Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Mbili ( 42 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Mbili ( 42 )

Written By Bigie on Tuesday, March 27, 2018 | 5:19:00 PM

 AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Akanipiga kofi jengine huku akiniporomoshea matusi mengi,akaendelea kufanya anacho kifanya akaanza kuufungua mkanda wa suruali yangu,kabla hajamaliza nikstukia kuona jitu jengine kubwa na lakutisha,lenye mabawa likisimama mbele ya gari letu na kusababisha kishindo kikubwa hadi gari ikatingishika
 
ENDELEA
Rahma akaniacha na nikamsukumia kwenye siti yake na tukabaki tukiwa tumetazamana na jitu hili ambalo linatisha kupita maelezo.Rahma kwa haraka akawasha gari na kuaanza kuirudisha nyuma kwa mwendo wa kasi,Cha kushangaza jitu hili halikuwa na habari na sisi zaidi ya kubaki likitutuzama.
 
“Tunaelekea wapi?” Nilimuuliza Rahma
“Hata mimi sijui”
“Twende kwenu”
“Kwetu!!?”
“Ndio kuna kazi nataka kwenda kuifanya”
“Kazi gani?”
“Wewe twende,utaiona huko huko”
Tulizungumza huku Rahma akiendelea kuongeza mwendo wa gari,Tukafika nyumbani kwao na kukuta geti likiwa wazi,Tukashuka ndani ya gari na kujibanza pembezoni mwa geti huku tulichungulia ndani kuangalia kama kuna hali yoyote ya watu kuwemo.Giza zito lililopo kwenye jumba la kina Rahma ikazidi kutopa hofo,Nikatangulia mbele huku Rahma akinifwata nyuma.Tukaingia ndani sote tukiwa makini,Hali ya kuzizima ndani ya nyumba ya kina Rahma ikatufanya tushindwe hata kuwasha taa,mwanga hafifu wa mbalamwezi unao pita kwenye madirisha makubwa ya kioo,unatusaidi kuona vitu vilivyomo ndani ya sable.
 
“Kipo wapi chumba cha kuhifadhia vitabu?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini ya kumnong’oneza Rahma ambaya alinitazama kwa mshangao
“Eddy,umejuaje kwetu kuna chumba cha kuhifadhia vitabu?”
“Rahma hilo sio jibu ninalo litaka mimi.Wewe niambie ni wapi kilipo”
“Twende”
Tukapandisha ngazi za gorofani taratibu huku sote tukiwa makini sana.Tukaingia kwenye moja ya chumba kimoja na kukuta vitabu vingi vikiwa vimepangwa kwenye mbao zilizo pangiliwa vizuri ukutani,Nikabaki nikiwa nimeshika kiuno kwani sikujua ni wapi nianzie hii ni kutokana na wingi wa vitabu uliopo katika chumba hichi kikubwa
 
“Baby kwani unatafuta kitabu gani?”
“Kuna kitabu ambacho kinaelezea kuhusiana na majini”
“Kinaitwaje?”
“Hata mimi sijui”
“Sasa utatafutaje kitu usicho kijua?”
“Washa taa kwanza”
Rahma akawasha taa,tukaanza kushirikiana kutafuta kitabu kimoja baada ya kingine.Huku tukiwa tunatazama jina la kitabu na picha kama vinaendana na elimu ya majini.Zaidi ya nusu saa tukawa na kazi ya kutafuta ila hatukufanikiwa kukipata kitabu
“Eddy nimechoka ngoja nikanywe maji”
“Powa”
Raham akaondoka na mimi niakendelea kutafuta kitabu ambacho baba Rahma aliniagiza,Nikiwa ninaendelea endelea kutafuta kitabu nikastuka na kuhisi kuna kitu kinakatiza nyuma yangu,Nikageuka haraka na kukuta hakuna kitu
 
“Rahma”
Niliita ila sikusikia muitikio wa Rahma,kwa mbali wasiwasi ukaanza kuniajaa,Nikaendelea kuchukua kitabu kimoja baada ya kingine,gafla taa ikazima.Nikazidi kustuka nikageuka nyuma na kutazama kama kuna kitu ambacho kimeizima taa ila sikuona chochote.Haikuwa ni umeme kukatika kwani nyumba ya jirani inawaka taa.Nikapiga hatua za haraka hadi ilipo swichi na kuiwasha.Nikarudi kwenye msururu wa vitabu na kuendelea kutafut,na safari hii nikaongeza kasi ya kutafuta.Nikastukai vitabu kama sita vikianguka kutoka juu ya kabati lililopo eneo hili.Nikastuka ila baada ya kuoni ni panya ndio amevigusa vitabu hilivyo anguka kidogo nafsi yangu ikatulia
 
Nikavitazama vitabu vilivyo anguka na kukiokota kimoja kati ya sita vilivyo anguka,nikakutana na picha ya majitu yanato tisha huku juu yake kukiwa na maandishi makubwa yaliyo andikwa
“EVIL SPIRIT”(Nafisi ya kishetani)
Nikakifuta vumbi na kufungua kurasa ya kwanza,kitu kilicho nichanganya ni kukuta maandishi yakiwa yameandikwa katika luhga ya kifaransa japo jina limeandikwa kwa kingereza
“Umekipata”
Sauti ya Rahma ikanistua na kunifanya nimtazame kwa woga
“Ndio nimekipata,ila kimendikwa kwa lugha ya kifaransa”
“Unaijua kuisoma?”
“Hapana”
“Hembu nione”
Nikampa Rahma kitabu na akakitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kukisoma taratibu na kunitafsiria taratibu
 
“Dunia itabadilika na kutawaliwa na nguvu za shetani.Ambazo zitawateka watu wengi na kuwaweka katika sehemu moja.Utawala huu utaanzia katika bara la Afrika upande wa mashariki,utaendelea kusambaa kwa kasi kuelekea upande wa magharibi mwa dunia”
Rahma akameza mate kidogo na kuendelea kukisoma kitabu
“Watu watagawanyishwa miili yao kwa kunyofolewa baadhi ya nyama katika miili yao na mashetani yanayoitwa LUSIFA”
Moyo ukapoteza hata muelekeo baada ya kusikia jina la mwanangu ambaye wala simuelewi elewi
“He...hee mbu rudia hapo”
“Wapi?”
“Yanaitwaje?”
“Lusifa”
“Endelea”
“Halii hiyo itaendela kuwaangamiza wanadamu wote watakao kutana na majini hao wabaya.”
“Hembu nenda nenda mbele,Hakuna sehemu iliyo andikwa jinsi ya kuwazuia”
“Acha kihere here mtoto wa kiume kama ungekuwa unaweza kukisoma kifaransa ungekuja kukisoma”
 
“Haya mama”
“Hali hii inaweza kuondoka pale tu,mtu mwenye nyota kubwa na yenye nguvu na mamlaka kupita nyingine atakapo weza kufanya mambo makuu maane”
“Eheee” Nilizungumza huku nikishusha pumzi nyingi
“Kwanza awe ni jasiri katika kupambana na kila hali”
“Pili awe na msimama juu ya jambo analo liamua”
“Tatu aweze kutoa kiasi cha damu yake na kwenda kuimwaga katika bahari”
“Nne awe tayari kuyapoteza maisha yake kwa ajili ya wengine.Kwani nilazima afe”
Sikuwa na usemi zaidi ya kuguna tu,Rahma akaendelea kuzungumza
“Endapo hayo yote yataweza kufanikiwa kwa wakati mmoja basi watu wote ambao walipotezwa au kuuawa na majini hao wataweza kurudi katika hali ya kawaida.Pia na dunia itarudi katika hali yake ya kawaida”
Nikajikuta nikiikutanisha mikono yangu juu ya kichwa changu huku nikiwa nimemtazama Rahma kwa mshangao hata anacho endelea kukisoma sikuweza kukisikia kabisa zaidi ya neno la ‘LAZAMA AFE’ likiwa linajirudia rudia kichwani mwangu
“Eddy hivi unanisikiliza au ninajisomea mimi mwenywe?”
“Ehee”
 
“Nakuona haunisikilizi,nitaacha?”
“Endelea endele kusoma”
“Vita hiyo ni ya mtu mmoja tu,hapaswi kusaidiwa na mtu wa aina yoyote la sivyo akipata msaada wa aina yoyote.Hali hii itazi kuwa kubwa na dunia nzima itakuwa chini ya utawala wa Lusifa”
“Mpambanaji anatakiwa,kuwa na mishale kumi na mbili.Kila mshale atautumia katika kuangamiza kichwa kimoja cha joka kubwa litakalo watanguliza wasaidizi wake ambao watauliwa kwa kutumia maneno haya”
“Bwana Eddy haya maneni sijui yameandikwa kwa kilugha gani?”
Rahma akanisogelea na kunionyesha maneno ambayo tangu nizaliwe ndio mara yangu ya kwanza kuyaona katika macho yangu
“Rahma”
“Bee”
“Nitakufa kwa ajili yako”
“Kwa nini ufe,mume wangu”
“Mtu ambaye anatakiwa kuifanya kazi hiyo ni mimi hapa”
“Ahaaa Eddy usinitanie”
“Sikutanii ila ni mimi hapa”
“Sasa itakuwaje”
“Sina jinsi,nitapambana na kitu chochote kitakacho kuja mbele yangu”
 
“Mmmmm,sasa Eddy.......”
“Hakuna cha sasa”
Nilizungumza kwa sauti iiyo maanisha kitu ninacho kizungumza ni cha kweli na hakina masihara ndani yake.Rahma akanikumbatia kwa huzuni,Gafla taa zote za mji mzima zikazima,na tetemeko la ardhi likaanza kutikisa sehemu zote za mji,Huku miale miale mingi ya kutisha ikiaanza kutoka ardhini huku ikiwa inafanana moto wa Volkano.Gafla jumba la kina Rahma likaanza kumeguka taratibu na kutufanya tuanze kukimbia kuelekea kwenye ngazi.
Kabla hatujaanza kushuka ngazi tukakutana na mtu aliye vaa mavazi meupe tupu akiwa amesimama mwazoni mwa ngazi katika sehemu ya kupandishia huku macho yake yakiwa yanawaka manga wa kutisha ulio ufanya mwili mzima kunisisimka,Tukiwa tunaendelea kumshangaa mtu huyo  nyuma yetu tukasikia kishindo kikubwa kitendo cha kugeuka tukakutana na jitu lenye mabawa na meno yake yakiwa ni makali na yakutisha,na nyumba ikaendelea kumeguka vipande vipande
 
  ITAENDELEA


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts