Home » , » Diamond Amuhaidi Mama Yake Kuoa Mwaka Huu.

Diamond Amuhaidi Mama Yake Kuoa Mwaka Huu.

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 10:48:00 AM

Mwanamuziki mkubwa Duniani Diamond Platinumz jana katika kusherekea  siku ya  wanawake Duniani amemtakia mama yake kheri ya siku hiyo na wanawake wengine wote Duniani huku akitoa ahadi kuwa mwaka huu kabla haujaisha atahakikisha kuwa anaoa mwanamke ambae hatomsumbua tena mama yake.

Diamond aliamua pia kutumia nafasi hiyo kumuomba mama yake msamaha kwa makwazo na magumu yote ambayo amekuwa akimpitisha  na kumdharirisha kuwa mambo mengi katika mitandao na kutukanwa kote anapokuwa anatukana.

"Happy women’s day kwa mama na wanawake wote ulimwenguni,nashukuru sana kwa kunizaa na kunilea ..wewe ni nguzo na mboni ya maisha yangu mama ..licha ya shida na mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea lakina hata sasa ambapo ulitakiwa walau kupumzika nimekuwa nikikukosa  kwa kukuingiza hata kwenye matatizo yasiyokuhusu..wanakutukana ,wanakukebehi, na kukutupia kila neno lililo baya  yote kwa sababu yangu mimi , lakini siku zote umekuwa ni mwenye kunisamehe , kunipenda na kunithamini ..nakupenda sana mama , nisamehe kwa yote niliyokukosea..inshalaah mwenyezi mungu anibariki mwaka huu mwanao nifanikishe ndoa yangu na kukuoa furaha ya milele ambayo siku zote umekuwa ukiitaka…@mama_dangote.

Ingawa maneno ya diamond yamekuwa kitendawili kwa sababu hajaweka wazi ni lini au nani anategemea kumuoa mwaka huu lakini hii imekuwa ni kama ameweka larm kwa watu mbalimbali hasa mashabiki  wake.

Tangu Diamond ameachana na zari amekuwa akionekana yupo karibu sana na diamond lakini pia anaonekana kuwa ameshamaliza tofauti zake na hamisa na kukubali kulea mtoto wao.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts