Home » , » TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Mbili ( 22 )

TANGA RAHA- Sehemu ya Ishirini na Mbili ( 22 )

Written By Bigie on Tuesday, March 6, 2018 | 11:52:00 AM

AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
     Akaanza kupiga hatua zenye vishindo vya hali ya juu huku akinifwata taratibu,nikaona sio sehemu nzuri ya mimi kukaa nikachomoka kwa kasi na kuufungua mlango wa kutokea njee na kwapupa nilizo nazo zilizo chaganyikana na woga nikajikuta nikipiga mwereka mmoja mkali na kuanguka kifudi fudi kama mtoto anayeanza kutembea.Nikastuka zaidi baada ya kuona miguu ya watu wawili wakiwa wamesimama mbele yangu.

ENDELEA
    Nikainyanyua sura yangu na kukutana na Hilda akiwa na msichana mwengine ambaye sikuwahi kumuona hata siku moja.Wakabaki wakinishangaa kwani hawakujua ni kitu gani kinachonikimbiza.Nikananyayuka na kuanza kujifuta futa vumbi lililo jaa kwenye mwili wangu
 
“Eddy unatatizo gani wewe?”
Nikatazama nyuma na sikumuona Mwajuma na kuukuta mlango ukiwa umefungwa,
“Eddy mbo haueleweki?”
“Wee niache tuu sijajua ni kwanini ulinileta kwenye hii nyumba?”
Nilizungumza huku nikipiga hatua za kwenda nje na kuwafanya Halda na mwanzake kunifwata kwa nyuma huku wakiniongelesha na wala sikuwaelewa ni nini wanacho kizungumza.Nikakaa kwenye msingi wa bustani ya maua iliyopo nje ya ukuta wa nyumba yangu na Hilda akasimama mbele yangu huku akiwa amejishika kiuno
“Eddy hembu niambie una tatizo gani?”
“Tatizo ni hii nyumba hembu tazama nina siku kadhaa nimesha anza kuchakaa kiasi hichi je nikikaa wiki hapa si nitakuwa tambara la deki”
 
“Jamani Eddy kwani humo ndani kuna tabu gani.....?”
“Hembu nitolee unafki wako hapa inamaana hujui kinacho endelea humo ndani?”
“Sawa japo na tambua ila sio wewe kukimbia kimbia utakuja uumie kwa vitu vya kitoto”
“Wewe unaumwa nini kwanza ninaomba umpigie simu baba mwenye nyumba aje hapa ili mkataba kama ni vipiti tuuvunje na mimi anipe nusu ya malipo na hiyo pesa nyingine mimi ninasamehe”
“Eddy.....”
“Hakuna cha Eddy wewe unaona Raha hivi mimi ninavyo teseka Si ndio?”
“Shem kwani tatizo ni nini?”
Rafiki wa Hilda akaniuliza na kunifanya nibaki nikimtazama pasipo kumjibu kitu cha aina yoyote hadi akajistukia
“Muulize huyo rafiki yako”
“Shosti wala hakuna kitu huyu mwanaume ni uwoga wake tuu”
 
Sote tukastuka baada ya geti kupigwa kikumbo hadi likafunguka na hapakuwa na mtu aliyetoka na tukajikuta tukikimbia huku kila mtu akishika njia yake.Baada ya kukimbia kwa muda nikajikuta nikiporomosha katika kilima cha bichi ya Raskazone.Nikatafuta sehemu na kukaa ili kijiupepo kinipige vizuri na nikapata wazo la kuingia ndani ya bichi hiyo,Nikalipa kiingilio na kutafuta sehemu iliyo tulia na kukaa huku nikijishauri jinsi ya kurudi nyumbani kwangu.Nikajikuta nikiyafwatilia mazungumzo ya wanaume wawili walio kaa pembeni yangu
“Katika ulimwengu huu hakuna kitu kinacho shindikana mbele ya Jina la Yesu kristo”
“Kweli mchungaji kwa maana nilipo toka ni mbali sana hadi leo ninatazamika kama mtu kweli Mungu ni mwema”
“Unajua shetani anamambo mabaya sana katika ulimwngu huu,Huwa hapendi kuona watu wa Mungu wakifanikiwa kiasi kwamba anawafunga kwa mambo ya ajabu ajabu kama wewe jinsi alivyo kupeleka kuzimu”
 
“Yaani kipindi kile sikujua ilikuwa vipi kwa maana nilikuwa ni muumini mzuri wa dini.Ila kuna siku nilikutana na dada mmoja katika mtandao wa Facebook....Basi tulikuwa marafiki wa kuchati chati hadi ikafikia hatau tukawa ni wapenzi kabisa...”
“Hembu ngoja kwanza......Inavyoonekana tatizo lilianzi hapo?”
“Ninavyo hisi kwa maana yule dada aliniambia kuwa yeye anatokea Zanzibar na tukapanga siku tukutane Dar kipindi nilipokuwa ninafanya kazi kwenye bandari ya Dar es Salaam.......Haikuwa ngumu kwa sisi kukutana na kutokana nilikuwa ninajuana na watuw engi ambao ni manahoza wa boti zinazo kwenda Zanzibar niliwatumia wao kufanya upelelezi juu ya binti huyo na wakanihakikishia kwamba yupo na anajiheshimu”
 
“Ehee ikawaje”
Nikakohoa kidogo na kuwafanya mchungaji na mtu wake kunitazama kisha wakaendelea na mazungumzo yao
“Basi nilimtumia tiketi ya boti nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa sita tarehe kama sita mwaka elfu mbili na tisa(2009).Akaja hadi Dar  baada ya ya kuipokea tiketi ambayo nilimkabihi rafiki yangu ambeye alijuwa ni mfanyakazi kweye boti za Baresa.Mchungaji nisiku danganye yule mtoto alikuwa ni mzuri na asili yake ni mwarabu....Ila kitu kilicho kuwa kikinishangaza mimi kila ilipokuwa ikifika saa sita usiku alikuwa anataka kwenda baharini kwa madai ya kwenda kuoga na kutokana tulikuwa tupo karibu na bahari nikawa ninamruhusu kama kawaida.

Ile tabia ikaanza kunichosha ikanibidi siku nimfwatile hadi baharini na kukuta akabadilika na kuwa kama hawa NGUVA......Aisee ile siku Mchungaji niliogopa kupita maelezo na mbaya zaidi alikuwa na wezake wawili ambao nao walikuwa kwenye maumbo kama lake wakichezea maji.
 
Kilicho niingiza kwenye matatizo ni simu yangu kuita na enzi zile ile misimu yenye makelele ya kichina ndio yalikuwa yameingi.Nikastukia kibao kimoja ambacho zikujua nimepigwa na nani na nikajikuta nimeangukia kwenya maji na wakanichukua hadi katikati ya kina kirefu  na kutokana na uzoefu wangu wa bahari nilipajua kuwa pale ni Nungwi”
Nikajikuta nikishusha punzi kwa nguvu baada ya jamaa kupiga fumba la soda kwani story ya jamaa ilizidi kunisisimua mwili wangu na nikajiweka vizuri kwenye kiti huku nikiendelea kusikiliza stori ya jamaa kwani kwa mbali nilisha anza kusahau yaliyonikuta kwangu
“Basi baada ya wao kunichukua  wakanizamisha kama mara mbili hivi nikanywa mafumba kadhaa ya maji nikajikuta nikiishiwa na nguvu za mwili wangu.......”
 
“Wakati wanakuchukua kwenye maji hadi mukafika nungwi mulikuwa munakimbia ua munafanyaje?”
“Mchungaji nilikuwa wala sielewi tunakimbia au tunakwenda taratibu kwa maana nilijikuta tu tumefika Nungwi na kufumba na kufumbua nikajikuta nipo kwenye mjia ambao sikuuelewa kama ni duniani au kuzimu kwani niliona watu wa ajabu sana kiasi kwamba mara kwa mara nikawa ninapoteza fahamu......Waliniingiza kwenye moja ya shimo ambalo kulikuwa na funza wa moto ambao hutoboa mwili kwa haraka kiasi kwamba nilipata maumivu makali”
“Pole Joseph....Unajua siku nilikuwa nimelala Mungu akaniletea maono kwamba kuna mwanadamu ambaye ni wewe upo kwenye hali ngumu sana na akanipa maagizo nifanye maombi juu yako na nifunge kwa siku 7 huku nikiomba na kula kipande cha mkate kwa siku na glasi ya maziwa”
 
Nikaanza kujifikiria sijui nimshirikishe mchungangaji majanga niliyo nayo  ila ikanibidi nikae kimya huku nikiwasikiliza
“Mchungaji sikuweza kuamini kama nitarudi tena duniani kwa maana walikuwa wakinileta hadi huku duniani kuangalia ndugu zangu wanavyo hangaika katika kunitafuta kiasi kwamba nikawa ninatamani niweze kuwasemesha ila nikawa ninashindwa......Nakumbuka mwaka 2010 wakaanza kunifundisha kazi ya kuua watu kwa kusababisha mambo yanayoweza kusababisha ajali.Hata ile ajali ya Nungwi ya kuzama kwa MV Speace mimi pia nilikuwa ni miongoni mwa vijakazi tuliokuwa tunaichukua miili ya watu waliokuwa wanakaribia kufa na kuwapeleka chini ya bahari kiasi kwamba wale watu tulikuwa tunawatumikisha katika kuwaleta wanadamu wengine amabao huku duniani wanakaa kihasara hasara”
 
“Ndio maana watu huwa ninawahubiria kila siku kuwa ndugu tubuni dhambi zenu mwisho wa dunia unakaribia ila bado wameiweka miiyo yao kuwa migumu”
“Kweli mchungaji unayo yasema.....Kule kuna mateso sana....Na usiombe ukatembea na jini lazima ipo siku atakupeleka kuzimu”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbioa kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi baada ya kusikia kuna safari ya kwenda kuzimu
“Na kabla sijapata nafasi ya pekee ya kutoka kule kuna Malkia wao alitumwa kuja Tanga kuiangamiza kupitia mwanaume mwenye nyota kubwa ambaye herufi yake inaanziwa na ‘E’ ila sikujua hiyo ‘E’ ni nani?”
 
Mwili mzima ukaanza kunitetemeka kiasi kwamba nikaanza kujihisi haja ndogo ikitaka kunitoka kwa woga
“Huyo Malkia wao anaitwa nani?”
“Sisi kule tulikuwa tunamuita Mtukufu Malkia ila jina lake nililisikia siku akiitwa na baba yake ambaye anaitwa Hitler na mtoto wake anaitwa sijui Oli.. nini?”
“OLVIA”
Nikajikuta nikiropoka na kuwafanya wanitazame kwa mshangao na kumfanya jamaa kutingisha kichwa akiashiria jina nililo litaja ndilo jina halisi la Malkia wao na kunifanya nizidi kuogopa.Mchungaji akanitazama kwa macho makali hadi nikajikuta nikitazama pembeni nikijifanya kama vile sielewi kitu kinacho endelea
“Kijana”
Mchungaji aliniita na kujikuta nikigeuka na kumtazama pasipo kuzungumza kitu chochote
“Unaweza kuja na kujumuika nasi hapa?”
“Ahhaa....Asanteni”
“Njoo tuu kijana wangu kwani kuna ujumbe wako nimeupata hapa nataka niseme nawe japo kwa ufupi tuu”
“Huo ujumbe umetoka kwa nani?”
“Wewe sogea Mungu atakonyooshea mkono wake na wala usiogope”
 
Nikanyanyuka na kukaa kweye kiti cha pembeni na mchungaji akaniomba nimpe mkono ka ishara ya kusalimiana.Nikaanza kujihisi mkono ukinitetemeka kiasi kwamba nikajikuta nikichomo kwa nguvu kuto kwenye viganja vya mchungaji.
“Kijana usiogope kijana....Mimi ninaona unamatatizo katika maisha yako ila jina la bwana wetu Yesu kristo litafanya maajabu juu ya maisha yako........”
“Umejuaje kuwa mimi ninamatatizo?”
“Nimekuona tuu jinsi unavyo teseka na majanga ya dunii hii na nafsi yako hivi sasa ipo kuzimu na wanaifanyia mpango wa kukufanya wewe kuwa kiongozi wa ambaye utaweza kuiteka hii Tanga na kuwa ndio Makao makuu ya kuzimu kwa Tanzania”
Nikabaki nikimtazama mchungaji huku  mdomo ukiwa wazi na mwili mzima ukazidi kunitetemeka
 
“Mchungaji twende kwangu kuna tatizo?”
“Kwako ni mbali na hapa?”
“Hapna ni hapo juu tuu”
“Sawa...Joseph kama huto jali ywende tukaifanye kazi ya bwana”
Tukanyanyuka na kutoka nje ya bichi na kwauzuri wanagari lao walilo jia katika sehemu hiyo,Tukaingia na nikaanza kuwaelekeza hadi tukafika nyumbani kwangu na sikuwakuta Hilda na mwenzake ila geti tumekuta limejifunga vizuri.Nikafunga geti na kuwakaribisha na kabla mchungaji hajaingia ndani nikaanza kumuona akizungumza zungumza mwenyewe maneno nisiyo yaelewa ila watu husema mtu akizungumza kwa mtindo huo ananena na roho.Mchungaji akafungua mlango na huku akiendelea kuomba na Joseph naye akawa na kazi ya kuomba ila mimi nikawa na kazi ya kuwafwata kwa nyuma hadi sote tukaingia ndani na  kwa bahati mbaya tukamkuta Mwajuma akiwa amelala chini huku akitoka damu za pua
 
Mchungaji akazidisha sauti ya kuomba na kila anvyozidi kuomba ndivyo jinsi hali ya hewa ikazidi kubadilika ndani ya nyumba hadi ikafikia hatua nikaanza kuogopa.Upepo mkali unaokwenda mithili ya kimbuka kikali ukaanza kuzunguka sebleni na baadhi ya vitu vikaanza kuanguka chini ikiwemo vyomvo vilivyopo ndani ya kabati.Nikastukia nikamuona Joseph akirushwa na kupiga ukutani na akatulia kimya na gafla nikamshugudia mchungaji akichmwa na kisu kilichoruka kutoka kabatini na kikatua kifuan kwake

 ITAENDELEA

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts