Home » » Khadija Kopa Atoa Siri ya Kuwa Kijana Kila Siku.

Khadija Kopa Atoa Siri ya Kuwa Kijana Kila Siku.

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 10:08:00 AM

Mwanamama ambae anafanya vizuri katika muziki wa taarabu tangu enzi za nyuma mpaka sasa bado anafanya vizuri ,Khadija Kopa amefunguka na kutoa siri ya yeye kuendelea kuwa kijana kila siku na kuonekana mrembo kimuonekano.

Khadija anasema kuwa hajawahi kutumia vipodozi vyenye kemikali  katika maisha yake kwa sababu anaamini kuwa hiyo ndio inaharibu sana ngozi.

"siri ni kujitunza tu , mimi sipaki malotion wala sipaki majitu ya kujichubua na hata kama napaka lotion sio ile ya kuchubua ngozi yangu,sibadilishi ngozi yangu , ngozi inabaki vile vile tu.na pia ninamshukuru mungu ninapata ridhki ya kula maana ukiwa na njaa pia nozi iakunyaa.

"lakini pia mimi siitumii mwili wangu vibaya, mwanamke ukitumia mwili vibaya mara umemparamia huyu na mara huyu vilevile unazeeka na ile nuru ya afya yako inapotea pia.

"lakini pia matumiz ya masigara, mapombe, mirumbi,mashisha vilevile yanazeesha, unakuta unakunywa pombe makali vile unavyokunywa  unakunja uso yale makunyanzi yanafata uso wako mama, upoooeeh…… mimi sivuti sigara wala situmii pombe nakunwa maji na nikinywa sana ntakunywa soda.

Akiongelea muziki wake kwa sasa, Khadija kopa anasema kuwa tangu alipofiwa na mume wake alikuwa amekuwa mweupe kabisa kwa sababu alikuwa amekaa ndani muda mrefu na hakuwa na sehemu ya kuingiza kipato zaidi ya kutoa tu alkini anamalizia kukamilisha nyimbo yake mpa ambayo itaanza kufanya vizuri kwa sababu amepanga kutoa audio na video kabisa tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo alikuwa anatoa nyimbo bila kutoa video.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts