Home » , » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 59 na 60 )

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 59 na 60 )

Written By Bigie on Saturday, March 24, 2018 | 3:54:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA      
‘Sekunde nne’
Nilijiseme moyoni huku nikiingiza tena namba ya siri ambayo Marim aliniambia. Polisi walio kuwa wakinikimbiza nao wakasimama mbali na mimi kwa maana katika kufa hakuangalii kama wewe ni polisi au laa. Nikaiingiza tena namba ya siri aliyo niambia Marima ila nayo ikagoma jambo lililo nifanya nikate tamaa na nikabaki nikitazama sekunde mbili ziishe na tulipuke na kufia katika eneo hili

ENDELEA
Wazo moja likanijia kichwani mwangu, kwa haraka sikuhitaji kuweza kulizembea kirahisi. Nikaandika jina la nchi ya Somalia kwenye batani za hili bomu, nikayafumba macho yangu kusubiria kulipuka kwa bumu hili huku nikisali sala yangu ya mwisho. Sekunde ambazo nilikuwa ninazisubiria ili bumu kuweza kulipuka zikapita pasipo chochote kutokea. Taratibu nikayafumbua macho yangu nikakuta bomu hili limezima. Jasho mwili mzima linanishuka, watu wote uwanjani walibaki wakinitazama mimi huku wengi wao wakiwa wamekaa umbali mkubwa kutoka sehemu nilipo hata mpira ulisimamishwa kutokana na taharuki hiyo iliyo jitokeza hapa uwanjani.
Nikamuona Mariam kwa mbali akinipunga mkono huku akininyooshea kidole gumba cha mkono wa kulia. Polisi wakaanza kunisogelea huku wakiniomba ninyooshe mikono juu, siwezi kukimbia kwa maana karibia polisi wote wamenizunguka.
 
Mashabiki walipo ona polisi wanataka kunifunga pingu mikononi, wakaanza kupiga kelelele huku wakikimbilia eneo nililopo na polisi hawa.
Hiyo ndio ikawa nafasi kwangu kuwatoroka polisi huu kwa maana umati mkubwa wa mashabiki umewazuia wasinikamate. Moja kwa moja nikaelekea kwenye maegesho ya magari, nikiwa ninalitafuta gari langu sehemu nikastulia risasi ikipiga kwenye moja ya gari la pembeni hadi kioo cha gari hilo kikapasuka, kwa haraka nikachuchumaa chini, na kujibanza kwenye gari hilo. Nikamuona Yudia akiwa na vijana wawili wenye bastola wakinyata kwa uangalifu wakija sehemu nilipo. Kitendo cha kuchungulia nikastukia risasi nyngine ikipiga kwenye gari hili na kujikuta nikirudi kukaa chini sehemu nilipo jificha huku nikihema sana kwa wasiwasi.
“Wewe malaya jitokeze huwezi kuharibu mipango yetu”
 
Yudia alizungumza kwa ukali jambo lililo nifanya nizidi kukaa chini nikifikiria nini cha kufanya kwa manaa, sina silaha yoyote ambayo inaweza kuniwezesha kupambana nao. Wakaendelea kufyatua risasai mfululizo ambazo zinatoka kimya kimya kutokana na  viwambo vya kuzuia sauti walivyo vifunga kwenye risasi zao.
“Wewe malaya toka hapo chini lazima tukuue ku**ko”
Yudia akaendelea kurupoka, kwa bahati nzuri nikasikia milio ya risasi, katika kuchungulia nikaona polisi wakishambuliana na kina Yudia wakihakikisha kwamba wanawaweka kati. Sehemi nilipo sikuweza kujitoa kutokana na mirindimo hiyo ya risasi ambayo sikufahamu zinaelekea wapi.
“Wekeni mikono juu na bunduki pembeni”
Niliisikia sauti ya kiume ikizungumza kwa kuamrisha, taratibu nikajinyanyua na kuchungulia sehemu inapo tokea nikamuona Yudia pamoja na jamaa mwengien wakinyoosha mikono yao juu, huku mmoja akiwa amelala chini akivunjwa na damu. 
 
“Heii na wewe nyanyuka”
Nilistuka sauti ya askari ikizungumza pembeni yangu, taratibu nikanyanyuka huku nikinyoosha mikono yangu juu. Yudia na mtu wake wakafungwa pingu, huku mimi nikiombwa kuongozana na askari wanne kuelekea katika chumba cha mahojiano ndani ya uwanja huu. Kutokana hakuna askari aliye weza kugundua kwamba mimi ni mwanaume, sikuweza kubisha nikaongozana nao hadi kwenye chumba cha mahujiano. Hapo nikakutana na mkuu wa askri wa upepelezi ambaye ninamfahamu vizuri japo yeye hanifahamu mimi. Askari walio niingiza kwenye chumba hichi wakatoka na kuniacha na mkuu  wao huyu.
“Binti unaitwa nani?”
“Lissa”
“Kwanza nitangulize shukrani zangu kwa kuweza kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania wengi katika huu uwanja. Pia…..”
Akanyamaza kimya baada ya simu yangu kuita, nikatazama ni nani anaye piga na kukuta ni mama ndio anaye piga, ikanibidi kupokea mbele ya mkuu huyu wa polisi  kitengo cha upelelezi.
 
“Ndio mama”
Nilizungumza kwa sauti ya kike.
“Vipi mbona unazungumza na sauti ya kike”
“Mama nahojiwa na polisi, nitakupigia baadae”
“Wamekukamata au kwa maana nimekuona kwenye Tv?”
“Hapana hawajanikamata wanahitaji kunihoji tu mama”
“Ahaa sawa kuwa makini nao wasifahamu uhalisia wako”
“Sawa mama”
Nikakata simu huku nikitabasamu
“Mama yako naamini anajifu kuwa na mtoto wa kike kama wewe”
“Yaaa hapa ananiambia kwamba ameniona kwenye Tv”
“Kweli naona waandhishi wa habari waliweza kuchukua picha zako. Ehee niambie ulifahamu vipi kwamba hapa uwanjani kuna mabomu?”
Nikanyamaza kimya kwa muda huku nikimtazama askari huyu kisha nikamjibu.
“Nilipo kuja hapa uwanjani, mapema sana leo, niliona kuna kaka watatu kwenye maegesho ya magari kule juu wakipanga mikakati ya kulipua huu uwanja. Nilianza kuwafwatilia nikaona jinsi wanavyo yatega chini ya viti hapo ndipo nilipo anza kutegua moja baada ya jengine, sasa yale ya mwisho mawili ndio yaliuwa kule kwa raisi”
 
Mkuu huyu wa polisi kitengo cha upelelezi akaka kimya kwa muda huku akiwa anatafakari kitu, kabla hajazungumza kitu chochote mlango ukafunguliwa na akaingia raisi na walinzi wake wawili huku mmoja wapo akiwa ni Babyanka. Nikajikausha kimya, mkuu wa polisi akanyanyuka kwenye kiti na kusalimiana na raisi.
“Binti habari”
Raisi alinisalimia huku akitabasamu, nikanyanyuka kwenye kiti na kuinama kwa heshima huku nikimsalimia.
“Aisee sijawahi fikiria kwamba hii nchi kuna wanawake majasiri ambao wanaweza kufanya kitu kama ulicho kifanya wewe leo”
“Asante sana muheshimiwa”
“Hivi umepitia kozi yoyote ya jeshi?”
“Hapana”
 
“Aiseee hongere sana. Mwaseba huyu anafaa kuingia kwenye kikosi chako bwana hakikisha munamchukua alicho kifanya sijawahi kuona kwenye maisha yangu”
“Sawa mkuu”
“Binti kusema kweli naruda tena kukushukuru kwa kile ulicho kfanya leo, nimetoka kuangalia yale mabomu kusema kweli leo ingekuwa ni historia mpya ya huzuni ingesomeka kwenye nchi yetu”
Nikatabasamu tu kwa maneno ya muheshimiwa raisi ila kimoyo moyo nikawa ninajisema kwamba laiti isinge kuwa mama yangu leo mbona wangefurahi na roho zao kwa maana ni lazima wangekufa.
“Ngoja nikaandae mpango japo leo uje kula chakula cha usiku ikulu”
“Asante sana muheshimiwa”
“Hembu nipatie namba yako ya simu”
Nikamtajia riaisi namba yangu ya simu, akainakili kwenye simu yake kisha akanipatia mkono na kuniaga, akaondoka na walinzi wake na nikabaki na mkuu wa polisi.
 
“Naona muheshimiwa raisi amekukubali”
“Yaa”
“Sasa ningeomba ombi moja kama alivyo seme muheshimiwa raisi unaweza kujiunga na kitengo cha polisi upande wa upelelezi na ukawa ni miongoni mwa vijana wangu”
“Mmmm siwezi kufanya maamuzi hayo peke yangu nilazima kumshirikisha mama yangu”
“Hilo halina tabu kwa maana ninatambua kabisa mama ndio kila kitu. Vipi baba yako sijasikia ukimzungumzia?”
“Baba alisha fariki tangu nikiwa bint mdogo”
“Aisee pole sana, sasa nipatie namba yangu na wewe uchukue namba yako ili tuweze kuwasiliana na wewe”
“Sawa muheshimiwa”
Nikamtajia namba yangu ya simu kisha na yeye akanitajia namba yake ya simu. Tukaagana na kuondoka katika chumba hichi huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa moyoni mwangu nikiamini mbinu ya kujifanya ni mwanamke imefanikiwa. Nikajikuta nikikohoa huku nikirekebisaha koo langu kwa maana kuzungumza sauti ya kike sio jambo rahisi. Nikaelekea kwenye gari langu, nikaingia huku nikishusha pumzi. 
 
Kabla sijaondoka kioo cha mlango wa dereva ukagongwa, taratibu nikashusha kiooo na kukutana na sura ya K2 akinitazama huku anatabasamu.
“Hongera binti”
Alizungumza huku akiubenua mdomo wake kwa dharau, moja kwa moja nikafahamu maana ya yeye kufanya hivyo.
“Asante”
“Ila take care usiingilie vitu visivyo kuhusu, utakufa”
Alizungumza maneno yaho huku akinyanyuka na kuondoka zake sikuhitaji kuzungumza chochote zaidi ya kufunga kioo cha gari langu na kuondoka eneo hili la uwanjani. Nikatoka nje ya uwanja salama salimini, nikatafuta maduka ya simu maeneo ya kariakoo nikanunua chaji ya smu yangu kwa maana imsha anza kupiga milio inayo ashiria kwamba chaji imekwisha, nikafanikiwa kununu chaji ya simu hii niliyo nayo, nikaondoka eneo la Kariakoo na kueleke kwenye moja ya hoteli iliyopo Mbezi Beach.
 
“Nitaka kwa siku saba”
“Sawa unaweza kufanya malipo na tukakufanyia punguzo la bei kutokana na kukaa kwa siku nyingi katika hoteli yetu”
“Ok nafanya kwa dola si sawa?”
“Ndio hakuna shida dada yangu”
Nikamuhesabia muhudumu kiasi cha pesa anazo zihitaji kisha akajaza jina langu na namba ya kitambulisho kwenye kitabu cha kumbukumbu za wageni, akanipa kalamu na kitabu hicho nikasaini kisha akanikabidhi funguo yangu na kueleke kwenye chumba changu nkiwa na beg langu la nguo.
Nikaingia ndani ya chumba hichi nikajifungia kwa ndani, nikaweka simu yangu kwenye chaji pasipo kuizima, nikavua nguo zote pamoja na umbo la plastki ambao hadi sasa hivi hakuna ambaye amweza kunifahamu uhalisia wangu. Nikaingia bafuni na kuoga kisha nikarudi chumbani, nikatoa laptop yangu na kuiweka juu ya kitanda, nikaiwasha na kungia kwenye mitandao ya kijamii kuangalia ni kitu gani ambacho kinaendelea, kutokana na uchomu nikajikuta usingizi mzito ukinipita.   
 
    Mlio wa mtetemesho wa simu yangu nikaanza kuusikia kwa mbali, taratibu nikaanza kufumbua amcho yangu kwa uvivu yaliyo jaa usingizi mzito. Muito ulipo zidi kudumu nikanyanyuka kabisa kitandan na kuichukua simu uliyopo juu ya sofa, nikakuta ni namba ngeni inayo piga, nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Habari binti”
Nikaisikia sauti ya muheshimiwa raisi, kwa haraka nikajitahdi kuibadilisha sauti yangu.
“Salama tu muheshimiwa za muda?”
“Salama sasa nimeandaa chakula cha usiku kwa ajili yako, upo wapi vijana wangu waje kukuchukua?”
Nikamtajia jina la hoteli niliyopo, akasema anaifahamu na anatuma vijana wake, baada ya nusu saa watakuwepo kwenye hoteli hii. Akakata simu, nikeeleke bafuni kuoga kwa haraka haraka, ili kutoa uchovu kisha nikarudi chumbani. Nikaanza kuvaa tisheti yangu aliyo nipatia mama, kisha nikavaa
na vazi la plastiki ambalo kwa haraka haraka lina nipa umbo la kike kwa maana lina maziwa pamoja na makalo makubwa kiasi.
 
Nikaanza kumwaga nguo kwenye kitanda kutafuta gauni gan nivae, nikaonga gauni la rangu nyekundu, nikalivaa, nikachukua wigi langu na kulichana vizuri na kuliweka kichwani mwangu. Ndani ya robo saa nikawa nimemaliza kujiandaa. Na muonekanao wangu ukazidii kuwa kama msichana, kwa maana kwa sasa ninajua jnsi ya kujipara vilivyo.
Ndani ya nusu saa kama alivyo zungumza rasisi, simu ya mezani kwangu ikaita, nikaisogelea na kuipoke.
“Samahani dada yangu una wageni kutoka ikulu”
“Asante ninakuja”
“Sawa dada”
Nikachukua kipochi changu, bastola zangu nikaziweka kwenye begi la nguo na kuondoka nikiwa na vitambulisho vyangu pamoja na pesa kadhaa kwenye kipochi changu.  Kila mwanaume niliye kutana naye kwenye kordo yangu hakusita kugeuza shingo yake nyuma kunitazama jinsi nilivyo pendeza. Nikafika mapokezi na kukutana na Vijana wawiliw alio valioa sut nyeusi wakiwa wamekaa kwenye sofa za mapokezi.
“Habar yako dada?”
“Salama”
“Tunaweza kuondoka sasa”
“Hakua shaka”
Nikatoka nao nje, na kuelekea kwenye gari lao aina ya bmw Z8.
“Ohoo jamani samani nimesahu simu yangu ndani naombeni nikaichukue”
 
“Hakuna shida dada yetu”
Nikarudi ndani kwa haraka nikafungua chumbani kwangu na kuchukua simu yangu niliyo iacha juu ya sofa nikaiweka ndani ya pochi yangu na kutoka ndani ya chumba changu huku nikifunga mlango. Nikawakuta vijaa hao wakinisubiria, nikaingia ndani ya gari na kuondoka nao huku nikiwa nimekaa siti ya nyuma.  Ukimya ukatawala ndani ya gari huku nikmtazama dereva anavyo zidisha na kupunguza mwendo kasi wa gari, ila machale yakaanza kunicheza pale dereva alipo badilisha njia.
“Tunaelekea wapi?”
“Tunapita barabara ya huku chini, huko juu kuna foleni kubwa”
Ikabidi kukaa kimya kwa miaka hii miwili ambayo sikuwa Dar es Salaam labda barabara zimeongezeka, ila tukwa katkat ya safari tukstukia gafla gari mbili aina ya Range rove, moja ikifunga barabara kwa mbele na nyingine ikifunga barabara kwa nyuma jambo llilo mfanya dereva kufunga breki za gafla na kusimama. Cha kushangaza dereva na mwenzake wakashuka na kwenye gari nikabaki peke yangu mbaya zaidi dereva ameshuka na funguo, na kwenye gari hizo wakashuka jamaa si chini ya kumi wakiwa na bunduki zenye uwezo mkubwa na kuanza kulishambulia gari nililomo jambo lilili nifanya nilale chini kwenye siti yangu huku vioo vikiniangukia mgongoni

                        AISIIIII……….U KILL ME 60

Milio ya risasi ikazidi kutawala huku nikishuhudia jinsi gari hili linavyo shambuliwa, na mashabulizi yakizidi zaidi ya hapa gari hili litalipuka muda wowote jambo ambalo ni hatari kwangu. Nikakumbuka kwamba nimevaa tisheti ambayo mama aliweza kunipa maelekezo ambayo kwa tukio hili lililopo sasa hivi itanisaidia kwa kiasi kikubwa. 
 
Nikafungua mlango na kujirusha nje huku nikibingirika kwa haraka huku kipochi changu nikiwa nimekishika vizuri mkononi, kuelekea pembezoni mwa barabara. Majambazi hawa ambao natambua ya kwamba wametumwa mahususi kuja kunimaliza, wakaanza kuelekezea risasi zao upande ninao elekea, uzuri ni kwamba sehemu nilipo ingia kuna kichaka ambacho kina uchochoro wa miti miti kadha. Nikajibanza kwenye moja ya mti huku nikihema. Ukimya ukatawala, majambazi hao wakaanza kunitafuta kwenye kichaka hicho nilicho ingia.
Nikamuona mmoja akimpa ishara mwenzake kwamba ni sehemu gani ambayo nipo, jambazi huyu akaanza kuninyatia tarataibu, nikapata wazo la haraka nikatoa simu yangu kwenye kipochi nikaingia upande wa kamera, kutumia mwanga wa kamrera nikampiga picha jambazi aliye karibia kufika sehemu nilipo, kitendo kilicho mfanya afumbe macho. Kwa haraka nikapokonya bunduki yake aina ya Ak47 na sikuwa na huruma naye zaidi ya kumtandika risasi moja ya kichwa.
 
    Sasa nikawa ninajiamini, sikuwa na haja ya kujibanza kwenye mti kwani risasi zote wanazo zipiga hakuna hata moja ambayo iliweza kuingia mwilini mwangu, ila risasi ninayo ipiga mimi inaingia pale nilipo kusudia, kama ni kichwani basi ni kichwani na kama ni kifuani basi inaingia kifuani. Ndani ya dakika tano nikawa nimewashusha majambazi ziaidi ya watano na wote wamepoteza maisha. Majambazi wengine walipo ona risasi zao hazifanyi kazi mwilini mwangu wote wakakimbia kueleka kwenye mgari yao, jambo ambalo sikulirhusu mapema. Nikafyatua risasi kwenye gari moja walilo panda, maiati yote yakapasuka na hawakuweza kwenda mbali na mimi. Nikazidi kuwaua hadi akabakia mmoja ambaye aliamua kujisalimisha yeye mwenyewe.
 
“Nani amewatuma?”
“K2 K2”
Nikamtoa nje ya gari kwa kumvuta, moja kwa moja tukaelekea kwenye gari lao jengine walio kuwa wamekuja nalo.
“Ukifanya ujinga ninakuu”
Nilizungumza hivyo huku nikimpapasa kuanzia chini hadi juu, sikumuona na silaha yoyote nikamuamrisha kukaa siti ya mbele na akatii ubishi wa ina yoyote. Nikaingia kwenye gari kwa bahati nzuri nikakuta fungua. Sikuzungumza kitu chochote zaidi ya kuwasha gari na kuondoka.
Moja kwa moja nikafika Ikulu nikiwa na jambazi huyu, sikuhitaji walinzi wanihoji nilicho kifanya ni kumpigia raisi simu na kumueleza nimefika nje ya geti la ikulu.
“Ngoja nipige simu wakufungulie”
“Sawa muheshimiwa”
Geti likafunguliwa na moja kwa moja nikaelekea kwenye maegesho, nikashuka nikiwa na bunduki yangu jambo lililo wafanya walinzi wote kuchomoa bastola zao na kunielekezea mimi.
 
“Weka silaha yako chini”
Mmoja wao alizungumza kwa ukali huku akinitazama usoni mwangu, nikatabasamu kidogo na silaha nikaiweka chini, nikafungua mlango wa gari na kumtoa jambazi huyu na kumtupia chini.
“Nahitaji kuzungumza na raisi”
Nilizungumza kwa sauti ya kike, kabla sijazungumza kitu chochote raisi na walinzi wake wengine akiwemo Babyanka wakatoka wakiwa anatazama tukio hili.
“Wekeni silaha zenu chini, binti ni kitu gani kinacho endelea”
“Heshima yako muheshimiwa, huyu ni miongoni mwa majambazi walio nivama. Tisa kati ya kumi nimewaua na huyu pekee ndio amejisalimisha na akakitu anacho hitaji kuweza kukizungumza mbele yako”
Niliendelea kuzungumza kwa sautii ya kike huku nikimtazama raisi usoni. Babyanka akabaki akiwa amenikodolea macho hakuamini kile ninacho kifanya kama mwamamke mwenzake isitoshe nimekiri kwamba sijapitia mafunzo yoyote ya kijeshi.
“Kijana zungumza”
Raisi ailizungumza kwa sauti ya kumbembeleza kijana huyu ambaye nimekuja naye.
 
“Muheshimiwa, tulitumwa kuja kum……….”
Kijana huyo hakumalizia sentensi yake tukashukia akianguka chini, huku damu zikimvuja kichwani. Kwa haraka walinzi wa raisi wakamzingira raisi na kumuweka kati huku wakiwa wamemuinamisha. Kazi yangu ikawa ni kutazama ni wapi mpigari risasi ametokea. Katika moja ya dirisha katika jengo hili la ikulu nikaona dirisha hilo likimaliziwa kufungwa.
Kwa vipimo vya haraka haraka vya macho nikagundua kwamba muuaji wa kijana huyu alikuwa katika dirisha hilo. Kwa haraka nikaanza kuingia ndani ya ikulu, baadhi ya walinzi wakanizuia kuingia ndani ila raisi ambaye yupo katikati ya walinzi wake akawaomba waniruhusu.
Tukaingia hadi sebleni, ila sikuhitaji kukaa kabisa kwenye kochi hizi. Nikatamani kuanzisha masako wa haraka kuhakisha ninamtambua muuaji.
“Muheshimiwa raisi, muuaji yupo ndani ya hii ikulu yako na maisha yako yanaonekena hayapo katika hali ya usalama”
Nilizungumza kwa sauti ya kike, jambo lililo mfanya raisi kukaa kimya pamoja na Babyanka amabaye muda wote ananitazama kwa macho ya umakini sana.
“Hakikisheni munampata muuaji na data za kamera zote zilizo rekodi tukio hili katika dakika chake nahitaji kuletewa hapa”
 
“Sawa muheshimiwa”
Walinzi wa raisi wakaondoka na kuanza msako ndani ya ikuku jambo ambalo sio kawaida, hata wafanyakazi wengien wakabaki kushangaa.
“Babyanka mpeleke mwenzio akabadilishe hizo nguo zake, na apewe nguo nzuri”
“Sawa muheshimiwa. Binti nifwate”
Nikaongozana na Banyanka hadi kwenye moja ya chumba, tukaingia woye wawili. Chumba hichi kina makabati yenye nguo nyingi sana za kike.
“Hadi sasa hivi siamini kama msichana ambaye hujapata mafunzo ya kijeshi au namna yoyote unaweza kufanya kama haya uliyo yafanya hii leo”
Babyanka alizungumza huku akichambua chambua nguo kwenye moja ya kabati akinitafutia nguo nzuri ya kuvaa.
“Inaweza kuwa ni kipaji”
“Eheee kipaji!! Umesha wahi kuona kipaji cha kutumia bunduki tena Ak47, hapo unatudanganya”
“Kwani kuna ulazima wa kujifunza?”
“Ndio maana kuna vitengo vya mafunzo. Isitoshe nimegundua kwamba wewe sio mwanamke, niulize kwa nini, au unabisha?”
 
Maneno ya Babyanka yakanifanya nimkodolee macho, akanisogelea akiwa ameshika gauni jeupe. Tukatazmaa macho kwa macho.
“Macho haya sio mangeni kwangu, unaweza kujibadisha kila kitu ila si macho yako haya Dany”
Kitendo cha Babyanka kuniita jina langu mwili mzima ukasisimka kwa woga.
“Ila sio mbaya kwa staili ambayo umeitumia, mimi hadi leo bado nakuamini kwamba wewe sio gaidi, ila kuna watu ndio wamekuchonga na kukufanya wewe uwe gaidi”
Sikuha na haja tena ya kubaki na wigi langu kichwani, nikalivua na kulishika mkono, Babyanka akafungua mlango akachungulia kwa nje kisha akaufunga kwa ndani.
“Ni kina nani ambao wamenipa kesi hii?”
“Hilo sio swali, watu hao unawajua fika na teas sasa hivi wameongezeka”
“Wameongezeka?”
“Ndio la kiongozi wao ni K2. Sasa hivi hii nchi haogozwi na raisi peke yake”
“lla?”
 
“K2 ndio mwenye kauli kuliko raisi, yeye ndio anapanga na kupangua, raisi yeye anafwata maelekezo tu. Hata hili swala la walinzi wasake muuaji ni mbwembwe tu, wewe ngoja utaoana”
Babyanka alizungumza huku akinipatia gauni jengine nijaribishe kuvaa.
 “Mmmmm sasa hapa inakuwaje?”
“Aahaa mimi natimiza majukumu yangu sitaki matatizo na mtu”
“Ila tunatakiwa kuhakikisha kwamba raisi anarudi kwenye mstar wake”
“Dany hilo swala ni gumu sana na ukumbuke hawa ni ndugu. Tumbo moja japo baba ni tofauti, kusema kwako ukweli leo Tanzama jinsi unavyo ishi maisha ya kutangatanga, tunajitolea maisha yetu kwa watu ambao hawahitaji sisi kujitoa”
Nikajaribu gauni alilo nipa Babyanka, likanikaa vizuri mwilini mwangu. Nikajiweka sawa huku Babyanka akinifunga zipu  kwa nyuma na kuniweka vizuri wigi langu.
“Ila kuwa makini K2 yupo hapa ikulu asije kuja kukustukia ikawa ni balaa”
 
“Usijali katika hilo, vipi sauti ninayo izungumza ipo vipi?”
“Ni sauti ya kike ambayo so rahisi mtu kukustukia kwamba wewe ni mwanaume”
“Ok”
Tukatoka katika chumba hichi na kurudi sebleni na kumkuta K2 akiwa amekaa na raisi wakizungumza mambo ya kifamilia. K2 alipo niona akanikata jicho kali, sikujali hilo zaidi ya kukaa katika sofa ambalo Babyanka alinikaribisha.
“Katherina huyu ndio yule binti aliye tegua yale mabomu uwanja wa taifa”
Kwa mara yangu ya kwanza maishani mwangu leo kufahamu kirefu cha jina la K2.
“Ahaa habari yako binti”
K2 alisimama na kuninyooshea mkono namimi nikasimama na kuupokea taratibu mkono wake huku nikiwa na tabasamu pana usoni mwangu ila moyoni mwangu, ninapata maumivu makali ya moyo wangu kunichemka kiasi kwamba ninatamani hata kuking’ofoa kichwa chake.
“Salama tu”
“Huyu binti kusema kweli nimependa sana, ni wasichana wachache sana ambao wanauwezo mkubwa kama alio kuwa nao yeye”
 
“Ahaaa sawa sawa kaka, hivi binti umepatia wapi mafunzo yako?”
Swali la K2 likanifanya nijisogeze taratibu kwenye sofa na kukaa vizuri huku nikimtazama usoni mwake.
“Sijajifunza sehemu yoyote nilikuwa ninapenda sana siku moja nije kuwa afisa upepelezi, hata nilipo waona wale jamaa nikajifanya afisa upelelezi na ndio nikafanikiwa kufanya kile nilicho kifanya”
“Ni vizuri, sasa kaka niachie huyu binti nimpeleke kwenye chuo cha mafunzo naamini atatufaa zaidi katika kulijenga taifa”
“Kweli, sasa wakati wa chakula umefika twende ukapate dinner”
Raisi alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa, sote tukanyanyuka na kwenda kwenye chumba maalumu cha familia nzima ya raisi kupata chakula. Raisi akanitambulisha kwa wanafamilia wake akiwemo mdogo wake aliye mpa siku majukumu kama raisi feki.
Tukaendelea kula chakula kwa pamoja, huku tukizungumza mambo ya hapa na pale, huku raisi akinihojia kuhusiana na maisha ya familia yangu. 
 
Kila kitu nilicho kizungumza ilinibidi kudanganya na nipo makini sana kwa kukumbuka kila jambo ambalo ninadanganya. Kwa mara kadhaa K2 akawa ananiangalia kwa macho ya kuiba iba akionekana kuchukizwa sana na uwepo wangu.
Chakula kikaisha, raisi akanikabidhi kwa Babyanka ili aweze kunirudisha kwenye hoteli niliyo fikia kwa maana muda umekwenda sana. Nikaagana na familia nzima ya raisi, akinikabidhi rasmi  kwa K2 na aliye ahidi kunisaidia kutimiza ndoto zangu kuwa afisa upelelezi.
“Mmmmmmmm”
Niliguna mara baada ya kuingia ndani ya gari na kufunga mlango wa gari. Babyanka akawasha gari taratibu tukaanza kutoka katika eneo la Ikulu.
“Lazima ugune, unahisi kuigiza mwanamke ni ishu ndogo”
“Yaa kweli sio ndogo, ila itakuwaje kama nikirudi tena chuoni katika muonekano wa kike?”
“Wewe ninacho kushauri endelea kula na vipofu, ipo siku watakuja kukubali”
 
“Kweli hilo ndio jambo la msingi”
“Ila kuwa makini sana K2 ni lazima aweke watu watakao kupeleleza, ana mtando mkubwa kuliko hata huyo kaka yake”
“Hapa ni mwendo wa kucheza nao, kama kweli hajaweza kunitambua katika muonekano huu unahisi anaweza kunitambua nikizidi kubadilika”
“Ahaaa kama nilivyo kuambia mimi kazi yangu ni kutimiza majukumu yangu tu”
Tukafika katika hoteli ambayo nimekodi chumba, sote tukashuka kwenye gari na kuelekea kwenye chumba changu. Kitendo cha kuufunga mlango kwa ndani, nikamshika makalio Babyanka, kitu kilicho mfanya kutulia kimya huku akijigeuza geuza.
“Nini bwana Dany, wewe si mwanamke jamani?”
“Mwanamke nani?”
Nilizungumza katika sauti yangu ya uhalisia, huku nikipandisha mikono yangu kwenye kifua chake na kuendelea kuzitomasa chuchu zake. Nikamgeuza na kuanza kumnyonya denda, taratibu Babyanka akaanza kuvua koti lake la suti, huku mimi nikiwa na kazi ya kumfungua vifungo vya shati lake jeupe alilo livaa. Tukiwa katika mahaba mazito gafla dirishani likaingizwa bomu la machozi lililo anza kutoa moshi mzito ulio tufanya tuanze kukohoa, hata hatujakaa vizuri taa za chumba chetu zikazima na kuanza kusikia vioo vikipasuka na kuanguka kwenye sakafu jambo lililo zidi kutuchanganya mimi na Babyanka
                                                                                  ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts