Home » , » Shamsa: Mume Wangu Kanikataza Kujichanganya na Marafiki

Shamsa: Mume Wangu Kanikataza Kujichanganya na Marafiki

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 10:11:00 AM

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa imekuwa ngumu sasa yey kutoka na kujichanganya na marafiki kama zamani kwani mumewe Rashid ‘Chid Mapenzi’ kampiga stop.

Kama ilivyo kwa kazi yoyote ni muhimu kujichanganya ndivyo ilivyo kwa wasanii wa Bongo movie hupenda kufanya matukio mbali mbali pamoja lakini safari hii imekuwa tofauti kwa Shamsa kwani tangu ameolewa amepunguza kabisa ushirikiano na wasanii wenzake.

Shamsa amefunguka na kusema yeye kupunguza muingiliano kwenye shughuli mbali mbali ni maagizo kutoka kwa mume wake ambayo hawezi kupuuzia ambayo anaelekezwa na mumewe.

Shamsa amepiga stori na Motomoto News, na kudai mara ya kwanza alikuwa akijichanganya mno kwenye ishu tofauti lakini kwa sasa anashindwa kutokana na kupigwa marufuku na mumewe baada ya kuwa na ujauzito mchanga uliochoropoka kutokana na kuzurura:

"Mume wangu alinipiga marufuku kutoka toka licha ya kwa mbali mara ya kwanza nilikuwa natoka kibishi bishi tu lakini kwa sasa imebidi nimsikilize mume wangu zaidi maana mimba yangu changa ilitoka kwa sababu ya kutoka toka ovyo kwenda kwenye shughuli”.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts