Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 39 na 40 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 39 na 40 )

Written By Bigie on Tuesday, March 13, 2018 | 4:08:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA     
Dada huyo mwenye weusi wa maji ya kunde, akaanza kuminya batani za kompyuta yake, alipo maliza, akanitingishia kichwa na kuniambia kwamba pesa tayari imesha ingizwa kwenye akaunti yangu. Gafla tukasikia mlio wa risasi ulio tufanya watu wote ndani ya benki kuhamaki, nikageuza macho yangu mlangoni nikamuona askari mmoja akiwa amenguka chini damu zikimwagika, huku majambazi sita wakiingia ndani ya benki wakiwa na bunduki pamoja na mabomu ya kurusha kwa mkono na mmoja kati ya majambazi hawa ni mwanamke na yeye ndio anaye ongoza msafara wa majambazi wezake huku mkononi mwake akiwa ameshika bunduki aina ya AK 47, bila hata ya kuhofia akapiga risasi mbili hewani na kufanya watu wote kulala chini hadi mimi mwenywe.

ENDELEA
Kila mmoja aliyopo kwenye eneo hili hususani ndani ya hii benki, mwili wake uliweza kutetemeka kwa woga, hapakuwa na mtu ambaye anapenda kufa kwa muda huu, hususani mimi ambaye ni masaa machache tu nimetoka kupewa zawadi nono kutoka kwa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Toa pesa wewe malaya”
Aliongea jambazi mmoja wa kiume huku akipapasa, watu waliokuwa wapepanga foleni ya kueleka katika dirisha la kuweka pesa au kutoa pesa. Jasho likazidi kunimwagika. Mtoto wa kiume ujanga sikuwa nao kusema kweli, japo nina mafunzo tosha ya kupambana na majambazi kama hawa ila hakuna kitu kibaya kwa mwanausalama yoyote dunia, kuwahiwa kushambuliwa, wenyewe kwa lugha yetu tunaita Ambushi.
Nikatazama jinsi watu wakipapaswa huku majambazi wengine wakiwashika wahudumu wa benki na kuingia nao kwenye vyumba ili waonyeshwe pesaa. 
 
‘Natakiwa kufanya kitu’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikitazama majambazi hawa kwa umakini japo kichwa changu nimekilaza chini na mikono yangu nimeiweka kichani ila usawa wa macho yangu ulinitosha kuweza kuoana jinsi majambazi hawa walivyo simama huku wengine wakiendelea na shuhuli ya kutafuta pesa zilipo wekwa. Nikamuona jambazi mmoja akimfwata dada aliye kuwa ananihudumia, akamtandika kofi zito la shavu.
“Toa pesa wewee”
“S..si….si….na mimi”
Jambazi huyo akamtandika, kitako cha buduki cha tumbo na kumfanya dada hyo kuanguka chini na kutoa mlio mkali wa maumivi.
“Nyamaza wewe malaya nitakuchangua ubongo”
Kauli ya jambazi huyo ilinizidi kunitisha, kwani bunduki yake amemuelekezea dada huyo huku akiwa ameikoki vizuri tauyari kwa kufyatua risasi.
‘Unapo kuwa peke yako kwenye uvamizi, mfano uvamizi wa benki, super makert na kadhalika, hakikisha kwamba unamuwahi kiongozi wa hilo tukio, ukimpata tu huyo wezake hawato weza kufanya chohcote dhidi yako’
 
Maneno hayo ya mwalimu  wangu yakajirudia kichwani mwangu kwa kasi ya ajabu na kunipa ujasiri wa haraka ulio nifanya, nimtafute mkuu wao ambaye ni mwanamke, nikamuona akimpitia mtu mmoja baada ya mwingine akimgonga gonga kwa mguu na kutazama kama ana silaha au laa. Taratibu akazidi kunisogelea mimi, na mimi nikajiweka tayari kufanya shambuli la haraka sana kwa maana nina hapa nilipo nina silaha za kutosha. Kitendo cha kunikaribi, ikawa ni moja ya kosa kubwa kwake, kwani kwa sekunde moja niliweza kujigeuza na kurusha teka lililo izoa miguu yake na kuanguka chini huku bunduki yaki ikiwa pembeni, nikampiga kabali, na kunyanyuka naye, na kuwafanya wezake zote kusitisha kile walisho kuwa wakikifanya.
 
“Wote silaha zenu wekini chini”
Nilizungumza kwa kufuko huku bastola niliyo kuwa nimeiweka kiunoni nikiwaelekezea bosi wao kichwani. Majambazi wakabaki wakiwa wameduwaa, nikarudia tena kwa ukali kwamba waweke silaha zao chini lasivyo nina mwaga ubongo mwenzao huyu. Dada huyu akatoa ishara ya vidole akiwaamrisha waweke silaha zao chini, kila mmoja akafanya hivyo.
“Dany unafanya nini?”
Sauti ya dada huyu ikanistua sana kwa mana ni sauti ya mtu ambaye ninamjua vizuri tena vizuri sana.
“ASAMA………!!!”
Nikataka kumvua kinyago alicho kivaa usoni mwake, ila nikastukia kitu chanye ncha kali kikizama kwenye mbavu zangu za kushoto na kujikuta nikimuachia Asma na mimi nikidondoka chini, hapo ndipo nikaona kisu alicho nichoma nacho kikivuja damu huku kikiwa kiganjani mwake. Majambazi wezak wakaokota bunduki zao kwa haraka. Mmoja wao akataka kunipiga risasi, ila Asma akamzuia kwa haraka.
 
“Tuondokeni haraka haraka”
Asma alizungumza na wakaanza ktoka huku wakiwa wamebeba mabegi yaliyo jaa pesa. Nikajajaribu kiusimam huku mkono mmoja ukiwa umeshika bastola na mwengine umejiziba sehemu niliyo chomwa kisu, nikajikuta nikirudi chini, ila kwa ukakamavu nikafyatua risasi mbili zilizo mpiga jambazi wa mwisho mgongoni na kumuangusha hata kabla hajaufikia mlango, na begi alilo lishika likaangukia pembeni. Wezake hawakuweza kurudi ndani kulichukua begi hilo kwani hali imesha kuwa tete kwa upande wao.  Taratibu nikalala chali huku maumivu makali ya kisu nilicho chomwa yakizidi kuongezeka. Watu waliopo karibu yangu wakanyanyuka taratibu baada ya hali kutulia, wakanisogelea huku wakitaka kufahamu hali yangu.
 
“Jamani yupo hai tumsaidie mkombozi  wetu”
Jamaa mmoja alizungumza huku akininyanyua kichwa na kukiweka kwenye mapaja yake, watu wakanza kunyanyuka mmoja baada ya mwengine.Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo zidi kujisikia vibaya hadi ikafikia hatua macho yangu ninaanza kuyaona yakiingiwa na ukungungu na taratibu giza likatawala na kwa mbali niliyasikia mazungumzo ya watu ambayo sikuyaelewa wala kuyatilia maanani kabisa.
                                                                                                              ***
   Macho yangu nikayafumbua taratibu, kitu cha kwanza kukiona ni taa iliyopo kwenye chumba hichi inayo waka kwa mwanga mweupu.    Taratibu nikakigeuza kichwa changu pembeni na kumkuta mama akiwa amekaa kwenye sofa huku mkononi mwake akiwa ameshika simu. Nikajaribu kukichunguza chumba hichi kwa umakini na kugundu kwamba hapa ni hospitali kwani madhari yote yananionyesha kwamba hapa ni hospitali.
“Mama”
Niliita kwa sauti ya chini na kumfanya anyanyue kichwa chake, kwa haraka akasimama kwenye sofa na kunifwata hadi kitandani, akaka pemebeni yangu na kunitazama usoni mwangu huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
“Dany mwanagu umeamka?”
“Mmmmm”
“Ohoo asanye Yesu, vipi unajisikiaje?”
“Salama”
Nikataka kukaa ila maumivu makali niliyo yapata kwenye mbavu nikajikuta nikiwa nimelala tena.
 
“Usiamke mwanangu utapata maaumivu”
“Nipo wapi hapa mama?”
“Upo hospitali mwangu”
Nikashusha pumzi taratibu huku nikiendelea kutazama eneo la chumba hichi. Kumbe sikuwa nimekosea pale nilipo tambua kwamba hapa ni hospitalini.
“Nipo hapa tangu lini mama?”
“Ni siku ya tatu leo, tangu nifike hapa, na tukio la ujambazi lilivyo tokea”
“Wale maajmbazi walikamatwa?”
“Ndio waliweza kukamatwa na wewe umepemba vichwa vya habari ukiwa kama shujaa uliye weza kupambana na majambazi”
“Shujaa, mimi niwe shujaa mama…….!!?”
Nilizungumza huku nikitabasamu, mama akanyanyuka akafungua pochi yake aliyo iweka juu ya kochi, akatoa gazeti na kurudi, akaka kitandani na kulikunja vizuri. Akanionyesha gazeti hilo la Mwananchi lilio andikwa kwa maandishi makubwa meusi. (MWANA USALAMA AKOMBOA MAMILIONI YA MAPESA BENK YA NNB)
 
Chini ya maneno hayo kuna picha yangu, inayo nionyesha picha yangu iliyo patikana kupitia kamera za ulinzi jinsi nilivyo ishika bastola yangu na nikiwa nimemuelekezea jambazi aliye kuwa katika harakati za kukimbia.
“Ila mama wameandika taarifa hii, si itakuwa ni tatizo kwa kazi yangu?”
“Hapana sio tatizo, kwa maana unalindwa sana na hapo nje kuana walinzi kutoka katika kitengo chenu cha kazi wakiendelea kuimarisha ulinzi.
“Ahaa sawa, gari langu umeliona?”
“Ndio, kila kitu chako kipo salama”
Malango ukagongwa na mama akanyanyuka na kuelekea kuufungua.
“Karibu mwanya”
“Asante mama”
Mama akaongozana na yule muhudumu wa benki, aliye kuwa akinihudumia kabla ya tukio la uvamizi wa majambazi halijatokea.
 
“Habari yako Dany”
Dada huyo alizungumza huku akiwa ameachia tabasamu pana.
“Salama tu za kwako”
“Safi, pole sana mwaya Dany. Yaani siku zote nilikuwa na wasiwasi mkubwa juu yako”
“Dany huyu binti alikuwa nawe pamoja tangu nafika hapa hospitalini na yeye huwa kila siku jioni anakuja kukutazama”
“Ahaaa”
“Naamini sura yangu sio ngeni kwako Dany eheee”
“Yaa sio ngeni, si yule muhudumu pale benki?”
“Ndio”
“Nakukumbuka”
“Naitwa Rosemary ila wengi wananikatisha wanaita Rose”
“Ok asante”
“Dany ngoja niwaache mara moja”
Mama akanyanyuka na kutoka nje, sikufahamu lengo la yeye kutoka nje na kuniacha na Rose ambaye taratibu akaka kwenye sehemu aliyo kuwa amekaa mama. Ukimya ukatawala kati yangu na Rose sikuwa na kitu cha kuzungumza ziaid ya kutazamana. Rose aliye valia nguo zake za kazi akaendelea kunitazama usoni mwangu, huku akitamani kuzungumza kila ila akashindwa kabisa.
 
“Vipi, tumbo lako limepona?”
“Ndio, sasa hivi lipo vizuri sisikii maumivu”
“Ahaa pole, ivi wale majambazi walikamatwa?”
“Yaa walikamatwa, na mmoja wao ni mwanamke, yaani ni dada mzuri sijui kwa nini aliamua kufanya ujambazi”
“Mmmm”
“Picha zao ninazo hapa kwenye simu, zimeenea kwenye mitandao ya kijamii”
“Hembu nizione”
Akatoa simu yake kwenye kijipochi kidogo na kuanza kuiminya minya kwneye kioo, baada ya sekunde kadhaa akanigeuzia na kunionyesha picha za majambazi hao. Picha ya kwanza ni ya jambazi wa kiume, hata ya pili ila picha ya tatu, ikanifanya kidogo nikae sawa. Hakuwa mwengine zaidi ya Asma. Kusema ukweli ninajionea mapicha picha kwenye maisha haya. Asma anasema Jumaa ni jambazi, na yeye anajiweka ni msichana ambaye ni mnyonge na kila siku anapigwa na Jumaa, ikiwa ana uwezo mkubwa wa kutumia bunduki tena AK47.
 
“Mbona sielewi hapa?”
“Huelewi, huelewi nini Dany?”
“Ahaa hakuna”
Sikutaka Rose afahamu ni kitu gani kinacho endelea. Mlango ukafunguliwa pasipo kibishwa hodi, mama akaingia, kisha nyuma yake akafwatia Diana mdogo wangu. Diana alipo niona kitandani kwa haraka akanikimbilia na kunikumbatia kwa furaha.
“Ohoo kaka Dany, mambo”
“Poa vipi?”
“Safi”
“Dany nimekufanyia suprize, nilitoka kwenda kumpokea mdogo wako amekuja leo”
Mama alizungumza huku akitutizama kwa furaha. Diana akanikumbatia tena kwa furaha kwani ni miaka kadhaa hatujaonana tango aondoke kueleke masomoni nje ya Tanzania
“Yaani mama ulipo niambia kwamba kaka Dany amepata tatizo kiroho kilikuwa kina nicheza cheza wee acha tu”
“Ila sio tatizo kubwa mama alikutisha”
“Sio tatizo kubwa wakati unajeraha hapo”
 
“Si dogo tu”
“Mmm mama muangalie mwanao, eti jeraha dogo. Mimi tangu sijafunga shule hadi nimeondoka Marekani na kufika hapa alafu unaseme jeraha dogo”
“Tuyaache hayo, huyo ni rafiki yangu anaitwa Rose. Rose huyo ni mdogo wangu anaitwa Diana”
“Ohoo nashukuru kukufahamu”
“Hata wewe pia nakushukuru kukufahamu, Dany ndio wifi yangu nini?”
Swali la Diana likatufanya sote kukaa kimya huku tukitabasamu.
“Ohoo nimeshafahamu ukimya pia ni jibu. Ila kaka Dany hapa una chombo aiseee”
“Diana acha maneno mengi mwanangu”
Tukaendelea kuzungumza stori nyingi hususani za Diana huko alipo toka masomoni. Ilipo timu saa tatu usiku Rose akaondoka na mimi nikabaki na mama pamoja na Diana. 
 
Siku zikazidi kwenda na kusonga mbele, baada ya wiki moja nikaruhusiwa kutoka hospitalini na kwa kipindi cha siku nne nyuma mama aliweza kuondoka hospitalini na kurudi Tanga akiwa ameteuliwa kama mkuu mpya wa mkoa wa mji huo. Siku hii ambayo nimeruhusiwa, Rose na Diana waka wapo hospitali, nikaongozana na walinzi kutoka katika kitengo cha NSS. Wakatupeleka hadi kwenye jumba langu nililo kabidhiwa na raisi kama zawadi. Diana na Rose hawakuamini kwamba ninaweza kumiliki jumba kubwa kama hili.
“Ina maana Dany jumba hilo lote ni lako?”
Rose aliniuliza huku akitizama usoni, cha kushukuru Mungu, ninaweza kutembea mwenyewe na kidonda kimesha kauka, japo kina maumivu kwa mbali.
“Ndio”
“Kaka Dany hii nyumba umeitolea wapi?”
“Kwani nyumba mdogo wangu zinatolewa wapi?”
“Ahaa unaweza ukawa umepanga ukasema ni yako”
 
“Kweli ni yangu”
Nikaka sebleni huku nikiwa ninamtazama Rose ambaye kwa leo amekuja amevalia mavazi ya nyumbani. Uzuri wake unaendana kabisa na jina lake.
“Nyumba yako ni bubu, haina hata chakula cha kupika”
“Nikupe kadi ya malipo muende Mlimani City mukanunue vyakula”
“Utakuwa umefanya la maana, nataka kuendesha hiyo gari lako hapo nje”
“Sawa, kwenye ile suruali yangu ndani ya hilo begi hapo kuna waletu yangu, nitolee”
Diana akafanya kama nilivyo muagiza, akaitoa waleti yangu na kunikabidhi, nikatoa kadi yangu ya malipo ambayo huwa nina itumia kulipia vitu ninavyo nunu kwa baadhi ya maeneo yanayo tumia huduma hiyo ya malipo ya kadi. Nikamkabidhi Diana kadi, akaitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akaanza kutangulia kutoka na kumuacha Rose akinyanyuka kwenye sofa taratibu, Diana alipo toka nje, kwa haraka Rose akanifwata nilipo kaa, akainama kidogo na kuanza kuninyonya midomo yangu kwa hisia kali.
 
“I love you Dany”
Rose alizungumza huku akiniachia na kukimbilia nje akiwa amejawa na furaha, Diana akaingia tena ndani.
“Dany gari lako mbona silielewi?”
“Ulielewi nini?”
“Njoo bwana unielekeze”
Nikanyanyuka taratibu na kutoka nje, nikafungua mlango wa gari na kukuta likiwa linawaka.
“Huelewi nini hapa?”
“Sasa nimewasha nalirudisha nyuma halirudi?”
“Sasa Diana utarudishaje gari nyumba wakati lipo kwenye hand brake?”
“Aahaa ushamba jamani”
Diana na Rose wakaingia kwenye gari, Diana akageuza gari taratibu na kuondoka, Bob akawafungulia geti gari likatoka, kisha Bob akalifunga geti na kuanza kunifwata kwa mwendo wa haraka, akanisalimia kwa heshima.
 
“Vipi”
“Bosi kuna mzigo wako uliletwa juzi na dereva bodaboa mmoja”
“Upo wapi?”
“Nimeuacha kule chumbani kwangu, ngoja nikauchukue”
Bob akakimbie hadi kwenye nyumba ya pembeni iliyopo katika uzio wa nyumba yangu, baada ya dakika kama mbili akarudi akiwa ameshika bahasha ya kaki. Akanikabidhi na nikamruhusu kuondoka, bahasha hii iliyo fungwa na gundi na kuandikwa maandishi makubwa kwa rangi ya blue, nikaichunguza vizuri huku nikitingisha, nikagundua ndani kuna simu. Nikaichana bahasha kiungalifu na kweli ndani nikakuta simu aina ya Samsung J7 pamoja na kijikaratasi kidogo. Nikakisoma kikaratasi hicho kilicho nipa maelezo ya kuwasha simu hiyo na kuelekea upande wa video, nikafanya hivyo na simu ilipo waka nikafungua upande wa video na kukuta video moja tu iliyo andikwa maandishi madoho Me and Dany.
 
Kwa shauku kubwa nikaifungua huku nikihitaji kufahamu ni kitu gani kilichopo ndani ya video hiyo, sikuamini macho yangu nilipo jiona mimi na Yudia tukifanya mapenzi sebleni kwa mama yangu, mwili na mikono vyote nikajikuta vikinitetemeka, nikajaribu kuipeleka mbele huko ndipo nilipo kutana na video ya Yudia akizungumza.
“DANY FANYA ASMA ATOROKE JELA, LA SIVYO MAMA YAKO, MDOGO WAKO WATAKUWA MIKONONI MWANGU ISITOSHE PIA HII VIEDO NITAISAMBAZA HADI KWA RAISI WAKO ALIYE KUPA HIVYO NYUMBA”
Nikajikuta nikkikaa chini mimi mwenywe hadi Bob akastuka na kuanza kunifwata nilipo kufahamu ni kitu gani kimenipata.
                                                                                         
  AISIIIII……….U KILL ME 40

“Bosi una tatizo”
Bob alizungumza huku akinikaribi, nikamzuia asinisogelee kwa kumnyooshea mkono. Taratibu nikanyanyuka huku akinitazama. Kwa mwendo wa taratibu nikaingia ndani, moja kwa moja nikapandisha gorofani na kuingia katika chumba changu. Nikaka kitandani na kuyarudia kuitazama video hii, nikahisi  kichwa kinataka kupasuka kwa mawazo.
 
Nikiwa katika dibwi la mawazo simu hii niliyo letewa ikaita, nikatazamana kukuta namba tu isiyo andikwa jina. Taratibu nikakipitisha kidole ngumba kwenye kioo cha simu hii kisha nikaiweka sikioni.
“Haloo Dany, inaonekana unashangaa, nimepajuaje kwako”
Niliisikia sauti ya Yudia akizungumza kwa dharau huku sauti yake akiwa ameilegeza kimahaba.
“Unataka nini kwangu?”
“Ahaaa….ahahahaaaaa unauliza ninahitaji nini kwako, wakati nimesha kupa maagizo, au unahitaji nikuonyeshe kitu ambacho kitakufanya uweze kujua ni nini ninacho kihitaji?”
Nikajikuta nikisimama huku mapigo ya moyo yakinienda kasi sana. Hata kujibu, nikajikuta ninashindwa kutokana na kigugumizi kilicho ambatana na hasira kali sana. 
 
“Ohooo Dany, kwa nini umefanya haya yote, natambua kwamba upo chumbani kwako na ninakuona kama huuamini hilo nenda sebleni, washa Tv yako na utajua ni nini nina maanisha”
Kwa haraka nikatola chumbani kwangu huku nikiwa natazama kila kona ya kuta za nyumba yangu kuona kama kuna kamera ila, sikuona chochote. Nikafika sebleni, nikaitafuta rimoti ya Tv kwa haraka nikaiona ikiwa juu ya meza, nikaichukua na kuwasha Tv. Macho yakazidi kunitoka baada ya kumuona Yudia amekaa kwenye kiti huku nyuma yake wakiwemo wanaume wawili walio zifisha sura zao na mikononi mwao kila mmoja ana bunduki aina ya AK47.
“Unaniona sasa?”
Niambie umetega nini nyumbani kwangu?”
“Ohoooo Dany Dany usikasirike mpenzi, wewe bado hujapona vizuri. Kazi niliyo kupa utaifanya ua hito ifanya?”
“Siwezi kufanya kazi ya Mbwa, Malaya, Changudoa kama wewe”
 
Niliachia matusi yote hayo huku nikiendelea kumkazia macho Yudia, aliye tabasamu kisha akanyoosha mkono wa ishara kwamtu aliyopo nyuma ya kamera yake. Kamera taratibu ikageuka, moyo ukazidi kwenda kasi baada ya kuanza kumuona Rose, karera haikuishia hapo nikamuona na Diana wakiwa amefungwa kamba miili yao, huku machoni wakiwa wamefungwa vitamba vyeusi wakilia kwa uchungu sana. Nikajikuta machozi ya hasira yakianza kunimwagika kwani ni muda mchache sana wametoka nyumbani kwangu hapa wakiwa wanakwenda Mlimani City.
“Huyu naona ni ndio Malaya atatangulia kuzimu, kabla ya mdogo wako kwenda”
Niliisikia Sauti ya Yudia akizungumza hivyo huku bunduki akiikoki.
“Yudia ngoja kwanzaaaaa”
Nilizungumza kwa uchungu huku nikiendelea kulia, maisha yangu tayari ninaona yameingia kwenye mgogoro mkubwa wa maisha mdogo wangu, Rose ambao wote hawana makosa wameingia kwenye mikono ya adui.
 
“Nakusikiliza Dany, mtoto wa kiume kulia sio jambo la busara, ukitegemea unazungumza na mtoto wakike”
“Ok ok ok, niambie chochote nitafanya ila si kumuua mdogo wangu na Rose”
“Ohoo, ok. Nimekuagiza namuhitaji Asma hapa, humjui Asma kwangu ni nani hadi ukathubutu kuvuruga mipango yangu na siku zote huwa sihitaji mtu aweze kuvuruga mipango yangu”
“Ok niambie ni wapi alipo niweze kumfwata”
“Hiyo ni kazi yako, nakupa masaa mawili nitakupigia kutambua ni wapi alipo Asma”
Yudia akakata simu, nikamuona anavyo msogelea Diana mdogo wangu, akamshika kichwa chake na kumgeuza geuza huku akimtazama kwa dharau, kisha akampiga busu la mdomoni na kamera hiyo ikazimwa na kufanya kioo cha Tv yangu kutawaliwa na rangi nyeusi.
Taratibu nikajikuta nikiwa nimekaa kwenye sofa, kichwa kikizidi kuniuma, moyo ukiwa haujatulia kabisa, machozi yanazidi kunimwagika.
‘Lazima niwaondoe hawa washenzi wote kwa mkono wangu mwenyewe’
 
Nilizungumza huku nikisimama, nikafungua begi langu nililo kuja nalo kutoka hospitalini, nikatoa bastola zangu ambazo nililetewa na mmoja wa wafanyakazi katika kitengo changu. Sikuwa na haja ya kuvaa nguo au kubakidi, kijikoti chepsi nilicho kivaa juu ya tisheti nyeusi, nikaona kinanifaa kabisa katika kuanza kuifanya kazi hiyo.
Nikachomeka bastola moja kwenye soksi ya mguu wa kulia, kisha nikaichomeka ya pili katika mguu wa kushoto kisha nikafwata kuichomkea nyingine kiunoni kwa nyuma na nyingine nikaificha chini ya kochi. Ujumbe wa meseji  ukaingia kwenye simu hii, nikaufungua kwa haraka na kuusoma.
(HAPO ULIPO IWEKA HIYO BASTOLA SIO SALAMA)
Ujumbe huu unatako wa Yudia, nikastuka sana, nikasimama sebleni na kauza kutazama ni wapi kulipo fichwa kamera zinazo onyesha kila ninacho kifanya katika nyumba yangu. Nikajitahi kadri ya uwezo wangu kutafuta kamera hizo ambazo huwa ni ndogo sana na wala si rahisi kwa mtu kuweza kufahamu ila ikaingia meseji nyingine iliyo nifanya kusitisha zoezi hilo na kuisoma.
 
(UNAPOTEZA MUDA LIMEBAKI LISAA MOJA NA NUSU)
Nikashusha pumzi huku jasho likinimwagika usoni mwangu, nikatoka nje. Bob akaniuliza swali ambalo wala sikulisikia vizuri kichwani mwangu zaidi ya kufungua geti na kutoka. Nikatembea hatua kadhaa hadi barabarani. Nikasimamisha muendesha pikipiki mmoja niliye muelekeza kunipeleka hadi katika jengo la ofisi yetu.  Njia nzima nikawa ninawaza ni nini cha kufanya, ili niweze kujitoa mikononi mwa Yudia ambaye sasa amsaha tangaza na kuudhihirisha ukatili wake na ugaidi wake, kwa maana sikujua ni muda wagi Rose na Diana wanaweza kukamatawa. Nikafika katika jengo la ofisi yetu, nikashuka kwenye bodaboda kwa haraka na kuanza kualekea ndani. 
 
“Kaka kaka kaaa”
Niliisikia sauti ya bodaboda huyo akiniita na kunifanya kusimama huku nikigeuka na kumtazama kwa macho makali.
“Pesa yangu hujanilipa na umeshuka tu na kukimbilia huko ndani”
“Sina pesa yako kwa sasa”
“Unasemaje wewe”
“Nimekuambia sina pesa yako kwa sasa, fanya uondoke mbele ya macho yangu kabla sijakuvuruga”
“Kum**ako wewe mseng*** unahisi hii pikipiki amenunua basha wako eheeee?”
Dereva pikipiki alizungumza huku akiporomosha matusi mazito na kunisukuma nyuma, kwa hasira nikarusha ngumi iliyo mpata usoni mwake na kumuangusha chini, akanyanyua sura yake na kunitazama kwa mshangao huku damu zikimwagika puani mwake. Akataka kunyanyuka kwa haraka nikachomoa bastola na kumuelekezea ya uso.
 
“Danyyyyyy”   
Nilisikia sauti ya kike nyuma yangu, nikageuka na kumkuta Lucy binti niliye msaidia kumuokoa katika ajali ya moto katika jumba lao la kifahari, akiwa ameuziba mdomo wake kwa mshangao. Nikamtazama dereva bodaboda aliye nywea kama sio yeye aliye leta kibesi juu yangu.
“Sina pesa yako”
Nilizungumza huku nikirudisha bastola yangu kiunoni na kugeuka na kuanza kutembea kuelekea kwenye lifti ya kupanda gorofani kwa jengo hili zilipo ofisi ninazo fanyia kazi. Nikageuka nyuma na kumuona Lucy akimalizia kumkabidhi pesa dereva bodaboda niliye mpiga kisha akaanza kunifwata mimi kwa kasi. Nikasimama mbele ya lifti hii inayo onyesha inapanda juu na kunilazimu kuisubiria kwa muda.
“Dany”
Lucy aliniita huku akisimama pembeni yangu akihema kwa wasiwasi, sikuwa na sura ya kutabasamu wala kufurahi, sura yangu safari hii imejaa hasira na uchungu mwingi ambao hakuna mtu yoyote anaye ufahamu.
 
“Nimekutafuta kwa wiki kadhaa sasa, huku nikija hapa ofisini kwako kukuulizia, ila ninaambiwa haupo”
“Unahitaji nini?”
“Ahaa…ahaaa nili….nilikuwa nataka kukuomba msamaha”
Kwa jicho kali nililo mtazama nalo Lucy, akajikuta akiwa ameinamisha kichwa chake chini huku akitetemeka kwa woga. Lifti ikafunguka, nikaingia ndani, Lucy akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha na yeye akaingia. Milango ya lifti hii ikajifunga na taratibu ikaanza kwenda juu, sikuzungumza kitu chochote kwa Lucy, moyo, akili na nafsi kwa wakati havifikirii mwanamke yoyote zaidi ya Diana mdogo wangu, hata Rose hana umuhimu mkubwa sana kwangu.
  Hadi lifti inafunguka tukiwa gorofa ya nne, Lucy hakuzungumza kitu cha aina yoyote. Nikaanza kutembea kwenye kordo ya vyumba vya ofisi zetu, nikapishana na wafanyakazi wezangu walio jaribu kunisalimia ila sikuitika kabisa. Moja kwa moja nikaingia katika ofisi ya K2, na kukutana na sectretary wake.
 
“Mambo Dany”
“Bosi yupo wapi?”
“Ana mgeni subiri hapo kwenye viti”
Sikutaka kusubiri kama alivyo zungumza sectretary wa K2, nikausukuma mlango kwa nguvu na ukafunguka. Nikamkuta K2 na Luka wakiwa wanazungumza, wote walipo niona macho yao yakawatoka kwa maana nina amini hakuna aliye tegemea kuniona eneo hili kwa muda na saa kama hii.
“Dany”   
K2 alizungumza huku akitabasamu, nikamtazama kwa macho makali yaliyo lifuta tabsamu lake usoni, kisha nikayaamishia macho kwa Luka, aliye jaribu kunyanyuka kwenye kiti chake. Nikamrudisha kwenye kiti chake kwa kumpiga teke la kifuani na kumfaya K2 kushangaa huku macho yakimtoka. Nikaichomoa bastola yangu  na kumuwahi Luka, nikamuwekea mdomo wa bastola kwenye kichwa chake huku nikiwa nimekwida shati lake.
“Wewe mwana haramu, yupo wapi mdogo wangu”
Jinsi swali nilivyo liuliza ndivyo jinsi liliyo toka na ksisitizo wa sauti nzito.
“Si…si sijui mimi?”
“Nitakuua na sihitaji kusikia hiyo kauli”
 
“Kwe…..kweeli Dany”
“Dany STOP heshimu ofisi yangu”
Nikamuacha Luka kwa haraka na kumnyooshea K2 bastola ya uso huku nikiendelea kumkazia macho, sikuwa Dany yule waliye zoea kuniona mchangamfu, mpole na mcheshi kwao.
“WHO ARE YOU………!!!?”(WEWE NI NANI………!!!!?)
“AM YOUR BOSS”(MIMI NI BOSI WAKO)
K2 alinijibu huku akinyanyuka pasipo kuiogopa hasira yangu na macho yake akawa amenikazia.
“Malaya kama wewe, unajiita bosi eheee”
“Dany linda heshima ya kitengo hichi”
“Heshimwa, heshima kwa kufirw*** mkund***. Eheeeeee!!”
K2 akabaki akiwa amenikodolea macho, sikuogopa kupeteza kazi yangu, ila ninacho kihitaji kwa sasa ni mdogo wangu Diana kuwa salama. Nikaishika bastola yangu vizuri huku hasira ikizidi kunitemesha mwili mzima. Simu mfukoni mwangu ikaanza kuita, kwa mkono wa kushoto nikaitoa na kuitazama na kukuta ni Yudia ndio anaye piga.
“Dany…..Mbona una haribu sasa. Kwa kosa hilo la kumtukana K2, basi huyu Rose atalipaa”
Nikasikia mlio wa bunduki, kisha ukafwatia ukelele mkali wa kilio cha maumivu kutoka kwa Rose. Nikamtazama K2 na kumuona akitabasamu huku akinipandisha na kunishusha.
“Huyu nimempiga risasi ya paja lake lililo nona, ukiendelea, basi nitafwata kichwa chake, fanya nilicho kuagiza”
 
Simu ikakatwa, nikajikuta nikizidi kupandwa na hasira, nikatamani kufyatua risasi na kummaliza K2 kabisa, ila ninashindwa kufanya hivyo kwani nikifanya hivyo basi Diana na Rose ninawakosa.
“Dany unayakumbuka maneno yangu pale ikulu. Enjoy the Game”
K2 alizungumza huku akikaa kwenye kiti chake cha kuzunguka, nikamtazama Luka naye, akatabasamu huku akinitazama juu hadi chini kama wafanyavyo watoto wa kike. Taratibu nikaishusha bastola yangu na kugeuka na kuanza kuufwata mlango wa kutoke.
“Dany kumbukaa, hii ni Tanzania, country of peacefull”
Maneno ya K2 yakazidi kunikereketa, nikafungua mlango na kuufunga kwa nguvu hadi secretary wake akastuka.
“Dany nini tatizo?”
“Hayakuhusu”
Jibu langu liliweza kumtosha secretary wa K2, nikatoka ofisini kwao na moja kwa moja nikaeleke hadi kwenye ofisi yetu. Nikawakuta wafanyakazi wezangu wanne wakiwa wanaendelea kufanya kazi zao.
 
“Dany vipi?”
Nikapitiliza hadi kwenye meza yangu, nikavuta kiti na kukaa, nikashusha pumzi nyingi kujitahidi hasira yangu kuweza kushuka taratibu.
“Dany kaka vipi una tatizo?”
Nikatingisha kichwa sikutaka kuzungumza chochote kwa maana nimegundua hii simu imetegwa vinasa sauti na chochote ninacho kizungumza lazima Yudia na watu wake kuweza kusikia ninacho kisema. Rafiki yangu mmoja akagundua lugha yangu ya ukimya, taratibu akaanza kunisogelea na kukaa karibu yangu. Nikaitoa simu na kuiweka mezani, hata kabla ya huyu rafiki yangu kuishika simu ikaita na kujikuta sote wawili tukiitazama. Nikaipokea na kuongeza sauti ya kusikia hata aliyopo pembeni yangu anaweza kusikia kinachozungumza na mtu wa upande wa pili.
“Dany muda umeisha, nipo ripoti”   
“Sijafahamu alipo?”
“Ohoo ujinga wako ndio umekufanya usifahamu alipo Asma, basi ngoja nimtangulize Rose kuzimu”
Nikasikia mlio wa Risasi, na kuisikia sauti ya Diana akilia kwa uchungu.
“Kaka Dany….wame…muuaaa wifiiiii”
Nikaisikia sauti ya Diana akizungumza huku analia kwa uchungu sana, nikajikuta machozi yakinimwagika, hadi Khalid aliye kaa pembeni yangu akajawa na huzuni kubwa usoni mwake.
                                                                                          ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts