gari lake pamoja na walinzi wake, wakawasubiria waondoke hapo kisha Rahab akashuka na kuelekea lilipo gari ambalo ni mali yake. 
 
“Sijui ametoroshwa toroshwa vipi”
“Nasikia walio mtorosha ni wanawake mmoja ni kama mchina machina hivi”
Rahab aliweza kuyasikia mazungumzo ya wauguzi hao wawili wanao fanya usafi katika eneo hilo la maegesho.
“Lakini nasikia yule ni mke wa raisi ndio maana mwenyewe akaja hapa”
“Yaani hao walio mtorosha watakiona cha mtemakuni, si unaona mzee alivyo toka hapa jicho jekundu kama ndimu”
Rahab aliendelea kuwasikiliza wauguzi hao wa kike wanao onekana kuutumia mdua wao mwingi katika kupiga stori pasipo kufanya kazi. Rahab akajaribu kuufungua mlango wa gari lake, kwa bahati nzuri haukufungwa. 
 
“Hivi huyo aliye toroshwa si ndio yule aliye pigwa na polisi”
“Ndio huyo, anaitwa Erickson”
“Samahani dada zangu”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wauguzi hao walio katisha mazungumzo yao haraka iwezekanavyo, wauguzi hao wakaonekana kumkazia macho Rahab, wakijaribu kumfananisha na mke wa raisi aliye pita, ila mavazi aliyo yavaa, wakaamini kwamba mke wa raisi hawezi kuvaa mavazi ya aina hiyo wakiamini watakuwa wamemfananisha.
“Eti Erickson ametoroshwa?”
Wauguzi hao wakatazamana kisha wakamtazama Rahab anaye wauliza swali hilo.
“Ahaa naamini mutakuwa munanishangaa kuweza kuwauliza swali kama hilo, ila Erickson ni kaka yangu”
“Waooo kumbe ni mkwe wa raisi?”
Rahab akatabasamu huku akitingisha kichwa akikubaliana na wauguzi hao ambao wanaonekana kufurahishwa na kauli hiyo.
 
“Sasa basi, ila hizi ni fununu fununu tu. Tunasikia eti jana, Erickson alivyo letwa na mchumba wake Manka kuna wanawake walikuja wakamteka, huyo mmoja wanasema ni mswahili ila mwengine ni Mchina. Tena wamepigaje huyo Manka nasikia kwamba eti ni bwana wao”
“Bwana wa nani hapo?”
Rahab aliuliza kama vile hawajui Madam Mery pamoja na Sa Yoo.
“Huyo mwanamke nasikia ndio mpenzi wake na huyo mchina amekuja naye kupiga kug fu, wamemtandika Manka hadi kalazwa huko ndani”
“Asanteni jamani”
“Ila umbea nao dili dada. Yaani umefanana na mke wa raisi Godwin aliye pita”
Kauli ya muuguzi huyo mmoja ikamstua Rahab, ila akajikata kuutoa mstuko huo ili wauguzi hao wasimstukie.
“Ahaa si unajua kwamba duniani watu ni wawili wawili”
“Kweli aisee mumefanana, hadi kucheka”
 
“Kweli jamani asanteni”
Rahab akaingia kwenye gari hilo, na kuikuta funguo ya gari ikiwa eneo la funguo na inavyo onekana jana Manka alivyo fika nalo hapo hospitalini hakuichomoa. Akawasha na kuliweka sawa gari hilo, akaliendesha hadi sehemu alipo muacha Phidaya ndani ya gari la Agnes.
“Endesha hilo tuondoke”
“Imekuwaje?”
“Sa Yoo na Madam Mery wamemchukua”
“Sasa watakuwa wamekwenda wapi?”
“Bagamoyo nahisi?”
“Mmmm kwa bagamoyo itakuwa ngumu si unaona pale njiani kuna kizuizi cha Polisi”
“Sasa watakuwa wamekwenda wapi?”
“Nimepata wazo hembu tukawatazame nyumbani kwangu, tukiwakosa hapo basi tutajua ni wapi kwa kwenda”
“Sawa”
                                                                                                                  ***
Kwa haraka Madam Mery akamuwahi Shamsa na kuanza kusugua sugua kifuani mwake ila kutapika kupungue. Sa Yoo naye aliye kuwa amelala akakurupuka baada ya kusikia sauti ya Shamsa, akiugulia ugulia.
“Ehee vipi tena?”
Sa Yoo aliuliza kwa mshangao huku akisimama.
“Kamletee maji jikoni”
Sa Yoo akauondoka hospitalini hapo, baada ya dakika mbili akarudi akiwa ameshika kombe kubbwa lililo jaa maji pamoja na kidishi kidogo. Akamnywesha Shamsa maji, akasukutua na kuyatemea maji hayo kwenye kidishi hicho.
 
“Unajisikiaje?”
“Maumivu  mgongoni?”
“Ni risasi uliyo pigwa sijui na nani?”
“Kwanza nimefikaje fikaje hapa?”
Shamsa alizungumza huku akihema.
“Ulikuja jana na gari sisi tukasikia honi getini kutoka tukakukuta ni wewe”
Gafla kitu kizito kilicho rushwa dirishani na kuvunja dirisha hilo la kioo lililopo hapo hospitalini, kikaanza kutambaa huku kikitoa moshi mwangi mweupe na wenye hewa nzito inayo chefua kuanzia koo hadi macho ya kila mmoja aliye kuwepo katika sebule hiyo, alijikuta akikohoa huku machozi yakimtoka. Kabla hawajajua ni nini cha kufanya milio ya risasi ikaanza kusikaka nje ikivunja vunja vioo vya madirisha ya sebule nzima na kuwafanya Sa Yoo na wezake kuchanganyikiwa.
                                                                                          
SORRY MADAM (91) (Destination of my enemies)

“Nini hicho jamani?”
Sa Yoo aliuliza huku akikohoa sana, japo anaelekewa kabisa ni kitu gani kinacho tokea, ila alijikuta akiuliza swali ambalo hapakuwa namtu hata mmoja aliye weza kulijibu kwa haraka zaidi ya wote kukohoa kohoa.
“Sa Yoo msukumeni Eddy munifwate”
Shamsa alizungumza huku akijikaza kunyanyuka kwenye kochi, Sa Yoo na Madam Mery nao wakajikaza kusukuma kitanda hicho alicho lalia Eddy, ambaye naye muda wote ana kohoa.
 
Wakamfwata Shamsa aliye ingia kwenye moja ya chumba ambacho hakina kitu chochote zaidi ya picha picha nyingi zilizo bandikwa ukutani, Sa Yoo akafunga mlango wa chumba hicho na kumtazama Shamsa akitoa picha kubwa iliyopo ukutani. Shamsa aalipo fanikiwa kusogeza picha hiyo iliyo ficha  batani nyingi zilizopo kwenye ukuta. Shamsa kwa haraka kwa kutumia mkono ambao hauna jeraha, akaminya batani hizo akionekana zina namba ya siri, Sa Yoo na madam Mery wakajikuta wakishangaa, kipande cha ukuta mwengine ndani ya chumba hicho ambacho kikifunguka.
 
“Nendeni”
Shamsa alizungumza, Madam Mery na Sa Yoo wakamsukuma Eddy hadi ndani ya chumba hicho ambacho ni cha siri, kisha yeye akaingia na ukuta huo kujifunga. Shamsa akawasha taa zilizomo ndani humo. Ukubwa wa chumba hicho kilicho jaa mitambo mingi, kikawashangaza Madam Mery na Sa Yoo.
“Waoooo”
Sa Yoo alizungumza huku akisogelea moja ya mtambo mkubwa uliopo ndani ya chumba hicho, akiushangaa jinsi ulivyo.
“Hii ni nini?”
“Anaye fahamu ni Eddy mwenyewe, mimi huwa nina iona tu hiyo mitambo”
“Eti Eddy hii ni mitambo ya nini?”
“Nitawaambia pale muda utakapo fika”
                                                                                                    ***
     Kitu cha kwanza baada ya kufika ikulu, Mzee Godwin akaitisha kikao cha dharura. Wataalamu wake maalumu wanao husika na maswala ya teknologia, akakutana nao kwenye ukumbi huo wa mkutano huku akiwa na kartasi mbili zenye sura ya Sa Yoo pamoja na madam Mery.
“Nahitaji hizi sura muzitafute sasa hivi kwa kutumia satelait”
“Sawa mku”
 
Kazi ikaanza ya kuzitafuta sura za Madam Mery na Sa Yoo. Wataalamu hao wakazichukua picha hizo na kuzi scan na kuziingiza kwenye mtandao maalumu ambao wameuunganisha na satelaiti zenye rekodi ya kila kiumbe aliyepo juu ya ardhi. Sura za watu kadhaa ndani ya Tanzania zikaanza kupita kwa kasi kwenye kioo kikubwa cha Tv iliyopo humo ndani ya ofisi ya raisi, iliyo unganishwa na kompyuta inayo fanya kazi hiyo ya kutafuta sura hizo za watu.
 
Alama nyeukundu ikalia na kuonyesha sura ya madam Mery na sehemu ilipo, haikuchukua muda sana ikaonyesha na sura ya Sa Yoo na wote wanaonekana wapo sehemu moja.
“Andaeni kikiso ninakwenda kuwatafuta watu hawa hakikisheni kwamba wanapatikana wakiwa hai”
“Sawa mkuu”
Mzee Godwin akingia ndani kwake, akabadilisha mavazi yake, akavaa kombati za jeshi ambazo alikuwa anazitumia akiwa mkuu wa majeshi kabla ya kuliasi. Akachukua bastola zake mbili zenye silaha za kutosha. Akatoka nje na kukuta kikosi cha vijana wake wapatao ishirini wakiwa wamesha jiandaa kwenye magari maalimu yenye uwezo wa kubebe silaha nzito.
 
“Mkuu nakuomba usiende”
 Mlinzi wa mzee Godwin alizungumza huku akimzuia, ila kwa jicho kali alilo katwa na mzee Godwin akajikuta akitulia kimya, na kumfwata mzee huyo anaye onekana kushikwa na hasira kali sana. Wakaingia kwenye magari, mlinzi wa mzee Godwin akatoa simu yake na kuandika ujumbe mfupi wa mesiji na kuutuma kwenye simu ya mmoja wa walinzi wanao mlinda Manka hospitalini.
“Lazima huyu malaye leo nimuue kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Alizungumza Mzee Godwin huku magari yakizidi kusonga mbele kuelekea sehemu ambapo ndipo anaamini alipo Madam Mery pamoja na Sa Yoo walio muiba mkwe wake, aliye pelekea hadi Manka kuwa na gadhabu sana.
                                                                                                         ***
“Madam kuna ujumbe ambao nimepewa nikupatie”
Mlinzi huyo alizungumza huku akimkabidhi Manka simu yenye ujumbe ulio tumwa, unao someka ‘MUHESHIMIWA ANA GADHABU SANA, ANA KWENDA KUMVAMIA MADAM MERY NA INAONEKANA SEHEMU TUNAPO ELEKEA NI NYUMBA YA ZAMANI YA KAKA YAKO EDDY’
Ujumbe huo ukamkurupusha Manka kitandani na kujikuta akishuka na kusimama, akamtazama mlinzi huyo aliye simama pembeni yake.
 
“Kuna gari?”
“Ndio muheshimiwa”
“Nahitaji kuondoka hapa sasa hivi”
“Ila muheshimiwa alisema kwamba usiondoke”
“Unataka kumuona muheshimiwa wako anaingia kwenye matatizo mengine ambayo yataigharimu serikali eheeee”
Manka alizungumza kwa hasira hadi mlinzi huyo akawa ana tetemeka. Hapakuwa na jinsi zaidi ya kukubali kuondoka hospitalini hapo. Mlimzi mmoja akawa na jukumu la kuiendesha gari hilo la ikulu huku mwengine akiwa ameketi siti ya nyuma, na Manka akawa na kazi ya kumuelekeza mlinzi huyo ni wapi kwa kwenda. Kwa njia za mikato mikato wakafanikiwa kukuta msafara wa Mzee Godwin ukiwa unakaribia kabisa kufika nyumbani kwa Eddy.
 
“Uzuie kwa mbele”
“Sawa madam”
Mlinzi huyo akaongeza mwendo ulio zipita gari zote hizo, akafunga breki kwa mbele, na kuiziba barabara nzima ya lami na kusababisha gari zote zilizopo kwenye msafara kusimama gafla. Manka akaitazama saa iliyomo ndani ya hilo gari inaonyesha ni saa moja kasoro. Akashuka kwenye gari na kusimama mbele ya msafara wa magri hayo.
“Huyu mtoto mwendawazimu amekuja kufanya nini?”
Mzee Godwin alizungumza huku akishuka kwenye gari hilo macho yake yakiwa na hasira kali sana, akamtazama Manka aliye simama mbele ya msafara huo huku mikono yake akiwa ameinyoosha kama yesu alivyo sulubishwa. Akaachia msunyo mkali na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka hadi sehemu alipo simama Manka.
 
“Baba kwa nini unaf…….”
Kofi zito lililo tua shavuni mwa Manka likamfanya akatishe ile kauli ambayo alianza kuizungumza. Kila mlinzi aliyopo eneo hilo akawa kimya akitazama vita kati ya baba na mwana.
“Ondoka mbele ya uso wangu”
Manka huku machozi yakimwagika, akanyoosha tena mikono yake kama alivyo kuwa ameinyoosha hapo awali.
“Baba kwa nini unataka kumuua mama mdogo amekufanyia nini wewe?”
Kofi jengine zito likatua shavuni mwa Manka, hili likamfanya kuyumba mara kadhaa, kisha akaka sawa na kurudia mtindo wa kunyoosha mikono yake na kumzuia mzee Godwin asifanye chochote juu ya madam Mery.
 
“Huwa nikiwa katika hali kama hii sinto jail kama wewe ni mwanangu au laa, nitakuchangua ubongo wako. Toka mbele ya uso wangu”
“Baba siwezi kufanya hivyo”
Mzee Godwin kwa hasira akachomoa bastola yake na kumnyoshea Manka aliyo isogelea karibu kabisa na kuigusa bastola hiyo kwa paji lake la uso.
“Kama utakubali kuona damu ya mwanao mpendwa wa kike ikimwagika mbele yako nipige risasi”
Mzee Godwin akamtazama jinsi Manka alivyo simama mbele hapo, bila ya Manka kujua ni kitu gani kinaweza kufwata akastukia akipigwa na kitako cha bastola hiyo kwenye shingo yake na kuanguka chini na kupoteza fahamu.
 
Mzee Godiwin akawaamuru walinzi hao hao ambao walikuja na Manka wamchukue na kumpekea ikulu, huku safari ikaendelea. Wakafika kwenye geti kubwa, mzee Godwin akashanga kuona ni nyumbani kwa Eddy na anapafahamu vizuri sana.
“Pumbavu huyu mshenzi ndio aliye watuma hawa malaya zake kumteka mkwe wangu, pumbavu sana”
Mzee Godwin alizungumza huku akishuka kwenye gari, akawaamuru askari wake alio kuja nao kuvamia ndani ya nyumba hiyo na kuhakikisha kila aliye kuwemo ndani ya nyumba hiyo anatiwa mikononi akiwa hai.
Askari wenye mabomo ya machozi wakingia ndani ya geti kwa umakini huku wakiwa wamavalia vifaa maalumu vya kujikinga na moshi mkali wa mabomu hayo. Wakakuta gari mbili zikiwa nje hapo huku moja likiwa ni gari la wagonjwa, lililo ibiwa jana hospitalini.
 
“Wamo humu humu ndani”
Mmoja wa askari alizungumza huku akinyata hadi dirishani, akasikia sauti za kike bila ya kuuliza mara mbili mbili akarusha bomu moja la machozi  mwenzake akarusha bomu la pili la machozi, kisha wakarudi nyuma. Askari wengine walio kuwepo nyuma yao wakanza kushambulia kwa risasi. Kwenye vioo pamoja na milangoni.
“Acheni kushambulia”
Mzee Godwin alipaza sauti na kuwafanya askari wote kuacha kushambulia kwa risasi ndani humo
“Nimesema ninahitaji wakiwa hai sitaki hata mmoja nimkute amekufa”
“Sawa mkuu”
Ikawabidi askari hao kuvamia ndani, na kukuta sebleni hakuna mtu ila kuna vitu vina ashiria kwamba watu wapo humu humu ndani ya hii nyumba.
                                                                                                                  ***
Rahab akajikuta akipunguza mwendo kasi wa gari lake, baada ya kuona gari mbili za ikulu ambazo hutumika kwenye mashambulizi hususani pale ikulu inapo vamiwa zikiwa zimesimama nje ya geti la nyumba ya Eddy.
 
“Kuna nini pale?”
Phidaya aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka. Tayari wasiwasi mwingi ulisha anza kumvaa
“Pale kuna uvamizi”
“Uvamizi wa nini tena”
“Walinzi wa mzee Godwin ndio wamevamia eneo hili”
“Mungu wangu wamesha jua ni wapi Eddy alipo”
“Usishuke kwenye gari”
Rahab alizungumza huku akishuka ndani ya gari, baada ya kulisimamisha gari lake mbali kidogo na ilipo nyumba ya Eddy. Akaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari. Milio ya risasi, ilimuashiria kabisa, ajiweke tayari kwa lolote. Akazidi kupiga hatua hadi karibu kabisa na lilipo simama gari moja, akachungulia ndani ya gari hilo akakuta hakuna mtu wa aina yoyote.
 
Akanyata hadi kwenye gari la pili akakuta kuna askari mmoja amesimama nje hapo huku akiwa ameshika bunduki yake. Bila ya kupoteza muda Rahab akamrukia askri huyo, akampiga ngumi kadhaa na kumuzimisha hapo hapo.
Akaichukua bunduki hiyo na kusimama getini, akachungulia na kuona jinsi Mzee Godwin anavyo pandisha ngazi za kuelekea ndani ya jumba la Eddy. Nje ya kuna askari wanne wamesimama wakiwa na bunduki zao.
 
Rahab akatoa magazine ya bunduki hiyo aina ya AK-47 na kukuta ina risasi za kutosha, akashusha pumzi kidogo huku akifumba macho yake, kumbukumbu za bomu lililo muua mume wake aliye kuwa raisi, zikamjia kichwani mwake na kujikuta akifumbua macho huku ameyeng’ata meno, akaanza kuzimimina risasi hizo kwa askari hao walio simama akili na macho yao zikiwa kwenye tukio hilo.
Rahab alipo hakikisha kwamba askari hao wote wamekufa, akaingia ndani huku bunduki yake ikiwa mkononi mwake, akajibanza kwenye gari la wagonjwa na kusikilizia ni nini kinacho endelea huko ndani.
 
“Nenda kaangalie ni nini kilicho tokea nje huko”
Mzee Godwin akamuagiza mlinzi wake akatazame nje baada ya kusikia milio ya risasi. Milio mlio wa risasi ukwastua Mzee Godwin na askari wake na kuwafanya akili zao zote kuzipeleka nje na kuachana na swala la kuwaska Madam Mery na Sa Yoo.
“Mlindeni raisi”
Mmoja wa askari hao alizungumza huku wakiwa wanatoka nje, wakiwa wamemzunguka raisi Godwin na kumuweka katikati.
“Yes nafasi nzuri sana”
Rahab alizungumza huku akinyanyuka kutoka katika sehemu aliyo jibanza. Kila risasi moja anayo ipiga inaondoka na askri mmoja. Mzee Godwin akajikuta akichanganyikiwa baada ya kuzidi kuwaona askari wake wanaanguka mmoja baada ya mwengine hadi akabaki yeye mwenyewe.
 
“Mikono juu”
Rahab alizungumza huku akimuamuru Mzee Godwin aliye inyoosha mikono yake juu pasipo kupenda. Bastola zake zote mbili akazitupa pembeni akiashiria kushindwa.
“Rahab…….?”
“Ndio mimi, una shangaa sana kuniona eheee?”
Rahab alizungumza huku akiwa ameushikilia mtutu wa bunduki akipiga hatua za taratibu akimfwata mzee Godwin katika eneo alilo simama.
“Wewe na mumeo si niliwaambia muondoke nchini kwangu?”
“Nchi hii wala sio ya kwako. Huna maamlaka ya kunifukuza mpumbavu wewe”
“Mshezi wewe nitaku…….”
Rahab akamtandika mzee Godwin risasi ya mguu na kumfanya aanguke chini na kutoa ukelele mkali wa maumivu. Ukimya ulio tawala kwa dakika kadhaa ukamfanya Phidaya kushuka ndani ya gari na kuanza kutembea kwa umakini huku akielekea getini, alipo fika, akachungulia, akamuona Rahab alivyo mshikia bundiki Mzee Godwin. Phidaya akaingia kwa kujiamini hadi sehemu alipo simama Rahab
 
“Phidaya!!”
“Mshenzi mpumbavu huyu mzee muue”
Phidaya alizungumza kwa hasira huku akiwa amemkodolea macho mzee Godwin.
“Phidaya nenda ndani ukawatazame kina Sa Yoo”
“Sawa”
Phidaya akapandisha ngazi hizo kwa haraka hadi sebleni, hakukuta mtu kwa haraka akili yake ikamtuma kupandisha gorofani ambapo pia hakukuta mtu wa aina yoyote. Kwa haraka akashuka na kukumbuka kuna chumba ambacho siku za nyuma mume wake alisha mueleza kukiwa na tatizo anaweza kukimbilia kwneye chumba hicho na kujificha.
 
Akaingia kwenye chumba hicho na kukuta sehemu ambayo kuna batani nyingi, picha yake ikiwa imeondolewa. Akaingiza namba za siri za kuufungua mlango huo ulio kaa mithili ya ukuta, ukafunguka na kukutana na mwanga wa taa ukionyesha kwamba watu wamo humo ndani.
Phidaya akaingia ndani humo, hakuamini macho yake baada ya kuwakuta Shamsa, Eddy, Sa Yoo na Madam Mery wakiwa wanatizama ni nani anaye ingia. Sa Yoo akamkimbilia Phidaya na kumkumbatia kwa nguvu.
 
“Tumeshinda jamani”
Phidaya alizungumza kwa furaha huku akimuachia Sa Yoo na kumfwata mume wake sehemu alipo lala. Cha kwanza kukifanya akampiga busu la mdomo Eddy aliye achia tabasamu pana baada ya kumuona mke wake huyo.
“Honey tumemtia Godwin mikononi mwetu”
“What……?”
Madam Mery alizungumza huku akimtazama Phidaya usoni, kwa maana jambo alilo lizungumza hakuna mtu ambaye anaweza kuliamini kwa haraka kiasi hicho.
“Rahab yupo hapo nje kwenye ngazi amemshikia bunduki”
Sa Yoo akajikuta akishangilia kwa furaha, ila sura ya Madam Mery ikapoteza furaha, na kumfanya Eddy naye kupoteza furaha yake.
 
“Ina maana hamuniamini au?”   
“Phidaya nina mjua Godwin hawezi kukamatika kiholela kiasi hicho”
Madam Mery alizungumza kwa msisitizo, huku akiwa amemkazia macho madam Mery
“Jamani nimemkuta akiwa amelala chini mguuni amepigwa risasi”
“Kwa nini tubishane twendeni tukamuone”
Sa Yoo akaanza kukisukuma kitanda cha Eddy huku Phidaya na Madam Mery wakiwa wametangulia mbele, huku Shamsa akifwata kwa nyuma. Wakatoka kwenye vyumba hivyo na kwenda nje. Walipo fika kila mmoja akabaki ameduwaa hususani Phidaya kwa maana Raisi Godwin na Rahab wametoweka eneo hilo.
                                                                                           ITAENDELEA- USIKOSE SEHEMU YA 92

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts