Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 17 na 18)

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 17 na 18)

Written By Bigie on Thursday, March 1, 2018 | 5:46:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA 
ILIPOISHIA       
“Mama kuna nini?”       
“Kuna nyaraka za serikali ambazo ni muhimu sana, zimeibiwa. Sijui nitafanya nini mimi”
Mama alizungumza kwa unyonge huku machozi yakimlenga lenga mikono yake akiwa ameiweka kichwani, hapo ndipo taratibu nikaanza kupata picha ya mtu ambaye alitoka kasi na nilimuhisi kwamba ni mwaume wa Yudia kumbe sivyo hivyo ni mwanaume aliye kuja kuiba nyaraka muhimu za mama.
“Dany mwanangu unatakiwa kufanya kitu, la sivyo kazi sina mwanaungu”
Mama alizungumza huku machozi yakimwagika kitendo kilicho nifanya nijisikie vibaya sana moyoni mwangu.
   
ENDELEA
Kwa ishara nikamuomba Yudia kutoka chumbani kwa mama, naye akafanya hivyo akiwa katika hali ya woga. Taratibu nikamshika mama na kumkalisha kitandani kwake.
“Nitafanya nini mwanagu, mkataba huo ni muhimu na kesho kutwa raisi anakuja Tanga na anahitaji kuweza kuusaini”
Mama alizungumza machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Ikanibidi kukaza roho kama mtoto wa kiume kuto kulia mbele ya mama yangu kwa maana, machozi yake yanaufanya mwili wangu wote kusisimkwa na kujihisi na mimi ninaweza kudondosha chozi muda na wakati wowote.
“Kwani mama kuna kitu watu ambao una bifu bifu nao?”
Mama akakaa kimya kwa muda, kisha akatingisha kichwa kuashiria kwamba kuna watu ambao ana ugomvi nao.
“Ni kina nani hao?”
“Kuna huyu meya mpya, wao nina uhakika kwamba ndio wanao winda hizi nyaraka, wanataka kuziteketeza ili mpango wa ujenzi wa bandari mpya usifanikiwe”
 
“Na huyo meya ana kaa wapi?”
“Raskazoni kule”
“Ok ngoja nianze kuifanya hivyo kazi muda huu, ila nina kuomba usilie sawa mama yangu”
“Sawa”
Nikamfuta mama machozi kwa kitambaa chake, kisha nikanyanyuka na kutoka chumbani humo. Nikakutana na Yudia kwenye kordo akiwa kama ni mtu mwenye wasiwasi na kitu fulani, ila sikutaka kumsemesha chochote kwa maana mambo ya muhimu ya mama yamesha haribika. Tukiwa hapo kwenye kordo tukasikia sauti ya kungele ya getini ikiita. Yudia kwa haraka akaondoka na mimi nikaingia chumbani kwangu.
Nikafungua kabati na kutoa begi langu la nguo, nikaitoa bastola yangu, niliyo iweka chini kabisa ya nguo zangu, nikaitazama huku nikitoa magazine yake, nikaikuta ikiwa na risasi za kutosha na wala sijaitumia muda mrefu. Nikaiweka pembeni kisha nikatoa suruali yangu ya jinzi nikaiweka pembeni, nikiwa katika hatua hizo nikasikia mlango ukigongwa, kwa haraka nikaichukua basola yangu na kuirudisha ndani ya begi na kwa mwendo wa taratibu nikaelekea mlangoni na kuufungua.
 
“Kaka Dany daktari amesha fika”
“Nakuja”
Nikaufunga mlango mara baada ya Yudia kumaliza kunipatia ujumbe wake, nikalifunga begi vizuri na kutoka chumbani kwangu nikakutana na daktari ambaye mama alizungumza naye muda mchache ulio pita, nikamsalimia kutokna ni mzee wa makamo ya kina mama.
“Muheshimiwa yupo wapi?”
“Amejipumzisha mama, unaweza ukaanza kunihudumia tu”
“Ok sawa ninakuomba nione kidonda chako”
Taratibu nikavua shati na kumuonyesha daktari Kidonda hicho.
“Kimeanza kukauka”
Alizungumza, huku akikigusa gusa kwa juu. Akafungua kiji begi chake kidogo cha mkononi, akatoa kichupa kidogo pamoja na bomba la sindano lililo jipya kabisa.
 
“Nitakuchoma sindano ya kukikausha ndani ya siku mbili hizi kitakuwa kimepona kabisa”
“Ina maana na ngozi yake itarudi kama kawaida?”
“Hapana ngozi itarudi taratibu taratibu”
“Sawa”
Akachukua pamba na kuipaka dawa ya kusafishia, kwenye mshipa wa mkono wa kushoto. Alipo maliza kufanya hivyo akanichoma sindano hiyo yenye dawa ambayo nilisha wahi kuchomwa hospitalini juzi.
“Kijana unaonekana unafanya sana mazoezi”
“Kwa nini?”
“Mishipa yako imejitokeza kiurahisi ni tofauti sana na watu wengine mishipa yao kujitokeza ni kazi sana”
“Ahaaa, huwa na fanya sana mazoezi”
Daktari akachomoa sindano yake baada ya kuisukuma damu taratibu. Akanipatia pamba iliyo na dawa nikajiziba nayo katika eneo ambalo amenichoma sindano.
“Kesho asubuhi ukija Hospitalini kwangu nitakuchoma nyingine ya kumalizia”
 
“Sawa sawa hospitali yako ipo eneo gani?”
“Barabara ya pili pale”
“Ahaa ok asante”
Nikamuga daktari huyo na kuingia chumbani kwangu, nikafungua begi langu na kuitoa bastola kisha nikavua pensi na kuvaa jinzi, sikuona haja ya kulivua shati nililo livaa. Nikaichomeka bastola yangu kiunoni kwa nyuma na kutoka chumbani kwangu. Nikaingia jikoni kwa ajili ya kunywa maji kabla sijaanza upelelezi wangu wa kuifwatilia nyumba ya meya ambaye mama anamtilia mashaka.
Nikiwa hapo simu ya Yudia ikaingia mesiji, mwenyewe hakuwepo nikaona bora niichukue na ili kuifungua meseji hiyo niliyo hisi labda ni mtu ambaye ni bwana wake.
(Mambo yameharibika, kaeni kwa tahadhari mjulisheni na meya)
Meseji hiyo ameituma Yudia kwenda kwa mtu huyo aliye jibu ‘SAWA’. Nilijikuta nikianza kupata mashaka makubwa, kwa haraka nikaituma namba ya mtumaji wa meseji hiyo kwenye simu yangu, nilipo hakikisha kwamba nimemaliza kuituma. Nikaifuta meseji yake aliyo tuma na niliyo jitumia na simu ya Yudia nikairudisha sehemu nilipo itoa, nikatoka jikoni humo nikiwa nimejikausha na nikamkuta Yudia akingia kwenye mlango wa sebleni akitokea nje.
 
“Kuwa makini na mama”
“Sawa”
Nikataka kutoka ila ikanibidi kuelekea chumbani kwa mama. Nikagonga mlango wake, kwa sauti ya unyonge akaniruhusu kuingia. Nikaingia na kumkuta akiwa amelala kitandani amejikunyata huku akitazama makatuni kwenye Tv kubwa iliyopo ukutani mwake.
“Unajisikia kutoka leo mama”
“Hapana Dany, kichwa changu hakipo sawa”
“Basi nakuomba tuweze kutoka”
“Dany”
“Mama tafadhaki nakuomba tuweze kutoka, tazama kukaa kwako kwa huzuni kisukari inaweza kupanda”
Mama akanitazama kwa macho ya uchovu, kishwa kwa msaada wangu nikamnyanyua kitandani na kukaa kitako. Akashusha pumzi kidogo kisha akashusha miguu yake kitandani.
“Unataka twende wapi?”
“Sehemu yoyote japo kupunga upepo”
“Mmm”
“Ndio, jiandae basi”
“Sawa nipe dakika kumi”
“Poa”
 
Nikatoka chumbani kwake na kwenda kumsubiri sebeleni ila nikiwa kwenye kordo ambapo unaweza kuona mtu aliyopo jikoni nikamuona Yudia akikata simu baada ya kuhisi uwepo wangu na kujifanya yupo bize anaendelea na kazi zake. Sikutaka kumuonyesha labda kuna kitu ambacho nimesha kitilia mashaka juu yake. Nikapita zangu na kukaa jikoni huku nitoa simu yangu na kujaribu kukagua majina ya marafiki zangu. Nikaona jina la Joseph, rafiki yangu ninaye fanya naye kazi moja ila yupo kwenye kitengo cha mawasiliano ndani ya ikulu. Nikampigia namba yake iliyo anza kuita taratibu kisha ikapolewa.
“Dany Dany babaa niambie”
“Safi mwanangu, lete habari”
“Daaa safi kaka, nasikia upo likizo hata kupeana shavu?”
“Ndugu yangu shavu la wiki moja”
“Ahaaa wiki moja mbona ndefu sana”
“Yenyewe imekuja kimazabe zabe sikutegemea kabisa”
“Wacha wee”
“Sasa ndugu kuna meseji nitakutumia hapa, naomba unisaidie”
“Poa poa, ila Dany ukirudi nijie na wale samaki wadogo wadogo ulio kuja nao kipindi kile”
“Uono?”
 
“Ewalaaaa hao hao uwono”
“Poa nitakujia nao”
“Sawa ndugu yangu”
Nikakata simu na kumtumia Joseph namba niliyo ichukua kwenye simu ya Yudia, anisaidie kupata habari ya mtu huyo aliye tumiwa meseji ile. Sikukaa sana sebleni mama akatoka chumbani kwake akiwa amevalia vitenge vyake.
“Yudia pika wali leo”
“Sawa mama ndio ninapika”
“Ok sisi tunatoka uwe makini na getini, hakikisha haingii mtu”
“Sawa mama”
Tukatoka ndani, mama akanikadhidhi funguo ya gari, Yudia akatoka na kutufungulia geti. Tukaondoka taratibu katika eneo la nyumabi kwetu huku ukimya ukiwa umetawala.
“Mama Yudia umemtolea wapi?”
“Kwa nini?”
“Nakuuliza tu”
“Umesha anza tabia yako ya kuwatamani wadada wa kazi eheee”
“Hapana mama nia yangu sio hiyo”
“Kama sio hiyo kwa nini unamuulizia”
Sikutaka kumueleza mama juu ya kitu ninacho kihisi kwa Yudia, kwa maana ana onekana kumuamini sana msichana huyu. 
 
“Hamna”
“Uache tabia yako, usije ukacheza cheza na watoto wa watu”
“Sawa mama”
Moja kwa moja tukaeleka kwenye hoteli ya Tanga beach Resort. Tukaa sehemu ya mapumziko, nikaagizia vinjwaji pamoja chakula kwa maana ninatambua mama hajapata chakula cha mchana.
Nikiwa katika harakati za kuanza kula, simu yangu ikaanza kuita nikaitoa simu yangu mfukoni na kukuta ni Joseph ndio anapika, nikaipokea na kuiweka sikioni.
“Jose”
“Naam kaka”
“Nipe ripoti”
“Ebwana huyu mtu uliye niambia niweze kumtafuta anatokea katika kikosi cha Al-Shabab na kwa sasa yupo hapo mkoani Tanga”
Maneno ya Joseph yakanifanya nisimame kwenye kiti na kuanza kutembea kusogea pembeni ili nizungumze vizuri na Joseph.
 
“Unasema Al-Shabab?”
“Ndio tena huyo ni mpelelezi wa Al-Shabab. Kwani kuna kitu gani kilicho tokea”
Nikamtazama mama alipo kaa kwenye kiti akiendelea kula, akanitazama nikatabasamu na sikuonyesha sura yoyote ya wasiwasi. Mama naye akatabasamu na kuendelea kula.
“Kuna ishu imetokea nyumbani kwa bi mkubwa. Kuna nyaraka zimeibiwa na ni muhimu sana, si unajua Magu kesho kutwa anakuja Tanga?”
“Ndio nalitambua hilo na makachero wamesha tumwa tangu majuzi”
“Sasa wanalitambua juu ya hawa makachero wa Al-Shabab?”
“Hapana wewe ndio wa kwanza kulitambua hili, hata mimi nimeshangaa sana”
 
“Ok poa nitumie picha yake, na full detail zake”
“Poa dakika moja”
“Na usimuambie yoyote, hapa nahisi kuna mtandao mkubwa wa viongozi wanajihusisha na watu hawa”
“Sawa kaka”
Nikakata simu na kurudi kwenye kiti. Mama akala kipande cha kuku licho kuwa amekishika mkononi, alipo kitafuna na kukimeza, akaniuliza swali.
“Yaani hadi sasa hivi unaogopa kuzungumza na wakwe zangu mbele yangu?”
“Ahaa mama mimi sina mchumba”
“Wewe Dany ninaye kujua, labda si mimi. Kesi za kipindi upo sekondari, una tembea na vijisichana vya watu unahisi sizikumbuki?”
Ikanibidi kutabasamu tu kwa maana mama amesha wahi kunifumania sana na wasichana kipindi cha uvulana wangu, na anatambua kwamba mwanaye nina nyote ya kupendwa na mabinti.
 
“Mama nikuulize kitu tena”
“Niulize”
“Yudia umemjuaje juaje?”
“Mmmmm, ameniletea rafiki yangu mmoja hivi amemtoa huko Lushoto”
“Ahaaa huyo rafiki yako ni nani?”
“Ninafanya naye kazi hapo Jiji”
“Ok, na je anasema Yudia ametokea katika family gani?”
“Baba yake na mama yake ni wakulima wa nyanya na viazi. Amefeli form four amekuja nyumbani kwangu basi ananisaidia kufanya fanya kazi”
“Ok, na ana muda gani pale nyumbani?”
“Kama miezi mitatu, huu unakwenda mwezi wa nne”
“Tangu aje nyumbani mgogoro wa wewe na huyo meye ulisha anza?”
“Yaaa ulisha anza. Mbona unaniuliza maswali mengi hivyo kuna kitu gani kinacho endelea?”
“Ni mapema sana kukizungumza kwa leo ila nitakuhitaji usirudi nyumbani leo hadi nizipate hizo nyaraka”
“Dany”
 
“Ndio mama hakuna usalama kabisa pale nyumbani, kuanzi hadi hapa ninapo zungumza, itabidi ubaki hapa hotelini hadi nitakapo pata nyaraka”
Nikaanza kumuona mama jinsi alivyo jawa na woga, kiasi kwamba hata kula akaacha kabisa. Akashusha pumzi huku akinitazama wakati huu, aliweza kunielewa kabisa kwamba kitu ninacho kizungumza kinatakiwa kwenda kama nilivyo sema.
“Na yule mtoto wa watu atabaki peke yake pale nyumbani?”
“Muache abaki peke yake ni mtu mzima anaweza kujilinda”
“Ila Dany kama kuna kitu kibaya kinacho endelea ni vyema ukanieleza”
Kabla sijamjibu mama kitu chochote macho yangu, yakawa yanamuangalia muhudumu wa kiume anaye kuja eneo nililo kaa na mama, huku mama akiwa amempa mgongo muhudumu huyo aliye beba sahani pana huku juu yake ina chupa ya whyne pamoja na glasi mbili na chini ya sahani hiyo kuna kitaulo kidogo cha kufutia mezani, ila ndani ya kitaulo kwa umakini sana nikaona bastola, iliyo fungwa kiwambo cha kuzuia risasi, kikiwa kimefungwa. Pasipo kusubiria aweze kutekeleza lengo ambalo linamleta mezani kwetu nikachomoa bastola yangu kiunoni na kumpiga risasi mbili za miguuni na kumfanya anguke, huku chupa, sahani, glasi na bastola yake vikiangukia pembeni. Ila mlio wa risasi bastola yangu ambayo sijaifunga kiwambo cha kuzuia sauti, ukawafanya watu walio kuwepo katika eneo hilo kutawanyika kwa woga, huku mama akiwa ameshikwa na bumbuazi akinitolea macho.

   AISIIIII……….U KILL ME 18

Nikanyanyuka kwa haraka kwenye kiti nilicho kalia huku nikitembea kwa tahadhari bastola yangu ikiwa mikononi nikimsogelea muhudumu huyo. Nikachuchumaa, na kumgeuza kwa maana amelala kifudifudi. Nikamkuta muhudumu huyo akiung’ata ulimi wake kwa ajili ya kujiua. Nikajaribu kumzuia kujiua ila nikawa nimesha chelewa kwa maana tayari alisha ng’ata kipande cha ulimi wake na kukimeza na kusababisha damu nyingi kumwagika umdonini mwake.
Nikakumbuka maneno ya mwalimu wangu kipindi nipo chuoni nina somea maswala ya upelelezi, aliniwahi kuniabia kwamba maadui wapo wa aina nyingi, ila endapo maadui hao wanapo jikuta wanakaribia kuingia mikononi mwa askari, mbinu yao ya kwanza kuifanya ni kuung’ata ulimi na kuumeza, kitu kinacho peleka wao kufa haraka pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote ili kuto kutoboa siri.


Nilipo ona hivyo nikaachana naye na macho yangu yakawa na kazi ya kutazama maeneo mbali mbali ya hoteli hiyo ili kuweza kuona kama kuna maadui wengine wapo katika eneo hilo. Nikarudi sehemu alipo mama, na kumshika mkono na kumnyanyua kwenye kiti alicho kali.
“Mama tuondoke hii sehemu sio salama”
“Dany ni nini umefanya?”
“Mama tuondoke”
Nilimshika mama mkono na kuanza kutoka naye katika eneo hili, huku bastola yangu ikiendelea kuwa mkononi na muda wote nikiwa makini sana kwa kumtazama kila mtu aliyopo mbele yangu na muda mwengine nikalazimika kugeuka nyuma na kuangali kama kuma mtu ambaye anaweza kufanya shambulizi. Nikiwa hapo nikakutana na askri waona linda hoteli hii, wote ambao ni wanne wakaninyooshea bunduki zao na kuniomba nisimame na niweke bastola yangu na mikono yangu niiweke juu.
Kutokana ni moja wapo ya sheria, pale unapo kunata na kitengo kingine cha ulinzi ambacho hawakufahamu wewe ni nani, ikanilazimu kuweka bastola yangu chini na kuinyoosha mikono yangu juu kwa haraka huku mama yangu akiwa amesimama pemebeni.


“Jamani huyu ni askari”  
Mama alizungumza kwa kunitetea, kutokana ni mkuu na anajulikana hata kwa askari hao, kidogo wakaanza kuniamini ila bado mitutu ya bunduki zao wakiwa wamenielekezea.
“Muheshimiwa hujaumia?”  
“Sijaumia huyu ni kijana wangu”
Kwa haraka ikanibidi kutoa kitambulisho changu ambacho popote ninapo kwenda huwa ninakibeba, kwa ajili ya kujilinda pale nitakapo kamatwa. Askari hao walipo ona kitambulisho changu wakaniamini na kuniomba msamaha. Nikaokota bastola yangu, kisha nikasimama huku ninawatazama kwa macho makali yaliyo waogopesha hata askari hao ambao ni wakampuni ya ulinzi hapa Tanga. Tukiwa hapo tukasikia kelele kwenye moja ya chumba na akatoka msichana mmoja ambaye ni muhudumu huku anakimbia. Nikamuwahi kwa kumdaka na kumziba mdomo asipige kelele.
“Kuna nini?”
“Luka kafaaa, wamemuua Luka”
Msichana huyo alizungumza huku akilia, ikatubidi mimi na askari hao kwenda katika chumba hicho ambacho anadai ndipo alipo uwawa huyo Luka. Tulipo ingia, tukakuta mauaji ya kikatili sana kwa maana kichwa cha mfanyakazi huyo kimekatwa na kuwekwa juu ya meza huku kiwili wili chake kikiwa kmelazwa sakafuni na akiwa amevuliwa nguo zote na kubakiwa na boksa.


“Huyu ni nani?”
“Ni muhudumu wa hii hoteli”
Hapo ndipo nikapata picha kwamba yule muhudumu niliye mpiga risasi, si muhudumu wa hoteli hii bali alimuua huyu Luka kisha nguo za muhudumu akavaa yeye. Kwa haraka nikaanza kukagua chumba hicho kuweza kupata japo kijiushahidi, kwa bahati nzuri nikapata waleti iliyo angushwa na ipo chini ya kitanda. Nikaifungua na kukutana na passport y ya kusafiria ya jambazi niliye muua, nikakuta ni raisi wa Somalia na ameingia nchini Tanzania siku tano zilizo pita, nikakuta vikaratasi vingine vingine vikiwa vimeandikwa lugha ya kiarabu.
“Pigeni simu polisi”
“Tayari imesha pigwa”
Nikatoka katika chumba hicho na kurudi mapokezi ambapo nikamkuta mama akiwa amekaa kwenye moja ya kiti ametulia akionekana ana mawazo mengi sana.
“Mama tuondoke”
“Kuna nini huko chumbani?”
“Kuna muhudumu mmoja ameuwawa na yule jamaa niliye mpiga risasi”


“Mungu wangu, sasa kwa nini wamefanya hivi?”
“Hao wapo kwa ajili yako wewe”
Mama akanishangaa huku akiwa kama haamini kitu ambacho ninakizungumza ila huo ndio ukweli halisi ambao tayari nimesha ugundua. Tukaingia kwenye gari na kuondoka eneo hilo, tukiwa njia tukapishana na gari za polisi mbili zinazo elekea eneo la hoteli hiyo zikiwa katika mwendo wa kasi.
“Mama hapa inabidi nikupeleke kwa baba mkubwa Eddy ukakae huko kwa muda”
“Sawa”
Mama alijibu kiunyonge tayari woga ulisha mjaa. Nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari huku muda wote nikiwa makini sana katika hilo. Tukafika nyumbani kwa baba mkubwa ambapo ni maeneo ya Nguvumali karibu na ikulu. Nikapiga honi ambapo mlinzi akafungua geti na tukaingia, gari nikalisimamisha maeneo ya maegesho ya magari. Nikashuka na mama naye akashuka kwa bahati nzuri tuliweza kumkuta baba mkubwa akiwa amekaa kwenye moja ya bustani yake akijisomea vitabu. Tukatembea hadi eneo alilopo, alipo niona akatabasamu kwa maana ni muda mrefu sana hatujaonana.


“Shikamoo baba”
“Marahaba, Dany siku hizi huji kabisa nyumbani kwangu”
“Shemeji shikamoo”
“Marahaba shemeji, karibuni”
“Asante”
“Baba mkubwa si unajua mizunguko yetu hii ya kibiashara kidogo inatuweka bize sana”
Nilizungumza hivyo kutokana mtu pekee anaye ifahamu kazi yangu ni mama yangu mzazi tu, hadi mdogo wangu wa kike alifahamu hilo.
“Ahaa uwe unakuja hata kututembelea, au unataka kusikia kwamba baba yako mkubwa nimekufa ndio uje?”
“Hapana baba leo nimeamua kuja na mama, tutalala huku”
“Ahaa, Shemeji ni kweli anayo yazungumza mtoto hapa?”
“Ni kweli shemeji, alikuja juzi leo basi analalamika anataka kuja kulala huku”
“Karibuni sana, tena mama yako mkubwa naye ametoka Marekani jana yupo huko ndani na wanae”
“Ahaa basi ngoja nikawaone”
Nikanyanyuka na kumuacha mama na baba mkubwa, nikaingia ndani bila hata kubisha hodi nikamkuta mama mkubwa na mabinti zake wawili mapacha ambao nimewapita umri wakipiga stori sebleni, walipo niona kwa haraka wakanyanyuka na kunikimbilia huku wakiwa na furaha.


“Kaka Danyyyy”
Xaviena na Xaviela ambao ni watoto wa baba mkubwa Eddy, wakanikumbatia huku wakiwa na furaha sana kwa maana ni kipindi kirefu sijaonana nao.
“Jamani kaka Dany umetususa, hupigi simu wala kuwasiliana na sisi?”
“Xaviena si unajua maisha mdogo wangu, maisha ni magumu”
Nilizungumza huku wakiwa wamenishika mkono na kueleka nao kwenye masofa yaliyopo hapo sebleni. Nikamsalimia mama mkubwa ambaye anaitwa Rahma.
“Marahab, Dany umekua haraka haraka?”
“Msosi mama”
“Hata mimi naona, vipi umekuja na mama?”
“Ndio nimekuja naye wapo hapo nje na baba mkubwa”
“Wacha nikamsalimie, tena nilikuja na zawadi yake kutoka Marekani”
“Ya kwangu ipo wapi?”
“Mmmm wewe umesaulika na kukaa kwako kimya”
Mama mkubwa akatoka na kuniacha nikiwa nimekaa na wanae hawa mapacha wanao fanana sana na kama mtu hujawazoea basi utawachanganya sana. Nikaona picha ya Xaviena akiwa amevalia taji la umesi ikiwa imebandikwa ukutani.
“Xaviena umesha wahi kuwa miss kumbe?”
“Ahaaa tena sasa hivi tupo kwenye mikakati ya kugombania umiss Tanzania”


“Wacha weee”
“Ndio”
“Xaviela na wewe?”
“Mimi nipo nipo tu”
“Dany sasa hivi una misuli, kipindi kile ulikuwa kimbau mbau”
“Hahaaa napiga tizi gym sasa hivi”
“Nichukue basi na mimi nikapige tizi Gym”
“Xaviela unataka kupiga gmy?”
“Yaa mbona nimesha anza”
“Waoo basi, nipo Tanga tutawasiliana”
“Tupatie basi namba yako ya simu”
Nikatoa simu yangu na kuanza kuwatajia kila mmoja akaingiza namba yangu kwenye simu yake na kila mtu akanipatia simu yake. Kabla sijaingiza simu yangu mfukoni, ikaanza kuita na anaye piga ni K2, nikanyanyuka na kueleka chooni kuzungumza naye.
“Baby mbona kimya jamani?”
“Honey si unajua nyumbani huku, nipo na mama yako mkwe basi nakosa hata muda wa kupiga simu”
“Wee upo na mama mkwe alafu unaongea na simu mbele yake?”


“Hapana kwa sasa nimesogea pembeni kidogo”
“Ahaa, nimepata taarifa muda huu, nasikia tanga kuna mauaji yametokea kwenye hoteli moja waiita…….”
“Wanaiitaje?”
“Ahaa nimesahau jina nikikumbuka nitakuambia. Ila kuwa makini mpenzi wangu, hapa nilipo yaani nina kukumbuka, natamani hata uje”
“Usijali nitakuja siku si nyingi”
“Ila vipi kidonda?”
“Nimechomwa sindano za kutosha”
“Pole mwanya ehee”
“Asante honey”
“Poa honey baadae”
“Sawa baby I love you”
“I love you too honey”
Nikaka simu, kitendo cha kufungua mlango nikakutana na Xaviela na Xaviena mlangoni wakiwa wamesimma, kumbe muda wote walikuwa wananisikiliza.
“Dany unamchumbaaaa”
Xaviela alizungumza kwa kunitania huku akitabasamu. Wote wakaanza kucheka na kunifanya nicheke.
“Sasa ulikuwa unakimbia nini, si ungezungumza mbele yetu tumjue wifi yetu ni nani?”


“Acheni hizo bwana”
“Tunamuambia baba”
“Weee Xaviena musimumbie mzee bwana, mbona unataka kumwaga mchele mbele ya kuku wengi”
“Kama ni hivyo mpigie tena mchumba wako tuzungumze naye”
“Ahaa mbona munataka kunizinguza wadogo zangu”
“Kubaliana na sisi mpigie, au tumueleze mama mdogo na baba kwamba Dany una mchumba”
Nikashusha pumzi haraka hara huku nikiwatazama, kusema kweli nina wafahamu Xaviela na Xaviena, huwa wakilikazania jambo huwa hawapendi kuliachia, lipite kirahisi. Nikakumbuka nina namba ya Mariam, kwa haraka nikaitafuta na kumpigia, kwa bahati nzuri simu ya Mariam ikaanza kuita. Sikutaka wazungumze na K2 kwa maana kwanza sauti yake dhairi inaonyesha ni mtu mzima pili ana wivu sana na mimi kuliko hata mume wake wa ndoa. Maria akapokea simu kitu cha kwanza aliuliza mimi ni nani.
“Dany”
“Ohoo jamani honey za safari?”
Macho ya Xaviela na Xaviena yakawa yananitazama kwa umakini kwa maana wanahisi kama nina watania, ilinibidi kulipotezea swali la Mariam.
“Wifi zako hapa wanataa kukusalimia”
“Waoo wifi zangu, wape simu”
“Poa, nani aanze kuzungumza”
“Mkubwa kwanza”


Xaviela alizungumza huku akiichukua simu yangu na kuanza kuzungumza na Mariam, alimuhoji maswali mawili matatu kisha akamuachia Xaviena, ambaye naye maswali aliyo uliza mwenzake ndio aliyo uliza yeye, kisha akanirudishia simu.
“Dany mbona wifi zangu sauti ni kama mtu mmoja?”
“Mapacha hawa”
“Weeee, ndio maana sauti zao zinafanana”
“Ndio, sasa ngoja nitakupigia baadae”
“Sawa honey”
Nikakata simu na kuwatazama Xaviela na Xaviena
“Mume ridhika sasa?”
“Sanaaa”
“Twendeni nje, kuna sehemu nataka kwenda mara moja”
“Unataka kuondoka hivyo?”
“Hapana leo nalala huku”
“Kweli?”
“Ndio”
Nikatoka nao nje, tukaelekea kwenye bustani walipo kaa wazazi huku nikiwa nimewashika mikono. Tulipo fika wakamkumbatia mama kisha wakaka kwenye vitu vya pembeni. Nikawaaga na kuwaeleza kuna wafanya biashara ninakwenda kuonana nao, wote wakakubaliana name, ila mama pekee ndio anajua ni kazi gani iliyopo mbele yangu ambayo ni kuhakikisha ninazipata nyaraka zote zilizo ibiwa chumbani kwake.


Nikaingia kwenye gari la mama na kuondoka, safari hii nikielekea moja kwa moja katika mtaa wa nyumbani kwetu nikaliacha gari la mama kwenye moja ya baa inayo itwa Mwika, kisha nikaanza kutembea kwa miguu hadi eneo la karibu kabisa la nyumbani kwetu. Kigiza tayari kilisha anza kutawala angani nikaka kwenye moja ya nyumba iliyopo karibu na nyumba yetu, lengo langu ni kutaka kujua kama Yudia yupo au laa. Haukupita muda sana taa za nyumbani za nje ya nyumba zikawashwa, nikatambua kwamba yupo, ila nikiwa hapo nikaona gari nyeusi ikisimama nje ya geti. Akashuka jamaa mrefu kiasi na kuingia ndani humo na gari hiyo ikaondoka. Gari ilipo potea mbele ya macho yangu nikaanza kutembea kwa mwendo wa kasi hadi getini, nikachungulia kwenye kijiuwazi kidogo cha getini nikamuona jamaa huyo akizungumza na Yudia, ambaye anaonekana kufahamiana na mtu huyo.


“Ni upumbavu mulio fanya, munge muua. Sasa hii ni nafasi ya mwisho jifiche kwenye hiyo bustani wanarudi muda si mrefu. Sasa ole wako ufanye makosa nitakuua”
Maneno ya Yudia yalinifanya niishiwe nguvu kabisa kwa maana yale mawazo mabaya niliyo kuwa nina muwazia kumbe ni kweli na yeye ndio anahusika na mpango wa mauaji ya mama, nikatamani kuingia ila nilihisi kushindwa kabisa kwa maana jamaa huyo amejificha katika uwa kubwa lililopo kwenye bustani iliyopo karibu na getini na yoyote atakaye ingia ndani hapo ni rahisi kumuona ila mtu anaye ingia si rahisi kuweza kumuona muuaji huyo.
                                                                                       ITAENDELEA
   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts