Home » , » Snura Apanga Kuwa Mwalimu wa Kwaya Mashuleni.

Snura Apanga Kuwa Mwalimu wa Kwaya Mashuleni.

Written By Bigie on Friday, March 9, 2018 | 10:24:00 AM

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini snura mushi amefunga na kusema kuwa kwa sasa hana anachowaza kuhusu sanaa zaidi ya kujiajiri mwenyewe kwa sababu anaona kuwa kazi ya kufanya muziki imekuwa ina makwazo ambayo hayatatuliki.

Snura anasema kuwa kwa sasa anafikiria tu kufanya kazi ya kujiajiri ambapo amepanga kwenda  kufundisha kwaya mashuleni na kusema kuwa anawashangaa sana BASATA  kwa kuufungia wimbo wake wa chura kwa sababu walishaakaa chini  wakauzungumzia wimbo huo na kuweza kufanya baadhi ya marekebisho na kuruhusu kupigwa kwa sababu alitoa baadhi ya vipande ambavyo vilikuwa vinatakiwa kutolewa.

"kwa sasa najifikia kujiakiri mwenyewe zaidi na zaidi ndio maana najipanga niwe tu mwalimu wa kwaya shuleni kwa kuwa muziki wetu umekuwa mgumu sana kwa sababu mtu unafungiwa wimbo wako hata  kosa halijulikani.

"wakati mwingine unawapelekea kazi kabisa wanaikagua lakini wanakuja kukugeuka baaadae kama ilivyokuwa kwangu huu wimbo wa chura niliubadilisha na wakaukagua kabisa  na wakaniruhusu niwaite waandishi  wa habari na kuwaambia mabdiliko hayo na ukaanza kupigwa kwenye vyombo vya habari lakini sasa hivi  nimefungiwa tena sijui hata kosa ni nini..

Snura ni mmoja wa wasanii ambao wamekumbwa na adhabu ya kufungiwa nyimbo zake baaada ya kuonekana kuwa nyimbo zake mbili zilikuwa hazina maadili na zinakiuka taratibu za maadili ya Tanzania.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts