Home » , » “Naenda South Africa Kama Kazi, Hawezi Kunikataza Mtu”- Mama Diamond

“Naenda South Africa Kama Kazi, Hawezi Kunikataza Mtu”- Mama Diamond

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 11:30:00 AM

Mama mzazi wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra ametoa povu zito na kusema anaweza kwenda South Africa muda wowote akitaka kwenda kuwaona wajukuu zake na hawezi kukatazwa na mtu.

Mapema mwaka huu Zari the Bosslady alimpiga kibuti cha maana aliyekuwa mpenzi wake na  Baba watoto wake supastaa wa Bongo fleva Diamond siku ya Valentine’s baada ya kuchoshwa na tabia zake za kupenda michepuko.

Baada ya kuachana Diamond alienda South Africa kwa ajili ya maandalizi ya Albamu yake lakini cha ajabu ni kwamba hakufika kwenye nyumba aliyonunua aliyokuwa anaishi na Zari na watoto na Tena hakufika hata kwenda kuwaangalia watoto wake.

Baada ya sakata hilo kutokea habari zilianza kusikika kuwa Diamond na familia yake na mama yake mzazi hawatakaribishwa tena kwenye nyumba ya South Africa hasa kwa sababu wamejenga ukaribu na adui namba moja wa Zari, Wema Sepetu.

Siku ya jana Bi. Sandra alitoleana povu na shabiki baada ya kumuuliza kwanini hapendi kumposti mjukuu wake wa Hamisa au anamuogopa Zari kwa sababu hataruhusiwa tena kwenda South Africa kuwaona wajukuu wake? Basi bwana povu la Mama Diamond lilikuwa hivi:

"South Africa naenda kama kazi kwa taarifa yako na siwezi kukatazwa na mtu yoyote”.

Zari alishasema Kwenye Interview aliyofanya na BBC Swahili kuwa hana tatizo na familia ya Diamond kwani muda wowote wakitaka kuona watoto wao wanakaribishwa hata Diamond akitaka kuona wanaye.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts