Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Saba ( 17 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Saba ( 17 )

Written By Bigie on Wednesday, February 28, 2018 | 3:05:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  
‘MAMA NINAKUOMBA UNIPE BARAKA ZAKO ILI NIWEZE KUMUOKOA BABA YANGU’
‘NAKURUHUSU KWA MOYO MMOJA NA MWANANGU NITAKUPA MSAADA WA CHOCHOTE UTAKACHO KIHITAJI HATA NUSU YA NGUVU ZANGU NITAKUPA ILI BABA YAKO AWE HURU KWANI BADO NINAMPENDA SNA’
‘MAMA NIMEDHAMIRIA KUIANZISHA DUNIA MPYA NA YENYE KILA AINA YA NGUVU ZITAKAZO IPINGA MAMLAKA TULIYOPO JUU YETU’

ENDELEA
“Mazungumzo kati ya Hitlaer na mama yake ambaye ni Janet yaliendelea kwa usiri mkubwa huku mama yake akimfundisha mbinu ambazo zitamsaidia mwanae katika kuikamilisha kazi ya kumuokoa baba yake.Hitler alijipanda vizuri na kutokana ni mjukuu wa miongoni mwa Malaika wakubwa mbinguni aliweza kutumia kigezo hicho kushuka duniani bila ya kuhojiwa maswali mengi na walinzi wanao linda dunia ambayo ipo katika hali mbaya ya kuuguzwa moto.
 
Hitler akaaanza kufanya uchunguzi wake kwenye shimo kubwa la moto liitwalo KUZIMU lililo kusanya idadi kubwa ya watu walio tenda maovu,Ila katika kuzimu nako kumegawanyika madaraja ya mateso ambayo yapo saba.Na kila waliopo kwenye daraja moja wanatofautiana kwa adhabu na waliopo kwenye daraja la pili hivyo hivyo na kuendele mbele kiasi kwamba matendo yako ndio yanakuchagua uingie kwenye daraja lipi unalo stahili kuhukumiwa.Hitler akaendelea kufanya uchunguzi wake katika magereza yote saba ila hakufanikiwa kumuona baba yake ambaye kwa jinsi mama yake alivyo muelekeza sio rahisi kwake kushindwa kumtambua ila gafla Hitler akiwa kuzimu……”
“Sory Sir Eddy muda wa kipindi chako umeisha”
Madam Zena alizungumza huku akiwa ameshika vitabu vya somo la Kiswahili jambo lililo pelekea wanafunzi kuanza kuzomea wakikataa asiingie
 
“Jamani tutamalizia hii story yetu kesho”
“Ahhhh Sir EDDY endelea bwanaaa Kswahili bongo akawafundishe mabasha zakee”
Sauti mmoja ya kiume ikitokea nyuma ya darasa ilisikika na kumfanya madama Zena kuchungulia mlangoni huku sura yake ikiwa imekasirika
“Mwana idhaya nani aliye zungumza hayo maneno?”
“Si ninawauliza nyinyi watoto mulio laaniwa na wazazi wenu.Msio na haya mafirahuni wakubwa nyinyi munajua maana ya basha……..Ehhhhh au munavyo jiona nyinyi humu ndani kuna mwanaume aliye kamilika nyote si mashogaa”
Madam Zena alizidi kutokwa na maneno ya kejeli hadi ikafikia kipindi wanafunzi wa kiume wakaanza kuzungumza chini chini na neno lililo sikika kutoka nyuma ya darasa walipo kaa wanafunzi wengi wa kiume ni
“Shoga baba yako aliyekuzaa”
Nikabaki nimeshika mdomo kwani kwa jinsi madam Zena alivyo mweupe wa kujichubu taratibu nikamuona sura yake ikitawali  na wekundu kwa  mbli ulio tokana na hasira
“Nasema nyote tokeni nje mupige magoti”
Wanafunzi wote wakakaa kimya wakisikilizia nani aanze kwenda nje kupiga mogoti ila kadri muda unavyo zidi kwenda hakuna aliye simama kwenda nje
“Monitres nenda kamuite Headmaster na mwalimu wa nizamu”
 
“MONITRES MSALITIIIIIIIIII”
Monitres baada ya kuisikia sauti hiyo ya wezake ikambidi akae kwenye kiti chake na kujikausha kimya na kumfanya madam Zena kuzidi kuchanganyikiwa na hasira ikazidi kumpanda
“Na wewe Malaya ndio umekataa kunyanyuka kisa hao washenzi wezako si ndio?”
“Mimi sio Malaya”
“Kama sio umalaya ni nini kinacho kufanya usiamshe hicho kidude chako uende nilipo kuagiza kuna mwanaume anaye kupak**?”
Madam Zena akazidi kumfokea mtoto wa watu ambaye kiumbo ni mdogo sana kiasi kwamba huwezi kumfananisha na maneno anayoyazungumza Madam Zena
“Zena hembu kausha basi hawa ni watoto usizungumze maneno machafu kama hayo”
“Tena wewe mwana hizaya nilikuwa ninasubiria uingize hilo domo lako lililo kosa haya kumbe wewe ndio unawatuma hawa watoto ili walate jeuri si ndio?”
 
“Hapana Zena ila heshima ni kitu cha bure na tambua mujibu wako wa kazi ni upi ila si kuwatukana watoto wawatu”
“Nenda kule………….Hanisi mkubwa wewe uliye na Jogoo asiye wika anakazi ya kujikunyata kama mbwa jike anayesubiri kupandwa na mbwa dume”
“ZENA……… ZENA……..ZENA”
“Zena jina langu mtoto wa pwani niliye fundwa na kujua jinsi ya kumkatikia yule anaye hitaji kuliko wewe mwanaume suruali”
Machozi ya hasira taratibu yakaanza kunimwafika huku mwili mzima ukitetemeka na kunifanya nitazame chini na sikutaka wanafunzi waitadhimini sura yangu ya hasira.Darasa zima limekaa kimya wakimsikiliza Madam Zena anavyo ropoka maneno machafu kiasi kwamba yanachafua masikio
“Wakisema wanaume watoke na wewe utatoka mwanaume unaye kimbia vita na kufungia watu milango kwa nje”
“ZENA FUNGA BAKULI LAKOOOO
“Heheee eti nifungea bakuli langu hata huyo anaye nit*** haniambii nifungee bakulii langu…..KANITANGAZEEE MWANAUME SURUALI WEEE”
 
   Meza ya mwanafuzi aliyepo mbele yangu nikainyanyua kwa hasira na kuirusha kwa nguvu na kutua kwenye miguu ya Madam Z ena na kumuangusha chini na kuwafanya wanafuni wote kushangaa huku wakimtazama Madam Zena akipiga kelele za kulalamika kuvunjwa mguu.Nikatoka darasani kwa hasira na kwenda moja kwa moja ofisini na kukaa kwenye kiti changu huku ninalia kwa hasira na kuwafanya waalimu wengine kunishangaa
“Eddy unatatizo gani….?”
Sikumjibu mwalimu anaye niuliza swali na sikujua ni mwalimu nani anaye niuliza swali hilo kutokana na machozi mengi kunitawala machoni mwangu na kingine nimeinama chini na kuegemzea sura yangu mwenye meza huku machozi yakidondoka chini sakafuni
“Eddy brother sema unatatizo gani…Umefiwa?”
     Nikatingisha kichwa kuashiria kuwa sikufiwa na mtu wa aina yoyote.Akaingia Madam Recho huku akihema akionekana ametoka kukimbia na kusimama katikati ya ofisi na kujifunga ushungi wake kiunoni
 
“Jamani Eddy amemuua rafiki yangu Uwiiiiii huyu mtu muuaji”
Waalimu wengine ikiwemo na mimi tukastushwa na maneno ya Madam Recho na kila mwalimu akaanza kuuliza huyo aliye uliwa yupo wapi
“Form Four A mimi leo asubuhi nimesema kuna watu humu ndani ni majambazi ila mumezoea kusema Ohhooo Recho mimi naongea sijui mimi kinywa changu kipo wazi.Haya sasa nendeni mukajionee maiti huko”
Waalimu wakaanza kutoka mmoja mmoja huku wakikimbia kuelekea nje akiwemo Madam Recho mwenyewe na nikabaiki na Madam Nyange ambaye ni mama wa makomo.Akatoka kwenye kiti chake na kuja kukaa karibu yangu
“Etii Eddy mwangu ni kweli umeua?”
“Mama yangu mimi hata sijui kama nimeua au laa?”
Nilizungumza huku nikilia na kumfanya Madam Nyange kutoa kitambaa chake kwenye mfuko wa koti alilo vaa na kunipa ili nijifute machozi
“Mmmmm sasa mwangu Eddy ilikuwaje kuwaje hadi ikawa hivyo?”
 
“Mama  Zena mchokozi”
    Nikaanza kumuadisia Madam Nyange jinsi ilivyo kuwa hadi nikachukau uamuzi wa kumuadhibu madam Zena na sikujua hali yake ipo vipi.Akaingia Sir John huku akionekana kuchanganyikiwa huku jasho likimwagika hadi limelowanisha shati lake.Akaniangalia kwa jicho kali kisha akapiga hatua za haraka na kunishika shiti langu na kuninyanyua kisha akanipiga kwichwa kizito na kuniangusha chini na kumfanya Madam Nyange kusimama na kumzuia
“Acha nimfunze adabu hawezi kumpiga demu wangu na mimi nimuache na nitahakikisha utafungwa wewe mbwa”
“John nakuomba utoke njee ”
“Mama siwezi kutoka kwani hajui ni kiasi gani namaliza mshara wangu kwa kumtunza Zena alafu leo kirahisi rahisi anakuja kunimpiga yeye kama nani?”
 
“Sawa John ila nakuomba uende nje mwangu please(tafadhali)”
“Tena ngoja niwapigie polisi waje wakubebe”
    Sir John akatoka nje huku akiitoa simu yake mfukoni na taratibu nikanyanyuka kutoka chini nilipoangukia na kukaa juu ya kiti changu huku machozi yakizidi kunimwagika
“Mwanangu ninakuomba uende zako nyumbani hali imeshakuwa mbaya sawa baba”
“Hapana mama kama wanakuja kunikamata waje wanikamatie hapa hapa kazini kwangu”
“EDDY Nakuomba nenda nyumbani sisi kama shule hili tatizo tutajua tunalitatua vipi?”
“HAPANA MAMA”
Madam Nyange akakaa kimya huku huku akinitazama kwa sura ya unyonge.Akaingia mkuu wa shule na  akanitazama kwa muda kisha akaniomba nimfwate ofisini kwake.Nikanyanyuka na kuanza kumfwata kwa nyuma mkuu wa shule na tukaingia ofisini kwake na kukaa kwenye kiti kilichopo pembeni ya meza yake
 
“Eddy hali ya Zena sio nzuri na hapa ameshakimbizwa hospitalini hembu niambie ni kitu gani kilicho kufanya umjeruhi Zena wakati unatambua sheria ya kazi moja wapo ni ugomvi haitajiki eneo la kazi sasa wewe umefanya nini?”
Nikakaa kimya nikimtazama mkuu wa shule na wala sikujua nianzie wapi katika kulizungumzia swala lililo nifanya nimpige Madam Zena.
“Eddy umeidhalilisha sana taaluma yetu ya ualimu hivi unadhani kuna mwanafunzi atajenga heshima kwako au kwa sisi waalimu ambao tunashindwa kuzizuia hasira zetu na kupigana mbele zao.Na sote tukisema tuwe ma JOHN CENA humu ndani si tutauana kweli na shule itageuka uwanja wa Miereka na….”
Kabla mkuu wa shule hajamalizia wakaingia askari watatu walio valia sare za kipolisi na mmoja wao akatoa kitambulisho na kujitambulisha huku nyuma yao akiwepo Sir John
“Eddy mwenyewe ndio huyo hapo”
“John ni nini umefanya?”
 
“Mkuu huyu ni mwalifu na anastahili haki hii ya kukamatwa wala musinilaumu katika hilo”
“Eddy tunakuomba tuongozane na wewe kwenda kituoni tukahojiane na wewe  mswali mawili matatu”
“Vijana wangu ninawaoba hili swala tulizungumze kwa herufi kubwa kutokana hili swala limetokea kihofisi basi nawaombeni tulizungumze”
Mkuu wa shule alizungumza huku akitoa wallet yake iliyo jaa noti za elfu kumi kumi za kitanzania kiasi kwamba wallet haifungi vizuri na akaanza kuhesabu pesa kwa lengo la kuwapa polisi
“Mzee tunayaheshimu sana mawazo yako ila hatujaja kuchukua pesa yako ila sisi tunamuhitaji Eddy na kama hana kosa la aina yoyote basi tutamuachia huru”
“Sawa ila mukitoka mumeongozana naye kidogo inaweza ikaleta hofu kwa wanafunzi wetu ndio maana ninawaomba tuyamalize humu humu ofisini.Kumbukeni bila sisi nyinyi musinge vaa hizo nguo zenu munazo ringia”
“Mzee sasa hayo ni matusi…..Asee wewe Eddy nyanyuka jinsi unavyokaa hapa ndivyo unajiongezea uzito wa kesi”
“Vijana wangu nawaombeni jamani tafadhali”
 
“Mkuu ngoja mimi niende ila Mngu mwenyewe ndio atakaye nipigania wala usiwe na wasiwasi”
    Nilizungumza huku nikijifuta machozi kwa kitambaa alicho nipa Madam Nyange kisha nikanyanyuka taratibu na kuanza kupiga hatua za kutoka nje huku askari wakifwa nyuma yangu.Nikakutana na waalimu wengine wakabaki wamenitazama kwa sura za huruma kasoro Madam Recho aliye nizomea kisiri siri.Wanafunzi wa kidato cha nne walipo niona nimeongozana na maaskari wakatoka huku wakinikimbilia wakiwa wanaliita jina langu na baadhi yoa wakitokwa na machozi
“Sir Eddy hatuto soma hadi wewe uachiwe huru kwani ukweli wote tunaujua sisi”
“Hapana wadogo zangu nyinyi someni kwani kusoma ndio msingi wa maisha yenu.Hata ikitokea nimefungwa sinto wasahau wadogo zangu”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika na kuwafanya wanafunzi wa kike kuongeza vilio huku kila mmoja akihitaji kunipa mkono wa kwaheri kabla sijaingia ndaniya gari la polisi
“Sir kweli tutaandamana ili usifungwe…Wewe ndio tunaye kuelea peke yako na hakuna mwengine tunaye muelewa zaidi yako”
 
       Mwanafunzi mmoja alizungumza kwa niamba ya wezake huku machozi yakiwa yanamwagika.Askari mmoja akanishaka suruali yangu na kutaka kuninyanyua kwa nyuma huku akinihimiza nipende kwenye gari.Wanafunzi wakaanza kumzomea askari aliye nishika na ikambidi aniachie huku askari wengine wakizishika bunduki zao vizuri kwani gari lao lilianza kuzungukwa na wanafunzi hata wa vidato wengine ambao hawakujua ni nini kinacho endelea
“Wadogo zanugu muna nisikializa?”
“Ndio Sir Eddy!!!”
“Ninawaombeni murudi darasani siwezi kwenda jela nawahakikishia kesho asubuhi tutakuwa pamoja SAWA”
      Nilizungumza na kupanda kwenye gari la polisi na taratibu gari likaanza kuondoka endeo la shule na kusababisha wanafunzi kuanza kulikimbiza kwa nyuma huku wengine wakilirushia mawe na baadhi ya wanafunzi wanao kuja shule na pikipiki na baiskeli wakaanza kulifukuzia kwa nyuma gari la polisi.Tukafika katika kituo cha polisi cha Mabawa na nikaingizwa kwenye chumba cha mahojiano na askari mmoja akaichukua simu yangu.Ila baada ya muda kidogo nikasikia kelele za wanafunzi wakiimba huku wakisema wanamtaka Mwalimu Eddy.Kelele zikazidi kutawala kiasi kwamba ikapelekea askari kuanza kupiga mabomo ya machozi ili kuwatawanya wanafunzi
 
“Aisee hiyo miwanafunzi yako inakupenda eheee”
    Askari mmoja aliniuliza huku akizungumza kwa lafudhi ya kikuria na sikumjibu kitu zaidi ya kukaa kimya.Ilaa baada ya muda sikusikia tena nyimbo za wanafunzi wakiniimbia wakiwataka polisi waniachie huru.Nikaendelea kukaa katika chumba nilicho ingizwa huku kila askari akionekana hana haja na mimi na kila mmoja aliendelea na shuguli zake.Mida ya jioni nikaitwa na askari mmoja na kutoka nje ya chumba nilichopo na kukutana na mwanamke nisiye wahi kumuona katika maisha yangu
“Upo huru nenda zako”
    Askari yule alizungumza huku akainipa simu yangu na kujikuta nikiwa siamini kwa kitu kilicho toke kwani moja kwa moja nilijua maisha yangu ndio yanaelekea ukingoni.Mwanamke niliye ambiwa amenichukulia zamana akaniomb niongozane naye hadi alipo lisimamisha gari lake na sikuwa mbishi na nikamfwata huku njia nzima nikimshukuru kwa kitu alicho nifanyia ila mweznangu hakunijibu kitu chochote zaidi ya kutabasamu.Tukaingia kwenye gari lake aina ya OPA na kukaa siti za mbele na hatukuelekea sehemu yoyote  zaidi ya gari kusimama
 
“Nakushukuru tena sana dada yangu”
“Eddy hauna haja ya kunishukuru nilitaka nikuonyeshe jinsi nilivyo iongezea uwezo nyota yako na lile lengo nililokambia nahitaji kukufanya mtu mwenye dhamani daniani ndio linakwenda kukamilika”
Sauti ya mwanamke huyo inafanana na sauti ya Olvia Hitler ila umbo na sura havifanani naye kabisa jambo lililo nifanya nianze kupata wasiwasi
“EDDY utataniogopa hadi lini?”
“Hapana sikuogopi”
“Eddy unajua sisi tuna uwezo mkubwa wa kukiona kile kilichopo moyoni  mwa mwanadamu na ndio maana ninakuambia Eddy kuwa bado unaniogopa.Na nimeamua kuja katika umbo ili na sura nyingine”
“Ila ni kwanini Olvia umeamua kunifanyia hivi unavyo nifanyia?”
“Eddy huo ni mtihani wako wa kwanza na umebakisha mitiani mingine sita ili itimu saba na ukishafikia katika kiwango ninacho kihitaji mimi na wala sinto kuambia ni lini mitihani hiyo itakamilika”
 
“Ila bado hujanijibu swali langu ni kwanini umeamua kunifanyai hayo unayo nifanyia?”
Olvia Hitler hakunijibi kitu cha aina yoyote zaidi ya kushuka kwenye gari na kuanza kuondoka ikanilazimu na mimi kushuka kwenye gari ila mwezangu akawahi kuvuka upande wa pili wa barabara na kuniacha mimi nikiwa nimesimama nikisubiria gari mbili zilizo ongozana zipite ndio nivuke.Gari zikapiata na mimi nikavuka barabara cha kushangaza sikuweza kumuona mwenzangu ameelekea upande gani ikanibidi nirudi upande nilio kuwepo na kilichozidi kunichanganya sikuikuta gari tuliyo kuwepo.
Nikapata wazo la kwenda nyumbani kwa bibi niliye kuwa ninaishi jirani naye,kwa woga nikaogopa hata kupanda bodaboda na ikanilazimu nianze kutembee kutoka maeneo ya Mabawa hadi  Chuda,nikaingia kwenye duka moja na kurusha vocha kisha na kuitoa simu yangu na kumpigia Hilda
“Shem mbona hadi sasa hivi haujarudi?’
“Kuna sehemu nitapitia hadi baadaye nitakuambia uje unifwate?”
“Sawa ila upo salama kweli?”
“Ndio….kwanini unaniuliza hivyo?”
“Kwa sababu unazungumza kama unaumwa?”
“Kidogo sipo sawa kivile”
“Powa shem wangu kipenzi cha roho yanngu”
“Powa”
Nikakata simu na kuendelea na safari yangu na kwa mbali kutoka nilipo hadi ilipo nyumba ya bibi nikaona nje kumefungwa turubai huku watu walio valia kanzu wakiwa wamekaa kwenye majamvi huku ukimya ukiwa umetawala katika endeo hilo.Nikazidi kuongeza mwendo huku akilini wazo la bibi kuwa amefariki dunia likaanza kunitesa,Kabla sijafika karibu na sehemu ilipo nyumba ya bibi nikastuka mtu akinishika mkonno kwa nyuma huku akinivuta kwa nguvu

ITAENDELA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts