Home » , » Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 09 na 10

Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 09 na 10

Written By Bigie on Tuesday, March 6, 2018 | 12:13:00 PM

Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
***ilipoishia***

Bi'chenda akabaki akiendelea kufanya usafi..
wakati anaendelea kusafisha kumbe zile irizi hakuziweka vizuri ndani ya mfuko wa dela alilokuwa amelivaa zikadondoka pasipo yeye kujua zikaanguka nyuma ya mtungi wa jiko la gesi..hivyo hakuweza kuziona
baada ya nusu saa kupita Bi'Chenda alimaliza kufanya usafi....akatoka na kuelekea chumbani kwake...wakati huohuo alionekana Rose akiingia ndani ya nyumba kutokea sokoni..akapitiliza moja kwa moja mpaka jikoni...akachukua sufuria pamoja na kisu ili akatekate nyama aliyoinunua buchani..ghafla kisu kikamponyika na kudondoka nyuma ya mtungi wa gesi...

***Endelea***
Kule chumbani alionekana Bi'chenda akivua dela alilokuwa amelivaa kisha akaungiza mkono kwenye mfuko wa dela hilo ili atoe zile irizi aziweke ndani ya mkoba wake wa kichawi....akastuka sana baada ya kukuta irizi hazipo...akafungua mlango haraka ili awahi jikoni kuchukua irizi zake......kutokana na kuchanganyikiwa alisahau kuvaa nguo alitoka chumbani hivyohivyo akiwa uchi wa mnyama....akili yake iliwaza kuwa Rose bado hajarudi kutoka sokoni....alipoingia jikoni Rose akapiga kelele kwa uwoga....hakutarajia kumuona mama mkwe wake akiwa uchi wa mnyama....

Bi'chenda akastuka kumkuta Rose amesharudi yumo jikoni....akajiziba nyeti zake kwa viganja vya mikono huku akitimua mbio kurudi chumbani kwake...... akafungua mlango haraka akaingia upande wa ndani...
kelele za Rose zilimfanya kulwa aamke usingizini akaanza kulia...ikabidi Rose aende kule chumbani kwake ili kumchukua kulwa...

wakati huohuo alionekana Bi'chenda akiwa chumbani mwake akachukua kitenge akajifunga haraka akatoka na kurudi kule jikoni....akaanza kutafuta irizi zake......ghafla Rose akaja huku amembeba kulwa...Bi'chenda akajifanya kuuliza,,"kuna kichupa kilikuwa na dawa yangu ya macho sikumbuki nimekiweka wapi ndio nakitafuta hapa...aliyasema maneno hayo huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa...,,Rose akasema,,''ngoja nikusaidie kutafuta...
 
Bi'chenda akadakia na kusema,,"hapana usijali mwanangu ngoja nitafute mwenyewe....
Rose akaandaa uji wa kulwa kisha akamuogesha..
wakati huo Bi'chenda alikuwa anajaribu kuvuta kumbukumbu ili akumbuke ni wapi atakuwa alizidondosha irizi zake.....uji ulipokuwa tayari Rose akauweka kwenye kikombe na kutoka jikoni akaelekea sebuleni....
Bi'Chenda alipo ona Rose kaondoka,,akaanza tena kutafuta irizi zake.....alitafuta bila mafanikio...akili zikamruka akahisi kuchanganyikiwa.....akatoka jikoni akajipitisha sebuleni huenda akaona irizi zake...lakini pia hakufanikiwa kuziona akaamua kwenda chumbani kwake......
Rose alistahajabu sana sio kawaida ya Bi'xhenda kuwa katika hali hiyo ya kuonekana kuwa na wasiwasi.....lakini Rose hakujali akaendelea kumnywesha uji mwanae.....

*******************
upande mwingine kule Gamboshi kijiji cha wachawi...palionekana kuwa ni eneo lililokuwa wazi kama kiwanja cha mpira....yani mchana haionekani nyumba hata moja.....wala watu wa kijiji hicho.....lakini inapofika usiku kinakuwa ni kijiji chenye makazi ya watu......
kwa binadamu wa kawaida hawezi kuona chochote badala yake ataona ni kama kiwanja kikubwa kilicho wazi.....kwa mbali walionekana watu wa nne wakipita eneo hilo la Kijiji cha wachawi.....kumbe mmoja kati ya watu hao wa nne,,alikuwa kafanyiwa zindiko la kimila.. hivyo alikuwa anauwezo wa kuwaona wachawi...walipokaribia eneo hilo alistahajabu kuwaona watu wengi.....

wakiwa uchi wa mnyama mchana kweupe huku wakiendelea na shughuli zao kama kawaida bila wasiwasi,,akaona nyumba nyingi zilizojengwa kwa miti na udongo zimeezekwa kwa majani makavu upande wa juu....akasita kutembea,,akasema,"jamani kumbe tumetokezea kwenye kijiji cha wachawi tazama kijiji kizima wapo uchi!!!!!
wale wenzake watatu wakatazama ule upande ambao mwenzao amenyoosha kidole...lakini hawakuona kitu chochote!!!waliona ni kiwanja kikubwa kilichokuwa wazi kama uwanja wa mpira..
mmoja akasema ""mbona mimi sioni kitu chochote!!!.hao watu waliouchi wako wapi?!
Yule mwenzao aliyefanyiwa zindiko akakumbuka kuwa...yeye pekee anauwezo wa kuwaona wachawi kwa sababu amefanyiwa zindiko...akaamua kusema,,"nilikuwa nafanya utani....wakaendelea na safari yao....

*************
upande mwingine alionekana Rose akinyanyuka kutoka kwenye kiti,baada ya kumaliza kumpa kulwa uji,,akazipiga hatua kurudisha kikombe jikoni kisha ampeleke kulwa chumbani ili akamlaze kwa sababu amesinzia tena.....akazipiga hatua kuelekea chumbani kwake akamlaza kulwa kisha akarudi jikoni ili aikatekate nyama aibandike jikoni haraka...akakumbuka kuwa kisu kilidondoka nyuma ya mtungi wa gesi...

akaukuta mtungi akapapasa papasa ili akichukue kisu...akastuka baada ya kugusa kitu kilichokuwa kikibonyea akaamua kuondoa mtungi na kuosogeza kando ili aone ni kitu gani...akastuka hofu ikamjaa baada ya kuona zile irizi mbili za Bi'chenda..akajisemea moyoni,,"nani kaweka hivi vitu vya kishirikina humu jikoni!!?akaamua kuchukua kijiko pamoja na mfuko wa plastiki akachukua zile irizi mbili na kuziweka ndani ya mfuko huo wa plastiki kisha akaamua kutoka na kuelekea chumbani kwake ili kuzificha....ili Seba akirudi amuonyeshe.....
wakati huohuo kule Gamboshi aliinekana doto kuanza kukoroma na kutoa mngurumo wa kutisha.

*************
upande mwingine alionekana Bi'chenda akiwa chumbani kwake.... ameketi kitandani huku ameshika tama akijaribu kukumbuka....ghafla akakumbuka kuwa huenda irizi zake zilidondoka nyuma ya mtungi wa gesi kule jikoni...akatoka haraka kuelekea jikoni akakuta mtungi wa jiko umesogezwa kando..haupo ile sehemu ulipokuwepo mwanzo....Bi'chenda akachanganyikiwa akajisemea moyoni,,''nimekwisha....na sijui nitamueleza nini mkuu wa wachawi na nitaendaje kule Gambushi bila irizi....ghafla Rose akaja...Bi'chenda akajiuliza ataanzaje kumuliza Rose kuhusu irizi zake.

 SEHEMU YA KUMI(10)

Akaamua kubaki kimya....baada ya masaa mawili kupita Seba alirudi nyumbani......Bi'chenda alipo ona Seba karudi...akawa na wasiwasi huenda Rose akamwambia kuhusu zile irizi.......akamuwahi Seba kabla hajaingia chumbani,,akamuita Sebuleni...Seba akaketi ili amsikilize mama yake labda kunajambo anataka kumwambia...lakini Bi'chenda akaanzisha maongezi kwa kuongea mfululizo.....Seba alicheka sana kutokana na stori za ucheshi wa mama yake...Bi'chenda aliongea mfululizo alihakikisha Rose hapati muda wa kumwambia kitu chochote Seba.......ilipofika majira ya saa mbili chakula kilikuwa tayari,,Rose akatenga chakula mezani....

Bi'chenda na Seba wakanyanyuka kutoka kwenye sofa walipokuwa wameketi,,wakazipiga hatua kuelekea kwenye meza ya chakula......Bi'chenda akaanzisha sara ya kukibariki chakula...kisha wakapakua chakula na kuanza kula......lakini Bi'chenda alikula huku akionekana kuwa na mawazo,,,,,hali hiyo ilimfanya Seba awe na wasiwasi akauliza,,"mama mbona hivyo!!!au haujakifurahia chakula???
 
Bi'chenda akaonesha tabasamu la usoni lakini moyoni alikuwa na chuki kubwa juu ya Rose..
akasema,,"Hapana mbona chakula kitamu..namuamini mkwe wangu huwa habaatishi mapishi.....baada ya dakika kadhaa kupita Seba alikuwa wa kwanza kumaliza kula akamshukuru Mungu kisha akanyanyuka akamtakia mama yake usiku mwema na kuelekea chumbani kwake....
Bi'chenda aliitikia kiunyonge alitamani Seba aendelee kuwepo sebuleni hapo..ili Rose asiweze kumwambia kuhusu zile irizi..lakini hakuna namna kwa vyovyote vile lazima Seba angeenda kulala na angeonana na Rose kwa sababu ni mkewe.....

*******************
baada ya dakika kadhaa kupita Rose pia, alimaliza kula chakula..akanyanyuka na kuanza kutoa vyombo kuvipeleka chumbani...lakini sahani ya bi chenda ilionekana bado inachakula kingi... Rose alikuwa anajua nini kinachomsumbua mama mkwe wake..lakini akajifanya kama hajui kinachoendelea....wakati Rose akiendelea kutoa vyombo,,Bi'chenda alikukuwa akimuangalia Rose kwa jicho la chuki ya hali ya juu.......

Rose alipohakikisha kuwa ameiacha meza ipo katika hali ya usafi..akamtakia usiku mwema mama mkwe wake..kisha akazipiga hatua kuelekea chumbani..........Bi'chenda alinyanyuka akazipiga hatua za kunyatia mpaka kwenye mlango wa chumba cha Seba na Rose....akatega sikio ikawa anasikiliza kwa makini kama Rose atamwambia Seba kuhusu zile irizi...

wakati huohuo alionekana Rose akijiandaa kwenda kuoga....wakati huo Seba alikuwa akimsogeza kulwa katikati ya kitanda ili yeye alale upande mwingine..ghafla kulwa akastuka usingizini.....Seba akasema,,''Mwanao kaamka
Rose akajibu akiwa bafuni,,"wewe ndio umemuamsha,,,sidhani kama atalala tena..ngoja nimalizie kuoga nije nimnyonyeshe...

wakati huohuo alionekana Bi'chenda akiendelea kusikiliza kwa umakini maongezi yao......Rose alipomaliza kuoga akajifuta maji na kuachukua kulwa akamnyonyesha...baada ya dakika kadhaa kulwa alisinzia tena...... Rose akamlaza kitandani akazipiga hatua kwenda kuzima taa alipoukaribia mlango akasikia vishindo vya mtu akikimbia kutoka mlangoni na kuelekea upande mwingine...Rose akastuka akasimama kwa sekunde kadhaa akazima taa..na kurudi kitandani...

***************

upande mwingine alionekana Bi'chenda akichungulia mlangoni kwake kutazama ule upande ulipokuwepo mlango wa chumba cha Seba....akatoka kwa kuzipiga hatua za kunyatia kuusogelea mlango huo....akasikiliza kwa makini ili ajue kinachoongelewa lakini aliona ukimya umetawala akajisemea moyoni,,"watakuwa wameshalala....sijui leo itakuwaje kule Gamboshi.
nisipokwenda nitapewa adhabu....Bi'chenda alikata tamaa ya kuzipata irizi zake usiku huo...akachukia sana akaamua kurudi chumbani kwake na kuutafuta usingizi.....

******************
ilipofika majira ya saa saba za usiku,,alionekana Bi'chenda akiamka akafungua begi lake na kutoa kaniki nyeusi akajifunga akachukua ungo wake wa kichawi uliokuwa chini ya uvungu wa kitanda akasimama juu ya ungo huo akajaribu kutoweka kimiujiza.....akashindwa..akajaribu tena kwa mara nyingine akashindwa...akaamua kuchukua ule mkoba wake wa kichawi akatoa jino la mnyama FISI akalishikilia kwa mkono wa kushoto akarudi kusimama juu ya ungo wake wa kichawi..alipojaribu akatoweka kimiujiza...akiwa angani,,kabla hajafika mbali..akadondoka kutoka angani mpaka chini..kwa sababu hakuwa na nguvu za kichawi za kutosha,,,kwa sababu irizi zinazomfanya awe na nguvu zaidi hajazivaa shingoni......

Bi'chenda aliteguka mguu baada ya kuanguka upande wa chini...akaogopa sana...akabeba ungo wake wa kichawi akatembe huku akachecheme kuifuata nyumba ya Seba ili aingie upande wa ndani..alipofika akajaribu kuingia kimiujiza.... akashindwa kwa sababu alipodondoka kutoka angani,,lile jino la mnyama FISI lilimponyoka kutoka mkononi likadondoka chini....wazo likamjia Bi'chenda akakumbuka kuwa hawezi kuinfia ndani ya nyumba kimiujiza bila kuwa na jino hilo la mnyama FISI....akaamua kuelekea ule upande alipokuwa amedondoka....

kutokana na giza kuwa totoro hakuweza kuliona jino hilo...alilitafuta kwa kupapasa papasa chini kwa muda wa masaa matatu mfululizo tangu saa saba mpaka saa kumi lakini hakufanikiwa kulipata....hofu ikaanza kumjaa..akawaza asipofanikiwa kuingia ndani...ataumbuka watu wakimkuta nje huku amejifunga kaniki na ungo wake wa kichawi..pia itakuwa aibu kwa mwanae Seba atakapogundua kuwa mama yake ni mchawi...jasho lilimtoka Bi'chenda..alihisi kuchanganyikiwa...dakika zilizidi kusonga sasa hivi ikatimia saa kumi na moja za alfajiri......Bi'chenda akaamua kuingia kwenye choo cha nje akajifungia humo.

************

asubuhi palipokucha alionekana Rose akifungua mlango na kutoka nje....kwa lengo la kwenda dukani dukani...kabla hajatoka nje ya geti akahisi haja ndogo imembana akazipiga hatua kuelekea kwenye chooni.......

ITAENDELEA.......

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts