Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 92 & 93 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 92 & 93 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Wednesday, February 14, 2018 | 10:21:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Sa Yoo akajikuta akishangilia kwa furaha, ila sura ya Madam Mery ikapoteza furaha, na kumfanya Eddy naye kupoteza furaha yake.
“Ina maana hamuniamini au?”   
“Phidaya nina mjua Godwin hawezi kukamatika kiholela kiasi hicho”
Madam Mery alizungumza kwa msisitizo, huku akiwa amemkazia macho madam Mery
“Jamani nimemkuta akiwa amelala chini mguuni amepigwa risasi”
“Kwa nini tubishane twendeni tukamuone”
Sa Yoo akaanza kukisukuma kitanda cha Eddy huku Phidaya na Madam Mery wakiwa wametangulia mbele, huku Shamsa akifwata kwa nyuma. Wakatoka kwenye vyumba hivyo na kwenda nje. Walipo fika kila mmoja akabaki ameduwaa hususani Phidaya kwa maana Raisi Godwin na Rahab wametoweka eneo hilo
 
ENDELEA
“Wamekwenda wapi?”
Phidaya aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka. Madma Mery akajikuta akikaa chini, huku nguvu za mwili zikiwa zimemuishia.
“Tuondokeni eneo hili si salama”
Eddy alizungumza huku akijaribu kukaa kwenye kitanda, maumivu makali aliyo yapata kwenye mbavu zake hayakumzuia kabisa kuweza kunyanyuka na kukaa kitako.
“Utataka kwenda wapi Eddy?”
“Ni bora nyinyi kuondoka kuliko kuingia mikononi mwa askari”
 
“Unataka kusema kwamba…….”
Phidaya aliuliza huku macho yake akiwa amemtolea Eddy aliye lala kwenye kitanda hicho.
“Ondokeni eneo hili sio salamaa”
Eddy alizungumza kwa msisitizo na kuwafanya  Shamsa kuelewa maana yake ni nini. Shamsa kwa haraka akaingia ndani, moja kwa moja akaelekea katika chumba ambacho walikuwepo. Akachukua mbastola nne zenye magazine zilizo jaa risasi kisha akatoka nje kwa haraka.
“Inabidi kuondoka eneo hili sasa hivi”
“Na Eddy?”
“Mimi mutaniacha hapa, ondokeni”
Taarifa hiyo, ikauingiza moyo wa Phidaya simanzi kubwa sana, kwa maana hakujua ni kwanini mume wake amechukua maamuzi kama hayo. Kwa haraka akamfwata Eddy kitandani na kukumbatiana huku Phidaya machozi yakimwagika, na Eddy machozi yakimlenga lenga.
 
“Nitakuwa salama”
Phidaya hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzidi kumwagikwa na machozi, tayari Shamsa alisha ingia kwenye moja ya gari, ambalo ni mali ya ikulu. Madam Mery na Sa Yoo nao wote wakaingia ndani ya gari hilo na kumsubiria Phidaya anaye endelea kumng’ang’ania mume wake.
“Nenda mke wangu nitakuwa salama”
“Niahidi hauto kufa?”
“Nakuahidi, kimbia kabla askari hawajafika hapa”
Phidaya akamuachia Eddy na kumpiga busu la mdomo, kisha akashuka kwenye ngazi hizo kwa haraka na kuingia ndani ya gari, Shamsa ambaye tayari alisha lifungua geti hilo muda alipo kuwa anashuka chini, akakanyaga mafuta ya gari hilo ambalo ni aina ya Aud 5q lenye sifa ya kuto kuingia risasi na ndio gari ambalo hutembelea raisi Godwin.
Kipindi gari hiyo inamalizikia kutoka nje, machozi yakatiririka usoni mwa Eddy ambaye hakuweza kujumuika katika safari hiyo, kwanza kutokana na mshono wa oparesheni aliyo fanyiwa jana tu, pili ni kutokana hajulikani kama yeye ndio Eddy, ila anajulikana kwa jina la Erickson Forrd hii ni kutokana na sura yake.
 
Hazikupita hata dakika tano, ving’ora vya gari za polisi pamoja na usalama wa taifa vikasikika nje ya nyumba ya Eddy. Alicho kifanya Eddy ni kujilaza kitandani hapo huku machozi yakiendelea kumwagika.
Askari wengi wenye bunduki mikononi mwao wakaingia ndani humo kwa umakini, wakaanza kukagua maiti moja baada ya nyingine.
“Erickson”
Eddy akamuona Manka akimfwata sehemu alipo lala. Taratibu Manka akapiga magoti chini, na kumbusu Eddy mdomoni.
“Nashukuru Mungu nimekupata”
Eddy hakujibu kitu zaidi ya kumwagikwa na machozi usoni mwake. Madaktari wa jeshi walio fika eneo hilo la tukio, wakamchukua Eddy na kumuingiza kwenye gari ya wagonjwa, huku akiambatana na Manka ambaye hakuhitaji kumpoteza tena.
 
Askari walio baki huku nyuma kazi yao ikwa ni miili ya askari walio pigwa risasi, kati ya askari ishirini walio fika katika eneo hilo, ni mmoja tu ambaye ni mlinzi wa raisi Godwin aliye weza kuwa hai japo hali yake ni mbaya
“Muheshimiwa raisi…..a…me..ch…..u”
Hakumalizia kitu alicho kuwa anakizungumza akapoteza fahamu.
“Muwahisheni hospitalini, huyu atatufaa”
Mkuu wa kitengo cha polisi kanda maalimu bwana Erinest Komba aliwaeleza vijana wake, ambao wakafwata amri kama alivyo zungumza mkuu wao. Habari ya raisi Godwin kutoweka ikaanza kusambaa kwa kasi kupitia mitandao  ya kijamii, huku vituo vya televishion na maredio vikiwa vinatafuta ukweli juu ya jambo hilo. Hapakuwa na mkuu yoyote wa jeshi aliye weza kudhibitihs habari hizo kwa maana hapakuwa na mtu mwenye ushahidi katika hilo.
                                                                                                         ***
“Jikaze usilie, unavyo lia unadhani mimi nitafanyaje?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Phidaya anaye lia njia mzima
“Ila mume wangu atakuwa kwenye matatizo”
“Sio rahisi kwa Eddy kuingia kwenye matatizo ndio maana akatuambia tuondoke”
Muda wote madam Mery akawa kimya akilichunguza gari hilo, kwa bahati nzuri akaona kifaa maalumu ambacho kipo siti ya nyuma ya dereva eneo alilo kaa yeye kinacho weza kuonyesha ni sehemu gani raisi yupo, hata walinzi wake wanapo kaa ikulu.
“Shamsa simamisha gari?”
“Kuna nini?”
“Simamisha gari kwanza”
Shamsa ikambidi kutii kile kitu ambacho madam Mery amemueleza, kwa haraka madam Mery akashaka kwenye gari, akamuomba Shamsa kufungua buti ya gari, Shamsa akaminya batani iliyo ruhusu buti ya gari hilo kufunguka, madam Mery akalinyanyua, akakuta kifaa kidogo kinacho ongoza kifaa alicho kiona ndani ya gari hilo.
 
“Ohoo ni GPRs system”
Sa Yoo alizungumza mara baada ya kuona kifaa hicho.
“Ndio nini?”
Shamsa aliuliza mara baada ya kushuka kwenye gari na kuzunguka nyuma kwenye buti ya gari hilo.
“Sehemu yoyote  tunapo kwenda nah ii gari lazima tuonekane”
“Sasa inakuwaje?”
Hata kabla Sa Yoo hajajibu swali hilo, wakaziona gari nne nyeusi, aina ya GVC zinazo piga ving’ora zikiwafwata kwa kasi katika eneo hilo.
“Ohooo rudini kwenye gari wote”
Shamsa alizungumza kwa haraka akafunga buti ya gari hilo, wote wakaingia ndani gari, bila ya kupoteza muda, Shamsa akakanyaga mafuta ya gari na kuondoka eneo hilo kwa kasi kubwa.
“Fungeni mikanda”
Shamsa alizungumza huku akifunga mkanda wa siti aliyo kalia. Gari  hizo nne za makachero wa usalama wa taifa, zikazidi kuifukuza gari hiyo ya raisi huku mkuu wao aliye panda gari la mbele akiwa na simu maalumu inayo onyesha gari hilo la raisi kila sehemu anapo kwenda.
 
“Ongeza mwendo, hawa watu ndio walio mteka raisi”
“Sawa mkuu”
Dereva huyo, ambaye naye ni kachero anaye sifika katika maswala ya uendeshaji wa gari kwa kasi, akawa ndio kama amechochewa, akazidi kukanyaga mafuta kwa kasi, hadi madereva wezake wanao endesha magri matatu yaliyo nyuma yao akawaacha kwa umbali kidogo.
“Wanazidi kutufwata”
Sa Yoo alizungumza huku mara kwa mara akigeuza kichwa chake nyuma. Katika uendeshaji wa gari, Shamsa anajimudu sana, ila kitu kinacho mfelisha kwa wakati huu, ni bega lake lililo pigwa risasi, na ndio kwanza kidonda hakijapona na maumivu anayo yaoata hapo ni makali kupindukia sema tu anajikaza kuwaokoa wezake kwa maana wakiingia mikononi mwa Makachero hao, hakuna mtu mwenye jawabu la kujua ni nini atakacho fanywa.
 
“Sa Yoo”
“Mmmmm”
“Nasikia kizunguzungu”
Shamsa alizungumza na kuwafanya wezake wote kumkodolea mamcho, kwani mwendo anao tembea nao Shamsa unaelekea kwenye spidi mita mia mbili isitoshe barabara waliyopo Sa Yoo haifahamu, na madam Mery naye hawezi kuendesha gari kwa mwendo huo, wala Phidaya ambaye anaonekena kichwa kujawa na mawazo mwengi. Kadri jinsi Shamsa anavyo zidi kuendesha gari hilo ndivyo jinsi maumivu ya bega yalivyo pelekea kizunguzungu zidi kumtawala na kusababisha macho yake kutoa anza kuona mbele vizuri.
                                                                                                                           ***
   Breki ya kwanza ikawa ni ikulu, madaktari walio andaliwa kumpokea Erickson waka tayari wamesha andaa kitanda maalumu cha kumpakiza Erickson. Gari la wagonjwa linalo milikiwa na jeshi lilipo simama tu, mlango wa nyuma ukafunguliwa, wakaingia madaktari wawili, wakakishusha kitanda cha Erickson huku Manka naye akifwatia kwa nyuma. Moja kwa moja wakamkimbiza katika chumba maalumu anacho tibiwa raisi.
 
“Dokta vipi hali yake itakuwaje?”
“Tunamchoma sindano ya usingizi kidogo maumivu anayo yapata yapungue na baada ya hapo tunauchunguza mshono wake kama utakuwa na mapungufu basi tutaufanyia marekebisho”
“Sawa nakuamini daktari hakikisha hali ya Erickson inakuwa sawa, na endepo ataamka hakikisheni munanijulisha mimi kwanza kabla ya mtu mwengine”
“Sawa madam”
Baada ya Manka kutoa maagizo hayo, moja kwa moja akaelekea kwenye chumba cha mawasiliano na kukuta wakuu wa majeshi na viongozi baadhi wa serikalini, akiwemo makamu wa raisi pamoja na waziri mkuu wakiwa wanafwatalia mashindano ya gari hilo la raisi na makachero wa usalama wa ataifa, yanayo chukuliwa muda huo moja kwa moja na helcoptar ya jeshi inayo tumia katika maswala ya habari.
 
“Mumefanikiwa kujua ndani ya gari kuna raisi?”
Manka aliwauliza viongozi hao huku macho yake yakitazama tv kubwa iliyopo ndani ya ofisi hiyo kubwa ya mawasiliano.
“Hapana ila tuna imani kwamba wamemshikilia”
“Wanaelekea wapi kwa sasa?”
“Wapo katika barabara ya Morogoro, sasa kuna baria Chalinze nina imanigari hiyo itasimamishwa”
Manka akakaa kwneye moja ya kiti, huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio. Japo baba yake ni mkosaji na amewakosea watu wengi sana ila moyo wake umejaa mapenzi tele kwa baba yake, hakuwa tayari kuweza kusikia kwamba baba yake amepata tatizo baya.
                                                                                                                     ***
“Muheshimiwa tuombe ruhusa ikulu kuweza kuishambulia hii gari?”
Mmoja wa makachero alizungumza huku akimtazama bosi wake aliye kaa siti ya nyuma.
“Hatuwezi kufanya hivyo raisi yupo ndani ya gari hilo”
“Wanakwenda kasi sana”
“Ni lazima tuwapate, nimeambiwa hapa Chalinze kuna kizuizi cha jeshi, naamini tukifika hapo watasimama”
Mkuu huyo alizungumza huku akilitupia macho gari hilo la raisi linavyo zidi kwenda kasi, gafla gari hiyo ikaanza kuyumba yumba na kuwafanya makachero wote kushangazwa.
Sa Yoo akagundua asipo fanya kitu basi wanapo elekea wanakwenda kufa, akayatupia macho yake kwenye helcopta iliyopo juu kidogo pembeni yao inayo wafwata.
“Sa Yoo, nisaidie”
 
Shamsa alilalama huku nguvu za mikono zikimuishia na kulifanya gari hilo kuyumba yumba. Kwa haraka Sa Yoo akafungua mkanda wa siti yake, kisha akaufungua mkanda wa siti ya Shamsa kisha kwa umakini mkubwa huku akiwa ameushikilia mskani wa gari hilo akijitahidi kuliweka sawa. Shamsa akahamia kwenye siti aliyo kuwa amekaa Sa Yoo kisha Sa Yoo akakaa kwenye siti hiyo.
Kitu cha kwanza kufanya Sa Yoo, akafunga breki za gari hilo na kuifanya isimame, gari zinazo wafukuzia kwa nyuma nazo zikajikuta zikipunguza mwendo.
“Wee Sa Yoo umefanyaje, wanakuja hao”
Phidaya alilalama huku akitazama nyuma. Sa Yoo hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kutema mate kidogo kwenye kiganja chake cha mkono wa kulia, kisha akayapekecha kwenye kiganja cha kushoto. Akatazama kwenye kioo chake cha pembeni na kuona jinsi gari hizo nne zinavyo zidi kuwasogelea.
 
“Shamsa funga mkanda”
Sa Yoo alipo maliza kuzungumza maneno hayo, akakanyaga breki pamoja na mafuta kwa kwa wakati mmoja na kuzifanya tairi za nyuma ya gari hilo kuserereka kwenye lami hiyo na kusasabisha moshi mwingi ambao uliwafanya madereva wa gari hizo za makachero, kuzidi kupunguza mwendo kwa maana mbele hawaoni. Sa Yoo alipo hakikisha kwamba moshi umekuwa mwingi akaachia breki na kuyaruhusu matairi yote kuanza kuzunguka kwa kasi ambayo alisha itafuta kwa dakika kadhaa.
“Anaondoka huyo munapunguza mwendo nini?”
Ilisikika sauti ya makamu wa raisi kwenye kinasa sauti cha mkuu wa makachero.
“Nenda nenda wanaondoka hao”
Mkuu huyo alizungumza na kumfanya dereva wa gari lake kuongeza mwendo.  Hadi wanaupita moshi huo, gari ya raisi ilisha waacha kw umbali mkubwa na kuwafanya madereva wa magari hayo kuchanganyikiwa na kuzidi kuendesha mwendo kasi.
 
“Shamsa unajisikiaje?”
“Ongeza AC kidogo”
Sa Yoo akafanya kama Shamsa alivyo muagiza, huku akizidi kuendesha gari hiyo kwa mwendo kasi, kwa wingi wa magari yanayo kwenda nje ya Dar es Salaam, na kuingia ndani ya Dar es Salaam, yakamfanya Sa Yoo mara kwa mara kupunguza mwendo na kuyapita pale anapo pata nafasi ya kufanya hivyo. Hata kwa upande wa magari hayo ya makachero hali ikawa ni hiyo ila kwao kidogo ikawa kina unafuu, hii ni kutokana na gari zoa kuwa na ving’ora na ni sheria kwa madereva pale wanapo sikia ving’ora vya polisi au vya gari za wagonjwa ni lazima kuzipisha gari hizo.
“Ongeza mwendo tunakaribia kuwafikia”
Mkuu huyo alizidi kulaalama na kumfanya dereva wake kuongeza mwendo. 
 
“Shamsa unataka kufanya nini?”
Sa Yoo aliuliza baada ya kumuona Shamsa akishusha kioo cha gari kwa upande alio kaa yeye. Shamsa akatoa bastola mbili akazichunguza vizuri, alipo pata uhakika zina risasi za kutosha. Akashusha pumzi kidogo na kuwatazama Phidaya na madam Mery alio keti siti za nyuma.
“Lipite hilo lori la mafuta”
“Mbele kuna basi linakuja?”
“Wewe lipite tu”
Sa Yoo akawasha taa zote za mbele, japo ni mchana, ila sababu ya kuwasha taa hizo ni kumushiria dereva wa basi hilo kupunguza mwendo, kisha akaanza kulipita lori hilo lenye matela, mawili ya mafuta. Dereva wa basi alipo ona ishara ya gari hiyo ndogo, yenye alama gari analo tumia raisi, akapunguza mwendo kasi wake. Sa Yoo akafanikiwa kulipita lori hilo, Shamsa bila hata ya kuhofia chochote, akajichomoza kwenye kioo, akapiga risasi tairi za mbele ya lori hilo na kulifanya kuanzakuyumba, akapata upenyo mwengine wa kufyatua risasi kwenye tanki hizo za mafuta na kusababisha mlipuko mkubwa katika barabara hiyo. Gari zote za makachero zikajikuta zikifunga breki baada ya lori walilo litarajia kulipita, kulipuka na kuanguka na kusababisha kuifunga barabara.
 
“Fuc*”
Mkuu wao huyo alijikuta akiachia matusi mengi kwani, huo ndio mwisho wa kulikimbiza gari hilo la raisi. Taratibu Shamsa akakaa kwenye siti yake na kufunga kioo cha gari.
“Kazi nzuri mwanangu”
Phidaya alijikuta akimsifia Shamsa huku akitabasamu kwa maana hakuamini kitu alicho kifanya, japo bado anaumwa.
“Asante mama”
“Shamsa angalia kule mbele”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akipunguza mwendo kasi wa gari, wote wakajikuta wakitazama mbele, kila mmoja akahisi kuchanganyikiwa kwa maana barabara nzima imefungwa na vifaru vya jeshi, huku mikonga yao ikiwa wameielekezea gari yao, ikiashiria kwamba wakifanya ubishi basi mizinga hiyo ya mabomo itakuwa ni alaki kwao.
“Jesus Christ”
Madam Mery alijikuta akitokwa na maneno hayo huku akibaki ameduwaa, na Sa Yoo akajikuta akisimamisha gari asijue nini cha kufanya.
                                                                                          
   SORRY MADAM (93)  (Destination of my enemies)

Ukimya ukatawala ndani ndani ya gari. Kila mtu hakujua ni kitu gani ambacho anaweza kukifanya kwa muda huo kwa maana wanajeshi wenye silaha walisha anza kujitokeza na wengine kadhaa wakaanza kulisogelea gari lao.
“Ngoja nishuke”
Madam Mery alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Unataka kwenda wapi, si unaona hao wanajeshi wana silaha watakukamata”
“Nalitambua hilo, kushuka kwangu kwenu itakuwa ni rahisi nyinyi kuokoka”
“Hembu acha upuuzi madam Mery, baki kwenye gario”
Phidaya alizungumza kwa kufoka, ila akawa amesha chelewa kwani Madam Mery alitoka kwenye gari huku mikono akiwa ameinyoosha juu.
                                                                                                    ***
“Najua munamtaka raisi Godwin, ila sisi hatunaye”
Sauti ya Madam Mery ilitoka kwenye vipaza sauti vilivyomo katika chumba hicho cha mawasiliano na kumfanya Manka kunyanyuka na kuzidi kupiga hatua kutazama Tv kubwa iliyopo katika chumba hicho.
“Wasifanye kitu chochote”
Manka alizungumza na kuwafanya watu wote waliomo ndani ya chumba hicho kumtazama mara mbili mbili.
“Kwa nini muheshimiwa?”
“Hawa hawana raisi, ila wawakamate kupitia wao tutajua ni wapi alipo raisi”
“Sawa mkuu”
Iikatolewa amri ya kuwakamata Madam Mery na wezake wote waliopo kwenye gari hilo.
                                                                                                    ***
   Jinsi wanajeshi wanavyo zidi kulisogelea gari lao ndivyo jinsi madam Shamsa, Sa Yoo na Phidawa walivyo zidi kuchanganyikiwa.
 
“Phidaya funga mlango”
Sa  Yoo alizungumza na kumfanya Phidaya kuufunga mlango wa upande alio kuwa amekaa madam Mery.
“Gari hii haiingia risasi, kwa hiyo hata wakitushambulia hatuwezi kuudhurika”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akianza kuirudisha gari hili nyuma. Wanajeshi wote walipokea amri ya kuto kushambulia gari hilo, na hilo ndilo lililo kuwa kosa kubwa sana kwao kwani Sa Yoo baada ya kuona hakuna kitendho chochote kinacho weza kuchukuliwa na wanajeshi hao. Kwa haraka akaigeuza gari na kurudi walipo toka kwa mwendo wa kasi sana.
“Tunarudi tena Dar?”
Phisaya aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka, Sa Yoo hakujibu chochote zaidi ya kuzidi kuendesha gari hilo kwa mwendo kasi sana. Akilini mwa Sa Yoo akawa anaifikiria njia ambayo aliiona imekatika kipindi wakiwa wanaelekea Chalinze. Kilomita mbili mbeleni, akakunja kushoto mwa barabara na kuingia katika njia ya vumbi iliyo jaa vibonde bonde vingi, ikiashiria kwamba haitumiki kwa magari.
 
“Helkopta hiyo bado inatufwatilia”
Shamsa alizungumza huku akiitazama kupitia kioo cha mbele.
“Haina shida hiyo helkopta ni ya kurusha matangazo, kwa hiyo hapo wanatuchukua video”
“Sasa ni lazima kuishusha kwa maana hatuwezi kujua tunapo elekea, kwa maana kwaa sasa ni lazima kuweza kujificha”
“Basi fanya kazi yako mama”
Sa Yoo alizungumza na kwa mara nyingine tena Shamsa akafungua kioo cha gari hilo, akachomoza mikono yake yote miwili na kuanza kuishambulia Helkopta hiyo kwa risasi mfululizo hadi ikafikia kipindi helkopta hiyo ikaanza kutoa moshi mwingi ulio ipelekea kuyumba sana na mwisho wa siku kuanguka na kulipuka ikiwa na rubani wake pamoja na fundi mitambo. 
 
Kwa umbali fulani kutoka eneo ilipo anguka helkopta Sa Yoo akalisimamisha gari na kushuka moja kwa moja akazunguka nyuma ya gari, akafungua buti na kuanza kukitazama kifaa ambacho kila gari ya riasi inapo elekea ni lazimwa waweze kuiona.
“Ina bidi kukitoa kwa maana bila ya kufanya hivyo, bado hatujawa salama”
Sa Yoo alizingumza huku Shamsa na Phidaya wakikitazama kifaa hicho, Shamsa akatoa bastola yake na kukitandika pasipo kujali chochote. Na kweli kifaa hicho kikasambaratika na kupoteza mawasiliano na Ikulu ya raisi.
 
“Sasa tunaelekea wapi?”
Hata mimi sifahamu, tujaribu jaribu kuelekea mbele labda tunaweza kupata makazi ya watu”
“Kweli?”
“Ndio”
Wakaingia kwenye gari, ikiwa ni majira ya jioni. Wakazidi kuchanja mbuga kuelekea wapipo pajua. Hadi inatimu saa moja usiku, wakawa wamfika kwenye moja ya kijiji cha Wamasai.
“Jamani tuombeni hata maji”
Phiday alizungumza, Shamsa akayachunguza mazingira ya eneo hilo wakiwa ndani ya gari hilo huku akijaribu kuwatazama watoto wa kimasai wanao lisogelea gari hilo na kulishangaa.
“Hii sehemu ni salama”
“Umejuaje Shamsa”
“Hawa ni watu jamii ya wafugaji, wanaitwa Wamasaidi. Ni watu wanao penda sana kutoa misaada kwa wale wenye shida ya uhitaji”
“Isije ikawa ni mtego tukashuka kwenye gari wakatushambulia?”
“Kila mmoja achukue bastola kwa ajili ya kujilinda yeye mwenyewe”
 
Shamsa akawapa kila mmtu bastola yake moja, Sa Yoo akatafuta sehemu yenye muembe mkubwa na kulisimamisha gari huku watoto wa kabila hilo la kimasai wakizidi kuwashangaa. Wa kwanza kufungua mlango na kushuka kwenye gari akawa ni Shamsa akawatazama watoto hao walio valia lubega kisha akaanza kuwapa mikono kwa ajili ya kuwasalimia.
Asili yao ya kiarabu, ikawafanya watoto hao kuzishangaa sana ngozi zao. Kwani kwa miaka yao yote tangu wazaliwe hawajawahi kuwaona watu weupe, na niwachache sana tena wakubwa wao, ndio walisha wahi kupewa siku misaada ya mambo mbalimbali na shirika moja la Wajerumani walio watembelea mwaka ya 2002.
 
 “Sogea sogea”
Sauti ya kijana mmoja mwenye cheo cha morani alizungumza huku akiwasogeza watoto hao wambao walimzunguka Shamsa.
“Habari yako muzungu”
Moran huyo alizungumza huku akimpa mkono Shamsa aliye utazama, kisha akaukutanisha na mkono wake huku akiachia tabasamu usoni mwake.
“Salama habari yako”
“Salama, nyinyi kuja tena tupa sisi musaada?”
“Ahaa tumekuja kuwatembelea”
“Basi njooni muone kina laiboni”
Kwa kuwakonjeza Shamsa akawaamuru Sa Yoo na Phidaya kushuka kwenye gari. Kila mmoja akashuka kwenye gari huku bastola yake akiwa ameichomeka kiunoni mwake na kuifunika na stati alilo livaa na si rahisi kwa wamasai hao kugundua kwamba wana silaha.
Watoto hao wa kimasai wakawazunguka huku kila mtoto akitaka kuwagusa Phidaya na Sa Yoo. Sa Yoo kwa kupenda watoto hakujali kushikwa na watoto hao muda wote akawa ameachia tabasamu huku na yeye akiwashika mkino watoto wawili. 
 
Wakapelekwa hadi kwenye moja ya kijumba kilicho ezekwa na na nyasi. Wakakaribishwa ndani na kukuta wazee wanne wakiwa wamekaa kwenye viti vidogo vinavyo itwa vigoda. Kijana huyo akatoa salamu kwa luga ya kimasai na kuwaanza kuwaeleza wazee hao kwamba wanawake hao wamekuja kutoa msaada kwenye kijiji chao ila alitumia lugha hiyo ya kimasai kuwaelezea wazee hao.
“Wanasema munatokea wapi?”
Kijana huyo alizungumza huku akiwatazama Phidaya na wezake. Sa Yoo akadakia kulijibu swali hilo.
“Tunatokea Japani”
Kijana huyo akazungumza kwa kimasai na kuwafanya wazee hao kutingisha vichwa vyao huku sura zao zikiashiria zina furaha kusikia hilo.
“Wanasema mumetuletea nini?”
Sa Yoo akatazamana na wezake huku akiwa hana kitu cha kujibu. Shamsa akameza fumba la mate kidogo na kulijibu swali hilo.
 
“Tumekuja kuwatembelea na kujua ni jinsi gani munavyo ishi na mazingira ya hapa na tukirudi kwetu Japan basi tutawaletea mahitaji yote ambayo mutakuwa munayahitaji”
Shamsa alizungumza kwa kujiamini, kijana huyo akawatasfiria wazee hao wakuu wa kijiji hicho kwa lugha ya kimasai.
“Wanawauliza munahitaji chakula?”
“Ndio”
Phidaya akawa wa kwanza kulijibu swali hilo huku akiwa ametabasama kwa maana ni njaa kali inausumbua utumbo wake.  Wakapelekwa kwenye moja ya nyumba, na kukuta wasichana wawili wa kimasai.  Wakawandalia chakula ambacho kila mmoja ndio mara yake ya kwanza kukila kwani ni madonge donge ya damu ya ng’ombe iliyo chemswa pamoja na maziwa yalio sindikwa.
“Mmmmm”
Phidaya aliguna, hata hamu ya kula chakula hicho, ikaanza kumakatika taratibu
                                                                                                               ***
    Kitendo cha helkopta ya kijeshi inayo husiana na maswala ya habari, kutunguliwa. Ikamuudhi kila mtu aliye kuwepo katika chumba cha mawasiliano hususani makamu wa raisi.
“Muheshimiwa kwa hili unatakiwa kutoa amri”
Mmoja wa kiongozi wa jeshi alizungumza huku akimtazama makamu wa riais aliye ikinja sura yake akionekana dhairi kwamba ameshikwa na hasira kali sana katika hilo.
Daktari wa ikulu akaingia katika chumba hicho(control room), moja kwa moja akamfwata Manka sehemu alipo kaa na kumnong’oneza sikioni. Kwa haraka Manka akaanza kutoka kwenye chumba hicho huku akifwatana na daktari hiyo.
Wakaelekea kwenye chumba alicho lazwa Erickson na kumkuta akiwa amefumbua macho yake akiwatazama wanavyo ingia kwenye chumba hicho. Moja kwa moja Manka akaelekea kwenye kitanda alicho lala Erickson.
 
“Unajisikiaje?”
Manka aliuliza kwa sauti ya unyonge.
“Safi tu”
“Dokta kidonda chake kinaweza kuwa vizuri hadi lini?”
“Ahaa kitachukua kama wiki mbili hadi tatu kukauka kabisa”
“Erickson usijali, upo katika mikono salama na wala hakuna mtu ambaye anaweza kukuteka tena”
Eddy kwa haraka haraka akafikiria kitu cha kuzungumza.  Akameza mate kidogo kisha akamtazama Manka usoni mwake.
“Agnes yupo wapi?”
Manka akabaki kimya huku akimtazama Erickson asijua ni nini atakijibu.
“Ahaaa.a..ahaa kwa sasa sio vizuri kumuulizia kikubwa ni kuangalia afya yako”
Mlango ukafunguliwa na akaingia mwanajeshi mmoja aliye piga saluti kwa Manka na kutoa maelekezo aliyo kuja nayo.
“Muheshimiwa makamu wa raisi amaruhusu jeshi kuwatafuta wale wasichana na kuhakikisha kwamba wanakamata ama kuuwa”
 
“Kwa nini ametoa ruhusa hiyo!?”
Manka aliuliza huku akisimama akionekana kushangazwa sana na ruhusa hiyo.
“Sijatambua muheshimiwa”
Manka akataka kutoka ila Erickson akamuuliza swali lililo mfanya kugeuka na kumtazama.
“Ni wasichana gani hao wanao taka kuuliwa?”
“Ni wale ambao walikuteka”
Eddy akaonekana kushushwa ila hakuhitaji kuzungumza chochote kuepuka kujulikana kwamba yupo pamoja na wasichana hao.
“Ngoja nikalizui hili swala”
Manka akaondoka katila chumba hicho huku akiongozana na mwanajeshi huyo na kumuacha Erickson na daktari. Eddy akatamani kuzungumza kitu ila akajizuia.
Manka akaingia kwenye chumba cha mawasiliano. Moja kwa moja akamfwata makamu wa raisi.
“Ni amri gani umetoa?”
 
“Nimeagiza vijana wakawakamate au kuwaua”
“Sihitaji kuona damu zinamwagika”
“Ila kumbuka mimi ndio mwenye mamlaka ya kuiongoza nchi, kama makamu wa raisi”
“Haijalishi na mimi ni waziri wa ulinzi, sihihitaji vijana wangu waende kufa”
Manka akachukua simu inayo tumika katika kuwasiliana na vikosi vya jeshi vilivyo anza kueleka katika njia ambayo wamepita kina Shamsa.
“Nimesema vikosi vyote virudishwe nyuma”
“Ila madam…..”
Ilisikika sauti ya kamanda wa vikosi hivyo.
“Sihitaji vya ila, nasema vikosi vyote v….”
Makamu wa raisi akampokonya mkonga wa simu Manka na kuuweka sikioni mwake.
“Endesha majeshi hakikisheni munaleta maiti za hao mawanawake”
Manakamu wa raisi alizungumza na kuurudisha kwa nguvu mkonga huo wa simu kwenye sehemu yake maalu. Manka akamtazama mzee huyo kwa macho makali na kuachia msunyo mkali ulio wafanya watu wote ndani ya chumba hicho kikubwa kumgeukia na kumtazama kwa mshangao.
                                                                                                            ***
   Vikosi vya majeshi vyenye silaha vipatavyo nane, vyenye watu zaidi ya kumi na mbili vikazidi kusonga mbele kama amri ya makamu wa raisi ilivyo tolewa. Wakiwa kwenye magri yao ya kijeshi kila mmoja kati yao akawa na uchu mkali wa kihitaji kuwakamata wasichana hao wanao sadikika kumteka raisi wa nchi mbaya  zaidi mwanamke waliye mkamata hajafungua kinywa chake kusema ni wapi raisi alipo japo wamempatia kipigo kikali ila hajazungumza neno la aina yoyote
 
“Jamani mimi nimeshindwa kula hiki chakula”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza, japo ana njaa ila akashindwa kabisa kula chakula hicho. Sa Yoo hakujali chakula hicho kimepikwaje, akazidi kukila na kuonekana kukifurahia sana.
“Kula hata kidogo”
Shamsa alizungumza, ila Phidaya akasimama, na kumnyooshea Shamsa mkono.
“Nini?”
“Naomba funguo ya gari nikalale kwenye gari mimi?”
Shamsa akamkabidhi Phidaya funguo ya gari, akatoka chumbani hapo. Binti mmoja wa kimasai akaliona jeraha la Shamsa kwenye bega lake. Taratibu akamsogelea na kulitazama vizuri na kumfanya Shamsa kuacha kula na kumtazama binti huyo aliye nyanyuka na kuchukua kibuyu kimoja kilicho fungwa kwa juu na mfuko mweusi.
 
“Hii ni dawa ya vidonda”
Binti huyo alizungumza Kiswahili fasaha hadi Shamsa akashangaa kwa maana walidhani kwamba mabinti hao walio waandalia chakula hawajui lugha ya Kiswahili zaidi ya kimasai. Binti huyo akamimina unga unga huo kwenye kiganja chake cha mkononi na kuumpaka Shamsa kwenye kidonda chake na kumfanya asikie maumivu makali yaliyo dumu kwa dakika tano mfululizo na kupotea.
“Unajisikiaje?”
“Ahaaa kidogo afadhali”
Shamsa alizungumza huku jasho likimwagika.
“Ndani ya siku mbili kitakauka na kupona”
Phidaya alipo toka ndani humo hakwenda moja kwa moja kwenye gari, akaanza kuzunguka zunguka kutazama mazingira ya kijiji hicho kilichopo katikati ya eneo lenye majani mengi. Akapanda kwenye moja ya kichuguu kilihopo katika eneo hilo. Kwa mbali akaona taa za mianga ya magari zikikaribia kufika kwenye kijiji hicho.
 
‘Mungu wangu’
Phidaya akashuka kwa haraka kwenye kichuguu hicho na kukimbilia hadi kwenye nyumba alipo waacha Shamsa na Sa Yoo.
“Kuna nini mbona mbio mbio?”
Phidaya akawatazama wasichana hao kisha akachuchumaa na kumnong’oneza Shamsa
“Nahisi kuna askari wanakuja maeneo haya kututafuta”
Shamsa akawa kama mtu aliye lipiliwa na jambo fulani kwa haraka akanyanyuka na kutoka katika chumba hicho, ikawabidi wezake wote kumfwata hata binti huyo wa kimasai anaye fahamu Kiswahili akawafwata kwa nyuma.
 
“Wapo wapi?”
Shamsa aliuliza, Phidaya akakimbilia kwenye kichuguu hicho wote wakapanda wakaziona gari hizo zinavyo zidi kuja kwa kasi katika kijiji hicho. Binti huyo wa kimasai akaanza kupiga vigelegele vya kuashiria kuna jambo limejitokeza. Vijana wa kimasaid wakiwa na mikuki pamoja na ngao zao wakatoka kwenye boma zao na kukimbilia kwenye kichuguu hicho.
“Tunavamiwa”
Binti huyo alizungumza kwa lugha ya kimasai. Kiongozi wa vijana hao wa kimasai akawaamuru wezake wote kutawanyika, na kujificha na endapo watu hao wanao kuja watakuwa na jambo lolote baya basi wawavamie.
 
“Tnafanyaje sasa?”
Phidaya aliuliza huku mwili mzima ukimtetemeka.
“Nifwateni mimi”
Binti huyo wa kimasai alizungumza na kushuka kwenye kichuguu hicho. Wote wakamfwata kwa nyuma akwapeleka kwenye moja ya handaki wanalo jificha pale kunapo tokea uvamizi.  Wakakuta wamama na watoto pamoja na wazee wakiwa wamasha ingia kwenye handaki hilo wamejificha baada ya kupigwa kwa vigelegele hivyo.
“Munaweza kujificha humu na maadui wasijue ni wapi nyinyi mulipo”
Hata kabla hawajazungumza chochote, milio ya risasi ikaanza kusikika ikirindima nje ikiashiria kwamba watu hao walio kuja kwenye kijiji hicho si wema kabisa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts