Home » , » Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 11 na 12

Riwaya: SIKU YANGU- Sehemu ya 11 na 12

Written By Bigie on Wednesday, March 7, 2018 | 3:36:00 PM

Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
 ***ilipoishia***

hofu ikaanza kumjaa..akawaza asipofanikiwa kuingia ndani...ataumbuka watu wakimkuta nje huku amejifunga kaniki na ungo wake wa kichawi..pia itakuwa aibu kwa mwanae Seba atakapogundua kuwa mama yake ni mchawi...jasho lilimtoka Bi'chenda..alihisi kuchanganyikiwa...dakika zilizidi kusonga sasa hivi ikatimia saa kumi na moja za alfajiri......Bi'chenda akaamua kuingia kwenye choo cha nje akajifungia humo.

asubuhi palipokucha alionekana Rose akifungua mlango na kutoka nje....kwa lengo la kwenda dukani dukani...kabla hajatoka nje ya geti akahisi haja ndogo imembana akazipiga hatua kuelekea kwenye chooni....

***Endelea***
Alipoukaribia mlango....ghafla akasikia mtu anagonga hodi upande wa nje ya uzio...akaamua kuacha kuingia chooni akazipiga hatua kwenda kufungua geti ili aone ni nani anayegonga geti...alipofungua geti akafurahi sana kumuona rafiki yake kipenzi aitwae Tamala....wakasalimiana wakakumbatiana kwa furaha..akamkaribisha na kumuongoza mpaka ndani ya nyumba...

kule chooni alionekana Bi'chenda akiwa na wasiwasi na hofu kubwa..alipo ona ukimya umetawala akafungua mlango taratibu,,akachungulia upande wa nje..alipo ona hakuna mtu yeyote,akaamua kutoka haraka akazipiga hatua huku akichechemea....akazunguka pembeni ya nyumba,,kulikuwa na bustani ya mauwa...akajifanya anachuma matawi ya miche ya mauwa..akawa anayaweka kwenye ungo...kwa lengo la kudanganya kuwa ni dawa......alipomaliza akazunguka nyuma ya nyumba akaketi kwenye ngazi...ghafla mlango wa nyuma ukafunguliwa..kumbe alikuwa ni Rose anayefungua mlango huo..akastahajabu kumuona Bi'chenda ameketi nje!!!akajiuliza moyoni,,"inamaana Mama katoka ndani saa ngapi!!.mbona sijamuona akitoja nje,wakati mimi ndiye niliyefungua milango yote!!!
Rose akamsalimia Bi'chenda,,"Shikamoo Mama
Bi'chenda akajibu,,"marahaba umeamkaje?
 
Rose akajibu,,"salama,,sijui wewe umeamkaje??
Bi'chenda akadakia na kusema..leo nimeamka mgongo na miguu inaniuma sana hasa huu mkono wa kushoto....unaona haya matawi ni dawa...nayaandaa hapa kisha niyachemshe ninywe maji yake..nitajisikia nafuu...Rose alimtazama kwa mshangao akajisemea moyoni,,"mmh! hii ya leo kali matawi ya mauwa,, tena mauwa Rose kama jina langu..labda huenda nidawa..Rose akasema,,"pole mama,,kisha akarudi ndani....
Bi'chenda akanyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi akaingia ndani....akawasha jiko..akaweka yale matawi kwenye sufuria...akamimina maji na kuyabandika jikoni kama ushahidi ili Rose asigundue kitu chochote.....

********************
Baada ya lisaa limoja kupita Tamala alimuaga Rose akaondoka zake kurudi nyumbani kwake..

Kule chumbani alionekana Seba akijiandaa kwenda kazini....
Rose akaonekana akifunga geti..baada ya kutoka kumsindikiza Tamala....akazipiga hatua kuingia ndani ya nyumba,,akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani...akaamua kumueleza Seba kuhusu zile irizi alizozikuta jikoni,,nyuma ya mtungi wa gesi...akazitoa irizi hizo na kumuonesha Seba...
 
Seba alistuka sana.....akajisemea moyoni..."mmh! haiwezekani,Mama yangu sio mchawi...bila shaka Rose anatafuta sababu ili nimfukuze mama yangu..na kama huo ndio mpango wake basi amekwama....
Seba hakuongea kitu,alibaki kimya bila kujibu kitu chochote alichokuwa akiulizwa na Rose....
kitendo hicho cha Seba kutojibu maswali..kilimfanya Rose ahisi kuwa huenda hata Seba anajua yote anayoyafanya mama yake..au wanashirikiana kwa mambo ya kishirikina.....
Rose aliendelea kuhoji na kuuliza maswali....lakini bado Seba hakuongea kitu chochote.alibaki kimya.
 
Rose alichukia sana aliona kama Seba anamdharau..akazirusha zile irizi juu ya kabati..akafungua mlango na kutoka kwa hasira....
Seba alipomaliza kujianda akatoka nje akaingia ndani ya gari lake na kuondoka kuelekea kazini..
baada ya dakika kadhaa kulwa akaamka kutoka usingizini...akaanza kulia....Rose akaenda chumbani akamchukua kulwa na kwendanae sebuleni.....akamnyonyesha....akamuogesha na kumbadilisha nguo.....
 
Bi'chenda akasema,,mlete nimbebe,,wewe uendelee na shughuli nyingine..Rose akampeleka kulwa kwa bibi yake kisha akazipiga hatua kuelekea jikoni...akaandaa uji wa mtoto...kisha akaandaa chai...alipomaliza akakumbuka kuwa kunadawa ya Bi'chenda kwenye sufuria.....na sufuria hilo ndo kubwa kuliko masufuria yake yote huwa analitumia kuchemshia maji ya kunywa.....akaamua kumuuliza Bi'chenda,,"mama hii dawa yako niiweke wapi? nataka kutumia sufuria hili kuchemshia maji ya kunywa...Bi'chenda akasema,,"niwekee kwenye kikombe inatosha.....na hiyo iliyobaki imwage....
 
Bi'xhenda aliamua kusena hivyo kwa sababu alijua kabisa kuwa hiyo siyo dawa....bali ilikuwa ni janja yake ili Rose asimshtukie kuwa hakuwemo ndani ya nyumba usiku wa kuamkia leo.....na kwa sababu alijua ni matawi ya mauwa tu...hayana madhara hata akinywa hayo maji ya mauwa hayo.....

pasipokujua kumbe matawi ya mauwa hayo yakichemshwa yanatengeneza asidi....ambayo ikichanganyika na Oxygen inatangeneza Sumu hatari sana.....ambayo ukiiramba/kuila/au kuinywa.....ni hatari kwa uhai wako
Rose akamimina sawa hiyo ya uwongo wa Bi'chenda..akazipiga hatua kuelekea sebuleni na kumpa Bi'chenda kikombe hicho kilichokuwa na dawa hiyo ya uwongo wa Bi'chenda..... Bi'chenda akakipokea kikombe hicho......
Rose akasema,,"mmh!!!nyinyi wazee wazamani mnazijua sana dawa za asili....
Bi'chenda akacheka kisha akasema,,"yani dawa hii ni nzuri sana ukiinywa unajisikia nafuu muda huohuo.....aliyasema maneno hayo huku akikipeleka kikombe mdomoni.....

*********************
upande mwingine kule Gamboshi alionekana Doto akibadilikabadilika...kila siku zilivyozidi kwenda...Mkuu wa wachawi akaanza kupata wasiwasi.....akajiuliza kwa nini Bi'chenda siku ya jana hakuhudhuria kikao cha wachawi..na ilikuwa ni siku maalumu..ambayo alitakiwa yeye amtairi Doto na kile kipande cha ngozi kitakachokatwa..kichanganywe na dawa ya kichawi kisha kifungwe kwenye irizi ambayo itafungwa kiunoni mwa Doto mpaka atakapotimiza umri wa miaka kumi na moja(11)

*****************

upande mwingine alionekana Seba akiwa tayari amefika kazini..ghafla simu yake ikaita...

 SEHEMU YA KUMI NA MBILI(12)
 
Alipoipokea akasikia Rose akiongea huku analia!!mara simu ikakata...alipojaribu kuipiga,,ikawa haipatikani,,, Seba akastuka akahisi huenda na kulwa kafariki.. akanyanyuka kwenye kiti cha kuzunguka..kilichokuwa ndani ya ofisi yake..akakimbia akauparamia mlango..akaufungua na kutoka nje huku akitimua mbio...wafanyakazi wenzake walistuka kumuona Seba anakimbia...alafu kauacha mlango wake wa ofisi,,ukiwa wazi....Seba akatimua mbio mpaka kwenye geti la uzio wa kampuni aliyokuwa anafanyia kazi....hata mlinzi wa getini alishangaa kumuona Seba akitimua mbio na sio kawaida yake...
 
Seba alikimbia hatua kadhaa kutoka usawa wa geti..akakumbuka kuwa alikuja na gari lake...akarudi haraka akaingia ndani ya gari na kuliwasha....akaliondosha kwa kasi ya ajabu.nusu agonge nguzo iliyokuwa imesgikilia geti....
akaliendesha gari huku anapiga simu ya Rose..lakini ikawa bado haipatikani..Seba alizidi kuchanganyikiwa,aliramani aruke na kupaa kama ndege..aliona anachelewa kudika nyumbani....aliliendesha gari bila kufata sheria za barabarani..alipita upande ambao haruhusiwi kupita.....matrafki walimsimamisha kutokana na mwendo wa kasi aliokuwa akiliendesha gari lake,,lakini hakuthubutu kusimama aliwapita kama hawaoni vile!!!

******************
upande mwingine,kule nyumbani kwa Seba,alionekana Rose pamoja na majirani wachache...wakimbeba Bi'chenda na kumuingiza ndani ya gari...Bi'chenda alikuwa hoi,,alikuwa akitokwa na mapovu mdomoni...gari likawashwa wakamkimbiza hospitali..

*********************
upande mwingine alionekana Seba..akizidi kukanyaga mafuta na kuzioanga gia sanjari..alipofika Tazara,,alikuta kunamsongamano wa magari.(Trafk Jum/folen) akaxhukia sana..akapiga honi kwa mfululizo lakini hakuna aliyemjali..watu waliishia kumtazama na kumshangaa.,,walimuona kama mwendawazimu..anapiga honi wakati anaona taa za kuongoza magari barabarani hazijaruhusu..

Seba aliona kama anachelewa akaamua kufungua mlango wa gari..akatoja nje..na kuanza kutimua mbio..huku ameacha mlango wa gari ukiwa wazi..
ikasikika sauti ya mtu akiropoka, ikitokea ndani ya daladala ikisema,,"acha bangi wewe..
Seba aliendelea kutimua mbio nusu agongwe na magari,,,alivuka barabara bila kutazama kushoto kulia..
akaamua kukodi bodaboda...huku akisisitiza dereva amuwahishe haraka nyumbani...dereva bodaboda aliendesha,,aliendesha kwa kasi pikipiki yake huku Seba akisisitiza,,"NIWAHISHE..NIWAISHE!!!
 
baada ya dakika kumi Seba alifika nyumbani kwake..akagonga geti...kwa nguvu...huku akimuita Rose..alipo ona geti halifunguliwi akaamua kupanda ukuta..ili aruke upande wa ndani...ghafla ikasikika sauti ikimwambia,,"kakuna mtu humo ndani wamekwenda hospitali Mnazi mmoja.yule bibi,sijui ni mama yenu anatokwa na povu mdomoni..Seba akastuka akaacha kupanda juu ya ukuta..akageuza shingo yake haraka kumtazama yule mtu aliyeongea maneno hayo..kumbe ni jirani yake....yule aliyelimishwa kichawi shamba kule Gamboshi pasipo yeye kujijua..
Seba hakuongea neno lolote akapanda kwenye bodaboda...kisha akasema,,NIPELEKE MNAZI MMOJA.

*******************
kule hospitali alionekana Bi'chenda akishushwa kutoka ndani ya gari na kukimbizwa wodini...akatundikiwa dripu ya (solution)kwa ajili ya kupunguza makali ya sumu iliyokuwa inazunguka kwenye damu...kisha daktari akasema,,"tunaomba mtupishe kwa ajili ya mgojwa kupumzika.......
Rose pamoja na majirani watatu wakatoka nje ya wodi..... wakakaa kwenye viti vya maalumu kwa watu wanaowahudumia wagonjwa ambao ni ndugu,jamaa na marafiki.

**************
upande mwingine alionekana Seba akishuka kwenye bodaboda akaingia kwenye geti la Hospital...akatimua mbio kuelekea ndani kabisa ya hospital..akakutana na yule jirani miongoni mwa waliomleta Bi'chenda hospitalini hapo.. akamuongoza mpaka wodini...lakini hakuruhusiwa kuingia....
Rose alionekana akilia,,kama ilivyo kawaida kwa wanawake,,wakiona jambo kama hili.. walibaki hapo nje wakisubiri waruhusiwe kwenda kumuona mgonjwa.... baada ya lisaa limoja Bi'chenda alipata nafuu...daktari akaruhusu waingie kumuona...

Seba akataka kujua ni kipi hasa kilikuwa kinamsumbua mama yake...Daktari akasema,"inaonekana mgonjwa alipewa sumu..na mngemchelewesha kumleta ingekuwa ni habari nyingine sasa hivi...Seba akastuka akajisemea moyoni,,"huyu mwanamke kumbe ni mkatiri kiasi hiki!!! anataka kumuuwa mama yangu..sasa nimegundua ukweli,,na ndio maana leo ameanzisha visa kwa kuniambia kuwa mama yangu mchawi.....

Seba akamtazama Rose kwa macho ya hasira....akamsogelea Rose huku kakunja ngumi,,,alipomkaribia...........akasita kufanya alichotaka kukifanya...Rose hakuona kitendo hicho,,kwa sababu macho yake yalikuwa yakimtazama Bi'chenda kwa huzuni huku yakitoa machozi ya huruma....wakati huo kambeba kulwa mgongoni...Rose alikuwa anahisi njaa kali,kwa sababu hajala chakula tangu asubuhi..

***************
ilipofika mida ya saa kumi za jioni..hali ya Bi'chenda ikawa nzuri zaidi..Daktari aliamua kumruhusu Bi'chenda kurudi nyumbani...Seba akalilipia gharama zote za matibabu...wakatoka nje ya hospitali na kuingia katika gari la jirani..wakaianza safari ya kurudi nyumbani..
wakiwa njiani,,Seba alikuwa akifikiria kuwa wakifika nyumbani ampige Rose kisha amfukuze..
 
Rose hakulijua hilo..alikuwa kamkumbatia Bi'chenda begani huku akimwambia maneno ya kumfariji mama mkwe wake...
baada ya mwendo wa nusu saa hivi...wakafika nyumbani...jirani akalioaki gari nje ya geti la nyumba ya Seba..wakashuka kutoka ndani ya gari na kuingia ndani ya nyumba..kisha jirani akaondoka kuelekea nyumbani kwake....uso wa Seba ulionekana kuwa na hasira...akamuita Rose chumbani...ghafla kumbukumbu ikamjia kuwa ameliacha gari lake katikati ya barabara kule Tazara..Seba akafungua mlango akatoka nje haraka nusu akimbie..

ITAENDELEA.......

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts