Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini ( 40 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini ( 40 )

Written By Bigie on Sunday, March 25, 2018 | 1:24:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Nikakimbilia ndani na kwenda moja kwa moja nikaingia chumba alipo mtoto,Sikuyaamini macho yangu kwani nilimkuta amekuwa mkubwa na kufikia ukubwa babu mtu mzima mwenye mandevu mengi na anatisha kupita maelezo,akanitazama kwa jicho lake kililo kubwa kama gololi za kuchezea pooltable
“NATAKA DAMU YAKO”

ENDELEA
Nikabaki nikiwa nimesimama kama ninasubiri kupapigwa picha ya mnato,kukimbia ninataka ila miguu inashindwa,Nikajikuta nikitabasamu kama mtu aliye pumua kwa njia ya haja kubwa mbele ya mama mkwe.Likasimama na kuanza kunifwata kwa mendo wa taratibu kuja sehemu nilipo.Nikataka kurudi nyuma ila nikijikuta miguu inazidi kuwa mizito na kubaki nikiwa nimesimama kama mlingoti.Likanisogelea na kuushika mkono wangu wa kulia,akautazama sehemu ya giganja na gafla sehemu ya juu ya kiganja,akaing’ata na kuanza kuinyonya damu.

Kitu kilicho nishangaza,sikuweza kupata maumivu ya aina yoyote japo ninaona damu zinanichuruzika pembeni.Kitu kilicho zidi kunishangaza,kila jinsi anavyozidi kunyonya damu yangu ndivyo jinsi anavyo badilika.kutoka katika uzee kurudi kwenye ukijana zaidi.Akaniachia mkono wangu na kuwa kijana mdogo kama wa umri wa miaka kumi na mbili huku akifanana na mimi kila kitu ambacho mimi ninacho,kuanzia sura
“Nikinyonya zaidi,damu yako nitarudi kuwa mtoto”
Alizungumza na kuzidi kunishangaza.Akanitazama kwa macho makali kisha akarudi na kukaa kitandani,akachukua shuka na kujifunga
“Baba njoo ukae hapa”
Alinionyesha sehemu ya kukaa,pembeni ya kitanda,taratibu nikajizoa zoa hadi kitandani na kukaa pembeni yake.Ukimya wa dakika kadhaa ukakatiza wakati wote nikiwa nikimtazama jinsi alivyo
 
“Baba,ninaamini kuwa mutakuwa munaniona kuwa mimi ni kiumbe cha ajabu sana kutokea kwenye maisha yanu”
“Hapaana,mwanangu”
Nilijikaza tuu kusema hiyo mwanangu ila kiukweli,sina imani naye kabisa huyu mtoto ambaye kwa sasa ninafanana naye na wala siwezi kupinga kitu cha aina yoyote.
“Baba mimi ni binadamu ila pia ni shetani”
Nikastuska kidogo,japo nimepewa mamlaka yakuwaongoaza viumbe wa aina hii,ila kwa hapa mapigo ya moyo yakapoteza kabisa muelekeo wake
“Usistuke,baba.Kwa jina munaweza kuniita Lusifah”
Kwa mara ya kwanza maishani mwangu kuona mtoto anajichagulia jina la kujiita tena jina lenyewe ni lakishetani.
“Kwa nini nikuite hivyo?”
“Ndilo jina ambalo mimi nimepewa kabla ya kuzaliwa”
“Kabla ya kuzaliwa kivipi?”
 
“Kipindi nilipokuwa tumboni mwa mama yangu wa kwanza,sikuweza kuelewa kitu chochote ila baada ya kupelekwa tumboni mwa mama yangu wa pili hapo ndipo nilipo anza kusikia kila kitu ambacho kinaendelea duniani”
Nikashusha pumzi nyingi,Kigugumizi cha gafla kikatawala kooni mwangu.Hata nilicho hitaji kumuuliza kikayayuka kichwani nikabaki nikiwa ninamtizama
“Naomba ukamuite mama”
“Mama?”
“Ndio mama yangu,Si Rahma”
Nikanyanyuka,kitendo cha kufungua mlango nikamkuta Rahma akiwa amesimama mlangoni akiwa analia.NikamtizamaLusifah kitandani kisha nikamtazama Rahma ambaye hakutaka hata kunitazama usoni
“Unaitwa huko ndani”
“Eddy,siwezi kuwa na toto kama hilo jibabu”
“Shiiii taratibu,atakusikia”
“Na anisikie,Eddy kumbe umenidanganya kuwa mtoto umemuokota ila kumbe ni lijibabu”
“Mama mimi sio babu”
 
Sote tulistushwa baada ya kumuona mtoto akiwa amesimama pembeni ya Rahma.Lusifah akamshika mkono Rahma na hapo ndipo nilipo muona Rahma akitetemeka mwili mzima hadi haja ndogo ikaanza kumtoka
“Baba na mama,nimekuja kuwaokoa kwa maana munapo elekea nyinyi ni kwenye vita ambayo nyinyi kama nyinyi hamuta weza kuimudu”
Rahma akazidi kutetemeka,kunishika akawa anatamani ila kimbebe mkono wake wakulia umeshikwa na Lusifah.
“Mama usiniogope,mimi ndio mwanao uiye niweka tumboni kwa kipindi kifupi kabla sijatolewa na kwenda kulelewa kuzimu na shetani”
Kilio cha Rahma kikazidi kusikika kwani mara ya kwanza alikuwa akilia kimya kimya.
“Leo tumepatikana”
Nilijisemea kimoyo moyo,huku nikimuonea huruma Rahma wangu
 
“Baba wala hamjapatikana,ni woga wenu tuu.Ila mutanizoea”
Akaanza kutembea na Rahma kuingia naye ndani na kukaa naye kitandani.Kwa ishara akaniita nikae na mimi kitandani.Akaishika mikono yetu na kuikutanisha kwa pamoja
“Ninafuraha sana kuwa na nyinyi kwa wakati huu”
Alizungumza huku akiwa ameyafumba macho yake na sura yake akiwa ameigeuzia juu.
“Unalia nini na wewe?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini sana huku tukitazamana na Rahma.
“Mama,kwa nini unanikana kuwa mimi sio mwanao?”
“Hapana”
Rahma alijibu huku mwili wake ukiendelea kumtetemeka hadi nikamuonea huruma,
“Nawapenda sana wazazi wangu”
“Hata mimi pia”
Nilijibu mimi mwenyewe pasipo Rahma kuzungumza chochote.Lusifah akatuomba tutok nje apumzike kwani tayari gizi lilisha tawala anga.Moja kwa moja Rahma akakimbilia chumbani kwetu,nikamfwata na kumkuta akipanga nguo zake kwenye kijiegi kidogo
“Unakwenda wapi?”
 
“Eddy mimi ninaondoka”
“Tatizo ni nini linalokufanya uondoke?”
“Eddy unadhani,hayo mambo niyakawaida?”
“Ila mke wangu,yule ni mtoto wetu?”
“Eddy mtoto gani,si alikuwa ni jizee la miaka hata tisini,sasa hivi unaliita mtoto”
Rahma alizungumza kwa sauti ya kufoka
“Sawa,basi kama ni kuondoka subiri hata kupambazuke ndio uondoke ila si huu usiku”
“Eddy,siwezi kulala tena hapa.Waala kuendelea kuishi hapa”
“Sasa mpenzi wangu......”
“Eddy hakuna cha sasa.Ninakupa uchague,Kati yangu na hao mapepo yako?”
Nikashusha pumzi na kupiga hatua za taratibu hadi sehemu ambayo Rahma yupo.Nikamkumbatia kwa nyuma taratibu
“Mke wangu,unanipenda?”
Nilizungumza kwa sauti nzuri na nzinto kiasi iliyo jaa mahaba
“Hata kama Eddy,hilo sio swali la kuniuliza mimi?”
“Hapana,nijibu”
“Ndio,ninakupenda”
“Mimi ni nani yako?”
“Mume wangu”
“Una nisikiliza”
 
“Ndio,ila kwa hilo jitoto lako mimi sinto kusikiliza ng’oo”
Nikaipandisha mikono yangu hadi kifuani mwa Rahma na kuanza kuyashika maziwa yeke,ila akaitoa mikono yangu kwa nguvu.
“Eddy niache,sipo kwenye masihara”
Rahma akafunga zipu ya kibegi cheka,akafungua droo na kuchukua funguo za gari la mzee Ngoda alilo kuja nalo siku ambayo alitafunwa na majini.Akatoka nje huku akiwa katika mwendo wa haraka.Sote tukafika sehemu yenye gari,kabla hajaingia ndani ya gari akanigeukia
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho,UNANIPENDA MIMI AU HAO MAPEPO WAKO?”
“Ninakupenda wewe”
“Ingia kwenye gari”
“Ngoja kwanza”
Nikataka kuondoka ila Rahma akanishika mkono
“Ingia kwenye gari”
Nikaingia ndani ya gari,kila Rahma anavyojaribu kuliwasha gari likakataa kuwaka.Akajaribu kila mbinu anayo ijua yeye ila gari linawaka kidogo na kuzima
 
“Shuka basi usukume”
Nikashuka,nikaanza kusukuma.Ila gafla nikastuka kumuona Lusifah akiwa pembeni yangu akinisaidia kusukuma,Nikataka kuzungumza akakiweka kidole chake mkononi akinizuia nisizungumze chochote.Gari ikawaka,Lusifah akakunja ngumi mkono wake wa kulia akiniomba tuigonganishe mikono yetu,watu wengi wamezoea kusema nikampa Tano.Akaniomba niingie ndani ya gari
“Wewe nenda,nitawaangalia hawa wengieni”
Nikaingia ndani ya gari na kujifunga mkanda.Safari ikaanza huku njia nzima kila mtu akiwa kimya,Rahma akazidi kuongeza mwendo wa gari,japo ni usiku sana anajua jinsi ya kuyakwepa mashimo na madogo madogo yaliyopo barabarani.Tukafika barabara ya horohoro  na kuendelea na safari yetu.Hadi tunaingia Tanga mjini muda ilisha timu saa tisa usiku.Jiji zima lipo kimya kila sehemu ambayo tunapia.Hata zile heka heka za watu wanao lala nje kwenye vibaraza vya watu hatukuweza kuwaona.
“Tunakwenda kwangu au wapi?”
“Tunakwenda kwetu”
 
“Kwenu kufanya nini?”
“Kule ni kwetu na nikwa wazazi wangu”
“Hembu simamisha gari kwanza”
Rahma akasimamisha gari pembeni na kulizima.
“Rahma,kumbuka kwenu tuliondoka vipi.Iweje leo unataka twende?”
“Eddy nisikilize kwa umakini.Nilikuvumilia kwa kipindi kirefu.Sasa nimechoka tena nimechoka”
“Umechoka na nini?”
“Eddy,huna mapenzi ya dhati na mimi “
“Haaaa hayo yote yametokea wapi tena?”
“Eddy,sikupendi na sikuhitaji tena katika maisha yangu.Niliona nikuzungumza hivi kule porini utanifanya chochote utakacho.Ila nipo nyumbani sasa,Sitaki unitafuta wala unisumbue kwa chochote”
Maneno ya Rahma yakanifanya niishiwe nguvu kabisa.Na jinsi Rahma anavyo zungumza anaonekana hana masihara kabisa na kitu anacho kizungumza
“Wewe si mtu wa kutembea na Halida,wale walimu wezako machangudo.Nashukuru kwa kunileta ninacho kuomba ushuke ndani ya gari”
“Lakini Rahma ni nani aliye kuambia haypo mambo?”
“Ahaaa ulizani dunia ina siri.Kamuulize yule bibi yako uliye niacha naye nje pale”
 
“Ndio amekuambia haya maneno?”
“Jibu,swali.....”
“Shuka,ndani ya gari”
Rahma alizungumza huu akinisukuma sukuma nishuke kwenye gari.Hasira zikaanza kunipanda juu ya bibi aliye nitibu.Nikashuka ndani ya gari na Rahma akawasha gari na kuondoka kwa kasi.Maumivu makali yakakatiza kwenye moyo wangu,kwani kila kitu kinacho tokea kwenye maisha yangu ninaona kama ni ndoto.Sikujua ni kitu gani kilicho mpata Rahma.Sikuwa na jinsi zaidsi ya kwenda nyumbani kwangu.Nikiwa maeneo ya Mkwakwani gafla nikaanza kuhisi upeppo mkali ukija kwa kiasi mbele yangu.Radi nyingi zikaanza kutawala kwenye anga huku mawingu mazito ya mvua yakikusanyika kwa kasi.Ndani ya dakika kadhaa mvua kubwa iliyoongozana na radi kali ikaanza kunyesha.Nikatafuta sehemu ya kujibanza pembezeni ya ukuta ili kuacha mvua ipite
Nikiwa nimeuegemea ukuta niskastukia nikikabwa shingo kwa nguvu na mkono ulio tokeza kwenye ukuta nilio uegeme huku mkono huo ukiwa na kucha ndevu za kutisha
 
 ITAENDELEA
Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts