Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 45 na 46 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 45 na 46 )

Written By Bigie on Friday, March 16, 2018 | 2:06:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                              
ILIPOISHIA  
“Mariamuuuuuuuuuuu”
Niliisikia sauti ya Mama Marim iliyo zidi kunichanganya na kujikuta nikikaa chini sakafuni huku machozi yakinilenga lenga. Nikanyanyuka taratibu na kumtazama Mariam, jinsi alivyo lala hajabadilisha hata mkao, mapigo yake ya moyo yamesimama kabisa jambo lililo zidi kunichanganya maradufu na saa yangu ya ukutani inaonyesha ni saa mbili kasoro usiku na muda si mrefu Babyanka atakuja kunipitia kwa ajili ya kwenda Marekani kuifanya kazi ya muheshimiwa riaisi.

ENDELEA
Mlango wa chumbani kwangu ukagongwa na kuyafanya maoigo yangu ya moyo kuzidi kwenda kasi kwa maana ninatambu atakuwa ni mama Mariam. Nnikashuka kitandani kwa haraka, nikafungua friji nikatoa chupa yenye maji ya baridi na kumwagia maji hayo Mariam usoni. Cha kumshukuru Mungu, akakurupuka huku akiwa anagema sana.
Nikawahi kumziba mdomo ili asiweze kupika kelele zitakazo sikika nje kwa maana mama yake amesha fika.
“Dany”
“Shiii”
“Mariammuuuu”
Tuliisikia sauti ya Mama Mariam akiita akiwa uwani na ttayari alisha ondoka mlangoni mwangu. Wasiwasi ukaanza kumjaa Mariam, akaanza kushuka kitandani huku akiwa anahema, akajaribu kupiga hatua mbili mbele ila nikagundua kwamba mwendo wake umebadilika na ana chechemea.
“Mungu wangu, Dany mama si atajua kwamba nimeutoa usichana wangu”
 
“Jikaze utembee vizuri, hatokustukia”
Nilizungumza huku nikimkalisha kwenye sofa taratibu. Tukatazama usoni, hapakuwa na aliye muongelesha mwenzake, hata sauti ya mama Mariam inayo ita ikawa haiendelei tena.
“Ngoja nitoke nikamzuge mama yako, hakikisha unafanya unatoka humu ndani asije kukustukia”
“Sawa”
Nikachukua taulo langu na kujifunga kiunoni mwangu,  nikachukua sabuni yangu na kutoka chumbani kwangu, kwenye kordo sikumkuta mtu wa iana yoyote. Nikaelekea kwenye mlango wa mbele ambapo nilihisi naweza kumkuta mama Marim, kwa bahati nzuri nikakutana naye mlangoni akiwa anaingia. Nikamshika mkono na kutoka naye nje.
“Vipi mbona unamwagikwa na jasho?”
“Nilikuwa ninafanya mazoezi, nikaoge kwa maana kuna sehemu nahitaji kuelekea”
“Unaeleka wapi tena honey”
“Ninakwenda nje ya nchi kikazi, kwahiyo sinto kuwepo Tanzania kwa siku kadhaa”
“Jamani Dany, hata kiu yangu hujaimaliza na wewe unataka kuondoka?”
“Imetokea kwa dharula tu, ndio maana nilipo isikia sauti yako nikatafuta ili niweze kukueleza juu ya hili mpenzi wangu”
“Na safari hiyo unaondoka saa ngapi?”
 
“Saa mbili hii ndio naondoka, hapa nimemaliza kufanya mazoezi na ninahitaji kueleka bafuni, nijiandae niondoke”
Mama Mariam akatazama kila sehemu ya eneo hili la nje tulipo kisha akanikumbatia na kuanza kuniyonya mdomo wangu. Tukalifanya tendo hilo kwa dakika kadhaa kisha tukaachiana.
“Nakuomb nikaoge”
“Sawa honey, ila Marim umemuona?”
“Nilimuona pale nilipo rudi na nikamuomba ufunguo, baada ya hapo sikufahamu ni sehemu gani aliyo elekea”
“Yaani huyu mtoto sijui atakuwa amekwenda wapi, ngoja nikamtazame hapo mbele kwa mama Jenifa”
“Sawa”
Mama Mariam akanipiga busu la mdomo kisha akatoka getini, alipo funga geti kwa haraka nikaingia ndani moja kwa moja nikaeleka chumbani kwangu, nikaufungua mlango na kuingia ndani. Sikumkuta Mariam, nikashusha pumzi na kuelekea chumbani kwake, nikamkuta akiwa amesimama katikati ya chumba huku amefunga kanga kifuani.
“Mama yako amekwenda kwa mama Jenifa, sasa fanya ukaoge kisha urudi ulale sawa?”
“Sawa”
 
Tukatoka kwa pamoja, kisha akeleka kuoga na mimi nikarudi chumbani kwangu, nikalitoa shuka lenye damu kitandani kwangu na kuliweka chini ya uvungu, nikachukua shuka jengine na kulitandika vizuri, nilipo hakikisha chumba changu kipo vizuri, nikaanza kitoa nguo za kuondoka nazo haraka haraka, nikaziweka kwenye begi langu la mgongoni. Kila kiitu changu cha kusafiria ninakiweka kwenye meza, nikatoka na kuelekea bafuni na kukuta Mariam akiwa amemaliza kuoga. Kwa haraka haraka nikaoga na kurudi chumbani kwangu, nikaanza kuvaa kwa haraka. Nilipo hakikisha kwamba nimemaliza kuvaa, nikachukua simu ambayo nilipatiwa na kina Yudia. Nikaitoa laini na kuiwasha, nikatoka nje ya chumba changu, kwenye kordo hapakuwa na mtu yoyote nikausogelea mlango wa Mariam, nikaita kwa sauti ya chini kwa bahati nzuri akaisikia na kufungua mlango.
“Utatumi hii simu hadi nitakapo rudi”
“Asante sana Dany si Iphone hii?”
“Ndio”
Akataka kunikumbatia nikamzuia, nikarudi chumbani kwangu. Bastola zangu nikazichomea sehemu ambazo huwa ninazichomeka kila ninapo kuwa nazo. Nikabeba begi langu na kutoka nje ya chumba, nikaufunga mlango wangu na moja kwa moja nikaelekea nje, nikafungua geti na kukuta gari la Babyanka likiwa ndio linasimama. Nikafungua mlango wa gari na kuingia ndani.
“Umependeza Dany”
“Asante hata wewe umpendeza”
 
Taratibu tukaondoka mtaani kwetu na kueleka uwanaja ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
“Naomba unizime simu yako”
Babyanka akanipatia simu yake, nikaingiza namba za mama na kuiweka simu sikioni, Ikaanza kuita kwa muda kisha ikapokelwa.
“Shikamoo mama”
“Marahaba, mbona kila siku una namba mpya?”
“Simu yangu si imepotea”
“Ahaa haya vipi?”
“Diana amesha fika nyumbani?”
“Yaa amesha fika muda mrefu”
“Sawa, mimi nipo njiani ninaeleka uwanja wa ndege, ninakwenda Marekani”
“Marekani!!! Kufanya nini?”
“Kikazi mama”
“Eheee”
“Yaa ndio nimekupa taarifa hiyo”
“Sawa kuwa mkini tu”
“Sawa mama yangu, ila vipi mumefikia wapi katika kumkamata Yudia?”
“Bado anatafutwa na polisi?”
“Sawa pia kuna gari langu moja nilipewa na raisi, walanalo nisaidieni kulitafuta”
 
“Nitumie namba zake za usajili”
Nikamtajia namba za usajili za gari langu, kisha nikakata simu.
“Mama yako anaonekana ana kupenda ehee”
“Yaa ananipenda, mimi ndio mtoto wake wa kiume”
“Hivi ni kwa nini watoto wa kiume munawapenda sana mama zenu na watoto wa kike tunawapenda baba zetu?”
“Kusema kweli hili mimi sifahamu ila huwa linakuja lenyewe”
Tukafika uwanja wa ndege, tukashuka kwenye gari, tukashusha mabegi yetu na moja kwa moja tuakeleka kwenye ofisi maalumu za usalama, tukaorodhesha majina yetu na kukabidhi salaha zetu pamoja na funguo ya gari.
“Twendeni huku”
Tukaongozana na askari huyu wa ukaguzi, tukaingia kwenye moja ya ofisi na kumkuta mzee mmoja mweusi aliye valia nguo za kiaskari. Tukasalimiana naye na kutukaribisha kukaa kwenye viti. Akatupa moja ya faili tuweze kulipitia.
 
“Huyo ni Cosmas Damson, ni miongoni mwa wana Interpol ambao wapo nchini Marekani na ndio atakaye wapokea nyinyi na kuwaatia silaha, ndio maana tukaamua muweze kuziacha hapa Tanzania kwa maana kwa sasa mfumo wa ulinzi wa dunia umebadilika sana hususani mpelelezi kutoka nchi moja kwenda kufanya kazi nchi nyingine kubwa kama Marekani. Kuingia kwenu na silaha nchini Marekani kunaweza kuvuruga mfumo wenu wa kazi ambayo mumeagizwa kuifanya na muheshimiwa raisi”
“Je ana taarifa zetu?”
“Ndio anazo taarifa zenu hadi picha zenu anazo na atawapokea katika uwanaje wa ndege kuwapokea”
“Sawa muheshimiwa”
“Nawatakia kazi njema”
“Aante muheshimiwa”
Tukatoka kwenye ofisi hizo tukiwa na mabehi yetu moja kwa moja tukaeleka sehemu ya abiria kupumzika.
“Hii kazi inaweza kuwa ngumu sana mbele yetu”
“Kwa nini?”
 
“Yaani naanza kuiona dalili ya ugumu”
“Ndio mara yako ya kwanza kuelekea Marekani nini?”
“Yaa”
“Usijali, mimi ninapafahamu vizuri Marekani nilisha wahi kumpeleka mdogo wangu Diana masomoni, na nilikaa huko kwa miezi kadhaa”
Tukiwa tumekaa tunaendelea kuzungumza mazungumzo ya hapa na pale, tukaona kundi kubwa la askari wenye mbwa wakija usawa wetu, ikatubidi tusitishe kuzungumza stori zetu na kuwaangali, pasipo kuwa na wasiwasi wa aina yoyote. Gafla wakatuzunguka huku wakiwa wametunyooshea mitutu ya bunduki, jambo lililo tifanya tuwashangae.
“Daniel upo chini ya ulinzi”
Askari mmoja alizungumza huku akinisogelea na kujikuta nikisimama pia Babyanka akasimama.
“Kwa kosa gani?”
“La mauaji”
“Mauaji…..!!! Mauaji ya nani?”
 
“Hilo sisi halituhusu, ila unatakiwa kuongozana nasi”
“Hei ngojeni kwanza mutajua sisi ni wakina nani?”
Babyanka alizungumza kwa ukali sana huku akimtazama askari ambaye anazungumza na mimi.
“Hili sisi tunalifahamu, Dany ni NSS na wewe ni NPS”(National President Service).
“Hamuwezi kumkamata Dany ikiwa tupo katika kazi”
“Hilo sisi
Hatulifahamu tunacho kihitaji ni kumkamata kama tulivyo agizwa na bosi wetu basi”
Nikawatazama askari hawa pamoja na mbwa wao, nikamgeukia Babyanka aliye aliye fura kwa hasira. Nikamkonyeza, akaelewa, kwa kasi ya ajabu tukaanza kuwashambulia hawa askari kwa kuwatembezea kipigo huku mbwa wao tukiwadhibiti kwa kuwapiga na vitako vya bunduki walizo kuja nazo. Ndani ya dakika tano askari pamoja na mbwa wao wakwa wamelala chini, tukachukua mabegi yatu na kuanza kukimbilia sehemu ya abiria wanao elekea kwenye ndege wanapaswa kwenda. Askari wengine wakaanza kutukimbiza huku ving’ora vya hatari vikiwa vinasikika vizuri.
 
     Kadri ninavyo kimbia ndivyo jinsi nilivyo kuwa ninajiuliza kuhusiana na kesi hii ya mauji waliyo kuja nao hawa askari. Tukakimbilia moja kwa moja kwenye uwanja na kuingia kwenye moja chumba cha kuhifadhia mizigo na kujificha huku kwa muda.
“Mbona sielewi kinacho endelea Dany”
“Babyanka nakuomba utulie”
“Kutulia ndio naweza kutulia ila nielezee ni kitu gani kinacho endelea na ni mauaji gani ambayo umeyafanya”
“Hapa ninahisi ni jana nilivyo kwenda kumuokoa mdogo wangu, niliwez kupambana na watekaji baadhi na kuwaua, ila sijui hapo kosa langu mimi lipo wapi kwa maana nisinge waua mimi, wao ndio wangeniua”
“Ohoo Dany vitu kama hivyo unatakiwa kivizungumza mapema”
 
“Ila si nilimuambia raisi kwamba mdogo wangu ametekwa, mpigie aweze kutuokoa katika hili”
Babyanka akafikiria kwa sekunde kadhaa huku jasho likimwagika. Akatoa simu yake mfukoni na kuminya namba kadhaa kisha akaiweka sikioni.
“Ndio muheshimiwa”
“Samahani kwa usumbufu, tunataizo, kuna askari wanamuandama Dany na wanamuhisisha na kesi ya mauaji, nakuomba utusaidie mkuu”
Babyanka akaa kimya kidogo akisikilizia, akaanza kunitazama kwa umakini kisha akanipatia simu na nikaiweka sikioni.
“Ndio muheshimiwa”
“Huwa sikuzote sipendi watu wazembe na wajinga kama ulivyo wewe, umeua watu na unategemea msaada wangu wa nini, kama unayapende maisha yako jisalimisha mikononi mwa hao askaeri la sivyo utakufa”
Maneno ya raisi yakanishangaza sana, nikabaki nikiwa nimetoa macho, hata kabla sijafanya chochote mlango wa chumba cha mizigo tulicho jificha wakaingia askari wengi wakiwa na bunduki zao mikononi na kutuamrisha kunyoosha mikono yetu juu jmbo lililo zidi kuninyong’onyeza.

                                   AISIIIII……….U KILL ME 46

    Sikuwa na ujanja wa kufanya zaidi ya kunyanyua mikono yangu juu. Hata Bayabyanka akatii amri ya askari hao. Wakatusogelea kwa umakini na kutuvisha pingu. Tukatoka katika chumba hicho moja kwa moja wakatupeleka kwenye magari yao na kutuingiza. Njia nzima sikuzungumza chochote zaidi ya kuifikiria hii kesi ambayo ipo mbele yangu na nilihisi raisi anawesa kuwa msaada mkubwa kwangu ila ndio hivyo amenigeuka na kunikana kabisa. Tukiwa hatua chache kutoka uwanja wa ndege, gari za polisi ambazo kwa haraka haraka zipo sita, zikasimama. Nikashusha mimi na kulishwa kigunia kidogo cheusi kilicho nifanya nishindwe kuona kinacho endelea. Nikashangaa nikisukumwa na kuamrishwa kwamba niweze kutembea mbele.
“Ingia kwenye gari pumbavu wewe”
Nilisikia sauti nzito ya kiume ikizungumza huku nikisindikizwa na kofi zito la mgongoni. Nikaingia kwenye gari ambalo wala sijui ni gari la aina gani, nikaisikia milango ikifungwa tu, galfa nikaihisi kitu chenye ncha kali kikiingia kwenye shingo yangu upande wa kulia na taratibu usingizi mkali ukanipitia.
                                                                                                 ***
    Milio ya vyuma vinavyo gongwa gongwa, ndio vilivyo nifanya kuanza kuyafumbua macho yangu taratibu, kwa haraka sikuweza kuona chochoteza zaidi ya mawingu mawingu yaliyo tanda mbele ya uso wangu. Nikajitahidi sana kuyafikicha macho yangu ili niweze kuona hivyo vyuma vinagongwa na kina nani, kwa kitendo hicho cha kufikicha macho yangu, macho yangu yakaongeza ufanisi wa kuona mbele. Nikaona watu walio valia kaptula nyeupe pamoja na mashati meupe wakiwa wamefungwa nyororo za miguuni huku mikononi mwao wakiwa wameshika nyundo kubwa wakipasua mawe makubwa. 

Afya zao zimezohofika sana, kwa haraka nikazungusha kichwa changu kutazama hii sehemu ambayo nipo nikagundua kwamba tupo kwenye moja ya pango ambalo lina taa nyingi kila sehemu huku kukiwa na ulinzi mkali wa wanajeshi wenye silaha pamoja na mbwa wakubwa mara mbili ya mbwa ambao niliweza kukabiliana nao nikiwa katika uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere. Nikajichunguza na mimi, ninajikuta nikiwa nimevalia kapula nyeupe, na shati jeupe, huku miguu yangu ikiwa imefungwa nyororo ndefu inayo niwezesha kutembea.
Nikahisi labda nina ota kwa hichi ninacho kiona, nikafumba macho ili niweze kurudi tena usingizini ili hata nikifumbua macho yangu niweze kuona nipo sehemu nyingine. Ila haikuwa hivyo kwani kufumbua kwangu macho kukanifanya nimuone mwanajeshi mmoja mwenye mwili mkubwa akiwa amesimama mbele yangu huku ameshika bunduki, kichwani mwake amenyoa nywele zote na kukipaka mafuta mengi kichwa chake na kukifanya king’are nga’are.
“Simama wewe mtoto wa malayaa”
Alizungumza kwa ukali sana, taratibu nikanyanyuka huku nikiwa nimechoka sana, viongo vyote vya mwilini mwangu vinaniuma kisawa sawa.
 
“Nifwate”
Sikumjibu chohcote zaidi ya kutii amri, nikaanza kumfwata nyuma nyuma huku nikiendelea kuwatazama wafungwa hawa walio kundeana sana, wengine wanashindwa hata kufanya kazi y akupasua miamba hii, ila wanakutana na kipigo kikali kutoka kwa wanajeshi hawa. Tukakatiza kwenye kordo moja ndefu iliyi jaa taa zinazo fanya paonekane kama machana. Tukaingia kwenye maja ya chumba ambacho kina viti viwili pamoja na meza moja tu.
“Kalisha makalio yako hapa”
Akanionyesha kiti kilichopo mbele ya meza hiyo nikakaa pasipo kuwa na kipingamiza. Akatoka na kuniacha ndani ya chumba hichi. Kila nilipo jaribu kuvuta kumbukumbu zangu kufahamu nimefikaje hapa katika hili eneo, ninashindwa kabisa na kitu cha mwisho ninacho kikumbuka ni jinsi nilivyo amrishwa kuingia ndani ya gari hilo na kuchomwa na kitu chenye ncha kali ambacho moja kwa moja ninatambua ni sindano ya usingizi.
 
    Nikiwa katika mawazo hayo mlango wa chumba nilichopo ukafunguliwa kwa nguvu. Sikuamini macho yangu nilipo muona K2 akiwa ameingia huku ameshika faili moja, akalitupia mezani, kisha taratibu akavua koti lake la suti kisha akaliweka kwenye kiti kinacho tazamana na mimi.
“Kwa nini imekuwa hivi?”
Nilimuuliza K2 kwa sauti ya upole na unyenyekevu kwa maana sina ujanja wa kuseme kwamba nitoke kwenye mikono yake. Hakunijibu kitu cha iana yoyote zaidi ya kukaa kwenye kiti hicho. Akaanza kufunua faili  hilo lililo jaa picha nyingi wau walio  uwawa. Katika kuzitazama vizuri nikaweza kuzigundua kwamba picha hizo ni za majambazi walio mteka Diana na kwakushirikiana na wezangu tuliweza kuwadhibiti kikamilifu.
 
“Unawatambua hawa?”
K2 alizungumza huku akinigeuzai faili hilo, nikazitazama picha hizo kwa mara nyingine tena kisha nikamtazama yeye usoni mwake. Nikatingisha kichwa na kumueleza kwamba nina wafahamu.
“Nani aliye kupa oda ya kwenda kuwaua?”
Nikaka kimya huku nikikosa cha kuzungumza. K2 akasimama taratibu na kunifwata sehemu nilipo kaa.
“Nakuuliza ni nani aliye kupa oda ya kuwaua?”
“Walinitekea mdogo wangu, ndio maana nikaamua kufanya hivyo”
“Ohooo, walikutekea mdogo wako?”
“Nilkuuliza wewe na Lu…….”
Akanitandika ngumi nzito ya shavu iliyo nifanya nianguke na kiti changu chini. K2 pasipo kuwa na huruma akaanza kunitandika mateke ya tumboni huku akinishushia matusi mengi. Mlango ukafunguliwa na kwa haraka wakaingia wanajeshi wanne wa kike na kumshika K2 na kumtoa katika chumba hichi cha mahojiano. Machozi mengi yakanitiririka kwa maumivu makali niliyo yapata, mwanamke wambaye alinipa uhuru wa kuufanya mwili wake chochote nijisikiacho leo hii ananishushia kipigo kama hanifahamu.
 
“Nyanyuka”
Mwanajeshi aliye niiingiza kwenye chumba hichi alizungumza na mini, nikajikaza kume na kunyanyuka taratibu, sehemu ambayo nilichomwa kisu na Asma, ikaanza kuvuja damu iliyo nipa wasiwasi mkubwa sana, mwanajeshi huyo wala hakulijali hilo zaidi ya kuniongoza hivyo hivyo na kunipeleka kwenye chumba kingine chenye kijidirisha kidogo kwa juu na kunisukumia humo.
“Ohoooo Mungu wangu ni nini hichi jamani”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika. Chumba hichi hakina kitanda zaidi ya choo kimoja cha kukaa. Nikanza kujifungua fingo vya shati langu, nikaangalia kidonda changu na kukuta nyuzo zilizo kuwa nimeshonwa zimefumuka kidogo. Kwa kiganja changu cha mkono wa kushoto nikajiziba huku nikiwa nimekaa sakafuni.
    Maskaa yakazidi kukatika na kwenda mbele, mlango ukafunguliwa, akaingia mwanajeshi mwengine aliye niletea sahani iliyo jaa ubwabwa na maharage, hakunisemesha kitu chochote zaidi ya kuweza sahani hiyo mbele yangu na kutoka kabla hajafika mlangoni nikamuita.
 
“Sahamani kaka”
Akasimama, taartibu akageuka na kunitazama.
“Sahani kaka, hapa nipo wapi?”
Akatingisha kichwa chake, kwa ishara ya macho akaniambia niweze kutaza kwenye koza za chumba hichi kwa juu, nikafanya hivyo nikaona kamera za ulinzi pamoja na kinasa sauti, akageuka na kutoka ndani ya chumba hichi. Kutokana nina njaa, sikuona haja ya kuacha kuto kula chakula hichi nilicho letewa taartibu nikaanza kukila, japo sio kitamu ila nikaendelea kukila hivyo hivyo hadi nikakimaliza.
Masaa siku zikazidi kwenda, huku kila siku nikiletewa chakula kwa mara moja kwa siku.
Nywele zangu zikazidi kukuka, pamoja na ndefu, kiufupi nilizidi kuchakaa, na kuwa mbaya sana.  Nikiwa nimeamka kutoka usingizini, kabla sijaanza kufanya mazoezi mlango ukafunguliwa. Wakingia wanajeshi wawili walio valia vitambaa vyeusi machoni mwao huku wakiwa wamayaacha macho yao wazi tu.
 
Mmoja wao akaniamrisha kunyoosha mikono mbele, nikafanya hivyo na wakanifunga pingu za mikononi, kutokana miguuni nimefungwa nyororo ndefu hawakuwa na haja ya kuweza kunifunga na miguu yangu.
Mmoja akatangulia mbele na mwengine akawa nyuma yangu, tukaanza kutemeba kwenye kordo hii ndefu nyenye vyumba vingi. Tukatokea kwenye kiwanja kimoja kilicho jaa gari nyingi za jeshi. Nikakutana wanajeshi wengine wanne walio valia kama hawa wawili walio kuja kunichukua, wakiwa wamesimama na bunduki zao.
Hapakuwa na mazungumzo zaidi ya kuniongoza na kuningiza kwneye moja ya gari jeusi ambalo ni kubwa kiasi. Ndani ya gari hilo nikaingia na wanajeshi wanne, wakiwemo wawili walio kuja kunichukua. Huku wengine wawili wakikiingia mbele ya gari hilo na safari ikaanza.
Tangu kuzaliwa kwangu sijawahi kuona hili eneo nililipo wala kulisikia kwenye maisha yangu. Safari ikazidi kusonga mbele huku wanajeshi nilio kaa nao kwenye gari wakiwa makini sana katika kunilinda.
 
    Safari ikazidi kusonga mbele kwa kupitia kwenye kioo cha mbele cha gari hili nikaweza kugundua ni wapi tulipo. Ni katika mji wa mlalo, wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Imekuwa ni rahisi kwa mimi kuweza kuufahamu mji huu ni kuutokana nimesoma katika shule moja ya dini iliyopo kwenye eneo hili. Safari ikazidi kusonga mbele huku kwenye gari sote tukiwa kimya. Tukapita maeneo ya Lukozi, kisha tukafika kwenye eneo la Magamba kwenye msitu mmoja uno itwa Kha’ndekapaa. Gafla gari likayumba huku kwa nyuma tukiwa tumeangukiana. Dereva akajitahidi kwa uwezo wake na kuliweka gari sawa huku akifunga breki. Wanajeshi wote wakaniwahi na kuniweka sawa, huku kila mmoja akwia na wasiwasi mkubwa.
“R one, ni nini kinacho endelea?”
“Gari imepasuka tairi la mbele”
“Ok wote kwa pamoja tuweni makini mmoja abaki kwenye gari na mfungwa wengine tushuke kuimarisha ulinzi”
“Sawa mkuu”
 
“A one baki  kwenye gari”
“Sawa mkuu”
Sauti ya huyu mwanajeshi aliye ambiwa abaki na mimi kwenye gari na ndio aliye kuja kunichukua kwenye chumba nilicho kuwepo, ikanishangaza sana, nikajaribu kuvuta kumbukumbu zangu ni sehemu gani ambayo niliweza kuisikia sauti hii, ila sikuweza kukumbuka. Wanajeshi wakashuka huku wakiwa makin katika kuimarisha ulinzi wa eneo hili.
Waakanza kufanya matengenezo ya gari lao, huku huyu A one, akinotazama kwa umakini huku bunduki yake akiwa ameishika vizuri mkononi mwake.
“Muna nipeleka wapi?”
Akaka kimya pasipo kunijibu kitu chochote, akatazama nje na kuwaona wezake wawili wakiendelea kulioshuhulikia  gari huku mmoja wengine wakiwa wameimarisha ulinzi katika barabara hii. Isitoshe msitu huu ni msitu ambao unatisha sana kwa wingi wake wa miti na kipindi cha nyuma nilipo kuwa ninasoma, majambazi walikuwa wakiteka magari katika eneo hili na kuwapora kila kitu abiria na madereva.
 
A one akatoa funguo ya pingu na kunipatia, sikujua maana ya yeye kufanya hivi ila akanikonyeza, nikaaificha funguo hii, baada ya kumuona mwanajeshi mmoja akichungulia. Alipo ona tupo salama, akaendelea kuimarisha ulinzi. Nikaanza kujifungua taratibu huku nikiwa makini, nilipo maliza kujifungua pingu hizo, akanipatia fungua nyingine za kufungua pingu za miguuni. Nikafanya haraka haraka, kisha akanionyesha bastola yake alipo ichomeka, nikaichomoa kwa haraka. Nikaikoki tayari kwa mashambulizi, taratibu tukanyata kwenye mlango, nikawatazama wanajeshi hawa jinsi walivyo kaa, nikautazama msitu huu na njia ambayo ninaweza kupita nikitoroka. Kwa kasi ya ajabu nikajirusha nje ya gari huku nikifyatua risasi kwa wanajeshi walio shika bunduki. Shambulizi langu likasaidiwa na A one ambaye naye yupo bega kwa bega na mimi katika kunisaidia.
 
    Wajeshi watano wote tukafanikiwa kuweza kuwaua. Kwa haraka, nikamvu mwanajeshi mmoja nguo zake, nikachukua bastola za kutosha na kuanza kuingia msituni nikiwa nimeongozana na A one. Pasipo kupumzika tukazidi kukimbilia ndani yam situ kuhakikisha kwamba tunaondoka kabisa karibu na eneo la tukio kwa manaa muda si mrefu jeshi linaweza kutumwa kututafuta.
“Naomba….naomba nivae hizi nguo”
Nilizungumza huku nikisimama nina hema sana. A one, akasimama na kunitazama usoni. Kwa ishara akaniambia nina weza kuvaa nguo  hizo. Kwa haraka haraka nikavua nguo zangu hizi za kifungwa ambazo zinanuka, tangu nivalishwe siku niliyo ingia kwenye gereza hili ambalo lipo maeo ya Kitivo, sikuweza kubadilisha nguo. Kwa haraka haraka nikazivaa nguo hizi za kijeshi. Nilipo hakikisha kwamba nipo poa, tukaendelea kusonga mbele, pasipo kufahamu tunapo elekea ni wapi.
“Huku”
A one alizungumza huku akiongoza msafara huo wa kukimbia, kusema kweli hadi sasa hivi sijamfahamu kwamba yeye ni nani. Hadi inafika saa mbili usiku bado tukawa kweye msitu huu wa kiutisha.
 
“Nimechoka naomba tumpumzike”
Nilizungumza huku nikiinama, mikono yango nikaiweka kwenye magoti nikizidi kuhema sana. A one, akaninyoshea bastola yake kwa ishara akaniomba ninyanyuke na kuendelea na kukimbia. Sikuwa na jinsi zaidi ya kukaza moyo. Tukazidi kukimbia huku nikiwamfwata kwa nyuma. Tukafika kwenye moja ya njia inayo ruhusu gari kupita japo ipo poridini. Akasimama huku akitazama barabara hiyo, akatoa karatasi moja mfukoni mwake pamoja na kijitochi kidogo, akaangalia ramani ya msitu huu, alipo ielewa akaanza kuongoza njia huku tochi na karatasi yake akivizudisha mfukoni. Kutokana na mwanga wa mbalamwezi ulituwezesha kuona tunapo elekea. Tukafika mbele tukakuta gari moja jeusi aina ya BMW X5. Kidogo nikasita A one akalisogelea karibu, akagonga kwenye kioo la upande wa dereva, kioo kikashushwataratibu, sikuamini macho yangu nilipo muona mama yangu akiwa ndani ya gari hilo. Kwa haraka akashuka na kunifwata kwa kasi, akanikumbatia kwa nguvu huku sote tukiangua kilio cha uchungu. Mama akaniachia huku akinitazama usoni mwangu, akanishika uso wangu huku  akitingisha kichwa akiendelea kulia sana. Akamgeukia A one na kumkumbatia naye kwa nguvi kisha akamuomba avua kitambaa alicho jifunga kichwani. Macho yakanitoka, huku mapigo ya moyo yakininienda kasi, kumbe mtu aliye nisaidia ni Asma, ambaye siku zote nilikuwa ninamtafuta kama adui yangu.
 
ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts