Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Nne ( 44 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Nne ( 44 )

Written By Bigie on Thursday, March 29, 2018 | 4:52:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Asante sana mke wangu”
Nilizungumza huku nikimvuta karibu Rahma, na akakilaza kifua kichwa chake juu ya kifua changu
“Ila mume wangu, ninasiri moja kubwa sana katika maisha yetu, ambayo inanisumbua sana kwenye kipindi chote cha maisha yangu”
“SIRI.....!!, Siri gani?”

ENDELEA
“Nitakuambia tu mume wangu, subiri kwanza watu waondoke”
“Hapana, naomba uniambie mke wangu”
“Nitakuambia tu mume wangu, nakuomba uwe mvumilivu.Ngoja kwanza nikazungumza na hao watu nje, alafu nitarudi kukuambia”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali ya kumchunguza, akayakwepesha macho yake katika kunitazama usoni.Akanipiga busu la shavu na akatoka nje, nikajilaza kitandani huku amani ikiwa imenitoweka kwani sijui ni siri gani ambayo Rahma anataka kuniambia.Nikasikia kelele za watu wakishangilia kwa furaha, sikujua ni kitu gani ambacho Rahma alizungumza hadi kuwafanya watu kushangilia kwa furaha namna hii.Nikanyanyuka kitandani na kuanza kutembea tembea ndani ya nyumba kutazama ubora wa chumba chetu, kusema ukweli kimetengenezwa kwenye hathi ya halil ya juu, kila kitu kimewekwa kwenye mpangilio mzuri wa kuvutia kwenye macho ya kila ambaye ataingia ndani ya hiki chumba
 
Nikaingia bafuni,na kukuta bafu zima, kuta zake zimesilibwa na vioo vigumu sana, Nikajitazama sura yangu na kukuta kidogo ninamabadiliko, kwini hali ya ukijana imeanza kupotea kwa mbali
“Duuu, kweli nimekuwa sasa”
Nilizungumza huku nikijichunguza vizuri, sura yangu
“Ni wakati wa mimi kuwa baba, mwenye familia bora”
Nilizungumza huku nikitabasamu, nikavua shati langu, na kubaki kifua wazi.Hapa ndipo nikaona kovu lililopo nyuma ya mgongo wangu.Nikakumbuka mara ya mwisho nilitua kwenye kisiki cha mti wa mkoko kipindi ninapambana na Joka kubwa.Nikiwa ninaendelea kujitazama kwenye kioo, gafla nyuma yangu nikaiona sura ya Olvia Hitler ikicheka pasipo kuwa na mwili, nikageuka kwa haraka huku nikihema kwa wasiwasi, ila sikuona kitu cha aina yoyote.Nikataka kupiga hatua mbele nikastukia mlango ukifunguliwa, akaingia Rahma
 
“Baby kumbe upo huku?”
Rahma alizungumza huku akinitazama usoni kwa umakini
“Mbona upo hivyo Eddy, kuna tatizo lolote?”
“Haa, hapana”
“Mbona kama una wasiwasi?”
“Hakuna kitu mke wangu”
Rahma akanisogelea na kunikumbatia, huku akiniminya minya mgongo wangu kwa kutumia vidole vyake
“Haumii, nikikuminya hapa?”
“Kwa mbali ninahisi maumivu, ukiniminya kwa nguvu kwenye hilo kovu”
“Pole mume wangu”
“Asante”
“Watu wako, wamesha ondoka”
“Hawajakuletea tabu?”
“Hapana, ila nimewaambia waje kesho kutwa, nitaandaa kasherehe ka kukukaribisha nyumbani”
“Sawa, mke wangu”
“Pia, nimewaambia waandishi wa habari waje wazungumze na wewe”
“Sawa mke wangu”
 
Rahma akafungua maji ya bomba, nne zilizo jengewa kwa juu kwenye kila kona ya bafu na zote zikaanza kuwaga maji kama mvua kubwa inayo nyeshe, Rahma akanza kuninyonya midomo yangu taratibu, huku na mimi nikianza kumvua nguo moja baada ya nyingine.Kila mmoja anaonekana kuwa na hamu na mwenzake, kwani ni kipindi kirefu sana kimepita pasipo kukutana kimwili.Tukaanza kupeana haki sahihi kama wapenzi wawili wanao penda, Utamu wa Rahma ukazidi kuongezeka, kila anacho nifanyia ninakiona kipya kutoka kwake.Mechi ikatawaliwa na furaha na matusi ya nguoni kwa kila mmoja alipojisikia kutoa tusi lake aliweza kufanya hivyo ili mradi kuongeza utamu wa mechi yetu.Hadoi tunamaliza kila mmoja, akabaki akiwa na tabasamu usoni
“Mume wangu, mbona umekuwa mtamu, umeutolea wapi?”
“Nikuulize wewe mke wangu, umekuwa zaidi ya kipindi cha nyuma”
“Ahaaa, ila asante sana mume wangu”
“Hata wewe asante mke wangu”
“Mume wangu, niliweza kuvumilia kwa kipindi chote ambacho wewe ulikuwa hospitalini, japo nilikutana na vishawishi vingi, ila Mungu aliweza kunisaidia hadi leo hii nakutana tena na wewe”
 
“Asante sana mke wangu, kwa maana niwanawake wachache sana wenye roho na moyo kama wako”
“Kweli mume wangu, mimi sikukutamani, nilikupenda na ninaendelea kukupenda.Kwenye maisha yangu sikuwahi kufikiria kumpenda mwanaume kama wewe, amini usiamini wazazi wangu wanakupenda tena sana, ile chuki kwao imekwisha kabisa”
“Kweli?”
“Ndio, hadi baba ametoa mamilioni yake kuijenga hii nyumba, ujue kweli kakupenda”
“Ehaaa, alafu nimekumbuka”
“Umekumbuka nini baby?”
“Naomba uniambie siri ambayo uliniambia inakusumbua?”
Rahma akanitazama usoni, sura yote ya tabasamu ikapotea nasura ya huzuni ikaaanza kuchukua nafasi yake, jambo ambalo likaanza kunipa wasiwasi wakujiuliza kuna kitu gani amabcho kimempata, Akaniachia mwili wangu na kutoa bafuni, ikanilazimu kumfwata nyuma.Sote tukakaa kitandani
“Mke wangu kuna, tatizo?”
Rahma hakunijibu na taratibu akaanza kumwagikwa na machozi, nikabaki nikiwa nimemtumbua mimacho sijui ni kitu gani kinacho mwaga machozi 
 
“Mume wangu, unanipenda?”
“Rahma ni swali gani ambalo unaniuliza, wakati unajua fika mimi ninakupenda kuliko kitu chochote kwenye maisha yangu”
“Eddy, sijui hata nianzie wapi?”
“Kivipi?”
Rahma akanitazama huku machozi yakiendelea kumwagika, hadi sura yake ikaanza kujawa na uwekundu fulani kwa mbali
“Eddy, nakupenda sana mume wangu, sipo tayari kukuona unakufa pasipo....”
“Pasipo kufanya nini?”
Rahma alizidisha kulia, na wasi wasi mwingi ukaanza kunijaa mwilini mwangu na kubaki nikiwa nimemtazama mke wangu huku kigugumizi kizito kikinijaa.Rahma akakiweka kidole kimoja kwenye lipsi zangu, kisha akanipiga busu zito la taratibu sana kisha akaendelea kuzungumza
“Eddy, na uzuri wangu wote huu.Ila sinto weza kukuzalia mtoto, sina kizazi mimi”
 
Nikabaki nikiwa nimeduwaa, kiasi kwamba kuzungumza ninatamani, kukaa kimya ninatamani.Taratibu nikajikuta nikinyanyuka kitandani na kuanza kutembea tembea ndani ya chumba bila ya kuwa na kituo maalumu
“Baby, siku ambayo nilipata mimba yako ya kwanza.Olvia alinitoa kizazi changu, na aliniambia kwamba sinto zaa maisha yangu yote”
Rahma alizungumza huku akisimama, akanishika mkono na kunitazama machoni huku akiendelea kuniangalia.Kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga, sikuamini kama Rahma anaweza kukosa kizazi isitoshe mtoto wa kwanza hakuwa binadamu aliye kamilika
“Nisamehe mume wangu”
“Hupaswi kuniomba msamaha mke wangu, tumuombe Mungu”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika, taratibu.Rahma akanikumbatia na kulala kifuani kwangu taratibu kisha akanipiga busu jengine la mdomoni, ambalo nikashindwa hata kulipokea vizuri
Siku nzima nikashinda nikiwa ninamawazo, japo usoni mwangu nikawa na kazi ya kuilazimisha furaha yangu kujengeka ila nikashindwa kufanya hivi nilivyo tegemea.Hata chakula sikukila kwa raha kabisa
“Mume wangu, nakuomba usiwaze sana juu ya kuta kupata mtoto”
 
“Ahaaa, usijali baby”
Rahma akawa na kazi ya kunifariji
“Hivi kipindi chote ninaumwa maisha yalikuwa yapo vipi?”
“Baby nilipitia sana maisha ya shida, nilihangaika huku na huku kutafuta njia ya kuweza kuyaokoa maisha yako, kusema kweli nilipata tabu sana kutokana hospitalini waliniambia kuwa wewe ni.....”
Rahma akanyamaza na kuniangalia kwa macho ya kuiba kisha akanitazama tena
“Waliniambia kuwa mimi nini”
“Waliniambia kuwa wewe ni mfu aliye hai”
“Kivipi, mbona sijakuelewa?”
“Waliniambia kuwa, ulisha kufa siku nyingi”
Nikabaki nikiwa nipo kimya, kama nimemwagiwa maji ya baridi, swali la kwanza kujiuliza kichwani ni mbinu gani waliyo itumi hadi mimi leo nipo hai.Nikiwa ninaendelea kuliwazia ninalo liwaza nikamuona Olvia Hitler akiwa amesimama nyuma ya Rahma huku macho yake yakimwagikwa na machozi ya damu
 
   ITAENDELEA
Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts