Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Tatu ( 43 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Tatu ( 43 )

Written By Bigie on Wednesday, March 28, 2018 | 3:22:00 PM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Nikaanza kushangulia huku nikiruka ruka juu, nikaanza kupiga hatua nikiondoka baharini huku nikiwa nimejawa na furaha sana.Gafla nikasutkisha nikastukia nikirushwa juu na nikiwa angani nikalishuhudia joka likiwa limeufumbua mdomo wake, huku likiningojea niingie ndai ya kinywa chake.Nikaanza kurudi chini kwa kasi kubwa huku nikipiga kelele nyigi na moja kwa moja nikaingia ndani ya mdomo wa joka
 
ENDELEA
Kwa, haraka nikachomo mshale ulipo kwenye podo langu nililo livaa mgongoni, Nikiwa ninaendela kushuka katika tumbo la mwili wangu, huku nikiwa nimeibana pumzi yangu.Nikaukita mshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza kuuchana mwili wake huku nikimshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza kuuchana mwili wake huku nikiwa ninaendelea kushuka nao chini hadina kumfanya joka hili kuanza kubingiria bingiria huku maji mengi, ya bahari yakiwa yanakingia mwilini mwake
Wingi wa maji unao ingia mwilini mwa joka, yakanifanya niweza kupata nafasi ya kutoka nje ya joka hili ambalo bado linaendela kutapa tapa kwenye maji huku likitoa ukelele mkali.Jokaa likaanza kufutuka huku likiwa moto mkali, Kwa bahati mbaya likanipiga kikumbo, kwa kutumia mkia wake kilichorusha mbali na eneo alilo kuwepo na kunitoa nje ya bahari na kwabahai mbaya nikangukia kwenye kisiki cha mti wa mkono, na kutulia tuli huku giza zito likitawala macho yangu
 
  ***
 “Eddy......Eddy”
Kwa mbali niliisikia sauti ya Rahma ikiniita,nikayafumbau macho yangu taratibu na kukutana  na mwanga mkali ulio nipiga kwenye macho yangu, huku nikiwa, nimelala kwenye kitanda nikipelekwa nisipo pajua na pembeni yangu akiwepo Rahma naye akionekana akitembea huku machozi yakimwagika.Kila ninapojaribu kuyafumbua macho yangu, nikajikuta nikiona maruweruwe hata watu wanao kisukuma kitanda nilicho kilalia sikuweza kuwaona vizuri.Nikajikuta nikitawaliwa tena na giza kwenye macho yangu, na sikuelewa kilicho endelea.
 
Macho yangu yakaanza kupata mwangaza tena wakuona mwanga, nikajaribu kuyapitisha pitiasha kwenye kila kona ya chumba na kufanikiwa kutambua kuwa hapa nilipo ni hospitalini.Pembeni ya kitanda changu, kuna meza ndogo, na juu yake imejaa maua mengi pamoja na kadi nyingi, sikujua ni nani aliye ziweka, kwenye mkono wangu wa kushoto nimechomekwa mrija unaodondosha maji taratibu kwenye mishipa yangu.Tumboni kwangu kumefungwa bandeji lililo kaza, lililo zunguka sehemu nzima ya tumbo hadi mgongoni.Nikaiona kadi moja iliyo andikwa maandishi makubwa kwa kalamu ya wino
(Eddy tunakupenda sana endelea kuugua pole,MUNGU atakuponya)
 
Nikaunyoosha mkono wangu na kuchukua moja ya kadi na kulifungua ndani na kukuta maandishi yanayo nitakia mimi kuugua pole.Mlango ukafunguliwa na akaingia nesi akiwa amevalia mavazi mazuri.Baada ya kuniona akaachia tabasamu pana
“Habari yako kaka Eddy?”
“Salama mambo?”
“Salama, karibu tena duniani”
“Duniani kivipi?”
“Ni story ndefu, ila kwa muda huu pumzika kwanza”
“Sawa, ila Rahma wangu yupo wapi?”
“Amekwenda kupata chakula cha mchana”
“Kwani nesi, hapa nipo wapi?”
“Upo hospitali ya mkoa, Bombo”
“Sawa, ila ninaomba kama una namba ya Rahma mpigie”
“Usijali kwa hilo, kaka yangu”
Nesi alizungumza huku akionekana kuwa na furaha kubwa sana, akatoka baada ya muda kidogo akaingia Rahma, ila kitu kilicho nishangaza kidogo ni ukuaji wa Rahma.Kwani amebadilika kwa kiasi fulani, ameongezeka mwili na kuwa mrefu kidogo.Machozi ya furaha yakaanza kumwagika taratibu akapiga hatua hadi kitandani, akanikubatia huku akiendelea kumwagikwa na machozi ya furaha.Taratibu na mimi machozi yakaanza kunimwagika
 
“Eddy”
“Naam”
“Upo hai tena?”
“Ndio mke wangu”
“Asante sana Mungu kwa yale yoteuliyo nitendea kwenye maisha yangu, Wewe ndio muweza wa kila kitu.Ohooo asante sana MUNGU wangu”
Rahma alizungumza huku akiendelea kunikumbwatia kwa nguvu zake zote, tukakumbatia kwa dakika zaidi ya kumi huku macho yangu nikiwa nimeyafumba.Nikayafumbua macho yangu na kukutana, kama kumi na tano wakiwa na kamera za video na kamera za picha, huku kila mmoja akiendelea kuchukua tukio analo liona yeye linamfaa.
Taratibu Rahma akaniachia, akaanza kuninyonya midomo yangu taratibu huku akimwagikwa na machozi mengi.Hakujali kama kuna waandishi wa habari
“Nakupenda sana, Eddy wangu”
“Hata mimi pia mke wangu ninakupenda sana”
Baadhi ya waandishi wa habari wakaanza kupiga makofi wakifurahia tukio ambalo linaendelea kati yangu na Rahma.Mmoja wao akaguna mimi na Rahma tukamtazama
“Samahani, kwa kuwaingilia katika mazungumzo yenu”
“Bila samahani kaka” Rahma alijibu
“Kwajina ninaitwa Jumaa Hassan ni muandishi I.T.V, ningependa kujua, unajisikiaje bwana Eddy kwa sasa?”
“Mimi nipo vizuri tuu, najisikia sawa”
 
“Je, kwakipindi chote cha nyuma tunaweza kupata japo dondoo moja, mbili tatu hivi kwa yale yaliyo kukuta”
“Jamani samahani, natambua uwepo wenu hapa na ninawaheshimu sana ndugu zangu kwani bila nyinyi kushirikiana na watanzania wengine katika swala zima la kuendeleza maombi kwa mume wangu, leo asinge fikia hapa.Kitu amacho mimi ninawaomba kwa wakati huu.Mumuache mume wangu apumzike kidogo, na nitajaribu kupanga naye siku ambayo anaweza kuzungumza na nyinyi na mukamuhoji kila swali ambalo munalihitaji, SAWA NDUGU ZANGU”
Rahma alizungumza kwa sauti ya upole na unyenyekevu iliyowafanya waandishi wa habari kumuelewa, kila mmoja akanipa mkono wa kunitakia heri katika kupona na kutoka nje ya chumba
“Baby, hayo maua na makadi yametokea wapi?”
“Ni zawadi za watu ambao wanaendelea kukuombea kwa kipindi kirefu sasa”
“Kipindi kirefu?”
“Ndio mume wangu, ila tutazungumza siku nyingine juu ya hilo swala”
“Nidokezee japo kidogo mke wangu”
“Hapana Eddy siwezi kukuambia kuhusiana na chochote hadi madaktari wanihakikishie kuwa umepona vizuri”
“Baby mimi mbona nipo powa”
 
“Eddy, bado haijawa powa”
Rahma hakuweza kuniambia kitu cha aina yoyote, nikakaa hospitalini wiki mbili, huku kila sikuwatu wengi wakija kunitembelea hadi badhi ya viongozi wa ngazi za juu nchini akiwemo raisi wa nchi, nikaruhusiwa kutoka hospitalini.Siku ambayo ninatoka sikuamini macho yangu kukutana na wananchi wengi wakiwa nje ya hospitali wakinisubiri kwa hamu.Kila mmoja akaanza kushangilia kwa furaha na wengine hawakusita kuyazuia machozi yao.Baadhi yao wamevalia tisheti yeupe na yeusi zenye picha yangu huku zikiwa na maandi chini ya picha hiyo yaliyo andikwa
(EDDY WEWE NI SHUJAA WETU)
“Baby wapungie mkono watu”
Rahma aliniambia, nikawapungia watu mkono na kuwafanya wazidi kunishangilia.Kila kitu kinacho tokea kwenye maisha yangu ninaona ni kama ndoto ambayo sikutarajia kama ipo siku watu wengi watanipenda na kunishangilia kwa kiasi kikubwa kama hawa.Askari wakawa na kazi ya kuwazuia watu wasifike karibu yangu.Hadi ninaingia ndani ya gari la kifahari nikawa bado siamini kwa kile ninacho kiona.Waendesha wengi wa pikipiki wakatangulia mbele ya gari tulilo lipanda mimi na Rahma, huku likiendesha wa dereva ambaye simjui
 
Magari mengi nyuma yakawa yanalifwata gari letu, ikamlazima dereva kutembea kwa mwendo wa taratibu.
“Baby tunakwenda wapi?”
“Tunakwenda kwetu”
“Kwetu wapi?”
“Ni sapraiz mume wangu”
“Mmmm haya”
“Mbona umeguna, huamini au?”
“Naamini”
Rahma akanilalia kifuani kwangu, huku vidole vyake, vya mkono wa kulia, vikiwa na kazi ya kukikiminya minya kifua changu.Waendesha pikipiki wanao ongozwa mbele na gari ndogo ya polisi wakasimama kwenye jumba moja kubwa lililojengwa kwa aina yake, huku wakipiga honi nyingi, Taratibu gari yetu, ikingia ndani ya geti kubwa.Mandhari ya jumba hili yamepambwa kwa maua mazuri yakupendaza.Tukashuka kwenye gari na kwamsaada wa polisi nikaingia ndani kwani watu wengi wanatamani kuniona.Tukapandisha gorofani na kutokea kwenye sehemu ya mbele ya nyumba ambayo hata nikisimama watu wote wataniona
 
Sauti za wanawake zikilitaja jina langu zikaendelea kunishangilia huku wengine wakisema wananipenda sana
“Habari yenu”
Nilizungumza na watu wote wakashangilia kwa furaha
“Hatujambo”
“Jamani, sina mengi ya kuzungumza kikubwa ninachotaka kuwaambia ni kwamba ninawapenda sana na ninashukuru kwa ibada zetu mulizo zifanya kwa kipindi chote ambacho mimi nilikuwa ninaumwa hadi hapa nilipo fikia”
Watu wakaendelea kushangilia kwa furaha, kiasi kwamba nikajikuta machozi yakinimwagika na mimi.Nikashindwa kabisa kuzungumza kwa furaha niliyo nayo kwenye kwa wakati huu, rahma akanichukua na kunipeleka kwenye chumba ambacho kimejaa vitu vingi vya dhamani ya hali ya juu huku hata kitanda chake kikiwa kimetendgenezwa kwa muondo wa kipekee
 
“Rahma vitu vyote hivi, vimetokea wapi?”
“Ni zawadi kutoka kwa baba na mama”
“Wao mbona siwaoni?”
“Wamehamia Dubai”
“Baby, hawa watu wote wametokea wapi?”
“Eddy mume wangu, ni miaka miwili na miezi nane imepita tangu ulipo kuwa hujitambui, wala hujielewi.Sikukata tamaa juu yako ila, Mungu ni mwema hadi umerudi kwenye hali hiyo”
“Asante sana mke wangu”
Nilizungumza huku nikimvuta karibu Rahma, na akakilaza kifua kichwa chake juu ya kifua changu
“Ila mume wangu, ninasiri moja kubwa sana katika maisha yetu, ambayo inanisumbua sana kwenye kipindi chote cha maisha yangu”
“SIRI.....!!, Siri gani?”
 
 ITAENDELEA


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts