Home » , » Alikiba Awashauri Wasanii wa Zamani Kucheza na Nyakati, Muziki Umebadilika.

Alikiba Awashauri Wasanii wa Zamani Kucheza na Nyakati, Muziki Umebadilika.

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 11:07:00 AM

Msanii wa bongo fleva nchini, Alikiba  ametoa ushauri kwa wasanii wa zamani kuwa pamoja na kwamba muziki wao ulikuwa na changamoto nyingi sana enzi zao lakini wanatakiwa kukumbuka kuwa muziki umebadilika hivyo wanatakiwa kuyakubali hayo.

Alikiba anasema kuwa anajua kuwa wasanii wa zamani ndio walioufikisha muziki huu hapa lakini wanapaswa kujua kuwa kwa sasa muziki umebadilka sana hivyo ni lazima kukubaliana na hayo na endapo watabadilika pia itawasaidia kwa sababu muziki wa sasa una pesa sana kuliko ule wa zamani.

"Napenda changamoto wanazopitia wasanii wa zamani, kwa sasa  wanapaswa kujua kuwa muziki umebadilika sana .Ukiangalia wao wameutoa muziki mbali sana  kitu ambacho sisi tunashukuru kwa sababu tumeukuta na tunauendeleza.

"Sisi tunaona unatupatia faida kuliko wale wa zamani,zamani muziki ulikuwa hauna ela ila siku hizi muziki una pesa  japokuwa hata mimi nimeutoa mbali  hivyo hivyo.-Aliongea Alikiba alipokuwa akiongea na XXL ya Cloud Tv.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts