Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 49 na 50 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 49 na 50 )

Written By Bigie on Monday, March 19, 2018 | 3:47:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   
Nikaichukua simu na kuiweka mfukoni mwangu.
“Ila kaka Dany na huo upara huko kichwani mmmmm”
“Una nini?”
“Ahaaa sijazungumza mimi”
Nikakumbatiana nao wote watatu, kisha nikaingia kwenye gari, nikafunga mkanda na kufungua kioo kidogo. Mama akanifwata na kuinama kidogo.
“Hakikisha unarudi na kichwa cha K2 hapa sawa”
Maneno ya mama yakanifanya nimtumbulie macho, akanikazia macho na kunifanya nimjibu bila kupenda kwa kutingisha kichwa.
   
ENDELEA
Mama akanishika shavu lango na kulifinya kidogo kisha akasimama akiwa na sura iliyo jaa tabasamu. Asma akainama pale alipo kuwa ameinama mama na kunibusu mdomoni mwangu.
“Mwanao nitahakikisha anakua katika mazingira mazuri ya kupendeza”
“Asante mke wangu”
“Kuwa makini lakini”
“Usijali katika hilo”
Asma akanibusu tena. Diana akanipungia mkono, taratibu nikafunga kioo cha gari langu, na taratibu nikaanza kuondoka katika eneo la nyumba hili huku nikiwatizama kupitia kioo cha pembeni jinsi wanavyo nitazama. Ramani iliyopo kwenye tv ndogo ya hili gari, inaaniongoza njia za kupita kwa kutumia kijimshale maalumu cha kunielekezea. Mwendo wa masaa mawili nikawa nimefanikiwa kutoka msituni na kuingia kwenye kijiji kimoja ambacho sikukifahamu kinaitwaje. Ni kijiji kilicho jaa watu wengi pamoja na nyumba za udongo. 
 
Nikaendelea kuifwatisha ramani hiyo hadi nikatokea mji mmoja unao itwa Soni. Sikuhitaji kusimama sehemu yoyote zaidi ya kuendelea na safari yangu ambayo ni ndefu sana bado sijafahamu huko mbele nitakutana na changanoto gani.
    Kutokana sio mara yangu ya kwanza kupita kwenye hii barabara ya Soni kuelekea Mombo, nikawa makini sana kwenye kuhakikisha kona zote ninazipita kiusalama, hata mwendo wangu wa gari nikawa nimeupunguza kwa kiasi kikubwa. Nikiwa katikati ya kona, nikakutana na foleni kubwa za magari yaliyo simama, jambo ambalo si la kawaida kwa njia hii kuwa na foleni kubwa kiasi hichi. Ikanibidi na mimi kuweza kusimamisha gari langu huku nikiwa na wasiwasi mkubwa sana. Nikataka kushuka ila roho yangu ikasita kidogo.
Nikiwa nimetulia huku nikisubiria foleni hiyo kwenda mbele, nikaona watoto wawili wakiwa wanatembea kwa miguu wakitokea huko ilipo foleni, taratibu nikafungua kioo cha gari ili niweze kuwauliza kitu.
“Nyie watoto kuna nini huko chini?”
Wakanitazama pasipo kujibu kitu chochote, akilini mwangu nikajiuliza hawaelewi Kiswahili au ndio ukimya.
“Eti watoto wazuri kuna kitu gani kinacho endelea huko chini?”
 
“Weshu tutonge”   
Mmoja alizungumza huku akimvuta mwenzake mkono, kwa haraka haraka nikatambua kwamba neno alilo lizungumza linamsisitizia mwenzake waondoke. Wakaondoka pasipo kunijibu kitu cha aina yoyote, taratibu nikafunga kioo cha gari na kuendelea kusubiria magari yasogee taratibu. Taratibu magari yakaanza kusegea.
Kwa mbali kidogo nikaona askari wa usalama barabarani, wakikagua gari moja baada ya jengine, hapo ndipo wasiwasi ulipo anza kunipanda. Mapigo ya moyo yakanienda mbio sana, kwa maana sikuhitaji kukamatwa mapema kiasi hichi wakati nina jukumu  zito mbele yangu. Kutokana gari zimesimama tena nikashuka kwenye gari na kuzunguka kwenye buti la gari, nikalifungua. Begi lenye pesa nikalifungua taratibu pasipo mtu wa gar lililopo nyuma yangu kuweza kuona chochote. Nikachukua kibunda kimoja cha dola za kimarekani, nikalifunga na kurudi ndani ya gari.
 
    Taratibu magari yakaanza kusonga mbele, na mimi nikafika kwenye sehemu ya kukaguliwa. Akanifwata askari wa kike aliye valia sare zake vizuri na kupendeza. Nikafungua kioo cha gar taratibu huku nikiwa nimeandaa noti tano za dola mia. Askari huyo akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akatabasamu.
“Naomba leseni yako”
Nikajifanya ninajipapasa huku kibunda cha noti za kimarekani nikikiweka kwenye siti ya pembeni. Nikamuona askari huyo anavyo tupia jicho lake kwenye kibunda cha pesa hizo.
 
“Ahaaa samahani dada yangu kidogo, nimesahau waleti yangu nyumbani”
“Shuka kwenye gari”
“Ahaa dada kuna hichi kipesa hapa chukua ukale na watoto nyumbani”
Nilizungumza huku noti hizo tano nilizo zikunja nikiwa ninamkabidhi. Askari huyo akatazama wezake wanao endelea kukagua magari mengine, kisha akapokea noti hizo.
“Uwe makini siku nyingine barabarani”
Askari huyo alizungumza huku noti hizo zkizibana kwenye sidiria yake na kufunga kifungo cha shati lake.
“Ahaa asante, ila naweza kukuuliza swali?”
“Bila shaka kaka yangu”
“Kuna nini kinacho endelea, kwa maana juzi nilipita hapa sikuona foleni kubwa hapa?”
“Yaa ni kweli, kuna gaidi mmoja ametoroka akiwa anasafirishwa kutoka gerezani. Basi ameua wanajeshi wengi na mmoja amachukua mateka”
“Aisee kumbe Tanzania nako kuna magaidi?”
Niliuliza nikiwa kama sifahamu vile, kwa jinsi nilivyo nyoo upara na hili gari la kifahari nililo nalo si rahisi sana kwa polisi wa kawaida kuweza kufahamu kwamba mimi ndio wanaye nitafuta.
 
“Wee acha tu kaka yangu, ndio hivyo”
“Haya asante”
Nikafunga kioo cha gari langu na kuondoka. Nikafanikiwa kufika Mombo salama salimini, sikuishia hapo zaidi ya kuzidi kuendelea na safari yangu kuelekea jijini Tanga, njiani ukaguzi wa magari ya kumtafuta gaidi huyo bado unaendelea kwa kutumia pesa, nikafanikiwa kupita vikwazo vyote na kuingia jijini Tanga.
Moja kwa moja nikaelekea ilipo nyumba ya mama. Nikasimamisha gari langu pembeni ya nyumba hii, kisha nikashuka na kuanza kuichunguza vizuri, mandhari ya hii nyumba yamebadilika kwa kiasi kikubwa hata rangi ya nyumba imebadilishwa. Nikasimama getini na kuminya kengele ya hodi. Baada ya dakika mbili mlango ukafunguliwa na mtoto kibonge mwenye asili ya kiarabu. Akanitazama huku akiwa amevimbisha mashavu yake na mkononi mwake ameshika ice cream iliyo mchafua mdomo mzima.
 
“Wa…taaka nini?”
Aliongea kwa sauti ya dharau.
“Mama au baba yako wapo wapi?”
“What do you wa……”
Kabla hajamalizia kingereza chake cha ajabu ajabu, nikamninya shingoni kwenye sehemu ya mshipa wa fahamu na likapoteza fahamu, hata kabla hajadondoka, chini nikamuwahi, taratibu nikambeba, uzuri mtaa huu hauna watu kabisa, na watu wengi mida hii ya mchana huwa hawapo. Nikamuingiza kwenye gari na mimi nikaingia na kuondoka naye.
    Sikuhitaji kukaa hotelini, sehemu sahihi ya mimi kuishi kwa siku zote za maisha yangu katika hii kani ni ndani ya gari langu. Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia mama yangu.
“Nimefika mama”
“Ehee hujakunata na vizuizi njiani?”
“Nimekutana navyo, ila wakaguzi wenyewe ni askari wetu hawa, njaa tupu. Nimewahonga honga nimepita”
“Hawajakufahamu?”
 
“Kwa huu upara sio rahisi kwa wao kuweza kunifahamu”
“Ahaa sasa umeanzia wapi?”
“Nimeenda kwenye ile nyumba yetu kule Chumbageni, nimekuta kuna wahindi wanaishi mule”
“Ehee”
“Basi kuna litoto moja la kihindi, nimeliteka”
“Umemteka…..?”
Mama aliuliza kwa hasira
“Ndio nimemteka kupitia huyu kazi yangu itakuwa ni rahisi kwangu”
“Dany Dany wewe kwa nini umteke huyo mtoto wa watu”
“Tulia mama nitakueleza kila kitu nilicho panga kukifanya”
Nikamsikia kabisa mama akishusha pumzi nyingi kwa wasiwasi mkubwa alio kuwa nao.
“Utakapo hitaji msaada niambie”
“Sawa mama”
Nikakata simu na kuelekea ya fukwe za bahari inayo itwa Jet, nikasimamisha gari langu sehemu ambayo sio rahisi sana kwa mtu kuweza kuona kinacho endelea ndani ya gari, uzuri vioo vya gari hivi vyote ni vyeusi kasoro kioo cha mbele tu na nyuma. Toto hili la kiarabu likazinduka kutoka katika usingizi wa kupoteza fahamu, likanitumbulia macho huku likiyafikicha.
 
“Weee ni nani?”
“Rafiki yako”
“Sina rafiki mtu mweusi mimi”
Niliongea kwa dharau, nikamzaba kibao kikali kwenye mshavu wake wa kuliana kulifanya lilie kwa sauti kubwa, nilipo ona haitoshi nikatoa bastola yangu moja ya kumuelekezea. Hapo ndipo nikatambua kwamba bastola haina mtoto ua mtu mzima. Kilio chote kikamkauka ndani ya sekunde moja tu, hata makelele aliyo kuwa akiyapiga yakakatika.
“Nuamza kimya, nakuuliza swali, nijibu swali, ukileta ujinga nakuua”
Akatingisha kichwa kukubaliana na mimi kwa kile ninacho hitaji kukifanya kwa wakati huu.
“Ile nyumba niliyo kukuta ni ya nani?”
“Ya baba”
“Ahaa baba yako anaitwa nani?”
“Raji”
 
“Aahaa unaijua namba yake ya simu?”
“Ndio kaka”
Nikatoa namba ya simu, akaanza kunitajia namba za baba yake, zilipo kamilika nikampigia baba yake. Simu ikaita kwa muda kidogo kisha ikapokelewa.
“Halo”
“Habari yako bwana Raji?”
“Nani wewe uliza mimi habari yangu?”
“Sio muhimu wewe kunijua mimi ila mimi ni rafiki wa Raji kwa sasa”
“Mwanagu hana rafiki sauti besi kama hiyo”
“Ok ngoja niende kwenye mada yangu. Ile nyumba unayo ishi ninaomba uhame”
“Pumbavu saa wewee taka mimi hapa kwenye nyumba yangu”
Mzee huyo alizungumza huku akicheka sana kwa dharau.
“Ohoo usipo hama, kesho asubihi nakuletea kichwa cha mwanao”
“What…….??”
Kicheko chote nilicho kisikia kwa mzee huyo, kikakatika.
“Unataka mtoto, hama kwenye nyumba ile kama uhitaji subiri uone”
“Ngoja ngoja mwanangu yupo wapi?””
Nikamgeukia mwaye na kumuwekea simu sikioni.
“Baba babaa”
Mtoto huyo alipo zungunza maneno hayo nikairudisha simu yangu sikioni mwangu.
 
“Naamini umesikia, kama unamuhitaji leo, hama, Hati ya nyumba nina ihitaji na kila kitu cha ndani mukiache sawa?”
“Sawa elewa wewe, wapi mimi pata mutoto, kwenda hama sasa hivi nyumbani”
“Kila hatua unayo ipiga nitaifahamu kuanzia sasa, na ole wako uwasiliane na polisi nitamkata mwanao mkono na kumtoboa jicho moja kwa kosa hilo”
“Usifanye hivyo, toto yenyewe moja banaaa”
“Nenda kahame sasa hivi”
Nikakata simu, kwa haraka nikampigia simu mama
“Ehee”
“Mama nahitaji ile program ya kumuona mtu kila anapo kwende kwenye simu yangu”
“Wait nakuunganisha, nitumie namba ya huyo mtu”
“Sawa”
Nikakata simu nikaingia upande wa meseji, nikamtumia mama namba hiyo ya simu. Kisha nikampigia tena.
“Yaap”
“Umeiona?”
“Ndio naiunganisha hapa. Kwani hiyo namba ni ya nani?”
“Ni namba ya mtu aliye inunua nyumba yako nahitaji aweze kuihama sasa hivi kwa kubadilishana na mwanaye”
“Your so clever boy”
 
“Asante mama”
“Tayari angalia kwenye simu yako”
Nikaangalia kwenye simu yangu, nikakuta meseji, nikaifungua na kunionyesha alama nyekundu ya sehemu alipo bwana Raji. Ramani ya simu yangu ikanionyesha akiwa anaelekea maeneo ya Chumbageni kulipo na nyumba yetu. Nikawasha gari na kuelekea chumbageni. Sikuchukua muda mrefuni nikawa nimefanikiwa kufika. Nikasimamisha gari mbali kidogo na nyumbani kwetu ila kila kitu mtu anaye ingia na kutoka katika geti la nyumba yetu ninaweza kumuona. Alama ya alipo Bwana Raji, inanionyesha yupo katika eneo la nyumba. 

Nikiwa nimetulia huku mwanaye akiwa amekaa siti ya nyuma kimya kabisa, akihofia kufa. Nikaona gari nyeusi moja aina ya Range Rover, akashuka kijana mweusi aliye valia suti, akazunguka upande wa pili wa gari na kumfungulia bosi wake mlango, nikamuona K2 akishuka akiwa amevalia suti nyeusi na kuingia ndani ya geti jambo lililo anza kunikumbusha mateso na machungu niliyo yapata gerezani na taratibu nikajikuta nikianza kuichomoa bastola yangu nilipo iweka na nikashika kitasa cha mlango tayari kwa kushuka kwa kwenda kukikata kichwa chake kama alivyo niaeleza mama.

                         AISIIIII……….U KILL ME 50

ILIPOISHIA   
Nikiwa nimetulia huku mwanaye akiwa amekaa siti ya nyuma kimya kabisa, akihofia kufa. Nikaona gari nyeusi moja aina ya Range Rover, akashuka kijana mweusi aliye valia suti, akazunguka upande wa pili wa gari na kumfungulia bosi wake mlango, nikamuona K2 akishuka akiwa amevalia suti nyeusi na kuingia ndani ya geti jambo lililo anza kunikumbusha mateso na machungu niliyo yapata gerezani na taratibu nikajikuta nikianza kuichomoa bastola yangu nilipo iweka na nikashika kitasa cha mlango tayari kwa kushuka kwa kwenda kukikata kichwa chake kama alivyo niaeleza mama.
   
ENDELEA
Kabla sijashuka simu yangu ikaita na kunifanya nigairi kufanya nilicho kuwa nimekidhamiria kukifanya. Nikaitoa simu yangu mfukoni na kukuta ni bwana Raji ndio anaye piga. Nikashusha pumzi huku nikilitazama toto lake lililo kaa siti ya nyuma.
 
“Ndio”
Nizungumza kwa sauti nzito
“Nipo tayari hama kwenye nyumba hii, kabidhi managu”
“Unacheza na akili yangu?”
“Kwa nini?”
“Huyo mwanamke aliye ingia kwako ni kutoka katika serikali, sasa kuanzia sasa njoo ushuhudie kichwa cha mwanao”
Nikakata simu, nikawasha gari, nikalirudisha nyuma kwa haraka na kuondoka katika eneo hili, kwa haraka akili iliyo nituma ni kueleka katika barabara ya kuelekea Mombasa Kenya. Nikafika maeneo ya daraja la Utofu, gani nikalisimamisha pembeni. Kwa haraka nikashuka kwa hasira nikiwa nimeshika bastola yangu. Nikafungua mlango wa nyuma, na kumchomoa mtoto huyu kibonge. Nikatazama kila sehemu ya daraja hili hapakuwa na mtu wala gari linalo hitaji kupita. 
 
“Simama hapo”
Kabonge kakasimama huku mwili mzima ukimtetemeka, nikatoa simu yangu na kuingia upande wa video, nikaanza kurekodi tulio ninalo kwenda kulifanya huku bastola nikiwa nimeiweka sikioni mwa mtoto huyu kibonge.
“Moja, mbili, tatu”
Nikafatua risasi pembeni ya mtoto huyu, kwa ule mlio na mstuko akajikuta akianguka chini na kuzimia. Nilipo hakikisha kwamba video yangu ipo vizuri, nikamnayanyua kibonge na kumuingiza ndani ya gari kisha na mimi nikaingia na kugeuza gari hilo na kurudi Tanga mjini. Nikafika nje ya mgahawa mmoja uliopo pembezoni mwa uwanja wa Mkwakwani. Nikashuka kweye gari langu, nikaka kwenye moja ya kiti katika mgahawa huu huku gari nikiwa nimelifunga kutokana kibonge hajazinduka.
“Nikusaidie nini kaka?”
Kijana mmoja ambaye ni muhudumu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Nahitaji chipsi kuku na juisi”
“Chipsi yai au?”
“Ndio”
Akaondoka, nikaitoa simu yangu mfukoni, nikatafuta namba ya Bwana Raj na kumtumia video hiyo kwa njia ya Whatsapp. Ndani ya sekunde selathini video hiyo ikafunguliwa na mzee huyo, nikatambua kwamba ujumbe utakuwa umemfikia kisawa sawa. Hata kabla simu yangu sijaiingiza mfukoni, ikapigwa na anaye piga ni bwana Raji.
“Ndio”
“Bana bana acha fanya hivyo toto yangu ya pekee bwana”
Bwana Raji alizungumza huku akilia kwa uchungu
“Huwa sipendi kuchezewa akili, umewasiliana na mtu kutoka kikosi cha NSS, nahitaji hati ukiwa umeibadilisha jina kisha ninakupatia mtoto wako”
“Tutaonana wapi sasa ndugu yangu”
“Nitakujulisha”
Nikakata simu, hata sikuona haja ya kuendelea kukaa eneo hili, nikanyanyuka na kuingia kwenye gari, nikaliwasha na moja kwa moja nikaelekea eneo la Forozani. Nikasimamisha gari langu pembeni nikashuka huku nikiwa makini sana kutazama kila mtu aliyopo katika eneo hili. Katika kutazama tazama kwa umakini nikafanikiwa kumuona Monnica, msichana ambaye anafanya kazi yake na kujiuza mwili wake na ninakumbuka nilisha wahi kulala naye akiwa na mwenzake Lissa na mimi nikiwa na rafiki yangu Hassani.
 
     Nikatembea kwa hatua za taratibu hadi katika kiti alicho kaa peke yake, akichezea chezea simu yake ya mknoni. Nikavuta kiti cha pembeni na kukaa pasipo kumsemesha kitu cha ina yoyote.
“Samahani kaka, nina mtu hapo anakuja kukaa, ningeomba ukatafute sehemu nyingine ya kukaa”
Monica alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikatabasamu kwa maana ninaamini ya kwamba amenisahau kabisa.
“Rafiki yako Lissa hajambo”
Nikaona sura ya Monica ikibadilika kidogo, akijaribu kuvuta kumbukumbu kama ananifahamu ila hana uhakika sana kwa maana tangu nikutane naye ni miaka miwili sasa imepita.
“Umemjuaje Lissa?”
 
Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama Monica usoni mwake.
“Unaweza kuniambia kwa sasa Lissa yupo wapi?”
“Samahani wewe kaka, siwezi kukuambia rafiki yangu yupo wapi ikiwa sikufahamu wewe ni nani”
“Ok kuna siku nilikuwa na rafiki yangu, tuliwachukua hapa hapa na kwenda kulala na nyinyi pale Mtendelea vipi hapo utakuwa umenikumbuka”
Monica akanyamaza kimya huku akinitazama
“Ahaaaa wewe ndio yule kaka mwenye naniliu kubwa eheeee”
“Ewalaaa”
“Nimekukumbuka, za masiku?”
“Salama tu naona unazidi kupendeza”
“Ahaa si unajua biashara yangu pasipo kupendeza huwezi kupata wateja”
“Kweli hadi leo bado unaifanya?”
“Ndio Dany, maisha yenyewe yapo wapi haya”
“Duu sasa hapa unamsubiria nani?”
“Kuna jamaa mmoja ananihitaji leo, ndio nina msubiria hapa”
“Ohoo sasa naweza kumpiku?”
“Kama una cha juu unaweza”
“Ok twende basi kwenye gari langu”
“Ok”
 
Tukanyanyuka na Monica moja kwa moja tukaeleka nilipo lisimamisha gari langu, tukaingia ndani ya gari na kukaa.
“Ehee vipi huyu kibonge wa kiarabu naye humu”
Monica alizungumza huku akimtazama mtoto huyu  wa kiarabu ambaye bado amelala ndani ya gari langu.
“Huyo anaweza kukufanya uwe tajiri chap chap”
“Kivipi?”
“Nitakuelezea kama upo tayari kufanya hii kazi, pesa ninayo ya kutosha ya kuweza kukulipa wewe”
Nilizungumza huku nikichomoa noti mbili za dola mia na kumkabidhi Monica mkononi mwake huku mkono wangu wa kushoto nikiwa nimeshika kibunda cha pesa.
Monica akazichukua kwa haraka huku akiwa ameachia tabasamu pana.
“Huyo mtoto nahitaji itakapo fika saa mbili usiku leo umpeleke kwa wazazi wake”
“Hakuna shida ila ni wapi anatakiwa kupekwa?”
“Nitakuambia ni wapi anatakiwa kupelekwa”
“Hilo hali shida baada ya kumpeleka?”
“Nitakupatia dola elfu kumi hiyo dola mia mbili niliyo kupa ni ya kunywa maji tu”
 
“Asante sana Dany utakuwa umeniokoa, ehee Mungu nitaanza kufanya biashara sasa”
“Kwani ndoto zako ni kufanya biashara”
“Sana napenda sana kufanya bishara seme pesa ninayo pata katika kuuza ku* ni pesa ya madafu huwezi kufanya chochote cha maana zaidi ya kununu vipodozi ili uendelee kuwa katika chati”
“Aisee sawa, sasa sijui hapa Tanga ni wapi wanabadalishi pesa”
“Barabara ya kumi”
“Ok twende”
Nikawasha gari na kuelekea katika eneo hilo ambapo wanabadilisha pesa za kigeni, hatukuchukua dakika nyingi tukawa tumefika, akanionyesha sehemu wanapo badilisha pesa, nikashuka kwenye gari na kuingia kwenye duka hilo. Nikabadilisha dola elfu moja ambazo ni sawa na milio mbili za kitanzania, kisha nikarudi kwenye gari.
“Nina njaa balaa”
Nilizungumza huku nikifunga mkanda wa gari
“Ina maana hujakula?”
 
“Yaa tangu asubuhi sijapata chakula”
“Pole twende sehemu nikakununulie japo chakula”
“Sehemu gani?”
“Mmmmm unataka chakula gani?”
“Hata nyama choma”
Monica akanieleza sehemu zinapo chomwa nyama, kutokana muda wa saa mbili usiku bado haujafika, ikanibidi tuelekea eneo hilo. Tulipo fika nikampatia Monica laki moja, akashuka kwenye gari na mimi nikabak nikiwa na kibonge aliye anza kunyayuka huku akifikivha fikicha macho yake kutokana na usingizi mzito alio lala.
“Umeamka?”
“Natamkata baba yangu”
Bonge alilia huku akizungumza kwa sauti ya chini.
“Unajua baba yako hana akili. Nilumueleza asipo fanya kile ninacho kihitaji basi ninaweza kukuua na ninampekekea kichwa chako”
“Usiniueeeee mimi bado mdogooo”
Maneo ya bonge yalinifanya nicheke. Nikamgeukia huku ninamtazama usoni mwake.
“Futa machozi, wanaume majasiri huwa hawalii, ila wanahakikisha wanakabiliana vipi na changamoto zilizopo mbele yao”
“Sasa si utaniua nikiacha kulia?”
“Hahaha hapana, futa machozi”
Kibonge akafuta machozi yake huku akinitazama usoni mwangu. Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia baba yake.
 
“Ndio”
“Wewe ua manangu”
“Mwanao yupo hai, nahitaji hati nikupatie mwanao”
“Mimi leta hati ya nyumba, tayari hama kabisa nyumba hii”
“Ikifika saa mbili usiku tuonane ndani ya uwanja wa mpira wa Mkwakwani sawa”
“Sawa elewa wewe, kitu ingene hitaji”
“Ahaaa nahitaji nusu ya pesa uliyo nunulia hiyo nyumba”
“Ahaaa banaaa wewe sio kubaliano yetu hiyo”
“Ukifanya makosa namuua mwanao”
“Basi nitaleta, taka sikia Roja”
Nikamuwekea simu sikioni kibonge
“Baba……”
Akamalizia na maneno ya kiarabu ambayo sikuelewa hata moja.
“Umemsikia”
“Ndio, mimi letea wewe hiyo hati pesa na kidogo hapa”
“Ulinunua kiasi gani hiyo nyumba?”
“Milioni mia tatu”
“Utanipatia milioni mia”
“Sawa sawa mzee”
Nikakata simu, Monica akaingia kwenye gari akiwa ameshika kifuko cheusi
 
“Ehee kibonge ameamka”
“Yaaa”
“Aissee huyu mtoto mbona ana mijishavu, kama ile mimbwa ya kizungu”
“Hahaaa usizungumze hayo, mtoto huyu utampeleka kwenye uwanja wa Mkwakwani, saa mbili usiku”
“Kwa sehemu gani pale Mkwakwani?”
“Kwa ndani mule, nikakuambia nini cha kufanya”
“Sawa”
Tukaondoka eneo hilo, nikatafuta sehemu nzuri nikasimamisha gari langu, tukaanza kula hadi kibonge akashiriki katika kula. Ilipo timu saa mbili kasoro kumi tukaelekea katika uwanja huo. Nikamuomba Monica kushuka kwenye gari kutazama kama kuna dalili ya askari katika eneo hili. Monica akafanya kama nilivyo mwambia. Akatazama kila sehemu ya uwanja huu, kisha akarudi.
“Hakuna dalili ya askari”
“Poa, mchukue kibonge uingie naye humo ndani ya uwaja kupitia geti hilo”
“Poa”
“Nipe namba yako nikupigie simu”
“Poa”
Wakashuka kwenye gari, nikatafuta sehemu nikasimamisha gari, kisha na mimi nikashuka nikawaona wakiwa wanaingia ndani ya uwanja huo, nikaparamia moja ya ukuta wa uwanja, na kuingia ndani nikiwa na bastola yangu. Nikatafuta sehemu ambayo ninauona uwanja vizuri. Nikawaona wakiwa wamesimama pembezoni mwa goli moja la mpira. Nikampigia simu Monica.
 
“Ndio”
“Simameni hapo hapo hadi nitakapo kuambia usonge mbele”
“Poa”
Nikakata simu na kumpigia mzee huyo, akapokea simu
“Upo wapi?”
“Mimi fika hapa uwanjani?”
“Ingia ndani ya uwanja, pesa za hati nazuhitaji”
“Kuna shida”
Baada ya dakika moja nikamuona mzee huyo mfupi na kibonge akiingia ndani ya uwanja akiwa peke yake. Nikampigia simu Monica
“Moni unamuona huyo mzee mwenye brufcase, hakikisha kwamba anafikupa hati ya nyumba pamoja na hiyo brufcase ndani iwe na pesa”
“Sawa”
Nikaka simu na kumpigia mzee huyo
“Mpatie huyo binti mwenye mwanao hiyo brufcase pamoja na hati”
“Sawa”
“Ukifanya ujinga nakupasua kichwa”
“Mimi hakuna tania wewe, mimi taka mwangu”
Mzee huyo akamfikia Monica, nikamuona akiifungua brufcase hiyo, nikampigia simu mzee huyo
“Ndio”
 
“Mpe simu huyu binti”
“Ndio”
“Pesa ipo?”
“Ndio zipo nyingi sana”
“Akupe hati”
Nikasikia Monica akimuambia mzee huyo anahitaji hati, mzee huyo akampatia bahasha, Monica huku simu akiwa ameibana sikioni mwake, akatoa hati ya nyumba.
“Ni hati yenyewe?”
“Ndio ni hati nyenyewe?”
“Ina jina gani?”
“Raja Bahamuz”
“Ok mpatie mtoto wake”
Nilipo hakikisha Monica amekabidhiwa kila kitu nikasimama sehemu niliyo kuwa nimelala nikilifwatilia tukio hilo.
“Nyoosha mikono yako juu na bastola yako itupe pembeni”
Niliisikia sauti ya K2 nyuma yangu, jambo lililo nifanya mwili mzima kunisisimka kwa hasira kali
 
   ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts