Home » , » Skendo:Jini Kabula Adaiwa Kuiba Nguo

Skendo:Jini Kabula Adaiwa Kuiba Nguo

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 10:28:00 AM

Muigizaji wa Bongo movie Miriam Jolwa maarufu kama Jini Kabula aliyejizolea umaarufu miaka ya nyuma baada ya kuonekana kwenye mchezo wa Jumba la dhahabu, amekumbwa na skendo nyingine ya kuiba nguo kwa rafiki yake aliyempa hifadhi.

Habari zilizosambaa zimedai kuwa mwanadada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Candy alidai kuwa alimpa hifadhi Jini Kabula nyumbani kwake huko mkoani Mwanza lakini amedai  kamuibia nguo mpya za thamani na kisha kuondoka na kutimkia nchini Oman.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Soudy Brown Kupitia kipindi cha XXL, Candy amedai kuwa ameshangazwa na kitendo hiko kwani alimfanyia we na kumkaribisha kwake lakini amedai tangu ameandoka amemblock Kwenye WhatsApp na Instagram akijua wazi ameiba.

Baada ya tuhuma hizo Jini Kabula aliulizwa na kutokea nchini Oman alifunguka yafuatayo:

"Kwanza simjui huyo Candy alafu kama anatafuta kiki aseme halafu isitoshe mimi nimeshazoea hayo mambo kwaiyo hayaniumizi kichwa  na sahivi nimeshachoka na habari za watanzania  ngoja nile bata alafu kama hamjui huyo Candy mshamba anavaa malonya malonya kwaiyo siwezi kumuibia kitu kila mtu apambane na hali yake”.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts