Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 37 na 38 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 37 na 38 )

Written By Bigie on Monday, March 12, 2018 | 10:00:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA       
“Umechukua kila kitu?”
“Ndio ila kuna hii karatasi hapa ina namba ya huyo bosi wao wa majambazi, pamoja na namba nyingine za wezake Jumaa.”
“Hembu nipatie”
Asma akanipatia karatasi hiyo iliyo kunjwa vizuri, nikaikunjua na kutazama namba za simu zilizo andikwa humo hususani namba ya huyo bosi wa Jumaa, sikuamini macho yangu kuikuta nama ya K2 ambayo ninaifahamu vizuri hata kama nikiwa sina simu. Nikahisi sio yenyewe labda nimekosea, nikamuomba simu Asma, akanikabidhi, nikajaribu kuingia katika upande wa kutuma pesa wa Tigo pesa, nikaiingiza namba hiyo ya simu na kiasi ninacho hitaji kutuma, yakatokea maandishi kutoka katika hudumu hii yanayo someka ‘Ingiza namba yako ya siri kutuma pesa kwa K2 kiasi ni shilingi elfu kumi’. Nikajihisi nguvu zikiniishia huku taratibu nikikaa kwenye sofa, huku mapigo ya moyo yakianza yakinienda kasi sana.

ENDELEA   
“Vipi Dany mbona umeogopa hivyo?”
“Hapana, nahitaji nikuondoe usiku huu huu”
“Mimi sina tatizo nakusikiliza wewe”
Sikuwa na haja ya kuingia bafuni na kuoga zaidi ya kuanza kuvaa nguo zangu kwa haraka sana, kitu ambacho ninahofia ni Asma kuziona bastola zangu jambo ambalo silihitaji alifahamu kwa muda huu. Nilipo maliza kufaa nguo, nikatoka nje ya nyumba yetu ikiwa tayari ni saa nne usiku. Nikaelekea kwenye sehemu wanapo egesha taksi za kukodi, nikamuita dereva mmoja nikaelekea naye hadi nyumbani. Nikaingia ndani huku nikiwa makini sana. Nikamkuta Asma akiwa amekaa kwenye sofa ananisubiria,
 
“Una baibui?”
“Ndio”
“Lipo karibu uweze kulivaa?”
“Ndio”
Haya litoe fasta fasta na ulivae”
Asma akafanya kama nilivyo mueleza, begi lake la nguo nikaliweka kitandani, nikalifungua kwa haraka, akaanza kuchambua nguo huku akitafuta basibui lake, alipo liona, akavua dera lake kwa haraka, na kuanza kuvaa baibui lake hilo lenye kitambaa kinacho ificha sura yake. Nikamsaidia kurudisha nguo zake kwenye begi haraka haraka kisha nikachungulia kwenye kordo sikuona mtu, tukatoka huku nikifunga chumba changu na kuanza kutembea kwa mwendo wa umakini sana huku macho yangu yote yakiwa mbele na Asma akinifwata kwa nyuma. Tukafanikiwa kutoka nje kabisa ya nyumba pasipo kuonekana na mtu anaye tufahamu ila Asma ni ngumu zaidi kufahamika kwani sura yake ameificha kwa kitambaa hicho cha baibui kilicho mbakisha macho wazi.
 
Tukaingia kwenye taksi, nikaanza kumpa dereva maelekezo ya wapi atupeleke. Safari ikaanza huku muda wote Asma akiwa amenishika mkono wangu wa kulia, akiwa na wasiwasi mwingi sana usoni mwake. Tukafika katika hoteli ya MK, iliyopo kwenye eneo la Mbezi Beach. Nikawa wa kwanza kushuka kwneye taksi na kumuacha Asma ndani ya taksi, nikaeleka hadi mapokezi, nikalipia chumba kimoja cha gorofani kisha nikarudi kwenye taksi.
“Ngoja nikusaidie begi”
Nilizungumza huku nikilishika begi la Asma.
“Kaka haujanilipa bado”
“Ohoo sorry ndugu yani nimejisahau bei gani?”
“Elfu ishirini na tano”
Nikanipapasa kwenye waleti yangu na kukuta shilingi elfu kumi, jambo lililo anza kunipa wasiwasi, kwani hoteli niliweza kulipia kwa kadi ya malipo ambayo ninatembea nayo popote niendapo.
“Vipi?”
“Nimepungukiwa elfu kumi na tano”
“Ngoja”
Asma akafungua kipochi chake na kutoa shilingi elfu shirini na tano na kumkabidhi dereva huyo aliye tuaga na kuondoka. Tukaeleka ndani ya hoteli, tukaingia kwenye lifti na kuelekea gorofa ya tano. Tukaingia kwenye chumba nilicho kikodisha. Nikafunga kwa ndani na Asma akaanza kuvua baibui lake kisha akanirukia na kunikumbatia kwa nguvu huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Ohoooo Dany nakuomba usije ukaniacha, nimefanya haya yote kwa ajili yako”
 
“Siwezi kukuacha Asma, natambua ni kipindi gani ambacho unapitia, ninakuahidi nitakulinda katika maisha yangu yote”
Nilizungumza kwa hisia kali na kumfanya Asma azidi kunikumbatia kwa furaha na hisia nzito, tukaachiana na kuanza kunyonyana midomo yetu safari hii, kila mmoja akajiachia na kuwa huru kwa mwenzake kwa maana tumesha jihalalisha mioyoni mwetu kuwa wapenzi. Kusema kweli Asma ni mzuri na ana vigezo vyote vya kuwa mwanamke wa ndoa.
Akaanza kunivua nguo na kubaki kama nilivyo zaliwa. Tukaingia kwneye mzunguko mwengine wa kupeana raha na burudani. Haikuwa mechi kama ya kwanza ila hii ikawa ni zaidi ya mechi ya kwanza. Tukapeana utamu halisi wa mume wa mke huk u kila mmoja akiwa anamwaga sifa kwa mwenzake, tukamaliza kwa wakati mmoja huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa moyoni mwake.
“Una njaa?”
“No dady yaani nipo na wewe wala sitamani kula, uwepo wako kwangu ndio kila kitu”
“Kweli?”
“Ndio Dany, sikutaka kuziweka hisia zangu karibu yako kuogopa kuniona mimi ni malaya au mtu wa aina gani ila kusema kweli ninakupenda tena sana. Wewe ndio mwanaume uliye ifahamu thamani yangu”
 
“Kivipi?”
“Kama ile siku nilipo kuwa ninakimbwizwa na Jumaa, ulinisaidia na ingekuwa si kufanya hivyo sidhani kama leo hii ningekuwa hai, kwa maana aliniambia ataniua na kunizikia ndani kwake”
“Mmmm ivi ulikana kutana vipi na Jumaa”
“Kipindi nina umri wa miaka kumi na saba, wazazi wangu walifariki huko kijijini kwetu Songea. Nilibaki mimi na dada yangu ambaye alikuwa ameolewa na jamaa mmoja muendesha magari makubwa ya mizigo. Sasa yule shemeji yangu, rafiki yake mkubwa ni Jumaa na jinsi walivyo kuwa wanakuja nyumbani kwa dada pale, akatokea kunipenda na kuamua kunileta mjini Dar es Salaam, kuanzia hapo sijawahi kurudi tena Songea”
Asma alizungumza katika hali ya unyonge sana, taratibu nikamsogeza karibu yangu na kumkumbatia. Kutokana na uchovu mwingi ambao umenijaa, usingizi mzito ukanipitia wala sikufahamu Asma amelala saa ngapi. Alfajiri na mapema, nikasikia sauti ya Asma akainiamsha.
“Mmmmm”
“Amka honey kumekucha”
“Saa ngapi sasa hivi?”
“Ni saa mbili”
Nikakurupuka kitandani na kukaa kitandani, hadi Asma mwenyewe akanishangaa. Yamebaki masaa mawili tu ya kijana niliye panga naye ahadi ya kuja kunichukua nyumbani kwangu Sinza kutimia.
 
“Mbona umestuka hivyo?”
“Kuna mtu nimepenga kuonana naye nyumbani mida saa nne”
“Sasa utaniacha mimi hapa peke yangu?”
“Ndio baby, ningeomba nikuache hadi mchana kisha tutawasiliana”
“Sasa Dany ndio unataka kunifanyia nini mimi, umenitoa kule nikihisi kwamba nitakuwa salama kumbe na wewe unataka kuwa kama huyo Jumaa”
Asma alizungumza huku machozi yakimlenga lenga.
“Sio hivyo mpenzi wangu, ni swala la kawaida nina kwenda kulishuhulika, niamini kwamba sinto weza kukuacha wala kukutelekeza. Nakwenda kuandaa nyumba ya sisi kuishi, nilitaka kuliweka hilo kama siri ila inalazimika mimi kuweza kulizungumza hilo”
“Nyumba ya kuishi?”
“Ndio Asma, niamini mimi nitarudi saa saba naamini nitakuwepo  hapa”
Asma akanitazama vizuri usoni mwangu, kile ninacho kizungumza ni kweli nina kimaanisha, tukashuka wote kitandani na kwenda bafuni, tukaoga kisha tukarudi chumbani, nikaanza kuvaa nguo zangu haraka haraka, kitu kinacho nifanya niweze kuwahi hivi ni kutokana kwamba sina simu ya mawasiliano. Nikachukua mkonga wa simu ya mezani, nikaminya namba kadhaa na kumpigia muhudumu wa mapokezi.
“Nakuomba ufike chumba namba 226”
“Sawa”
Nikarudisha mkonga wa simu sehemu ulipo na kujiweka sawa suruali yangu.
 
“Umemuita muhudumu wa nini?”
“Nahitaji kumuachia maagizo ya kuongeza muda wa kukaa hapa hotelini pamoja na chakuka cha asubuhi na mchana”
“Sawa”
Mlango ukagingwa nikapiga hatua hadi mlangoni, nikafungua na kukutana na muhudumu ambaye jana usiku niliweza kumkuta mapokezi.
“Ingia tu ndani”
Akaingia, akamsalimia Asma aliye kaa kitandani amejifunga taulo jeupe.
“Huyo hapo ni mke wangu, nahitaji muweze kumpa huduma zote atakazo zihitaji, pia nahitaji kuweza kuongeza muda way eye kukaa hapa”
“Hilo halina tatizo, ila kwasababu mimi ndio ninajiandaa kutoka, basi nitamuachia mwenzangu mwengine maagizo hayo”
“Ok, kama hutojali, ninakuomba tuongozane hadi mapokezi nikayatoe hayo maagizo na kila kitu nitalipia kwa kadi yangu ya malipo”
“Sawa kaka”
Nikapiga hatua hadi kitandani na kumbusu Asma mdomoni, kisha tukatoka chumbani humu nikiwa nimeongozana na muhudumu.
“Kaka umepata mke mzuri”
“Asante”
“Kaka yangu kama kweli ni mke wako, pale unatakiwa kutulia, ana kila sifa ya kuwa mwanamke wa mtu”
“Kwa nini unazungumza hivyo?”
“Mimi japo ni mwanamke ila nina wajua wanawake wezangu, wengi tuliopo hivi sasa tunapenda pesa, ila huyu ni msikivu sana”
 
“Asante”
Tukafika mapokezi na kumkuta dada mwengine, nikampa maelelezo yote kisha nikalipia muda wa chumba changu kuongezewa muda wa siku nyingine, nikatoka nje ya hoteli nikapanda pikikipi iliyo nipeleka hadi kwenye moja ya benki, nikatoa kiasi cha pesa cha kutosha na kuelekea nyumbani kwangu nilipo pangisha chumba kimoja. Nikamlipa dereva pikipiki pesa yake na kuingia, ndani. Nikiwa kwenye kordo nikakuta mama Maria, Mariam na Jumaa wakiwa wamesimama huku wakionekana kuzungumza mada fulani.
“Dany”
Mama Mariam alipo niona akaonekana kufurahi sana, ila akajizuia kuja kunikumbatia. Hata Mariam mwenyewe akanikonyeza huku akiachia tabasamu  pana.
“Habari za hapa?”
“Salama za safari?”
“Safi tu vipi mbona mumesimama kuna nini?”
Niliuliza swali huku nikijifanya kama sielewi ni kitu gani ambacho kinaendelea.
“Kaka mke wangu ametoroka, nimerudi nimekuta amechukua kila kilicho chake, sijui atakuwa amekwenda wapi?”
Jumaa alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge, nikajifaya kushangaa, huku nikisikitika ila kika ninacho kifanya hapa ni kumng’ong’a  Jumaa kwani mimi ndio kisababishi cha mkewe kuondoka katika maisha yake huku nikijiapia moyoni mwangu kwanba hato kuja kumpata Asma hadi kufa kwake.
 
“Sasa kuna utaratibu wowote mumeuchukua, kama wa kuwauliza majirani, marafiki zake hata ndugu zake?”
“Nimefanya hivyo ila kila mmoja anadai kwamba hajafika huko ninapo paulizia?”
“Mulikuwa na ugomvi kwani?”
Jumaa akabaki kimya huku akinitazama machoni, swali hilo hakulijibu kabisa mbele yangu kwa maana anatambua kuna siku nilisha wahi kumpa onyo kali kama akifanya ujinga wa kumpiga tena mke wake basi nitamshuhulikia.
“Au unaweza kwenda kutoa ripoti polisi?”
“Hapana siwezi kwenda polisi, nitamtafuta hivi hivi kimya kimya hadi nitampata”
Baada ya Jumaa kuzungumza mazungumzo hayo akageuka nyuma na kuingia ndani kwake na kuufunga mlango kwa nguvu. Sote tukabaki tukiwa tumeyatumbua macho yetu, hakuna ambaye aliweza kuchagia lolote katia wazo la Jumaa.
“Za huko kwenu Tanga?”
“Safi tu za hapa?”
“Safi”
Mama Marim dhairi furaha yake iliweza kuonekana hadi Mariam akakosa uhuru wa kuzungumza.
“Mbona hujatujia na zawadi?”
“Ahaa nimekuja mara moja, zawadi hakuna wapendwa”
“Mmmmm Dany na wewe”
“Kweli”
 
Nikaingia chumbani kwangu na kuwaacha Mariam na mama yake kwenye kordo, nikafunga kwa ndani huku nikiwa sihitaji mtu wa aina yoyote kuweza kuingia ndani humu. Niakaanza kuchumbua nguo za kuvaa kabatini huku bastola zangu nikiwa nimeziweka juu ya meza. Nilipo pata moja ya suti ninayo ipenda, nikaivaa, kila bastola yangu, nikaificha sehemu ambayo ninapenda kuificha. Nikaichukua karatasi aliyo nipatia Asma jana usiku  yenye namba za majambazi wote wakuu wakuu, huku kiongozi wao akiwa ni K2. Nikaiweka vizuri kwenye waleti yangu sehemu ambayo si rahisi kwa mtu kuweza kuiona. Nilipo hakikisha nipo tayari nikapiga hatua hadi mlangoni kabla hata sijashika ufunguo, ukagongwa na kujikuta nikijizuia kuufungua kwa muda.
“Kaka Dany”
Niliisikia sauti ya Mariam na kujikuta nikufungua, na kumkuta akiwa amesimama mlangoni.
“Kuna mgeni wako nje?”
“Yupoje?”
“Yupo kwenye gari ni kijana mdogo mdogo na mpole kiasi”
“Ok muambie ninakuja”
Nikaurudishia mlango nikamuacha Mariam kuondoka mlangoni kwangu, kisha na mimi nikatoka. Nikaufunga mlango wangu, kabla sijapiga hatua nikamuona Jumaa akitoka chumbani kwake kwa haraka. Akanitazama kwa macho ya mashaka kisha akanisogelea huku akwiwa ni mtu wa kuhitaji kufanya jambo fulani dhidi yangu.
“Vipi?”
“Umempeleka wapi mke wangu”
Jumaa alizungumza kwa sauti nzito iluyo jaa hasira kali huku macho yake yote akiwa amenikodolea mimi jambo lililo mstusha sana moyoni mwangu.
                                                                                         
                       AISIIIII……….U KILL ME 38

“Kivipi, sijakuelewa kuhusiana na swali lalo?”
“Ninazungumza kiswalihi sahihi na kinacho eleweka, umempeleka wapi mke wangu?”
Sikutaka kuonyesha wasiwasi wowote usoni mwangu wala kuhofia kwa kile anacho kizungumza Jumaa kwa maana nimesha elewa ni kitu gani anacho kifanya alicho kiziba nyuma ya pazia kwa kujifanya mjinga kumbe ni mtu hatari.
“Na mimi nina zungumza kiswahili fasaha, sijui unazungumza nini?”
 
“Jana kuna mtu amekuona unatoka humu ndani na mwanamke amevaa baibui akiwa ameshika begi na ninatambua kabisa Asma naye ana baibui jeusi na ameondoka na begi?”
“Ohooo hivi kila mtu akiwa anatoka humu ndani ni Asma. Fungua akili yako ndugu, huwezi kuishi na mwanamke anaye mtesa, unaye mnyanyapaa na kumuumiza. Leo ndio ninarudi kutoka safarini na wala jana sikuwa hapa. Huyo aliye niona nenda kaumuulize tena aliniona wapi kama yeye hausiki katika swala hilo”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimkazia macho Jumaa, akabaki akiwa amenitumbulia macho ya kuniamini kile ninacho kizungumza. Nikakatoka na kumuacha Jumaa kwenye kordo nikiamini kwamba ana maswali mengi ambayo anajiuliza kichwani mwake. Nikaingia kwneye gari nikasalimiana na dereva na safari ikaanza ila kichwani mwangu wasiwasi mwingi ukawa umenijaa.
 
‘Lazima nimlinde Asma kwa hali yoyote’
Niliwaza kichwani huku safari ya kuelekea Masaki ikiendelea. Dereva akasimama kwenye moja ya jumba lenye geti kubwa na jeusi. Nikataka kumuuliza kwamba hii sehemu anayo nilete ndio aliopo agizwa au amekosea. Ila nikaa kimya kwa maana sikuhitaji kuwa na papara nisije nikaonekana mshamba wa mjini. Geti likafunguliwa na mlinzi wa getini, taratibu gari likaingia na kusimama kwenye maegesho yaliyopo katika eneo hili, ila kitu kilicho nifanya nifahamu kwamba hapa nilipo sio nyumba ninayo takikiwa kukabidhiwa, ni gari moja la kifahari aina ya BMW X6, likiwa katika maegesho haya.
“Kaka tumefika”
“Hapa ndipo ulipo agizwa kunileta?”
“Ndio kaka”
Nikashuka taratibu huku nikitazama madhari mazuri ya jumba hili la gorofa moja kwenda juu. Kijana akatangulia mbele huku na mimi nikiwa ninamfwata kwa nyuma nikiwa na shauku ya kufahamu ukweli wa hili jumba. Tukaingia ndani na kukuta vitu muhimu vya ndani vikiwa vinamaliziwa kupangwa na vijana wawili wanao onekana ni wafanyakazi kutoka ikulu.
 
“Karibu bwana Daniel”
Nilisikia sauti moja ya kike kutoka katika chumba kimoja cha jiko kilichopo karibu na seble hii kubwa. Nikamuona dada mmoja aliye valia suti nyeusi akinifwata sehemu nilipo simama, akanipa mkono na mimi nikampa wa kwangu kama ishara ya kusalimiana.
“Ninaitwa Lutfia Magese, mimi ni mwanasheria wa raisi wa Jamuhiri ya muungano wa Tanzania”
“Asante kwa kukufahamu”
“Nilisha kufahamu tangu jana ila sikupata nafasi ya kuweza kuzungumza nawe. Lengo kubwa lililo niita hapa ni makabidhiano ya hii nyumba kama raisi alivyo ahidi kuwapa zawadi na kuwa watu weke wa karibu sana. Lutfia alizungumza huku akitembele kuelekea jikoni huku nami nikiwa pembeni yake kusikiliza kwa umakini kile anacho kizungumza. Tukaingia jikoni nikaona sururi mbili zikiwa juu ya meza.
 
“Samahani bwana, nilikuwa ninajaribu jaribu haya majiko kama yana fanya kazi kwa maana hii nyumba ni mpya kabisa na kila kitu kimeingizwa leo”
“Unataka kuseme vitu vyote vimeingizwa leo?”
“Yaa tangu saa kumi na moja asubihi mimi pamoja na timu yangu tulikuwa hapa. Kusema kweli raisi amewafanyia kitu kimoja kizuri ambacho kwa uzoefu wangu wa kumjua raisi, tangu akiwa waziri hakuwahi kufanya kitu kama hichi kwa mtu yoyote ila wewe na Babyanka mumepata nafasi nzuri sana”
“Duu, kweli Mungu ni mwema”
“Yaa sasa niendelee na kile kilicho nileta hapa na kukusubiria kwa muda wote huo. Hii nyumba pamoja na vitu vyake vyote ndani vimegarimu zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja na nusu. Ni nyumba nenye vyumba vinne vya kulala na vyote vipo gorofani na ni master room. Chini huku kuna chumba cha mazoezi(GYM). Kuna jiko hili, kuna seble, kuna stoo, na sehemu ya kusomea”
 
“Hati na nyaraka zote nitakukabidhi na utasaini na kuanzia hapo kila kitu kitakuwa cha kwako”
“Shukrani sana”
“Usinishukuru mimi, mtu wa pekee wa kumshukuru ni raisi, kitu kingine ni kwamba ile gari ambayo raisi alipanga kuwapa kila mmoja amegairi na gari hilo ulilo liona hapo nje ni gari lako kuanzia sasa na funguo zake hizi hapa, na kila kitu kimesajiliwa kwa jina lako”
Nikajikuta nikikosa hata kitu cha kuzungumza kwa kushangaa, kila kitu kinacho tokea kwenye maisha yangu nikahisi kama ni ndoto ila ndio uhalisia halisi wa maisha. Lutfia akaanza kunitembeza sehemu moja hadi nyingine ya jumba hili, kuanzia vyumba vya chini hadi gorofani. Nikatamani sana kumpigia mama simu ili aweze kufahamu zawadi niliyo pewa na raisi ila sikuweza kutokana na kutokuwa na simu. 

Baada ya kumaliza kutazama vyumba vya ndani, tukatoka nje na kutembea kwenye maeneo yote ya nyumba, kusema kweli ni nyumba ambayo katika maisha yangu nilikuwa nikiiwaza ila uwezo wa kuweza kuipata nilikuwa sina, ila kwa kazi ya kujitolea maisha yangu kwa ajili ya raisi basi hii ndio zawadi ninayo stahili.
“Hata mwenzako Babyanka naye amepewa nyumba yenye thamani kana hii ila sema yake ina muundo tofauti na hii”
“Gari?”
“Gari mumepewa yanayo fanana”
Katika maisha yangu nimewahi kuwa na furaha ila hii niliyo nayo leo imezidi mara dufu. Tukaingia ndani na kukuta vijana wakiwa wamesha maliza kuweka Tv aya ukutani yenye ukubwa wa inch 55. 
 
“Karibu ukae kwenye sofa hilo”
Nikaka huku nikiwa na shauku ya kuhitaji kufahamu ni nini kinacho endelea, Lutfia akatoa bahasha ya kaki kwenye pochi yake kubwa na kuiweka mezani. Akatoa na kalamu kisha akanikabidhi kalamu hiyo pamoja na hati ya nyumba na gari alizo zitoa kwenye bahasha. Akanionyesha sehemu ya kusaini baada ya kumaliza kusoma ninacho kisoma kwenye hati hii ya nyumba. Hapakuwa na kitu kilicho koswa, kila kitu kipo sahihi kuanzia jina langu. Nikasaini nilipo maliza, Lutfia na yeye akachukua hati hiyo na kusaidi na makabidhiano yakawa rasmi yamekamilika.
“Sasa kila kitu ni cha kwako hapa”
“Shukrani sana”
“Usijali, pia kuna cheki hapa muheshimiwa amenikabidhi niwapatie”
“Muheshimiwa raisi?”
“Raisi wa pili muliye rudi naye kutoka Tanga naye ameona kazi mulio ifanya ya kuyaokoa maisha yake”
Akanikabidhi cheki, nikaisoma kwa haraka nikakuta imendikwa kiasi cha shilingi miliioni kumi na tano.
“Amekuambia hizo zitakusaidia kuanza maisha mapya ya utajiri”
“Asante sana”
“Usijali, sisi hatuna cha zaidi cha kufanya, wacha tuondoke tukaendelee na majukumu ya kusongesha hili gurudumu”
“Asante sana dada Lutfia”
“Usijali ila piga kazi uzidi kumfaidi raisi, ila ukiwa mzembe, atakutumbua jipu”
 
“Haaahaha haya”
Nikaagana na Lutfia pamoja na vijana wake wawili, nikatoka nao hadi getini.
“Bob huyu ndio bosi wako mpya, sasa mutamalizana”
Alimuambia mlinzi wa getini aliye wafungulia geti dogo hapo ndipo nikagundua kwamba nje kuna gari liekuja kuwachukua likitokea ikuli.
“Sawa sawa muheshimiwa”
“Dany kijana wako wa ulinzi huyu, ila kila kitu analipwa kutoka serikalini”
“Sawa sawa”
“Bob umakini katika kazi ndio unahitajika, usione umetoka kule kwangu huku ukaja kucheza cheza”
“Hapana muheshimiwa siwezi kufanya hivyo”
“Haya kuwa makini”
“Sawa”
Wakatoka na Bob akafunga geti, akanipa mkono wa salamu kwa maana tangu niingie hapa sikusalimiana naye, kiumri hatujapitana sana na hata kama nimempita basi atakuwa nimempita miaka miachache sana. Nikarudi ndani na moja kwa moja nikaelekea kwenye chumba changu huku nikiwa na hati zangu mikononi nikafika, nikafungua kabati langu ambalo halina kitu chochote. 

Nikaziweka vizuri, kisha nikalifunga na funguo nikaziweka mfukoni. Kitanda kilichopo katika chumba hichi ni kitanda ambacho sikuwa kukilalia kwenye maisha yangu, nimesha zoea kuona vitanda vya pembe nne ila hichi ni kitanda cha duara. Nijairusha godoro lake likanipokea vizuri sana huku kilinirusha rusha vizuri. Furaha hii ni kubwa kusema kweli, nimetoka chini hadi hapa nilipo ni kwa neema za Mungu.
Nikanyanyuka kitandani na kusimama mbele ya kioo cha dreasing table kubwa nikaanza kujitazama huku nikizunguka zunguka.
“Yeaaahaaaaaaaaaa”
Maneno ya ajabu yalinitoka kinywani mwangu kwa furaha kubwa niliyo nayo, kwa haraka nikatoka chumbani kwagu na kuufunga mlango, nikaanza kushuka kwenye ngazi kwa haraka hadi nje. Nikaufunga mlango wa sebleni, na kuingia kwenye gari, kitendo cha kuliwasha nikasikia sauti ya kike ikitokea kwenye spika ndogo za gari hili.
“Karibu Mr Daniel, funga mkanda kwa maelezo zaidi”
“Mmmmm”
 
Nilijikuta nikiguna huku nikifunga mkanda kwa maana haya mambo ni mageni kwangu na sijawahi kuyaona kwenye magri mengine.
“Sasa gari lipo tayari kwa safari, kama unahitaji huduma ya ramani minya hapa na kama huitaji basi nakutakia safari nje”
“Asante”
Nikawasha gari na kuligeuza taratibu. Bob akanifungulia mlango na kutoka ndani hapa huku nikiwa makini sana na gari langu, nikatamai lipite hewani hata lisichafuke, ila ndio hivyo haliwezi. Moja kwa moja nikaeleka kwanza benki kwa ajili ya kuipata pesa ambayo nimepewa kwenye cheki. Nikashuka kwneye gari, kitendo cha kutaka kuingia kwneye mlango wa benki, vingora vya mlangoni hapo vikaanza kupiga kelele na kuwafanya askari wote kunielekezea mitutu yao ya bunduki kwangu huku wateja na wahudumu wakianza kuhaha kila mmoja kwa namna na jinsi ajuavyo mwenyewe.
 
Askari wawili kwa pamoja wakaniamrisha mikono yangu ninyanyue juu nikatii, mwingine akaniambia nilale chini kifudifudi huku mikono yangu nikiwa nimeiweka kichwani, nikafanya hivyo. Wakaanza kunipapasa na kuanza kuzitoa bastola zangu. Mmoja alipo toa waleti yangu na kuifungua na kukuta kitambulisho changu cha kazi, akawaomba wezake kushusha bunduki zao chini.
“Samahani mkuu”
Mmoja alizungumza huku akinipa mkono wa kuninyanyua, nikanyanyuka nikiwa na tabasamu pana usoni mwangu kwa maana swala hili wala halijanitisha sana kwani nina furaha yangu moyoni na wala sikuhitaji mtu kuweza kuichafua furaha yangu. Wakanirudishia bastola zangu na kuzichomeka katika sehemu walipo zichomoa. Watu wakatangaziwa na muhudumu wa benki waendelea na shuhuli zao kwa manaa hakuna tatizo baya. Nikafika sehemu ya huduma kwa wateje, nikamsalimia dada mmoja mrembo aliyopo katika eneo hili.
“Salama tu nikusaidie nini kaka?”
 
“Kuna hii cheki yangu, hembu ifanyieni utaratibu”
“Sawa”
Msichana huyu ambaye ni kivutio karibu cha watu wote tulipo eneo hili la huduma kwa wateja, akachukua cheki yangu na kuandika namba kadhaa kwenye kompyuta yake iliyopo pembeni yake.
“Kaka utasubiria kama dakika kumi hivi, ngoja niiipeleke kwa bosi hii cheki”
“Hakuna shida mrembo”
Akageuka na kuanza kuondoka, hapo ndipo nilipo jikuta mimacho nikiitumbua, si mimi peke yangu hata wanaume tulipo katika eneo hili sote macho yetu yakawa katika kalio lake kubwa lililo banwa vizuri na kijisketi cha rangi ya blue iliyo kolea.
“Umalaya utakuua”
Nilisikia sauti ya kike pembeni yangu na kunifanya nigeuke nikamkuta dada mmoja akimalizia kumsuta mpenzi wake kwa kidole na kumfanya akasirike.
“Useng** wako siutaki”
Jamaa naye alizungumza kwa sauti ya chini chini huku sauti yake ikiwa nzito
“Useng** gani, mkeo nipo hapa unakazi ya kutazama makalio ya wanawake wengine”
“Ahaa sasa mwenzako si anayo, kwani kuyatazama mimi nitayachukua si nayaacha kwake”
“Hembu niachie upuuzi wako, nitaondoka sasa hivi na pesa sinto kutolea”
 
“Ahaa basi yaishe mpenzi wangu, ni shetani tu”
“Endelea kujibu jeuri, uone kama pesa yangu nitakupa”
“Yaishe honey”
“Haya”
Hapo ndipo nikagundua kwamba mwanaume mzima hasira yake imetishiwa kwa kunyimwa kupewa pesa, nikajikuta nikitabasamu tuu kwa mana urembo wa dada huyo umeweka matatani mahusiano ya watu walipo katika eneo hili la huduma kwa wateje. Baada ya dakika tano dada huyo akarudi huku akiwa na tabasamu pana, moja kwa moja akanifwata usawa wangu na kuniambia kwa sauti ya upole na kubembeleza.
“Bosi amesha ishuhulikia, si una akaunti hapa?”
“Ndio ninayo ila sijaitumia muda mwingi sasa sijui hata kama itakuwa bado hai au imefungiwa”
“Hembu nitajie jina lake”
Nikamtajia jina langu, akaliingiza kwenye kompyuta, kisha akanitazama kwa macho malegevu kiasi yanayo tamanisha ukiwa mshamba unaweza kuhisi labda amekutamani na kukulegezea, ila ndivyo jinsi Mungu alivyo muumba macho yake.
 
“Akaunti yako mbona ipo?”
“Ipo?”
“Ndio na ina salio la laki moja na ishirini na mbili”
“Daa afadhali”
“Pesa tunaziingiza sasa hivi”
“Sawa, pia nitahitaji kutoa kiasi kidogo”
“Sawa”
Dada huyo mwenye weusi wa maji ya kunde, akaanza kuminya batani za kompyuta yake, alipo maliza, akanitingishia kichwa na kuniambia kwamba pesa tayari imesha ingizwa kwenye akaunti yangu. Gafla tukasikia mlio wa risasi ulio tufanya watu wote ndani ya benki kuhamaki, nikageuza macho yangu mlangoni nikamuona askari mmoja akiwa amenguka chini damu zikimwagika, huku majambazi sita wakiingia ndani ya benki wakiwa na bunduki pamoja na mabomu ya kurusha kwa mkono na mmoja kati ya majambazi hawa ni mwanamke na yeye ndio anaye ongoza msafara wa majambazi wezake huku mkononi mwake akiwa ameshika bunduki aina ya AK 47, bila hata ya kuhofia akapiga risasi mbili hewani na kufanya watu wote kulala chini hadi mimi mwenywe.
                                                                                          ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts