Home » , » Mr. Nice Amefungukia Tetesi Za Kuwa Muathirika Wa Ukimwi

Mr. Nice Amefungukia Tetesi Za Kuwa Muathirika Wa Ukimwi

Written By Bigie on Thursday, March 8, 2018 | 12:32:00 PM

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Mr. Nice aliyewahi kutamba kipindi cha nyuma na nyimbo zake kama Kikulacho na nyinginzo amefunguka na kuwatolea povu zito watu wote wanaosambaza habari kuwa yeye ni muathirika wa virusi vya Ukimwi.

Kwa kipindi kirefu Mr. Nice alikuwa kimya  kwenye gemu ya Bongo fleva na alipokuja kuibuka alizua maneno mengi hasa kwa sababu ya muonekano wake kubadilika na kukongoroka na kukonda mwili hali iliyopelekea taarifa kuenea kuwa ni muathirika wa virusi vya Ukimwi.

Mr. Nice amefunguka kuhusu tuhuma hizo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv anbapo amekataa kata kata tuhuma hizo:

"Kwanza wanaoninyoshea vidole kuwa nimeathirika wataathirika wao mimi niko sawa sawa kabisa tatizo ni kwamba watu hawajui maisha ninayoishi wamekuwa wangapi na ngoma lakini mimi bado nipo nadunda nachotaka kuwaambia ni kwamba tuhushimiane nimeenda kusemwa nimeathirika tangu 2002 sasa mpaka leo si ningekuwa nimekufa”.

Mr. Nice pia amefunguka na kusema anajua watu wanaomsema ameathirika pia wanamsaidia kuepuka kupigwa mizinga maana hata wanawake akikutana naye hawampigi mizinga kama zamani.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts