Home » , » Idris Sultan Adaiwa Kuwa Ndani Ya Penzi Jipyaa

Idris Sultan Adaiwa Kuwa Ndani Ya Penzi Jipyaa

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 11:22:00 AM

Mchekeshaji maarufu mtandaoni ambaye alijipatia umaarufu baada ya kushinda mashindano ya Big brother 2014, Idris Sultan amesemekana kuwa ndani ya penzi jipya na mtoto mkali balaa.

Idris ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Muigizaji maarufu wa Bongo movie Wema Sepetu aliwahi kukiri kuwa alikuwa hana mpenzi kwa muda mrefu yaani alikuwa single.

Habari za chini ya kapeti zilizopokelewa na gazeti la Ijumaa zimedai mrembo huyo anajulikana kwa jina la Aya ambaye ana asili ya Tunisia na inasemekana ni mrembo maarufu nchini humo.

Chanzo cha habari hizo kimeliambia gazeti la Ijumaa umbea huu ambapo kimezidi kufunguka;

"Nyie muulizeni tu Idris atawaambia sasa ana kifaa kipya kutoka nje ya nchi anaitwa Aya, Hivi karibuni alitua Bongo wakafanya matanuzi ya maana hadi kuna picha nyingine zilisambaa wakiwa kwenye swimming pool wakiogelea kimahaba”.

Baada ya kupata ubuyu huo gazeti la Ijumaa lilimsaka Idris ili kupata ukweli juu ya habari hiyo na Idris alifunguka:

"Aya ni kweli namfahamu ni mtu wangu wa karibu sanaa lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi. Tumekutanishwa na programu ya mstaafu Raisi Jakaya  Kikwete, na yeye alikuja Bongo kwa ajili ya kikao na project na kuhusu suala la kuogelea mimi sioni tatizo ijulikane tu ni mtu wangu wa karibu”.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts