Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Moja( 41 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Moja( 41 )

Written By Bigie on Monday, March 26, 2018 | 2:26:00 PM

 AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA

Radi nyingi zikaanza kutawala kwenye anga huku mawingu mazito ya mvua yakikusanyika kwa kasi.Ndani ya dakika kadhaa mvua kubwa iliyoongozana na radi kali ikaanza kunyesha.Nikatafuta sehemu ya kujibanza pembezeni ya ukuta ili kuacha mvua ipite
Nikiwa nimeuegemea ukuta niskastukia nikikabwa shingo kwa nguvu na mkono ulio tokeza kwenye ukuta nilio uegeme huku mkono huo ukiwa na kucha ndevu za kutisha

ENDELEA
Cha kwanza kukiwahi ni kuishika shingo yangu kwa haraka na kuanza kuminyana na kiganja hiki kilicho ikamata shingo yangu,nikafanikiwa kujinasua kwenye kiganja,kitendo cha kugeuka nyuma nikakikuta kikimalizikia kuingia ndani ya ukuta.Nikataka kuondoka ila ujasiri mkubwa ukauvaa mwili wangu,nikarudi nyuma hatua chache na kuiangalia jinsi nyumba hii ilivyo kuanzia juu hadi chini.Ni nyumba inayoonekana kujengwa miaka mingi ya nguma,kwani hata kuta zake ni zile zilizo jengwa kipindi cha ukoloni.Nikiwa ninaendelea na uchunguzi wangu wa macho nikaanza kuzisikia sauti za watu wakingong’oneza ndani ya ukuta ambao nilikuwa nimeuegemea.
 
Kila ninapojaribu kuitafsiri hii lugha siipatii jibu kwa maana,kinacho zungumza hakieleweki ila watu hao wanazungumza kwani wanaonekana wanamambishano ya wao na wao.Nikazunguka upende wa pili wa nyumba na kukuta milango na madirisha vikiwa vimefunga,gafla taa zilizokuwa zinawaka nje zote zikazima gafla na kiza kinene kikatawala kila eneo,huku mvua iliyo andamana na radi zikiendelea kurindima kwa kasi ya ajabu.Nikaanza kuondoka taratibu,hatua chache kutoka nyumba ilipo nikasikia jina langu likitajwa ndani kwa sauti ya juu na kunifanya nigeuke nikiwa na mshangao mkubwa
 
Nikatamani kurudi nyuma ila nikaanza kuondoka,kila ninapopiga gatua moja mble ndioyo sauto ya mtu anaye liita jina langu huku akilia ikizidi kuongezeka.Nikayaziba masikio yangu na kwenda mbele zaidi ila nikajikuta saut inayo niita ikizidi kongezeka.Wasasiwasi mwingi ukaanza kunitawala,niakageuka na kuanza kurudi sehemu ilipo nyumba,hadi ni nafika mlango ukafunguka na wala sikumuona mtu aliye ufungua mlango zaidi ya giza nene lililo tawala ndani ya nyumba.
 
“Njoo”
Sauti ambayo ilikuwa ikiniita ikaanza kuniiomba niingie ndani.Nikajitazama kuanzia juu hadi chini na kuanza kupiga hatua za taratibu na kuingia ndani,gafla mlango ukafunga kwa nyuma na nikaanza kuhisi vitu vikianza kunishika shika mwilini mwangu.Sikuwa na budi zaidi ya kuanza kupiga mayowe ya kuomba msaada,ujanja wote ukaniishia.Gafla taa za chemli zipatazo nne zikawaka kwenye kona zote za chumba.Sikuamini kuona watu wengi wakiwa wamerundikana kwenye nyumba hii ambayo kwa ndani haina vyumba kama nyumba nyingine.Watu ambao wapo humu ndani wanavuja damu kwenye miili yao
 
“Tusaidie.....”
Mmoja wao alizungumza huku sehemu ya bega lake ikiwa imenyofolewa badhi ya nyama.
“Kwani nyinyi ni kina nani?”
“Sisi ni watu ambao,tumetafunwa na majini,tusaidie mkuu”
Dada mmoja alizungumza huku machozi yakimwagika sana.Nikajikuna kichwa kwani sikujau hata nianzie wapi kwani kila ninaye mtazama amejeruhiwa kwenye sehemu ya mwili wake.
“Kwani,imekuwaje hadi mumeliwa hivi?”
“Kuna majini wametuteka huko nje,wametuingiza humu ndani.Humla yoyote kwa wakati wowote watakapo amua kufanya hivyo”
“Kuna watu wengi,wameliwa na muda huu wamekwenda kutafuta watu wengine wapya wa kuja kututafuna.Tafadhali tunakuomba utusaidie”
“Kwani munashindwa kutoka nje?”
“Hakuna mwenye uwezo wakutoka nje,hata mlango ukiwa upo wazi ukidhubutu kutoa mguu hata mmoja hapo nje unanata hapo hapo”
 
Nikabaki nikiwa nimesimama,sikujua hata ni vipi niwasaidie,katika kupitisha pitisha macho yangu nikawaona wazazi wa Rahma wakiwa wamejilaza kwenye moja ya pembe huku baba Rahma akiwa ametafunwa sehemu ya shavu la upande wa kulia.Katika kuangalia angalia tena nikaona baadhi ya waalimu wezangu wakiwa katika kundi hili la watu wanaosubiria kutafunwa na majini hao
Nikawafwata wazazi wa Rahma,walipo niona wakastuka hususani baba Rahma,ambaye hadi meno yake yanaonekana  kwani nyama yote ya shavu imeliwa.Nikachuchumaa na kuwatizama kwa macho yaliyo huruma kwani hali zao zipo mbaya.Mara ya kamza sikumuona mama Rahma vizuri.Ila yeye ametafunwa sehemu kubwa ya mbavu zake 
 
“Mwa....na..ngu,naku...omba utusaidie”
Kwa mara ya kwanza baba Rahma kuniita mwanangu,hapo ndipo nikaamini kuwa matatizo hayana mbabe,Japo alizungumza kwa shida ila niliweza kumuelewa.Nikasimama na kuwatazama watu wengine.Sehemu nyingi ya chini kuna mafuvu mengi na mifupa ya watu walio tafunwa.Moyo ukazidi kuniuma sana baada ya kukuta baadhi ya wanafunzi wangu wakiwa wamejeruhiwa vibaya wengine wapo katika hali ya mwisho katika maisha yao.Kitu kingine kinacho zidi kuwaumiza watu wa humu ndani ni njaa kali iliyo changiwa na kukaa kwa muda mrefu pasipo kula.
“Hayo majini wapo wangapi?”
“Wapo wengi tuu,kuna madogo dogo ambayo yanakuja kuja humu na kumchukua wanaye muona amenono na kumtafuna”
Dada mmoja alizungumza,kidogogo akionekana ananguvu nguvu.
 “Sasa hivi wamekwenda kukusanya watu walio salia salia”
Nikasikia sauti ya baba Rahma ikiniita kwa shida,nikaenda hadi sehemu walipo na kuchuchumaa tena
 
“Mwa...nang...u mji mzim...a hauna....watu.Ila wewe ninakuele..kez..a Sehemu moja hivi?”
“Ni wapi baba?”
“Kweny...e nyumba ya...ngu,kuna chumba c...ha maktaba ya vitabu,Humo kuna kitabu ambacho kinaelezea maji...tu ya aiana hii.Ukikisoma hicho kitakusaidia kutuokoa sisi humu nd....ani”
“Sawa baba”
“Pia kuna sehemi,ina mishale....kama Rahma yupo hai muu...lize atakuo....nyesha”
Nikakaa kimya kwani kwa hali ambayo ninaambiwa juu ya hawa majini ninaimani ni lazima watakuwa ametafunwaa.Nikanyanyuka pasipo kumpa jibu lolote baba Rahma nikawafatwa watu ambao nilikuwa ninazungumzanza nao,kabla sijawauliza chochote nikaisikia sauti
 
 “Wanarudi,”
Mzee mmoja alizungumza huku akichungulia nje kwenye uwazi mdogo sana.Moyo ukanipasuka ila watu wawili wakanikumbatia na kunipakaza damu zao na kuniambia nikae nyuma yao kwa ni majini hao wanautambuzi wa kiumbe kipya kinacho ingia ndani ya jumba lao,isitoshe mimi ni mtu wa pekee ambaye nimeweza kuingia ndani ya nyumba hii,wakazizima taa ambazo wameziwasha na giza kali likatawala.Mlango ukafunguliwa kwa fujo na yakasimama majini mawili yaliyo shiba huku mojalikitafuna kichwa cha mtu huku likimalizia malizia kuunyonya ubongo uliopo ndani ya kichwa alicho kishika.
 
Yakanza kunusa nusa na pua zao zilizo wafunuka kama visima visivyo toa maji kwa kipindi kirefu.Yakapiga hatua hadi mbele ya watu walio nificha nyuma yao,wakaendelea kunusa nusa.Kajacho kembamba kakanza kunimwagika,huku mapigo  ya moyo nikiyasikilizia jinsi yanavyokwenda kwa kasi,Gafla mtu aliye simaa kando yangu akashikwa kwa mkono mmoja na jijini hili na kuyanyuliwa juu,Bila ya huruma akamgawanyisha vipande viwili  na damu zinazo toka jini likawa linajimwagia kwenye kichwa chake kilicho kaa vibaya na kina mabonde bonde mengi.
 
Likaanza kuutoa utumbo wa mtu aliye mchukua na kuanza kuutafuna kama linakula soseji,mwili mzima ukanisisimka,nikashindwa kuvumilia na kujikuta nikisimama kwa hasira,kitu ambacho kinanishangaza jini hili lianendela kuutafuna utumbo wa mtu huyu huku likinitazama na mijicho yake mikubwa.Mkono wangu wa kushoto ukaanza kunitetemeka,nikautazama vizuri na kuziona pete zikiwa zinawaka mwanga mkali ambao tangu nizivae sijawahi kuuona mwanga kama huu.Jini likamtupa mtu linalo mla na kuanza kuyaziba macho yake liliuogopa mwanga.Nikamnyooshea mkono wenye pete na jini likazidi kurudi nyuma na kuungana la jingine ambalo linakula ubongo.Nikazidi kuyafwta hadi sote tukatoka nje na mlango ukajifunga.Yakaanguka chini na kutulia gafla mwanga wa pete ukazima,nikashusha pumzi nyingi.Nikarudi kwenye mlango nikajaribu kuusukuma kwa ndani ila haukufunguka.Nikaitazama mijini na kupiga hatua za haraka hadi sehem ilipo angukia.
 
Nikaitazama  kwa umakini,kusema kweli inatisha kwani miili yao imevimbiana vimbiana viyaya sana,Galfa jini moja likafumbua jicho lake na kunistua.Nikajaribu kuinyoosha pete yangu ila hakuna hata moja ambayo haikuwaka.Jini la pili nikafumbua macho yake na wote wakawa wananitazama huku wakikoroma kwa milio ya kutisha.Sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kuaza kukimbia,nikastukia jini mmoja likinipiga kofi lililo nitoa kabisa kwenye barabara na kunigongesha kwenye mti ulio pembezoni mwa barabara.Nikayashududia yakisimama huku yakionekana kuwa na hasira sana.
 
Picha ya mtu aliye katwa katika vipande viwili vya mwili muda mchache ulio pita ikanijia kichwani.Nikayaweka maumivu kando na kusimam na kuanza kukimbia kwa kasi ambayo Mungu amenijali.Yakaanza kunikimbiza,hatua yao moja kwangu ni sawa na hatua kumi nikiwa ninatembea kwa mwendo wa kawaidia.Ikanilazimu kukimbia kwa kasi kubwa huku,nikastukia kumuona  Lusifah akiwa pembeni yangu
“Habari yako baba?”
Lusifah alizungiumza huku naye akikimbia kwa kasi ambayo ninaikimbia mimi,nikashindwa hata kujibu salamu yake kutokana na pumzi kuanza kuniishia kifuani mwangu.Gagla nikalikwepa gari ambalo lilikuwa linakuja kwa kasi mbele yetu na likaenda kugonga majini ambayo yalikuwa yananikimbiza na kuyarusha pembeni.Nikazisikia breki za gari hili zikililazimisha gari hilo kusimama barabarani.Sikuwa na hata hamu ya kutazama nyuma zaidi ya kuendela kukimbia,sikumuoa Lusifah sehemu aliyo kwenda.Taa za gari zinazokuja nyuma yangu zikanifanya nilipishe.Hadi linafika usawa wangu ikanibidi nilitazamame
 
“Eddy ingia ndani ya gari”
Ni sauti ya Rahma ndio ilinisemesha na kujikuta nikijirusha ndani ya gari baada ya kunifungulia mlango wa gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikayashuhudia majini yanayo tukimbiza yakitufwata kwa kasi.Nikamuona Lusifah akipambana nayo huku na yeye akiwa anabadilika badilika katika maombo tofauti.Rahma akatafuta sehemu iliyo tulia na kulisimamisha gari,tukaka kimya tukisubiriana kila mmoja aanze kuzungumza aanacho taka kuzungumza.
“Eddy wazazi wangu....”
Rahma alizungumza huku machozi yakianza kumwagika,nikajizuia kumuambia kuwa wazazi wake wapo kwenye jumba linalo mililiwa na majini,
“Eddy sehemu zote za mji zipo kimya,hakuana mtu hata mmoja,nyumba zimeharibiwa vibaya”
“Yote hii ni kwaajili ya hayo majini yako”
Rahma akaendelea kunilaumu,nikabaki kimya kwani sikujua nijitete vipi kwake.Rahma akanitazama kwa macho makali kisha akaupitisha mkono wake kweny shingo yake na kuanza kuuninyonya mdomo kwa fujo.Akauagungua mkanda wa siti aliokuwa amefunga na kunikalia mapajani huku akiaendelea kuninyonya midomo yangu.Rahma huwa akifika katika swala zima la mapezi huwa hana masihara hata kidogo,akaanza kulivuta shati langi hadi likakatika vifungo yote.Akaendelea kuninyonya kifua changu kwa hasira hadi akaanza kunikwaruza kwenye mbavu kwa kutumia kucha zake
 
“Mapenzi,fujo”
Nilijikuta nikiropoka hii ni baada ya Rahma kunikwaruza kwa nguvu kwenye mgongo wangu,akasitisha kulifanyan zoezi analo taka kulifanya,Akaniangali kwa macho ya makali na akanipiga kofi
“Eddy umesemaje?”
“Ahaaa....eende...”
Akanipiga kofi jengine huku akiniporomoshea matusi mengi,akaendelea kufanya anacho kifanya akaanza kuufungua mkanda wa suruali yangu,kabla hajamaliza nikstukia kuona jitu jengine kubwa na lakutisha,lenye mabawa likisimama mbele ya gari letu na kusababisha kishindo kikubwa hadi gari ikatingishika
     ITAENDELEA


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts