Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Sita ( 16 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi na Sita ( 16 )

Written By Bigie on Tuesday, February 27, 2018 | 2:54:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   

“NAHITAJI SIRI HII UITUNZE NA USIMWAMBIE BINADAMU WA AINA YOYOTE NA LAITI UKIDHUBUTU KUMWAMBIA MWANADAMU KUWA UMEKUTANA NA MIMI NITAITOA ROHO YAKO UMENIELEWA……?”
“Ndi….ooo”
“Na kingine nitahitaji uwe rafiki yangu”
“Siwez….”
Kabla hata sijaimaliza sentensi yangu nikajikuta akinisukuma na kunikandamiza ukutani huku mkono wake akiwa umenikaba kwenye koo lango na nikaanza kuhisi roho yangu ikitaka kunitoka kwani ananguvu nyingi na kingine kinachozidi kuniogopesha ni macho yake kaunza kuwaka moto huku akitokwa na machozi ya damu

ENDELEA
      “Katika maisha yangu haijawahi binadamu wa aina yoyote kunikataa”
Olvia Hitler alizungumza na sauti nzinto iliyo nifanya nizidi kuogopa,kisha akaniachia na nibaki nikiwa nina elea elea angani.Sura yake ikarudi katika hali yake ya kawaida huku akiwa ananitazama kwa tabasamu zuri
“Eddy narudia tena kuzungumza mimi sio kiumbe mbaya wa kuwadhuru wanadamu ila ninauwezo wa kumdhuru yule tu anaye hitaji mimi nimfanyie hivyo……Nahitaji kukufanya kuwa mtu maarufu na anaye fahamika sana Tanzania na Duniani kwa ujumla”
“Ki…v…ipi?”
“Sawali zuri,kwanza unatakiwa usiniogope.Pili unatakiwa kufwata zile amri zangu nitakazo kupa na nilizo kupa……Natambua sana moyo wako unampenda Rahma japo huyo mwnamke mchafu anakufanya ummsaliti…..Kutokana hukuwa unajua ni kitu gani kinachoendelea kwa leo nitakusamehe ila kwa sharti moja tu nahitaji ummuamshe huyo mwanamke na aende zake kwake wakati huu kisha ndio nitaendelea na mazungumzo na wewe”
 
“Sa..sawaa”
     Nilizungumza kwa kigugumizi kisha taratibu akanirudisha kitandani na gafla akapotea na hali ya chumba ikarudi kama kawaida na nikajikuta nimekaa kitandani huku shuka likiwa limenifunika kuanzia miguuni hadi kwenye kiunoni,Nikamtazama Halda mwenzangu hana hata analo lijua ndio kwanza ananazidi kukoroma kiasi kwamba nikaanza kujipa moyo labda  inaweza ikawa ndoto.Nikaanza kumtingisha Halda huku nikiliita jina lake hadi akaamka  na kukaa kama nilivyo kaa mimi huku akipiga miyayo ya usingizi
“Nakuomba uvae uende kwako”
“Eddy”
“Wewe ninakuomba uvae uende kwako sasa hivi”
“Eddy umechanganyikiwa?”
“Sijachanganyikiwa nina akili zangu ni nzima kama unavyo niona ila nakuomba tuu uvae na uenda kwako kama kulala tutalala siku nyingine”
“Eddy kama unaota nakuomba uniache mimi nilale shughuli uliyo nipa ni kubwa sawa mpenzi wangu”
Halda alizungumza huku ikijilaza tena kitandani na kunifanya nimuamshe kwa nguvu hadi akaanza kukasirika
“Eddy saa tisa yote hii unataka mimi niende wapi mwanaume gai huna huruma au unataka usiku huu nikabakwe huko barabarani?”
 
“Kama utabakwa ukiwa ndani ya gari basi ila ninacho taka mimi vaa nguo zako uende zako kwako sitaki matatizo na mpenzi wangu”
“Eddy siondoki”
“Kumbuka upo kwangu?”
“Hata kama ila siondoki lije WINCHI,TREKTA au KATAPILA haliwezi kuning’oa hapa kitandani na wala siondoki”
“Hilda unanijua tena vizuri? Sihitaji nikubamize ndio uondoke”
“Eddy nipige,nikate kate,nivunje vunje,nisage sage ila mimi siondoki NG’OO”
 Nikazidi kuchanganyikiwa kwani Halda hakutaka kabisa kusikia kitu kinacho itwa kuondoka ikanilazimu kushuka kitandani na kujifaunga taulo langu na kumbukumbu ya maji aliypo nipa bibi ikanijia kichwani nikakaumbuka nimeyaweka jikoni
“Unakwenda wapi sasa?”
“Wewe lala kama hutaki kuondoka niache”
“Sasa Eddy huko nje usiku huu unapo kwenda untaka kwenda kufanyaje?”
“Kwani nimekuambia ninakwenda nje hembu lala huko”
“Nakufwata”
 
Halda akanyanyuka kitandani huku akiwa ameijifunga shuka na kuanza kunifwata jikoni ninapo elekea,Nikaikuta chupa ya maji katika sehemu niliyo iweka kaisha taratibu nikayatoa kwenye kifuko cheusi nilipo kuwa nimeyaweka
“Sasa hayo maji ni ya kazi gani?’
“Hilda hembu niache wewe rudi chumbani kalale”
“Mmmm haya mwaya kama ndio uchawi wa kwenu kunywa maji ya Dasani usiku wa manae”
  Halda alizungumza huku akirudi zake chumbani kwangu,nikamchungulia na kuona tayari ameingia ndani kwangu na kuufunga mlango.Nikapiga hatua za kwenda nje nikashika kitasa cha mlango na kufungua.Moyo ukanipasuka kiasi kwamba nikajikuta natamani kuzirai kwanik eneo zima la nje ya nyumba yangu nikakuta ni bahari tena yenye maji mengi huku Olvian Hitler akiwa amekaa kwenye kiti cha dhahabu huku pembeni yake kukiwa na wasichana wawili wanao mpepea kwa mikia ya Simba iliyo tengenezwa vizuri huku wakiwa juu ya maji
“Eddy nashindwa kuamini kama mwanamke huyo umeshindwa kumtoa ndani kwako”
Nikageuka nyuma ili nifungue mlango na kustuka baada ya kuukuta mti mkubwa nyuma yangu na urefu wake hauishi katika kutazamika kuelekea juu huku mimi nikiwa nimesimama juu ya mzizi mkubwa na mpana
“Eddy wala usiogope hapo ulipo ni sehemu salama na hauwezi kuudhurika”
 
“Hivi lengo lako haswa wewe ni nini?”
“Lengo langu ni wewe kuweza kukubaliana na mimi kuwa miononi mwa rafiki zangu nitakao wafanya kuwa watu wenye dhamani sana duniani”
“Kwa staily hii unadhani mimi kweli nitakubali?”
Nilizungumza kwa kujiamini kwani tayari nilisha anza kumzoea Olvia Hitler ila kitu kinacho niogopesha ni bahari kuwepo nje ya nyumba yangu
“Eddy natambua kuwa katika maisha yako umeweza kupitia mambo mengi ya kusikitisha na yaliyo jenga makovu makubwa makubwa katika moyo wako na maisha yako kwa ujumla.Uliweza kuwapoteza wazazi wako katika mazingira ya kutatanisha pili ukaweza kumpoteza mdogo wako mbele ya macho yako kwa kubakwa na watu usio wajua ila cha kustaajabisha watu hao hadi sasa hivi wapo na wanaishi maisha ya amani na furaha bila ya serikali kuwachulia sheria ya aina yoyote.Tatu umekuwa ni mwanaume wa kuomba omba na kusaidiwa na mwanamke amabye kwako bado hujampa dhamani kama anayo kupa yeye.”
“SASA HAYO YOTE YAMETOKA WAPI NAKUOMBA UNIACHE NA MAISHA YANGU”
 
Olvia Hitler akacheka kwa sauti ya juu na kufanya majani ya mti kuanza kupeperuka huku mengi yakiniangukia kichwani
“Hembu kwanza tupa hicho kijichupa chako ulicho kishika.Usidhani kuwa unaweza kunizuia kwa maji hayo ulio pewa na binadamu mwenye uwezo mdogo sna”
“Mimi mbona sikuelewi wewe?”
“Utanielewa….Wewe ni mwalimu wa masomo ya science ila ninakuomba kuanzia muda utakapo rudi kazini uende ukafundishe somo la Historia na nitakupa kitu kizuri utakacho weza kufundisha na utakuwa mwanadamu wa kwanza kufundisha kile kitu nitakacho kufundisha mimi”
Gafla Olvia Hitler akapotena na watu wake na kujikuta nimesimama nje ya mlango wa nyumba yangu na kichupa changu kikiwa mkononi huku mwili wangu ukinitetemeka kwa hofu
“Hayo maji ndio umeamua kuja kuyanywea huku nje?”
   Sauti ya Hilda ikanistua na kunifanya nigeuke nyuma kwa haraka na kumkuta amesimama huku ameshika kiuno kwa mikono yeke miwili.Nikajikuta ninataka kuzungumza nilicho kiona ila kinywa changu kikashindwa kufumbuka na kujikuta nikirudi ndani huku Halda akiiufunga mlango na kunifwata nyuma.Nikajutupa kitandani na kuanza kufikiria yaliyo mengi huku jacho likinimwagika na kujikuta nikianza kujutia ni kwanini niliamua kuhama uswahilini kwangu
“Eddy mbona jasho linakumwagika unaumwa?”
“Hapana?”
 
“Mmmm wewe mwanaume una matatizo hembu niambei una tatizo gani mpenzi”
“Hapana sina tatizo”
“Basi nyanyuka uende ukaoge”
“Ahhh henbu ligeuzie hilo feni upande wangu”
Hilda akafanya kama nilivyo muagiza kisha taratibu feni likaaanza kunipepea huku naye akiwa na kazi ya kunifuta jasho linalo nitoka mithili ya mtu aliye toka kukimbia mbio ndufu.Usingizi mzito ukanipitia na kulala fofofo,Halda akaja kuniamsha asubuhi
“Eddy chai tayari”
“Ok nakuja”
“Amka basi tukanywe wote kwani itapoa”
“Sawa tangulia ninakuja”
Nikajinyanyua kiuvivu vivu kisha nikaingia bafuni nikapiga mswakii na kuoga na kurudi chumbani na kuvaa nguo kwa ajili ya kwenda kazina kwani hata hamu ya kukaa ndani ya nyumba niliyo hamia tayari ilishaanza kunipote
“Eddy natai saa hizi unakwenda wapi?”
“Nataka niende kazini”
“Saa hizi?”
“Kwani ni saa ngapi?”
 
“Saa nne na nusu asubuhi”
“Haina tabu nitakwenda hivyo hivyo”
Ok basi njoo unywe chai”
Nikakaa mezani na kuanza kunywa chai aliyo iandaa Hilda huku kichwani kwangu nikiwa na mawazo ya kumfikiria Olvia Hitlar kwa vituko anavyo nifanyia
“Mbona unaonekana kuwa unamawazo?’
“Nipo kawaida”
“Kawaida? Eddy japo sijakaa na wewe kwa muda mrefu ila nimesha kuzoea hiyo hali yako sio ya kawaida”
“Kawaida nizoee”
“Asubuhi nilikwenda sokoni nikanunua vitu muhimu vya ndani na kama utahitaji matunda yapo kwenye friji”
“Sawa”
“Mmmmm mbona unanijibu shoti shoti au  kwasababu nimejipendekeza kwako?”
“Hapana”
Nikamaliza kunywa chai na kuchukua begi langu lenye laptop na baadhi ya vitabu na kulivaa mgongoni
“Mchana nikupikie nini?”
“Chochote ila leo uende kwako”
“Sawa nitakupikia mapishi ya kihindi ukija wewe mwenyewe utafurahi”
“Sawa”
 
“Nikupeleke kwa gari?”
“Hapana nitapanda daladala”
“Mmmm haya kazi njema”
   Kabla sijatoka Halda akanishika mkono na kunipiga busu la mdomoni kisha akainiachia na nikaelekea kwenye kituo cha daladala nikapanda na sikutaka kusemeshana na mtu hadi nikafika sehemu ninayo shuka na kumuomba konda kusimamisha gari na mimi nikashuka na kulipa pesa yake anayo ihiyaji.Nikafika shuleni na kuingia moja kwa moja ofisini na kuwafanya waalimu wengine kunishangaa kwani hawakutarajia kuniona katika siku ya leo
“Eddy si unaumwa?”
“Kidogo najisikia vizuri nikaona ni bora nije kazini kuwajibika”
“Aaisee ningekuwa ndio mimi nimepewa ofa kama yako ningekaa mpaka ninenepe”
Mwalimu John alizungumza na kuwafanya waalimu wengine kucheka kwa furaha kwani kwa jinsi alivyo mwembamba ni vigumu sana kwa yeye kunenepa kwa likizo fupi
“Sir John una kipindi kidato cha nne ‘A’?”
“Ndio ninavyo viwili vya historia”
“Basi nakuomba kidogo nikawafundishe Physics”
“Sawa hakuna tatizo”
 
Nikachukua vitabu vyangu vya somo la Physics nikiwa natoka mlango wa ofisini nikakutana na Madam Recho akanipandisha na kunishusha kisha akaachia msunyo wa chini chini nikampotezea wala sikusemeshana naye na nikaeelekea katika darasa la Kidato cha nne.Wanafunzi wakanisalimia kama kawaida
“Monitor hembu nenda kaangalie form four B kama hawana mwalimu waambie wale wano soma Physics wote waje”
    Monitor akatoka na kuniacha nikiwa ninapiga mistari ubaoni kwa kutumia chaki kujiandaa kwa kufundisha somo hilo linalopendwa na wanafunzi wachache.Kilicho nishangaza ni wale wanafunzi wasio soma somo hilo kubaki darasani kwani tumezoea kuwaona katika vipindi cha Physics hutoka darasani na kwenda kujisomea.Wanafunzi wa kidato cha nne B wakaja wote hata wale waiso soma somo hilo na nikabaki nimeshaangaa
 
“Walio kosa viti wakachukue viti vyao na haraka tuje tuendelee na somo hili la leo”
Wanafunzi wakafanya kama nilivyo waagiza na baada ya muda darasa likawa limejaa vizuri na wakaanza kunisikiliza kwa umakini.Kila nikijaribu kuiweka akili yangu sawa ili niandike vitu vinavyo husiana na somo la Physics nikajikuta ninashindwa na taratibu nikaanza kuisikia sauti ya Olvia Hitler kwenye akili yangu akinielezeea kitu cha kufanya
“Leo naona tuiache Physics kidogo na tuangalie somo la history kama mtu utakuwa na sehemu ya kuandika notce basi fanya hivyo.Hata nyuma ya daftati wewe andika
 
“Sir hata nyuma ya daftari la Physics?”
“Ndio”
Akilini mwangu nikaanza kupata picha ambayo Olvia Htler akaniomba niielezee kama ninavyo iona
“Kulikuwa na vijana wawili mmoja akiitwa Janet na mwengine akiitwa Eddy……Hawa vijana walikuwa wamependa katika chuo kimoja kinaitwa HALLTON.Katika hali ya kawaida vijana hawa wanaonekana ni binadamu wa kawaida japo wanauzuri wa kuvutia machoni mwa watu wengine….Janet yeye alikuwa ni jamii ya malaika kutoka kwa Mungu ila mama yake ni binadamu wa kawaida ila baba yake ni malaika.Ila kwa upande wa huyu Eddy yeye alikuwa ni jamii ya kishetani na babu yake alizaa na shetani na kuweza kutengeneza familia yenye watoto wenye nguvu za ajabu
 
   Kwa upande wa Eddy aliweza kumshawishi Janet ambaye alikuwa ni mpenzi wake kufanya naye vitu vya ajabu vilivyo weza kumfanya Janet akiuke katika yale mambo muhimu aliyo takiwa kuyafanya kama mtu wmema.Kitendo hicho kilizidi kumuudhi muumba wa mbingu na nchi mpaka ikafikai hatua akaamua kuingamiza dunia.Ila kwa upande wa Eddy akisadiana na Dareen binti mwenye asili ya kishetani huku kukiwa na binti mwengine anayeitwa Minaele ambaye naye ni jamii ya shetani toka katika falme nyingine ya kishetani inayoitwa Golden Kingdom na kwapamoja wakawa na lengo kubwa la kuweza kuiokoa dunia isiangamie jambo lililokuwa gumu na ikapelekea Eddy kuingia kuzimu hii ni baada ya kumsukuma shetani aliye jipa jina la Dulah
 
    Dunia yote ilaanza kuwaka moto huku Janet akichukuliwa na wazazi wake ambao ni Malaika japo Janet alikuwa na mwenye dhambi.Kwa usiri wa hali ya juu Janet aliweza kuitunza mimba alitopewa na Eddy na akajifungua mtoto wa kiume ambaye kila jisi muda na wakati ulivyozidi kwenda ndivyo jinsi navyokuwa.Na mukumbuke kuwa Eddy ana asili ya kishetani na Janet anaasili ya Kimalaika.

Janet akampa mtoto wake jina la Hitler na akawa ni miongoni mwa malaika walio na nguvu nyingi kupita wengine wote.Hitler akazidi kumsumbua mama yake juu ya alipo baba yake ndipo mama yeke akaamua kumueleza ukweli wa nini anachopaswa kukifanya katika kumfungua baba yake alipo katika bwawa kubwa la moto linalo lindwa na Malaika wenye nguvu na hakuna anayeweza kudhubutu kutoka kwani waliomo ndani ya bwawa hilo wamefungwa na minyororo mikubwa na migumu kupita maelezo.Kuna siku Hitler alizungumza na mama yake katika maficho ya siri yaliopo mbinguni kiasi kwamba ni vigumu kwa wengine kusikia wanacho kizungumza
‘MAMA NINAKUOMBA UNIPE BARAKA ZAKO ILI NIWEZE KUMUOKOA BABA YANGU’
‘NAKURUHUSU KWA MOYO MMOJA NA MWANANGU NITAKUPA MSAADA WA CHOCHOTE UTAKACHO KIHITAJI HATA NUSU YA NGUVU ZANGU NITAKUPA ILI BABA YAKO AWE HURU KWANI BADO NINAMPENDA SNA’
‘MAMA NIMEDHAMIRIA KUIANZISHA DUNIA MPYA NA YENYE KILA AINA YA NGUVU ZITAKAZO IPINGA MAMLAKA TULIYOPO JUU YETU

 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts