Get the latest updates from us for free

Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 57 na 58 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 57 na 58 )

Written By Bigie on Friday, March 23, 2018 | 11:21:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  
Nikaona gari tatu za ikulu ambazo anatembelea raisi zikiwa zimesimamishwa kwenye maegesho huku walinzi walio valia suti nyeusi wakiranda randa kika eneo.  Nikamuona Babyanka akitoka kwenye mlango wa jumba hili la kifahari, akamuita mmoja wa walinzi na kuzungumza naye kisha akageuza kuchwa chake na kutazama sehemu nilipo na macho yetu yakakutana jambo lililo mfanya Babyanka kuchomoa bastola yake na kuanza kufyatua risasi kadhaa kueleka sehemu nilipo.

ENDELEA
Nikajiachia na kwenye ukuta na kutua chini kwa umakini wa hali ya juu, nikaanza kukimbia kwa kasi kuelea kwenye mti nilipo iacha pikipikia. Nikafanikiwa kufika, nikashuhudia gari mbili za ikulu zikitoka nje ya geti hilo kwa kasi sana jambo lililo nifanya niiwashe pikipiki yangu kwa haraka na kuondoka eneo hili kwa kasi huku, huku gari hizo kutoka ikulu zikinifwata kwa nyuma. Sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kukatiza vichochoro na nikafanikiwa kupotezana na gari  hizo kwa umbali mkubwa. 
 
Sikuwa na namna ya kuendelea kuwepo katika eneo hili la Tegeta, moja kwa moja nikarudi hadi Sinza kwa mama Marima, pikipiki nikaisimamisha pikipiki sehemu nilipokuwa nimemsimamisha dereva bodaboda. Nikaanza kutembea kwa miguu huku nikiwa makini, gari langu nikalikuta nje likiwa kama nilivyo liacha hapakuwa na tofauti yoyote.
Nikainga ndani na kumgongea mama Marim dirishani kwake. Nikamsikia akifungua mlango wa chumbani kwake, kisha akaufungua mlango wa mbele katika hii nyumba. Tukaingia chumba kwa mama Marim na akafunga milango yote.
“Vipi?”
Mama Marim aliniuliza huku akinitazama usoni.
“Wale wasichana wanafanya kazi chini ya raisi, na muda wowote wanaweza kurudi hapa, inanibidi kuondoka eneo hili”
“Usiku huu?”
 
“Yaaa usiku huu”
Mama Marim hakuwa na kitu cha kuzungumza ziidi ya kukubaliana na kile ambacho nilikuwa nimekikusudia, nikaanza kuvaa mwili wa plastiki unao nifanya niwe na muonekano wa mwamake, nilipo hakikisha nimemaliza kuvaa gauni langu, nikatoka nje nikiwa na funguo ya gari, nikafungua nyuma ya gari kwenye buti. Nikafungua begi la pesa, nikatoa kibunda kimoja cha dola kisha nikafunga na kurudi ndani.
“Chukua hizi pesa hakikisha unafungua biashara itakayo kusaidia maisha yako, sihitaji urudi kwenye hoteli kuendelea na ile kazi ya kuzalolishwa na watoto wadogo”
Mama Mariam akazitazama pesa zangu ninazo mpatia huku macho yakimtoka. Nikamshikisha pesa hizo mkinoni kisha nikachukua nguo zangu za kiume nilizo kuwa nimezivaa nikazikunja vizuri na kuzishika mkononi.
“Dany siamini kama ninaweza kupata pesa nyingi kiasi hicho”
“Ndio uamnini, mimi kwa sasa sina muda wa kuendelea kukaa hapa ninaondoka”
 
“Sawa Dany asante sana”
“Nitaendelea kumtafuta Marim sawa”
“Sawa Dany nashukuru”
Nikamiga busu la mdomo mama Marim, kisha nikabeba kila kilicho kuwa changu na kutoka nje, nikaingia kwenye gari langu na kuondoka. Japo ni usiku sikuwa na sehemu ya kueleka zaidi ya kutafuta sehemu nitakapo simamisha gari langu na kupumzika hadi itakapo timu asubuhi. Nikafika kwenye moja ya msitu maeneo ya Mbezi Temboni, nikasimamisha gari langu na kuzima taa kisha nikaikunjua siti yangu kidogo kisha nikalala.    
    Mtetemesho wa simu yangu niliyo iweka pembeni mwa siti ya gari, ndio ukanistua, nikafumbua macho yangu, nikaichukua kwa mkono wangu wa kushoto na kukuta ni mama ndio anaye nipigia.
“Shikamoo mama”
“Marahaba, sasa upo wapi?”
“Nipo kwenye moja ya msitu nimepumzika”
“Nina habari mbaya”
Ikanibidi kukaa vizuri kwenye siti yangu huku nikijiandaa kuisikiliza hiyo habari mbaya.
 
“Habari gani hiyo mama?”
“Kuna kikosi maalumu kutoka nchini Somalia leo, kimeingia kwa siri nchini Tanzania, na kina mpango wa kutekeleza tukio la kigaidi katika uwanja wa taifa wa mpira na mechi itakuwa ni Simba na Yanga”
Nikashusha pumzi kwa maana ni moja ya tukio ambalo sikuwa nalo kabisa katika mipango yangu
“Ila mama hiyo sio kazi yangu”
“Natambua sio kazi yako, ila tazama ni watu wangapi watakao poteza maisha yao pasipo kuwa na hatia na hichi wanacho kuja kukifanya leo ni ulipizaji kisasi kwa wezao walo uwawa kipindi kile kwenye dhiara ya raisi”
“Mungu wangu, sasa mama mimi nina anzia wapi?”
“Nakutumia picha za vijana hao watakao jitoa muhanga leo katika uwanja wa taifa. Wapo vijana wanne, ukiweza kuwatambua picha zao basi unaweza kufanikisha swala hilo la kuwaokoa maelfu ya watanzania”
 
“Sawa mama”
Mama akakata simu, nikaiweka siti yangu ya gari vizuri huku nikiwa ninasubiria picha hizo, haukupita muda picha hizo zikainga kupitia ujumbe wa Whatsapp. Nikafungua picha ya kwanza nikakuta ni kijana mwenye ndevu kiasi na nywele zake zimelala. Nikafungua picha ya kwanza nikakutana na jamaa mwenye umri kati ya miaka thelethini na tano mpaka arobaini na tano. Picha ya pili nikakutana na mtoto wa miaka si zaidi ya kumi na tano. Picha ya nne hapo ndipo nilipo hisi utumbo ukinicheza kwa woga na wasiwasi kwani ni msichana ambaye ninamfahamu kabisa na  ndio msichana wangu wa kwanza kamvunja bikra yake na si mwingine ni Marima.
 
Nikahisi mikono ikiishiwa nguvu, Marim kwenye picha hii amejifunga mtandio ulio bakisha sura yake tu ya kirembo. Simu ikaita nikaipokea taratibu huku nikiwa nimeishia wanguvu kabisa.
“Umeziona hizo picha?”
“Ndio mama”
“Sasa hiyo habari nimeipata katika watu ambao wapo katika kikundi chao huko Somalia na nimemuweka kwa ajili ya kuhakikisha ananipatia habari zote wanazo zifanya kikundi hicho”
“Shambulizi limepangwa kufanyika muda gani?”
“Ni saa tisa na nusu, mechi ikiwa imefikisha dakika thelethini na kama ni kuwahi basi inabidi uhakikishe kwamba unawahi kabla ya mechi kuanza lisaa moja kabla”
 
“Sawa mama”
“Dany hakikisha unakomboa maelfu ya Watanzania wananao kwenda kutazama huo mpira”
Mama alizungumza kwa sauti ya msisitizo na iliyo jaa huzuniko kubwa
“Sawa mama nimekuelewa nitahakikisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri”
“Sawa nakutakia kazi njema”
“Poa”
Nikakata simu, nikarudia kuitazama picha ya Mariam kwa mara nyingine, japo nilijidanganya na msemo unao sema duniani watu ni wawili wawili, ila moyoni mwangu hicho kitu sikikubali kabisa. Nikatoa bastola zangu kwenye pochi yangu nikatoa magazine moja baada ya nyingine, nilipo hakikisha kwamba zipo sawa nikazirudisha kwenye kijipochi. Nikawasha gari langu na kuondoka porini hapa. Nikafika kwenye hoteli ya Blue Peal liyopo Ubungo, nikaingia kwenye moja ya mgahawa na kupata kifungua kinywa huku nikiwa na mawazo mengi sana kichwani mwangu nikifikiria jinsi ukubwa wa uwanja wa Taifa na jinsi kazi ambayo nitakwenda kuifanya.
 
“Dada Dada”
Muhudumu aliniita na kunifanya nitoke kwenye dibwi kubwa la mawazo na kumtazama. Akanikabidhi kikaratasi.
“Cha nini?”
Nilizungumza kwa sauti ya kike huku nikiwa nimemtazama usoni mwake
“Kwa yule kaka pale”
Akanionyesha jamaa aliye kaa kwenye moja ya kibanda akiwa peke yake akinywa maji yake taratibu. Nikakichukua kikaratasi hicho na kukifungua na kukuta maandishi yaliyo andikwa namba ya simu. Nikakikunja na kumrudishi muhudumu ambaye amesimama akisuribiria jbu
“Muambie sihitaji upuuz”
“Sawa”
Muhudumu akaondoka akiwa ametabasamu, hata chai ambayo ninakunywa sikuona ladha yake kutokana na msongamano wa mawazo. Jamaa aliye tuma kikaratasi nikamuona akinyanyuka huku ameshika chupa yake ya maji na kuanza kuja sehemu nilipo, nikagundua kwamba hawa ndio wanaume wanao data kwa kusa ya mwamke pasipo kufahamu kwamba mimi ni mwanaume mwenzake tena rijari sana.
 
“Habari yako dada?”
Alinisalimia huku akininyooshea mkono wake, sikuhitaji kuupokea mkono wake huo zaidi ya kuutazama. Akaurudisha huku akikaa kwenye kiti cha pembeni.
“Nimeona nisiondoke hivi hivi pasipo kuja kukusalimia mtoto mrembo kama wewe. Kusema kweli nimeona wasichana wengi ila wewe umewazidi wote aisee”
Jamaa huyu mwenye lafudhi ya kisambaa alizungumza maneno yake huku akitabasamu, jambo lililo zidi kunikera.
“Najua mtoto mzuri kama wewe, unatakiwa kuwa na wagosi wajanja kama sisi. Hapa nimefikia kwenye hii hoteli hapo pembeni kama vipi twende basi tukaenjoy”
“Umemaliza?”
“Hapana mremboooo, hata ukitaka milioni moja mimi nakupa, tena tunakwenda kucheki mechi ya Simba na Yanga mchana”
“Nakuomba undoke mbele ya uso wangu kabla sijakudhalilisha”
Nilizungumza kwa sauti ya kike, ila jamaa huyu akacheka kicheko hadi watu walio kaa vibanda vya pembeni wakatazama sehemu tuliyopo.
“Binti mimi ninapesaa, nitakununulia chochote unacho kihitaji acha kunywa chai binti mzuri kama wewe”
 
Nikashusha pumzi kidogo huku nikimtazama jamaa huyu, nikatabasamu huku nikilegeza macho kidogo
“Ok twende”
“Kweli?”
“Yaa twende”
Nikanyanyuka, nikachukua kipochi changu na kuongozana na jamaa huyu mwenye sura mbaya japo mimi ni mwanuame ila Mungu amenibariki kunipa sura na hata zoezi langu la kujiweka kama mwanamke linafanikiwa kirahsi kutokana na sura yangu ila kama ningekuwa na sura kama ya huyu jamaa basi zoezi lingekuwa ngumu. Tukaingia kwenye mlango wa hoteli hii, moja kwa moja tukaelekea eneo la lifti, akafungua na sote tukaingia. Tukafka gorofa la tano na kuelekea kwenye chumba.
Akafungua mlango wa chumba chake kwa kadi maalumu ya kufungulia mlango huo na tukaingia ndani.
“Binti ninapesa nyingi sana nipe mambo”
“Weka pesa mezani nikupe mambo”
“Pesa tu ngoja”
Akafungua kabati lake, akatoa begi la mgongoni na kulifungua, akanionyesha noti zake nyingi zilizo fungwa na rababend. 
 
“Nipe tu mrembo pesa hapa ipo”
Alizungumza huku akinisogelea, akanishika kiuno, changu. Kwa kasi ya ajabu nikamshika mkono alio nishika kiuno, nikamgeuza na kumlaza chini, sikutaka kumupiga na kumuumiza, nikauchomoa mkanda wa suruali yake na kuanza kutandika mikanda mfululizo kwa kumshikisha adabu, kila alicho jaribu kujinasua mikononi mwangu akajikuta akishindwa kutokana nina ujuzi mkubwa wa kupambana na mtu kuliko yeye pili nina nguvu kumpita.
Nilipo hakikisha ameorojeka kwa kichapo cha mkanda wake, nikamlaza kifudi fudi na kuifunga mikono yake kwa nyuma kwa mkanda huo. Kisha nikachukua rimoti ya Tv na kuiwasha Tv kubwa liyopo ndani humu.
“Mpira wa Simba na yanga utautazama humu ndani mr sawa”
Nilizungumza kwa sauti nzito jambo lililo mfanya atokwe na macho ya mshangao. Katika kutazama taarifa kwenye hii Tv nikasikia taarifa kwamba mgeni rasmi kwenye mechi ya Simba na Yanga ni raisi wa hii nchi.
 
“Shitiiii”
Nilizungumza huku nikitazama Tv hii, mtangazaji akazidi kuzungumza kwamba raisi ataongozana na mkewe na mtoto wake. Nikatoka nje ya chumba hichi nikimuacha jamaa huyu akiwa chini akijibiringisha akitafuta jinsi aya kusimama. Moja kwa moja nikaelekea kwenye gari langu, nikaingia na kuondoka. Nikaelekea maeneo ya uwanja wa Taifa wa mpira wa miguu, moja kwa moja nikaelekea kwenye ofisi za kuka tiketi za kuingilia katika kiwanja. Kutokana magari yanaruhuswa kuingia kwenye uwanja huu wa kisasa wenye maegesho ya magari ndani kwa ndani, sikuona ubaya wa kulipia gari langu huku nikiwa na kazi moja kuhakikisha ninaokoa maisha ya watu ambao wamekususia kuja kulipoa kwenye uwanja huu. Gari langu nikalisimamisha kwennye moja ya maegesho ya ndani. Nikashuka kwenye gari, saa ya simu yangu inaonyesha ni saa saba mchana na kuna watu mashabiki wamesha anza kuingia uwanjani. 
 
Sikutaka kuingia uwanjani na bastola kwa maana kuna mashine maalumu ambazo hukagua watu wanao ingia na silaha. Moja kwa moja nikaelekea ndani ya uwanje, sikuhitaji kuelekea kwenye siti niliyo lipia, nikaanza kuzunguka uwanjani huku nikiwa makini sana kuzitafuta sura ambazo tayari kwa sasa nina zifahamu. Japo ulinzi wa askari ni mkali sana ila natambua hawatambui ni kitu gani kinacho endelea. Hadi inafika saa nene kamili sikuona mtuhumiwa hata mmoja, sikukata tama kwa maana muda huu watu ndio wanazidi kumiminika kiwanjani kutazama mechi hii ya watani wa jadi. 
 
Haja ndogo ikanishika, sikuwa na budi zaidi ya kuamua kueleka kwenye vyoo, sikuhitaji kuingi kwenye vyoo vya kiume kutokana na muonekano wangu, nikainga kwenye vyoo vya kike ambavyo wa kwati huu hakuna mtu zaidi yangu, nikaingia kwenye moja ya kijichoo na kujihudumia haja ndogo huku nikiwa makini hakuna mtu anaoniona jinsi ninavyo jisaidia haja ndogo kwa maana nimesimama kama kawaida. Nilipo maliza nikajiweka nguo zangu kama kawaida. Nikafungua kijimlango cha choo nilichopo, kitendo cha kupiga hatua mbili mbele nikamuona Marima akingia ndani ya choo huku akiwa ameshika begi mkono wa kushoto ambalo linaonekana limejaa vitu vizito.

                                          AISIIIII……….U KILL ME 58

Tukakatazama na kwa mda na Marima kisha akanisalimia huku akiwa ameweka tabasamu pana usoni mwake. Akanipita pembeni yangu na kuingia katika choo ambacho nimetoka mimi akiwa na beg lake. Nikatamani mlango wa choo hicho ila wakainga wadada wengine wawili wakiwa wanacheka sana wakiendelea na stori zao. Nikajikausha, nikatembea hadi sehemu ya kunawia mikono taratibu nikaanza kunawa mkono huku nikiwasubiria wadada hawa wawili watoke kisha niufunge mlango kwa ndani na nibaki na Marim tu.
Wadada hawa wakafanya walicho waleta humu kisha wakatoka, kwa haraka nikausogelea mlango na kuufunga. Kitendo cha kugeuka nyuma nikakutana na Mariam akiwa amenishikia bastola iliyo fungungwa kiwambo cha kuzuia sauti ya risasi pale inapo toka na kaama ni kunipiga risasi anaweza kunipiga pasipo mtu yoyote kuweza kugundua kitu ambacho kimetokea ndani.
 
“Marima”
Niliita na kujiwahi kumtaja jina lake kwa maana ninaelewa kitu ambacho kinakwenda kutoka, hususani mtu akiwa katika kikundi kama hichi cha magaidi huwa wanapandikizwa roho ambayo ni mbaya sana na huwa hawana huruma kabisa likija swala la wao kufwatiliwa.
“Umelijuaje jina langu?”
Marima aliniuliza huku akiwa ameikunja sura yake. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuzungumza kwa sura yangu halisi ya mwanaume.
“Mimi ni Dany, nimektafuta siku zote mpenzi wangu”
Marima akacheka kwa dharau huku akiendelea kuishia bastola yangu, hakunielewa kabisa kwa kile ambacho ninakizungumza. Akaikoki bastola yake vizuri, kabla hajafanya maamuzi yake ambayo tayari nilishasoma, nikamrukia na kumungusha chini, bastola yake ikaangukia pembeni. Marima akajitoa mikononi mwangu na kusimama kwa haraka, akajaribu kunipiga teke ila nikabingiria na pembeni na teke hilo likapita pasipo kunipata. 
 
    Nikanyanyuka huku nikiwa makini sana, Mariam paisipo kufikira mara mbili akaanza kurusha mateke mfululizo. Kusema kweli Marim amabadilika sana kwani ufanisi wake katika kupigana upo vizuri na mafunzo aliyo yapata yameweza kumsaidia sana. Sikutaka kumpiga Marima kwa maana hatambui halitendalo na kama ni uwezo wa kupigana nimemzidi kwa kiasi kikubwa. Kitu ambacho ninakifanya ni kumkwepa mateka yake. Marim akachomo kisu kwenye kiatu chake alicho kivaa, akaendelea kufanya mashambulizi ambayo yote niliweza kuyakwepa.
“Marima acha  kukifanya unacho kifanya unajisumbua”
Nilizungumza kwa ukali huku nikiwa nimethibiti kwa kumpiga kabari ya shingo huku mkono ulio shika kisu chake nikiwa nimeuthibiti vizuri.
“Dany tangu lini umekuwa mwanamke?”
“Tulia nikuonyeshe”
Nikamsukuma Marim pembeni umbali ambao hato weza kunishambulia. Nikavua wigi nililo livaa na ninakabakiwa kwenye sura yangu ya kawaida. Marima akanishangaa jinsi nilivyo kwa maana muda wote hakuamiini kwamba mimi ndio Dany halisi.
“Mimi ni Dany halis, mwanaume niliye kutoa bikra yako”
“Dany ulikuwa wapi siku zote?”
 
“Ni historia ndefu, ila natambua ni kitu gani kinacho endelea kwako kwa muda huu”
Marim kwa haraka akanifwata na kunikumbatia kwa nguvu huku macho yakimwagka usoni mwake. Tukajikuta tukianza kunyonyana mdomo yteu kwa hisia kali sana huku kila mmoja akiwa anahema kwa pumzi nzito sana.
“Baby hatuna muda wa kuendelea kukaa hapa naomba unieleze ni wapi mulipo yatega mabomu?”
“Umejuaje ikiwa wewe bado ni gaidi?”
“Natambua  nyendo zetu ndio maana nipo hapa na ninamshukuru Mungu kwa kunikutanisha na wewe”
Marima akachukua wigi mkononi mwangu na kunivalisha kichwani mwangu, akaliweka vizuri. Kisha akaingia kwenye choo ambacho niliingia. Nikamfwata kwa nyuma, akanitoa bumo moja alilo kuwa amelitega nyuma ya mlango wa choo hichi.
“Kuna mabomu zaidi ya kumi yamo ndani ya huu uwanja, mimi nina mawili wezangu watatu nao wana mabomu mawili mawili kila mmoja”
 
“Yesu wangu!!”
Nilijikuta nikizungumza hivyo huku nikimtazama Marima usoni.
“Kila bomu moja lina kilo hamsini na mlipuko wake unaweza kuangamiza vitu vilivyopo zaidi ya umbali wa mita mia tano kutoka hapo lilipo”
Marim alinipa mazungumzo hayo huku akilizima bomu hilo ambalo tayari alisha litega tayari kwa mashambulizi.
“Sasa tunafanyaje?”
“Hapa kitu kibaya ziaidi ni kwamba sifahamu ni wapi wezangu walipo na kila mtu aliweza kuingia kwa njia yake na kati ya wote mimi ndio mwanamke”
“Hilo ninalifahamu, je una namba za hao wezako?”
“Tukiwa katika mission kubwa kama hii huwa simu hatuwashi na wala hatuwi na mawasiliano ya aina yoyote hii inasaidia kuepusha muingiliano wa kazi na ndani ya dakika kumi hichi kiwanja kinakwenda kuwa chini juu, juu chini na raisi akiwa ndani”
 
Maneno ya Marima yakazidi kunichanganya, akaliweka bomu lake kwenye begi kisha akaokota bastola yake sehemu ilipo, tukatoka chooni na kusimama nje ya mlango kutazama ni wapi ambapo tunaweza kuanzia kwa maana kila sehemu imejaa watu wengi na mpira umesha anza kuchezwa kiwanjani na kinacho tawala sasa hivi ni kelele za mashabiki.
“Una simu hapo?”
“Ndio”
“Iwashe tuweze kupata kufahamu ni wapi wezako walipo?”
“Nikiwasha simu ni kosa kubwa sana, makao makuu watafahamu na zoezi linaweza kuharakishwa kufanyika hata ndani ya dakika tano milipuko ikaanza kulipuka hapa uwanjani”
Nikatoa smu yangu kwenye siridia yaliyo yabana maziwa haya ya bandia. Nikampigia mama, simu yake ikaita kwa muda.
“Mama kuna kaz hapa nahitaji unisaidie?”
“Kazi gani?”
Nikaanza kumpa maelekezo mama ya kufanya pamoja na kuanza kumtajia namba za mabomu ambayo Marim amezishika kwa kichwa.
 
“Dakika moja nipe”
Nikakata simu huku nikia ninahema, wasimwasi mkubwa umenitawala, ila Marima hakuonyesha wasiwasi wowote.
“Ila Dany huu ndio mthani wangu wa mwisho nikifanikiwa katika mlipuko huu ninapewa cheo kikubwa sana kwenye kikundi changu”
“Marima hapa hatuzungumzii kuhusiana na cheo unacho kwenda kukipata. Hapa tunazungumzia kuhusiana na maisha ya watu, maisha ya wamama, watoto wababa na kiongozi wa nchi. Ni damu za watu wangapi zitamwagika na isitoshe mama yako anaweza kuwepo eneo hili je yeye unataka aweze kufa?”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimemkazia macho Marim usoni mwake hadi machozi yakamlenga lenga.
“Kwani mama yangu bado yupo hai?”
“Yupo hai na jana nilikuwa naye nyumbani kwenu, mama yako amebaki mpweke, anafanya kazi kwenye hoteli na anadhalilisha na mabosi wake kwa kutukanwa, yote kwa sababu haupo, laiti ungekupo na ungekuwa umeajiriwa ungemsaidia na yeye akaka nyumbani na kula matunda yako”
 
Nilizungumza maneno ya kumuhamasisha Mariam hadi machozi yakaanza kumwagika usoni mwake. Mama akapiga simu, nikaipokea kwa haraka
“Hayo mabomu yote yapo ndani ya uwanja, na sita yametengwa chini ya viti vya viti vya mashabiki ambavyo havina watu. Mawili yametengwa chini ya gorofa alipo raisi,  kwa hiyo yakilipuka kwa chini raisi anashuka na watu wake”
“Sasa mama vtu hapa vipo vingi”
“Nakutumia ramani inayo onyesha mabomu yote sehemu yalipo”
“Asante mama”
Nikakata simu huku nikishusha pumzi, marima akatazama simu yake ya mkononi, kisha akanitazama usoni mwangu.
“Zimebaki dakika saba”
“Mungu wangu”
Ujumbe ulio ingia kwenye simu yangu kupitia emila, nikaufungua na kuona ramani ambayo inaonyesha mabumu hayo yalipo kwa kuonyesha alama nyekundu inayo waka waka na kuzima.
“Tunatakiwa kuhakikisha kwamba mabumu yote tunaweza kuya tegua”
 
“Huwezi kuyategua peke yako pasipo mimi kwa maana ni lazima kuingiza namba ya siri ili yasilipuke”
“Eheee. Ok”
Tukaanza kazi ya kukimba kwa haraka huku Mariam akiwa amelivaa begi lake mgongoni. Tukafanikiwa kufika lilipo bomu la kwanza, Marim akalitoa chini ya kiti kwa haraka akaingiza namba ya siri na bomu hilo likazima. Ikawa ni mshike mshike kuhakikisha kwamba tunayategua mabomu yangu, kazi yangu kubwa ni kuongoza ni wapi yalipo mabumu hayo.
    Kadri jinsi tulivyo zidi kuoyategua mabumu hayo ndivyo jinsi muda ulivyo zidi kupungua tena kwa kasi sana.
“Yamebaki mawili kule”
Marim alinonyesha sehemu alipo kaa raisi pamoja na wapambe wake, umbali uliopo kati ya eneo tulipo na alipo kaa raisi ni kama mita mia moja na kumi ni lazima kuhakikisha kwamba tunakatiza katika kiwanja ili kufika eneo hilo.
“Niambie namba za siri”
Marima akanitajia kwa haraka namba za siri, nikazikremisha. Nikataka kuondoka Marima akanishika mkono wa kulia.
“Watu wote wanakutegemea wewe, na zimebaki sekunde sabinini tu”
 
“Sawa”
Mariam hakujali wingi wa watu walipo uwanjani, akanipiga busu la mdomoni kisha akaniachia mkono wangu, simu yangu nikaishika vizuri na kuanza kuporomoja kwenye ngazi zilizopo kwenye huu uwanje, nilipo fika kwenye fensi nikaziruka na kuingia uwanjani jambo lililo wafanya baadhi ya watu kunishangaa dada mzuri nikikatiza kiwanjani tena ninakimbia.
Polisi wakaanza kunifukuzia kwa nyuma, sikulijali hilo nilicho hakikisha ni kwamba ninaongeza mwendo wa miguu yangu kufika sehemu yalipo mabomu hayo. Watu wakazidi kushangilia, hata wachezaji wenyewe wakabaki wakiwa wamesimama wakinishangaa. Polisi wawili wakanizuia njia wakiwa wmashika virungu, nilicho kifanya ni kuruka juu ya kifua cha mmoja kwa kutumia mguu wangu wa kulia kisha huyu mwengine nikammalizia kwa kumtandika teke lililo mpeleka chini. Uzuri wa gauni nililo livaa lina mpasuo wa kutosha na litavutika kwa kiasi kikubwa na hata kitendo nilicho kifanya kikawa chepesi sana. 
 
‘Sekunde hamsini’
Nilijisema kimoyo moyo huku nikirukia fensi za kuingilia upande wa pili chini ya jukwaa alipo kaa raisi, kwenye baadhi ya viti viwili ndipo yalipo mabumu hayo. Nikapandisha ngazi kwa haraka, cha kushukuru Mungu mashabiki hawakunizuia, walicho kifanya ni kupiga makofi wakinishangilia pasipo kufahamu kwamba vicheko vyao dakika chache vinaweza kubadilika na kuwa vilio vya kusaga meno kwa uchungu. Nikafika kwenye kiti cha kwanza, nikalichomoa bumu chini ya kiti jambo lililo wafanya hata mashabiki kubaki wakiwa wameduwaa. 
 
Nikaingiaza namba za siri kwa haraka, bomu likazima sekunde zimebaki ishirini tu na bomu jengine lipo kiti cha mbali kidogo na sehemu nilipo, sikukata tama zaidi ya kuzidi kukimbia kueleke kwenye bomu hilo lilopo na kama ni kulipuka basi litanilipukia na mimi na nitakuwa mmoja wapo kati ya watu watakao kufa.
Nikafanikiwa kufika lilipo, nikalitoa chini ya kiti na kuanza kuingiza namba za siri huku sekunde zikiwa zimebaki saba. Cha kushangaza namba za siri nilizo ziingiza, zikakataa na sekunde za bomu zikazidi kurudi nyuma, sikuraka kuchanganyikwa, nikatuliza kichwa watu walio pembeni yangu wote wakakimbia na kuaniacha peke yangu
‘Sekunde nne’
Nilijiseme moyoni huku nikiingiza tena namba ya siri ambayo Marim aliniambia. Polisi walio kuwa wakinikimbiza nao wakasimama mbali na mimi kwa maana katika kufa hakuangalii kama wewe ni polisi au laa. Nikaiingiza tena namba ya siri aliyo niambia Marima ila nayo ikagoma jambo lililo nifanya nikate tamaa na nikabaki nikitazama sekunde mbili ziishe na tulipuke na kufia katika eneo hili
                                                                                  ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts