Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 47 na 48 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 47 na 48 )

Written By Bigie on Saturday, March 17, 2018 | 2:05:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   

Kidogo nikasita A one akalisogelea karibu, akagonga kwenye kioo la upande wa dereva, kioo kikashushwa taratibu, sikuamini macho yangu nilipo muona mama yangu akiwa ndani ya gari hilo. Kwa haraka akashuka na kunifwata kwa kasi, akanikumbatia kwa nguvu huku sote tukiangua kilio cha uchungu. Mama akaniachia huku akinitazama usoni mwangu, akanishika uso wangu huku  akitingisha kichwa akiendelea kulia sana. Akamgeukia A one na kumkumbatia naye kwa nguvu kisha akamuomba avue kitambaa alicho jifunga kichwani. Macho yakanitoka, huku mapigo ya moyo yakininienda kasi, kumbe mtu aliye nisaidia ni Asma, ambaye siku zote nilikuwa ninamtafuta kama adui yangu.

ENDELEA
Nikamsogela Asma huku nikiwa nimekunja ngumi mkononi mwangu. Nikakaribia na kumkaba koo lake na kumuegemeza kwenye gari kwa nguvu huku nikiwa na hasira kali.
“Dany unafanya nini?”
“Mama huyu ndio aliye nichoma mimi na kisu nikizani kwamba ni mtu mwema kwangu”
“Dany nalijua hilo, acha kufanya hicho unacho kifanya”
Mama alizungumza kwa sauti ya msisitizo huku akiniangalia, sikutaka kumuachia Asma koo lake, nikazidi kumkaba kwa nguvu.
“Dany kwa nini unataka kumuua mzazi mwenzako?”
Maneno ya mama yakanifanya nistuke sana huku taratibu nikiulegeza mkono wangu, nikamtazama mama nikaona jinsi anavyo mwagikwa na machozi usoni mwake. Hata Asma mwenyewe machozi yanamwagika, hakunifanya kitu cha aina yoyote zaidi ya kukubaliana na mimi katika kumkaba koo lake.
“Mzazi mwenzangu?”
“Yaa Dany, una mtoto wa kike”
Nikamgeukia Asma na kumtazama, akatingisha kichwa na kunihakikishia kwamba ana mtoto wa kike.
“Naomba unieleze huyo mtoto imekuwaje kuwaje?”
“Ingia kwenye gari kila kitu tunakwenda kukizungumza nyumbani”
 
Mama alizungumza huku akiwa amenishika mkono wangu wa kulia. Taratibu nikajikuta nikiingia kwenye gari huku nikiwa nimejawa na mawazo mengi kichwani mwangu. Mama akawasha gari na kuondoka eneo hili. Kwenye gari ukimya ukatawala, hapakuwa na mtu ambaye  anazungumza jambo. Mama akasimamisha gari kwenye jumba moja lililopo katikati ya msitu maeneo haya haya ya Lushoto. Jumba hili limejificha sana na wala sio rahisi kwa mtu mwengine kuweza kuliona. Tukashuka kwenye gari na kuingia ndani. Sebleni nikamkuta Diana akiwa amembeba mtoto mchanga wa kike ambaye kaika kumuangalia tu usoni mwaili wangu mzima ukasisimka, na sura yake imeendana na mimi kabisa.
    Diana akanifwata na kunikumbatia huku akimwagikwa na machozi. Taratibu akanikabidhi mwanagu niliye mpokea kwa mikono yangu miwili. Asma akashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio kikubwa huku akinitazama usoni mwangu, nikamvuta karibu yangu na kumkumbatia na mwanagu. “Nimekumbuka sasa”
 
Nilizungumza maneno hayo huku nikimtazama Asma usoni, kwa maana siku ambayo tulikutana kimwili anisha wahi kuniambia kwamba nimpatie mtoto japo nilimuuliza kuhusiana na maneno yake hayo yana maana gani ila anikataa na kudai ni burudani ninayo mpatia kitandani.
“Dany namuomba mtoto, Asma atakupeleka chumbani kwenu na atakufanyia usafi wa mwili”
“Sawa mama”
Nikabidhi mama mtoto, kisha Asma akanishika mkono, tukaondoka sebleni huku tukiwaacha Asma na mama wakitutazama kwa furaha. Tukaingia chumbani kwetu, kitendo cha kufunga mlango Asma akanikumbatia na kuanza kuninyonya mdomo wangu. Kutokana na uchu mkali nilo kuwa nao kwa kipindi kirefu ambacho nimekaa kwenye grereza, sikutaka kuipoteza nafasi hii anayo nipatia Asma. Sikutaka manjonjo mengi, nikamvua suruali yake ya kijeshi hadi ikafika magotini na mimi nikafungua zipu na kumtoa jogoo wangu, nikaishusha chupi yake na kuanza kukila kitumbua chake huku nikiwa nimemuinamisha na ameshikilia ukuta. 
 
    Asma kama kawaida yake aliyo barikiwa na Mungu, hakuacha kunikatikia kiuno, huku akitoa miguno ya kusisimua. Nikajikuta nikiwatoa waarabu weupe, ila jogoo akaendelea kusimama na kuunganisha mchezo. Mechi ikazidi kuwa kali hadi pale hamu ilipo katika ndipo nikamuachia Asma aliye choka sana. Tukakumbatiana kwa nguvu huku miili yetu ikiwa inamwagikwa na jasho.
“Twende ukaoge mume wangu”
Asma alizungumza huku akinishika mkono, taratibu tukaelekea bafuni. Tukavua nguo zote, nikasimama kwenye kioo, bado kidogo nikimbie kwa maana uso wangu umejaa mandevu ambayo ninaweza kujifananisha na gaidi moja wa Dunia anaye julikana kwa jina la Osama Bin Laden. Manywele marefu nayo yakapoteza kabisa muonekano wangu. Hata ule uzuri ambao nilikuwa nao umepotea kabisa.
“Pole sana Dany wangu, ni mateso makubwa ambayo wameweza kukupatia”
 
Asma alizungumza huku akichukua mashine maalumu  ya kunyolea ndevu na kunipaka dawa maalumu, ya kunyolea ndevu.
“Nina kipindi gani mimi kuwa gerezani?”
“Ni mwakana na miezi nane sasa”
“Mungu wangu?”
“Yaa, nimebeba mimba ya mwanao hadi nimejifungua. Na mtoto ana miezi nene sasa”
Nikajikuta nikifumba macho kwa uchungu na hasira kali ambayo nimeibana kifuani mwangu kwa kipindi kirefu. Nikiwa kama mfanyakazi wa serikali tena mpelelezi, siku stahili kuweza kufanyiwa hili nililo fanyiwa na serikali yangu pamoja na raisi wangu.
“Ilikuwaje kwa uapande wako baada ya kukamatwa pale banki”
“Niliachiwa, kwa maana nilikuwa katika kazi maalumu ya kumpeleleza Jumaa na kundi lake lote na wale ni watu ambao wapo chini ya K2”
 
“Una taka kuniambia kwamba wewe sio jambazi?”
“Ndio, mimi ni mpelelezi kutoka NPS, niliifanya kazi hiyo kwa siri sana pasipo mtu yoyote kuweza kufahamu. Kazi hiyo niliachiwa na raisi aliye pita ya kuweza kuchunguza kundi la majambazi ambao katika kipindi chake cha madaraka waliweza kumtesa na kumsumbua sana”
Asma alizungumza huku akiendelea kuninyoa, nikabaki nikiwa nimejawa na mchangao kwa maana katikakumtazama wala huwezi kufahamu kwamba ni mpelelezi na ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuigiza misha ya unyonge kwa maana kipigo alicho kuwa anapatiwa na Jumaa ni kipigo ambacho kwa msichana mwengine ni lazima kuweza kuachana na ndoa hiyo.
“Japo kwa sasa sipo katika kitengo hicho, nimejitoa kutokana na kuona mambo yanayo endelea katika kitengo changu yamejaa usaliti mkubwa”
“Hawajakutafuta kwa sababu umeacha kazi yao?”
“Nilifanyiwa mpango na raisi mstafu na kunipeleka katika gereza lile uliopo, siku zote zikufahamu kwamba upo pale, kwa maana chumba chako hakikuruhusiwa mu yoyote kuingia zaiid ya yule ambaye alikuwa anakuletea chakula”
“Amri hiyo ya kufungiwa alikuwa anaitoa nani?”
“Raisi, na siku ya leo alihitaki upalekwe kwenye kikosi maalumu cha kwenda kufanya kazi Pakistani, ambapo kulikuwa na mpango wa wewe kwenda kuuwawa”
Maneno ya Asma yakazidi kunijaza chuki dhidi ya riasi aliyopo madarakani.  Asama akamaliza kuninyoa ndevu, akachukua mashine ya kunyolea nywele na kuanza kuninyoa taratibu.
 
“Ninyoe nywele zote”
“Sawa”
Ukimya ukatawala huku mngurumo wa mashine ya kunyolea nywele ukitawala ndani ya bafu. Ndani ya dakika kumi kichwa changu kikawa hakina nywele hata moja. Nikasimama mbele ya kioo na kujitazama, sura yangu sasa ambayo nilisha zoea kuiona imerudi sawa sawa.
Nikafungua maji ya bomba la mvua, yakaanza kunimwagikia mwilini mwangu. Uchafu mwingi wa nongo ukayabadilisha maji yanayo tiririka na kuingia kwenye kijishimo cha kutolea maji kwenye bafu hili. Asma akaanza kunisugua na dodoki, zoezi la kunisafisha mwili likachukua zaidi ya nusu saa, sasa hata rangi yangu ya mwili ikaanza kurudi taratibu na kubaki nikiwa katika muonekano ulio zoelekea kuonekana mwilini mwangu.
Tukatoka bafuni baada ya Asma na yeye kuoga, nikajilaza kitandani huku nikiwa ninafikiria kitu cha kufanya. Asma akalala pembeni yangu.
“Dany huu ni wakati wetu wa kulipiza kisasi kwa wale wote ambao wametufanyia unyama na ukatili. Tazama jisni malengo yako, yangu ya mama yalivyo vunjika”
“Ya mama kivipi?”
 
“Mama alisha fukuzwa kazi, tena kwa shutuma mbaya sana”
Asma alizugumza huku akinyanyuka kitandani, akapiga hatua nadi kwenye droo ya dreasing table na kutoa gazeti moja na kurudi nalo kitandani. Akanikabidhi na taratibu nikaka kitako huku nikilifungua. Nukakutana na kichwa cha habari kinacho sema MKUA WA MKOA TANGA AIBA BILIONI MIA MOJA.
Taarifa hiyo nikataza tarehe yake na mwaka wake nikaona ni ya mwaka juzi na hadi sasa imepita mwaka.
“Hiyo taarifa ilitengenezwa na mkuu wako wa NSS, mis K2. Na yeye pia ndio aliye husika katika kuhakikisha kwamba mama anafukuzwa kazi na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufilisiwa kila kitu alicho kuwa nacho.”
“Hii nyumba mama aliweza kunielezea kwamba aliijenga akiwa na baba yenu, japo nyinyi hamkulifahamu hilo ila ameijenga na leo ndio inayo tusitiri kwa kuishi humu japo ni porini sana ila tuna amani sana”
“Naomba suruali kama ipo?”
Asma akafungua kabati na kunitolea suruali pamoja na tisheti, nikavivaa kwa haraka kisha nikatoka kwenye chumba chetu na kuelekea sebeleni. Nikamkuta mama akiwa amekaa peke yake.
 
“Diana yupo wapi?”
“Amekwenda kumlaza mtoto”
Nikaka kwenye sofa la pembeni na kumtazama mama usoni, ujio wangu uliweza kumuashiria kwamba nina mambo mengi ambayo ninahitaji kuweza kuzungumza naye.
“Mama naomba unieleze kitu kinacho endelea kwenye hii familia kwa sasa”
Mama akaka kimya huku uso wake akiwa ameuinamisha chini, akashusha pumzi nyingi kisha akanitazam usoni mwangu tena.
“Dany maisha yetu kwa sasa sio maisha kama yale uliyo wahi kuishi pale awali. Mama yako sio mtumishi tena kwenye hii serikali. Utajiri hadi wa urithi alio kuwa ameuacha marehemu baba yako nimepokonywa. Lati nisinge kuwa na akili ya kumiliki hili jumba, leo hii ingekuwa ni aibu kubwa sana kwenye maisha yetu”
“Imekuwaje kuwaje mama, ni kwa sababu yangu mimi au?”
“Sio kwa ajili yako wewe na wewe usijilamu kwa kile ulicho kifanya kwa maana ulikifanya hicho kwa ajili ya kuyaokoa maisha ya mdogo wako, ndio maana ikawa hivyo”
“ Mama nitahakikisha mali na utajiri wa baba yangu unarudi, na ni kweli ulichukua hizo pesa?”
 
“Mwangu nimekuwa nikiishi kwa kuisimamia haki, sikuwahi kuchukua pesa ya serikali kwa matumizi yangu binafsi nilisingiziwa”
Nikamtazama mama kwa muda, kisha nikanyanyuka na kurudi chumbani, nikamkta Asma akiwa anafanya usafi wa chumba chetu.
“Kesho ninahitaki kueleka Tanga mjini, kuna vitu nahitaki kuhakikisha kwamba vinarudi kwenye mikono yetu”
“Dany haujawa sawa kwa kuweza kufanya kazi hiyo unayo taka kwenda kuifanya”
“Ninaweza kuifanya, hakikisha kwamba unailinda familia vizuri, na unamlinda mwangu vizuri sana”
“Ila hadi sasa hivi mtoto hatujampa jina lolote zaidi ya kumuita Baby”
“Mulikuwa muna subiri nini?”
“Tulikuwa tunahitaji wewe kurudi ndio uweze kumaptia jina”
“Ahaaa hivi ilikuwaje hadi ukafahamu kwamba mimi nipo kule”
“Wapi?”
“Kwenye lile gereza?”
“Kuna siku nilipata nafasi ya kuingia kwenye chumba cha mawasiliano hapo ndipo nilipo kunona ukiwa katika kile chumba kwa maana tulisha kutafuta sana pasipo kupata mafanikio ya kukuona”
 
“Niandalie silaha zangu kesho ninaianza kazi yangu, nitahakikisha raisin a K2 wanalipa katika hili”
“Kuwa makini mume wangu kwa maana watu una dili nao wana nguvu sana”
“Usijali mke wangu”
“Nikundalie chakula?”
“Hapana sina haja ya kula kwa usiku wa leo”
“Ila hujakula chochote tangu asubuhi”
“Yaa asubuhi naamini utanipikia chakula kitamu”
Asama akapanda kitandani na kunikalia kiunoni mwangu.
“Dany kila nikutazamapo huwa natamani sana kupata penzi lako, hata mtoto uliye nipatia ameweza kunipa furaha kubwa kwenye maisha yangu na kila siku niliweza kumkumbuka kupitia wewe”
“Kweli?”
“Ndio mume wangu, naamini hapa tutakuwa tunatafutwa ila nitahakikisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri ni lazima tuwaonyeshe hawa wanaharamu kwamba tunaweza kuitingisha hii ichi”
Maenoya Asma yakazidi kunipandisha munkari wa kutamani kulipiza huki walicho nifanyia K2 na raisi.
“Una mpango gani mke wangu?”
“Mpango nilio kuwa nao kwa sasa ni kusoma mazingira ambayo wanayo kwa sasa, kisha kisasi chetu sisi tunakirudisha kupitia familia zao”
Nikaa kimya huku nikitafakari kitu cha kufanya, wazo la Amsa ni wazo zuri sana nikaona hilo ndio nitakalo anza nalo kulifanyia kazi pale kutakapo pambazuka.

                         AISIIIII……….U KILL ME 48

    Sikupata suingizi kabisa, kila muda nikawa ninawaza ni kitu gani ambacho ninaweza kukifanya kwa hawa washenzi walio haribu maisha yangu. Nikamtazama Asma na kumkuta akiwa amelala fofofo, nikashuka kitandani, nikachukua suruali yangu pamoja na tisheti. Nikapiga hatua hadi kwenye dreasing tabla nikafungua droo moja na kutoa bastola pamoja na magazine yake. Nikaichomeka vizuri na kutoka nje. Japo kuna baridi kali usiku huu ila sikulijali hilo. Nikaanza kuizungu nyumba yetu kuhakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha. Nilipo ridhika na ukaguzi wangu nikarudi chumbani kwangu.
Hadi kuna pambazuka sikufumba kabisa macho yangu, kama kawaida yangu niliyo jizoesha tangu nikiwa nipo gerezani, nikaanza kufanya mazoezi ya viungo, na kuzidi kuimarisha mwili wangu. Nilipo maliza nikaingia bafuni na kuoga.
“Umeamkaje”
Nilimsalimia Asma aliye kaa kitandani, bado akiwa na mawenge ya usingizi usingizi.
“Salama baby, umeamka saa ngapi?”
“Muda mrefu sana”
“Ngoja nikamchukue mtoto”
“Sawa”
 
Amsa akachukua tenge na kujifunga kifuani kisha akatoka chumbani na kuniacha nikiwa ninavaa nguo kujiandaa kwa mpango wangu mzima wa kuhakikisha kwamba kisasi changu ninakifanya kwa kutumia akili kubwa sana na si kutumia nguvu.
Asma akarudi akiwa amembeba mtoto wangu, akanikabidhi mikononi mwangu. Japo ni mtoto wa kike ila ana fanana sana na mimi.
“Weeee”
“Mpe jina mwanao, kwa maana jina la Baby sio jina official”
“Mmmmm kuanzia leo atachukua jina la Anjelina”
“Waooo jina zuri”
“Yaa hilo ndio ninalo lihitaji”
Asma akaingia bafuni na mimi nikatoka na mwanagu hadi sebleni na kumkuta mama akitazama Tv, taarifa ambazo zipo kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni kutoroka kwangu, cha kushanga zaidi ni kwamba, wananitangaza maka gaidi.
“Jamani kwa nini mwanangu wanaamua kumfanyia hivi”
Mama alizingumza kwa lugha ya unyonge huku akiitazama taarifa hiyo ya asubuhi inayo tangazwa na kituo cha Star Tv. Nikaka kwenye sofa huku nikiwa nimembeba Anjelina, nikatazama picha zangu zinazo onyeshwa kwenye kituo cha hicho huku baadhi zikinionyesha nikiwa na ndevu nyingi.
 
“Mama”   
“Mmmmm”
“Nimempa mjuku wako jina lako la Anjelina”
“Weee Dany”
“Yaa mama nimeamua kumpa jina hilo kwa maana linampendeza na sikuona haja ya kuweza kuchagua majina ya watu wengine wakati mama yangu wewe upo”
“Asante sana mwangu, vipi hiyo taarifa hapo umeielewa?”
“Yaa, nina mpango wa kwenda Tanga mjini leo, kuhakikisha kwamba kila kitu kilicho potea mikononi mwetu kinarudi kwenye mikono yako”
“Mmmmm sasa mwangu, huoni kama hiyo ni hatari na wanaweza kukukmata tena na ikawa ni kesi nyingine?”
“Kwa sasa mama roho yangu na nafsi yangu zimebadilika sana, hakuna anaye weza kunikamata. Kama niliweza kuyahatarisha maisha yangu kwa ajili ya raisi, alafu leo hii pasipo sababu yoyote wananiita mimi gaidi. Sasa nataka maneno yao wanayo yazungumza yawe kweli”
 
“No no no Dany, sikukulea hiyo na wala sihitaji uwe hivyo mwanangu. Tazama Anjelina anakutegemea baba yake kuweza kuishi maisha marefu ili aweze kufaidi matunda yako. Tanzama mdogo wako, mtazame mke wako, nitazame mimi sisi site macho yetu yapo kwako. Familia pasipo baba bado haijawa familia mwangu”
Mama alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, japo maneno anayo yazungumza yana uzito kwenye maisha yangu. Ila nimesha apa kwa Mungu kwamba hakuna anaye weza kuyabadilisha yale niliyo weza kuyapanga. Nilio wawekea nia nao ni lazima waweze kulipa kwa kile walicho nifanyia.
 
“Dany nakuomba mwangu, kaa nasi sihitaji urudi huko mjini, kuishi kwako hapa kutaongeza furaha, amani na upendo.”
“Mama nina kupenda, wewe kwanini wakuite mwizi, kwa nini mimi wakaniweke huko gerezani kwa miaka zaidi ya mmoja na miezi yake. Kwa kosa gani, kwa mdogo wangu kutekwa na watu ambao wanafanya kazi chini ya muamvuli wa serikali eheeee”
Nilizungumza kwa hasira hadi mwanagu Angelina akaanza kulia, Diana kwa haraka akanifwata na kumchukua Angelina na kuondoka naye.
“Mama sisi pia ni watu, tuna haki, maisha yetu hayawezi kuharibiwa na watu wachache mama, nahitaji kuwaonyesha kwamba sisi sio watu wabaya ila ubaya wameutafuta kwetu. Nimeishi miezi hiyo nikiwa kama mnyama. Siogi, fifui sitoki nje, naishi na kinyesi changu ndani ya chumba unahisi kwamba hayo ni maisha mama yangu eheee”
 
Ni wewe na Asma tu ndio munao weza kusema kwamba sikuwa ninatoa harufu, ila nilikuwa ni mchafu, nanuka. Leo hii mama kweli nisiwalipizie kisasi wale walio fanya hivi?”
Niliendelea kuzungumza kwa ukali huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Taratibu mama akanyanyuka kutoka kwenye sofa alilo kali na kuja kujaa jaribu yangu. Taratibu akaanza kufuta machozi yangu.
“Dany wanangu ninaelewa ni uchungu wa kiasi gani ulio kuwa nao ila nakuomba utulie, nakuomba utazame familia kwanza”
“Mama familia yangu ninaipenda tena sana, tambua leo hii ninkamatwa kwa kuitwa gaidi, watu wanao nifahamu, waliokuwa wakiniheshimu leo hii watanischukuliaje mimi, eheee. Leo nikikamatwa tambua wanakwenda kuninnyonga, so ni familia ipi nitakayo iangalia. Mwanangu atakapo kuwa atakuja kujivunia kama alikuwa na baba aliye nyongwa kwa kuitwa gaidi kwa kosa la kusingiziwa.”
 
“Mama ninakuomba  unipatie baraka zako tu, kama huyo nipatia nitafanya kile ninacho hitaji kukifanya. Hata baba huko alipo nina imani atakuwa akubaliani na kile unacho kizungumza. Atafurahi pale atakapo ona ninaweza kurudisha mali alizo zotafuta kwa miaka yake yote ya uhai wake zinarudi kwenye mikono ya hii familia na hilo ndio jambo la msingi mama”
Mama akanitazama huku akishusha pumzi nyingi, kwa kile nilicho kizungumza, kikamfanya mama kuishika mikono yangu yote miwili huku akimwagikwa na machozi, akaiweka kifuani mwake.
“Nakuruhusu Dany wangu, nakuomba  urudi na ushindi mwangu”N
“Asante mama”
Nikanyanyuka, nikageuka nyuma nikawakuta Dianana Asma awakiwa wamesimama huku nyuso zao nao zikiwa zimejawa na machozi mengi. Wakanifwata na kunikumbatia kwa nguvu, naye mama akasimama na kunikumbatia huku machozi yakitumwagika.
 
“Nawaahidi nitarudi na ushindi”
Nilizungumza huku nikiwaachia, Asma akanishika mkono na kuniomba nikae kwenye kiti kilichopo pembezoni mwa meza ya chakula.
“Naomba unywe chai hii mume wangu, niliyo kuandalia”
Asma alizungumza huku akijifuta machozi usoni mwake. Sikuwa na kipingamizi chochote, nikaanza kunywa chai na wote wakajumuika na mimi na tukaendelea kunywa chai.
“Anjelina yupo wapi?”
“Anjelina, ndio nani?”
“Ahaa Anjelina si mtoto wangu, nimempa jina la Anjelina”
“Alafu muna tabia mbaya jamani, mimi hata hamujaniambia Shangazi wangu anaitwa Anjelina”
“Basi ndio ufahamu shangazi yako anaitwa Anjelina”
“Jamani naombeni simu kwa manaa huko ninapo kwenda nitahitaji kuwasiliana na nyinyi”
“Simu, mimi nitakupa”
“Hapana Asma usimpe, huyo Diana anatakiwa kumpa kaka yake simu, kwa mana namuona na simu simu nyingi tu”
“Kwani mimi nimekataa mama kumpa simu, si wifi tu aliniwahi kuzungumza”
“Sawa, mama hivi gari ni hili moja tu?”
“Hapana kuna gari kama tatu, nitakuonyesha baada ya kula”
“Sawa”
 
Tukamaliza kula, mimi na mama tukatoka nje, tukazunguka nyuma ya nyumba kuna moja ya geti kubwa ambalo jana usiku sikulitilia maanani nilipo kuwa ninazunguka hii nyumba.
Mama akaingiza namba za siri kwenye sehemu ya ukuta, geti hilo likafunguka taratibu hadi mimi mwenywe nikashangaa. Akawasha taa, sikuamini macho yangu kuona ukumbi mkubwa kwenye hii nyumba, ambao ndani yake umejaa vitu vingi vya thamani.
“Hii nyumba mimi na baba yako, tulipata ramani yake kutoka kwa mjerumani mmoja hivi alikuwa ni mkurugenzi wa pale Simba Saruji alipo kuwa anafanya kazi baba yako”
“Eehee sasa mama mbona hamkutuambia kwamba muna jumba kubwa hivi?”
“Baba yako aliniambia nisifanye hivyo hadi pale utakapo oa ndio nikueleze au utakapo pata mtoto”
“Mmmmm sasa kwa mfano kama ungeondoka duniani pasipo kutuambia ingekuwaje?”
“Munge fahamu kwa mana ramani ya kufika huku iliikuwa katika nyaraka zangu za siri”
 
“Ahaa sawa sawa mama”
Mama akaanza kuvuta turubai moja baada ya jingine ambayo yamefunika vitu vyote ndani ya ukumbi huu. Tukasaidiana kuyachomoa maturubai yote, gari mbili za kifahari ambazo ni Aud A7, Benz AMG 565 na Rane rover Voge.
“Mama hizi gari umezinunulia wapi?”
“Ahaa Tanzania hapa mwanangu, hizi gari nilikuwa ninaziagizia kwa jina la Diana na wala hapakuwa na mtu aliye weza kugundua kwamba ni zangu na huku nilikuwa ninazileta kwa siri sana tena usiku”
“Mmm mama una hatari wewe”
“Yote haya maisha niliwaandalia wewe na mdogo wako, na kila mmoja atakapo pata watoto wake atawarithisha hizi mali”
Mama alizungumza huku akifungua moja ya kabati la chuma. Sikuamini macho yangu kwa kuona vibunda vya dola mia mia za kimarekani vikiwa vimejaa kwenye kabati hilo. Mama akaanza kutoa vibunda na kuviweka kwenye meza ya pembeni.
 
“Hizo pesa ni sawa na dola laki tatu, nakuomba uwe makini nazo kwenye mipango yako yote utakayo iendesha huko mjini”
“Sawa mama”
“Ngoja”
Mama akafungua kabati jingine, nikaona bastola za kila aina zikia wa risasi zake, zimepangwa vizuri kwenye kabati hilo. Nikasoge karibu na kuanza kuzitazama. Kuna bastola mbili za rangi ya silva, nikatokea kuzipenda sana. Nikazichukua pamoja na magazine kumi zilizo jaa risasi.
“Hapo kimebaki nini kingine…..?”
Mama aliniluliza huku akinitazam usoni, sikuwa na chakujibu kwa maana kila ninacho kihitaji ameweza kunipatia. Akapiga hatua za haraka hadi kwenye kabati jingine, akafungua kabati hilo na kutoa tisheti moja nyeusi na ina uzito kisai.
 
“Ivae”
“Eheee ?”
“Ivae”
Nikavua tisheti niliyo ivaa na kuivaa tisheti hiyo iliyo ubana mwili wangu vizuri, mama akafungua kabati lenye bastola, akachukua  bastola moja na kuiweka magazine kisha akaninyooshea, jambo lililo nifanya nistuke sana. Pasipo kugopa mama akafyatua risasi na kujikuta nikifumba macho kwa woga.
“Acha uoga”   
Kauli ya mama ikanifanya kuyafumbua macho yangu, nikakuta risasi aliyo ifyatua kuja kwangu ikiwa imeanguka chini.
“Hiyo tisheti haiingii risasi, kipindi nilipo kuwa jeshini nikiwa binti mdogo, maremu baba yangu alikuwa ni ngunduzi na alikuwa ni meja wa jeshi. Aliweza kuitengeneza hiyo tisheti ili ziweze kutumiwa na wanajeshi wakiwa jeshini hususani kipindikile cha vita ya Kagera. Ujuzi wake uliweza kupuuziwa na viongozi wa serikalini na kumjita kwamba ni mchawi na anataka wanajeshi kuwafanya kama wanajeshi wa Kinjikitile Ngwale, alio kuwa akiwanywesha maji na kuwaambia risasi kwamba hazito ingia kwenye miili yao, ila kwa bahati mbaya ndio hivyo wakafa”
 
“Kitendo kile kilimkera sana babu yako na kuamua kunirithisha ujuzi huo wa kutengeneza tisheti hizo, kadri siku zilivyo zidi kwenda ndivyo nilivyo jikita ninakuwa mbunifu mkubwa sana japo hilo jambo sikuhitaji kulirithisha kwa mtu yoyote”
“Kwa nini?”
“Linaweza kuleta maafa makubwa sana hususani majambazi wakitambua tisheti hizi watakuwa ni hatari sana katika kufanya ualifu na hakuna risasi ambayo inaweza kupenya kwenye miili yao”
“Kwa mfano nikiwa ninahitaji kukulenga kichwani au miguuni, risasi haito weza kukufikia kwani mita mbili kutoka ulipo inaishiwa nguvu na kuanguka chini”
Mama alizungumza maneno hayo, kisha akafyatua risasi akiwa amenilenga kwenye mguu, na kweli risasi hiyo haikuweza kunifikia na ikaanguka chini. Nikajikuta nikitabasamu kwa manaa ni moja ya kifaa changu kikubwa kikacho nifanya niweze kuifanya kazi yangu ya kulipiza kisasi pasipo kuogopa kitu chochote.
 
“Asante sana mama”
Nilizingumza huku nikimfwata nikamkumbatia kwa nguvu, kisha nikamuachia huku uso mzima ukiwa umeja na furaha.
“Hapo kwenye hiyo sura sasa ndio mtihani”
“Usijali kuhusiana na swala la sura”
“Ok nilitaka kusahau, kuna hizi kalamu hapa”
Mama akanitolea boksi la kalamu, za kila aina na kalamu hizi sio mara yangu ya kwanza kuweza kuziona kwani kati ya kalamu hizo nimeshawahi kuzitumia kipindi nina soma.
“Hizi kalamu ni mabomu ambayo yanaweza kusambaratisha watu hata watano amambao wanaweza kukaa karibu. Kalamu hizi nilizibuni mimi mwenywewe na nimezifanyia majaribio. Sio rahisi kwa mtu kuweza kufahamu kwamba kalamu hizi ni mabumu, kwa sababu zipo kama kalamu nyingine. Kalamu hizi zipo kwenye mifumo miwili, hizi ambazo zinafunguka kwa kuchomoa vifuniko, pale mtu anapo chomoa kifuniko basi analipuka na kuwa vipande vipande. Hizi za kuminya mimya mtu akiminya hili kuweza kuondika basi atalipukua. Kwa hiyo unatakiwa kuwa makini sana, na wala sihitaji kuonyesha majaribio yake kwa maana tutakufa”
 
“Mama”
“Bee”
“Huu ujuzi wote umeupata wapi?”
“Nilisha kuambia alinirithisha babu yako, na mimi niliutumia kufanya vitu ambavyo siku moja nilikuwa na ndoto ya kuja kuwa mbunifu wa silaha za kijeshi ila kila niliyo buni nikaona ina weza kumaliza hichi kizazi, naomba hapo uchukue kalamu nne tu zitakutosha nyingine narudisha kwenye kabati”
Nikachomoa kalamu nne mbili zikiwa na vizibo na mbili zikiwa ni za kuminya ili mtu kuweza kuandika. Mama akasimama kwneye moja ya meza, akamina chini ya meza, hiyo ambapo kuna batani nyekudu. Pembeni ya meza hiyo kukatoka kioo kikubwa cha Tv ambacho kwa haraka haraka ni kama inch 52.  Akaanza kugusa gusa kwenye kioo hicho.
“Hapa ninaweza kuona kila kitu kinacho endelea maili moja kutoka hapa kwenye nyumba yangu, kila anaye ingia katika usawa wa maili moja nina weza kumuona, kwa hiyo kama ni mtu ana nia mbaya basi nina weza kumalizia huko huko”
“Kummaliza?”
 
“Yaaa, katika miti karibi elfu moja nimefunga kamera pamoja na silaha ambazo kupitia compyuta hii ninaweza kuziongoza nitakavyo mimi mwenyewe”
“Kwa mfano ngoja nikonyeshe kitu hapa”
Mama akaanza kuminya minya tena kioo cha compyuta hiyo, akanionyesha nyama mmoja aina ya swala akiwa katika msitu wa jumba hili.
“Kama ninataka kumuua huyu swala, nafanya hivi”
Mama akaminya kwenye kioo cha copyuta hii kilicho andikwa FIRE, sote kukashuhudia Swala huyo akianguka chini na damu zikianza kumwagika sana.
 
“Risasi zake zinapo toka huwa hazitoa sauti, na kazi hiyo pia ninaweza kuifanya kwenye simu yangu tu na si lazima kuja huku ukumbini”
Nikamtazama mama usoni na kijikuta nikikosa cha kuzungumza kwa manaa ukimuona kwa haraka haraka unaweza kusema ni mama wa kawaida sana na hata alivyo singiziwa kuiba pesa za serikali, sikuweza nikauona ameonewa, ila ni mtu mmmoja hatari sana.
“Tuachane na hilo, hizo gari zote hapo hakuna hata moja inayo ingia risasi, ni gari ambazo kwa Tanzania wanazo watu wacheche japo kuna watu wana gari kama hizo ambazo zinaingia risasi, ila kuna utofauti mkubwa sana katika hilo”
“Sasa hapa mama nitumie gari gani?”
“Tumia hiyo Aud, hiyo Benzi iache ukiingia nayo mjini watu wengi watakushangaa, kwa maana sio kama benzi nyingine, hembu fungua mlango na utazame humo ndani. Nikafunua mlango upande wa dereva.
 
“Ohooo my God!! Spidi mia nne”
“Yaaa spidi mita mia nne, kwa hiyo ukiendesha hiyo gari, unaweza kujiua wewe mwenyewe wakati tunahitaji bado”
“Mama nipe hili gari”
“Noo chukua hiyo Aud hilo liache, naomba nielekeweke katika hilo”
    Sikuwa na ubishi, tukaanza kuuingiza pesa alizo nipatia kwenye begi alilo npatia mama, kisha ni nikafungua nyuma ya gari na kuliweka begi hilo, tisheti aliyo nipa sikutaka kuivua. Niakalitoa gari kwenye ukumbi huo na kulisimamisha mbele ya jumba letu. Asma na Diana wakanifwata nilipo simama huku Asma akiwa amebeba begi la nguo.
“Humu nimekuwekea nguo za kubadilisha”
“Asante honey”
Asma akaliingiaza begi la nguo siti ya nyuma, mama akaja sehemu tulipo simama.
“Simu uliyo pewa ipo wapi?”
“Sijampa hii hapa”
Diana akanipa simu aina ya Iphone six, mama akaichukua na kuanza kuminya minya huku akiwa na simu ambayo ni sawa na hii aliyo nipatia Diana
 
“Mama unafanyaje au unakagua meseji zangu?”
“Meseji zako za nini, hembu niachie ujinga”
“Kwani hujafuta meseji zako?”
“Nimefuta ila nilikuwa nina mtania mama”
Mama akanikabidhi simu baada ya kumaliza alichi kuwa anakifahanya. Ukipata tatizo lolote simu yangu itaweza kunionyesha hapa, sehemu na tatizo ambalo umelipata hakikisha kwamba huiachi mbali na wewe hii simu”
“Sawa mama”
Nikaichukua simu na kuiweka mfukoni mwangu.
“Ila kaka Dany na huo upara huko kichwani mmmmm”
“Una nini?”
“Ahaaa sijazungumza mimi”
Nikakumbatiana nao wote watatu, kisha nikaingia kwenye gari, nikafunga mkanda na kufungua kioo kidogo. Mama akanifwata na kuinama kidogo.
“Hakikisha unarudi na kichwa cha K2 hapa sawa”
Maneno ya mama yakanifanya nimtumbulie macho, akanikazia macho na kunifanya nimjibu bila kupenda kwa kutingisha kichwa.
 
   ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts