Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 96 & 97 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 96 & 97 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Sunday, February 18, 2018 | 10:43:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Wasiwasi wake alio kuwa nao tayari Shamsa alisha anza kuustukia. Mzee huyo akazidi kukanyaga mafuta hadi akafanikiwa kufika Kibaha. Akkunjaa upande wa pili wa barabara na kuanza kuelekea kilipo kituo cha Polisi
“Huko ndio Dar?”
“Ahaa kuna jamaa ninakwenda kumuona hapo mbele kidogo”
Shamsa akachomoa bastola na kuielekezea kwenye tumbo la mzee huyo, huku akiwa amekazia macho na kama atafanya uzembe hali ya hewa itaharabika.
“Ukilete ujinga nalipasua hili tumbo lako lililo jaa maji”
Shamsa alizungumza huku jasho likimwagika na kumfanya mzee wa watu kusimamisha gari lake, huku mwili mzima ukimtemeka, na haja ndogo ikianza kuichafua suruali yake ya kitambaa aliyo ivaa.

ENDELEA
“Rudisha nyuma gari”
Mzee huyo taratibu akajikuta akirudisha gari lake nyuma kwa amri ya Shamsa aliyo elezwa. Wakaingia tena barabarani na kuendelea na safari yao huku Shamsa akiwa ameielekezea bastola yake kwenye tumbo la mzee huyo.
                                                                                                              ***
    Kikao cha wakuu wa kundi la D. F.E kikamalizika na kutoa maamuzi ya kutuma vijana wenye mafunzo ya kijeshi katika kikosi hicho kuja kumumtafuta mkuu wao huyo anaye sadikika kutekwa.
Eddy macho yakamtoka huku akitazama viongozi hao wakipeana mikono, kupitia laptop hiyo iliyopo kwenye meza ya raisi Godwin.
“Inakuwaje hapa?”
Eddy aliwaza huku akikosa jibu la kuzungumza kabisa. Akatoka katika upande huo wa video na kuanza kufungua faili moja baada ya jingine.  Akakuta faili moja limeandikwa ‘TOP SECREATY’. Akajaribu kulifungua akakutana na namba za siri.
 
‘Anaweza kutumia namba zipi za siri hiyu mzee?’
Eddy alijiuliza huku akiendelea kuingiza ingiza namba za siri baadhi ambazo alizikumbuka kichwani mwake na zilikuwa zinatumiwa na baba yake huyo. Ila namba zote alizo ziingiza hazikuweza kufanya kazi. Akiwa anawaza ni nini cha kufanya. Pembeni kabisa ya kioo hicho, alama nyekundu ikaanza kuonekana, ikiwaka na kuzima. Akasogeza kimshale cha laptop hiyo na kufungua alama hiyo. Kwa haraka ikaja ramani kubwa iliyo jaa kwenye kioo chake.
“Ni nini hiki?”
Eddy alijiuliza huku akikodolea macho ramani hiyo, ambapo alama hiyo nyekundu iliendelea kujitokeza kwenye lapotop hiyo. Eddy akajaribu kuumiza kichwa chake ili kuweza kufahamu ni nini hicho kinacho waka na kuzima ila hakupata jibu kabisa
                                                                                                              ***
   Rahab akamtazama Raisi Godwin jinsi anavyo hema kwa shida baada ya kumwagia maji baridi na kuzinduka baada ya kuzimia kwa maumivu makali ya kupigwa shoti ya umeme katika sehemu zake za siri.
“Nieleze ni kwani nini uliamua kumuua mume wangu?”
“Sifahamu mimi, kusema kweli sifahamu”
Mzee Godwin alilalama huku machozi yakimwagika. Ubabe, ujanja wote ulizima kama mshumaa unavyo zima.
“Nielekeze D.F.E ni nini na ulikuwa na lengo gani la kuianzisha?”
Swali hilo likamstua sana mzee Godwin na kujikuta akimtole mimacho Rahab ambaye amesimama mbele yake. Kwa maana katika maisha yake anatambua kwamba kikundi hicho ni cha siri sana na si kawaida kwa mtu wa kawaidia kuweza kukifahamu, hata viongozi wengi wa serikali yake hawakijui kikundi chake.
“Nieleze usinitumbulie mimacho”
“D…….D….F.E ni nii kikundi chaa umoja”
“Ni kikundi cha umoja? Hembu zungumza kitua ambacho kinaelekeweka”
 
Rahab alizungumza huku akiinyanyua suruali ya Mzee Godwin. Akaanza kuingiza kuingiza kiganja cha mkono wa kulia kwenye mfuko mmoja baada ya mwengine. Mfuko wa kwanza hakukuta kitu, ila katika mfuko wa kwanza akakutana na simu, aina ya Iphone 6.
Akaiwasha simu hiyo, kitendo cha kuiwasha simu hiyo kikamfanya mzee Godwin kutabasamu kidogo kwa maana simu yake hiyo imeungwanishwa na mtandao maalumu ambao endapo inapo kuwa hewani basi, wanachama wake kwenye kikundi hicho wote wanafahamu ni wapi alipo mkuu  wao.
   Rahabu akaingiza namba za Agnes ambaye aliweza kumpatia. Akaona si vyema kuzungumza akiwa katika chumba hicho akatoka kabisa ndani ya handaki huku simu akiwa ameiweka sikioni, akisikilizia mziki ambao ni muito wa namba hiyo ya Agnes.
                                                                                                         ***
“Shiii jamani, simu yangu inaita. Raisi ananipigia”
Agnes alizungumza na kuwafanya wezake wote kukaa kimya na kumsikiliza. Agnes akakohoa kidogo kisha akaipokea simu hiyo iliyo anza kuita sekunde kadhaa nyuma zilizo pita.
“Mbona unachelewa kupokea simu wewe”
“Rahab…..!!?”
Agnes alizungumza huku akikaa na kuwafanya Fetty, Halima na Anna kushangaa.
“Ndio, nisikilize, nimemteka huyu fala nipo naye kwenye yale makazi yetu chini ya ardhi”
“Kweli…..?”
“Ndio, nimekuambia wewe kwa maana nahitaji msaada wako”
 
“Sikia, sikia Rahab. Sasa hivi unakuja huko. Nipo na timu nzima na tulikuwa na mpango wa kuungana nawe kuhakikisha huyo mjinga tunamkomesha na mwanaye”
“Poa kama vipi nyinyi njooni, ila kuweni makini”
“Ahaa makini wapi, siis ni viongozi wa hii nchi bwana au umelisahau hilo”
“Poa fanyeni chap”
Simu ikakatwa, Agnes akawatazama wezake ambao wana shauku ya kutaka kufahamu ni wapi alipo rafiki yao Rahab.
“Yupo kwenye lile handaki letu”
“Kweli?”
“Ndio”
“Kazi imeanza”
Wote kwa pamoja wakatoka ndani, Anna na Fetty wakaingia kwenye gari moja huku Halina na Agnes wakiingia kwenye gari jengine. Safari ikaanza kuelekea nje ya jiji la Dar es Salaam kwenye msitu ambapo ndipo kuna handaki hilo. Kwa jinsi wanavyo ziendesha gari zao kwa mwendo kasi, kila watu walio weza kuziona wliweza kutambua kwamba madereva hao wapo kwenye mashindao
                                                                                                            ***
   Simu ya Manka ikaita, taratibu akamuachia madam Mery na kuitoa mfukoni mwa koti la suti alilo vaa. Akakuta ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano ikulu, akamipokea na kuiweka sikioni simu hiyo.
 
“Ndio”
‘Muheshimiwa, tumeweza kupata singal za simu ya muheshimiwa raisi na inavyo onenyeasha imepigwa na mtekaji’
“Wapi hiyo signal inaonyesha?”
“Ni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam”
“Ok, nitumie ramani ya sehemu simu hiyo ilipo tokea sasa hivi kisha andaa kikosi maalumu kwa ajili ya kuelekea huko alipo shikiliwa mzee”
“Sawa muheshimiwa”
Manka akakata simu huku akiwa na tabasamu usoni mwake.
“Kuna nini kilicho tokea mwanangu?”
“Tumepata sehemu alipo baba, na sasa hivi naamini vikosi vinakwenda kulishuhulikia hilo”
Habari hiyo ikamstua madam Mery kwa maana anatambua kwamba maisha ya Rahab aliye weza kuondoka na raisi Godwin basi yapo hatarini. Taratibu madam Mery akamshika mkono Manka taratibu.
“Manka….”
Madam Mery aliita huku machozi yakimwagika usoni mwake. Manka akabaki akimtazama mama yake mdogo huyo jinsi anavyo mwagikwa na machozi.
 
“Nakuomba usiondoke na kuniacha peke yangu humu”
“Sawa mama, ninatoa amri sasa hivi kwamba uachiwe na nitahitaji twende huko alipo shikiliwa mzee”
Madam Mery hakuwa na jambo la kuzungumza, Manka akamshika mkono na wakatoka kwa pamoja ndani ya chumba hicho.
“Mfungulieni sasa hivi?”
“Muheshimiwa?”
Mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa alishangaa kusikia kauli hiyo kutoka kwa bosi wake.
“Nina hitaji kuondoka naye sasa hivi kwa maana amenipa ushirikiano wa wapi alipo raisi Godiwn, sasa jinsi munavyo chelewa kumfungulia hapa ndivyo hali ya baba yangu itakavyo kuwa mbaya”
Manka alizungumza kwa ukali, hapakuwa na jinsi nyingine zaidi ya kiongozi huyo kumuamrisha kijana wake kuweza kumfungulia pingu madam Mery.
“Nahitaji vijana nane niongozane nao sasa hivi”
“Sawa mku”
 
Kiongozi huyo kwa haraka akatoa amri kwa vijana wake kuungana na mkuu wao kuelekea sehemu ambapo ndipo alipo tekwa raisi Godwin. Kwa haraka wakatoka nje na kiingia kwenye magari, huku Manka akipanda gari moja na madam Mery ambaye muda wote amekaa kimya akifikiria ni kitu gani ambacho kitakwenda kutokea huko. Manka akaitoa simu yake mfukoni na kukuta ujumbe wa email alio tumiwa, akaufungua na moja kwa moja ramani ya sehemu alipo mzee Godwin ikatoke huku alama nyekundu ikionekana kwenye sehemu hiyo. Msafara ukaondoka huku gari zote zikiwasha ving’ora kuashiria, gari, bajaji pikipiki, baiskeli na watembea kwa miguu kupisha barbara kwa maana kiongozi wao anapita.
                                                                                                        ***
“Muheshimiwa kuna signal ya simu ya mkuu hapa”
Mlinzi alimuonyesha John, kupitia simu hiyo ya mkononi wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano. John akaitazama vizuri na kugundua kwamba ni sehemu ambayo ndipo alipo raisi Godwin.
“Warudishe ndani viongozi wote walio toka mkitano unaendelea”
“Sawa mkuu”
Mlinzi huyo kupitia kipaza sauti akawaomba viongozi wote walio toka nje ya ukumbi kurudi tena ukumbina kwa maana kuna swala la dharura limejitokeza. Viongozi hao ambao wengi wao walikuwa ndani ya ukumbi huo wakisalimiana na kuzungumza mawili matatu, kila mmoja akarudi kwenye kiti chake na kikao kilicho kuwa kimesha malizika kikaendelea tena.
 
John akawaeleza viongozi hao wote kila mwenye simu kuweza kuwsha simu yake ua laptop yake kwa maana kuna signal inayo onyesha ni sehemu gani ambapo kiongozi wao mzee Godwin yupo.
“Ina bidi kuweza kumpata kabla hajaingia mikononi mwa serikali”
John alizungumza na kuwafanya baadhi ya viongozi kutazama. Kiongozi mmoja akawasha maiki iliyopo kwenye meza yake na kuuliza swali.
“Na je akipatikana na majeshi ya serikali?”
“Inabidi kutumia hata nguvu kuweza kumtoa mikoni mwao kwa maana ndani ya serikali yake kuna wasaliti na endapo watafahamu kwamba kiongozi amepatikana basi atauwa”
“Kiongozi wa ulinzi wataarifu vijana wako waliopo hapa tanzania kuweza kufanya kazi ya kumchukua muheshimiwa”
“Sawa makamu mwenyekiti”
                                                                                                       ***
Eddy akaifunga laptop hiyo na kunyanyuka kwenye kiti hicho. Akatoka nayo huku akiwa ameificha kwenye jishati kubwa la wagonjwa alilo livaa. Akiwa kwenye kordo hiyo akaona walinzi hapo ikulu wakikimbia kimbia huku kukionekana kama kuna jambo la hatari limetokea. Kwa haraka akarudi kwenye chumba cha matibabu na kumkuta daktari akiwa anaitazama simu yake.
“Dokta kuna kitu gani ambacho kimetokea?”
“Muheshimiwa amepatikana na hii ndio signal ya sehemu inayo muonyesha alipo kiongozi”
 
Daktai huyo alizungumza huku akiwa amekenua meno yake akionekana kuwa na furaha sana. Eddy akaitaza alama hiyo nyekundu hapo ndipo akapata jibu kwamba alama hiyo aliyo kuwa ameiona kwenye laptop ya raisi Godwin kumbe ndio sehemu alipo mzee Godwin.
Akili ya Eddy ikafanya kazi haraka haraka. Daktari hiyo aliye mpa mgongo, akachusogelea karibu na kumpiga ngumi nzito ya kisogo na kumfanya daktai huyo kuanguka chini na kupoteza fahamu. Eddy akaichomoa laptop hiyo na kuiweka kitandani, akaanza kumvua daktari mavazi yake pamoja na koti lake la udaktari. Alipo hakikisha amemaliza, akavua nguo zake japo ana maumivu makali ila hakuona haja ya kuendelea kukaa eneo hilo na kumuoan raisi Godwin anarudi tena kwenye mamlaka.
 
Akazivaa nguo za daktari huyo pamoja na koti hilo kubwa. Akachukua kichupa cha dawa ya kupunguza maumivu pamoja na bomba la sindano ambalo halijatumika. Akaviweka kwenye  mfuko mkubwa wa kati hilo. Alipo maliza, akachukua kitambulisho cha daktari huyo pamoja na miwani yake kubwa kiasi. Akaichukua lapotop hiyo na kuifunika na koti hilo.
Akafungua mlango na kuchungulia nje kwenye kordo, hapakuwa na mtu wa aina yoyote. Akatoka na kuanza kutembea kwa kujiamini huku mara kadhaa akionana na watu anainamisha sura yake nje. Akafanikiwa kutoka nje, akakuta walinzi wengi wa ikulu wakiwa wanaingia kwenye magari yao kwa haraka.
 
Akiwa ameuingiza mkono wa kulia kwenye mfuko wa suruali, kwa bahati nzuri akakuta mfuko huo una fungua ya gari la daktari huyo na uzuri wa funguo hiyo una batani ambayo ukiminya gari husika linatoa mlio, na si ngumu kuanza kulitafuta.
Akafanya hivyo na kuona gari aina ya Vitz ikiwa lipo kwenye maegesho yaliyopo hapo ikulu. Akalifwata na kuingia akaliwasha kwa bahati nzuri akakuta mafuta yakiwa full tanki, akaiweka laptop katika siti ya pembeni huku akiifunua na kuona signal hiuo ni wapi inapo tokea. Taratibu akaanza kuelekea kwenye geti la kutokea huku akiwa nyuma ya gari nne za walinzi wa ikulu zinazo toka eneo la hapo.
 
Kutokana na hali hiyo ya hatari, walinzi wa getini hawakuweza kulikagua gari lake, akafanikiwa kutoka na kuanza kuzifwata gari hizo zinazo kwenda kwa kasi. Kutokana na maumivu makali, Eddy akalisimamisha gari lake pembeni, akatoa kichupa cha dawa ya kutuliza maumivu. Kisha akalifunga sindano kwenye bomba hilo akavuta dawa karibia kichupa kujaa, akakunja mkono wa koti hilo la daktari. Akakunja mgumi kwenye mkono huo wa kushhoto, alipo hakikisha kwamba mishipa imejitokeza vizuri, akajidunga sindano hiyo na kuisukuma dawa yote aliyo ivuta kwenye bomba la sindano, kisha akalichoma.
“Ahaaaa”
Eddy aligugumia kwa maumivu huku akiweka sindano na kichupa hicho pembeni, maumivu yaliyo kuwa makali sana yakaanza kupungua kwa haraka na kumpa nafasi Eddy ya kuwasha gari hilo na kuondoka kwa kasi huku akijitahidi kufwata ramani inayo onekana kwenye laptop hiyo.
                                                                                                           ***
“Mbona umesimamisha gari?”
Shamsa alimuliza mzee huyo ambaye njia nzima aliendesha gari kwa woga kutona na kushikiwa bastola na msichana huyo ambaye alisha ona bahari zake ni za kutisha na kitu kilicho muumiza kichwa mzee huyo ni kwamba, kama binti huyo ameweza kumteka raisi wa nchi ambaye alikuwa ni mbabe, itakuweje kwake yeye na tumbo lake hilo lililo ahidiwa kutumbuliwa tumbuliwa atakapo leta ujinga.
 
“Ku….una msafara wa kiongozi wa juu gari zote zinakaa pembeni ya barabara”
Ni kweli kwa maana gari zote zilizopo bararani ziliweza kusogezwa pembeni na gari za polisi walio anza kupewa taarifa kwamba aliye kaimu nafasi ya raisi kuna sehemu anaelekea kwa wakati huo.
‘Kuna nini?’
Shamsa alijiuliza, huku akitazama gari za polisi nyingine mbili zikipita kwa kasi ya ajabu wenyewe wanaiziita safisha njia. Zikaanza kupita gari tatu nyeusi zikiwa katika mwendo wa kasi, ila kwa bahati nzuri katika gari ya katikati, katika siti ya mwisho nyuma ya dereva. Shamsa aliweza kumuona madam Mery.
“Madam Mery?”
Shamsa akastuka sana, huku akitazama gari nyingine tatu kutoka kitengo maalumu cha usalama wa taifa nazo zikikatiza.
 
“Shuka kwenye gari?”
“Ahaa jamani binti gari yangu nimenunua juzi tu pesa ya mkopo wa benki leo unataka kunipokonya”
Mzee huyo alilalamika huku machozi yakimlenga lenga. Shamsa akaikoki bastola hiyo kwa haraka. Mzee wa watu kuona hivyo akashuka kwenye gari na kumshuhudia binti huyo akihamia kwenye siti aliyo kuwa amekalia, bila hata ya kujali kwamba gari hilo ni jipya au laa. Shamsa akaligeuza kwa haraka, kabla magari mengine hayajaruhusiwa na kuanza kuzifukuzia gari hizo zinazo kwenda kwa kasi na kumuacha mzee wa watu akiangua kilio mbele za watu walio baki wakimshangaa.
                                                                                                             ***
     Kikosi maalumu cha D.F.E, chenye vijana wanne ila wenye ujuzi mkubwa wa mapambano, wakaingia kwenye gari lao huku wakiwa na silaha za kutoasha pamoja na mitambo ya kuonyesha ni wapi alipo mzee Godwin. Vijana hao ambao kwenye maisha yao jambo kuua ni sawa na mtu kwenda haja ndogo au kubwa kwa siku. Na amri ambayo wamepewa na mkuu wao ambaye ni John, ni kuhakikisha kwamba wanarudi na Mzee Godwin. Iwe isiwe ni lazima wafanya hivyo hata kwa kutoa roho za walinzi wa raisi huyo ambaye inavyo onekana ndio wanaweza kuwahi kumpata kabla ya wao hii ni kutokana taarifa kuwafikia.
 
Gari yao aina ya Range Rover Sport, kwa jinsi dereva wao huyo anayo liendesha kwa kasi unaweza kuhisi kwamba ana upungufu wa akili na wala haogopi kitu kinacho itwa kifo.
“Kunja kushoto”
Mmoja aliye kaa na laptop inayo onyesha alip raisi alitoa maelekezo kwa wezake. Spidi aliyo kunjia kona hiyo, hadi watu walio kuwa wamekaa pembezoni mwa barabara hiyo walijikuta wakijirushia mitaroni kuyaokoa maisha yao kwa maana gari hiyo ilkaribia kuwafwata walipo.
Hadi wanafanikiwa kufika katika msitu huo ambapo signal hiyo inawaonyesha ni wapi alipo mzee Godwin, wakakuta kuna baadhi ya matairi ya magari ambayo tayari inaonyesha yamesha ingia kwenye kijinjia chembaba kinacho elekea ndani yam situ huo.
 
“Tunafanyaje?”
“Fwata kanjia hako”
“Inavyo elekea kuna askari wamesha ingia humu?”
“Wewe twende, askari kitu gani, kana ni noma iwe noma”
Dereva hakuwa na kipingamizi, akaanza kuifwata barabara hiyo kwa kasi japo ni ndogo na yenye nyasi nyingi ila akazidi kuifwata, wakiwa hata hawajaumalizia msitu huyo, tetemeko kubwa la ardhi likatokea huku likiambatana na mlipuko mkubwa wa bomu ulilolifanya gari lao kuyumba na kugonga kwenye mti uliopo mbeni na likatulia hapo hapo. Wakiwa katika hali ya kushangaa wakanaza kuona jinsi ardhi inavyo titia na kuifanya miti yote inayo pitiwa na tetemeko hilo kutitia chini.
                                                                                                
SORRY MADAM (97) (Destination of my enemies)

   Woga ukamjaa kila mmoja wao, hapakuwa na mtu aliye kuwa jarisi aliye weza kukabiliana na hali hiyo ya kutisha. Wakatamani kushuka kwenye agri lao ila wakashindwa, kila muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi ardhi ya eneo hilo ilivyo zidi kugawanyika na kupasuka.
Gari za askari wa ikulu, pamoja na makachero wa usalama wa taifa nazo zilisombwa na tetemeko hilo, nyingine ziliagukiwa na miti mikubwa na kupondeka pondeka. Ni gari la Manka ambayo ilisimama sehemu ya mbali kidogo kutoka lilipo handaki ndio lilisalimika.
                                                                                         **(LISAA MOJA NYUMA)
  Rahab baada ya kumalizi kuzungumza na Agnes, akatambua fika kwamba namba simu hiyo lazima itakuwa imeunganishwa na satelaiti na kitendo cha kuiwasha tu ni lazima iwe imeonekana katika chumba cha mawasiliano ikulu, ambao wanahusika na kumlinda raisi kupitia mtandao.
Rahab akalisogelea gari la jeshi walilo kuja nalo, akafungua turubai lililopo nyuma ya gari hilo. Akatoa madungu mawili ya mafuta ya petrol, akayabeba na kuingia nayo kwenye handaki.
 
“Unafanya nini?”
Raisi Godwin aliuliza huku akiwa amemtumbulia macho Rahab baada ya kumuona akifunua dungu moja la mafuta na kuanza kumwaga eneo zima la handaki. Alipo maliza Rahab akarudi kwneye chumba cha raisi Godwin na kumfungua kamba kwa haraka haraka. Akamvalisha nguo zake kwa haraka, akamfunga kamba mikononi na miguuni.
   Rahab akafungua moja ya chumba ambacho tangu aje hapo hakukiingia kwenye chumba hicho kwa maana ni chumba ambacho kinakaa silaha pamoja na mabomu ambayo waliyaweka tangu kipindi wanaianza kuishi katika chumba hicho huku mafunzo yao ya kijeshi wakifundishwa na dokta William.
 
Bunduki pamoja na mabaomu hayo ya kutega yaliyo jaa vumbi Rahab akaanza kuyatoa moja baada ya jengine na kuanza kuyapachika kwenye kuta za handaki hilo. Kila alilo lipachika basi aliweza kulitega kwa dakika tano tu. Akachukua bastola sita zenye risasi za kutosha akazichomeka sehemu mbalimbali za mwili wake kuanzia kwenye viatu, hadi kwenye kiuno.
   Akiwa katika harakati za kutega bomu moja kubwa, simu ya raisi Godwin ikita, akaitoa mfukoni mwake na kukuta ni Agnes ndio amepiga.
“Tumesha fika”
“Poa basi ingieni kwenye hadanki haraka”
“Poa”
Raisi Gowdin macho yakamtoka baada ya kuwaona viongozi wake alio waamini na ndio waliokuwa ni walinzi wake kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu, wakiingia humo ndani ya handaki na kukumbatia na Rahab kwa haraka haraka.
“Kumbe nyinyi ni wasaliti?”
Agnes akampiga teka la mbavu raisi Godwin na kumtemea mate ya uso.
“Nyamaza nguruwe mkubwa wewe”
“Jamani hatuna muda wa kupoteza mabomu yamebaki dakika tatu tu, ni lazima kuondoka eneo hili haraka iwezekanavyo”
 
“Sawa”
“Muna silaha sasa?”
“Hatuna”
“Ok chukueni kila mmoja bastola yake humo ndani”
Fetty na wezake kwa haraka haraka wakachukua kila mmoja bastola ambazo aliona zitamtosha mbele ya safari kwa maana hakuna hata mmoja ambaye anaweza kutambua nmi kitu gani kinaweza kutokea mbele zaidi ya Rahab peke yake.
Anna na Agnes wakambeba raisi Godwin hadi nje. Halima, Fetty na Rahab wakatoka kwenye hadaki mara baada ya kulitegesha bomu kubwa lenye kilo zaidi ya themanini na endapo litalipuka basi litateketeza eneo kunwa la msitu huo na kuligeuza kichwa chini miguu juu.
“Hii simu ngoja niche hapa juu”
Rahab alizungumza huku simu ya raisi Godwin akiiweka juu ya mfuniko mzito wa chuma wa kuingilia kwenye handaki hilo.
“Tutumie hizi gari tulizo kuja nazo,ninaamini kuna watu wanakuja huku”
 
Fetty alitoa wazo hilo, watatu ambao ni Halima, Anna na Rahab wakadandia gari moja huku Fetty na Agnes wakipanda gari hilo ambalo ndilo walipo muingiza raisi Godwin na kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana.
   Hawakupita njia walio ingilia wakiamini ni lazima kutakuwa na idadi kubwa ya askari wanao weza kufika katika eneo hilo muda wowote. Agnes na Halima walijitahidi kadri ya uwezo wao kuendesha magari yao wakikatiza katikati ya msitu wakihakikisha ndani ya dakika mbili wawe tayari wamesha toka kwenye msitu huo.
    Gari za kikosi maalumu kutoka usalma wa taifa wakiongozana na gari kutoka ikulu ambazo zimembeba Manka na madam Mery zikafika kwenye msitu, ila dereva wa gari la Manka akasimama na kuacha gari nyingine kuingia msituni.
 
“Kwa nini umesimamaisha?”
“Muheshimiwa acha kwanza watangulie askari wakaandae mazingira ya wewe kuweza kwenda”
“Nataka nishuke nikamuone huyo mpuuzi aliye weza kumteka babaa yangu”
“Muheshimiwa siwezi kufanya hilo kazi yangu ni kukulinda wewe, siwezi kukuacha uingie kwenye matatizo”
Dereva huyo aliye valia suti nyeusi na shati jeusi alizungumza kwa kujiamini, Manka akataka kushuka ila akawahi kuifunga milango yote mine.
“Fungua mlango wewe”
“Muheshimiwa siwezi kufanya hivyo, kwa maana huko tunapo kwenda hatuwezi kujua ni kitu gani kitatokea, kama ni matukio basi nahitaji uweze kuyaona ukiwa humu humu ndani ya gari”
“Sasa umelisimamisha hapa barabarani mimi nitaonaje?”
“Sawa tutaingia ndani kidogo”
 
Dereva huyo taratibu akaanza kuifwata njia zilipo pita gari nyingine, ila mbele akakuta njia panda, akakunja kulia kwake na kuelekea huko na hiyo sio njia ambayo wamepita wezao.
“Mbona hatuwaoni wengine?”
Manka alizungumza huku akitazama tazama mbele. Dereva hakuzungumza chochote akazidi kuendesha gari lake, huku machale mengi yakiwa yamemcheza akilini mwake.
Makachero pamoja na walinzi waona mlinda Manka wakafika eneo ambalo alama ya simu inaonyesha ipo. Wakakuta gari la jeshi likiwa eneo hilo lila mmoja akaamini kwamba ni lazima raisi Godwin atakuwepo katika eneo hilo. Wakashuka kwa haraka kwenye magari yao wakiwa na bunduki mikononi mwao. Wakaanza kujigawa kila mmoja kukaa katika nafasi yake. Bomu zilizo tegwa ndani ya handaki hilo, sekunde zake hazikusisimama zaidi ya kuzidi kurudi nyuma, zikabaki sekunde tano kabla ya kufika kwenye sekunde sifuri. Makachero hao na walinzi hao wa Manka pasipo kufahamu wakaanza kuusogelea mfuniko wa kuingilia kwenye handaki. Kila mmoja akaiona simu ya raisi Godwin.
 
“Simu yake hii hapa”
Kitendo cha mlinzi huyo kuinama na kuiokota simu hiyo, kila mmoja alihisi ni ndoto ya mchana ila ndio ukweli ulipo. Mlipuko mkubwa na mpasuko mkubwa wa ardhi ukatokea eneo hilo lote. Magari, watu miti vyote vikajikuta vikipata pigo moja lililo pelekea maisha ya makachero pamoja na walinzi kupoteza maisha hapo hapo huku wengine wakifukiwa na vifusi vya mchanga. Tetemeko hilo la ardhi pamoja na mlipuko huo mkubwa ukapelekea hadi gari ya Manka kuzima.
“Ni nini hicho?”
Manka aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka, huku woga ukimjaa. Si yeye mwenyewe aliye weza kupata woga huo bali hadi Madam Mery na dereva wake waliogopa sana kwa maana sio kitu ambacho walikitarajia kukutana nacho.
“Ni nini hicho?”
“Madam hata mimi mwenyewe sifahamu”
“Hilo ni bomu”
Madam Mery alizungumza huku akitazama moshi mwingi unao elea hewani huku miti ikiendelea kuanguka kwa mfufulizo.
“Tuondoke sasa unataka tufie hapa”
Dereva akajitahidi kuwasha gari ila halikuwaka, kila alivyo  jaribu kusasha gari halikuwaka wala milango kufunguka, na mpasuko wa ardhi ukazidi kuongezeka huku ukilifwata gari lao.
                                                                                                                 ***
    Shamsa aliweza kuzishuhudia gari hizo ambazo anaamini zinatoka ikulu zikikuacha kwa umbali mkubwa, na kupotea kabisa mbele ya uso wake hii ni kutokana na kuishiwa na mafuta.
“Shiti”
Shamsa alizungumza huku gari hilo likipunguza mwendo taratibu hadi likasimama kabisa. Sehemu aliyo kuwepo hakuna mji wala nyumba ambapo anaweza kuomba ata msaada wa kuelekezwa ni wapi zilipo sheli. Akashuka kwenye gari na kufungua buti ya gari hilo kama anaweza kukutana na kidungu ambacho kinaweza kuwa na mafuta. Hapakuwa na kidungu zaidi ya engo tatu zenye rangi ya kijani. Akazichukua na kutembea hatua kadhaa nyuma na kuisimamisha gari, ili kuwapa ishara madeva wengine wanao kuja katika eneo hilo kufahamu kwamba gari lake linamatatizo hii ni kutokana limesimama katikati ya barabara.
Akaelekea mbele ya gari lake, akatembea hatua chache na kuuiweka engo tatu hiyo kisha akarudi lilipo gari lake na kufungua boneti ya mbele ya gari hilo na kusimama pembeni akitazana tazana kana abaweza uoata nsaada wowote.
 
    Akiawa eneo hilo akaona gari nyingine za askari zinazo washa ving’ora huku zikienda kwa kasi zikipita karibu yake na kuelekea kule ambapo zimeeleea gari za Manka.
“Kuna nini huko?”
Shamsa alizungumza huku akizitazama gari hizo zinazo kwenda kwa kasi zikipotelea machoni mwake. Akageuka nyuma na kuona gari aina ya Vitz ikija katika eneo hilo.
“Namsimamisha huyu huyu”
Shamsa akaka katikati ya barabara na kuanza kuisimamisha gari hiyo inayo kuja kwa kasi na kumfanya dereva wake kuanza kufunga breki kali, hadi anamfikia Shama alipo simama gari hilo lilisimama.
“Kaka naomba msaada”
Manka alizungumza huku akikimbilia upande wa dereva. Baada ya kioo cha gari hilo kushushwa wote wakajikuta wakishangaana kwa maana dereva wa gari hilo ni Eddy.
“Eddy?”
“Shamsa?”
“Si….sii?”
“Panda kwenye gari tuondoke”
Kwa haraka Shamsa akazunguka upande wa pili wa gari, akaishika laptop na kukaa na kuipakata kwenye mapaja, akafunga mlango na kwakaondoka eneo hilo.
 
“Kuna kitu gani ambacho kinaendelea?”
Shamsa alizungumza huku akimtazama Eddy. Eddy akamtazama na kwa ishara akamuonyesha kwenye kioo cha laptop.
“Ndio nini sasa hii?”
“Ni Signal inayo onyesha ni wapi alipo mzee Godwin, na gari zote hizo uinazo ziona zinakwenda huko zinaeleka eneo hilo”
“Mungu wangu, ujue nimemuona Manka na madam Mery wanaelekea huko na mimi ndio nikawa nina wafukuzia ila sijafanikiwa”
“Madam Mery, Manka?”
“Ndio, sijajua ni kitu gani kilicho tokea kati yao ila nimewaona wakiwa kwenye gari moja?”
“Madam Mery kwani anatambua ni wapi alipo Rahab?”
“Hapana hatambui kwa maana alikamatwa akiwa na sisi”
“Phidaya na Sa Yoo nao wapo wapi?”
“Nimewaacha kwenye kijiji kimoja cha wamasai hapo watajificha kwa muda”
Eddy akazidi kuiendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi akijitahidi kadri ya uwezo wake kuweza kuzifikia gari hizo kutoka ikulu.
                                                                                                         ***
   Signal ambayo ilikuwa inaonekana kwenye vifaa mbalimbali kama simu na laptop ambayo ilikuwa inaonyesha ni wapi alipo raisi Godwin, ikapotea gafla. Gari kutoka ikulu ambazo zilisha karibia kufika katika msitu huo, zikabidi kusimamishwa na madereva wake baada ya mkuu wao kutoa amri ya msafara mzima kusimama.
“Signal imepotea”
Mkuu wao alizungumza kupitia kinasa sauti chake kinacho peleka mawasiliano kwa walinzi wake wote. 
 
“Mkuu sasa inakuwaje?”
“Tusonge mbele”
“Sawa”
Wakaamuru kuendelea kusonga mbele kwa maana hakuna jinsi tena, wakafika aktika njia ya kuingilia katika msitu huo hapo ndipo kila mtu aliweza kushangaa alicho kiona kwa manaa miti karibia yote imeaguka na mpasuko mkubwa wa ardhi umetokea kwenye eneo hilo.
“Jesus Christ what the hell is going on here”(Yesu wangu ni kitu gani cha kuzimu kinacho en delea hapa?)
Mkuu wa msafara alijikuta akizungumza maneno hayo huku macho yakiwa yamemtoka kwa maana kitu walicho kutana nacho ni kitu cha kushangaza sana korogo kubwa kwenda chini lililo pasuliwa na mlipuko huo wa bomu uliwatisha sana.
Wakashuka kwenye magari huku wote wakishangaa. Eneo karibia lote la msitu liliweza kulika na mti yote kuzama ndani ya korongo hilo. Taarifa hizo zikawafikia wanao ishi maeneo ya jirani na eneo hilo huku waandhisi wa habari kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya jiji la Dar ea Salaam wakiwahi ili kuripoti tukio hilo la kushangaza sana.
                                                                                                                        ***
    Eddy na Shamsa naow akawa ni miongoni mwa watu walio simamisha gari zao pembezoni mwa barabara hiyo ambapo pembeni yake kuna msitu huo ambao kwa sasa umebadilisha muonekano wake na kuwa korongo moja kubwa sana. Naye Signal ya sehemu ilipo tokea simu ya mzee Godwin ilipotea wakiwa wanakaribia kufika eneo hilo. Wakashuka kwenye gari hilo huku Edd akiwa amevalia koti hilo la udaktari na Shamsa akiwa na kashati kake akicho katwa mikono.
“Kuna nini kimetokea hapa?”
Eddy alimuuliza mmoja wa mashuhuda aliye simama eneo hilo la barabara.
“Nasikia sikia kuna bomu limelipuka maeneo haya”
“Ndio limesababisha haya yote?”
“Ndio nasikia kwamba kuna askari walikuja kumtafuta raisi Godwin, il ndio kama unavyo ona mwenyewe, bomu limefanya yake”
 
“Mungu wangu”
Eddy alizungumza huku akitembea kwa haraka kujishuhudi jinsi korongo hilo lilivyo refu kwenda chini. Shamsa naye alimfwata kwa nyuma akiwa makini sura yake isionekana kwa maaskari walio zagaa eneo hilo wakitafuta jinsi ya kupita pita pembezoni mwa korongo hilo kutafuta kama kuna majeruhi walio salia,
“Eddy tuondoke eneo hili naamini hakuna aliye pona hapa”
“Tuangalie angalie tuone kama kuna mtu aliye weza kupona”
“Mmmm wewe unahisi kweli kuna mtu anaweza kupona hapa, kwa maana kama miti mirefu iliyo kuwepo hapa, imezama kwenye korongo hilo, itakuwaje kwa binadamu”
Eddy na Shamsa wakasimama kwenye moja ya sehemu na kuchungulia chini, kitu pekee walicho kiona ni miti inayo onekana kwa mbali kwa maaana eneo hilo limechimbika kisawa swa kwenda chini.
“Eddy tazama kule”
Shamsa alimounyesha Eddy kwa kutumia mkono. Eddy akageuza macho yake, kwa mbali akaona gari moja ikiwa tairi zake zote za mbele zikielea hewani kwenye korongo hilo huku tairi za nyuma tu ndio zipo kwenye ardhi na ndnai yake kunaonekana kuna watu.
                                                                                                                       ***
   Kila mtu moyo wake ulizidi kumuenda mbio akiwa ndani ya gari hilo. Madam Mery taratibu akajikuta akianza kusali sala yake ya mwisho kwa maana wanapo elekea kifo kipo mbele yao.
“Fanya uwashe gari”
Manka alizungumza huku machozi yakianza kumwagika, kila jinsi dereva alivyo jaribu kuwasha gari lake, halikuwaka hadi ikafika kipindi akakata tama kabisa. Matairi ya mbele tayari yalisha anza kuelea hewani kwenye korogo hilo linalo endelea kulika taratibu taratibu na matairi ya nyuma pekee ndio yapo kwenye ardhi.
“Ohoo Mungu wangu tunakufa”
Manka alizungumza huku akiyafumba macho yake, akisubiria gari hiyo kuangukia kwenye korongo hilo na huo ndio utakuwa ni mwisho wa maisha yao.
                                                                                                 ITAENDELEA.....USIKOSE SEHEMU YA 98

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts