Home » , » “Sasa Nataka Kuurudisha Mziki Wa Dansi Kwenye Chati”- Christian Bella

“Sasa Nataka Kuurudisha Mziki Wa Dansi Kwenye Chati”- Christian Bella

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 10:21:00 AM

Mwanamuziki mashughuli wa Dansi nchini Christian Bella ‘Obama’ ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kuurudisha muziki wa Dansi juu kwenye chati ulipokuwepo miaka ya nyuma.

Baada ya muda mrefu kuweka kwa malalamiko kutoka kwa mashabiki wakidai muziki wa Dansi umepotea, sasa Christian Bella ana mpango wa kuurudisha mziki huu juu kwa kuacha kufanya mziki wenye ladha ya Bongo fleva na kujikita kwenye Rhumba.

Siku za nyuma Bella aliwahi kulalamikia muziki wa Bongo fleva na kudai ndio uliopelekea kuua kabisa soko la muziki wa Dansi nchini kwani Bongo fleva imeonekana kuzoa mshabiki wengi zaidi na kupelekea kuua soko la mziki wa Dansi.

Christian Bella alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv:

"Mimi kijana wenu kijana wa kazi nataka kurudisha muziki wa bendi mashabiki walilalamika kuwa namix sana na Bongo fleva lakini sahivi nataka kuwarudishia muziki wa bendi, nimetoa wimbo mpya unaitwa ‘Rudi’ ili kurudisha mziki wa Rhumba”.

Christian Bella amehaidi kurudisha muziki wa Dansi kwenye zile Enzi ambazo walikuwa wanajaza shoo na mapedeshee kuwatunza stejini na kuwamwagia mahakama usiku Kocha.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts