Home » , » Ray Kigosi: Chuchu ni Mama Bora Kwa Mwanangu

Ray Kigosi: Chuchu ni Mama Bora Kwa Mwanangu

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 11:10:00 AM

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie, Ray Vincent Kigosi amefunguka na kumwagia misifa kibao mpenzi wake na mzazi mwenzake na msanii mwenzake wa Bongo movie Chuchu Hansy.

Ray na Chuchu wamezaa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaden ambaye ana umri wa mwaka mmoja. Miezi michache iliyopita Kwenye birthday ya jaden alizua gumzo mtandaoni huku kila mmoja akizungumzia uzuri wa mtoto.

Siku ya jana ikiwa ni siku ya wanawake duniani Ray amemwagia sifa kibao mzazi mwenzake Chuchu akidai ni mama bora kwa mtoto wao Jaden kwani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anakua katika mazingira bora kabisa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Ray amefunguka na hakusita kumwagia Baby mama wake masifa yote hayo akiamini anayastahili:

"Unajua angekuwa mwanamke mwingine angeona mtoto anamzibia vitu vingi hasa kwenye upande wa kuendelea kucheza filamu, lakini aliweka pembeni na lengo likawa moja tu nalo ni kumuangalia mtoto wetu tu”.

Lakini pia Ray alisema anajua ana jukumu la kumlea mtoto wake lakini anaamini anahitaji kumuombea sana mama watoto wake afya njema kwani yeye ndiye mlezi mkuu na ndiye atakayeweza kulishikilia jukumu hilo haswa.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts