Home » , » Papii Kocha Amefungukia Mapenzi Yake Kwa Mwanaye

Papii Kocha Amefungukia Mapenzi Yake Kwa Mwanaye

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 10:13:00 AM

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Papii Kocha aliyewahi kutamba miaka ya nyuma na wimbo wake wa ‘Seya’ amefunguka na kusema hakuna kitu kinachompa Faraja na ushujaa kama kumuangalia mtoto wake.

Papii Kocha alitumikia kifungo jela kwa takribani miaka minne na katika kipindi hiko chote alimuacha binti yake aliyemtaja kwa jina la Asha uraiani akiwa mdogo sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la ‘Amani’ Papii Kocha amekiri kuwa kwa kipindi chote alichokaa gerezani kwa miaka kumi na nne hakupata muda mzuri wa kukaa na mtoto wake huyo zaidi ya alivyokuwa akienda kumsalimia gerezani lakini kwa sasa ameona afanye kila analoweza ili mwanaye aweze angalau kufaidi matunda na furaha aliyoikosa kwa muda mrefu.

"Unajua sijakaa na mtoto wangu kwa Kipindi kirefu sasa na hivi sasa ndio anafaidi matunda kutoka kwa baba yake hivyo ni lazima nifanye kazi kwa jasho jingi ili ayafaidi matunda yangu”.

Lakini pia Papii Kocha amewasisitizia mashabiki zake kumiminika kwa wingi kwenye Show yao inayotarajiwa kufanyika tarehe 10 machi katika ukumbi wa King Solomon Hall.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts