Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini ( 20 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini ( 20 )

Written By Bigie on Sunday, March 4, 2018 | 9:21:00 AM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOSIHIA
   Nikanyanyuka kwenye kiti kwa hasira na nikapiga hatua za haraka kumfwata Hilda sehemu aliyo simama  na akaanza kukimbia kuelekea ndani kwangu huku na mimi nikimkimbiza kwa nyuma na kabla hajashika kitasa cha mlango wa kuingilia chumbani kwangu akakanyaga maji yaliyopo juu tarzi na gafla akateleza na kuanguka kwa kwa nyuma na kichwa chake kikapiga chini kwa nyuma na damu zikaanza kusambambaa taratibu kutoka sehemu kilipo angukia kichwa cha Hilda na kuufanya mwili wangu kuanza kutetemeka kwa woga

ENDELEA
   Nikamsogelea Hilda na kukuta akirusha rusha miguu yake kama mtu anaye kata roho na kuzidi kunichanganya huku jasho jingi likianza kunitoka mwilini mwangu.Nikasimama kwa muda nisijue nini cha kufanya nikapiga hatua za haraka na kuingia jikoni na kuanza kutafuta kitu nisicho jua,Kwa kuchanganyikiwa nikajikuta nikizunguka jikoni zaidi ya dakika kumi huku kila ninacho kishika kwangu ninakiona ni kibaya.Nikachukua kitambaa cha kukaushia vyombo baada ya kuoshwa kisha nikatoka nacho hadi sebleni.Mapigo ya moyo yakazidi kunidunda kiasi kwamba hadi sauti ya mapigo ya moyo nikaanza kuyasikia yakidunda kwenye kifua changu hii ni baada ya kuto na kutokuuta mwili wa Hilda zaidi ya kuona michuruziko ya damu inayo elekea mlango wa kutokea nje
 
    Nikajishauri kwa muda kisha taratibu nikaanza kupiga hatua za taratibu kuelekea mlango wa kutokea nje na kabla sijaufungua mlango wa mbele ambao umefugwa na funguo kama Halda alivyo ufunga nikaamua kurudi jikoni huku akilini nikiwaza kwenda kuchukua kisu kwa ajili ya kujilinda kwa chochote kitakacho jitokeza mbele yangu.Nikanza kusogeza kitu kimoja baada ya kingine nikitafuta kisu na sikukiona kwa haraka nikachukua uma wa kulia chipsi na kutoka huku mkono mmoja nikiwa nimeshika kitambaa ambacho sikujua nitakitumia kwenye nini.Nikafungua kwa tahadhari  mlango wa nje na kuchungulia na sikuona kitu chochote zaidi ya gari la Hilda
 
    Nikaanza kujiuliza ni wapi mwili wa Hilda emekwenda na mbaya michuruziko ya damu imeishia katika mlango wa kutokea nje .Nikageuka na kuufungua mlango na kuingia ndani huku akili ikiwa imevurugika nikapiga hatua za taratibu na kukaa kwenye mguu wa sofa kabla makalio yangu hayajafika kwenye mguu wa sofa taa zote za nyumbani kwangu zikazimika na nikajikuta nikisimama wima kama askari anaye subiria wimbo wa taifa lake.Gafla nikasikia watu wawili sauti ya kiume na yakike zikibishana chumbani kwangu na kujikuta nikizidi kutetemeka kwa woga huku mwili wangu ikinisisimka na vinyweleo vyote vikanisimama.
 
   Mabishano ya watu hao yakazidi kupamba moto huku mwanamke mwenye sauti kama Hilda akimuomba mwanaume huyo asitoke nje ila mwanaume anang’ang’ania kutoka.Akili yangu kwa haraka ikarudisha kumbukumbu ya mazungumzo ya bibi kuwa Hilda ni mke aliye olewa na jini lililopo kifungoni na sikujua kama ndio lenyewe linalo bishana au kuna jingine.Mwili mzima ukazidi kusisimka huku ukitetemeka na gafla nikastukia nikishikwa begani na kitu chenye mkono wa baridi kiasi kwamba hata kama umevaa jaketi baridi yake ni lazima ipeye kwenye mwili wako
 
Nikajua tayari nimekwisha na taratibu nikageuka huku nikiwa nimeyafumba macho yangu ili nisione ninacho kwenda kuonana nacho,Nikastukia kikinigusa  shavuni kwa mkono wake wa baridi na kujikuta nikizidi kutetemeka kwa woga na kwa mbali nikaanza kuyafumbua macho yangu na nikajikuta nikizidi kuyafumbua kwa mshangao kiasi kwamba ninajikuta nikimeza fumba kubwa la mate kulisuuza koo langu ambalo limekauka
 
“Rahma”
Niliita kwa sauti ya chini huku nikitazamana na Rahma ambaye amesimama mbele yangu huku akiwa amevalia gauni jeusi kama anakwenda msibani
“Shiiiiii”
    Rahma alikiweka kidole chake mdomoni akiniashiria nisizungunze kitu cha aina yoyote na kunifanya nikae kimya huku nikijiuliza maswali imekuwaje kuwaje hadi Rahma ametokea sehemu hiyo.Akanishika mkono na taratibu tukaanza kupiga hatua za kutoka nje huku macho yangu nikiwa nimeyaelekeza mbele na sikutaka kutazama nyuma na laiti kama nitasikia mlio wowote miguu yangu imejiandaa kwa kazi ya moja tuu ambayo ni kukimbia kuyaokoa maisha yangu
Tukatoka hadi nje huku Rahma akionekana kuwa na furaha ila kwangu sikuwa na furaha ya aina yoyote na isitoshe bado Rahma ananipa wasi wasi kwani mara ya mwisho kuzungumza naye jana mchana alidai kwamba anakwenda Dubai sasa siji imekuwaje Dubai imekuwa ni kwangu nilipo hamia.Rahma akanishika kiuno na kaniomba nifumbe macho kuna zawadi nzuri anahitaji kunipa,nikafunga jicho moja huku jengine nikiwa nimeacha kajiuwazi kadogo cha kuweza kuona ni nini anacho taka kukifanya Rahma
 
‘Hujafunga baby?”
“Nimefunga jamani”
“Mbona hilo jicho lako la kushoto linaona?”
“Haya ng…….”
“EDDY KMBIAAAAAAAAAAAAA………..!!!”
    Nikaisikia sauti ya Hilda ikiniomba nifanye ninacho takiwa kukifanya kwa wakati huo,Nikayafumbua macho yangu na kutazama  ni wapi alipo Hilda nikastuskia macho yangu yakitua kwenye sura isiyo eleweka ni kipi ni kichwa na yapi  ni macho kwani kwa haraka haraka mtu ambaye nilimdhania ni Rahma macho yake yameongezeka na kuwa matatu huku jicho moja likiwa kubwa katikati ya uso wake huku mengine madogo mawili yakiwa pembeni kwenye usawa wa mashavu yake.Kichwa chake kina mapembe marefu pamoja na ulimi mrefu na ndevu nyingi huku mwili wake ukiwa na umbo la Rahma
 
Nikachomoka kwa kasi ya ajabu hadi getini na kukuta limefungwa na funguo ambayo sikujua ni wapi Hilda ameiweka cha kushangaza mtu huyo ambaye kwa haraka haraka nikajua atakuwa ni jini akapiga hatua za taratibu huku akicheka na kupiga makofi huku ulimi wake amabao ni mrefu kama ulimi wa kinyonga akiutoa nje na kuuingiza ndani huku vidole vyake virefu vikiwa na kicha ndefu kiasi kwamba nikazidi kuchanganyikiwa
“KWA JINA LA YESU PEPO MCHAFU TOKAA MBELE YANGU”
Nilizungumza huku nikiwa nimeunyoosha mkono wangu wa kulia kama wanavyofanya wachungaji wangi wanao ombea watu katika huduma zao mbali mbali za kidini na wala sikujua ni wapi maneno haya yalipo tokea.Mtu huyo akazidi kupiga hatua za taratibu huku akiendelea kucheka kwa kicheko cha kejeli
“Eddy wewe una dhambi kama sisi Halllllooooooo…kwahiyo huwezi kunidhuru kwa lolote”
Alizungumza huku ulimi wake akiutoa na kunilamba lamba nao kwenye mashavu yangu huku taratibu kucha zake akizipitisha kwenye kifua changu kusababisha shati nililo livaa kuchanika na kujikuta nikizidi kutetemeka na kuchanganyikiwa
 
“Kuomba kwenyewe huwezi sembuse leo uje kunikemea……UMESHINDWA BWANA MDOGO”
Nikaanza kusali kimoyo moyo huku nikizidi kuongeza juhudi za kuliita jina la Mungu wangu amweze kuniokoa.Jamaa akaninusa nusa kisha akapiga hatua mbili nyuma
“UNA BAHATI LEO DAMU YAKO NA NYAMA YAKO HAIJAIVA IKIIVA JIANDAE KUWA CHAKULA CHANGU KAMA ULICHOKILA MEZANI LEO”
Jamaa alizungumza huku akipiga hatua za kurudi nyuma na kuufanya mwili wangu uzudi kutetemeka hapo ndipo nikamuona Hilda akiwa ameegemea kwenye mlango wa kuingilia ndani huku akiwa analia,Jamaa akamsogela Hilda na kumsika kichwani na kumuachia kisha akapotea na kujikuta nikiburuzika taratibu kwenda chini huku mgongo wangu ukiwa unaburuzika kwenye geti nililo liegemea na kunifanya nizidi kuchoka kwani kwa siku mbili nilizo hamia kwenye hii nyumba zimekuwa ni sawa na miaka 200 ya mateso na shinda nynigi
 
Nikazidki kuchanganyikiwa baada ya kumuona Halda akinifwata getini kwa haraka nikanyanyuka na kuanza kujaribu kulifungua geti
“Eddy usinikimbie mimi sio jini”
Halda alazungumza huku akiongeza kupiga hatua za kunifwata getini na nikajikuta nikisitisha zoezi la kwenda nje na kumtazama kwa umakini
“Edy nakuomba unielewe mimi sio jini kama unavyo fikiria wewe.Kuna kitu ambacho sikuhitaji nikuambie mapema ila nitalazimika kufanya hivyo”
“Hilda sikiliza kama ulinileta kunipangisha kwenye hii nyumba ili muje kunila nyama mumeshindindwa nipo tayari nipoteze pesa nilizo lipa kodi niondoke zangu kwenye hii nyumba”
“Eddy kukimbia nyumba sio suluhisho lamatatizo”
“Ila”
“Kuwa na mimi ili haya matatizo yaishe”
“Wee wee weee usinichanganye  kabisa kwanza sijui yule aliyekuja kunilamba lamba sijui ni mumeo alafu bado unaniambia mimi nibaki na wewe.Ndio maana tangu jana nilikuwa nikikuambia uondoke ila hukutaka kunisikia”
 
“Eddy hembu tulia nikusimulie ninacho hitaji kukuambia ukweli kuhusu mimi”
“Hiyo ndio gia yako ya kunitongozea mimi si ndio?”
“Hapana Eddy tulia basi nikuambie kitu…….nakuomba twende ndani tukazungumze hilo swala”
“Wewe na giza lote humo ndani unataka mimi niingie”
“Wewe twende”
Hilda akanishika mkono na kuanza kunikokota japo nafsi yangu inasita ila sikuwa na ujanja zaidi ya kumfwata Hilda anapo elekea.Kitendo cha kufungua mlango taa za nyumba nzima zikawaka pasipo kuwashwa na sisi,Michirizi ya damu yote nikakuta haipo kwenye sakafu na nikabaki nimeduwaa hadi Hilda ananikalisha kwenye Sofa ndio nina stuka
“Eddy”
“Naam”
“Upo tayari kusikliza nitakacho kuambia?”
“Nipo tayari endapo na wewe utakuwa tayari kuondoka ndani ya nyumba yangu”
“Sawa nitafanya hivyo…….Eddy ninakuomba unisamehe kwa kukuficha ukweli wa maisha yangu,Mimi nimezaliwa katika mchananyiko wa binadamu na Jini”
 
“TOBAAAAA….KWA HIYO WEWE NI JINI?”
“Usiwe na papara…….Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mimi ni jini japo ninazitambua sheria na misingi yao…..Baba yanguni ni jini ila mama yangu ambaye sasa ni marehemu yeye alikuwa ni binadamu wa kawaida….Wtu wengi husema watoto wa aina hii wengi wao hawaonekani ila si kweli kuna mambo ukiyafanya kipindi mtoto wa aina hii akiwa mdogo basi maisha yake ataishi kama bidanamu wengine…..Mimi nimeolewa na jini na yule aliye kuja pale ni mdogo wa mume wangu aliyopo gerezani”
“Haaa shemeji gani ana sura mbaya kiasi kile?”
“Hahaaaa pale alijaribu kukutisha ila kama mwanzoni ulimuona alivyo kuja katika muonekano kama Rahma”
“Sasa kwanini siku zote hukuniambia hili swala?”
“Usinge weza kustahimili na ungepata wasi wasi ambao ungeyagharimu maisha yako”
“Kivipi?”
“Ungeweza kuwa hata kichaa au ungekufa kabisa”
“Mmmmmmm…….”
“Usigune kila ninacho kuambia kipo kwenye ukweli wa maisha yako na kinacho kutokea si ndoto japo kwa wakati huu mimi sina nguvu za kijini na nibinadamu kama ilivyo wewe”
 
“Acha zako wewe haupo sawa na mimi…..Sasa lipo wapi jeraha la kichwani mwako mbona silioni?”
“Niliponywa na shemeji yangu”
“Sasa ilikuwaje nilisikia unazungumza naye chumbani na huku yeye akiwepo hapa sebleni”
“EADDY SIKU ZOTE MAJINNI YANAWEZA KUJIGAWA KATIKA MAUOMBO TOFAUTI TOFAUTI KWA WAKATI MMOJA”
“Basi ninakuomba mimi leo nisilale hapa”
“Unataka kwenda wapi?”
“Popote bora iwe nje ya hapa”
“Sawa nenda kajiandae”
“Wewe huondoki?”
“Wewe nenda kajindae”
Nikanyanyuka na kuingia ndani kwagu nikafungua droo na kutoa nguo nyingine safi na kuzivaa nikachukua kiasi chote cha pesa kilichopo kwenye kabati langu na kurudi sebleni na kumkuta Hilda akiwa amesimama akinisubiri huku akiwa amevali kanga moja
 
“Unakwenda hivyo na kanga?”
“Ndio”
“Kwa nini sasa?”
“Nimeamua”
Sikutaka kubishana naye zaidi ya kutoka nje na sote tukaingia ndani ya gari na tukafika kwenye hotelo moja iitwayo NAIVERA nikaingia ndani na kumuacha Hilda kwenye gari.Nikalipia chumba na kutoka nje kuzungumza na Hilda ila sikumkuta yeye wala gari lake,nikaingia kwenye chumba nilicho kodi kwa siku tatu ili niipumzishe akili yangu kwa majanga yaliyo nikuta kidogo nikapata usingizi ambao sikuota kitu ca aina yoyote.Nikaja kustuka baada ya simu ya mezani kuita.Nikaitazama kwa muda kisha nikaipokea na kusikia sauti nzuri ya kike
“Za asubuhi ndugu mteja”
“SALAMA”
“Unakaribishwa katia kupata kifungua kinywa je uletewe chumbani kwako au utakuja kunywa katika kumbi zetu”
“Nileteeni huu huku”
“Asante na asubuhi njema”
 
Simu ikakatwa na nikajirudisha kitandani na kuanza kufikiria hii hatua ngumu ninayo ipitia kwenye maisha ya ngu,Mlango ukagongwa na nikaufungua akaingia msichana mwenye uzuri wa pekee huku akiwa ameshika sinia lenye vikombe vya chai na sahani iliyo funikwa.Kiuno chake chembaba kimebeba mzigo wa makalio makubwa kiasi yaliyo jifichwa kwenye kijisketi cheusi kifupi kinacho yaacha mapaja yake wazi kwa sehemu kubwa na nikajikuta mwili wangu ukianza kusisimka.Kifua chake kikabeba chuchu kubwa kiasi na kunifanya nibaki ninameza mate ya uchu huku koki yangu ikisimama taratibu.Kwenye sura ndio amenimaliza kabisaa kwa jinsi alivyo jipara huku nywele zake akiwa ameziweka kama Rihana nikabaki nimeduwaa huku nikikiangalia kidoti chake cheusi kilichopo karibu na pua yake
“Karibu kifungua kinywaa”
Nikaendelea kumtazama kwa mshangao na wala sikuweza kusikia anacho niambia ni nini
“Kaka karibu chai”
 
“UMEOLEWA”
“Ndio na nini mtoto mmoja”
“Ni muda gani unaweza ukapata muda tukazungumza?”
“Sasa hivi tunaweza tukazungumza tuu kwani ndio muda wa mimi kutoka kazini”
“Una itwa nani?”
“Habiba”
“Ohoo unajina zuri kama wewe mwenyewe”
“Asante zungumza haraka haraka kwa maana ninahitaji nika singout niende nyumbani”
“Ok unakalia wapi?”
“Karibu na Makorora Hospitali”
Nikajikuta hata ninacho hitaji kumuambia kikiyayuka akilini mwangu kama barafu ukiliweka juani na kubaki nikimtazama kama ninajiandaa kupiga picha ya mnato
“Halooo kaka”
“Eheeee”
“Mbona kimya?”
“Mmmm haya mwaya shemeji ana faidi”
“Asante wangu basi ninaomba niende”
“Haya mwaya ila jioni si utakuja?”
 
“Wapi?”
“Kazini”
“Ndio ninaingia saa nne usiku”
“Haya mwaya”
Habiba akafungua mlango na kutoka nikabaki nikijirusha kitandani na kuurudia tena usingizi na wala sikuwa na wazo la kwenda shule kufundisha.Nikastuka mida ya saa saba mchana nikaingia bafuni nikaoga na kunywa chai kisha nikawasha tv na kuanza kutafuta kipindi kizuri kitakacho ifurahisha nafsi yangu.Nikapata kipindi kizuri na kuanza kufwatilia kwa umakini mchezo wa mereka hadi inatimu saa tisa na nusu nikatoka nje ya hoteli nikapata chakula cha mchana na kurudi chumbani kwangu na kujitupa kitandani na kuanza kuutafuta usingizi ambao haukuja kabisa.Mida ya usiku nikatoka na kwenda kula chakula cha usiku.Nikiwa ninarudi chumbani kwangu nikamuona Habiba akiwa anaingia Hotelini akiwa amevalia nguo za kawaida kiasi kwamba uzuri wake umezidi kuongezeka.
 
Akanipungia mkono kwa ishara ya kunisalimia na mimi nikamjibu kwa kumpungia mkono kisha nikapiga hatua za kumfwata ila akanikonyeza na kunionyesha mzee wa pembeni aliye kaa kwenye kiti na nikajikuta nimesimama huku nikizuga kwa kuitoa simu yangu mfukononi na kuanza kuiminya minya.Kwa ishara akanimbia aliye kaa kwenye kiti ni bosi wake sikuwa na jinsi zaidi ya kuelekea chumbani kwangu,Hazikupita dakika nyingi mlango ukagongwa na nikaufungua mlango na kumkuta Habiba akiwa amevalia nguo zake nilizo muona nazo,nikamkaribisha ndani na moja kwa moja akakaa kitandani
“Za muda Habiba?”
“Sio salama”
“Kwa nini?”
“Ninamatatizo makubwa kaka yangu wee acha tuu”
“Matatizo gani hayo ndugu”
“Ni historia ndefu kidogo ila ngoja tu nikuambie”
“Ehee”
 
“Nilikuabia nina mume na mtoto mmoja?”
“Ndio”
“Basi mume wangu mimi anafanya kazi Saruji…..na siku zote huwa nilikuwa ninasikia kuwa anamwanamke wa nje tofauti na mimi”
“Ehee”
“Watu ambao walikuwa wananimbia siku zote nikawa ninawabishia nikijua ni wafitinishaji wa ndoa yangu…..Sasa leo mchana muwe wangu amefumaniwa na mke wa mtu,amepigwa kiasi kwamba amelazwa hapo Bombo hospital”
“Duuu pole sana”
“Weee acha tu kaka ninaumia sana mwanaume ninaye mpenda na kumuamini kunifanyia kitu kama hiki sijui ni nini alikosa kwangu”
Habiba alizunumza huku machozi yakianza kumwagika na taratibu akaanza kujifuta kwa kutumia kitambaa alicho kishika
 
“Sasa hali yake inaendeleaje?”
“Hali yake sio nzuri…..na mbaya zaidi huyo mwanamke aliyekuwa akimchukua mumewe ni bondia maarufu hapa mjini”
“Duuu pole sana kwa hilo sasa itakuwaje?”
“Yaani hapa nilipo sielewi…..kurudi kwangu ni aibu watu wananicheka mimi?”
“Mtoto wako yuko wapi?’
“Yupo Kange kwa bibi yake mzaa baba”
“Mmmm pole sana”
“Yaani kaka yangu hapa sijui nifanyaje nimeomba ruhusa ya kumuuguza mume wangu ila hata hamu ya kwenda huko hospitalini sina”
Habibi alizungumza huku taratibu akijisogeza nilipo huku akiendelea kulia na taratibu kichwachake akakilaza kwenye mapaja yangu na mkono wangu mmoja nikauweka kwenye ziwa lake na kuliminya kumfanya astuke na kunitazama kwa jicho kali la hasira

ITAENDELEA


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts